Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 987 | 988 | (Page 989) | 990 | 991 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Msanii Nyasa Boy kutoka Rock City Mwanza

  Na:George Binagi-GB Pazzo
  Nyasa Boy ni Msanii wa Kizazi kipya kutoka Jijini Mwanza ambae anachipukia vizuri sana.
  Katika audio ya wimbo huu unaoitwa Chongoroa, Nyasa Boy amewashirikisha Wasanii Mc.Darada pamoja na D'Maladha wote pia kutoka Jijini Mwanza.
  BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

  0 0

  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya nane ya Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Rebu iliyopo Wilayani Tarime George Obuto ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Wilaya hiyo akizungumza katika Mahafali hayo.
  Mgeni Rasmi akikabidhi cheti kwa mhitimu
  Mhitimu akipokea cheti. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0
 • 09/25/15--21:07: DAR ES SALAAM TAMBARARE


 • 0 0

   Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
   Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
  Na Mwandishi Wetu,


  MTANDAO  wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika katika usafirishaji wa mizigo. 

  Usafirishaji nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na maji na anga.  Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”

  Wakati ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake, kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.

  0 0

  TAARIFA
  Assalamu Alaykum: Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Allah Subhanahu Wa Taala kwa kutujaalia kuwa wazima na kuadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-Adh-ha ya mwaka 1436H (2015). 
  Idd Al-Adh'ha ni Siku Kuu kubwa kati ya Siku Kuu mbili katika Uislamu, ni siku ya furaha, kwa familia na jamii kwa ujumla. Kwa niaba ya Uongozi wenu wa ZADIA, naungana na WanaZadia wote, Wazanzibari, na Waislamu kwa ujumla katika kuadhimisha siku hii adhimu.
  Kwa vile hii ni Siku Kuu Kubwa, furaha yangu ingekuwa kubwa zaidi katika kusherehekea. Hata hivyo, furaha hiyo imeingia doa kutokana na maafa yaliyowakumba ndugu zetu Waislamu waliofunga safari kwenda kuhiji, kuitikia wito wa Mola Wao Mlezi wa kuizuru Nyumba Yake
  Tukufu.
  Kutokana na hilo, napenda kuchukua fursa hii kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Waislamu wote ulimwenguni ambao wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki katika maafa hayo.
  Tunamuomba Allah awaingize wenzetu waliotangulia peponi kwa Rehma zake. Kama ambavyo, natoa pole kwa Mahujaji wote waliopata ajali na kujeruhiwa, na kumwomba Allah SWT awape afya na uzima na kuwarejea katika familia zao wakiwa katika afya na uzima.
  Ndugu Wanazadia na Wazalendo kwa ujumla,
  Huku tukiwa tunaendelea kusherehekea Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha, napenda kuwakumbusha kuhusu majukumu ya kila mmoja wetu ya kuendeleza umoja, mshikamano na amani katika Jumuiya yetu na nchi yetu Zanzibar kwa ujumla. Na hakuna njia nyepesi ya kufikia malengo hayo ispokuwa kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu.
  Tujifunze kutokana na somo la Hijja ambalo Waislamu kutoka sehemu zote duniani hukutan sehemu moja wakiwa katika vazi la aina moja kwa ajili ya kuabudu Mola mmoja, bila kujali kabila, nchi wanazotoka, umri, jinsia, vyeo au tofauti nyenginezo. Wote wako sawa wakiwa na lengo moja.
  Siku Kuu hii kwa mwaka huu inakuja ikiwa imebakia si zaidi ya mwezi mmoja kabla Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuingia katika Uchaguzi Mkuu. Mara tu baada ya kumalizika kwa shamra-shamra za Siku Kuu, akili, macho na masikio yetu yote yataelekea kwenye kampeni za uchaguzi na vioja vyake.
  Kwa hivyo, nasaha kwetu sote, wadau wote, kulitumia funzo tulilolipata katika Hijja na Siku Kuu yake kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa njia moja au nyengine kuufanya uchaguzi ujao upite kwa salama na amani kama ulivyopita ule uliotangulia wa mwaka 2010. Tukumbuke kuwa Umoja ni nguvu na Utengano ni Udhaifu. Kwa hivyo, kampeni na ushabiki wetu wa kisiasa vyote vilenge kwenye kuendeleza Serikali ya Umoja Wa Kitaifa Zanzibar na kuipa nguvu Zanzibar kuleta maendeleo.
  Ikumbukwe kuwa, Malengo Makuu ya ZADIA ni kuleta umoja wa Wazanzibari na Maendeleo yao nje na ndani ya nchi yetu tuipendayo. Hata hivyo, malengo hayo hayawezi kufikiwa bila kuwa na amani, usalama na utulivu ndani ya nchi yetu ya Zanzibar na hata Jamhuri yote ya Muungano wa Tanzania.
  Kila mmoja wetu ajaribu kuyalinda malengo hayo kwa kuzingatia kauli ya Bwana Mtume SAW aliposema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya kile anachokichunga".
  Nawatakia Idi Njema, nawapa pole wafiwa na nawaombea majeruhi shifaa.
  Omar H. Ali,
  Mwenyekiti,
  ZADIA.

  0 0

  Rais wa Simba Sport Klabu Evans Aveva (Kulia) akiwa na afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani kajula wakati wa Uzinduzi wa tunzo za Mchezaji bora wa Mwezi .
  Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabuya Simba imeanzishaTunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015. 
  Akizungumza jijini Dar es salaam Raiswa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenziwa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu  yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu  ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora. Tunaamini kuwaTunzo yaMchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha  kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma  zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.

  Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenziwa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitiamtandaowaVoda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wamweziwa Simba’’
  Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ilikuwapa  wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiungana Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

  Jinsi ya kumchagua mechezaji bora wa mwezi September 2015.

  1. Jiunge na Simba News kwa kutuma neno Simba kwenda namba 15460.

  2. Tuma jina la mchezaji kwenda namba 15460.


  Kwa maelezo zaidi tembelea www.simbasports.co.tz

  0 0

  Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakimsikiliza  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kujinadi kwa kuwaomba wampigie kura ya ndio asubuhi na mapema Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu,ili aibuke mshindi na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Waananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.

  Dkt.Magufuli Ijumaa  amefanya mikutano yake ya kampeni  katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita  na baadae halmashauri mpya ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni  uliofanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na umati wa watu uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV.

  Akizungumza katika mikutano hiyo  wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu kumpigia kura za ndiyo, Dkt Magufuli amesema kuwa Serikali yake itashughulikia migogoro ya madereva na kuhakikisha wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao ili kuboresha maslahi yao.
  Amesema Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu,lakini maslahi yao hayatiliwi maanani,hivyo amesema kuwa atahakikisha yanaboreshwa ili na waone faida ya kazi yao,na iwe yenye kuthaminika ,hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli italifanyia kazi ipaswavyo.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Bukombe mapema Ijumaa mchana, alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
   Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama Ijumaa jioni  kwenye mkutano wa kampeni za Urais uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu. Mh.Sitta a.k.a Mzee wa viwango na kasi pia alimnadi Dkt Magufuli na kumwombea kura kwa wananchi hao za ushindi na hatimaye akaibuke mshindi kwa nafasi ya Rais na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
   Maelfu ya wananchi wa mji wa Kahama wakiwa wamekusanyika mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama Ijumaa jioni.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Wachimbaji wadogo wadogo waishio eneo la Nyarugusu,Wilayani Geita wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mapema leo jioni alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake.

  PICHA NA MICHUZI JR-KAHAMA SHINYANGA

  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

  Na John Gagarini, Chalinze 
  HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo imeshauriwa kuisitisha mikata ya umiliki wa ardhi iliyochukuliwa na wawawkezaji ambao hawajaiendeleza ardhi hiyo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 wairejeshe kwenye serikali za vijiji kwa ajili ya matumizi ya umma. 
  Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete wakati wa mikutano ya hadhara ya kampeni kwenye Vijiji vya Makombe na Kinzagu kwenye kata ya Lugoba na kusema kuwa wamiliki hao kama wameshindwa kuiendeleza ardhi hiyo ni vema wakairudisha kwa wananchi.
   Ridhiwani alisema kuwa inashangaza kuona kuwa wananchi kwenye vijiji hivyo wamekuwa wakihangaika kutafuta ardhi kwa ajili ya kilimo pamoja na matumizi mengine lakini wanakosa maeneo ambayo yamehodhiwa na watu wachache. 
  “Kwa sasa ni vema halmashauri zikasitisha mikata ya umiliki wa ardhi hiyo kutokana na kushindwa kuiendeleza kwa kipindi cha miaka zaidi yha 10 ambapo sheria inataka mwekezaji kuiendeleza ardhi ndani ya kipindi cha miezi 32 na endapo atashindwa kuiendeleza anaweza kufutiwa umiliki,” alisema Ridhiwani. 
  Alisema kuwa haipendezi kuona wananchi wanahangaika kutafuta maeneo huku baadhi ya watu wakiwa wamehodhi maeneo bila ya kuyaendeleza na kuacha yakiwa mapori ambayo yanahatarisha usalama wao.
   Diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
   Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Sehemu ya wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Msanii Hafsa Kazinja akitumbuiza huku akicheza na mshabiki mbele ya  wakazi wa Kijiji cha Makombe wakati wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  0 0

  Ch10: Tafiti za uraisi zaendelea kutofautiana na kuzua maswali tata! fuatilia hilo na mengine mengi kupitia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/iWBNxVRs8l0
  Star tv:Tafiti mpya yampaisha lowassa je kulikoni? tazama uchambuzi wa kina wa magazeti na simu.tv. Tazama. https://youtu.be/w2bHdFxxqWM
  Tbc:Je nini kimejiri kunako ulingo wa siasa na mbio za kampeni kuelekea uchaguzi mkuu? Tazama uchambuzi wa Magazeti hapa. https://youtu.be/9hNTcAdohig

  0 0

  Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha Helikopta yake ya kwanza inayozunguka kwenye kila pembe ya nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais. Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Field Marshall  Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia Ushindi wa kishindo. 
   Makada imara wa CCM  Field Marshall Mwigulu Nchemba na Dkt. Hamis Kigwangalla waki-Magufulika kuonesha sapoti kwa Mgombea wao Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
  Field Marshall Mwigulu Nchemba akilakiwa kwa nderemo mjini Nzega
  Dkt Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Nzega Mjini.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Field Marshall Mwigulu NChemba ambaye  ameanza safari za Anga-kwa-Anga kusaka kura Nchi nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI TU na rafiki yake Mkubwa ni TANZANIA. Comrade  Mwigulu amesema, Uchaguzi wa mwaka 2015 ni mwepesi sana kwa CCM  kwa kuwa wagombea wote ni zao la Chama tawala  na wanawajua vizuri. 
   Mbunge Ubunge wa jimbo la Nzega Mjini Ndg. Hussein Bashe akizungumza na Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini. Bashe amewaomba Wana-Nzega kumpatia ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega, Kusimamia haki za Bodaboda na Mamantilie wa Nzega, shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi wa Taifa letu.Mbunge Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe. Picha zote na Sanga Festo Jr. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwigizaji mchekeshaji nyota King Majuto akiwa na mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na Yanga Sunday Manara 'Computer' wakiwa mjini Makka wakati wa Hijja. Hawa ni miongoni mwa Watanzania  walionusurika katika maafa ya msongamano wa watu Mina juzi uliochukua maisha ya mahujaji zaidi ya 700 kutoka kila pembe ya dunia.

  0 0
  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa 70 wa Umoja wa Maiataifa akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi  Liberata Mulamula 
   Rais Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Lars Loekke Rasmussen 

   Rais Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Finland Mama Tarja Halonen

   Rais Kikwete na ujumbe wa Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje na ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee,  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi  Liberata Mulamula na .Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.

   Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Bahamas Mhe Perry Christie. Hapo Mhe Rais alimfahamisha Waziri Mkuu huyo kwamba yey anamaliza muda wake na Waziri Mkuu akaeleza matumaini yake kwamba atakayemrithi ataendelea kuimarisha uhusisno wa Tanzania na Bahamas na nchi za Caribbean.  
  Rais Kikwete akiwa na Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Mzumbiji na mawaziri wao wa nchi za nje
  Rais Kikwete na Ujumbe wake wakimlaki Baba Mtakatifu Francis alipowasili kuhutubia Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza. Picha kwa hisani ya Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na kiongozi wa Ujerumani Kansela  Angela Merkel kwenye ubalozi wa kudumu wa Ujerumani Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Ijumaa  jioni.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi nchini Marekani ambapo mbali na kukutana na wadau wa Maendeleo anatarajiwa kutoa hotuba yake katika kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umioja wa Mataifa(UN General Assembly
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kiongozi wa Ujerumani Kansela  Angela Merkel kwenye ubalozi wa kudumu wa Ujerumani Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Ijumaa. Picha na Freddy Maro.


   ------------------------------------
  JK: Kampeni zinaendeshwa kwa uhuru wa kumwaga kabisa

  ·         Afafanua kuwa Tanzania inataka mchakato utakaozaa uchaguzi huru na wa haki


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  Ijumaa, Septemba 25, 2015 amemwambia Kiongozi wa Ujerumani, Kansela Angela Merkel kuwa upo uhuru mkubwa na usiokuwa kifani kwa vyama vyote ya siasa kufanya kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, 2015.


  Aidha, Rais Kikwete amemwambia Kansela Merkel kuwa Jopo la Watu Mashuhuri Duniani linalotafuta kufanya mapendekezo ya jinsi dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kwa magonjwa ya milipuko, sasa linakaribia kumaliza kazi yake na lipo katika hatua ya kuandaa mapendekezo kuhusu nini dunia ifanye katika siku zijazo.


  Rais Kikwete amekutana na kuzungumza na Kansela Merkel katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York na kuombwa na Mama Merkel mwenyewe. Viongozi hao wawili wapo New York, Marekani kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly (UNGA).


  Katika mazungumzo hayo, Kansela Merkel alitaka kujua kutoka kwa Rais Kikwete kuhusu mwenendo mzima wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea nchini na uhuru unaotolewa kwa kila chama kufanya kampeni zake.


  “ Kama unavyojua Mheshimiwa Kansela tuko katikati ya Kampeni ya Uchaguzi Mkuu. Kampeni zinakwenda vizuri. Tunao wagombea wa urais nadhani kiasi cha wanane hivi na kila chama kinaendesha kampeni zake kwa uhuru mkubwa na usiokuwa na kifani. Tunataka mchakato ambao utazaa uchaguzi huru na wa haki na hivyo ni muhimu kwa kila chama kuendesha shughuli zake za kampeni kwa uhuru,” Rais Kikwete amemwambia Mama Merkel.

  Rais pia amemwambia Kansela Merkel kuhusu baadhi ya mambo makubwa ya kampeni yakiwemo mambo yanayohusu masuala ya huduma za kijamii kama vile afya, elimu na mapambano dhidi ya umasikini. “Kampeni zote kwenye ngazi zote – ngazi ya urais, ngazi za wabunge na ngazi za Serikali za mitaa zinakwenda vizuri kwa uhuru wa kumwaga kabisa.”

  Rais Kikwete pia ametumia mkutano wake na Kansela Merkel kumweleza Mama huyo kuhusu kazi ya Jopo ya Watu Mashuhuri Duniani kuhusu Matatizo ya Afya akisisitiza kuwa baada ya hatua ya kuwasilikiza watu mbali mbali, sasa Jopo limeanza kuandaa maoni yake na mapendekezo.

  Jopo hilo ambalo liliteuliwa Aprili mwaka huu na Katibu Mkuu wa UN Mheshimiwa Ban Ki Moon kufuatia majonzi makubwa yaliyosababishwa na ugonjwa wa Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone, linatarajiwa kukabidhi ripoti yake kwa Mheshimiwa Ban Ki Moon Desemba mwaka huu.

  Ujerumani ni moja ya nchi zinazoongoza dunia katika kuunga mkono na kugharimia shughuli za Jopo hilo na pia imewekeza fedha nyingi katika kugharimia uboreshaji wa mifumo ya afya katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.


  Baadaye usiku, Rais Kikwete alikuwa mmoja wa viongozi wa nchi nane duniani ambao wamehudhuria chakula cha usiku ambacho kimeandaliwa na Kansela Merkel kwa ajili ya viongozi ambao wanaunda kundi la nchi ambazo zimekubali kubeba wajibu wa kuhakikisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals –SDG) ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) ambayo muda wake wa utekelezaji wa miaka 15 umemalizika.


  0 0


  0 0  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  WANAFUNZI waliosoma  Shule ya Forodhani na Sasa St.Joseph Cathedral  wameanzisha  umoja wa shule hiyo kwa ajili ya kusaidia elimu pamoja na masuala ya kijamii.


  Wakizungumza nyakati tofauti wanafunzi waliosoma hapo wamewataka wanafunzi kufuata nyayo zao kutokana na shule hiyo kuwa na historia nzuri ambayo hadi sasa haijaweza kufutika.


  Wamesema kuwa umoja huo utakuwa imara katika kusaidia shule hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo na kusaidia jamii kutokana na malezi walioyapata katika shule hiyo tangu Ukoloni.


  Akizungumza katika uzinduzi huo mwanafunzi aliosoma shule hiyo,Mariam Zialor, amesema umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent school  iliodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969, na Forodhani Sekondari  ilokuwapo 1970 hadi 2008 ( ilitaifishwa na serikali) na baada ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurushwa kwa kanisa la katoliki)  hadi leo inatambulika   St. Joseph & Forodhani  ALUMNI .

  Miriamme amesema katika shule hiyo  kuna wanafunzi waliosoma shule hiyo, wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka  Canada, Australia, New Zealand Uingereza na Seychelles wameungana kuhudhuria mkutano huu wa kishitoria wa kuanzisha umoja wa ALUMNI.


  Amesema baadhi ya wanaWengine hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30.  Wanarudi kuona shule iliowalea.


  Aidha amesema katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles  ambaye alisoma hapo na kumaliza kidato cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo  kuendelea na masomo ya juu.


  Kwa upende wa Mbunge wa Viti Maalumu ,mwanafunzi wa shule hiyo zamani Ashymaa Kwegyry ametaka wanafunzi kuwa wadhubutu na kuweza kufanikisha ndoto zao.


  Amesema amesoma shule kutokana na kuwa na ulemavu lakini walimu walimfundisha na kuamini kuwa na anaweza kufanya kitu kama binadam wengine.
  Mwanafunzi wa Zamani wa Forodhan,Mariam Zialor akizungumza wakati wa uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma shule ambayo kwa sasa ni St.Joseph Cathedral leo jijini Dar es Saalaam.
  Mwananfunzi wa zamani wa shule ya Sekondari ya St.Joseph hivi sasa, Ashymaa Kwegyry akizungumza katika uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph walioshiriki katika uzinduzi wa umoja wa wanafuzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph zamani wakiwa wameshuriki katika uzinduzi wa wanafunzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Wanafunzi wakitumbuiza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai mara baada ya kucheza ngoma inayowakilisha kabila la wamasai katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo. 
  Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph 
   Picha ya pamoja ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph mara baada ya kumalizika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Telephone: 2863748/2860485,

  Fax: 0255 - (022) 286 0486

  Websitebasata.or.tz

  CONTACTS

  P.OBox4779,

  BASATA Arts CentreIlala Sharif Shamba,.

  Dar es SalaamTanzania

  National Arts Council BASATA  26/09/2015   

  PRESS RELEASE

  BASATA KURUDISHA HADHI YA MUZIKI WA REGGAE

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House iliyo chini ya Msanii Mkongwe wa reggae Innocent Nganyagwa limeandaa programu maalum kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini.


  Programu hiyo ambayo itafanyika makao makuu ya BASATA yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Tarehe 28/09/2015 kuanzia saa 4:00 hadi saa 6:30 Mchana kupitia Programu ya Jukwaa la Sanaa, itakuwa mahsusi kwa ajili ya kuurudisha muziki wa reggae jukwaani, kujadili mwelekeo wa muziki huu na kuja na mikakati bora ya kuurudishia hadhi yake.


  Ieleweke kwamba katika siku za karibuni muziki huu wa reggae umekuwa umeganda na kutokupiga hatua kubwa hali ambayo imewafanya wadau wa muziki kukosa burudani ambayo wamekuwa wakiipata huko nyuma kupitia kwa wasanii wakongwe kama Innocent Nganyagwa, Innocent Garinoma, Justine Kalikawe na wengineo.


  Changamoto kubwa si tu ni muziki huu kutochezwa kwenye vyombo vya habari bali pia kuna changamoto ya wasanii wenyewe kutokubadilika na kutengeneza muziki unaokwenda sambamba na soko pia hitaji la mashabiki.


  Ni nia ya BASATA kuona wasanii na wadau wote wa muziki nchini wanahudhuria programu hii mahsusi kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja hatma ya muziki wa reggae, kupata historia ya jinsi ulivyokuwa huko nyuma, kutazama na kuburudika Jukwaani na muziki wa mmoja wa wasanii wakongwe wa muziki huu.


  BASATA linaamini kwamba baada ya programu hii wasanii wa reggae na wadau kwa ujumla watakuwa na mwanzo mpya katika kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini na kuhakikisha unaendelea kudumu.

  Sanaa ni Kazi, tuikuze, tuitunze na kuithamini


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI BASATA

  0 0

  Mwenyekiti Kamati ya maandalizi ya Amani kuelekea uchaguzi mkuu, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa waimbaji solly Mahlangu wa Afrika Kusini na Ifeanyi Kelechi wa Uingereza kutumbuiza matika tamasha hilo.
  Aidha Msama amesema kuwa katika Tamasha hilo Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete.
  Kulia ni Mratibu wa maandalizi ya Tamasha la  kuombea amani kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, Khamis Pembe.

   Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa maandalizi yamekamilika pia waimbaji wa nyimo za Injili wa nje ya nchi wataanza kuingia hapa nchini.

  Msama aamesema kuwa viingilio ni kama kawaida hakuna mabadiliko yoyote kwa watoto watachangia shilingi 1000 na watu wazima na viti vya kawaidi shilingi elfu 3000  na VIP ni shilingi elfu 5000
  pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani katika nchi yetu.

  Aliongeza kuwa  katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagiza maombi hayo kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

  Aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.

  0 0

    Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akizungumza na viongozi  na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe leo  kabla ya kukabidhi msaada wa  shuka 176 kusaidia wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
   Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akikabidhi msaada wa shuka 176 kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela (kulia) leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na uhaba wa mashuka.
   Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya  wilaya ya Kisarawe  Dkt.Martin Msokelo(kulia) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige kwa pamoja wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE kwenye  wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
  Wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe wakifurahia msaada wa mashuka yaliyotolewa kwa wagonjwa na Chuo cha Elimu ya Biashara, CBE leo.
  Picha/Aron Msigwa - MAELEZO.

  Aron Msigwa -MAELEZO.
  WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga utamaduni  wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata katika kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

  Wito huo umetolewa leo mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof.Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa shuka 176 zilizotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

older | 1 | .... | 987 | 988 | (Page 989) | 990 | 991 | .... | 3286 | newer