Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA PROIN PROMOTION ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bw. Johnson Lukaza (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya kuigiza Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(kushoto) akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bw. Johnson Lukaza (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kitaifa mmkoani Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bi. Marrystella Louis.

Picha na: Frank Shija, WHVUM


RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA KIGODA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda ambaye aliaga dunia jana, Jumatatu, Oktoba 12, 2015 katika Hospitali ya Apollo mjini New Delhi, India, ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu tokea Septemba 19, mwaka huu. Alikuwa na umri wa miaka 62.


Katika salamu za rambirambi ambazo amemtumia Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda, Rais Kikwete amesema: “Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za kifo cha Waziri Kigoda ambacho nimetaarifiwa kuwa kimetokea India ambako alikuwa anapata matibabu tokea mwezi uliopita.”


Ameongeza Rais Kikwete katika salamu zake hizo za rambirambi: “Kama unavyojua, namfahamu vizuri Mheshimiwa Kigoda. Alikuwa Waziri wangu. Nimefanya kazi naye  kwa karibu na kwa miaka mingi ndani ya Serikali yetu. Alikuwa mtumishi hodari, mtumishi mwaminifu na mwadilifu kwa wananchi wa Tanzania, na hasa wananchi wa Jimbo la Handeni, ambao aliwawakilisha kwa miaka mingi akiwa Mbunge wao. Tutakosa utumishi wake mahiri sana.”


“Nakutumia wewe Mheshimiwa Pinda, Waziri Mkuu wa nchi yetu salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Mheshimiwa Kigoda. Aidha, kupitia kwako namtumia rambirambi nyingi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Semamba Makinda na Wabunge wote kwa kuondokewa na mwenzao.”


Ameongeza Rais Kikwete: “Nakuomba pia unifikishe salamu zangu za rambirambi kwa wananchi wa Jimbo na Wilaya ya Handeni ambao wamepoteza Mbunge wao aliyewatumikia kwa ustadi mkubwa kwa miaka mingi. Aliwawakilisha vizuri na kujali sana maslahi yao. “


Amesisitiza Rais Kikwete: “Kupitia kwako, Waziri Mkuu pia naitumia familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Mheshimiwa Kigoda kwa kuondokewa na mhimili wa familia na rafiki yao mpenzi. Yajulishe makundi yote hayo kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa, uchungu wao ni uchungu wangu na majonzi yao ni majonzi yangu. Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi. Pia naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema peponi roho ya Dkt. Abdallah Omari Kigoda”. Amen.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

13 Oktoba, 2015 

WIKI YA VIJANA MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo  Mheshimiwa Juma Nkamia (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa maandalizi ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kinachotarajiwa kufanyika Oktoba 14 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
 Mfugaji wa Vipepeo kutoka mkoani  Tanga Jane William akitoa ufafanuzi leo kwa wananchi waliofika katika maonyesho ya wiki ya vijana kwenye Uwanja wa Barafu mjini Dodoma  jinsi ya ufugaji wa vipepeo kwa ajili ya biashara. Moanyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
 Katibu Mtendaji  wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo akitoa maelezo kwa Maafisa Utamaduni mbalimbali juu ya hatua wanazozichukua katika kukagua filamu za kuziwekea madaraja na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kujenga uchumi wa  Nchi. Maelezo hayo ameyatoa leo mjini Dodoma wakati wa wiki ya vijana ikiwa ni kuelekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga(kulia ) akipata ufafanuzi wa hotuba na maandishi mbalimbali yaliyomo katika kitabu cha Mwalimu Nyerere cha Freedom and Unity  leo mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana . Kushoto ni Afisa Mipango  Msaidizi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Edgar Atubonekisye (kulia) . Maonyesho hayo yanaenda sanjari na Kilele cha Mwenge wa Uhuru ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgani rasmi tarehe 14.10.2015 mjini Dodoma.

KUMBUKUMBU YA KIFO

$
0
0
     SEKELA IRENE MULUNGU (Pichani)
 Mama yetu kipenzi, ni miaka kadhaa sasa imepita tokea ulipotuacha wapweke hapa duniani, kumbukumbu ya marehemu mama yangu aliyefariki tarehe (14thOktoba,1998).

Tunakukumbuka na tutaendelea kukuenzi kipenzi chetu. Unakumbukwa na wanao wapendwa,Juliana,Jane,na Jeremiah.Unakumbukwa na bibi,mama wadogo,wajomba,wajukuu,wakwe,ndugu,jamaa na marafiki.

MWILI WA DR KIGODA KUWASILI LEO NCHINI

$
0
0
MAREHEMU Dk Abdalala Kigoda enzi za uhai wake(Pichani) 

 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdalala Kigoda aliyefariki  nchini India unatarajia kuwasili leo mchana tayari kwa ajili ya mazishi.

Ofisa habari wa Bunge, Prosper Minja ameiambia Mwananchi kuwa mwili huo utawasili saa nane mchana kwa ndege ya Emirates na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo.

Minja amefafanua kuwa shughuli za kuaga mwili huo zitafanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wananchi,wabunge na viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

“Taratibu zote za kuaga zitafanyika Karimjee na hapo ndipo tunategemea watu wa kada mbalimbali watafika kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk Kigoda”amesema Minja.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa mazishi kufanyika siku ya Alhamisi.
“Kuna kamati maalum inayohusika na msiba nadhani ikifikia uamuzi itatoa taarifa ila ninachofahamu mazishi yatafanyika Alhamisi nyumbani kwako Handeni” amesema Uledi.

RAIS KIKWETE KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
 RAIS Jakaya Kikwete Alhamis Wiki hii anatarajiwa  kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.  

Mradi huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Turuka alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.

Eneo hilo  litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania, Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).

Chini ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 13 OKTOBA 2015

ASILIMIA 75 YA WANAWAKE HUKUTWA WAKIWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

$
0
0
 Afisa Elimu kutoka  Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Moza Makumbuli akuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu  ya  chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani  nchini unatokana na vijana wanaotumia dawa za kulevya, katika Kongamano la vijana wa kitanzania  kweye ukumbi wa Karemjee  jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya vijana walio shikiriki katika mkutano huo kweye ukumbi wa Karemjee jijini Dar es Salaam
 Picha na Emmanuel  Massaka wa Global ya jamii

IMEELEZWA kuwa chanzo kikubwa cha uvunjifu wa amani  nchini unatokana na vijana wanaotumia dawa za kulevya.

Hayo yamelezwa  Jijini dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Care & Help Bi Karyn David wakati wa Kongamano mahususi lilojadili changamoto za kijamii na uchumi zinazowakabili vijana wa kitanzania hasa wa kike.

Aidha Bi. Karyn amesema kwa sasa jamii imekuwa ikikumbana na tatizo la uvunjfu wa amani kutokana na vijana kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya.

Amendelea kufafanua kuwa Madhara ya dawa za kulevya ni makubwa kwani yanachangia kuleta utegemezi kwa kuwafanya vijana kushindwa kufanya kazi za kuwaletea maendeleo.

Amebainisha kuwa taarifa za Tume ya Udhibiti wa Dawa za kulevya,kwa manispaa yaKindoni,kwa mwaka 2014 imeonyeshwa kwamba kati ya watumiaji wa dawa za kulevya wa jinsi ya kike asilimia 75 kati yao wengi wakiwa na maambukizi  ya virusi vya Ukimwi.

Amesema kwamba maisha ya kijana wa kike wa Kitanzania huanza kupoteza Mwelekeo tokea siku za utotoni za kijana husika, Kwa upande wake  Mratibu  wa uaswa wa Jinsia katika mwitikio wa udhibi wa virus vya Ukimwi toka Tume ya kupambana na Ukiwi nchini TACAIDS,bwana Jacob Kayomba.
Amesema kwa sasa Jamii inapashwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya kwa kudai ndio yamekuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa wa ukimwi.

PSPF YAVUNA WANACHAMA KUTOKA KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WA VOWET

$
0
0

Meneja wa Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akiwaongoza wanachama wapya waliojiunga na mpango huo, wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha maafisa na mabalozi wa PSPF, na wanakikundi wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, (VOWET), kwenye ukumbi wa Belmonte jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Na K-VIS MEDIA


MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).

Wanachama hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la makao makuu ya PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.

Mabalozi hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo, ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la Elimu, na mengine mengi.
Kufuatia :Darasa” hilo, wanachama wa VOWET walijiunga na Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.
 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS KIKWETE AFUNGUA HOSPITALI YA UTAFITI NA TIBA DODOMA

$
0
0
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi ufunguo wa Hospitali ya Utafiti wa magonjwa ya The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital Waziri wa Afya Kebwe Steven Kebwe kama ishara ya kuikabidhi Wizara ya Afya hospitali hiyo leo wakati wa hafla ya ufunguzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali mpya ya The Benjamin Mkapa UltraModern Hospital mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TANO ZA MAGUFULI . UADILIFU .UCHAPAKAZI .UFUATILIAJI .UTEKELEZAJI NA UTUMISHI ULIOTUKUKA

$
0
0
MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amewataka wananchi kumchagua ili awe rais wa tano ajaye wa Tanzania huku akiahidi kushughulikia masuala mbalimbali ya wananchi na hivyo kuliletea Taifa maendeleo kwa muda wote atakaokuwepo madarakani.

Akizungumza na wananchi wa mkoani Lindi katika muendelezo wa kampeni zake, Dk Magufuli alisema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, pamoja na mambo mengine atakayoyafanya atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.

Amesema pia atatumia nafasi hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa korosho, tofauti na utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, alisema umekuwa ukiwasababishia umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.
Akiwa Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Lindi Mjini, Dk. Magufuli alisema tofauti na wapinzani wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchi nzima kwa siku 100 watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake itakachofanya ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

MIAKA 53 YA MAFANIKO: AWAMU YA PILI - MWINYI (1985 - 1995)

$
0
0
Miaka 53 ya Mafaniko: Awamu ya Pili - MWINYI (1985 - 1995)  
 Miaka 53 ya Mafanikio: Awamu ya Tatu - MKAPA (1995 - 2005)

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI LINDI MJINI, NACHINGWEA NA LIWALE

$
0
0
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akimnadi mgombea Urais kupitia CCM, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mpilipili huko Lindi Mjini tarehe 12.10.2015.
 Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete mara baada ya kumwombea kura kwa wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mpilipili tarehe 12.10.2015. Aliyesimama kulia ni Mgombea Ubunge katika Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye.

RAIS JK APOKEA TUZO YA KUKUZA NA KUTHAMINI UTAFITI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia akipokea zawadi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela kutokana na mchango wake mkubwa katika kukuza na kuthamini utafiti nchini, wakati wa Kongamano la 29 la Kisayansi lililoandaliwa na taasisi hiyo ili kuwasilisha na kujadili matokeo ya tafiti za tiba katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kongamano hilo linafanyika jijini Dar es Salam kwa siku tatu (Na Mpiga Wetu).

MAGAVANA WA AFRIKA WAKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA BI. CHRISTINE LAGARDE

$
0
0
Magavana wa Afrika wakutana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim kujadili namna ya kuchochea maendeleo  na kuimarisha uchumi barani Afrika.

 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile wakisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde wakati akiingia kwenye ukumbi wa mkutano.
 Magavana wa Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim nchini Peru – Lima.
 Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye mkutano wakujadili namna ya kuimarisha uchumi na kuchoche maendeleo Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Kamishna Idara ya Sera Bw. Bedason Shallanda, Mhasibu Mkuu Msaidizi Bw. Ishmael Kasekwa, John Mavura mchumi Wizara ya Fedha na Bw. Patrick Pima mchumi Wizara ya Fedha.

MAANDALIZI YA ROTARY DAR MARATHON 2015 YAKAMILIKA

$
0
0
Naibu mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso akiongea na waandishi wa habari leo hii katika ukumbi wa Hyatt Regency juu ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon 2015 ambayo huandaliwa na Rotary klabu za Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M. Mbio na matembezi ya Dar Rotary Marathon kwa mwaka huu zitafanyika katika viwanja vya Green, Oysterbay tarehe 14 October 2015. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Rotary Bi. Sharmila Bhatt, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi. Agnes Batengas, Makamu wa Raisi wa Rotary klabu Oysterbay Bi. Anne Saels na Rais wa Rotary Klabu Dar North Bw. Masato Wassira.
baadhi ya washiriki wa Rotary Dar Marathon kutoka Malawi na Kenya wakifuatilia mkutano huo, Marathon ya mwaka huu itajumuisha wakimbiaji kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Malawi, South Africa na Ethiopia.

Mbio na matembezi ya hisani za Dar rotary marathon yanatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 14.10.2015 hapa jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais mstaafu mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi. 

Mbio na matembezi hayo yameandaliwa na klabu sita za Rotary za hapa Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M na kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuponya maisha, badilisha jamii” ambapo fedha zitakazochangishwa ziltaelekezwa katika ujenzi wa kituo cha afya hapa Dar es salaam. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAGUFULI AMALIZA KAMPENI ZAKE MKOA WA LINDI,AANZA MKOA WA PWANI KWA KISHINDO

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkuranga kwenye mkutano wa kampeni.Dkt Magufuli amemaliza kampeni zake mkoa wa Lindi na baade ameendelea na kampeni zake ndani ya mkoa wa Pwani,ambapo anatarajia kujinadi maeneo mbalimbali ya mkoa Pwani katika kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi katika awamu ya tano,katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyia Oktoba 25 mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita chama cha Mapinduzi,Dtk John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mkuranga,Ndugu Abdallah Khamis Ulega mbele ya umati wa wakazi wa Mkuranga kwenye kutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupita chama cha Mapinduzi,Dtk John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mkuranga,Ndugu Abdallah Khamis Ulega mbele ya umati wa wakazi wa Mkuranga,kwenye kutano wa kampeni
Sehemu ya Umati wa Mkuranga wakishangila jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli uliofanyika Mkuranga.
Sehemu ya Umati wa Mkuranga wakishangila jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli uliofanyika MKuranga.
Dkt. Magufuli akiwa ameshika kadi za Wananchama wa upinzani walioamua kuhamia CCM katika mkutano wa kampeni
Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Mgombea ubunge Jimbo la Nchinga, Said Mtanda katika mkutano wa kampeni Kata ya Nangaru.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kilwa Kusini, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM  mjini Kilwa Masoko.
Wananchi wa Kibiti wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni na kuwaomba kura wananchi hao ili wamchague akawe Rais wa awamu ya tano kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa Oktoba 25 mwaka huu.


Kwaheri Dr. Abdallah Omari Kigoda.

$
0
0
Na Profesa Mark Mwandosya
Imenichukua muda wa zaidi ya saa ishirini kuandika machache kuhusu Dr. Abdallah Omari Kigoda, aliyetutoka akiwa Hospitali ya Apollo, New Delhi, India baada ya kuugua kwa muda mfupi.  
Katika kipindi hicho nimekuwa nikitafakari maneno gani yanaweza kumwelezea Dr. Abdallah Omari Kigoda, maneno ambayo yanaweza kumtendea haki, kuonyesha masikitiko yangu na familia yangu, na kutoa pole kwa familia yake, mkewe, watoto na ukoo wote wa Kigoda, wakiwa Handeni na popote pengine.  
Sijaweza kuyapata maneno hayo.
Kwani yangekuwa maneno mengi, na yenye kubeba ujumbe mzito.  Nakiri sina umahiri wa lugha hasa katika kipindi cha majonzi.  Neno kubwa na zito la kiswahili ni POLE kwa wote, labda kuongezea uzito ni kusema POLE SANA.  Pole hizi pia ni kwa wana Handeni aliowatumikia kwa muda mrefu wa maisha ya kazi; Mkoa wa Tanga, na wana Tanga, mliompa heshima ya uongozi wa kisiasa na maendeleo ya jamii; jamii (fraternity) ya uchumi na wachumi; na Watanzania kwa ujumla wetu.
Abdallah Kigoda ni mmoja wa Watanzania wasomi na wenye uzoefu mkubwa na aliyetoa mchango mkubwa kitaifa na kimataifa.  Hakuwa mzungumzaji sana kama ambavyo sisi wanasiasa tunategemewa kuwa.  Alizungumza pale tu ilipohitajika azungumze.  
Kwa wale tuliokuwa karibu naye tulishangazwa na kufurahishwa pia kwa majibu yake mafupi, sahihi na ya kifalsafa, ya maswali magumu.  Hakuna mtu ambaye angaliweza kuuliza imekuwaje Kigoda amekuwa Waziri, imekuwaje Kigoda amekuwa Mwenyekiti wa Kamati muhimu ya Bunge, au imekuwaje amekuwa Mbunge wa Handeni kwa muda mrefu.  Alikuwa anafaa, alikuwa na uwezo na alikuwa anamudu majukumu yake.  
Kati ya mambo ambayo yalimnyima raha ni tatizo la maji Handeni.  Nathibitisha hilo.  Kwani katika kipindi chote nikiwa Waziri mwenye dhamana ya maji, hakuna siku ambayo tukikutana Bungeni, au katika Baraza la Mawaziri, ambapo hakuniuliza, kunikumbusha, au kunisisitizia kuhusu maji Handeni.  Naamini waliofuata katika Wizara hiyo baada ya mimi kuhamishwa, wamefuatilia suala hilo na ahadi zetu kwake na wanatekeleza mpango wa maendeleo ya maji kuhusu Handeni.  Kama bado basi njia bora ya kumuenzi ni kutekeleza yale ambayo angependa kuyafanikisha alipokuwa hai.
Kwa kumalizia niwakumbushe tukio lililotokea wiki iliyopita la mitandao ya kijamii kutangaza au kama watakavyosema leo kifo kutabiri kifo chake.  Miaka kumi iliyopita yeye na mimi tulikuwa katika “timu” ya watu kumi na moja tulioomba ridhaa ya wana CCM ili mmoja wetu ateuliwe kuwa mgombea wa Chama katika ngazi ya Urais.  Kwa msemo wa kichama “Kura Hazikutosha”!  
Katika kutafuta wadhamini tulikutana Mtwara, yeye akitokea Lindi.  Taarifa zisizo rasmi lakini zilizagaa siku moja kabla zilihusu Dr. Kigoda kupoteza maisha!  
Mithili ya kukutana kwa Dr. David Livingstone na Henry Morton Stanley,Ujiji, Kigoma, nikamuuliza  “Bila shaka ni Dr. Kigoda”.  "Naam", akanijibu kwa kutabasamu.  
Baada ya mazungumzo mafupi akasema, “nawafahamu walionizushia kifo, nimewasamehe”.  Sio hilo tu alilokutana nalo katika mchakato ule, bali kama alivyoniambia alikuwa "mhanga wa siasa za maji taka!”  Na waliomtakia kifo miaka kumi iliyopita! Msihofu.  Kwani moyo wake ulikuwa mkubwa.  Alishawasamehe.
Kwaheri Abdallah.  Kama utumishi wa nchi ni vita,  basi kama askari umepigana vilivyo.  Wakati wa kupumzika umewasili.  Mwenyezi Mungu Airehemu Roho Yako.  Inna Lillahi wa Inna Ilahi Raji’un.

TASAF YAWAHIMIZA WAANIDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO HASA WAKATI HUU WA UCHAGUZI.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuzingatia maadili ya taaluma hiyo hasa wakati huu ambapo taifa linaingia katika hatua muhimu ya kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu.

Mwamanga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kongamano hilo amewasihi waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya taaluma yao ili kuepukana upotoshaji na kuitia nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Amesema taaluma ya uandishi wa habari ina umuhimu mkubwa katika kujenga Jamii na isipotumiwa vema inaweza kuhatarisha amani na utengamano wa taifa jambo ambalo amesema halifai kufumbiwa macho.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya PEACOCK mjini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akifunga komgamano la waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es salaam  lililojadili utekelezaji wa uhuru wa habari kwa uangalifu hususani wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano lililoandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam baada ya kufunga rasmi kongamano hilo lililojadili juu ya uchaguzi huru na haki bila waandishi wa habari kuzingatia maadili ni ndoto. 

MAMA SAMIA AANZA KAMPENI MKOANI KAGERA LEO, AWANADI KAGASHEKI NA MWIJAGE

$
0
0
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera leo.
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipozunguza na waliposimamisha msafara wake katika eneo la Buseresere, wakati akiwa njiani kutoka Geita kwenda Bukoba kuendelea na kampeni leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Chato kwa tiketi ya CCM, Dk. Karineli katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela akijadili jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Balozi Hamis Kagasheki wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Mgombea Ubunge jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera, Charles Mwijage akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images