Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN ATOWA MKONO WA EID EL HAJJ KWA WAZEE WA WELEZO NA SEBLENI ZANZIBAR

$
0
0
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Bi Asha Abdalla wakiongozana na mlezi wa Wazee Welezo wakiwasili katika viwanja vya Makaazi ya Wazee Welezo Unguja kumuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kutowa Mkono wa Eid kwa Wazee hao kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid El Hajj.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha akizungumza na Wazee wa Welezo wakati alipofika katika makaazi yao kuwajulia hali na kutoa mono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao kwa Niaba na Mama Mwanamwema Shein.
Wazee wa Makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha wakati alipofika katika makaazi ya Wazee Welezo kuwatembelea na kutoa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao. 
Imetayarishwa na Othmanmapara.Blogspot. zanzinews.com. 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

FAINALI YA MCHEZO WA BAO NA KARATA EACROTANALI ZANZIBAR

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akicheza bao la kete na mzee Abdalla Salim Kitambo wa Wilaya ya Mjini wakati alipofika kuyafunga mashindano ya fainali ya mchezo huo na mchezo wa Karata katika viwaja vya Eacrotanal leo

 Baadhi ya Timu mbali mbali za Michezo ya Bao la Kete na karata wakiwa katika fainali ya michezo hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,wakati mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 Timu za mchezo wa karata kutoka kibanda mawazo Miembeni Chake chake Pemba na kwamtipura Unguja zikichuana katika fainali iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
[Picha na Ikulu.]
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

MATUKIO MBALI MBALI YA ZIARA YA KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS WA UKAWA KUPITIA CHADEMA KATIKA JIMBO LA HAI, MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro  Septemba 26, 2015. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JESHI LA ANGA LA CCM LAMALIZA KAZI TABORA,WANANCHI WAAHIDI KUCHAGUA "KAZI TU"

$
0
0
FieldMashall Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Sikonge hii leo Mkoani Tabora wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi,Mwigulu Nchemba amewasisitiza Wananchi wa Sikonge Kuachana na siasa za Makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi,"Wananchi wote,WanaCCM wote tuunganishe nguvu zetu kukipa Ushindi chama cha Mapinduzi,Tuunganishe nguvu kuhakikisha tunapata Mbunge wa CCM atakayeweza kutatua Matatizo ya Tumbaku hapa Sikonge"
Mbali na hilo ,Mwigulu Nchemba ameendelea kusisitiza Uchaguzi wa Amani na Upendo kwa vyama vyote,Amewasihi Wananchi wajitokeze kupiga Kura ilikuwachagua Madiwani,Mbunge na Rais wa Chama cha Mapinduzi wenye Ilani inayotekelezeka.
Mjumbe wa timu ya Ushindi ya CCM Taifa Comrade Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Jimbo la Igagula Ndg.Ntimizi hii leo alipofika kwaajili ya kuinadi Ilani ya CCM na kuwasihi Watanzania walipojo Tabora kuichagua CCM kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwishoni mwa October 2015.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sikonge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.Said Nkumba aliyekuwa Mbunge wa sikonge akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la sikonge kuuonesha wazi Umma kuwa CCM kwa Sikonge ni Moja.Vijana wa kazi wa Chama Chama Mapinduzi Ndg.Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakionesha Umahili wao wa kupiga Push-Up kabla ya Kuanza kwa Mkutano wa hadhara Jimbo la Sikonge hii leo Mkoani Tabora.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Sikonge waliofurika kusikiliza sera za Chama cha Mapinduzi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Picha na Sanga Festo Jr. Picha zaidi BOFYA HAPA

MAGUFULI AWASHA MOTO SHINYANGA

$
0
0
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati umefika wa kujenga Tanzania mpya yenye viwanda vya kutosha kutoa ajira kwa vijana wengi.
Alisema pia kuwa Serikali yake itakuwa rafiki wa sekta binafsi na kuwajengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kujiendeleza.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wake wa Kampeni ambapo aliwaambai wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi kwa maendeleo ya nchi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Kambarage.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao Mgombea urais anazo changamoto za Shinyanga mjini na anaamini atazitatua hivyo amewataka watu wake kumpa kura nyingi za Dk. John Pombe Magufuli ifikapo tarehe 25 Octoba
 Wasanii wakipiga push up jukwaani kabla ya mgombea wa urais kupitia CCM hajahutubia.
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Mzee Samuel Sitta akihutubia wakazi wa mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa mji wa Shinyanga mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Kambarage.
 Wananchi wa Jimbo la Solwa wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Bajeti za nchi zizingatie ustawi wa wanawake: Kikwete

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa. 
(Picha:UN-Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema wanawake hawajengewi mazingira ya kutosha ya ustawi wa kijamii na  kiuchumi kama ilivyo wanaume hususani katika nchi zinazoendelea akitolea mfano wa bajeti za serikali ambazo hazizingatii ukuaji nwa kundi hilo. 
Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhutubia mjadala kuhusu kupambana na ukosefu wa usawa na kuwezesha wanawake na wasichana ikiwa ni sehemu ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, Rais Kikwete anataja mambo kadhaa ambayo ni muhimu kwa wanawake ikiwamo elimu.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI KATIKA TV LEO

dar es salaam usiku


DAVIS MOSHA AZIDI KUWAKUNA WANANCHI WA MOSHI KWA SERA

$
0
0
Mh, Davis Mosha akiwahutubia mamia ya waBondeniazi wa kata ya kata ya Bondeni.




Ikiwa zimesalia Takribani siku ishirini na tisa kuweza kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (ccm) Jimbo la Moshi Mjini Ndugu Davis Elisa Mosha amezidi kumtesa Mpinzani wake kutoka Kambi Pinzani ya Ukawa anayesimama kwa Tiketi ya Chadema Ndugu. Jafary Michael. Hayo yamedhihirika leo katika Mkutano wa Hadhara wa Mh. Davis Mosha katika viwanja vya Manyema vilivyopo kata ya Bondeni. 
Mkutano huo uliofurika mamia ya wakazi wa katahiyo huku wakionesha furaha ya waziwazi, Wakazi wa Kata hiyo wamesema hawawezi kufanya makosa tena katika kusimamisha Mbunge wa Jimbo la Moshi na watachagua Kingozi sahihi ambaye ni Davis Mosha. 
Akizungumza kwa Furaha huku akiwa na Picha ya Mh. Davis Mosha Bi. Veronica  Deus alisema kama ni kiongozi basi Mungu kawaletea Davis Mosha na atampigia kura na atahakikisha analinda kitambulisho chake cha kupiga kura ili aweze kukitumia kumpeleka Davis Mosha Bungeni ili alete Maendeleo. “Unajua huyu kijana Katosheka, Tayari ana fedha zake na Desturi yetu hatuwezi chagua Fukara asiye na fedha, Ndio maana tulimchagua Ndesamburo sababu ana Pesa, Sasa leo unaweza kumfananishaje Jafary na Davis Mosha, Hii ni sawa na Kifo na Usingizi” Alisema Bi Veronica deus.
Pamoja na yote Mh. Davis Mosha alisema huu ni wakati wa kufanya vitendo na si maneno ya siasa, Yeye si mwanasiasa ila ni mtendaji na amekuja kushirikiana na wana Moshii kuijenga Moshi tunayoitegemea. “Huu si wakati wa Kulala ni wakati wa Kufanya kweli, Tujumuike Pamoja kufanya kweli kuiondoa chadema tumewapa nafasi muda mrefu na wametumia Halmashauri ya Moshi Mjini kujinufaisha wao. Sasa ni zamu ya Wananchi  kula matunda ya kodi zao na hakuna mwingine mwenye uwezo huo. Nitumeni mimi” Alisema Mh. Davis Mosha huku akishangiliwa na ummati mkubwa wa watu.



Meneja Kampeni wa Mh. Davis Mosha h. Mwita akizungumza na wakazi wa Kata ya Bondeni.

Wakazi wa kata ya Bondeni wakimsikiliza Mh. Davis Mosha akinadi Sera zake za maendeleo ya Moshi Mjini.

Mh. Davis Mosha akizungumza na Wakazi wa Kata ya Bondeni

Mke wa Mh. Davis Mosha Madame Nancy Mosha  akisalimu wakazi wa Kata ya Bondeni.

Benki ya Afrika(BOA Bank) yapigia chapuo matumizi bora ya mikopo

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kukopa na kurejesha kwa wakati mikopo katika taasisi za fedha kwani huo ni msingi muhimu wa kujipatia maendeleo kwa mtu binafsi na katika ngazi ya taasisi pia.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Afrika, Bw. Mussa Mwachaga amesema mwishoni mwa juma wakati akikabidhi msaada wa Tsh. milioni 10 kwa shule ya Sekondari ya Baobab kuwa uaminifu katika kurejesha mikopo huleta maendeleo ya haraka kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali.

“Hili ni wazi, wale wanaojenga uaminifu na taasisi za fedha hufanikiwa kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Alisema uongozi wa shule hiyo ya sekondari ni mfano hai wa taasisi zilizojijengea uaminifu mkubwa wa kurejesha mkopo na sasa imejijengea mahusiano mazuri ya kuendelea kukopa zaidi na kufikia malengo yake.

Msaada huo ni sehemu ya ahadi ya Tshs milioni 40 zilizoahidiwa na benki kwa shule hiyo.

Pesa hizo zitatumika katika ukarabati wa bweni la wasichana ambalo nalo lilijengwa mwaka 2006 kwa mikopo toka benki hiyo.

Mkurugenzi na mmiliki wa shule hiyo, Bw. Halfan Swai aliipongeza benki hiyo kwa kuamua kumpatia msaada huo ambao utatolewa kwa awamu kwa jili ya ukarabati wa majengo ya shule.

“Kwa vile jengo hili lilijengwa kwa mkopo wao, leo nimewapa fursa ya kulizindua rasmi,” alisema na kuongeza kuwa kwa heshima ya benki hiyo bweni litapewa jina la ‘Bweni la Benki ya Afrika.’

Alisema benki hiyo imeisaidia shule yake na kuwa hadi ilipofikia imeshapata mkopo zaidi ya Tshs bilioni 2.

Alifafanua kwamba siri ya kuendeleza mahusiano na benki ni kurejesha mikopo kwa wakati sababu bila hivyo haiwezekani kuendelea kukopa.

Meneja wa shule hiyo, Bi. Sophia Mawenya alisema bweni linalokarabatiwa linachukua wanafunzi 408 ambapo kila chumba kina uwezo wa wanafunzi nane.

“Tunahitaji benki hii iendelee na ushirikiano huu kwa vile malengo yetu ya kujenga shule ya msingi na chuo kikuu bado hayajafikiwa,” alisema.

Alisema malengo hayo yatafikiwa tu kwa kukopa fedha katika taasisi za fedha kama Benki ya Afrika.

Katika tukio hilo, wafanyakazi wa benki hiyo walishiriki katika kazi ya kupaka rangi bweni  hilo.

TAARIFA YA WIZARA YA ULINZI NA JKT JUU YA UZUSHI KUHUSU AFYA YA MKUU WA MAJESHI

$
0
0
 KUMEKUWAPO UVUMI WENYE KUUPOTOSHA UMMA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUWEKEWA SUMU KATIKA CHAKULA NA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN ILIYOPO NAIROBI, NCHINI KENYA, HUKU WENGINE WAKIDAI KUWA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU. 
TAARIFA HIZO NI UONGO WENYE KILA DALILI YA KUTENGENEZWA KWA LENGO LA KUWATIA HOFU WATANZANIA JUU YA USALAMA WA KIONGOZI HUYU WA JUU WA MAJESHI YETU.

UKWELI NI KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE NI BUKHERI WA AFYA NA HAYUPO NCHINI KENYA WALA INDIA KAMA ILIVYOENEZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA VYOMBO VYA HABARI.

Jenerali Mwamunyange mara baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

TUNAPENDA KUWATOA HOFU WANANCHI KUWA TAARIFA HIZO NI UZUSHI MTUPU KWANI JENERALI MWAMUNYANGE ALIONDOKA NCHINI TAREHE 22 SEPTEMBA 2015, SAA 10.45 JIONI KWA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUELEKEA ROME, ITALIA KWA ZIARA YA KIKAZI KUFUATIA MWALIKO WA MKUU WA MAJESHI WA JAMHURI YA ITALIA, JENERALI CLAUDIO GRAZIANO. TUNAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA JENERALI MWAMUNYANGE PAMOJA NA UJUMBE WAKE WANAENDELEA NA ZIARA HIYO KAMA ILIVYOPANGWA NA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO.

WIZARA YA ULINZI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMESIKITISHWA NA TABIA HII YA UZUSHI INAYOPINGANA NA WELEDI NA KANUNI ZA UANDISHI KATIKA TASNIA YA HABARI. NI DHAHIRI TABIA HII INAIDHALILISHA TASNIA YA HABARI NA WANAHABARI WANAOZINGATIA WELEDI NCHINI. TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKEMEA TAARIFA ZA AINA HII ZISIZOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU NA ZILIZOLENGA KUWASUMBUA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATUMISHI WENYE MAPENZI YA DHATI NA JENERALI MWAMUNYANGE.

TUNAWAASA WANAHABARI KUTOZITUMIA VIBAYA KALAMU ZAO NA UHURU WALIONAO KWA NAMNA YOYOTE ISIYOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU. AIDHA, WIZARA NA TAASISI ZAKE WAKATI WOTE ZIMEKUWA TAYARI KUTHIBITISHA JAMBO LOLOTE AU KUTOA UFAFANUZI PALE ULIPOHITAJIKA. INASTAAJABISHA KUONA WALIOANZISHA UZUSHI HUO NA KUUENEZA HAWAKUWA TAYARI KUOMBA UTHIBITISHO WA NAMNA YOYOTE. JAMBO HILI LINATIA SHAKA JUU YA NIA YA MTU AU KIKUNDI KILICHOANZISHA UVUMI HUO. 
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA TAASISI ZAKE ZITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANAHABARI WENYE NIA YA DHATI YA KUJENGA NA KUILETEA SIFA TASNIA YA HABARI KWA KUZINGATIA WELEDI. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UWE NI UHURU WENYE KUZINGATIA WAJIBU ULIOBAINISHWA KATIKA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.

MWISHO, TUNAWATAKA WALIOANZISHA UZUSHI HUO KUMUOMBA RADHI JENERALI MWAMUNYANGE KAMA ISHARA YA USTAARABU NA KUTAMBUA KUTELEZA KWAO. KUTOFANYA HIVYO ITATAFSIRIKA KUWA NI KUKIRI KUWA KUENEZA UZUSHI HUO HAIKUWA KUTELEZA, BALI ILIKUSUDIWA KWA DHAMIRA FULANI, NA HIVYO KUSHAWISHI HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA.

JESHI NA WIZARA ZITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUWABAINI WATU WALIOHUSIKA KUUTUMIA VIBAYA UHURU WA HABARI NA HIVYO KUUPOTOSHA UMMA NA KULETA USUMBUFU KWA FAMILIA YA JENERALI MWAMUNYANGE, JESHI NA TAIFA KWA UJUMLA.

Imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na JKT

September 26, 2015.
 Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

 Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM MUDA HUU, WATUMISHI WA OFISI YAKE WAMLILIA

$
0
0
Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (pichani enzi za uhai wake).
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais-Utumishi wataendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako mzuri. Mola ailaze Roho yako 
pahala pema peponi - AMIN
-------------------------------------------------------------------
Wakati huo huo mwili wa Marehemu Celina O. Kombani umewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Utaratibu wa msiba unasimamiwa na serikali na ofisi za Bunge. Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. 
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili muda huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipelekwa kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipakiwa  kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani. 
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

STOP PRESS: DEVELOPMENT OF MCC COMPACT WITH TANZANIA TO CONTINUE

$
0
0
DAR ES SALAAM, TANZANIA – September 26, 2015.  The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) has released a statement indicating that Tanzania will pass the FY 2016 Control of Corruption Indicator.  The statement is available below and on the MCC website here:  https://www.mcc.gov/news-and-events/release/pressstmt-092615-tanzania-passes-fy16-corruption-indicator
The $472.8 million compact, when approved by the Board, will promote increased access to reliable electricity in Tanzania and will strengthen the energy sector overall.  U.S. Ambassador to Tanzania Mark Childress noted that “I am pleased by the news that the process towards finalizing a compact will continue.  However, while Tanzania has passed the required indicator, further efforts towards combatting corruption are essential for successful implementation of the compact, improving the business climate, and ensuring the public’s trust in its government and institutions.”
##### 
MCC Statement on Tanzania Passing the Fiscal Year 2016 Control of Corruption Indicator
WASHINGTON DC - September 26, 2015.  On September 17, MCC’s Board of Directors (“Board”) indicated that it would vote on a compact with Tanzania if the country scored above the relevant median in the Worldwide Governance Indicators’ latest annual Control of Corruption index.  
That index is now publicly available and Tanzania has scored above the relevant median, and therefore will pass the Control of Corruption indicator on MCC’s forthcoming fiscal year 2016 scorecard. 
 Accordingly, the Board will vote on whether to approve the proposed compact.  Projects funded under the compact will need to meet the agency's economic analysis standards.  Should the Board approve the compact, signing is expected to occur sometime in 2016.
MCC takes seriously all of its country partners’ commitments to combat corruption.  While Tanzania passes the Control of Corruption indicator, MCC will continue to monitor the Government of Tanzania’s efforts to combat corruption.

MCC expects that Tanzania’s October 25 general election will be free and fair, consistent with the importance MCC places on democratic rights.

Profesa Mark Mwandosya awa Mgeni Rasmi Siku ya Taifa ya Bima

$
0
0
Na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya alikuwa Mgeni Rasmi katika kongamano lililoandaliwa kusherehekea Siku ya Taifa ya Bima, Ijumaa tarehe 25 Septemba 2015. 
Kongamano hilo liliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Bima Tanzania (Insurance Institute of Tanzania - IIT) na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania ( Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA). 
Kongamano hilo liliwakutanisha wadau wa sekta ya bima kutoka ndani na nje ya nchi, kutoka Wizara mbalimbali na taasisi za umma na sekta binafsi. Mada kuu ya kongamano hilo ilihusu Usimamizi wa Bima katika ili kuleta Maendeleo Endelevu. 
 Akihutubia Kongamano hilo Waziri Mwandosya amesisitiza umuhimu wa sekta ya Bima katika uchumi kama njia moja ya kuelekeza rasilimaili za taifa katika maeneo yanayoleta tija na faida, kuongeza akiba ya taifa na ya mwenye bima. 
Amewataka wadau wa sekta ya bima wazingatie yafuatayo: 
 - kujenga uwezo wa rasilimali watu ili kukabiliana na mabadiliko makubwa katika uchumi na ongezeko la watu na mahitaji ya bima, 
- kuifanya sekta ya bima ieleweke kwa wananchi kwa kuwa na mkakati wa uenezi na kutumia lugha nyepesi na inayoeleweka katika kuelezea dhana mbalimbali za bima, 
- kutekeleza dhana ya " Bima katika Mstari wa Mbele" ili kuwafikia wananchi walio wengi waishio vijijini na maeneo ya miji wanakoishi wananchi wa kawaida, 
- kuharakisha mfumo wa malipo ya bima, - kuwa na ufahamu wa maafa yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi na matukio asilia kama vile matetemeko ya ardhi, na mafuriko, kwa kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Hali ya Hewa, Idara ya Mazingira, Vyuo Vikuu , taasisi na wataalamu wengine katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya majira na mabadiliko ya tabianchi. Kwani bima katika maeneo haya ni muhimu kwa taifa na jamii. 
- kuangalia na kuishauri serikali kuhusu maeneo ya ziada ambayo ingefaa iwe lazima kisheria kuwa na bima, eneo kama vile bima za nyumba mijini dhidi ya moto. 
- makampuni ya bima kufuatilia maendeleo utafiti, uchimbaji, usafrishaji na matumizi katika sekta ya mafuta na gesi. 
- makampuni ya bima kuungana ili kushindana na makampuni ya nje katika kutoa bima katika zsekta muhimu na inayokua ya mafuta na gedi asilia.
 Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi Profesa Mark Mwandosya akihutubia Kongamano lililoandaliwa kusherehekea Siku ya Taifa ya Bima, Ijumaa tarehe 25 Septemba 2015. 
Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi Profesa Mark Mwandosya
Waziri wa Nchi(Kazi Maalum) Ofisi Profesa Mark Mwandosya akiwa katika picha pamoja na viongozi wa kongamano. Kutoka kulia ni Ndugu Israel Kamuzora Kamisha na Mkurugenzi Mkuu wa TIRA, Ndugu Peter Ilomo Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Bima na Katibu Mkuu Ikulu, na Ndugu Bugali, Rais wa IIT.
 Waziri Mwandosya akitoa cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Sallam na Chuo cha Usimamizi wa Fedha waliofanya vizuri katika masoma ya yanayohusu Bima.
Waziri Mwandosya ,wa tano kushoto  waliokaa akiwa na wanakongamano katika picha ya pamoja.

Mkutano wa Kampeni Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Shein, Viwanja vya Bungi Zanzibar

$
0
0

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya mkutano Bungi akiwapungia mkono Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Kampeni katika viwanja vya mpira Bungi akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai . 
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar  kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. uliofanyika katika viwanja vya bungi.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wana CCM katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mpira Bungu Wilaya ya Kati Unguja na kuomba Kura kuendelea kuiongoza Zanzibar kwa Maendeleo katika sekta mbalimbali za Kijamii na kuendeleza kukuza Uchumi wa Zanzibar.  
Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wakati akiwahutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vha mpira Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia mgombea Urais wa Zanzibar  kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein katika mkutano  uliofanyika katika viwanja vya bungi. 
Kijana akitowa ishara kwa Wananchi wenye ulemavu wa kutokusikia kwa alama ya Ishara wakati mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya mpira Bungi Wilaya ya Kati Unguja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI - YANGA 2 SIMBA 0

KUTOKA MAKTABA: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotembelea Ikulu ya White House Marekani mwaka 1963

MLINZI No.1 KOPLO DOG DOMO BAYA WA RAS MAKUNJA AMFUKUZIA WAGENI BOSS !

$
0
0
 Kuishi kwingi kuona mengi ! katika hali ya utata juzi kati wageni waliokwenda kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mwanamuziki mahili na kiongozi wa Ngoma Africa band a.k.a FFU Ughaibuni kamanda Ras Makunja kule ujerumani walijikuta wakitimuliwa mbio na mlinzi namba one Koplo Dog Domo Baya (pichani)  wa Kamanda huyo. 
Mbwa huyo aliyechoka lawama za boss wake kuwa amekuwa mzembe kazini , siku ya jumamosi 19 Septemba 2015 majira ya saa 2.00 usiku aliamua kupiga doria ndani ya makao ya himaya Kamanda Ras Makunja, na kila mgeni aliyegusa au kukaribia geti alibwakiwa na kutemewa kibesi na mbwa huyo. 
Timbwili hilo lilichukua muda masaa mawili bila kibosile kamanda Ras Makunja kujua kinachoendelea nje ya nyumba,kwani alikuwa ndani na familia yake. dipo mmoja wa watu wake wa karibu alipomtumia ujumbe wa simu asitegemee wageni mbwa kachomoka ndani ya banda na kupiga doria ! baadhi ya marafiki wanamlalamikia Koplo Dog Domo baya kuwa anachagua watu wa kuwatimua... mbwa huyo anawajua wanamuziki wa Ngoma Africa band aka FFU.. tu. Lakini wa wageni wengine yeye kazi ni moja tuu.
Kwanza Ras Makunja kaamua kumtungia songi Koplo Dog Domo Baya, kisha akaamua Kumagufulika ili apambane naye akileta za kuleta. Kamanda kachachamaa

Baada ya kutunga wimbo wa Koplo Dog Domo Baya, Kamanda wa FFU Ughaibuni akaamua Kumagufulika ili isiwe taabu pindi akitaka kutoa adhabu...

JAPAN INTERNATIONAL COOPERATION AGENCY DELEGATION VISIT EAC HEADQUARTERS: Discuss dualling of Tengeru-Usa Road, Rehabilitation of Usa - Holili section, and Re-location of Kikafu Bridge

$
0
0
Dr. Enos Bukuku; Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure shares a handshake with Eng. Masataka Fujikuma; the JICA Technical Expert.
A group photo of Dr. Enos Bukuku; EAC Deputy Secretary General (DSG) in charge of Planning and Infrastructure with Mr. Hajime Iwama; JICA Tanzania Director (DSG's immediate right) and Eng. Hosea Nyangweso; Prinicpal Civil Engineer (DSG's second right) among other members of the Japan delegation and EAC Staff.
East African Community
East Africa Community Headquarters, Arusha, 27 September, 2015: A Japanese delegation led by Hajime Iwama; Director, Africa Division 2 in charge of the Japan International Cooperation Agency (JICA) Tanzania program, Africa Department, Kenji Isomoto; JICA Technical Advisor and Kimanari Takahashi; Team Leader of JICA Study among others paid a working visit to the EAC Headquarters on Friday 25 September to discuss funding for the completion of the dualling of the road from Tengeru to Usa in Arusha, rehabilitation of the Usa - Holili section including complete re-location of the dangerous Kikafu Bridge and the feasibility study.
The EAC Deputy Secretary General in charge of Planning and Infrastructure, Dr. Enos Bukuku welcomed the delegation to the EAC and noted that their visit was adding to the recent three visits made by the new JICA Chef Representative in Tanzania, the Ambassador Extraordinary and Plenipotentiary and the Deputy Ambassador of Japan to Tanzania, all aimed at cementing the cordial relationships not only between Japan and Tanzania but also between Japan and the East African Community. 
“It is in recognition of the need for facilitating integrated, efficient and cost effective transport systems along the EAC Corridors that the Government of Japan, through JICA, accepted the request made by the East African Community in May, 2014, to support the rehabilitation of the Tengeru-Holili road section”, affirmed Dr. Bukuku, adding that “the current constructions cover only 14.1km out of the envisaged 22.3km to Usa. This means that there is a gap of around 8.2km to be upgraded to dual carriageway”. 
The Tengeru-Holili road section has no Project Affected Persons and, therefore, no resettlement issues. “However, it has a very special safety consideration in particular at Kikafu Bridge”
Dr. Bukuku highlighted and urged that the JICA Study Team critically reviews the provisions of the current design and addresses all constraints that could become impediments to smooth flow of local and transit traffic along the road. 
Although the project section is wholly located in Tanzania, it has corridor-wide/regional impacts on traffic flows as it links the Northern Corridor, the Trans African Highway No. 8 (Great North Road) and ultimately the Central Corridor. It will also be a link to Rwanda and Burundi from the Port of Mombasa. 
The project road has been designed to conform to the EAC agreed standards, which are hybrids of existing standards among EAC Partner States. The EAC standards have been adopted through harmonization framework contained in the East African Transport Facilitation Strategy. 
The Deputy Secretary General thanked the Japanese Government for the interest shown in this project and requested that JICA considers providing a grant component to the funding support especially for the Kikafu Bridge.
 “The grant assistance we seek for the Kikafu Bridge and associated approach roads will enhance the symbolism of the Japanese emotional connection to the site, which has been an annual pilgrimage area for Japanese visitors to Tanzania.” 
The JICA Director for Tanzania; Mr. Hajime Iwama expressed his gratitude for the generous hospitality the delegation received from EAC and restated that the main purpose of their visit was to ensure smooth running and kick off of the rehabilitation operations and feasibility study respectively.

BAADA YA KUFUNGWA 2-0 NA MAHASIMU WAO YANGA, SIMBA WAMLALAMIKIA REFA

$
0
0
Ankal akiwa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba leo jijini Dar es salaam
Tarehe 26-9-2015 jana jumamosi kulifanyika mechi ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baina y a klabu yetu ya Simba na timu ya Yanga. Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa goli mbili kwa bila.
Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata.
Pili tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama. Hapa Mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia. Sababu washabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.

Refa Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na tena kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan kessi!!
Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo..
Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu..
Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashukuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.
Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..

Reclaming our glrory
Simba nguvu moja


Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba
Simba sports club
27-9-2015


Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.
Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015
👍👌👆☝☝Pamojaaaa. Sanaaa tuu!!
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images