Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 992 | 993 | (Page 994) | 995 | 996 | .... | 3272 | newer

  0 0

  DSC_0316
  CEO wa Kampuni ya MeTL Group, 
  Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.

  Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.
  Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.
  Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
  Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
  Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.
  DSC_0310
  Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:
  “Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .
  Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.
  Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
  MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.

  0 0

  Katika hali isiyotarajiwa  na wengi katika Jimbo la Moshi Mjini, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Davis Mosha ameanza utekelezaji wa ahadi zake katika Jimbo hilo,  wiki chache baada ya kuzungumza na wanamuziki na wasanii kuhusu kazi zao na wasanii hao kuomba kupata kituo cha Redio cha kisasa na Studio ya kisasa ambavyo vitaweza kufanya kazi zao kwa ubora zaidi na pia kufika mbali.
  Katika kutekeleza hilo Mh. Davis Mosha amekwishaanza ujenzi wa Studio ya Kisasa ya Kituo cha Redio chini ya Kampuni yake ya Africa Swahili Media na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema na vifaa vya Studio huyo vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutoka Dar es Salaam baada ya kuwasili Bandarini vikitokea Nchini Italy. Mh. Davis Mosha aliwaahidi wasanii hao kufungua kituo cha Redio kitakachoweza kusikika Tanzania Nzima na Duniani kote kwa njia ya Satelite. Pia aliwahakikishia kufungua na kituo cha televisheni. Kituo hicho cha Redio na Studio ya kisasa kianatarajiwa kufunguliwa katika jingo la Kilimanjaro Commercial Complex Maarufu kama jengo jipya la NSSF lililopo Moshi Mjini.
  Mbali na utekelezaji huo wa Kero ya Wasanii, Mh. Davis Elisa Mosha wiki iliyopita aliweza kufanya Ziara ya kimya kimya katika Soko la Mitumba la King George Memorial na kutazama Changamoto za Soko hilo lakini pia alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa Soko hilo na wafanyabiashara wa Soko hilo. Kwa pamoja walieleza MAzingira magumu wanayofanyia Biashara huku ikiwa Miundombinu mibovu ikiwemo vyoo na Soko halina Paa inapelelea iwapo mvua itanyesha basi kunakua hakuna biashara kabisa maana Bidhaa hunyeshwa na Mvua na mbali na Mvua pia jua ni lao. Katika kutatua changamoto hizo Davis Mosha aliwaahidi kulifanyia kazi mapema tatizo lao na hatosubiri mpaka muda wa uchaguzi ufike maana adha hiyo wanayoipata ni wananchi wa Moshi wakiwemo mama zake na baba zake waliopo hapo Sokoni. 
  Kutokana na Ahadi hiyo Jana Mh. Mosha aliwasili Sokoni hapo na Mainjinia kutoka Kampuni ya Group Six ltd ambao ni Raia wa China   kwa lengo la kufanya kufanya vipimo na Michoro ya uboreahwaji wa Soko hilo ili kuweza kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Soko hilo. Mainjinia hao walizunguka katika Soko hilo na kutazama eneo la Soko ili kuweka mipango ya kuanza ujenzi wa Soko hilo ambapo ujenzi huo hautoathiri wafanyabashara hao kuendelea kufanya biashara zao.


  Mh. Davis Elisa Mosha
    
  Hati ya Kontena la Vifaa vya Studio lililotoka Italy Baada ya kuingia Bandari ya jiji la Dar es Salaam.
  Mh. Davis Mosha alipotembelea Soko la Mitumba la Memorial na kujionea changamoto mbalimbali.


  Mh. Davis Mosha akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Memoria alipotembelea soko hilo.

  0 0

  Msigwa na wengine 62 mbaroni Mkoani Iringa .Fahamu kilichojiri katika nyanja za siasa kama yasemavyo magazeti ya leo;  https://youtu.be/yt0b6QW10-c

   Simba yamshitaki Donald Ngoma. Viti  vyaizuia Yanga kufanya mazoezi katika uwanja wa Jamuhuri,   https://youtu.be/mDzS67eL7wE

   NEC yapiga marufuku kusafirisha masanduku ya kura.Rais mpya kujulikana ndani ya masaa 72 tu; https://youtu.be/updRyyX0WSg

  Magufuli asisitiza kufa na mafisadi.Siri ya Lowasa kuhairisha mkutano Tanga yawekwa wazi, Lowasa asimamishwa na wakazi wa Muheza akiwa safarini kuelekea Dar; https://youtu.be/D3v9n1X91iM  0 0

   Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akizungumza wakati akinadi sera za chama Cha Mapinduzi,CCM  mbele ya wanaCCM wa mtaa wa Kisiwani, Kata ya  Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam na kuaidi kuwa endapo atachaguliwa kurudi katika kiti chake kuwa atatatua tatizo la maji linalowakabili wananchi wa kata hiyo.
    Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kinondoni, Marry Kalisinje wakati  wakati mbunge wa Kinondoni akinadi sera zake katika  mtaa wa Kisiwani, mtaa wa Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam. 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne amelihutubia kwa mara ya mwisho Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mtaifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
   Hotuba ya Mhe. Rais na ambayo iligusia mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, na maendeleo akitumia pia fursa hiyo kuwaanga viongozi wenzie na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake, iliwasisimua wajumbe wa mkutano huo kiasi cha kukatishwa mara kwa mara kwa makofi. 
   Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazomwonyesha Mhe. Rais katika Matukio mbalimbali Moja wapo likiwa ni hafla ambayo Rais wa Marekani, Mhe Barack Obama aliiandaa kwaajili wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Picha kwa hisani ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na   Mhe.Barack Obama na Mkewe  Michelle  Obama wakati wa hafla  ilioandaliwa na  Rais wa Marekani kwaajii ya   Viongozi wa Wakuu  Nchi na Serikali wanaohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ( Picha hii ni kwa hisani ya  Ofisi ya Itifaki ya White House)
   Mhe. Rais Kikwete akiwa na  Mhe. Sophia Simba, Katibu Mkuu  Balozi  Liberata Mulamula na mwanamitindo  Flaviana Matata muda mfupi mara baada ya kulihutubia  Baraza Kuu la  70 la Umoja wa Mataifa
   Mwakilishi wa Kudumu wa  Antigua na Bermuda  Balozi  Walton Alfonso Webson ambaye ni  mlemavu wa kutoona   akimwongoza Mhe. Rais Kikwete kwenda kuonana na   Waziri Mkuu wake, Mhe. Gaston Alphoso Browne aliyekuwa na mazungumzo wa Mhe.Rais mara baada ya Mhe. Rais kulihutubia  Baraza  Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa.
   Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na  Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Mhe. Gaston Alphonso Browne,  wengine katika mazungumzo hayo ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako  Manongi,  Mwakilishi wa kudumu wa Antigua na Barbuda, Balozi Walton  Webson mwenye miwani myeusi na Mkurungezi wa  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi  Celestin Mushy
  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu,Damian Lubuva akizungumza na wamiliki  wa vyombo vya habari (hawapo pichani) jinsi ya tume hiyo inavyofanya kazi kuelekea uchagauzi Mkuu katika mkutano ulifanyika leo katika Ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dk.Reginard Mengi akichangia maada katika mkutano wa Wamiliki na Vyombo vya habari  uliotishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Waamiliki wa Vyombo na waandishi habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu ,Damiani Lubuva (hayupo pichani)katika mkutano uliotoshwa na tume hiyo kuelekea uchagauzi Mkuu uliofanyaika leo jijini Dar es Salaam, 
  (picha na Emmanuel Massaka)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 alipofika kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi. Picha na OMR

  0 0

  Bw . Hassan Mtenga Katibu wa Ccm Mkoa wa Iringa

  CHAMA cha mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Iringa kimelaani  shambulio lililofanywa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) kwa wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli juzi.

  Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw.Hassan Mtenga aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa chama chake kinawapa pole wananchi waliopigwa na wafuasi hao wa Chadema waliotumwa na Mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.

  Mtenga alisema kuwa idadi kubwa ya waliopigwa fimbo ni wanawake kuwa tukio hilo haliungwi mkono na udhalilishaji mkubwa kwa wanawake hao 

  Hata hivyo alisema kuwa vitendo hivyo vya Mchungaji Msigwa kutumia vijana kupiga wananchi na wanachama wa CCM havivumiliki na kuwa iwapo Mchungaji huyo akiendelea na vitendo hivyo na kukimbia Kama ilivyokawaida yake sasa atambue wazi kuwa watamkamata na kumkapeleka polisi.

  " Upole Wetu CCM ndio ambao umemfanya Mchungaji msigwa kuendelea kuwafanyia vurugu wanachama wetu ila kwa sasa tutajitolea kumkamata anaewatuma vijana hao kupiga wananchi"

  Alisema hadi sasa zaidi ya wana CCM 7 katika jimbo la Iringa Mjini wamevamiwa na kupigwa na wafuasi hao wa Chadema ambao wahifadhiwa katika Gesti ya Sambala na nyingine hapa Mjini .

  Akielezea kuhusu lugha za matusi anazozitoa Mchungaji Msigwa kwa Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Iringa Mjini Bw Frederick Mwakalebela alisema ni dalili za kuanguka kwa mchungaji Msigwa katika uchaguzi mkuu 

  Kwani alisema Kama angekuwa ni mbunge aliyewatumikia vema wananchi kwa kutimiza ahadi zake asingekuwa anatumia muda mwingi kutukana badala ya kueleza wananchi nini amefanya kwa miaka mitano .

  Hivyo alisema kuwa iwapo Mchungaji Msigwa angekuwa na uwezo basi angesimama jukwaani kujibu zilipo Pesa za mfuko wa jimbo na kiasi cha tsh milioni 340 alizopewa na Mgombea Urais wa Chadema Edward Lowasa .

  Mtenga alisema ushindi wa Mwakalebela jimbo la Iringa Mjini upo wazi kabisa na kuwa katika Mkoa wa Iringa kwa uchaguzi huu hakuna jimbo litakalokwenda upinzani.


  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
       Na Jamiimojablog.
         Watu watano wamefariki dunia   Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
         
           Katika tukio la kwanza gari  lenye namba za usajili  T.519 Akh aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva  asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili  T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.

        Ajali hiyo imetokea Septemba  29 majira ya  Saa 4 usiku katika eneo la  Nane-Nane, Kata Ya Isyesye,  barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .

          Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha  pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja  ambao walikuwa wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.

         Aidha Katika ajali hiyo  Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye  Haice alijeruhiwa na amelazwa katika   Hospitali ya Rufaa Mbeya. 

            Kwa mujibu  wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi  amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.

         Amesema  dereva wa hiace alikimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka zikiendelea kufanyika na jeshi hilo miili ya  marehemu imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Mbeya.

          Katika tukio jingine mtu mmoja  Mkazi wa  Masoko Wilaya ya Rungwe  Ndugu  Tukupyelesya Enock Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria  T.913 Amb aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva asiyefahamika  kuacha njia na kupinduka  huko katika kijiji cha  Masoko,  Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya Tukuyu/Lwangwa.

        Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya  Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha . ajali hiyo ni mwendo kasi  dereva .

       Kufuatia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Msangi ametoa o wiito  Kwa madereva kuwa  Makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika.


  0 0
 • 09/30/15--12:13: Fashion For Peace - Tanzania
 • ABOUT

  Late American President John F Kennedy stated “ask not what your country can do for youask what you can do for your country”
  Fashion as an art has a strong will to convince and educate the public on the importance of peace in the society.
  Fashion for Peace aims to expand the potential power of fashion as a tool to promote peace and harmony during this year’s General elections through creativity.
  Many countries in the region know human rights abuse, civil unrest and war. We aim to change perceptions by exploring and bridging cultures through fashion.
  Fashion for Peace is a result of the belief that positive change can only come when we stop focusing on the negative and encourage the positivity by working together in a spirit of harmony and celebrate the diversity of our country in a spirit of unity.

  SUPPORT

  SHARE this email with as many people you can within your network.
  PURCHASE Ticket and Attend this EVENT (more info in next email)
  SPONSOR this event by projecting your Company/Organization as CHAMPIONING a cause towards Emphasizing PEACE during this Upcoming elections on 25th October
  CONTACT us for more information on +255767123055
       
  LIKE TWEET FORWARD
  Mustafa Hassanali
  P.O. Box 10684
  Dar es Salaam
  United Republic of Tanzania
  Should you NOT want to Receive MY EMAILS, you may

  0 0


  0 0

  Mbunge mtarajiwa wa Moshi Mjini Ndg.Davis Mosha akisalimiana na Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wa hadhara ndani ya kata ya Sokoni.Mwigulu Nchemba akimnadi Davis Mosha mbunge Mtarajiwa kwa Moshi mjini.Mwigulu Nchemba akiwasili Same Mashariki.Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Same Mashariki Bi.Anna Kilango Malecela mapema hii leo wakati alipokwenda kuinadi Ilani ya CCM.Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Same Mashariki kuhusu Umuhimu wa kufanya Uchaguzi kwa Amani,Pia kuichagua CCM kwasababu imefanya kazi kubwa kuiletea Maendeleo Nchi yetu,Kwa Same serikali ya Magufuli nakwenda kujenga Barabara kwa kiwango cha Rami kuelekea Nkomanzi na Same Mashariki.Wananchi wa Mwigulu Nchemba akimndai Mathayo David Mgombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Vunjo kupitia CCM Ndg.Innocent Shirima hii leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Johansen Bukwali akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya usimamizi wa rasilimali za mafuta na gesi asilia kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi -TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia katika ukumbi wa hoteli ya NAF Beach mkoani Mtwara.
   Mkurugenzi wa Utafutaji na Uchimbaji wa gesi asilia na mafuta kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
  Eng. Kelvin Komba akitoa mada kuhusu hali ya utafutaji na muendelezo wa uzalishaji katika shughuli za gesi asilia na mafuta. Baadhi ya mada zilizowasilishwa ni kuhusu sera, sheria na mipango ya serikali katika sekta ya gesi asilia na mafuta; na fursa za ushirikishwaji wa watanzania katika mnyororo wa shughuli za gesi asilia na mafuta.
   Wadau wa sekta ya gesi asilia na mafuta kutoka taasisi mbali mbali wakifuatilia warsha hiyo. Mada zingine
  zilizowasilishwa ni madhara ya kijamii na kimazingira kutokana na uchimbaji wa nishati hizo; pamoja na wajibu wa wadau wa serikali za mitaa katika kuendeleza sekta hiyo. 
  Wadau wa sekta ya mafuta na gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha warsha ya siku moja iliyokuwa inahusu nafasi ya wadau kutoka ngazi za mkoa, wilaya na halmashauri katika usimamizi wa rasilimali za mafuta na gesi asilia iliyofanyika mkoani Mtwara.   

  0 0


  0 0

    Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.

  Akitoa hotuba yake katika moja ya mikutano  yake alioufanya katika mji wa Kibaigwa Dk. John Pombe Magufuli amesema hakuna kitu kinachomuumiza kama mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea kati ya wilaya za Kongwa Mkoani Dodoma na Kiteto  mkoani Manyara.

  Dkt Magufuli ameahidi kuwa mara baada ya kuchaguliwa  na kuunda Serikali yake,jambo hilo atalipa uzito wa juu na kulifanyia kazi kwa umakini mkubwa. “Yaani Mimi Magufuli Nimteuwe Waziri na watendaji wengine wa serikali halafu Mauaji yatokee watu wafe, Mkuu wa mkoa yupo , Mkuu wa wilaya yupo  na Kamanda wa Polisi yupo wabaki wanapunga upepo, wamiliki wa Ng’ombe wabaki  wanakula maisha haiwezekani,nitalala nao mbele na  Ng’ombe wataliwa msibani kwa uzembe waliousababisha”,alisema Magufuli kwa msisitizo mkubwa.

  Magufuli amewataka wafugaji na wakulima kuishi kwa amani bila kubaguana, lakini pia akasema atatumia sheria za ardhi na kuhakikisha maeneo ya wafugaji na wakulima yanatengwa, ili wafanye shughuli  zao na kukuza kipato na  uchumi wao bila kusumbuliwa. 
   Baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakimsiiliza Dkt Magufuli alipokuwa akinadi sera zake za kuomba kura ili kushika nafasi  ya Urais ya awamu ya tano.

    Waziri Mkuu wa zamani, Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimnadi Dkt.Magufuli ambapo alimfagilia kwa kuhubiri amani katika mikutano yake ya kampeni kuliko,na pia amewaasa vijana kuilinda amani ya nchi iliopo kwa gharama yoyote,kuishi bila kubaguana. 
   Dkt. Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa Dodoma Mjini,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Ndugu Anthony Mavunde wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Jamhuri mjni Dodoma leo.
    Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje,mjini MPwapwa katika uwanja wa mgambo.
   Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Kongwa, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo.
    Mawaziri wakuu wa zamani, John Samuel Malecela na Jaji Mstaafu Joseph  Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Dodoma kwenye mkutano wa kampeni. 
    Dk Magufuli akijipigia kampeni  kwa wakazi wa Kibaigwa , wilayani Kongwa leo.Akiwa wilayani Kongwa, Dk Magufuli amesema kuwa akishinda urais atahakikisha anadhibiti mapigano  kati ya wakulima na wafugaji yanayoendelea nchini na kusababisha vifo vya watu wengi 
    Dkt. Magufuli akiwapungia mikono wananchi alipowasili kwenye kampeni Uwanja wa Jamhuri Dodoma leo.  0 0
 • 09/30/15--20:15: MSIBA MAREKANI NA TANZANIA
 • Bettisheba Pole Ketang'enyi enzi ya uhai wake
  Tunasikitika kutangaza kifo cha mama Betisheba Ketangenyi, mama yake Yvonne Matinyi, Felicia Simms, Fredderek Ketangenyi pia ni Dada yake na Rossie Musika, Neema Musika, Daudi Musika, Sijaona Musika kilichotekea 9/30/15 katika hospitali ya NIH Maryland mipango ya kusafiri mwili wa marehemu inaendelea kwa mdogo wa marehemu Daudi Musika
  3819 Gateway terrace Burtonsville MD 20866
  Unaweza kuwasiliana
  Frederick Ketangenyi 267 809 5124
  Felicia Simms 240 608 8686
  Rossie Musika 240 408 2693
  Neema Musika 571 991 9819
  Specioser Musika 571332 2215
  Sijaona Musika 202 487 8412

  0 0


  Mgurugenzi Kissa Pharmacy Ltd Ndugu Gaspar Kilango Singo akizungumza na wafanyakazi wake katika sherehe hiyo iliyofanyika kijijini kwao Mnazi Makanya Wilayani Same Moshi Kilimanjaro

  ·       Wafanyakazi  Kissa Pharmacy Ltd  Pharmaceuticals Whole Sale And Retali Mbeya Tz wenye makao makuu jijini mbeya wakiserebuka katika sherehe ya wafanyakazi iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndugu Gasper Kilango Singo kijijini kwao Mnazi Makanya Kilimanjaro Moshi
  Ndugu na jamaa wa familia ya Kilango wakijumika pamoja katika sherehe hiyo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.  0 0

                           KUSOMA  ZAIDI  kliks  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
  Na  Bashir  Yakub

  Mara  kadhaa  mkopaji  anaposhindwa  kulipa  mkopo  hukimbilia  mahakamani  ili  kuona  kama  anaweza  kupata unafuu  hasa linapokuja  suala  la  wakopeshaji  wake  kutaka  kuuza    nyumba/kiwanja  alichoweka  rehani. 

  Ni  ukweli  usiopingika  kuwa  hatua  hii  imewasaidia  wengi  hasa  wale  wanaowahi.  Yapo  makala   tuliwahi  kuandika kuhusu  hatua  za kuchukua  hasa  inapotokea  kuwa  nyumba  yako  inataka  kuuzwa.


   Makala  yalieleza  namna na hatua  za  kufuata ili  kuokoa  nyumba.  Kwenda  mahakamani  kuzuia  nyumba  isiuzwe  baada  ya  kushindwa  kurejesha  kiasi  cha  rejesho  sio ukorofi  isipokuwa ni  kutekeleza  lililo  ndani  ya  sheria hasa  pale panapo  sababu  za  msingi  za  kufanya  hivyo. 

   Mahakama  za  ardhi  za  wilaya  na  mahakama  kuu  hasa  ya  ardhi  ndizo  mahakama  zenye  mamlaka  katika  kutoa  mazuio  haya  kutegemeana   na thamani  ya  nyumba/kiwanja  na kiasi  cha  deni  kilichohusishwa  katika  muamala  huo. 

  Swali  kwetu ni  kama  baada  ya  kuwa  umeenda  mahakamani  na  kubahatika  kupata  zuio la kutouzwa  nyumba  yako, je  upande  wa  wakopeshaji  wanaweza kukata  rufaa  kupinga  amri  hiyo na  kufanikiwa. Majibu  ya  swali  hili ndio  makala  ya  leo.


  1.HAKI  YA  RUFAA.

  Kifungu  cha  74   cha  sura  ya  33 Sheria  mwenendo  wa  madai kinaeleza  rufaa  katika  amri  mbalimbali  za  mahakama.  Kifungu  kilieleza  wazi  kuwa  kutakuwa  na  rufaa  kutoka  mahakama  za  wilaya  na  zile  za  hakimu  mkazi  ambapo  rufaa  hizo  zitatakiwa  kwenda  mahakama  kuu. Kwa  wasiojua  maana  ya rufaa,  hii  ni hatua  ya  kupeleka  malalamiko  mbele  zaidi  baada  ya  kuwa  hukuridhishwa  na  uamuzi  wa  mahakama   iliyoamua  shauri  lako katika  hatua  za  awali.


  Nje  ya hilo  kifungu  cha  78  cha  sheria  hiyohiyo  kiliruhusu  pia  kufanyika kwa  marejeo  iwapo  mtu  hakuridhika  na  maamuzi  ya  amri  ya  mahakama.  Marejeo  ni  hatua  ya  mahakama   kuitisha  faili  tena  na  kupitia  kilekile  ilichoamua  ili  kujiridhisha  na  uhalali  wake.  Hii  hutokea  baada  ya  upande  wa  pili  kuomba  hilo kufanyika.  Kwahiyo  ilikuwa  ikiwezekana  kutolewa  amri  ya  kuzuia  nyumba  kuuzwa  halafu  baadae  faili  likaitishwa  tena  na  kurudiwa  na  kutolewa  amri  nyingine  ambayo  inaweza  kuwa ileile  ya kutouzwa au  ikabadilishwa  ikawa  amri  mpya  ya  kuuza.


  2.   SHERIA  YA  UKOPAJI  FEDHA  NA  KUWEKA  REHANI.

  Mwaka  2008  ilikuja  sheria  ambayo  iliitwa  kwa  jina  la sheria  ya  ukopaji  fedha  na  kuweka  rehani.  Sheria  hii  inazungumzia  masuala  yote  nyeti  yanayohusu   kukopeshwa  fedha  na  kuweka  rehani  mali . Ni  sheria  inayoratibu  masuala   yahusuyo  kuuzwa  kwa  mali  zilizowekwa  rehani na  kutouzwa  kwake. Inazungumzia  haki  za  mkopaji  na  mkopeshaji  halikadhalika  wajibu  wao  wote  katika  nafasi  zao.  Kutokana na  ujio  wa  sheria  hii  masuala  kadhaa  katika  sheria  ya  ardhi  ya 1999  sambamba  na  sheria  ya  mwenendo  wa  madai sura ya  33  zimelazimika  kufanyiwa  marekebisho  ili  kukidhi  malengo  kadhaa .


  3.  AMRI  YA  KUTOUZA  NYUMBA  YA  MKOPO  HAIKATIWI  RUFAA.

  Hapo  juu  tuliona  kuwa  awali  ilikuwa  ni  ruhusa kwa  mtu  kukata  rufaa   hata  kwa  amri  iliyotolewa  kuzuia  nyumba/kiwanja    cha   mkopo  kuuzwa.  Mahakama  ya  wilaya  ingeweza  kutoa  amri  kuwa  nyumba  fulani isiuzwe  hata  kama  mkopaji  yuko  nje  ya  makubaliano  kwasababu  kadha  wa  kadha. Hata  hivyo   ilikuwa  ni haki  ya  mkopeshaji ambaye  ndiye  hutaka  kuuza  nyumba  kukata  rufaa  na  kupinga  amri  hiyo. 

  Kama  amri  hiyo  ingetolewa  mahakama  ya  wilaya  au  ya  hakimu mkazi basi  mkopeshaji  angeweza  kukata  rufaa  kwenda  mahakama  kuu.  Na  huko   ingewezekana  kutolewa  uamuzi  uleule  au  uamuzi  mpya  ambapo  pengine  amri  ya  kutouzwa  ingebatilishwa  na  kuruhusu  uuzaji  kuendelea.


  Kwa sasa kutokana  na   sheria hii  ya  masuala  ya  ukopeshaji fedha  na rehani  kifungu  hiki  kimefanyiwa  marekebisho  na  sasa  ni  kuwa  amri  ya  mahakama  iwe  ya  wilaya  au  mahakama  kuu  ikishapita  na  kutoa  zuio  la  kutouzwa  nyumba  ya  mkopaji   basi   huwezi  tena  kukata  rufaa  kupinga  jambo  hilo.  Amri  hiyo  ikishatolewa  basi  inakuwa  imetolewa. Ni  kutokana  na  hilo  kichwa  cha  makala  haya kimekuwa ,  amri  ya  kutouza  nyumba  ya  mkopo  haikatiwi  rufaa.


  MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi leo amefunga kozi ya waamuzi chipukizi wasiokuwa na beji za FIFA katika hoteli ya Holiday, ambapo jumla ya waamuzi 30 kutoka nchi 28 barani Afrika walihudhuria.
  Akiongea wakati wa kufunga kozi hiyo Malinzi alitoa wito kwa wahitimu wajikite kwenye maadili kwa kuzingatia mafunzo waliyopata ili katika kipindi kifupi wote wapate beji za FIFA na waonekane kweye mashindano makubwa kama fainali za AFCON na mashindano ya Kombe la Dunia.
  Kabla ya Hotuba ya Mgeni rasmi mwakilishi wa CAF Eddy aliishukuru TFF kwa maandalizi mazuri na usimamizi bora kwa kipindi chore cha kozi hii, na kuahidi kuleta kozi nyingine kubwa hapa nchini.
  Naye mwakilishi wa FIFA Carlos Hendrique alitoa shukurani zake za dhati kwa TFF kwa kuwa tayari wakati wote kushirikiana na FIFA hali ambayo imefanyika TFF iaminike na itegemewe na FIFA kweye program mbalimbali
  Kozi hiyo ya waamuzi imefanyika kwa mara ya kwanza hapa barani Afrika.
  FIFA iliiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa kozi hii kwa nchi zinazo zungumza kiingereza. Kwa upande wa nchi zinazo zungumza kifaransa kozi ya aina hii imefanyika nchini Morocco

  Washiriki 30 kutoka nchi 28 barani Afrika wamehudhuria kozi hii ilivyokuwa itafundishwa na Wakufunzi wa Sita kutoka CAF na FIFA.

older | 1 | .... | 992 | 993 | (Page 994) | 995 | 996 | .... | 3272 | newer