Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 986 | 987 | (Page 988) | 989 | 990 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Wasanii kutoka Rock City Mwanza wanaounda kundi la TANZANIA ONE MUSIC ambapo kushoto ni D'Maladha, Katikati ni Lady Shushu na Kulia ni Nyasa Boy.
  Na:Binagi Media Group
  Ukiwataja wasanii wanaofanya vizuri kutoka Jijini Mwanza, lazima utawataja Nyasa Boy, D'Maladha pamoja na mwanadada Lady Shushu ambao wanaunda kundi la Tanzania One Music ambalo tayari linatesa na ngoma mbili sokoni.

  Wasanii hao kupitia kundi hilo, wameweza kuliteka soko la Muziki wa Mwanza kupitia ngoma zao mbili ambazo ni Nasema Nawe (Bonyeza HAPA Kuitazama) pamoja na Thamani ya Penzi (Tazama Hapo Chini).
  Tazama Thamani ya Penzi hapa chini

  0 0

  Msafara wa Gari za  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein zikiongozwa na mapikipiki wakati ukiwasili katika Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskzani A Mkoa wa kaskazini Unguja palipofanyika mkutano wa baraza la Eid EL Hajj leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo
   Mke wa Makamo wa Pili wa rais wa zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (mwenye miwani) pamoja na Viongozi wengine mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa  Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi katika baraza hilo akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
   Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein

  Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
   Baadhi ya Viongozi wengine na Wazee na wananchi walioalikwa katika mkurano wa Baraza la Eid El Hajj wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wialaya ya Kaskazini A mkoa wa kakskazini Unguja,palipofanyika Baraza  hilo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj wakati mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa hutuba yake kwa wananchi wa Zanzibar katika Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini  Unguja ikiwa ni katika sherehe za Sikukuu ya Eid El Hajj,[Picha na Ikulu.] 

  0 0

  Vinara wa biashara Afrika walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika picha ya pamoja. Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa, Helen Hai na Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika hoteli ya Four Seasons Hotel mjini New York.
  Picha na African Business. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote speech during the 10th  Africa Travel Association  Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
   Some of the delegates to the 10th ATA Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the Minister for Natural Resources and Toursim Hon. Lazaro Nyalandu during the 10th  Africa Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center.
   The Director Africa House and Economics Professor at the  New York University Yaw Nyariko presents souvenir gift to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete during the 10th  Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in New York this morning. Center is the Minister for Tourism and Natural Resources Hon. Lazaro Nyalandu.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in a group photo with panelists and coordinators of the ATA 10th Annual Presidential Forum on Tourism  held at at New York University Kimmel Center in United States of America this morning. From left Executive Director Africa Travel Association(ATA) Mr. Edward Bergman, Namibia’s Minister for Environment and Tourism Hon. Pohamba Shifeta,(second left), Kenya’s Cabinet Secretary in the Ministry of East African Affairs, Commerce and Tourism Hon. Phyllis Kandie(Third left),  Mali’s  Minister for Culture, Crafts and Tourism Hon. N’Diaye  Ramatoulaye Diallo(fourth left),The President, The Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu, Director Africa House and Professor of Economics Dr. Yaw Nyarko(seventh left), ), Uganda’s Minister for Tourism Wildlife and Antiquities Hon.Dr. Maria Mutagamba,(eight left) and the panel moderator who is also the CBS News Travel Editor Mr. Peter Greenberg(photos by Freddy Maro)
  -------------------------------------------------------------------
  Rais Kikwete afafanua changamoto za utaalii wa Afrika

  ·         Asema habari hasi kuhusu Afrika zinavuruga utalii wa Afrika


  ·         Asisitiza Tanzania itaendelea kupambana na ujangili  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea changamoto kubwa zinazozuia kukua haraka zaidi kwa sekta ya utalii katika Afrika na hivyo kuliwezesha Bara hilo kuchuma matunda makubwa zaidi kutokana na sekta hiyo.

  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, Bara la Afrika, bado linabakia nyuma kwa kiasi kikubwa katika kuvutia watalii wa kimataifa na katika mapato yanayotokana na utalii.

  Rais Kikwete vile vile amesema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa ajili ya hifadhi na pia itaendelea kukabiliana na ujangili dhidi ya tembo, ambao hata hivyo amesema kuwa umepungua katika mwaka uliopita.

  Rais Kikwete ameyasema hayo leo, Alhamisi, Septemba 24 wakati alipotoa hotuba ya ufunguzi wa shughuli za Miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika – Africa Travel Association (ATA) na Miaka 10 ya Jukwaa ya Rais Kuhusu Utalii – Presidential Forum on Tourism kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York (New York University Kimmel Center) Africa House, mjini New York.

  Rais Kikwete yuko New York, Marekani kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambavyo pia vilifanyika New York.

  Rais Kikwete ametambulishwa na kukaribishwa kutoa hotuba yake na Dkt. Yaw Nyarko, Raia wa Ghana na Mkurugenzi wa Africa House ambaye pia ni Profesa wa Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha New York na Bwana Edward Bergman, Mkurugenzi Mtendaji Mwanzilishi wa ATA.

  Alikuwa ni Rais Kikwete na familia ya Bergman ya New York ambao walianzisha na kujadili wazo la  kuanzishwa kwa chama hicho miaka 10 iliyopita.

  Kabla ya kutoa hotuba yake, washiriki wa Kumbukumbu hiyo ya miaka 10 wamesikia maelezo ya kina kutoka kwa mawaziri wa nchi tano za Afrika kuhusu hali ya utalii katika nchi hizo na katika Bara la Afrika kwa jumla.

  Mawaziri waliozungumza kwenye shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bwana Peter Greenberg, Mhariri wa Usafiri wa Televisheni ya CBS ni Mheshimiwa Lazaro Nyalandu wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Maria Mutagamba, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Nyaraka wa Uganda ambaye pia ni Rais wa ATA na Mheshimiwa N’Diaye Ramatoulaye Diallo, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Usanii wa Vinyango wa Mali.

  Mawaziri wengine ambazo wamezungumza katika shughuli hiyo ni Mheshimiwa Phylis Kandie ambaye ni Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya na Mheshimiwa Pohamba Shifeta, Waziri wa Mazingira na Utalii wa Jamhuri ya Namibia.

  Akizungumza katika shughuli hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa changamoto kuu zinazokabili maendeleo ya utalii katika Afrika ni miundombinu ya kitalii, utangazaji wa masoko ya utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.”

  “Lakini pia kuna jambo kubwa la mtazamo hasi kuhusu Afrika. Kwa kawaida, vyombo vya habari vya nje vinalielezea Bara la Afrika kama Bara hatari ambalo sifa zake kuu ni migogoro, magonjwa na matatizo yanayotokana na umasikini. Haya yote siyo ya kweli ni upotoshaji wa makusudi.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na sisi wenyewe. Picha inayojengwa kuwa tatizo katika nchi moja ni tatizo la Bara zima siyo ya kweli na lazima itafutwe namna ya kulisahihisha jambo hilo. Afrika ni Bara la nchi 54 na siyo nchi moja ya majimbo 54.”

  Ameongeza: “Ni upotoshaji huu ambao ulisababisha watu kufuta safari za kitalii kwenda Afrika wakati ugonjwa wa Ebola ulipolipuka katika Guinea, Liberia na Sierra Leone. Lakini Zanzibar katika Tanzania ni safari ya saa tisa za ndege kutoka nchi hizo tatu za Afrika Magharibi. Kwa hakika nchi hizo tatu ziko karibu zaidi na Bara la Ulaya kuliko ilivyo Kenya. Hili ni tatizo kubwa ambalo lazima lisahihishwe haraka iwezekanavyo.”

  Kuhusu mapato ya utalii, Rais Kikwete amesema: “Mwaka jana, Afrika ilipokea watalii wa kimataifa milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa waliotembelea maeneo mbali mbali ya dunia na asilimia tano ya watalii wote waliotembelea dunia mwaka jana.”

  Kuhusu Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania inaendelea kutenga asilimia 36 ya eneo lake lote kwa ajili ya shughuli za hifadhi.

  “Tumefanya hivyo tokea uhuru wetu. Tutaendelea kufanya hivyo. Kama mnavyojua pia tumekuwa tunakabiliana na changamoto ya ujangili ambao ulitishia kumaliza idadi ya tembo wetu. Tumechukua hatua na kuendesha kampeni dhidi ya janga hili. Sasa tunaanza kuona matunda ya juhudi zetu. Mwaka 2012 walikuwa wanauawa tembo sita kwa mwezi. Katika mwaka mmoja uliopita, hajauawa tembo yoyote.”


  Rais Kikwete pia ameshangiliwa sana wakati alipowaambia washiriki wa shughuli ya leo: “Napenda kuchukua nafasi hii, vile vile, kuwaageni marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni yangu ya mwisho nikiwa Rais wa nchi yangu. Nitaondoka madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, 2015 baada ya kuwa nimekamilisha vipindi viwili vya uongozi wangu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.”
  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi na  kupokea Malalamiko yao Katika mkutano wa siku mbili wa tarehe 22 na 23, Septemba, 2015 katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi. 

  Wananchi wengi waliofika katika mkutano huo walisifu jitihada za Waziri Lukuvi katika kushughulikia Migogoro ya Ardhi ambapo tarehe 22 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Kinondoni na tarehe 23 Septemba 2015 alipokea Malalamiko ya Wananchi kwa Manispaa ya Temeke na Ilala.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujua jinsi alivyoshughulikia migogoro ya Ardhi nchini.
   Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi pamoja na Naibu wake Mhe. Angela kairuki wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
   Waziri wa Ardhi akimsikiliza kwa makini mwananchi mwenye malalamiko ya mgogoro wa ardhi kutoka manispaa ya kinondoni
  Baadhi ya Wananchi wa Dar es salaam wenye Migogoro ya Ardhi wakiwa katika mkutano huo.

  0 0

  Je UKAWA wametoka na yapi kuhusu utafiti wa Twaweza? Na  Je kulikoni matokeo utafiti mpya wa SYNOVATE? Tazama uchambuzi wa kina.https://youtu.be/D3r0HSv1jB4  
  Magufuli apaa tena utafiti wa SYNOVATE, pata habari hii na nyingine kibao kupitia udodondozi wa magazeti ya leo September 25. https://youtu.be/revJJ5vPRvs
  Magufuli aendelea kumtimulia vumbi Lowassa katika tafiti nyingine, fahamu hilo na mengine lukuki kupitia uchambuzi wa magazeti tarehe 25.https://youtu.be/TfclKnQ6qAs
  Je wafahamu matokeo mapya ya utafiti kuhusu nani kuongoza uraisi ?SYNOVATE yatoka na mapya.Tazama  yaliyojiri. https://youtu.be/1c4GsQJ9jM0

  0 0

   Haya ndiyo  Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (Ajenda 2030) ambayo  leo Ijumaa Wakuu wa Nchi na Serikali wanayapitisha katika Mkutano wao wa Kihistoria  Unaofanyika  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Ajenda 2030 ambayo utekelezaji wake unaaza mwakani inachukua nafasi ya  Malengo ya Maendeleo ya Millenia( MDGs) ambayo yamefikia ukiongoni mwaka huu.  Upitishaji wa Ajenda 2030 utatanguliwa na hotuba ya Baba Mtakatifu Francis 
   Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi  Liberata Mulamula akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa  kwa pamoja  na  Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani na Mashirika  ya Kimataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani, Mkutano uliokuwa ukijadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uhusiano wake na usalama wa chakula,  lishe na afya. Mkutano huu ulifanyika  siku ya alhamis katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa
   Sehemu ya washiri wa mkutano  kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa usalama wa chakula,  lishe na afya wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula ambaye alikuwa kati ya wanajopo watano waliozugumza katika mkutano huo.

  Na  Mwadishi Maalum, 
  New York
   Leo   Ijumaa,   Viongozi  Wakuu wa Nchi  na  Serikali zaidi  ya 150  kutoka mataifa mbalimbali duniani,  watapisha ajenda na malengo mapya   ya  maendeleo endelevu  ( Ajenda 2030)  kuchukua  nafasi ya  Malengo ya Maendeleo ya Millenia yanayomaliza  muda wake mwishoni mwa  mwaka huu.
  Katika mkutano huu wa kihistoria  unaofanyika  miaka kumi na tano tangu MDGs zilizopitishwa, utatanguliwa  na hotuba ya  Baba Mtakatifu   Francis.

   Baada ya  kupitisha ajenda 2030 na ambayo imejikita zaidi katika kuutokomeza  umaskini na  ulinzi wa mazingira pasipo kumwacha yeyote nyuma,Viongozi   hao Wakuu  wa Nchi na Serikali   kila mmoja wao atapata fursa  ya kuelezea matarajio ya serikali yake katika utekelezaji wa ajenda hiyo yenye malengo 17.

  Tayari   Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali  wamekwisha kuwasili Jijini New York , yaliko Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  unaongozwa na  Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

   Siku moja  kabla ya  kupitishwa kwa ajenda 2030, baadhi ya viongozi ambao wameambatana na  Mhe. Rais wameshiriki katika mijadala mbalimbali na ambayo maudhui yake yanashabihiana na   ajenda nzima ya  Maendeleo Endelevu.

  Akiwakilisha ujumbe wa  Tanzania katika mikutano hiyo ya pembezoni,  Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi  Liberata Mulamula, alishiriki katika majadiliano kuhusu  mabadiliko ya tabia nchi na  uendelevu wa   usalama wa chakula, lishe na  Afya

  Balozi Mulamula alikuwa  kati ya wanajopo watano katika majadiliano hayo  ambayo   yaliandaliwa na  Wizara ya  Ushirikiano wa Kiuchumi na  Maendeleo ya  Ujerumani na Mashirika ya Kimataifa .

  Katika  majadiliano hayo ambayo yalijikita katika kuangalia ni namna gani  utekelezaji wa  ajenda ya  maendeleo endelevu  unavyoweza kuathiriwa na  mabadiliko ya tabia nchi na hususani katika maeneo yanayomgusa mwananchi wa kawaida kama vile usalama wa chakula, lishe na afya.

  Aidha  wanajopo hao  walitakiwa kujibu  hoja mbalimbali zikiwamo  ni kwa namna gani kwa mfano Tanzania imejiandaa katika kukabiliana na  mabadiliko ya tabia  nchi na ambayo kwayo kwa namna  moja ama nyingine yanaweza kuleta  au yanasababisha  matatizo katika  eneo kama kilimo na lishe.

  Akijibu hoja hiyo pamoja na nyingine,  Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula  aliwaeleza  washiriki wa majadiliano  hayo kwamba kwa nchi kama  Tanzania mabadiliko ya tabia nchi ni  jambo lililo dhahiri na si nadharia.

  Akatoa mfano kwa kusema kwamba,  kuna  baadhi ya  maeneo ya nchi,  ambapo wakulima wanashindwa kutambua msimu halisi wa kuanza kulima   na kupanda  tofauti na miaka  ya nyuma.

  Aidha akasema,  maeneo mengine mvua zinanyesha kupita kiasi na wakati  maeneo mengine yana kumbwa na ukame wa kupindukia na hivyo kuathiri shughuli za kilimo na hatimaye ukosefu wa chakula na  chakula chenye viini lishe  ambavo ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo  hususahi ya watoto chini ya  miaka mitano.

  Mfano mwingine ambao  anasema ni wazi  umechangia  kwa namna moja ama nyingine katika ubaribufu wa mazingira ni pamoja na matumzi  yasiyo endelevu ya ardhi, ukataji wa   holela   wa miti na ile hali ya  mito  mikubwa kupingukiwa  maji na hivyo kufanya mabwana makubwa  yanatuyotumika kuzalisha umeme kukosa maji ya kutosha.

  “Nilipokuwa mdogo tulikuwa tunakatazwa sana na wazazi wetu kung’oa miti michanga, na wakati huo hatukuelewa kwamba wazee wetu walikuwa wanatufundisha utunzaji wa miti” akasema Balozi

  Akielezea ni mikakati  gani ambayo serikali   kwa  kushirikiana na wadau mbalimbali inachuka katika  kukabiliana na  mabadiliko ya tabia nchi na  hiyo kuwa na uhakika wa usalama wa chakula, na  upatikanaji wa lishe bora.

  Katibu Mkuu, ameeleza kwamba serikali  imejiwekea mipango  madhubuti ikiwamo ya  uhamasishaji wa wananchi  kuwa na matumizi bora na endelevu ya ardhi, misitu,  kilimo cha umwagiliaji pasi kutumia maji mengi na uhifadhi wa misitu.

  Akasisitiza kwamba  mipango yote  iwe  ile inayoandaliwa na Umoja wa Mataifa Mashirika ya Kimataifa n ahata Serikali ili  tekelezeka na kuwa endelevu inapashwa kumilikiwa na wananchi ambao  hasa ndio waathirika wakubwa lakini pia  wanamchango mkubwa wa kuleta mabadiliko ili mradi wawezeshwe.

  Akatahadharisha kwa kusema kama wananchi  hawatahusishwa  kwa  namna moja ama nyingine  basi utekelezaji wa  ajenda ya maendeleo endelevu  unaweza kuishia kwenye makabrasha.

  Wanajopo wengine wakichangia katika  majadiliano hayo akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa  Mapango wa Chakula Duniani, walieleza kwamba suala na usalama wa chakula na lishe linapashwa kupewa mkazo wa kipekee kwa kile walichosema, takwimu zinaonyea kwamba idadi kubwa na watu duniani wanathirika kwa ukosefu wa chakula lakini kubwa Zaidi  vyakula vyenye virutubisho na viini lishe.

  Wakatoa mfano  kwa kusema kuwa wakati bei ya  vyakula aina ya nafaka ikushuka, bei ya   matunda na mboga mboga,  vyakula vitokanavyo na wanyama na  ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa watoto chini ya miaka mitano vinazidi kupanda bei maradufu na wanaoathirika  ni watu maskini.

  Na kwa sababu hiyo wakasisitiza kwamba kuna uwiano mkubwa kati ya mabadiliko ya  tabia nchi,  tatizo la usalama wa chakula na lishe duni mambo ambayo  serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  zinatakiwa kushirikiana na  kuikabili changamoto hii ambayo athari zake ni kubwa.

  0 0

  Na Yusuph Kileo
  Naanza Andiko hili kwa kutambua na kuhamasisha Tukio la kipekee katika anga ya usalama mitandao ambalo limekua liki azimishwa kila mwaka katika mwezi wa October ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao duniani kote. 
  Kwa mwaka jana katika kuukaribisha mwezi huu Nilipata kuandika katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" na baadae kutoa tathmini ya mwezi katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA".
  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Naanza Andiko hili kwa kutambua na kuhamasisha Tukio la kipekee katika anga 
  ya usalama mitandao ambalo limekua liki azimishwa kila mwaka katika mwezi wa October ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao duniani kote. Kwa mwaka jana katika kuukaribisha mwezi huu Nilipata kuandika katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" na baadae kutoa tathmini ya mwezi katika andiko linalosomeka kwa "KUBOFYA HAPA".

  Naimani Mwaka huu Tanzania ita uchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.

  Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao. Tatizo kubwa kubwa ni kua njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.

  Leo nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.


  Njia hii si nyingine bali ni “Awareness Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda. Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.


  Kwa kupata elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana na uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam wa usalama mitandao.


  Kundi la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.


  Inaaminika asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo mengine tofauti na uhalifu mtandao.


  Kumekua na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.

  Tatizo ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.


  Kumekua na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni , Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua kwa kasi hivi sasa.


  Swali linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi  za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER – Cybersecurity Awareness Month”  na kupatikana kwa tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.


  Jibu ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni mwa jitihada hizi.


  Wengi bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEHAMA ndio pia wanausika.


  Inasahaulika kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote. Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.


  Cha kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.


  Kuna Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.


  Kwa ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni) Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na ushirikiano kama inavyoweza kufatiliwa katika video hii hapo chini.

  0 0

  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa Albanu ya nyimbo kumi ikiwa mpaka sasa ametimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa nyia ya nyimbo hapa nchini.

   ALBAMUya OMBA YESU ANASIKIA kuzinduliwa Septemba 27 mwaka huu(Jumapili hii) katika kanisa la TAG  la upanga mkabala na chuo cha Uzumbe kwa Askofu  Mwanesongore.

   hayo yalisemwa na Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendio Nkone wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa Mungu amemuokoa katika kifo ndio maana ameona aimbe kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na mambo aliyoyapitia, pia kumshukuru Mungu wa kutimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa njia ya Nyimbo.

  Nkone alisema kuwa katika uzinduzi huo wa albamu ya OMBA YESU ANASIKIA kutakuwepo waimbaji wa nyimbo za Injili  ambao watatumbuiza katika uzinduzi wa albamu hiyo atakuwepo  Masanja mkandamizaji, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Kwaya ya Kijichi, Mather Baraka, Christina Matai, Mesi Chengula pamoja na Bendi.
    
  Pia alisema kuwa katika uzinduzi wa albamu hiyo kutakuwa na viingilio tofauti, watu wazima watalipia kiasi za shilingi elfu tano(5000) na watoto shilingi elfu mbili (2000).

  0 0

  Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.

  Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki. 

  0 0
 • 09/25/15--13:00: Article 2


 • 0 0

  Baadhi ya Watanzania walioko Hijja na ambao wamenusurika na maafa ya msongamano wa watu huko Mina jana. Kulia nia Bw. Yahaya Sameja, kushoto ni mwigizaji mchekeshaji Bw. Amri Athumani al maarufu kama King Majuto. Wa katikati  jina lake halikuweza kupatikana.
  ------------------------------------------------------------------------------------

  Bismilah Rahman Raheem

  Assalaam alaykum warahmatullahi wa barakaatuhu.


  Taarifa hii inahusu tukio lilitokea jana Mina Saudi Arabia wakati mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat , palitokea msongamano mkubwa ( stampede) na kupelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa.


  Tayari tumethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine  wanne ni Watanzania.

  Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Bi Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.

  Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii.


  Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama.

  Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisi usiku walikua hawajapatikana hivyo hatukua na uhakika juu ya usalama wao hadi tutakapowaona ama kupata taarifa zao. Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho vyao ambavyo wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya marehemu.

  Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.


  Vilevile nimeagiza maafisa wetu wa Bakwata nilionao hapa Mina kuendelea kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wetu katika hospitali na sehemu za kuhifadhia maiti. Nimefanya hivyo ili niweze kuwa na uhakika juu ya usalama wa mahujaji wetu.

  Katika kipindi hiki cha taharuki kubwa tunafanya mawasiliano na wizara husika hapa Saudi Arabia kwa kushirikiana na serikali yetu kupitia ubalozi wetu hapa Saudi Arabia. Natambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa ambazo zinazidisha taharuki kwa ndugu na jamaa wa mahujaji wetu. Nachukua fursa hii kuwaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa watulivu na kuwa na subra katika wakati huu mgumu sana kwetu sote.
  Tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana na Insha Allah mara tu tukipata taarifa za uhakika basi tutawafahamisha.


  Kutokana na idadi ya maiti kuwa kubwa serikali ya Saudi Arabia wanaendelea na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili ili waweze kutoa taarifa tunatarajia wakati wowote tutakuwa tumepata taarifa zaidi.


  Wabillahi Tawfiiq.
  Sheikh Abu Bakari Zuberi

  Mufti wa Tanzania.

  MECCA, Saudi Arabia

   Mahujaji wakiwa Mina Saudi Arabia kwenye Jamaraat 
   Mahujaji wakiwa na marehemu na majeruhi katika msongamano wa Mina jana
  Hali ya taharuki baada ya msongamano mkubwa ( stampede) huko Mina uliopelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa.
  0 0

   Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

  Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.

  Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
  Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.
  "Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.


  0 0

   Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kwemye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Kahama leo
    Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia gharika ya wananchi i kwemye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Kahama leo
  Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia gharika ya wananchi i kwemye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Kahama leo

  0 0


  0 0

  Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Inspecta Harun akihamasisha wanaCCM na wananchi mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.  
  Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akisalimia wananchi.
  Mgombea mwenza Bi. Suluhu akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi. 
  Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi mgombea mwenza.

  Mgombea mwenza Bi. Suluhu akimkabidhi kadi mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.
  Katibu wa Chadema Wilaya ya Gairo, Yona Senyagwa (kushoto) akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katibu huyo pamoja na makada wenzake wametangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 09/25/15--20:03: EAMCEF FUNDRAISING GALA 2015


 • 0 0


  0 0

  ANNABEL msanii mpya akiwa na wimbo mpya unaitwa UNANIONEA  amemshirikisha Msanii mkubwa Barnaba ambaye ndiye mtunzi na producer wa wimbo huo.

older | 1 | .... | 986 | 987 | (Page 988) | 989 | 990 | .... | 3285 | newer