Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MIILI YA VIJANA WA JKT WALIOPATA AJALI YA GARI BULOMBORA YAAGWA LEO

$
0
0
  Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma akitoa heshima zake za mwisho kwa askari wa JKT wa kikosi cha 821 Bulombora Kigoma waliofariki jana kwa ajali ya gati.

Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma wakitoa heshima zao za mwisho kwa askari  wa kikosi cha 821 JKT bulombora waliopata ajali ya gari jana na kufariki dunia.

Askari kutoka vikosi na majeshi mbalimbali wakiwa mbele ya majeneza ya askari wenzao wa kikosi cha 821 JKT Bulombora waliofariki jana kwa ajali kwaajili ya kutoa heshima za mwisho.
 Askari wa majeshi yote wakishirikuana kuweka miili ya wenzao katika eneo la kutilea heshima za mwisho waliofariki jana kwa ajali ya gari.

Na Editha Karlo wa 
Globu ya Jamii, Kigoma
MIILI saba ya vijana wa  jeshi la kujenga Taifa(JKT)  kikosi cha 821 Bulombora waliofariki dunia  jana kwa ajali ya gari wameagwa leo na kusafirishwa makwao kwaajili ya mazishi.

Akiongea na waombolezaji waliofika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa kigoma(Maweni)kwaajili ya kuaga miili ya marehemu Mkuu wa vikosi vya Kigoma, Kanali Msuya alisema jeshi limepoteza nguvu kazi ya Taifa .

Alisema mpaka sasa taratibu zote za kusafirisha miili hiyo zimeshakamilika miili yote itaondoka kwa usafiri wa magari hadi mwanza na kesho watasafirishwa na ndege ya jeshi kwenda dar es salaam kwaajili ya kupelekwa kwenye mikoa yao kwa maziko.

Kanali msuya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni MT 54407 SGT Ally Kambangwa mkazi wa mtwara,MT 108151 PTE Abeli Maisha mkazi morogoro,SM Eugini Bitati mkazi wa kibondo.

Wengine ni AH 7190 SM Saidi Sadara mkazi wa Shinyanga,RES Bakari Kibaya mkazi wa Tanga,RES Fredrick Kahemela mkazi wa arusha.

Msuya aliwataja majeruhi pia majina yao kuwa ni Benadicto Ndokeye,Raphael Yohana,Athanas Emanuel,Abuu Nzoge,Abubakari peter,Abubakari Msubi na Denis Manyanya.

Wengine ni Edward Nyanda,Elias Magessa,Gofrey Maliki,King Kasefu,Kamilius Agida,Stive Denis,Saidi Omary,Saidi Zuberi,Shabaani Zakari,victor John,Jackson Nyarubu na Mohamed Nyimbo

Naye katibu tawala wa Mkoa wa kigoma eng.John Ndunguru alisema kuwa serekali ya mkoa imepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya askari hao saba na watashirukuana na wafiwa bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.

"Serekali ya mkoa ina masikitiko makubwa kwa kupokea habari hizi za kuondokewa na askari wetu tutashikiriana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu"alisema Ndunguru.

STOP PRESS: RUFAA ZA MRAMBA NA YONA ZAGONGA MWAMBA, KUTUMIKIA MIAKA 2 BADALA YA MITATU, FAINI YA MILIONI 5 YAFUTWA

$
0
0

Na Mwene Saidi wa Globu ya Jamii

Rufaa iliyokatwa na mawaziri wa zamani  Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yonah imegonga mwamba katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo, baada ya kuwapunguzia mwaka mmoja na kuwaondolea faini ya milioni 5 na kutakiwa kuendelea kutumikia kifungo cha miaka miwili  baada ya mahakama hiyo kuona hakuna ushahidi wa kuthibitisha shitaka la kusababisha hasara ya Sh. bilioni 11.7.


Kadhalika, mahakama hiyo imesema Mahakama ya Kisutu, ilikuwa sahihi kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja kwa kuwa hakuna ushahidi uliothibitisha kuhusika na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara hiyo.



Hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa mbili saa 3:28 hadi 5:00 na Jaji Projest Rugazia aliyesikiliza rufaa mbili zilizokatwa na pande zote mbili dhidi ya kesi hiyo.



Awali upande wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga hukumu ya kumwachia huru Mgonja na utetezi ulikata rufaa kupinga hukumu ya kuwatia hatiani Mramba na Mgonja.
Jaji Rugazia alisema hakuna ushahidi ulitolewa mahakamani kueleza namna gani washtakiwa walihusika kusababisha hasara na kwamba adhabu ya kosa hilo ilitolewa kimakosa dhidi ya washtakiwa.
Alisema kulingana na ushahidi uliotolewa hakuna lawama kwa Mahakama ya Kisutu, kumwachia huru Mgonja dhidi ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili kwenye kesi hiyo.
Pia, alisema haoni kama kuna sababu ya kumhusisha rais (wakati huo Benjamini Mkapa) kwa kuwa alitoa maelekezo kulingana na maelezo aliyopewa na mshtakiwa wa Yona.



"Sioni sababu ya kumtumia rais kwa makosa yaliyotokea kwa kuwa alitoa maekezo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na mshtakiwa wa pili, Yona... pia hakuna ushahidi uliowaweza kuelezea mahakama namna gani washtakiwa walifanya kosa la 11 la kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7, mahakama hii inatengua adhabu ya kosa hilo na washtakiwa watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja" alisema Jaji Rugazia.
Mapema Julai 6, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliwatia hatiani washtakiwa hao na kumwachia huru Mgonja.
Wafungwa hao kwa pamoja  wamekutwa na hatia ya makosa 10 ya kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation kwa ajili  ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.

JK AONGOZA KIKAO CHA TISA CHA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Bw.  Frank Kanyusi akitoa maelezo kuhusu wavuti mpya ya wakala huo ambayo kuanzia sasa mteja atakuwa anajisajili yeye mwenyewe kupitia huduma hiyo ya mtandaoni
  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha kikao cha tisa cha baraza hilo katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 2, 2015
   Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi wavuti mpya ya BRELA  ambayo kuanzia sasa mteja atakuwa anasajili kampuni ama taasisi yake yeye mwenyewe kupitia huduma hiyo ya mtandaoni. PICHA NA IKULU
Picha zaidi BOFYA HAPA

Maalim seif ahutubia mkutano wa kampeni katika uwanja wa Masumbani jimbo la Chumbuni,

$
0
0
Na Khamis Haji, OMKR
 Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema akichaguliwa atakuza uwezo wa Serikali kujiongezea mapato na ataongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia 400,000. 
Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika uwanja wa Masumbani jimbo la Chumbuni, Maalim Seif amesema Sera ya CUF imeonesha maeneo mengi ya kukuza uchumi na kuziba mianya inayochangia kupotea mapato ya Serikali, hivyo hakuna kitakachozuia Serikali kuwalipa wafanyakazi na wastaafu kiwango cha kuridhisha. 
Aidha, amesema kwa upande wa askari wa vikosi vya SMZ, majukumu yao ni makubwa na magumu zaidi na kima cha chini watakacholipwa itakuwa ni shilingi 450,000 ambapo kwa upande wa wastaafu pencheni yao itaanzia shilingi 200,000. 
Amesema kuwa hivi sasa uwezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kukusanya shilingi bilioni 30 kwa mwezi, lakini kwa mipango ya CUF kikichaguliwa kuongoza Serikali na kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi kitaongeza mapato hayo hadi kufikia bilioni 50 kwa kuanzia. 
Katika hatua nyengine, Maalim Seif amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, Serikali yake itatoa elimu bure kuanzia msingi hadi Chuo kikuu. 
Ameeleza kuwa huduma za afya pia zitatolewa bure katika hospitali na vituo vyote vya afya vya Serikali, ikiwa ni hatua ya kutekeleza malengo ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
 “Hivi sasa viongozi waliopo wanasema wanalinda misingi ya Mapinduzi, lakini huduma nyingi wananchi wanalipishwa, mimi ndiye nitakaye vaa viatu vya mzee Karume”, alisema Maalim Seif. Mwenyekiti wa timu ya Ushindi wa CUF, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali itakayoundwa na CUF iwapo wananchi watakichagua itaunda Tume Huru ya Mipango itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kubuni mipango ya kuiondoa Zanzibar kwenyeb umasikini. 
Amesema kuwa miradi mingi inayotekelezwa Zanzibar hivi sasa ni ya kutumia fedha badala ya kuingiza fedha, jambo ambalo linasababisha Serikali kushindwa kukusanya mapato vizuri na kuqweza kuwa na uchumi unaopaaa kwa kasi.
 Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika mkutano wa hadhara uwanja wa Masumbani jimbo la Chumbuni
Wanachama na wafuasi wa CUF wakimsikiliza Maalim Seif huko uwanja wa Masumbani 

Mkutano wa Kampeni Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Shein Gando Wete Pemba.

$
0
0

Mgombea Urais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Gando akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa Kampeni Kisiwani Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Uwakilishi wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 

Mgombea Urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Udiwani wa CCM Wilaya ya Wete Pemba wakati wa Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Gando Pemba. 
Picha zaidi BOFYA HAPA

MKALI WA SONGI LA 'AMARULA' ROBERTO TOKA ZAMBIA AWASILI NCHINI TANZANIA, ATUA MWANZA PATA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA JEMBA FM 93.7

$
0
0
Mtangazaji wa Jembe FM host wa kipindi cha HIT ZONE kinachoruka hewani siku za Jumatatu hadi Ijumaa saa saba mchana hadi saa kumi jioni Timoth Ngalula aka 'Mbaba' akifanya mahojiano na mwanamuziki toka nchini Zambia Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, ikiwa ni maandalizi ya show yake kali itakayofanyika kesho Jumamosi ya tarehe 3 oct 2015 Jembe Beach Resort Malimbe jijini Mwanza, Kiingilio ni shilingi 10,000/= Kawaida na VIP ni shilingi 50,000/=.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA SEHEMU YA KWANZA.  
Mwanamuziki toka nchini Zambia Roberto ambaye ni mkali wa songi linalokwenda kwa jina la Amarula, hapa akisikiliza kwa umakiini moja kati ya maswali yaliyoulizwa na HIT ZONE ya JEMBE FM Mwanza ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA SEHEMU YA PILI.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Tanzania salutes Republic of Korea on the country’s 70th anniversary of the National Day.

$
0
0
H.E Park Geun-hye, President 
of the Republic of Korea
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. PARK Geun-hye, President of the Republic of Korea. The message reads as follows:

Her Excellency PARK, Geun-hye,

President of the Republic of Korea,

Seoul,



Your Excellency,

On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to convey my warm congratulations to you and through you, to the Government of the Republic of Korea on the auspicious occasion of celebrating your country’s 70th anniversary of the National Day.  

The government of Tanzania highly values the ties, which exist with the Government of the Republic of Korea, and is ready to maintain and enhance the relations in a bid to benefit the peoples of the two countries. Together, we have built bridges between our two nations in every conceivable field, from education, health, infrastructure and commerce and trade. It is therefore vital that we continue to work together so as to contribute to the efforts of making the world a better place to live.

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your continued good health, progress and prosperity of the people of the Republic of Korea”.



Issued by: The Ministry of Foreign 
Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

2nd October, 2015

ICTR to Host Closing Events in December 2015

$
0
0



To honour the many victims of the genocide and mark the completion of the United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda (UN-ICTR)’s mandate, the ICTR will host a series of events including a formal closing ceremony at its headquarters in Arusha, Tanzania in December 2015.  The closing ceremony will be held on 1 December 2015 and will feature brief remarks from high-level officials of Tanzania, Rwanda, the UN, the ICTR and the ICTR Staff Association. 
In addition to formal speeches, the closing events will feature the launch of several legacy projects, including the completed ICTR Legacy Website, and compendium of legacy papers.  The Legacy Website will provide a user-friendly platform for easy access to all ICTR cases and other legacy materials. The compendium will be comprised of approximately 40 papers presented by leading practitioners at the ICTR’s 2014 20th Anniversary Legacy Conference on topics ranging from promotion of trial rights, case management, judgement drafting, evidence assessment, and witness protection.   
A special exhibition of major milestones in the ICTR’s fight against impunity will also be on display during the events.  In addition, a permanent UN-ICTR Peace Park will be unveiled in Arusha city to commemorate the Tribunal’s work and its many contributions to the local community. Other events include the launching of a book containing a collection of essays written in honour of the Prosecutor, and a Prosecutors Round Table Conference. 

The Tribunal is inviting all former ICTR staff members, interns, and defence counsel to attend these historic events.

WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA TEHAMA KUTOKANA NA KUKUA KWA TEKNOLOJIA HIYO.

BE YOUR OWN BOSS, FOR SALE THREE PIECES TYRE MACHINE FULL SET

$
0
0
 INCLUDING;
1. TYRE CHANGE
2. WHEEL BALANCER
3.COMPRESSOR

PRICE: 7,000,000 TZS

ITEM SPECIFICATIONS: ITEM IS USED BUT IN VERY GOOD CONDITIONS, JUST IMPORTED FROM THE UK

ITEM LOCATION: ZANZIBAR, BUT WE CAN SHIP ANYWHERE YOU ARE

FOR MORE INFORMATION CONTACT US:
MR. SALEH 0774-659895
MR MBARKA 0779100064



MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA SHULE YA SEKONDARI J.K.NYERERE HUKO TARIME

$
0
0
.
 Mama Salma Kikwete akitoa hotua ya uzinduzi rasmi wa Shule ya Sekondari ya J.K.Nyerere katika Kijiji cha Myamwaga kilichoko Mkoani Mara.

 Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa Mkoa wa Mara na wale wa Wilaya ya Tarime na wahisani waliojenga Shule ya J.K. Nyerere kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Shule hiyo iliyoko katika Kijiji cha Nyamwaga.
 Mama Salma Kikwete baada ya kukata utepe hapa anakiondoa kitambaa kukamilisha sherehe ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza Ndugu Jimmy Ijumba, Meneja wa ACACIA –North Mara Gold Mine mara baada ya kuzindua rasmi shule hiyo 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamwaga ikiwa ni ishara ya kuagana nao baada ya kuifungua rasmi Shule ya Sekondari J.K. Nyerere iliyoko katka Wilaya ya Tarime.

Vijana msitumike kwa maslahi ya Chama chochote cha siasa - Tume ya taifa ya uchaguzi

$
0
0
Na Ally Daud-Maelezo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa vijana kutojihusisha na vitendo vya fujo katika kipindi hiki cha  kampeni  badala yake waelekeze nguvu na  juhudi  zaidi katika kujenga uchumi wa taifa.
Akiongea katika mkutano uliowakutanisha NEC na wawakilishi wa vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid Mahmoud Hamid  (pichani) alisema kuwa  vijana wasitumike na vyama vya siasa kama kichocheo cha fujo .


“Vijana kamwe msikubali kutumika kwa maslahi ya chama cha siasa ila tumieni vizuri elimu yenu na upeo wenu wa kufikiri namna ya   kujenga na kuendeleza  taifa”,alisema Jaji Hamid.

Aidha Jaji Hamid aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuhamasisha watu mbalimbali umuhimu wa kupiga kura kwani wao ni sehemu muhimu na ndiyo nguvu pekee inayotegemewa katika jamii ya Tanzania.

Naye  Mkurugenzi wa NEC  Bw. Kailima Ramadhan amesema kuwa  wananchi wanatakiwa kuheshimu  sheria na kanuni za uchaguzi  kwa  mwaka  huu wa 2015 ili kufanya uchaguzi kuwa haki na amani.

“ Natoa wito kwa wananchi  wa Tanzania  kuepuka  kuingilia kazi za watumishi wa Tume ya uchaguzi kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi atapiga kura katika kituo alichojiandikisha ili kuepusha usumbufu “ alisema Bw. Ramadhan .


Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka utaratibu maalum wa namna ya  kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  Octoba 25 mwaka huu kwa  ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani ambapo madiwani watatangazwa na mkurugenzi wa NEC ngazi ya kata, Wabunge ngazi ya Jimbo na Rais atatangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dk. Binilith Mahenge akutana na mabalozi wa Uswisi na Ufaransa

$
0
0
Waziri wa  Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mh. Dk. Binilith Mahenge (wa kwanza kushoto), akijadiliana  na Balozi wa Uswisi  nchini, Bi Florence Tinguely Mattli (katikati),  kuhusu Mkataba wa Mazingira wa Minamata unaohusu matumizi ya Kemikali ya Zebaki na Madhara yake katika Mazingira, Majadilaino hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  Katibu Mkuu wa Ofis hiyo Bw. Sazi Salula (kulia), jijini Dar es Salaam leo

 Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Binilith Mahenge akiwa kwenye picha ya pamoja na Baloz wa Ufaransa nchini, pamoja na wageni waliotembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam  kwa ajili  kujadili  mchango wa Tanzania katika Mkutano wa Ishirini na Moja wa nchi wanachama wa Mkataba Mpya wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika jijini Paris nchini Ufaransa Desemba mwaka huu.

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dk. Binilith Mahenge akiwa na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi  Malika Berak wakionesha nyaraka zinazungumzia mchango wa Tanzania katika Mkataba mpya wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika katika Mkutano wa Ishirini na Moja wa nchi wanachama wa Mkataba huo jijini Paris, Ufaransa Desemba mwaka huu. Picha na OMR

West Wing Week 10/2/2015 or "Make It Matter"

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 02.10.2015


Maisha ni Siasa Official Trailer

WATANZANIA WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL ILIYOPO CHALIZE MSOLWA MKOANI PWANI

$
0
0
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakielekea kupandisha bendera ya Taifa wakati wakisherekea mwaka mmoja wa shule hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakiwa  ndani ya darasa la Komputa.
wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya majaribio ya masomo ya Sayansi ambayo ni Fizikia pamoja na Kemia katika chumba hicho cha majaribio ya masomo hayo shuleni hapo leo.
Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay akitolea ufafanuzi moja ya kifaa kinachotumika kuchuja maji ambayo yamechanganywa na mchanga mbele ya wazazi na walezi waliofika shuleni hapo kwaajili  ya siku ya Imperial iliyofanyika leo shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na vikombe na vyeti vyao walivyozawadiwa leo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperialwakitoa burudani katika siku ya Imperial iliyofanyika leo mkoani Pwani.

 KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. 

MAHAFALI YA SITA YA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

$
0
0
WATAALAM wa Ununuzi na Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya wanataaluma waliosajiliwa. 

Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha  Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).

Aidha Bodi imepongezwa kwa kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.

 Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi kwa kuongeza  masomo ya maadili, ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni  mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika matumizi ya rasilimali fedha. “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.

Aidha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa na Bodi.

Alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali, msingi na taaluma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Dr Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali.
 Dk Hamis Mwinimvua katikati aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho  na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya.
 Dk Hamis Mwinimvua akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi.
 Mgeni Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja
 Sehemu ya wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.

MAMA SAMIA SULUHU ASIMIKWA UMALKIA WILAYANI MASWA, WAMWITA NGOLE

$
0
0
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa. 

Aliyekuwa mbunge wa CCM Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Uwanja wa Nguzo Nane Maswa leo.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan leo amepewa heshima ya kusimikwa kuwa malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na kupewa jina jipya la Ng'walu Majura.

Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo leo na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Magharibi kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.

Mama Suluhu ambaye amepewa jina jipya la heshima hiyo la Ng'walu Majura alivishwa mavazi maalum ya kimila ya heshima 'Ngole' yaani malkia na kukabidhiwa mkuki maalum, ungo na usinge pamoja na kupewa zawadi anuai za vyakula vya kimila kwa kabila la Wasukuma eneo hilo.

Wakimpa heshima hiyo akinamama wa UWT walisema Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo kwa kuwa ni mwanamke aliyekuja kuibua mambo mazuri kwa ushindi wa CCM na Tanzania kwa wanawake. Akinamama hao waliahidi kumuunga mkono ili kuhakikisha anashinda na kuwatoa kimasomaso Wanawakea wa Tanzania.

Kwa upande wake Mama Samia Suluhu amewashukuru akinamama hao kwa heshima na zawadi mbalimbali walizompa na kuwaahidi kupigania maslahi yao zaidi endapo chama chake kitafanikiwa kuunda Serikali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Alisema licha ya kupigania maendeleo ya taifa zima yeye kama mwanamama ana ajenda maalum za kuwapigania akinamama kuanzia huduma za kijamii hadi uwezeshwaji kwao ili kuleta usawa na maendeleo kwa jamii hiyo.

Alisema amepokea kilio cha maji Maswa na kwa kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa maji atahakikisha Maji yanapatikana kupitia miradi anuai inayotekelezwa eneo hilo na kwa kuanzia watachimba visima 10 maeneo mbalimbali ya Maswa ili kuwapatia maji wakazi wa maeneo hayo.

Mapema majira ya asubuhi Mama Samia Suluhu alifanya mkutano wa kampeni katika Jimbo la Meatu akiinadi ilani ya CCM kwa wananchi, ambapo aliwaomba kuichagua CCM kwani imepanga kufanya mengi kwa wanaMeatu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, ujenzi wa malambo na majosho kwa ajili ya kuhudumia mifugo yao.

Alisema ili kuondoa migogoro kwa wafugaji na wakulima safari hii Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kupima ardhi yote ya vijiji na Wilaya na kisha kuainisha mipaka ya wakulima na wafugaji na kuwamilikisha jamii hizo kumaliza migogoro.

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Taifa akinadi Sera za CCM mkutano wa hadhara Meatu leo.
Umati katika mkutano wa mgombea mwenza leo.
CCM Oyeeeeeeee....katika mkutano wa hadhara Jimbo la Maswa Mashariki.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki akiwahutubia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

RAIS ALIPOKUTANA NA MADEREVA UBUNGO PLAZA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na madereva wa mabasi pamoja na kuwaanga madereva hao katika hoteli ya Blue Peal jijini Dar es Salaam leo.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images