Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 996 | 997 | (Page 998) | 999 | 1000 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Na Francis Dande
  NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki, amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mpango wake wa kujenga nyumba bora na kuwauzia wananchi kwa ajili ya  makazi na biashara.

  Waziri Kairuki aliyasema  hayo juzi  jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua  mauzo ya nyumba  za biashara  na makazi zilizojengwa eneo la Morocco Square,  Kinondoni,  jijini Dar es Salaam.

  Aliwapongeza Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu na wenzake kwa  kazi nzuri wanayoifanya kwa kiasi kikubwa katika kuleta  uhai na taswira nzuri ya  shirika hilo.

  Alisema kuwa serikali inatambua kuwa  makazi  ni jambo  muhimu kwa maendeleo ya taifa, ndiyo  maana imekuwa ikichukua hatua  mbalimbali ili kuwezersha sekta  ya nyumba kuwa endelevu na yenye  tija kwa wananchi  na uchumi wa nchi.

  Alibainisha kuwa moja ya mambo yaliyofanyika katika kukuza sekta hii ni kuwa  na Sheria ya Mikopo ya nyumba (The Mortgage Financing (Special Provision Act) ya  mwaka  2008,  iliyoanzishwa  kuweza kuwafanya wadau wa sekta ya  nyumba wakiwemo waendelezaji, wanunuzi wa nyumba  na taasisi za fedha  kushiriki kikamilifu katika kukukuza sekta hii muhimu.

  Aidha , alisema tangu kuwapo kwa  sheria  hiyo, tangu mwaka 2008 kumeshuhudiwa benki 19 kati ya  zaidi ya benki 50 zilizopo nchini zikitoa  mikopo ya nyumba kwa  Watanzania, 16  kati ya  hizo zikiwa zimesaini makubaliano na  na Shirika la Nyumba la Taifa ili kuweza  kutoa mikopo kwa Watanzania wanao nunua nyumba zinazojengwa na NHC.

  Naibu waziri huyo alisema kuwa  kutokana na  kuwepo kwa  changamoto  ya riba kubwa  ya  mikopo ya nyumbva inayotozwa  na benki mbalimbali ambayo ni kati ya asilimia 18  na 25, serikali itaendelea  kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania ili kuona namna bora ya kuewezesha  benki  kupunguza riba  katika  mikopo ya nyumba ili Watanzania wengi waweze kukopa na kununua  nyumba.

  Aliwahimiza Watanzania  kutumia  fursa zilizopo za mikopo ya Benki kununua  nyumba zinazojengwa na NHC, ikiwamo kujitokeza  kwa wingi kununua nyumba hizo za  za mradi wa  Morocco Square ambao una nyumba za ofisi hoteli, makzi na maduka makubwa.

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mauzo ya nyumba za biashara na makazi-Morocco Square uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande)
   Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
    Naibu Wazriri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu. 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Kipande cha barabara ya njia Panda Isanga karibu na Hotel ya Lifti Valey jijini Mbeya (LUPA WAY )ambacho kimejengwa upya kwa kuongezewa njia kimeleta sura mpya jijini hapa  lakini kimeleta pia changamoto kwa madereva hasa kwa nyakati za usiku  kwani hakuna taa hivyo nivema watumiaji wa barabara hii wakachukua tahadhari kwa kuto endesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zisizo za lazima ...JAMIIMOJABLOG

  0 0

  Kwa mbali kabisa, Kamera ya Binagi Media Group-BMG ikapata fursa ya kunasa picha za Shule ya Sekondari Kenyamanyori ambayo ilijengwa kwa nguvu za Wananchi miaka michache iliyopita na kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013 baada ya kukamilika ambapo wanafunzi waliokuwa kidato cha pili katika shule zilizokuwa mbali walihamia shuleni hapo na kuendelea na kidato cha pili huku wengine walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huo.
  Na:George Binagi-GB Pazzo
  Ni ukweli usiopingika kuwa uongozi wa kijiji hicho pamoja na wananchi wake ambao asilimia kubwa ni wakulima, wanastahili pongezi kwani wazo lao la kujenga shule ya sekondari ni wazo bora na limewasaidia watoto wa kijiji hicho na wale wanaotoka vijiji jirani kupata elimu karibu zaidi hivyo ni vyema wakaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wahisani wengi katika kuhakikisha kwamba wanaiboresha zaidi shule hiyo ili iweze kuwa mkombozi kwa ajili ya watoto wao kielimu.
  Kulia ni jengo la Utawala na Majengo mengine matatu kushoto ni majengo ya maabara tatu za Sayansi
  Majengo mawili ya Maabara.


  0 0

  Na Anna Nkinda – Tarime
  WANAWAKE wilayani Tarime wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu itakapofika na wachague viongozi watakaowaona wanafaa ambao watawaletea  maendeleo.

  Rai hiyo imetolewa leo na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Mara katika ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya CMG.

  Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema kupiga kura ni haki ya kila mtu hivyo basi haitakuwa busara kwa  wanawake hao kuharibu kura zao kwa kukaa majumbani siku ya uchaguzi ikifika bali waende kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha .

  “Kura ni siri ya mtu, wewe ndiye unayefahamu kiongozi gani wa kumchagua nawasihi chagueni viongozi wazuri na siyo bora viongozi, wahimizeni wanawake wote waliojiandikisha washiriki kupiga kura kwani kura zenu yako ndiyo itakayokupatia kiongozi unayemtaka”, alisema Mama Kikwete.

  Alisema siasa siyo uadui wala ugomvi bali ni mchakato wa kidemokrasia na kuwataka wagombea wote kunadi sera zao kwa kufuata utaratibu na amani kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopangwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi ili utulivu na Amani viendelee kutawala nchini.

  Aliwasihi, “Msigombane kutokana na tofauti ya itikadi za vyama vya siasa, angalieni siasa zisiwafarakanishe ikafika hatua mkashindwa hata kusaidiana ikiwa ni pamoja na kushindwa kuzikana kumbukeni nyinyi ni ndugu wa wilaya moja ya Tarime”.

  Aidha Mama Kikwete aliwataka  wanawake hao kujenga tabia ya  kujiwekea akiba Benki kutokana na fedha wanazozipata katika kazi wanazozifanya kwa kufanya hivyo wataweza kukopa fedha nyingi ambazo watafanyia shughuli za maendeleo na hivyo kujikomboa kiuchumi. 

  “Unganeni  pamoja ili muweze kujikwamua kiuchumi, simameni katika majukwaa teteeni haki zenu, pingeni mila zilizopitwa na wakati ambazo zinamkandamiza mwanamke na hivyo kumrudisha nyuma kimaendeleo kwa kufanya hivyo mtaweza kujikomboa  kutoka katika hali ya unyanyasaji”,alisisitiza .

  0 0


  0 0


  EALA SITTING TO BE HELD IN NAIROBI NEXT WEEK

  EAST African Legislative Assembly, Arusha, October 3, 2015: The East African Legislative Assembly (EALA) resumes its sitting in Nairobi, Kenya next week. The Plenary which takes place from Monday, October 5, 2015 to Thursday, October 15, 2015, is the Second Meeting of the Fourth Session of the Third Assembly.

  The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two week period is a Special Sitting that is expected to be addressed by President Uhuru Kenyatta. 

  The Assembly is also expected to debate on and pass key pieces of legislation, adopt reports and pose questions to the Council of Ministers.Three key Bills on the cards at the EALA meeting are the EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015, the EAC Electronic Transactions Bill, 2014 and the EAC Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2015. 

  The EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015 hopes to promote the development, protection, conservation, sustainable management and use of the forests in the Community especially trans-boundary forests ecosystems, in the interest of present and future generations.  It further wants to espouse the scientific, cultural and socio-economic values of forests and harmonise national forest laws.

  The Objective of the Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2015 is to provide a legal framework at regional and national level for timely intervention in disaster situations and to protect the people and the natural environment affected by disaster through comprehensive disaster risk reduction and management.

  EALA is further set to revisit debate on the EAC Electronic Transactions Bill, 2014 which was deferred at the last Sitting in Kampala, Uganda to pave way for additional stakeholders to make their input.   The Bill seeks to meet the need of exploiting electronic transactions in the modern day business transactions.

  The Bill further wants to promote technology neutrality in applying legislation to electronic communications and transactions and to develop a safe, secure and effective environment for the consumer, business and the Governments of the Partner States to conduct and use electronic transactions. 

  While in Nairobi, the House is also expected to receive and to debate on a number of reports.  They include that of the Committee on Regional Affairs on the goodwill mission to Kigoma, Tanzania and Eastern Province of Rwanda to interact with refugees from Burundi.

  The Committee on Communications, Trade and Investments on its part will table for debate its Report on the oversight of EAC One-Stop Border Posts (OSBP).

  At its last Sitting in Uganda in August this year, the Assembly passed the EAC Culture and Creative Industries Bill, 2015, adopted three Resolutions as well as six Reports.
   
  For more Information, contact: Bobi Odiko, Senior Public Relations Officer; 
  East African Legislative Assembly; Tel: +255-27-2508240 Cell: +255 787 870945+254-733-718036; Email:  bodiko@eachq.org This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it   Web: http://www.eala.org Arusha, Tanzania


  0 0

  SERIKALI imeshauriwa kuutumia vema mwezi Oktoba, mwaka huu kukuza uelewa  kwa wananchi juu ya masuala ya mitandao ili kupunguza kama si kuondoa kabisa uhalifu mitandaoni.

  Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Usalama wa Mitandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidijitali, Yusuph Kileo wakati akizungumza na Majira.

  "Nichukue nafasi hii kutambua na kuhamasisha tukio la kipekee katika anga ya usalama katika mitandao jambo ambalo limekuwa likiadhimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba, ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa masuala ya usalama wa mitandao duniani kote," alisema Kileo.

  Alisema, wakati mataifa mbalimbali duniani yakitarajiwa kuadhimisha tukio hilo anaamini Tanzania itauchukulia mwezi huo kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake.

   

  "Hilo ni tukio ambalo nategemea kampuni mbalimbali na maeneo mengine yataandaa programu mbalimbali za kukuza uelewa wa masuala ya usalama mitandaoni ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote wa mitandao duniani kote," aliongeza mtaalamu huyo.

  Aidha, alisema inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote kuwa ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa  tatizo la uhalifu kwenye mitandao. 

  "Tatizo kubwa  ni kuwa njia hizi zimekuwa zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama wa mitandao; mimi binafsi nilikuwa miongoni mwao," alifafanua Kileo.

  Alisema, baadhi ya njia za kukabiliana  na tatizo hilo ni kupitia elimu ya uelewa wa uhalifu katika mtandao na namna ya kujilinda. 

  "Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbalimbali za uhalifu kwenye mitandao, athari zake, njia ya kujilinda na namna ya kulinda wenzake," alisema Kileo.

  KUPITIA KIPINDI CHA KUMEPAMBAZUKA CHA RADIO ONE NIMEPATA KUSHIRIKI KWA NJIA YA SIMU HOJA ILIYO HOJI ---- IKIWA NI TAKRIBANI MWEZI MMOJA BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO HAPA NCHINI,WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA PAMOJA NA WADAU WENGINE WANATOA TATHIMINI GANI.  0 0

   Harakati za kusaka nafasi ya juu  ya uongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo zimepiga kambi mkoani Singida kwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli pichani kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo kwenye mkutano wa kampeni.

  Dkt Magufuli ameishauri tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutimiza wajibu wake wa kutenda haki kwa wagombea wote wa ngazi za Uraisi,pia amewataka Wananchi wakatae kulaghaiwa na baadhi ya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu,kwa kuzinunua shahada zao za kupigia kura,badala yake amewaomba wazitunze shahada hizo ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wapige kura.
   Maelfu ya Wananchi wa Singida wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia na kujinadi kwa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza iwapo watamchagua kuwa Rais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,kwenye uchaguzi mkuu,Dkt Magufuli amewaomba wananchi hao alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Peoples ,mjini Singida.
   Wakazi wa mji wa Singiga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt Joh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima mbele ya maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples  mjini Singida jioni ya leo.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi kwa wakazi wa Iramba mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya chama hicho. 
  Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza katika bonde la Sibiti kupitia barabara ya Nduguti kuelekea wilayani Mkalama,kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
   Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.

   Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa People's,mjini Singida katika mkutano wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kabla ya kuanza kuwahutubia jioni ya leo.
     Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akiwaomba wakazi wa mji wa Singida na vitogoji vyake waliofurika kwenye mkutano wa kampeni,kuwa ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mbunge na Madiwani ili wapate ushindi wa kishindo. 

    Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu January Makamba akimuombea kura za kutosha mmgomea Urais wa CCM Dkt Maguli pamoja na Mbunge na Madiwani wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples  mjini humo.
  Baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
   Maelfu ya wakazi wa Singida wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo.
  Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu),Mohamed Dewji akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Singida na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples ,mjini Singida,Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti chake cha Ubunge,Ndugu Mussa Sima.  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aonya wasimamizi wa uchaguzi mkoani humo kuzingatia na kufuata sheria katika zoezi la kupiga kura kuepusha vurugu.https://youtu.be/E4PqPs6h9uY

  Mgombea uraisi wa Zanzibar Dr.Shein aahidi kupandisha bei ya zao la karafuu endapo atachaguliwa ili kuinua kipato cha wakulima. https://youtu.be/hlUp7Y0XU1c

  Mgombea mwenza wa uraisi aahidi kutatua na kuondoa migogoro ya ardhi mkoani Simiyu kufuatia kukithiri kwa migogoro mkoani humo. https://youtu.be/AA3y7T9r0kk

  Raisi Kikwete serikali kwa kushirikiana na hosptiali ya CCBRT itahakikisha inatokomeza tatizo la fistula. https://youtu.be/q2t5paQ8x9M

  Zaidi ya shilingi milioni 6 zinatarajiwa kutumika kuzilipia bima ya afya Kaya 100 zikiwemo za watu wenye ulemavu, wajane na watu waishio kwenye mazingira magumu https://youtu.be/J3av9BxheLM

  Vyama viundavyo ukawa vyaitaka tume ya uchaguzi kuhakikisha daftari la wapiga kura linakuwa la haki ili kuondoa hofu. https://youtu.be/gKtVcvRPdA4

  Watanzania watakiwa kuwa makini na sera zinazotolewa na wanasiasa majukwaani kabla ya kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi https://youtu.be/Jrjfn1zUapo

  Mgombea wa Chadema Edward Lowassa aahidi kupitia upya katiba pendekezwa ili kuhakikisha inaingiza serikali tatu https://youtu.be/itbOcypzJDA

  0 0
 • 10/03/15--21:00: Kumbukumbu


 • 0 0

  Freight In Time (TZ) LTD (‘FiT’), the Authorized Service Contractor of UPS (NYSE: UPS), a global leader in logistics,opened its doors tovalued customers at a special event today at The Southern Sun Hotel in Dar es Salaam. 
  The event highlighted FiT’s appreciation to local customers and in turn provided customers with an opportunity to meet FiT’s management and ask questions first hand. FiT opened in Tanzania in 1997 and provides customers with a broad range of services with flexible pick-up and delivery times. 
  Since 2005, the company became the authorized service contractor in Tanzania ofUPS and has served its customers with the highest level of service backed by UPS’s world class network and technology, its focus on service quality, and a deep-rooted culture of precision and innovation..UPS is a recognized leader with expertise in international air freight forwarding, regional supply chain management and intra-Africa logistics. 
  Customers can combine package and freight services for greater supply chain efficiency and cost-effectiveness. 
  Shamit Shah, Group Executive Directorof FiT commented, “FiT and UPS’partnership in Tanzania has gone from strength to strength over the last 10 years and we wanted to give something back to our loyal customers. The event is a testimony of our commitment to providing our customers with an efficient, reliable service. Providing a platform for discussion and interaction, the event also offered an opportunity to demonstrate our appreciation of their loyalty.
  “Our customers are at the heart of what we do, we will continue to support our clients to develop their businesses, through our global network and innovative services facilities”, he added. FiTemploys 72 local citizens and operates at airports in Dar, Zanzibar, Kilimanjaro, Mbeya and Mwanza. UPS Border point offices include Namanga, Holili,HoroHoro, Tunduma, Kasumulu and Sirare, whilst also serving seaports in Dar Es Salaam and Mombasa. 
  UPS, a global leader in logistics with 435,000 employees worldwide, has been in the region since 1988, with its regional headquarters based in the UAE. 
  The India Sub-Continent, Middle East and Africa region is the largest UPS region with more than 70 active countries. Through access to a worldwide network serving over 220 countries and territories, UPS is invested to the success of a daily delivery average of more than 18 million packages and documents. Mr Shamit Shah,Group Executive Director FiT
  Mr Shamit Shah, Group Executive Director FiT.
  Mr Dave(Centre) Freight in Time Financia Controller and guests
  Mr Dave (Centre) Freight in Time Financial Controller and guests.
  Mr Fred Mlay Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests
  Mr. Fred Mlay, Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests.
  victor maina, air and sea freight commercial manager
  Victor Maina, Air and Sea Freight Commercial Manager exchanging views with the invited guests.
  CEO sign industries M.P Esmail
  CEO sign industries M.P Esmail giving a comment.


  0 0


  Je wafahamu magazeti ya leo yametoka na mpya gani kuhusu wagombea uraisi na wengine ? Tazama uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/C60J6zYwoCc

  DR.Magufuli ahofia ulanguzi wa shahada za kupigia kura,Lowassa ataka serikali 3 pata habari hii na nyingine kupitia udondozi wa magazet. https://youtu.be/vQK34Cbh-4o

  DR.Magufuli ahofia ulanguzi wa shahada za kupigia kura,pata habari hii na nyingine nyingi kupitia udondozi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/BrDxGSFap_k

  0 0


  Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni.

   Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini, amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia
   Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani  Jafari Mohamed na amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, kwa kusema kuwa Mchungaji Mtikila amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze. 
  "Gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na ndani yake mlikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya sana. Majeruhi hao walikimbizwa katika Hospitali ya Tumbi kwa matibabu", alisema.
  Kamanda Mohamed amesema  chanzo cha ajali kinachunguzwa na taarifa itatolewa mara tu baada ya kukamilika uchunguzi rasmi.
  Wakati huo huo wananchi wengi wameelezea masikitiko yao kwa vitendo vya watu wengi kurusha picha ya mwili wa marehemu Mchungaji Mtikila ukiwa umelazwa pembeni ya kinachoonesha ni gari alilokuwa akisafiria kabla ya kupata ajali.
  Wengi waliowasiliana na ofisi zetu wameitaka TCRA kuwa wakli na sheria zilizopo na ambazo tayari zimeshaanza kutumika zitumike na zioneshe zinatumika".
  Kwa kweli inatia uchungu sana kuona badi ya Watanzania sijui kwa ujuaji sana ama kwa kutaka sifa kwenye magurupu huko wamerusha picha ya mwili wa Mch. Mtikila.
  "Nimeiona na sikupendezwa nayo kabisa", amesema Benjamin Mbozila akiwa jijini Nairobi. "Afadhali wangerusha ile ya gari tu, lakini mwili mzima na sura inaonekana sio sawa kabis", Janeth Mtonyi alieko ujerumani ametuandikia.

  0 0

  Mzee Simon Kamillius Membe wa Rondo, Mkoani Lindi, amefariki jana tarehe 3 Oktoba 2015 huko Mumbai, India alipokwenda kwa ajili ya matibabu.

  Mipango ya mazishi inafanywa Dar es Salaam  nyumbani kwa mdogo wake Mhe Bernard Membe (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini siku ya jumatatu mchana tarehe 5 Oktoba 2015 saa 9 alasiri.

  Ibada na heshima za mwisho ‎kwa Dar es Salaam zitafanyika siku ya jumanne tarehe 6 Oktoba 2015. Mahala na muda wa tukio hilo utatangazwa hapo baadaye.

  Mwili wa Marehemu utasafirishwa kutokea Dar es salaam kuelekea Lindi siku ya jumanne baada ya ibada kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Rondo, Lindi siku ya jumatano tarehe 7 Oktoba 2015.

  0 0

  Na Anna Nkinda – Maelezo, aliyekuwa Tarime
  WAKAZI wa wilaya ya Tarime wametakiwa kuachana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa mila za ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.

  Mwito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua uboreshaji wa Hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo mkoani Mara.

  Mama Kikwete alisema ukeketaji unaleta matatizo  makubwa ikiwa ni pamoja na kupata matatizo wakati wa kujifungua, mtoto wa kike kupata maumivu makali wakati wa ukeketaji na pia kitendo hicho husababisha kutoka damu nyingi na matokeo yake ni kifo.

  “Wazazi na walezi acheni mila hizi ambazo hazina faida kwa wakati huu na ni ukiukwaji wa haki za binadamu bali wasomesheni watoto wenu wa kike ili waweze kuwa walezi bora wa familia zao na jamii kwa ujumla”, alisisitiza.

  Aliendelea kusema kuwa katika jamii baadhi ya wanawake wanadhalilishwa, kunyanyasika kijinsia na kupata mateso ya aina mbalimbali kama vile kupigwa, kunyimwa haki ya kumiliki mali na kutokuwa na maamuzi ya matumizi ya mali ya familia hata kama wao ndiyo wazalishaji.

  Alisema, “Tabia hizi hazikubaliki kabisa katika Dunia ya leo.Mwanamke anayo haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu pia anayo haki ya kufanya maamuzi  ya pamoja kwa kile alichozalisha kwani mwanamke ni binadamu na siyo chombo cha kuzalisha mali. Binadamu wote ni sawa”.

  Kwa upande wa  watumishi wa kada ya afya aliwahimiza kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia kwamba miundombinu ya Hospitali hiyo imeboreshwa  lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya hususani akina mama , watoto na wazee.

  Mama Kikwete aliwaomba viongozi, kina baba na wadau mbalimbali  waliohudhuria uzinduzi huo  kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza  na hatimaye kuokoa kabisa vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika wilaya hiyo pia wahakikishe kina mama na watoto wanapata huduma bora za afya. 

  “Akina mama wajawazito wahudhurie kliniki muda wote wa ujauzio pia hakikisheni wanajifungulia katika vituo vya afya na hospitali. Wapelekeni watoto kliniki hadi watakapotimiza umri wa miaka mitano ili wapate kinga wanazostahili”,  aliwasihi. 

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Dkt. Calvin Mwasha alisema wazo la uboreshaji wa Hospitali hiyo liliasisiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Glorius Luoga alipofanya ziara Hospitalini hapo mwanzoni mwa mwaka huu na kubaini kuna matatizo ya uchakavu mkubwa wa majengo.

  Uchakavu wa miundombinu ya maji safi na taka, ubovu wa mfumo wa umeme, uchakavu wa vitanda na matandiko,uchakavu na uhaba wa vifaa tiba na vitendea kazi, uhaba wa madawa, ukosefu wa jengo la utawala na upungufu wa watumishi mbalimbali.

  “Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya wilaya ya Tarime wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wakati, wachimbaji madini wakubwa (ACACIA North Mara Gold Mine) na wadogo, Taasisi za Umma na binafsi, watumishi wa Umma na wananchi walifanikiwa kuchanga shilingi milioni 345, mashuka 80 na vitanda tisa”, alisema Dkt. Mwasha.

  Aliyataja maboresho yaliyofanyika kuwa ni majengo ya wagonjwa wa nje, akina mama na watoto, maabara, upasuaji ambapo mwanzo kulikuwa  na chumba kimoja cha upasuaji baada ya maboresho kuna vyumba vinne na jengo la upimaji virusi kwa hiari (VCT).

  Wodi za wazazi, magonjwa ya akina mama na upasuaji, akina baba, TB wanaume na wanawake, majengo ya jiko ambalo kwa sasa litatumika kama jengo la kuhudumia wateja wa mifuko ya bima ya afya (CHF na NHIF) na jengo la ufuaji.Ujenzi ambao bado kuanza ni Jengo la utawala na sehemu ya kupumzikia  wagonjwa.

  Dkt. Mwasha alisema kuna  vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 263 ambavyo vimeagizwa kutoka China kupitia kwa mwenyekiti wa maboresho Peter Zacharia. Kutokana na mahusiano yake mazuri na wafanyabiashara wa huko vifaa hivyo ambavyo bado  havijalipiwa vimeshafika wilayani Tarime.

  Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine ya standard stabilizer moja, oxygen concentrator moja, vitanda 130, baiskeli za kubebea wagonjwa 20, mashine ya kupimia full blood picture moja, BP Machine Digital 50 na nguo za kuvaa wagonjwa.

  Hospitali ya wilaya ya Tarime ilijengwa mwaka 1956 tangu kipindi hicho inahudumia wananchi wa wilaya  hiyo, Serengeti na Rorwa.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  SERIKALI  imesema inafanyia kazi mpango mkubwa wa kupima ardhi zinazomilikiwa kimila na kutoa hati kwa wahusika.

  Mpango huu ambao uko mbioni kuanza kama majaribio ni moja ya maazimio ya mkutano wa 9 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  Akitoa majumuisho ya mkutano huo kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TNBC, Balozi Ombeni Sefue alisema kuharakishwa kwa mpango wa kutoa hati za umiliki wa ardhi za kimila kutasaidia watanzania walio wengi zaidi kuweza kwenda katika vyombo vya fedha, kupata mikopo na kuboresha maisha.

  Balozi Sefue ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi alisema tayari ofisi ya Mpango wa Kurasimisha Mali na Biashara Tanzania (MKURABITA) na Wizara ya Ardhi na Makazi zinaoanisha mifumo itakayowezesha mchakato huo kuwa wa haraka na gharama nafuu.

  “Hatua hii itasaidia kupunguza gharama na watu wengi zaidi kufikiwa,” alisema, na kuongeza kuwa timu ya wataalamu kutoka serikalini itaundwa kushughulikia swala hilo.

  Mpango huo utatumia vifaa na njia za kisasa na taarifa zote za ardhi zitaweza kupatikana kielektroniki.

  Mapema, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa TNBC alisema mpango huo utasaidia kuongeza thamani ya ardhi na kusaidia kuondoa migogoro ya ardhi hapa nchini.

  Kwa mujibu wa Balozi Sefue utaratibu wa kuanzisha idara itakayosaidia ushiriki wa watanzania katika uwekezaji wa ndani na nje unaendelea.

  Idara hiyo itakayokuwa katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) inalenga kujenga uwezo kwa watanzania na kuwafanya kuwa sehemu ya mchakato mzima ujenzi wa uchumi na sio kubaki kuwa watazamaji tu.

  Mkutano huo pia uliongelea maswala mbalimbali yanayolenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini na utalii.  Muda maalumu wa utekelezaji wa maswala hayo uliwekwa.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye alisema mkutano huo ulikuwa wa mafanikio.

  “Hii inaonyesha kuwa sekta binafsi na umma zinaweza kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya nchi,” alisema.

  Katibu Mtendaji wa TNBC, Bw. Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo ulikuwa ni uthibitisho kuwa maendeleo yanaweza kupatikana kwa haraka kama sekta hizo zitafanya kazi kwa ushirikiano wa dhati.

  Wakati wa mkutano huo, Rais Kikwete alizindua mfumo wa kielektroniki wa usajili wa majina ya biashara.

  Mfumo huo ulioanza kutumika na wateja wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mwezi wa Sita mwaka huu unamwezesha mwananchi kupata jina la biashara ndani ya dakika kumi tu kama kila kinachohitajika kipo.

  Mkutano huo ulikuwa wa mwisho kuendeshwa na Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa TNBC kabla ya kumalizika kwa muda wake wa uongozi mwaka huu.


  0 0

   Washiriki wa mchezo wa kukuna nazi wakishindana katika Bonanza la michezo ya Jimbo la Tunguu yaliyofanyika kiwanja cha Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
   Mmoja wa washiriki akifurahia kumaliza kukuna nazi.
   Mshiriki wa mbio za Baskeli Zainab Juma akimaliza mbio hizo akishikilia nafasi ya nne.
   Mgombea uwakilishi Jimbo la Tunguu kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Simai Mohommed Said akiteta kitu na Mwenyekiti wa CCM Jimbo Tunguu Khatib Ramadhan Iddi (katikati) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali.
   Mwenyekiti wa CCM Jimbo Tunguu Khatib Ramadhan Iddi akizungumza na washiriki wa CCM Bonanza lililofanyika Bungi Mkoa wa kusini.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali akimpa zawadi kepte wa tim ya Nage ya Bungi (B) Shida Saidi. (Kulia) mgombea Upunge wa Jimbo la Tunguu Khalifa Salim Suleiman. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Tatizo la watoto wa kike mkoani Mtwara kukatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali limepungua kwa kiasi kikubwa baada ya uwepo wa mradi wa “Hakuna wasichoweza” unaoendeshwa na T-Marc kwa ufadhili wa Vodacom Foundation. 
   Mradi huo umeonyesha mwelekeo wa kuweza kutatua matatizo yanayowakabili watoto wa kike kutotimiza wajibu wao wa masomo mashuleni, ikiwa ni pamoja na kutotimiza ndoto zao sambamba na kupunguza utoro. 
   Akizungumza wakati wakati wa mrejesho wa mwenendo wa mradi huo kwa wadau wa elimu wa mkoa huu, Meneja wa Mradi huo, Doris Chalambo alisema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2013 kwa mkoa wa Mtwara ulilenga kufikia wanafunzi 10,200 wa shule za msingi kuwapatia elimu ya afya, namna ya kujisitiri wakati wa hedhi na kupatiwa vifaa vya kujisitiri ambapo katika thamini yake iliyotolewa chini ya utekelezaji wake kwa mkoa wa Mtwara umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuweza kupunguza tatizo la utoro. 
   “Lengo la mradi ni kufikia wasichana 10,200 kwa mkoa wa Lindi na Mtwara lakini kwa mkoa wa Mtwara wanafunzi wapatao 7,077 tayari wamefikiwa na tumekuwa tukiwapatia elimu juu ya hedhi, elimu itakayomsaidia pindi anapokuwa kwenye hedhi afanye kitu gani pamoja na elimu ya afya na madhara ya mimba za utotoni sambamba na kumsaidia vifaa vya kujisitiri (pedi) na hii ni kutokana na kuwa suala la hedhi halizungumziwi kabisa katika jamii yetu hivyo mtoto anapata changamoto na kumpelekea kukosa shule kati ya siku 2 hadi tano ndani ya mwezi mmoja na kumrudisha nyuma kieleimu,”alisema Chalambo. 
   Aidha alisema changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo ni pamoja na baadhi ya shule kukosa miundombinu kama vyoo na chumba maalumu kwaajili ya kusaidia wasichana katika masuala ya afya na kuwa, Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili itakuwa mkoa wa Lindi. 
   “Katika kutekeleza mradi huu hatuwezi kufanikiwa bila ya miundombinu, tumegundua shule nyingi vyoo sio vizuri, kwahiyo bila kuendana na miundombinu sahihi hatuwezi kufanikiwa,”alisema Chalambo. Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Mtwara, Jose Kitenana alisema mradi huo umeweza kuleta mabadiliko katika mkoa huo na kuwa serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha miundombinu ya shule inakuwa rafiki. 
   “Mpango huu ni mzuri na kwa sisi serikali hatuwezi kufanya kila jambo, hivyo kuna wadau tunashirikiana nao kama T-Marc kutoa elimu ya afya kwa wanafunzi kwa udhamini wa Vodacom Foundation ili kusaidia watoto wetu wa kike, na suala la miundombinu bado zipo taratibu ambazo zinafanyika kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki,”alisema Kitenana 
   Naye Mkuu wa Vodacom Foudation, Renatus Rwehikiza alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa wanatekeleza mradi wa hakuna wasichoweza kwa lengo la kuongeza mahudhurio ya watoto shuleni na kuwa itapunguza kasi ya magonjwa,utoro na mimba za utotoni. 
   “Vodacom Foundation inatoa misaada kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa hivi tuna mradi wa ‘hakuna wasichoweza’ umegharimu kiasi cha 480 milioni ambao umetekelezwa kwa awamu na sasa kwa mkoa wa Mtwara tumefikia ukingoni tunasubiri kupata tathmini ya huu mradi na awamu ya pili tutakuwa mkoa wa Lindi lakini nina imani kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza ile kasi ya utoro na mimba za utotoni na kumwezesha mototo wa kike kutimiza ndoto zake,”alisema Rwehikiza 
   Akizungumza mwanafunzi, Doreen Mvungi alisema mradi huo umeweza kuwapa maarifa namna ya kukabiliana na changamoto walizokuwa wakizipata pindi wanapopatwa na hedhi shuleni na kuondokana na aibu ya kuzomewa waliyokuwa wakiipata toka kwa wavulana. 
   “Najivunia kuwa sehemu ya walionufaika na Mradi huu ni mkombozi umetupa elimu ya afya, elimu namna ya kujisitiri tunapokuwa katika hedhi na imewasaidia wengi kwani siku hizi hamna tena ile zomea zomea na hata mahudhurio ya darasani yameanza kuwa mazuri kwa sisi wasichana tofauti na zamani msichana alipokuwa akipatwa na ile hali anashindwa kujua nini cha kufanya,”alisema Doreen
  Baadhi ya wadau wa elimu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye warsha maalumu ya mrejesho  wa mradi wa”Hakuna wasichoweza” unaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
  Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi  Chuno ya Mkoani Mtwara,wakiendelea na masomo yao baada ya kunufaika na mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi ili waendelee na masomo yao mashuleni.Mradi huo umedhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
  Meneja Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark Tanzania Doris Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao ulikuwaunaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania. 
  Meneja Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark Tanzania Doris Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao ulikuwaunaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.


  0 0

  Mr. Radhey Mohan (Vice president – International Marketing, Apollo Health City, Hyderabad), Dr. Mahesh Verma (Ministry of Tourism & Civil Aviation), Hon. Sh. Pranab Mukherjee (Hon. president of India), Ms. Sangita Reddy (Joint Managing Director, Apollo Hospitals Group) and Mr. Vinod Zutshi (Secretary – Ministry of Tourism, Govt. of India).

  Hon. President of India presenting an Award for Best Medical Tourism facility to Apollo Health City, Hyderabad. This is the third consecutive year that Apollo Health City, Hyderabad is receiving this prestigious award.

  0 0

       
                       2015-09-28

  Jumuiya ya Watanzania Sweden  
  Mahali: Näsby Alle´6

  183 55 Näsby Park

  Siku: Jumamosi

  Tarehe: 31-10-2015

  Saa: 9:00 jioni

      

        Kwa watanzania tunatoa taarifa ya wito wa Mkutano Mkuu wa ziada kwa ajili ya kuchagua viongozi watakao chukua majukumu ya kuwaongoza watanzania waishio nchini Sweden, na kujenga uhusiano na taasisi mabali mbali na vyama vyengine viliopo nchi jirani.

       Uongozi wa kamati ya maandalizi ya Jumuiya ya Watanzania inawataarifu kwamba nafasi za uongozi huo ni kama zifuatazo;

   Uenyekiti

  Unaibu

  Ukatibu pamoja na bodi ya utawala wa chama.

    Tunawaomba watanzania wajutokeze kwa wingi katika mkutano huo ili tuweze kuboresha umoja wetu na kujenga maadili bora kwa watanzania, kujitolea kwenu ndio mafanikio ya taifa letu.


  Asanteni

  Kamati ya matayarisho
older | 1 | .... | 996 | 997 | (Page 998) | 999 | 1000 | .... | 3282 | newer