Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

Maafisa Mawasiliano wahitimu mafunzo ya kutumia mitandao ya jamii

$
0
0
 Mkufunzi kutoka  Uingereza, Bw. David Wiggins, akiwaaga Maafisa Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) baada ya kumaliza  mafunzo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) .
 Hivi karibuni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini  imewapatia mafunzo ya  kuwajengea uwezo Maafisa  Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jinsi  ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano. Mafunzo hayo yameendeshwa na  Taasisi ya Thomson Foundation na kugharamiwa na Serikali ya Uingereza. Pichani  Mkufunzi wa Mafunzo David Wiggins (katikati) akifurahia zawadi ya shati la kitenge baada ya kukabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Judith Mhina (kushoto ) kwaniaba ya wenzake, (kulia) ni Mkurugenzi  wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwa katika picha ya pamoja. baada ya kumaliza  mafunzo ya  jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii  kama facebook,twitter, flickr na blogs. 

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
MWanamama Abeti Masikini anakupa 'Likayabo' mambo ya manjano na mdalasini...

Basata yawapongeza waandaaji wa Miss Universe Tanzania

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) ambao hawapo pichani makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini. Kulia ni Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai (wanne kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kuwakilisha tathmini ya mashindano Miss Universe Tanzania mbele ya maofisa wa sanaa wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) makao makuu ya baraza hilo Ilala jijini.

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeipongeza kampuni ya Compass Communications kwa mafanikio makubwa waliyopata pamoja na kuandaa mashindano ya urembo nchini kwa muda mfupi.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya mashindano ya Miss Universe yaliyofanyika juzi makao makuu ya Basata, Afisa Sanaa baraza hilo Malimi Mashili alisema kuwa pamoja na kampuni ya Compass kuanza kushiriki katika mashindano ya Miss Universe mwaka 2007, waliweza kufanya vyema na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Alisema kuwa mrembo wake, Flaviana Matata ambaye alimaliza katika hatua ya sita bora, mpaka sasa anafanya vyema nje ya nchi katika sekta ya maonyesho ya mavazi au wanaminitindo.

Mbali na mafanikio hayo, Mashili alisema kuwa usimamizi bora wa kampuni hiyo imewafanya warembo kuwa na tabia njema na kuepukana na skendo mbali mbali ambazo zinawatokea warembo waliopitia mashindano tofauti na mashindano mengine ya urembo nchini.

“Ni mashindano bora ambayo kwa kweli yametuvutia sana, tunaomba muongeze bidii ili kuyaboresha zaidi kwani mashindano haya kwa sasa ni makubwa na warembo wengi wanayaulizia jinsi ya kujiunga nayo,” alisema Mashili. Pia aliwataka waandaaji wa mashindano hayo kutafuta udhamini wa televisheni ambayo itaonyesha moja kwa moja ‘live’ mashindano hayo ili kupanua wigo wa wafuatiiaji wake kama ilivyo kwa mashindano mengine ya urembo.

Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajiathidi kuongeza wigo wa washiriki kaika mashindano ya mwaka huu. 

Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo alisema kuwa wameongeza mikoa saba zaidi na kufanya jumla ya mikoa 14 ambayo warembo wake watawania mataji mbali mbali mwaka huu.

Mikoa hiyo ni Katavi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha, Mtwara, Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Kagera na Manyara. Kwa mujibu wa Maria, Miss Universe Tanzania imeweka mikakati ya kuwaendeleza warembo ambao hawakufanikiwa kushinda katika mashindano hayo. Alisema kuwa mpango wao mkuu ni kuwapa msaada wa kielimu kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za hapa nchini hususani zinazoshughulika na masuala haya ya elimu.

MWISHO WA KUBADILI LESENI ZA ZAMANI ZA UDEREVA NI APRILI 30,2013

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – SACP. Mohammed R. Mpinga (kushoto) na Mr. Salum Yusuph - Naibu Kamishna wa Kodi za ndani TRA (kulia) wakisikiliza maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu mwisho wa kubadili leseni za zamani za udereva utakao kuwa mwisho wa mwezi huu 30/04/2013.
Mr. Salum Yusuph - Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani TRA (kulia), akijibu moja ya swali lililoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano ulifanyika Katika ukumbi wa mikutano wa TRA Makao Makuu Tarehe 10/04/2013.

MAONYESHO YA TATU YA SEKTA YA NYUMBA TANZANIA-TANZANIA HOMES EXPO KUFANYIKA JUNE 2013

$
0
0
Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Zenno Ngowi akiongea wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 3 ya Tanzania Homes Expo yanayotarajiwa kufanyika Juni 2013. Kushoto ni mratibu wa maonyesho hayo Happy Geddi na kushoto ni Meneja Masoko Mesha Gobba.

Maonyesho ya tatu ya Tanzania Homes Expo yanatarajiwa kufanyika Mlimani City Juni 2013 na kushirikisha makampuni pamoja na taasisi mbalimbali za sekta ya nyumba Tanzania na Kenya. Mara ya mwisho maonyesho hayo yalifanyika Desemba 7 hadi 9 2012.

Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kufanyika kwa maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, ndugu Zenno Ngowi alisema, “Katika maonyesho hayo, watoa huduma wa sekta ya nyumba kama makampuni ya nyumba, wachora ramani, bima, makampuni ya ulinzi, mikopo, bima, wakandarasi na wengine wengi watapata fursa ya kuelezea huduma wanazozitoa.

Tanzania Homes Expo, itazialika taasisi zinazohusika na ujenzi kushiriki kwenye maonyesho yajayo ili kutoa elimu kwa uma. Kuna msemo maarufu usemao ‘’kutokujua sheria haihalalishi kutenda kosa’’. Kwetu sisi tunaamini Tanzania Homes Expo inatoa fursa nzuri kwa jamii yetu kupata taarifa na kujua masuluhisho mbalimbali ya ujenzi”.

Kuhusu ushiriki wa makampuni kutoka Kenya, mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Bwana Zenno Ngowi alisema “Tunaamini kupanuka kwa wigo wa washiriki toka kwenye Nchi ya jirani kutatoa fursa ya Wananchi kupata masuluhisho mbalimbali ya ujenzi. Nishati mbadala, ni eneo jingine ambalo tunategemea kupata washiriki wengi wapya ambao watakuja kuonyesha masuluhisho mbalimbali ya nishati mbadala”.

Kwa taarifa zaidi au kushiriki tembelea tovuti; 

NHIF YASAIDIA HUDUMA YA MADAKTARI BINGWASOKOINE HOSP LINDI TAREHE 08 APR HADI 13 APR MNAKARIBISHWA

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Nhif akitoa taarifa fupi ya mfuko wa Bima ya Afya kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuhusiana na mpango endelevu wa kuleta madaktari Bingwa Mikoani
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Abdallah Ulega akikabidhi msaada uliotolewa na NHIF kwa hospital ya Sokoine.
Baadhi ya madaktari Bingwa wanaotoa tiba katika Hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Ufadhili wa NHIF.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi,Abdallah Ulega akizungumza wakati wa kuzindua tiba ya Madaktari Bingwa toka Muhimbili watakaotoa tiba kwa wateja wa Nhif na wasio wateja hadi tarehe 13 April 2013.

TBL yakabidhi mradi wa maji kwa wananchi Wilayani Same

$
0
0
Kandarasi wa ujenzi wa mradi kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania TBL .Godwin Kalaghe wa kampuni ya Dr Gogo engineering limited ya jijini Dar es salaam akimkabidhi mkurugenzi wa mahusiano na sheria wa TBL Stephen Kilindo taarifa za kukamilika kwa mradi huo.
Mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania katika kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi milioni 51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
Mkurugenzi wa mahusiano na sheria wa kampuni ya bia Tanzania TBL Stephen Kilindo akisaidia kumbebesha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Makanya Asia Zuberi kuashiria uzinduzi wa mradi wa kisima hicho cha Maji.

TRA yaikaba koo TFF,Yaitaka kulipa Deni lake Jumatatu ijayo

$
0
0
MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA), imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulipa deni lake la Shilingi 573 milioni kuanzia Jumatatu ijayo au wakate rufaa.

Habari zilizoifikia Globu ya Jamii zinasema kuwa TRA iliwasilisha barua ya kuitaka TFF kulipa fedha hizo juzi na kwamba iwapo TFF itashindwa kufanya hivyo basi wataitumia kampuni ya Majembe kupiga mnada mali za shirikisho hilo.

Chanzo hicho kimesema kuwa TRA ilifanya tathmini Machi 14 mwaka huu kutokana na ukaguzi wa hesabu za TFF na kukuta wana deni linalotokana na kodi (PAYE) na ongezeko la thamani (VAT) la jumla ya shilingi573 milioni.



"Hizo fedha zinatokana na deni la miaka mitatu ambazo ni kodi na pia mapato yatokanayo na makato ya mechi mbali mbali za Ligi Kuu ambazo zinafikia jumla ya kiasi hicho cha fedha."kilisema chanzo hicho

Alipoulizwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kuhusiana na suala hilo alisema kwa kifupi "Sijaona barua yoyote kutoka TRA" Mwishoni mwa mwaka jana TRA pia ilishikilia akaunti za TFF na moja kati ya akaunti hizo ilikuwa na shilingi milioni 300 za udhamini wa Vodacom ambapo TFF ilikuwa ikidaiwa shilingi157 milioni kama kodi za makocha wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' tangu kipindi cha enzi ya Mbrazil Marcio Maximo.

Kwa hali hiyo, TFF iliomba msaada wa serikali ambao ndio walipaji wa mishahara ya makocha wa Taifa Stars, na suala hilo tayari Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amos Makala alishaweka wazi kuwa suala hilo lipo kwenye hatua nzuri kwani linashugulikiwa Hazina na siku yoyote fedha hizo za makocha zitalipwa.

Balozi Kamala awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya Mhe. Jose Manuel Barosso

$
0
0
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Kamisheni ya Jumuiya ya Ulaya Mhe. Jose Manuel Barosso

mambo ya lugha iliyokuja kwa meli

UFAFANUZI KUHUSU SERIKALI KUWAPATIA WANANCHI SEHEMUKUBWA YA ENEO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME MKOANI DODOMA LEO

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia huku Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lendhardt wakimponegza kwa ishsra hiyo ya uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku akishuhudiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) Bw. Daniel Wolde Johannes na Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lendhardt wakishuhudia uzinduzi huo wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili ya serikali ya Marekani kupitia MCC leo April 10, 2013 katika kijiji cha Mkoka, wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma. 

TAFF NA BASATA TOENI ELIMU KWA WATENGENEZAJI WA FILAMU ZA KITANZANIA NA WAIGIZAJI KUHUSU UMUHIMU WA FILM FESTIVALS

$
0
0

Zanzibar International Film Festival(ZIFF) imedai kusikitishwa na muitikio hafifu wa watengenezaji/waigizaji wengi wa films za kitanzania kutowasilisha filamu zao katika tamasha hilo la kimataifa kitu ambacho ni wazi kuwa watengenezaji wengi wa films Tanzania hawajui maana na faida za film  festivals huku wengine wakiwa na hofu na kutojiamini kuhusu kazi zao wakati wenzao wa Hollywood na Bollywood huwa films zao nyingine zinaanza kuonyeshwa/kuzinduliwa rasmi katika film festivals nchi mbalimbali kabla ya kuingia rasmi sokoni. 

Ni aibu kwa watengenezaji wa films za kitanzania kutaka tamasha hilo litawaliwe na films za nje na wao wakibaki kushangaa tu halafu eti wanataka wawe wasanii wa kimataifa au kutambulika kama international film makers kutoka tanzania. TAFF ni lazima itoe elimu kwa watengenezaji wa films za kitanzania kuhusu umuhimu wa film festivals maana kuwaachia waandaaji wa ZIFF pekee watoe elimu haisaidii kwa kuwa yapo matamasha mengine kama haya nchi mbalimbali so ni vigumu wao kuja Tanzania na kutoa elimu, lakini TAFF ikiwa na lengo la kukuza tasnia hii itambulike kimataifa inawajibu wa kutoa elimu, sio TAFF tu hata BASATA kama taasisi ya serikali yenye dhima ya kukuza na kuendeleza sanaa nchini inawajibu wa kutoa elimu hii. Hollywood na Bollywoood wamekuwa wakichangamkia sana matamasha haya miaka kibao kwa kuwa wanajua faida zake kwa mtengenezaj husika wa film, waigizaji na film yenyewe. Hata South Africa imekuwa mfano mzuri wa kuchangamkia films festivals. Baadhi ya Faida kubwa za film festivals ni kama ifuatavyo..................

1. Kuunda mtandao wa kikazi(Networking), matamasha haya likiwemo ZIFF hukusanya watu mbalimbali na professionals wa films kutoka nchi mbalimbali hivyo ni rahisi kwa muigizaji au mtengenezaji wa filamu kufanya kazi kimataifa kwa kuwa wataalam wa mataifa mengine wanaweza kuvutiwa na kazi zake hivyo kuingia mikataba ya kikazi.

2. Kukutana na wasambazaji wa kimataifa wa films. wasambazaji wa kimataifa wa films pia huwepo katika matamasha haya wakiangalia vipaji na kazi mpya hivyo producers wa Tanzania wanaweza kupata mikataba mizuri ya kusambaza kazi zao kimataifa na kuepukana na wimbo wa kuwa tunanyonywa na wasambazaji wa sasa.

 3. Kupata tuzo(awards), tuzo ni sehemu ya kujali na kuthamini kazi bora so kitendo cha film, director au actor kupata tuzo kinazidi kumpa thamani na kupaa zaidi ndani na nje ya nchi hivyo kukuza CV yake na mataifa mengine yanayotengeneza films ni rahisi kumfuata ili wafanye kazi pamoja.

4. Kutangaza vipaji vipya. Vipaji vipya hutangazwa katika matamasha haya hivyo kama new film, new director or actor akipata tuzo ni rahisi sana kupata attention kitaifa na kimataifa as an actor or director hivyo kufanikiwa haraka katika kazi zake.

5. Kuzidi kuvutia na kuhamasisha kampuni kubwa za ndani na nje ya nchi ziwekeze katika tasnia ya film. ni wazi kuwa kwa sasa hakuna wawekezaji wazuri kwenye industry lakini kupitia film festivals wawekezaji wa ndani na wa kimataifa ni rahisi kuvutiwa na kuwekeza kwenye tasnia ya film Swahiliwood hasa kwenye usambazaji na production kitu ambacho ni rahisi kuleta mapinduzi katika tasnia hii hasa ukichukulia kuwa utafiti usio rasmi na ulio rasmi tayari unaonyesha kuwa nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Africa zinapenda filamu za kiswahili lakini haziwafikii kwa kuwa hakuna wasambazaji wa kuzifikisha huko.

6. Serikali inaweza kushawishika zaidi ikiona kuwa tasnia hii inakubalika na kutoa ajira kwa vijana wengi so itatilia mkazo zaidi katika  kulinda haki za wasanii na hata kusaidia katika maeneo kama vile kupunguza kodi na hata kusaidia kwenye usambazaji ili ikusanye mapato zaidi tofauti na sasa ambapo serikali imejawa na maneno zaidi kuliko vitendo halisi.

7.Kukuza soko la utalii na ku-promote utalii, mara nyingi watalii hupenda kutumia pesa hivyo wakisikia kuna film festival huenda kwa wingi kushuhudia local talents hivyo hununua kazi zinazowavutia na kwenda nazo kwao na huko huzidi kutangaza films husika na hata kushawishi wawekezaji wa kwao waje nchi husika kuwekeza katika tasnia husika.

Ras Makunja aokoa jahazi

$
0
0
 Kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa Mkoa wa Dodoma kina mbwa wengi sana. Mmoja wao alikatisha katikati ya kadamnasi leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa miundombinu ya kusambaza umeme mkoani Dodoma chini ya ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Mfuko wa Changamoto za millenia (MCC) ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Mradi huo utanufaisha jumla ya vijiji 16 vya Dodoma kuwa na umeme wa uhakika
 Baada ya kuona mbwa huyo akielekea jukwaa kuu, Ras Makunja mmoja akajitokeza na kuzuia tafrani ambayo ingejitokeza endapo mbwa huyo angetinga jukwaa kuu...
Akionesha ukakakamavu wa hali ya juu Ras Makunja huyo aliweka mambo sawa kwa kumwelekeza mbwa huyo kwengineko. Ni tukio la sekunde tatu lakini Kamera ya Globu ya Jamii iliweza kurekodi kila hatua kama inavyoonekana....

VILLA FOR LEASE IN ZANZIBAR


Blue Ocean Strategy, Innovation and Competitive Intelligence Outsourcing Services

Watanzania Ujerumani kusherekea miaka 49 ya Muungano,Mjini Kolon

Article 13

VIDEO YA "" KUNATATIZO KWANI" BY KINGKAPITA FT. GODZILLA

$
0
0
HIT MAKER KINGKAPITA TOKA TANZANIA TENA NA TENA KATIKA UJIO MPYA NYIMBO ALIOFANYA NA GODZILLA KUTOKA STUDIO YA DEFATALITY PALE KWA MESSEN SELEKTA

NYIMBO INAITWA "KUNATATIZO KWANI"
HII SASA NDO VIDEO YAKE AMBAYO INAPATIKANA YOUTUBE KWA SASA KWA LINK HII


IKIWA IMEBEBA LINE KALI ZA KUELIMISHA NA KUBURUDISHA JAMII KAMA :
"BABA JAMBAZI MAMA CHANGUDOA MTOTO KAZALIWA KONDA OTEA NINI KITAFATIIA//"
//HII BAHATI HAIZIMWI KWA MIDOMO FORM SIX ALIPATA ZIRO NA LEO NDO BOSS WAO//
                              
     "KUNATATIZO KWANI"
HAPO NI KATIKA KUWAPA MOYO WOTE WALIOPATA MATATIZO KWENYE KUTAFUTA WAKA FAIL WASIKATE TAMAA NA MAISHA BADO YANAWEZEKANA PIA KUNA LINE KAMA
       //MI MKRISTO WEWE MWISLAM HAIJALISHI DINI GANI TUDUMISHE HII AMANI//
                                    "KUNATATIZO KWANI"
 HAPO NIKIWA NAELEZEA KUHUSU MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

KINGKAPITA ANANYIMBO HIT NYINGINE NYINGI KAMA:
1.MTOTO MLITO
2.MTOTO WA FISADI
3.SHIKAMOO PESA
NA SASA NAOMBA MSIKILIZE 4. KUNATATIZO KWANI IKIWA KAMA MSEMO MPYA KATIKA JAMII ETI KUNATATIZO KWANI???

HARAMBEE YA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI MOROGORO (WAVUMO) YAFANA!!

$
0
0
Tarehe 10/04/2013 taasisi ya wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro (WAVUMO) ambayo ni shirika lisilo la kiserikali na lisilotengeneza faida, waliandaa harambee kwa maendeleo na kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Ukimwi kwamba Ukimwi sio tatizo la Afya tu bali linahusu maendeleo ya Jamii kwa ujumla. Harambee hiyo yenye nia ya kujikwamua badala ya kutegemea wafadhili kutoka nje iliweza kufanikiwa kupitia watu na jamii mbalimbali ya Morogoro kutokana na mioyo yao mizuri na kwa michango yao. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mkuu wa Mkoa aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI. 

Shirika ili la Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro (WAVUMO) pia liliandaa chakula cha usiku katika kufanikisha harambee hiyo. kauli mbiu ilikuwa, "MLO WA JIONI KWA KUOKOA MAISHA / A DINNER A LIFE SAVED". Harambee hii ilifanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha 11,000,000/=, mradi wa soda kreti 15, friji kubwa, meza mbili na viti nane kutoka pepsi, vilevile ilifanikiwa kupata plot za Ardhi kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga ambacho kitakuwa kinaendelea kutunisha mfuko wa WAVUMO. 

Shirika la WAVUMO linawanachama zaidi ya 500 na linahudumia wagonjwa wa Ukimwi zaidi ya 3000 kwa manispaa ya Morogoro. Shirika lina miaka 12, kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti Bw. Ally Ramadhani. 

Kwa maelezo zaidi kuhusu harambee hii na taasi ya WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI MOROGORO (WAVUMO), Wasiliana nao kupitia +255 714 255 688, au +255 767 245 688.

Zoezi la Harambee likiwa limefunguliwa rasmi na Mgeni rasmi, kutoka kulia ni Mratibu wa Harambee, Mourine-Hawa Msangi na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI.

Mr. Signfrid Kayombo na Mr Mujungu Wajama ambao ni Wawakilishi kutoka TUNAJALI wakiotoa mchango wao.

Mr. Juma Ayoub Bitagera kutoka NIC akitoa mchango wao.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images