Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

NATHAN MPANGALA ‘KIJASTI’ KUWEKA WAZI MAISHA YAKE YA UCHORAJI VIBONZO KESHO

$
0
0
 Mchoraji wa  vibonzo maarufu nchini Tanzania, Nathan Mpangala.

MCHORAJI  wa vibonzo maarufu nchini Tanzania, Nathan Mpangala, ameandaa mazungumzo ya wazi yatakayofanyika katika Viwanja vya Nafasi Art Space, Mikocheni, Jijini Dar es Salaam, kesho (Ijumaa) ambapo atazungumzia maisha aliyopitia katika vyombo mbalimbali vya habari akiwa kama mchoraji vibonzo.

Ili kunogesha tukio hilo, nao wahudhuriaji watapata nafasi ya kuuliza maswali au kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali atakayogusia.

Mazungumzo hayo yana malengo makuu matatu;

(i)             Kueleza maisha ailiyopitia kama mchora vibonzo.
(ii)           Kukutana ana kwa ana na ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wake wa vibonzo kwa ajili ya kufahamiana zaidi.
(iii)          Darasa huru kwa wachora vibonzo wanaochipukia kusikia maisha aliyopitia ili kuwatia moyo wafike alipofikia au kupita.

Mazungumzo hayo ambayo hayatakuwa na kiingilio yataanza saa 10 alasiri ambapo watu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

Wakati huohuo, Mpangala ametoa rai kwa wachoraji vibonzo wote hasa waishio Dar es Salaam, wakongwe na chipukizi kuhakikisha wanahudhuria tukio hilo kwani ni fursa nzuri ya kubadilisha mawazo na kusemea taaluma yao.

Kwa maelezo zaidi 0713 262 902.

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAWAKALA WA FORODHA TANZANIA WAJIUNGA NA PSPF

$
0
0
 KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Florence Turuka, akihutubia wanachama wa chama cha mawakala wa forodha Tanzania (TAFFA), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa TAFA kwenye ukumbi wa Karimjee .
 Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin, akiwaeleza wanachama wa Chama cha mawakala wa forodha Tanzania TAFA, juu ya hufuma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa TAFFA jijini Dar es Salaam. PSPF na TAFFA wamefungua ukurasa mpya wa mahusiano ambapo wanachama kadhaa wa TAFA walijiunga na Mfuko huo
 Viongozi wakuu wa TAFFA, wakionyesha kadi za uanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari kwenye Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSS), baada ya kukuunga wakati wa mkutan o mkuu wa mwaka wa TAFFA. Kulia ni Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselem, Meneja Masoko, Mawasilioano na Uenezi, Costantina Martin (wapili kushoto) na meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Mwanjaa sembe
Baadhi ya wanachama wa TAFFA wakiwa kwenye mkutano huo.

MAWAKALA WA UTALII WA KIMATAIFA KUHUDHURIA ONYESHO LA S!TE 2015

$
0
0
Kundi la Mawakala wa utalii kutoka nchi mbalimbali limewasili jana jijini Dar es Salaam likitokea visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya kushiriki onesho la kimataifa la Utalii lijulikanalo kama “Swahili International Tourism Expo”. 
Onesho hili litafanyika kuanzia leo Oktoba 1 – 3, 2015 Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Mawakala hawa wanaojihusisha na kutoa huduma mbalimbali za utalii katika nchi zao, wamepata mualiko huu wa kuhudhuria onyesho la S!TE ili kuwapa nafasi ya kuvijuwa vivutio vya utalii vya Tanzania waweze kuwahamashisha watalii katika nchi hizo kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. 
Aidha, onyesho ili linatoa fursa kwa Mawakala wa Utalii wa Tanzania kuweza kufanya biashara na mawakala hao kutoka katika nchi mbalimbali duniani; Canada, Marekani, Ujerumani, India Ireland, Israel, China, Ethiopia,Uingereza, Australia na Afrika ya kusini. 
Wadau wa utalii wa kimataifa wamepata fursa ya kuvitembelea vivutio vya utalii vya viziwa vya Zanzibar na baada ya maonesho watatembelea Hifadhi za Taifa za Tarangire, Manyara na Bonde la Hifadhi la Ngorongoro. 
Onesho la S!TE limetayarishwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Pure Grit ya Afrika ya Kusini. Onesho la kwanza lilifanyika tarehe 1-4, October, 2014, Mlimani City, Dar es Salaam.
 Mawakala wakiwasili katika bandari ya Dar es Salaam wakitoka visiwa vya Zanzibar.

 Mawakala wakipata historia ya sehemu  ilipokuwa ikifanyika  biashara ya Utumwa Zanzibar.

1Mawakala wa utalii wakiingia katika kanisa la kihistoria “The Anglican Cathedral's Zanzibar.

BI. SAMIA SULUHU AAHIDI NEEMA KWA WAKAZI WA MUSOMA MKUTANO WA KAMPENI...!

$
0
0

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.
 Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.
Kulia ni baadhi ya wasanii maharufu wa uigizaji wakishangilia wakati Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Mwisenge.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie na wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

AIRTEL YATOA GAWIO LA TSHS BILIONI 5.3 KWA WATEJA WA AIRTEL MONEY

$
0
0

Meneja biashara wa kitengo cha  Airtel Money,  Bwn Asupya Naligingwa
(kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Airtel
kugawa gawio la faida la zaidi ya  shilingi billion 5 kwa wateja na
mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima.  Pichani
ni Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Bi Jane Matinde

KAMPUNI ya simu za mkononi
ya Airtel leo imetangaza kugawa zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa wateja
na mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money nchi nzima

Uamuzi huo wa kutoa gawio la faida lililopo katika akaunti  ya
udhamini ya wateja wa Airtel Money (Trust account)  litawawezesha
wateja wa Airtel kulipwa kiwango kizuri cha gawio la faida.  Kiwango
hiki cha pesa kitalipwa kutokana na  kiasi cha pesa mteja alichokuwa
nacho kwenye akaunti yake ya Airtel Money kila mwisho wa siku  kuanzia
March 2014 hadi April 2015.

Akiongea na waandishi wa habari,Meneja wa kitengo cha  Airtel Money,
Asupya Nalingigwa, alisema wanayo furaha kutangaza mgawanyo  huu wa
gawio la faida kwa wateja wao baada ya benki kuu ya Tanzania.
Kuidhinisha kutoa  pesa hizi katika akaunti ya udhamini ya pesa za
wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama trust  account.

Aliongeza kwa kusema wateja wa Airtel Money watapata sehemu ya gawio
lao  kulingana na salio wanalokuwa nalo kwenye akaunti zao kila siku

"Tunaamini kiasi hiki cha pesa kitachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuboresha maisha ya watanzania wengi , kuwahamasisha wateja
wasiofikiwa na huduma za kibenki kutumia mfumowa pesa kwa njia ya
simu.Vilevile wateja wetu wa Airtel Money wataendelea kutumia huduma
za pesa kupitia simu za mkononi, kufanya miamala yao ya kila siku na
kutunza pesa zao ili kupata gawio lao kila watakapo weka pesa katika
akaunti zao za Airtel Money". Aliongeza Nalingigwa

Uamuzi huu wa kutoa gawio la faida kwa wateja ni wakuungwa mkono kwani
unachochea na kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za
mkononi , ukizingatia takribani asilimia 85% ya watanzania bado
hawajafikia na huduma za kibenki

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za kibunifu  za
kifedha kupitia simu za mkononi ikwemo NFC huduma inayokuwezesha
kufanya malipo kupitia kadi, Mikopo ya Timiza na huduma nyingine
nyingi.

Katika  maelezo yake Naligingwa aliahidi  Airtel kuendelea na dhamira
yake ya kuzindua huduma bora na za kisasa katika mienzi ijayo ili
kuwanufaisha watanzania waishio maeneo ya mijini na vijijini.

PRESIDENT KIKWETE CALL UPON ADVANCED NATIONS TO CURB MARKET FOR ILLEGAL WILDLIFE PRODUCTS.

$
0
0
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during the International Conservation Caucus Foundation(ICCF) gala in New York's Harvard Club whereby he called upon advanced nations to curb the sale of illegally acquired wildlife products in their countries as a way of combating poaching and illegal wildlife trade in Africa.
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks with Malawi's President Professor Peter Mutharika during the ICCF Gala held at Harvard Club in New York.
 The ICCF is an umbrella organization that works to advance conservation governance by building political support, providing on the ground solutions and applying  a natural resource  wealth management framework to sustainably develop and manage the earth's natural resources
The Minister for Natural Resources and Tourism Hon.Lazaro Nyalandu Left and The Permanent Secretary in the Ministry Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata Mulamula escorts President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete out of the Harvard Club in New York shortly after the President attended a gala organized by the ICCF group
(photos by Freddy Maro)

GERMANY COMMITS 37 MILLION EUROS TO SUPPORT REGIONAL INTEGRATION IN EAST AFRICA

$
0
0

  Head of the German delegation Mr. Georg Rademacher and the EAC Deputy Secretary General in charge Finance and Administration, Mr. Liberat Mfumukeko signs the bilateral agreement.
The EAC team(on the right side) led by Deputy Secretary General in charge Finance and Administration, Mr Mr. Liberat Mfumukeko and the The Federal Republic of Germany team during the negotiations.

EAST African Community Headquarters, Arusha, 1 October, 2015The Federal Republic of Germany and the East African Community (EAC) have successfully concluded bilateral negotiations on development cooperation at the EAC Headquarters in Arusha,Tanzania. 

The Federal Republic of Germany committed a total of 37 million euros in grants to the EAC for 2016-2018, highlightingthe strong commitment to support the integration process in East Africa.   

·         10 million euro in financial assistance will be invested in the establishment of a regional network of reference laboratories for communicable diseases. With this project, the German Government responds to a request for support from the EAC for the prevention and control of epidemic outbreaks in the region. 

RAIS KIKWETE KUENDESHA MKUTANO WA TISA WA TNBC KESHO

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuendesha kikao cha 9 cha Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kesho jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kitaangalia jinsi ya kutekeleza kwa haraka maazimio ya mkutano wa 8 wa baraza hilo hasa katika kuimarisha mazingira ya biashara na kujenga sekta bora zaidi ya utalii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na TNBC, mkutano huo utahusisha mawaziri, makatibu wakuu, wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali.

“Mkutano huu utaangalia njia na suluhisho madhubuti za kuimarisha mazingira ya biashara kama kurahisisha njia za udhibiti na kutumia intaneti kutoa huduma za kiserikali na biashara,” ilisomeka taarifa hiyo.

Mkutano huo utazingatia mafunzo na uzoefu wa mikutano iliyopita.

TNBC chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete ni chombo kinachotoa mwanya kwa sekta binafsi na umma kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kuifanya Tanzania kuwa sehemu bora ya kufanya biashara na hivyo kuimarisha uchumi.

TNBC pia inaendesha mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya nchini yanayosimamiwa na wakuu wa mikoa na wilaya husika.

“Tangu kuanza kuongoza chombo hiki kama Mwenyekiti Desemba 2005, Rais Kikwete amefanikiwa kusaidia Baraza kufikia malengo yake kwa kiwango kikubwa,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, jambo hilo limeifanya TNBC kuwa uwanja maalum nchini wa kuibua mijadala ya kisera, tafiti na ushauri kwa sekta za umma na binafsi.

Mkutano wa mwisho wa TNBC ulifanyika mwanzoni mwa mwezi uliopita.

JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 IJUMAA OCTOBER 2, 2015

NEC:UTAPIGA KURA KWA KALAMU YOYOTE UTAKAYOITAKA

$
0
0

 
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva 

 Ili kuondoa shaka miongoni mwa wananchi kutokana na tetesi zinazosambazwa juu ya ubora wa kalamu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kila mtu anaruhusiwa kuja na kalamu yake kupigia kura Oktoba 25, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo na NEC wakati ilipofanya mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini ikiwa ni siku ya tatu ya kukamilisha utaratibu wa kuzungumza na wadau wa uchaguzi baada ya kufanya hivyo kwa wawakilishi wa walemavu na wamiliki wa vyombo vya habari nchini.
Akisisitiza juu ya ushiriki wa wadau kutoa elimu ya mpiga kura, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva amesema kipindi hiki cha kampeni kimeshuhudia kuzuka kwa maneno mengi yasiyokuwa na uhakika ambayo yanawachanganya wananchi.
“Kalamu yoyote inaruhusiwa kupigia kura hivyo watu wasiogope kwenda na kalamu zao ila wasiokuwa nazo watatumia zetu tulizoziandaa. Hazifutiki kama inavyosemwa huko mitaani,” amesema Jaji Lubuva.
Ametumia nafasi hiyo pia kubainisha mkakati wa kuzuia uwezekano wowote wa wizi wa kura kama inavyosemwa na baadhi ya wagombea na viongozi wa vyama vya siasa na kutoa wito kwa mtu au taasisi yoyote inayoona mwanya wa hilo kujitokeza ili hatua stahiki zichukuliwe.
Vile vile amewataka wanasiasa wote kuachana na maneno machafu wawapo majukwaani pamoja na kushambulia tume hiyo au baina ya wenyewe kwa wenyewe na badala yake wajikite kwenye kunadi sera zao.
“Tunaumizwa sana na matumizi ya maneno kama ‘tume inaandaa bao la mkono’ kwenye vyombo vyenu. Hakutakuwa na wizi na sisi tunaamini ushindi utatokana na wingi wa kura alizopata mgombea husika,” amesema na kuongeza:
“Kama chama cha siasa kimeishiwa sera za kunadi kwa wananchi basi ni vyema kikampumzisha mgombea wake na kusubiri siku ya uchaguzi badala ya kutoa lugha zisizofaa. Matumizi ya kauli za matusi, dhihaka au kejeli dhihi ya wagombea wengine ni kinyume na maadili ya uchaguzi. Hata kuituhumu tume bila kutoa ushahidi siyo jambo jema na kutowatendea haki wananchi.”
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hizo baada ya kupata michango kutoka kwa wahariri waliomueleza changamoto walizonazo katika kuruhusu matumizi ya baadhi ya maneno yanayotolewa majukwaani.

MAISHA MAGIC BONGO IMEFIKA! CHANELI MPYA INAYOZINDULIWA NA M-NET KUWALENGA WATANZANIA.

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa burudani barani Afrika, M-Net inazindua chaneli mpya yenye  kulenga watanzania, itakayokuwa na burudani mbali mbali zenye hadhi ya Kitanzania,  ni  MAISHA MAGIC BONGO itakayoanza kuonekana hewani Octoba 1 saa 10 Alasiri.   Moja ya madhumuni ya M-Net ni kuhakikisha inalifikia soko la wateja wake ikiwemo kuingiza maudhui wanayopenda wateja wake. Chaneli hii mpya inategemea kukidhi mahitaji ya soko la wateja wa Tanzania. 
Ikihusisha vipindi zaidi ya 6 vitakavyokuwa vikiruka kila siku, MAISHA MAGIC BONGO itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Afrika Mashariki  kupitia chaneli 160.  Mbali na kuonyesha filamu kali kutoka Bongo Muvi na tamthilia za Kiswahili zinazopendwa na kufatiliwa nchi nzima, chaneli hii pia itakuwa ikionyesha vipindi vya maisha ya wa Tanzania,  Muziki ukiwemo Bongo Flava , Maisha ya Mastaa na vipindi vya majadiliano ya moja kwa moja , bila kusahau sinema kali za kihindi kutoka Bollywood zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. 
Akizungumza juu ya uzinduzi wa 'MAISHA MAGIC BONGO, Mkurugenzi wa M-Net kwa Afrika Mashariki Theo Erasmus anasema, " Tumefurahi kufunua mkondo huu mpya na kwa kuendelea mbele tunatarajia chaneli hii itakuwa moja ya chaneli pendwa zaidi Tanzania kwa msaada wa watazamaji wetu wa Tanzania ambao daima wamekuwa waaminifu kwetu na ndio sababu M-Net leo tumeamua kuwaletea chaneli hii mahususi kwa ajili yao.

Tunashukuru zaidi tumeweza. 
kupata baadhi ya vipindi bora kutoka kwa wazalishaji wakubwa kutoka ndani ambao wanashirikiana nasi, pia tunaangalia namna ya kupanua ushirikiano wetu zaidi na wazalishaji hawa wa filamu na vipindi vya runinga ili kuhakikisha kwamba mafanikio yao yanakuwa makubwa zaidi.


Ni mwezi sasa, tangu DStv ilipotangaza kwenye maonyesho ya maudhui nchini Mauritius, MAISHA MAGIC BONGO ipo tayari kuzinduliwa, na baadhi ya vipindi vitakavyokuwemo kwenye chaneli hii ni: 
  • Filamu za kibongo zitaonyeshwa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 17:00 jioni, pia Jumamosi na Jumapili saa 19:30 usiku.  Wakati huo huo Filamu za kihindi zilizotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili zitakuwa zinaonyeshwa kila siku ya Ijumaa saa 19:30 usiku. Baadhi ya Bongo Muvi maarufu zilizopo kwenye ratiba sasa ni Hard Price, Jimmy, Nampenda Motika na Nusra, na baadhi ya za kihindi ni I am 24, Jimmy, Anwar na Amar Akbar Anthony.

 Upande wa Tamthilia , jiandae kupata Talaka ( Jumanne saa 19:00 usiku ), usikose Mtaro ( Jumatatu saa 19:00 usiku)  Isiyopitwa na muda Siri ya Mtungi ( Jumamosi na Jumapili saa 18:00) na  ya vijana zaidi  Dunia Tambara Bovu ( Ijumaa saa 19:00 usiku). Wasanii wenye vipaji  waliopo kwenye tamthilia hizi ni kama vile Hamis Korongo , Alafa Arobain , Paulo Francis, Juma Rajab Rashid, Hidaya Maeda, Daudi Michael, Caroline Hussein na Habibu Seif  na wengine wengi, hakika hii si ya kukosa! 
  • Bila shaka, MAISHA MAGIC BONGO pia itakuletea vipindi viwili vya muziki, Mzooka (Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 Alasiri) itakupa burudani ya video mpya kali kutoka Bongo, wakati kipindi cha Sifa Mix kitakuwa kikikujia ( kila Jumapili saa  11:00 asubuhi) ikikuletea muziki laini wa nyimbo za Dini. 
  • Pia kuna vipindi majadiliano  utaviona kwenye chaneli hii, kama vile Mkasi ( kila Jumapili saa 16:00 EAT ) ambazo inazungumzia maisha ya wasanii wakubwa Tanzania,  kisha hakikisha hauachi kumfuatilia  Mboni (Jumamosi saa 15:00 EAT) Mboni Masimba  akifanya mahojiano  na watu mashuhuri , wajasiriamali, viongozi wa jamii na siasa ,  kujadili mada mbalimbali kuanzia utamaduni wa kiuchumi. 
  • Pia kwenye MAISHA MAGIC BONGO, usikose kuangalia kipindi cha Ajabu, kinachoburudisha na wakati mwingine kuogopesha lakini muda wote kitakuburudisha (Jumatano saa 19:00 Usiku). 
  • Kwa kusherehekea uzinduzi wa Maisha Magic Bongo, DStv inafurahi kuwatangazia punguzo la bei kwenye vifaa vyake kuanzia tarehe 1 Oktoba 2015. Vifaa vya DStv sasa vitapatikana kwa Tshs 79,000 tu, vigezo na masharti kuzingatiwa.
Hii ni kuwawezesha waTanzania kuangalia chaneli mpya ya Maisha Magic Bongo itakayopatikana kwenye vifurushi vyote, ikiwemo kifurushi cha Bomba ambacho ni Tshs 23,500 tu kwa mwezi.



Hivi pamoja na vingine kibao ambavyo si vya kukosa kwenye  chaneli hii mpya,  hakikisha unaangalia MAISHA MAGIC BONGO kuanzia usiku wa leo! Tembelea tovuti www.maishamagic.tv kwa maelezo zaidi.

Nacte yatoa taratibu za uendeshaji wa mafunzo ya ufundi nchini

$
0
0
Kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Adolf Rutayuga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari hawapo (pichani) wakati alipokuwa akiongea nao makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo Mikocheni  jijini Dar es Salaam, kuhusiana na  maamuzi mbalimbali yaliyofanywa  na baraza hilo katika kuratibu uendeshaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi na ufuatiliaji wa Ubora wa Mafunzo wa (NACTE) Agnes Ponera na Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa  Baraza hilo ,Alex Nkondola. 
Waandishi wa habari wakimsikiliza  Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Adolf  Rutayuga wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam,juu ya maamuzi mbalimbali yaliyofanywa na  baraza hilo katika kuratibu uendeshaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. 

Loading.....

TANZANIA TUNA MIGODI YA THAMANI KULIKO DHAHABU NA GESI - SEHEMU YA KWANZA

Wafanyakazi watakiwa kufuatilia makato yao

$
0
0


Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao. 
Mbali na hilo, waajiri wa mmetakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao kujiunga na mfuko wasioupenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza. 
Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA, Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa. 
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.

MFUKO WA BIMA(NHIF) YA KIGOMA WAWAKUMBUKA WAZEE LEO KATIKA SIKU YAO.

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya NHIF kigoma wakikabidhi msaada wa vyakula kwa uongozi wa kituo cha Silabu cha kulelea wazee wasiojiweza ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
 Meneja wa Mfuko wa bima NHIF  ya kigoma akisalimiana na wazee wanaotunzwa katika kambi ya Silabu kata ya kibirizi
Baadhi ya wazee wasiojiweza wanaoishi na kutunzwa katika kambi ya kulea wazee ya Silabu kata ya Kibirizi Mkoani hapa


 

Na Editha Karlo.Kigoma
MFUKO wa Bima ya afya (NHIF)wametoa msaada wa  vyakula kwa wazee wasiojiweza uliopo katika kituo cha silabu kata ya kibirizi mjini hapa.


Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo wa chakula Meneja wa Mkoa wa mfuko huo Elius Odhiambo alisema kuwa mfuko unatumbua umuhimu na mchango wa wazee kwa jamii.


"Sisi kama mfuko wa bima ya afya tuna thamini sana na kutambua mchango wenu wazee kwa jamii kwani kila mmoja wetu ni mzee mtarajiwa"alisema odhiambo


Alisema wamekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya shilingi milioni moja na elfu sitini,vyakula walivyotoa ni mchele kilo 100,sukari kilo 100,unga wa ugali kilo 100,maharage kilo 100 na mafuta ya kupikia kilo 20


Meneja huyo alisema wataendelea kusaidiana na kuwasaidia wazee hao kila inapobidi.


Naye mkuu wa kituo hicho cha kutunzia wazee Juma Ndikamukana wasiojiweza aliushukuru mfuko wa bima ya afya kwa msaada wao huo na kuwakumbuka wazee katika siku yao leo.


Alisema kituo hicho kina jumla ya wazee 51 wasiojiweza wanaotunzwa wanaotoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa 

Kigoma

STOP PRESS: Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea taarifa za kuwepo Mahujaji wawili kutoka Tanzania ambao wamelazwa katika mojawapo ya hospitali nchini Saudi Arabia baada ya kujeruhiwa kutokana na tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah, tarehe 24 Septemba, 2015.


Mahujaji hao ambao wanaendelea kupata matibabu na hali zao zikiendelea vizuri ni Bi. Hidaya Mchomvu na Bi. Mahjabin Taslim Khan. 
Pia kwa mujibu wa taarifa za Ubalozi Hujaji mwingine anayejulikana kwa jina la Mustafa Ali Mchira amelazwa katika Hospitali ya Ansari Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Taarifa zinaeleza kuwa Bw. Mchira alipata ugonjwa tangu alipowasili Saudi Arabia na hivyo ugonjwa wake hauhusiani na ajali iliyotokea tarehe 24 Septemba, 2015. 
Vilevile, Serikali ya Saudi Arabia imeanza kutoa taarifa za alama za vidole za Mahujaji waliopata ajali. Hivyo, Ubalozi unazipitia na kuzihakiki taarifa hizo ambazo zitasaidia kuwabaini Mahujaji wetu waliokufa katika ajali hiyo. 
Kutambulika kwa Mahujaji hao waliolazwa, kunatokana na jitihada zilizofanywa na Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na Vikundi vya Mahujaji za kutembelea Hospitali zote zilizopo Makkah, Mina, Arafat, Muzdalifa, Jeddah na Taif kwa ajili ya kuwatafuta Mahujaji wa Tanzania waliofariki dunia au kulazwa katika hospitali hizo. 
Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam


01 Oktoba, 2015

STOP PRESS: HUKUMU YA RUFAA YA MRAMBA NA YONA KESHO

$
0
0
Mawaziri  wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona siku walipohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka Mwezi Julai mwaka huu. Picha ya maktaba
Na Mwene Said wa 
Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.
 MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kesho imepanga kutoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri  wa zamani, Bazil Mramba na Daniel Yona waliohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka. 
Mapema Agosti 5, mwaka huu mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Projest Rugazia iliagiza pande zote mbili kuwasilisha hoja za kusikiliza rufaa hizo kwa njia ya maandishi. 
Upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja, kwamba ushahidi uliotolewa haukuthibitisha makosa dhidi ya tuhuma za  matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
 Kadhalika, Mramba na Yona walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yao na jaji alipanga kutoa hukumu Septemba 18, mwaka huu lakini alipata maradhi akaahirisha hadi leo. 
Jaji Rugazia atasoma hukumu ya kuwaachia ama kukazia hukumu ya Mahakama ya Kisutu kesho. 
Wafungwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya makosa ya kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation kwa ajili  ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.

MCHAKAMCHAKA WA MWIGULU NCHEMBA WATUA SIMANJIRO,KONDOA NA KITETO,CCM YAENDELEA KUUNGWA MKONO KWA KISHINDO

$
0
0
Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba akiwasili Jimbo la Simanjiro na kupokelewa na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo Ndg.Ole Sendeka mapema hii leo.Mwigulu Nchemba akimnadi Ole sendeka kwa wananchi wake,Kubwa ni Ujasiri wa Ole sendeka kwenye kutetea maslahi ya taifa,Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kama barabara zinazokwenda kujengwa kwa kiwango cha rami kuunganisha na mikoa inayopakana na SImanjiro.Ole Sendeka akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Engesbert kuhusu Ilani ya CCM na maendeleo ya Jimbo la SImanjiro.Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Simanjiro linakwenda kujengwa barabara za Rami Zaidi ya Tatu za kutoka Arusha,Mererani na Dodoma na ile ya Babati kwenda Simanjiro.
Mbali na hilo,Uboreshaji wa Mfumo wa majini na Uchimbaji wa Visima ndio kipaumbele cha kwanza kwa Ole sendeka kwa Wananchi wa Simanjiro.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata ya Namalulu Jimbo la Simanjiro.Twende na Magufuli popote alipo.Wananchi wa kata ya Namalulu wakionesha Umoja wao kuichagua CCM kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na Urais katika Uchaguzi wa October 25 Mwaka huu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

VYAMA VITANO VIMEKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMZIA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU Part 1

$
0
0
Viongozi wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015 Tamko hili ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.
2. Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.
3. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea. 4.Viongozi wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na sio madhabahu. 5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6. Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.
7. Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images