Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

JUST IN: KITUO CHA MICHEZO CHAENDELEA KUJIZATITI: Aliyekuwa Kocha kwenye Ligi Kuu ya Uingereza aja Tanzania kuongoza kituo cha vijana cha michezo

$
0
0
Ndugu Ray Power, ambaye amewahi kuwa Kocha wa Chama Cha Soka na mkuu wa kitengo cha mpira wa miguu katika chuo kiitwacho Central College Nottingham; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika Kituo cha Vijana cha Michezo kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam (pichani). 
Katika nafasi yake mpya, Ndugu Power atasimamia mafunzo na Uongozi wa kituo kipya ambacho kinategemewa kufunguliwa tarehe 19 ya Mwezi huu. Ndugu Power anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo; Stewart Hall aliyejiunga na timu ya Azam kwa mara nyingine kama Kocha Mkuu.

 “ Hii ni changamoto kubwa kwangu na ninaichukua kwa moyo mkunjufu. Kuna kiwango kikubwa cha elimu kinachoendana bega kwa bega na michezo na sina shaka uzoefu wangu kama kocha na kama muelimishaji ayehitimu mafunzo yake; vyote kwa pamoja vitanipa uwezo unaotakiwa kwenye nafasi hii” alinena Ndugu Power ambaye ni kocha mwenye leseni ya kiwango cha daraja la ‘A’ inayotolewa na Shirikisho la Soka la Ulaya ( UEFA) na mwandishi maarufu wa ukuzaji wa soka la vijana.

Kituo cha Kijamii cha Michezo kitatoa uwanja wa nyasi bandia ulio na ukubwa wa 3G, pamoja na viwanja viwili vinavyoruhusu wachezaji watano watano kila upande, kiwanja kimoja chenye mchanga pamoja na viwanja viwili vya mpira wa kikapu n.k

 Ndugu Power aliongeza “ Filosofia yangu itakuwa kwa mtu mmoja mmoja katika kituo, kumsaidia kila mmoja kuendelea; maana kila mtu ana uwezo wake na udhaifu wake tofauti na mtu mwingine. Nimedhamiria kusaidia ukuaji wa fursa za michezo na njia maalumu za kimpira wa miguu zitakazo wawezesha vijana wa kitanzania kujiandaa kwa changamoto watakazo kabiliana nazo siku za usoni” 
Kituo cha vijana ambacho kimefadhiliwa na Symbion Power, kitapata msaada wa kiufundi na mazoezi kutoka kwa Timu iitwayo Sunderland AFC ambayo inashiriki ligi Kuu ya  Barclays ya Uingereza. Hii itakuwa ya kwanza ya namna yake ya kipekee kwa hapa nchini Tanzania. Maelfu ya vijana wa kitanzania watafaidika na muunganiko wa michezo, elimu na Ushiriki katika Shughuli za kijamii kwa kutumia maarifa na utaalamu wa wakufunzi kutoka timu ya mpira ya Sunderland. 

Paul Hinks, Mtendaji Mkuu wa Symbion Power alinena: “ Kituo cha Vijana Jakaya Mrisho Kikwete ni kiungo cha kati cha Ushirikiano wa kipekee kati ya Symbion Power, Timu ya mpira ya Sunderland na Tanzania na tunaamini ubora alionao Bwana Ray pamoja na uzoefu wa timu ya mpira ya Sunderland utatuwezesha kushuhudia ukurasa mpya wa maendeleo ya michezo nchini Tanzania


STOP PRESS: VIJANA SITA WA JKT BULOMBORA MKOANI KIGOMA WAPOTEZA MAISHA 21 WAJERUHIWA KATIKA AJALI JIONI HII

$
0
0
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma .
VIJANA sita  waliokuwa  katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jioni hii.

 Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. 

 "Ni kweli leo majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21. "Wengine  wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma"alisema Dkt Fadhili.

 Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.  "Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja  majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema. 

 Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka. 

 Alisema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori  hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na unga.
Kamati ya ulinzi na usalama ikitembelea vijana wa JKT Bulombora kikosi namba 821 ambao ni majeruhi wa ajali wakiwa wodi namba 7 katika hospital ya mkoa wa Kigoma wakiendelea kupatiwa matibabu
Baadhi ya vijana wa JKT Bulombora kikosi namba 821 ambao ni majeruhi wa ajali wakiwa wodi namba 7 katika hospital ya mkoa wa Kigoma wakiendelea kupatiwa matibabu
 Mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa wa kigoma Dkt. Fadhil Kibaya akiongea kuhusu ajali hiyo. 

2nd PAN-AFRICAN MOSQUITO CONTROL ASSOCIATION (PAMCA) ANNUAL SCIENTIFIC CONFERENCE, 6-8th OCTOBER 2015

KONGAMANO LA ELIMU YA JUU LAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) wa Tawi la Arusha, Regina Lema akitoa maelezo kwa mmoja ya wageni waliofika katika maonyesho yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu ya juu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Chuo Kikuu cha Muhimbili cha jijini Dar es Salaam kimeshiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Mmoja ya washiriki ambaye amebuni mtambo wa kuchuja maji akitoa maelezo machache.
Mwakilishi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambaye aliambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Mandela cha jijini Arusha, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania aliyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya. Picha zaidi BOFYA HAPA


FNB TANZANIA YAHIMIZA WATANZANIA KUWEKA AKIBA ZAIDI

$
0
0
Meneja wa Wateja Binafsi wa First National Bank, Francois Botha na Meneja wa Usambazaji na Matawi wa benki hiyo wakizindua mpango maalum unaohamasisha Watanzania kujiwekea akiba na kujiwekea mustakabali salama kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2015.

BENKI ya FNB Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujijengea mustakabali salama kifedha kwa kuendelea kuweka akiba zaidi benki kupitia fursa ya mpango mpya wa benki hiyo wa “Weka akiba na ushinde”.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha wakati akizindua mpango huo jijini Dar es salaam ambapo alisistiza umuhimu wa kuweka akiba. Mpango huo wa Weka Akiba na Ushinde utaanza tarehe 1 Oktoba na kuendelea mpaka mwisho wa Disemba 2015.

Ikiwa ni sehemu ya mpango huo utakaodumu kwa miezi mitatu, wateja waliopo na wateja wapya wataingizwa moja kwa kwenye droo kutokana na akiba ya kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao, kwahiyo watakaoweka akiba zaidi watapata nafasi ya kushinda shilingi milioni 5 ambazo zitatolewa kila mwezi kwa kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki.

Botha alisema, “Katika kuendeleza utamaduni wa benki hii kuwatunuku na kuwanufaisha wateja wake huku ikiendelea kutoa huduma za kisasa za kibenki, FNB inatoa fursa hii kwa wateja kuweza kujinufaisha kutokana na kuweka akiba huku wakijijengea mustakabali salama kifedha”.

UJENZI WA MSIKITI KIMBANGULILE , MKURANGA PWANI

$
0
0
 Msikiti mpya wa Kitongoji cha Kimbangulile, Mkuranga Pwani
 Msikiti wa zamani wa Kitongoji cha Kimbangulile Wilaya ya Mkuranga mkoni Pwani.
Tunamshukuru Mungu kwa wale wote walio tuunga mkono katika harakati hizi Mungu awabariki.

Zaidi pia Mungu awabariki waendeshaji wa blog hii ya Jamii kwa kutuunga mkono katika kupeleka habari kwa Jamii na kutuunga mkono katika harakati zetu.

Ndugu zangu Wapendwa Michango tuliyo kusanya toka mwanzo Program PROJECT zetu za kheri hizi ni Tshs 6,000,000 ( Milioni Sita ) .

Pesa hizi zimetumika katika kuwezesha kufanya Mambo Mawili katika sehemu tofauti , Sehemu ya Kwanza ni Mkoa wa Pwani , Wilaya ya mkuranga , Kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha Kimbangulile hapa tumewezesha kuubadilisha ki ujenzi Msikiti kutoka katika hali ya Nyasi kuwa hali ya bati kama mnavyo ona katika Picha . 

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE ATAKA NCHI ZILIZONYUMA KIMAENDELEO KUZUNGUMZA KWA KAULI MOJA

$
0
0
Mhe.  Mahadhi J. Maalim  Naibu Waziri, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akizungumza wakati wa Mkutano wa Nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Kundi hilo uliofanyia siku ya Alhamis hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Nyuma ya  Naibu Waziri, ni  Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa  Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania  katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan  M. Mwinyu 

Na Mwandishi Maalum, New York
 WAKATI  kila  Nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa,  ikijianda kwa utekelezaji wa Ajenda 2030 ambayo  inajikita zaidi katika kuondoa umaskini pasipo kumwacha yeyote nyuma, sanjari na kuilinda Sayari Dunia. Tanzania imehimiza  haja na umuhimu  wa nchi ambazo  ziko  nyuma kimaendeleo ( LDCs) kuzungumza kwa kauli moja.


Ushauri huo umetolewa  jana Alhamis na   Mhe. Mahadhi Juma Maalim ( Mb),  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa LDCs uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, sambamba na majadiliano ya  jumla ya  Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Katika mkutano huu wa  Mawaziri wa LDCs, Bangladesh  ilikabidhiwa uenyekiti wa  Kundi hilo kutoka kwa Benin inayomaliza muda wake. Pamoja  na Kuishukuru Benin kwa kuliongoza kundi hilo vema wakati wa  uenyekiti wake Mhe. Naibu Waziri ameiahidi Bangladesh ushirikiano  kutoka Tanzania.

“ Kundi letu linawachama wengi, tutumie basi wingi wetu  kuhakikisha  kwamba tunasukuma mbele na kuteteta masuala  yanayotuhusu kwa  kuzungumza kwa sauti  moja wakati wa majadiliano na kuhakikisha kuwa ajenda tunazosimamia  kwa maslahi yetu  hazikwami.” Amesema Naibu Waziri

Aidha Naibu Waziri Mahadhi, amelikumbusha kundi hilo kuwa moja  ya lengo kuu la kundi ni kuondoka katika kundi la nchi maskini na kuwa nchi zenye uchumi  wa kati.


“ Kwa bahati nzuri  suala la kuondoa umaskini ni moja ya eneo ambalo limepewa umuhimu wa kipekee katika Ajenda 2030, hivyo ni wajibu wetu  kama LDCs, kutumia fursa hii kwa kuhakikisha kwamba, katika kipindi cha miaka 15 ijayo nchi nyingi katika kundi letu  zina-graduate na  kuwa nchi zenye uchumi wa kati”. Amesisitiza.


Mhe. Naibu Waziri amerejea  kwa kusisitiza kauli  iliyotolewa na  Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipolihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, siku ya  Jumanne, Kwamba utekelezaji wa Ajenda 2030 ndiyo changamoto iliyombele yetu kwa sasa na kwamba utekelezaji wake ukikwama, LDCs ndizo zitakazo athirika zaidi.


Ni kwa sababu hiyo juhudi za pamoja katika kuhakikisha utekelezaji wa  Ajenda  2030 ni mihimu na  za lazima.


Kundi la   Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo na kama zinavyotambuliwa na Umoja wa Mataifa zipo 48

Ajenda 2030 ambayo ilipitishwa wakati wa mkutano wa kilele wa kisiasa uliofanyia kwa siku tatu hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  ni   Ajenda yenye malengo 17 ya maendeleo endelevu  yakichukua na nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ambayo yanafikia  ukingoni  mwaka huu wa 2015


Ajenda 2030 itaanza kutekelezwa mwakani ( 2016 )na utekelezaji wake ni wa miaka 15

TARATIBU ZA KUFUATWA NA WATANYABIASHARA WADOGO


VIWANJA 53 VYENYE HATI NA NYUMBA VINAUZWA.

$
0
0
1.     Viko Mbweni  usalama  wa  taifa, vina  hati miliki, viko  karibu na  barabara  ya  lami na viko  karibu  na  beach,  vipo  Sqm  600 – 1500, bei  ni  kuanzia  milioni 35 mpaka  45.

2.     Nyumba 3 zinauzwa, zipo Mwananyamala “A”, moja vyumba 12, nyingine vyumba  6 na  nyingine vyumba 4. Zote  zina  leseni  ya  makazi, gari  mpaka mlangoni, umeme  upo. Kila  moja  bei  milioni 65.


3.     Nyumba yenye geti  la  gari, vyumba 4, kimoja master, umeme, sebule, dining, jiko, stoo, na  hati miliki inauzwa. Ipo Mbagala  Kuu, bei  milioni  65.


4.     Pia  nyumba  za  milioni 65 – 70  zipo  Mbweni  na  boko.

Mawasiliano  0784482959.




DK.SHEIN KUIMARISHA SEKTA YA MICHEZO ZANZABAR

$
0
0
  
STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Zanzibar                                                                   2.10.2015
MGOMBEA nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atakapoingia madarakani katika awamu yake ya pili ya uongozi sekta ya michezo atazidi kuiimarisha.


Dk. Shein ambaye pia, ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyasema hayo katika Mkutano wa CCM wa Kampeni za uchaguzi huko Kiwani, Mkoa wa Kusini Pemba uliohudhuriwa na maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi yakiwemo makundi ya vijana.


Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa atahakikisha sekta ya michezo inaimarika zaidi katika kila nyanja ili Zanzibar irudi katika asili yake ambapo Zanzibar ilitambulikana ndani na nje ya bara la Afrika katika sekta hiyo.


Dk. Shein alisema kuwa tayari kwa upande wa Serikali Idara maalum imeshaundwa kwa ajili ya kushughulikia michezo ikiwa na lengo la kuiimarisha sekta hiyo hapa nchini.


Aidha, Dk. Shein alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha vuguvugu la michezo linaimarika sambamba na kuwapa kipaumbele wanafunzi ili nao wawe na muda wa kushiriki michezo.


Dk. Shein alisisitiza kuwa michezo kwa vijana na watoto wa skuli ina umuhimu mkubwa katika kuwajenga kiafya, kiakili pamoja na kuwajenga watoto na vijana kujenga ushirikiano, upendo na umoja miongoni mwao.


Kutokana na umuhimu huo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kwa kuwataka wazee kutowazuia watoto wao kushiriki michezo kutokana na umuhimu wake mkubwa katika maisha ya mwanaadamu.


Sambamba na hayo, Dk. Shein alisema kuwa sekta ya  michezo katika kipindi cha miaka mitano ijayo itaimarishwa kwa mujibu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka (2015-2020) ambapo Serikali itatekeleza mambo kadhaa kwa lengo la kuiimarisha sekta hiyo.


Katika uongozi wa Dk. Shein Serikali imetekeleza mambo mbali mbali katika kuimarisha sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa Sera mpya ya michezo ya Zanzibar itakayoimarisha na kuiendeleza michezo yote.


Aidha, Serikali imeanzisha mashindano ya riadha ya Wilaya, kwa Wilaya zote kumi za Zanzibar pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya michezo kwa wanariadha wa Zanzibar ili kurejesha vuguvugu la michezo ya riadha ambapo bado utaratibu wa kutoa vifaa hivyo unaendelea.


Pamoja na hayo, Serikali imewahamasisha wananchi waendeleze michezo ili wajenge afya zao kwa kufanya mazoezi ya viungo kila siku sambamba na kushiriki kwenye tamasha la mazoezi ya viungo linalofanyika tarehe 1 Januari ya kila mwaka.


Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

BEI YA MADAFU HII LEO

JAMII YAASWA KUTOKUTEGEMEA MISAADA KUTOKA NJE

$
0
0
Mwenyekiti wa Lotary Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt  katika mkutano unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.

JAMII ya watanzania wanatakiwa kutokutegemea misaada kutoka nje ya nchi  isipo kuwa tunatakiwa kujitolea  ili kusaidia jamii isiyojiweza  kwa jia ya harambee.

Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Lotary Marathon na mtoa maada, Sharmilla Bhatt katika mkutano unaofanyika kila Alhamisi ya kila mwezi unaoandaliwa na kampuni ya Solution Blocks jijini Dar es Salaam jana.

alisema kuwa jamii  na makampuni binafsi yatambue kua katika jamii huu hii tunayoiishi kuwa kuna watu ambao hawajiwezi katika mahitaji yao ya kila siku na hivyo makampuni yanaweza kuandaa harambee kutok vyanzo vya ndani kwaajili ya kuisaidia jamii inayo hitaji bila kutegemea misaada kutoka nje ya nchi.

aidha alisema kuwa Oktoba 14 ambapo ni siku ya kumbukumbumbu ya Mwalimu Julius Kamabarae  Nyerere  kutakua na matembezi ambayo yatakua na uchangiaji wa jamii.
Baadhi ya wadau waliohudhulia mkutano uliondaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikiliza mtoa maada katika hoteli ya Colesium jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 Mshiriki wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam jana akiuliza swali kwa mtoa maada. 

VODACOM YAPATA TUZO YA KUWA MWAJIRI BORA NCHINI AFRIKA YA KUSINI

$
0
0
-Inaongoza katika sekta ya mawasiliano
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imepata tuzo ya kuwa mwajiri bora katika sekta ya mawasiliano pia ipo miongoni mwa makampuni kumi bora yanayotoa ajira na kuwa na mazingira bora kwa wafanyakazi wake nchini Afrika ya Kusini kwa mwaka 2015.
Hafla ya kutangaza makampuni yanayoongoza kwa ajira nchini Afrika ya Kusini ilifanyika jana katika eneo la Gallagher Estate mjini Jahannesburg ambapo Vodacom ilitangazwa kuwa miongoni mwa makampuni 10 bora yanayoongoza katika ajira na kwa kufuata taratibu na kanuni za raslimali watu na ilitangazwa kuwa kampuni inayoongoza kwa kufuata misingi bora ya ajira katika sekta ya mawasiliano.
Tuzo ya waajiri bora ni mpango ambao uandaliwa kila mwaka na makampuni yanayoongoza kwa kufuata sheria na misingi bora ya ajira na raslimali watu hutangazwa na kupewa tuzo.
Akiongea baada ya kupata tuzo hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa raslimali watu wa Vodacom Matimba Mbungela alisema:”Tumewekeza kwa kisi kikubwa katika uendeshaji wa shughuli za raslimali watu katika kampuni yetu kuanzia teknolojia na kuweka mifumo bora inayokubalika kimataifa  ambayo inatoa mwanya kwa wafanyakazi wetu kufanya kazi katika mazingira mazuri na kampuni kuendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa”.
Mbungela alisema kuwa tuzo hii  inatoa taswira halisi ya kampuni yetu kwa kuwa kuwa mwajiri bora kunaendana sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja.
Tuzo hii imetolewa kwa Vodacom baada ya kubainika kuwa inafuata  na kutekeleza kanuni na taratibu za raslimali watu zinazokubalika kimataifa na imekuwa mstari wa mbele kuajiri wafanyakazi wazuri na kuendeleza vipaji vyao.

NDEGE YA JESHI LA MAREKANI YAANGUKA AFGHANISTAN NA KUUA 12

$
0
0
ccvv
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules iliyoanguka.ccvvb
Ramani inayoonesha eneo ambapo ndege hiyo ilipata ajali.ccvvf
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules imeanguka usiku wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Jalalabad nchini Afghanistan na kuua watu 12.
Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus ameiambia AFP kwamba watao kati ya waliokufa walikuwa wanajeshi wa Marekani, watano walikuwa raia wa kawaida na wawili walikuwa ni Waafghan.

Msemaji wa kundi la wapiganaji la Taliban, Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara inayoonesha ndege hiyo kama ilishambuliwa.

Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.

Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste kubadilishwa mapema mwaka huu.

Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.

NMB YAJIVUNIA MIAKA 10 YA MAFANIKIO

$
0
0
nmb (1)nmb (2)
Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
nmb (3)
Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.

BENKI ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita.

NMB pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini. Hii inaonesha ni jinsi gani Benki imekuwa kwa kasi na kuwa benki namba moja kwa ukubwa na faida kuliko benki nyingine yoyote nchini Tanzania.

Kwa miaka 10 pia NMB imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 7 kusaidia shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia madawati mashuleni, vifaa vya hospitali katika hospitali mbalimbali za serikali huku ikichangia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika sekta ya afya na elimu.

NMB Pia imechangia zaidi ya Bilioni 365 ndani ya miaka 5 tu fedha ambayo imechangia sana kwenye bajeti ya serikali na hivyo kutumika kwa maendeleo ya watanzania. Huo ni mchango mkubwa kuliko benki yoyote nchini. 

WASIMAMIZI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

$
0
0
 Mwanasheria wa tume ya uchaguzi Bw.Mtibora Seleman akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.
 Wanasemina wakifatilia kwa karibu mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
UCHAGUZI MKUU MAANDALIZI KANDA YA ZIWA YAENDELEA VIZURI
Na Atley Kuni- The Power of Media grew.
IMEFAHAMIKA kwamba maandalizi muhimu ya uchaguzi mkuu kwa mikoa ya kanda ya ziwa yanaendelea vizuri huku, waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mwanza na Mara wakiaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu wakati wa zoezi la mchakato kuelekea Octoba 25 mwaka huu ili kuepusha malalamiko yanayoweza kujitokeza mara baada ya uchaguzi kumalizika.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku mbili iliyo andaliwa na Tume ya taifa ya uchaguzi na kuhusisha Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi, na maafisa uchaguzi kutoka katika mikoa ya Mwanza na Mara Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Manju Msambya, amesema watumishi hao wanayo dhima ya kuhakikisha zoezi la uchaguzi linakwenda vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Msambya amesema nilazima dhamana waliopewa watumishi hao watambue  ni muhimu kwakua inakwenda kutoa mustakabali wa taifa letu na wapi tunako taka kuelekea kwa kuchagua viongozi kwa nafasi za udiwani, ubunge na urais. “Ndugu wanasemina tambueni kwamba, madhumuni ya semina hii nikuwajenge uwezo katika mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea, upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha pamoja na kutangaza matokeo ya uchaguzi” hivyo suala la umakini ni muhimu sana.
Msambya amesema, kwakutumia uzoefu walionao watumishi hao katika mazoezi mbali mbali ya kitaifa wataweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba wengi wao walishiriki katika zoezi kama hilo kwa mwaka 2010.
Awali akimkaribisha kufungua semina hiyo Mratibu wa uchaguzi wa kanda ya ziwa Deogratius Nsanzugwanko alisema tayari maandalizi kadhaa kuhusiana na uchaguzi yamekwisha kamilika ikiwapo madaftari ya mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na vifaa vyote muhimu kuwa tayari vimekwisha anza kusafirishwa kwenda kwenye mikoa husika.
Kanda ya ziwa inayoundwa na mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Simiyu na Mara, ambapo kwa mkoa wa Mwanza pekee inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,442,391 sawa na asilimia 103% ya lengo lililokuwa limewekwa hapo awali na bodi ya takwimu ya mkoa wa Mwanza ya kuandikisha wapiga kura 1,403,763.

KONGAMANO LA SABA LA ELIMU YA JUU LAENDELEA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Awadh Mawenya, ambaye ni mgeni rasmi katika kongamano la saba la elimu ya juu linalofanyika jijini Arusha akiongea machache mara baada ya kumaliza kutoa mada. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
Washiriki wakiwa katika picha za pamoja.

SSRA YATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI (TUCTA) MKOANI DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 

Mbali na hilo, waajiri wa metakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao, kujiunga na mfuko wasio upenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza. 

Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa. 

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.

DIANA CHILOLO AMFUNGUKIA LOWASSA KWA TUNDULISU MJINI IKUNGI MKOANI SINGIDA

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI SINGIDA,KESHO KUUNGURUMA SINGIDA MJINI LIVE

$
0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 

Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.
 Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
Wananchi  wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo.

PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images