Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

MKONO WA EID MUBARAK KUTOKA NGOMA AFRICA BAND AKA FFU UGHAIBUNI

0
0
Bendi maarufu ya muziki wa dasni barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuniyenye makao kule Ujerumani inawatakia wadau wote mkono wa Eid el Hajj.
Bendi hiyo inawatakia kila la heri na baraka katika kusherekea siku hii ya Eid Al Hajj, na kusema sikuu hii iwe ya amani, upendo na furaha. Ngoma Africa band inawapa mkono wa Eid Mubaraka.

usikose kufungua sikio at www.reverbnation.com/ngomaafricaband

MKUTANO WA KAMPENI WA LOWASSA LINDI

0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia Wananchi, katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akifurahi jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF kupitia Mwamvuli wa UKAWA, Salum Barwany.
Uwanja wa Pilipili ulikuwa ni shangwe tupu, muda wote wa Mkutano.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini, kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Pilipili,Lindi Mjini, leo Septemba 23, 2015.


VUGUVUGU LA AJENDA YA WATOTO NA UCHAGUZI MKUU LAENDELEA KIBAHA

0
0
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Simbani, Akram-Shabani,akizungumza katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.
 Baadhi ya wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani  waliohudhuria mdahalo huo.
Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka Plan International, Jastin Moses akizungumza  katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani, Ombeni Ally akizungumza  katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani uliofanyika Kibaha Mkoani Pwani jana.


JAMII imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa chama chake kinaangalia ni kwa namna gani watazingatia katika Lishe bora ya mtoto pamoja na namna gani mtoto atainuliwa Kielimu.

 Aidha Mgombea Udiwani wa kata ya maili moja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema chama chake kitaangalia zaidi afya ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya dawa inakuwa na dawa za kutosha.

Hata hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea kutimiza ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia malengo yao. 

Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya kuwalinda hasa wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda na kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na vishawishi vingi wanapokuwa njiani. 

Aidha watoto pia waligusia suala la rushwa na kwa namna gani linavyorudisha nyuma maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki zao.

Mdahalo huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF uligusa maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza kuokoa maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa maji katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
 
Mengine ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote, kuwekeza katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu, udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu. 

Vuguvugu hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea wa nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele kunaweza kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi na la usawa.

Unaweza kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org nawww.facebook.com/WalindeWatoto

DKT FENELA MUKANGARA AAHIDI KUWAINUA KIUCHUMI WANANCHI WA KIBAMBA KUPITIA SACCOS

0
0
Dkt Fenela Mukangara akizungumza na wana SACCOS wa kata ya Msigani
 akiahidi kuwainua kiuchumi wananchi wa kibamba kupitia SACCOS yao jijini Dar es Salaa jana.

 Baadhi ya akina mama na wana SACCOS wa kata ya Msigani wakimsikiliza Dkt Fenela Mukangara jijini Dar es Salaa jana.

CCM WAKUBALI MDAHARO WA WAGOMBEA URAIS JIJINI DAR LEO

0
0
 Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya (CCM) January Makamba akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kufanya mambo mapya  yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais ameyasema hayo jana  jijini Dar es Salaaam katika ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi CCM.
Wanahabari wakimsikilaza Mjumbe wa Halmashauli Kuu ya Taifa na ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya (CCM) January Makamba jana katika Ofisi ndogo ya chama cha mapinduzi  jijini Dar es Salam.
(Picha na Emmanuel Mssaka).

HABARI ZAIDI INGIA HAPA

MAGUFULI APIGWA NA BUTWAA NYOMI LA GEITA, AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala mjini Geita jana  na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mgombea Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu, moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.
Magufuli ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya  kuboresha uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha  kiwango cha  ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.


Dkt. Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania. 
Wananchi wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
 Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka. 
Magufuli Style ilitikisa pia ndani ya Geita kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli ambapo wasanii walipasha kwanza kabla ya kuanza kazi.
????????????????????????????????????
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea  mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Brigade cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita  na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
 Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.


JK AWAPA ZAWADI YA IDD MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

0
0
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda(wa pili kulia)kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi za Idd el Hajj Meneja wa Mahabusu ya Watoto mkoa wa Arusha,Mussa Mapua leo kwa ajili ya kusherekea siku kuu hiyo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo jijini Arusha
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.
"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda.
Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.

Mgombea ubunge Mafia anadiwa na kunadi ilani ya CCM

0
0
 Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgombea ubunge jimbo la Mafia bwana Mbaraka Kitwana Dau kabla ya kumnadi kisiwani Mafia

 Mama Samia Suluhu Hassan aki saini kitabu cha wageni, kisiwani Mafia. Kulia kwake ni bwana Mbaraka Kitwana Dau, ambaye anagombania ubunge jimbo la Mafia. Kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM Mafia bi Arafa. Mwisho kushoto ni Mhe Abdulkarim Shah, mbunge wa Mafia anaemaliza muda wake. Mwisho kulia  ni DC wa Mafia
Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na mgombea ubunge Mafia bwana Mbaraka Kitwana Dau, pamoja na mbunge wa Mafia Mhe. Abdulkarim Shah ambaye anamaliza muda wake

 Mgombea Ubunge wa Mafia Bw. Mbaraka Kitwana Dau akiwa katika kijiji cha Kanga wilayani Mafia akinadi kwa umakini mkubwa Ilani ya CCM

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA (DAWASA) MNADA WA HADHARA:

0
0
 UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na DAWASA  watauza Magari, Photocopy mashine, na Furniture za ofisi kama zilivyoorodheshwa hapo chini kwa mnada wa hadhara  tarehe 26, September, 2015  Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika  DAWASA makao makuu  jirani na Hospitali ya Mwananyamala .

MALI ZITAKOZOUZWA: Meza za ofisi, Viti, Book case, Cupboard, File cabinets, 

6 Photocopy m/c {Canon /Sharp} , Computer set, Printer, Scanner, A/c split unit & Window type na grili za milango nakadhalika.


MAGARI YATAKAYOUZWA:

Idadi

Muundo

Aina YA Engine

Mwaka

Ushuru

1

Toyota Hilux  D/Cabin

5L      Diesel engine

2009

Haujalipwa

1

Nissan Patrol S/Wagon

Z30    Diesel  engine

2004

Haujalipwa

2

Mitsubish P/Up double cabin  L200

4D56  Diesel engine

2005

Haujalipwa


Mali zote zinaweza kukaguliwa DAWASA jirani na Mwananyamala Hospital,  tarehe 23 mpaka 25 November,  2015 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.


MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huo mali itauzwa tena na dhamana haitarudishwa.

  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.

  3. Mnunuzi atatakiwa kuondoa mali baada ya kulipia malipo yote

       4    Ni wajibu wa Mnunuzi wa Magari kulipa Kodi zote


Kwa maelezo zaidi waone:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE

NKRUMAH STREET
MKABALA NA CO-CABS

SIMU NA:  0754-284 926, 0757 284 926               
Email : universalauction@hotamail.com

DAR ES SALAAM.

KAMATI YA KAMPENI YA MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI YASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID EL HAJJ MKOANI GEITA LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,akiwaongoza baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na wageni waalikwa kutoka Serikali ya Mkoa wa Geita kukata Ndafu  ikiwa ni sehemu ya  kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,wakati wa mapumziko ya shughuli za kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,ambapo leo alitarajia kuendelea na kampeni zake mkoani Shinyanga.

Wakati huo huo Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.John Magufuli ameahirisha mikutano yake ya kampeni aliyokuwa aifanye leo Mkoani Shinyanga ili kupisha sikukuu ya Eid El Hajj,pia amewatakiwa Watanzania wote popote pale walipo sikukuu njema na yenye Baraka mbele za Mwenyezi Mungu na na kuwa tuendelee kuidumisha Amani ya Nchi yetu.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa Kamati  Kuu ya CCM,Ndugu Abdallah Bulembo ambaye pia ni Kiongozi wa msafara wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,akizungumza jambo mbele ya baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama hicho na Serikali ya Mkoa wa Geita wakati wa mapumziko ya  kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj kwa pamoja,mapema leo mchana mkoani Geita.
 Ndafu akiwa ameandaliwa tayari kwa kuliwa.
 Ndafu ikikatwa kwa pamoja.PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.

introducing new single "Ningefanyaje" by Ben Pol featuring Avril

0
0
The undisputed Tanzania's King of RnB is back with a Brand new RnB Ballad called Ningefanyaje to be release 24th September, 2015. This song features Kenya’s Sweetheart Avril and Tanzania’s upcoming songbird Rossie M. This project is produced by Mswaki.
Ben Pol has taken part in Coke Studio Season 3 which will be aired on 10th October, 2015 and Ningefanyaje is among  the songs he performs with a live band of Coke Studio in Nairobi, Kenya. On Coke Studio Ben Pol is paired and collaborated with Kenya's Wangechi.
This single comes as a follow up of the successful hit record called "Sophia" which was released on 15th January, 2015. Sophia is rated the longest chart topping single of 2015 so far. Sophia has spread on airwaves and crossed boarders all over the East African Region and some other parts of Africa. 
The song in now available on a local channel called Mkito and internationally distributed by iTunes, Amazon, Spotify and all other music distribution channels.

Contact Details:
Instagram: @iambenpol

BASATA LATAKA KUONDOLEWA/KUSITISHWA MARA MOJA KUCHEZWA KWA NYIMBO ZOTE ZENYE KUKENGEUKA MAADILI, SHERIA NA TARATIBU

0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawaagiza wasanii, wamiliki na waendeshaji wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari hususan radio na runinga kuondoa na kuacha mara moja kurusha au kutangaza au kucheza nyimbo zote zenye maudhui ya kashfa, matusi, kejeli, udhalilishaji ambazo zinahatarisha kuigawa jamii ya kitanzania katika misingi yoyote hasa katika kipindi hiki Taifa linapoendelea na kampeni za kisiasa na kujiandaa na uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa kifungu namba 118 (a-d) cha Sheria ya Bunge namba 9 ya Mawasiliano ya Mtandao ya mwaka 2010 ni marufuku kwa njia yoyote kwa mtu au chombo chochote kutengeneza, kuzalisha, kusambaza au kutangaza ujumbe ambao una mlengo wa matusi, dharau, uzushi au jinai kwa lengo la kutukana, kutisha, kusumbua au kushusha hadhi ya mtu mwingine.
Aidha, Sheria ya Bunge namba 4 ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 45 (1) (a-c) kinatoa mamlaka kwa taasisi au mtu yeyote anayebaini uvunjifu wa Sheria katika mitandao kutoa notisi kwa yeyote yule anayesambaza au kutangaza ujumbe au maudhui yanayovunja sheria za nchi kuacha mara moja au vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekaidi.
Ni kwa msingi huu, BASATA linawaagiza wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na wale wenye akaunti kwenye mitandao ya kijamii kama sound cloud, U-Tube, ITunes nk. kuondoa ndani ya siku saba (7) kuanzia siku ya kwanza ya taarifa hii nyimbo zote zinazokengeuka maadili na kubeba mlengo wa matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji wa watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na kitaifa.
Aidha, BASATA linawakumbusha tena Wasanii wote nchini kuacha mara moja kubuni na kutengeneza kazi za Sanaa zenye kuashiria kuigawa jamii katika misingi yoyote ya kibaguzi na zaidi kutumia Sanaa kubomoa jamii badala ya kuijenga.
BASATA linawasisitiza wamiliki wa vyombo vya habari hususan radio na runinga pia watangazaji na Ma DJs kuhakikisha hawawi chanzo cha kusambaza maudhui yoyote ya Sanaa yenye mlengo wa kuibua chuki, matusi, kashfa na mgawanyiko wa Taifa.
BASATA kwa mamlaka yake chini ya Sheria namba 23 ya mwaka 1984 na yale ya Sheria ya Mawasiliano ya Posta na Mitandao ya mwaka 2010 na ile ya Makosa ya mitandao ya mwaka 2015 kwa kushirikiana na vyombo vya dola halitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kinidhamu kwa wasanii, wamiliki wa wavuti, tovuti na vyombo vya habari ambavyo vitaendelea kutangaza na kusambaza nyimbo zenye mwelekeo wa kuhatarisha usalama, umoja na mshikamano wa Taifa.
BASATA likiwa ni msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linatambua kwamba Sanaa ikitumiwa kwa ukengeufu inaweza kuwa chanzo kikuu cha machafuko, mivurugano na kupotea kwa amani nchini. Hivyo umakini unahitajika miongoni mwa wasanii katika kuzingatia weledi, maadili, uzalendo kwa taifa na kuitumia Sanaa kama chombo cha kujenga jamii yenye kuzingatia maadili. 

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

DAVIS MOSHA AKUTANA NA WASANII WA MOSHI

0
0
Mh Davis Mosha akiwa na
Mwenyekiti wa KDFAA Ndugu Msasu.


 Mgombea Ubunge wa Moshi Mjini kupitia Tiketi ya ccm Mh. Davis Mosha Amekutana na wasanii wa Filamu, Maigizo ya Jukwaani, Sarakasi na Muziki wa Mjini moshi. Wasanii hao wakiongozwa na Chama cha Wigizaji na wacheza filam Kilimanjaro (KDFAA)
Wasanii wakimsikiliza Mh. Davis Mosha wakati akizungumza nao leo jioni mjini Moshi.
  
Wasanii hao walioomba Mkutano na Mh. Davis Mosha leo katika ukumbi wa ccm Mkoa walipata fursa ya kuzungumza Changamoto zinazowakabili na Malengo yao kama wasanii wa Moshi na Mkoa Kilimanjaro. Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ukumbu huo mmoja wa Wasanii wa Muziki Ndugu Samwel Stephen aliweza kumuomba Mh. Davis Mosha awasaidie kupata studio ya kisasa na kuwapa wigo mpana wa kazi zao za muziki kuweza kupigwa katika Radio. 
Mh. Davis Mosha akijibu hilo aliwahakikishia Kujenga Studio ya Kisasa itakayoanza kufanya kazi mapema Mwezi ujao chini ya Kampuni yake ya African Swahili Media sambamba na Kufungua kituo cha Redio na Tv.

Wasanii wa Filamu waliomba kuweza kusaidiwa kurekodi Tamthilia ambayo itaweza kurushwa katika Tv na waweze kujitangaza na kujiajiri kupitia sanaa hiyo lakini pia hawakusita kutoa kilio chao juu ya Wizi wa kazi zao unaofanywa na wasambazaji pamoja na Wasambazaji kutoka Dar es Salaam kuwanyonya na kusababisha kazi zao za Film kubaki nyumbani badala ya kwenda Sokoni. Pia waliweza kutoa malalamiko yao juu ya uongozi uliokuwepo madarakani katika ngazi ya ubunge na Udiwani kuwaahidi maramara ahadi ambazo hazitekelezeki.
Mh Davis Mosha akifafanua Jambo
katika Mkutano na Wasanii leo

Bwana Mosha aliweza kuwahakikishia Soko la uhakika la filam zao na pia ulinzi wa kazi zao kupitia vyombo husika vinavyoshughulikia masuala ya haki miliki na pia kuweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao. Na pia aligusia suala la wasanii wa Ngoma za asili juu ya kuhakikisha anaweka kituo cha sanaa na utalii ili kuweza kuwakutanisha wageni wanaokuja kupanda mlima na kufanya ni kituo cha kubuudika kupitia ngoma za asili na sehemu ya kujifunzi aTamaduni za Makabila mbalimbali ya Tanzania. LAkini pia aliwaasa wasanii kutumia sanaa yao kutoa elimu ya uchaguzi juu ya wananchi kutumia haki yao ya msingi katika kuchagua na wasifanye makosa watumie Mitaji yao ya Vitambulisho vya kupigia kura kuhakikisha wanachagua Kiongozi atakayeenda kufanya kazi na si mwanasiasa.

Mwenyekiti wa KDFAA akitoa shukrani zake kw Mh. Davis Mosha kwa Kukubali kuja kuwasikiliza.



 Akifunga Mkutano huo wa wasanii, Mwenyekiti wa Chama cha waigizaji na Filamu Ndugu Msasu alitoa shukrani za Dhati kwa Mh. Davis Mosha huku akimfananisha na Mkombozi ambaye amekuja kuwakomboa kutokana na Viongozi wengi kuwadharau wasaniii na kupelekea Sanaa ya Moshi kuzidi kushuka. Alitumia nafasi hiyo kuwaasa wasanii kutochezea nafasi waliyopata ambayo Mh. Davis Mosha ameonesha nia ya dhati ya kuweza kuwakomboa kupitia sanaa yao na wao basi waoneshe hitaji lao kwake kwa kuhakikisha wanafanya kazi nzuri katika sanaa.

Majibu kwa dukukudu kuhusu kura ya maoni ya Uchaguzi Mkuu ya TWAWEZA

Nkone, Lissu, Mwangila waahidi makubwa Tamasha la Amani Dar

0
0
 

Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha la Kuombea Amani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Christopher Mwahangila na Upendo Nkone. (Picha na Francis Dande)

 Mwimbaji wa nyimbo za injili, John Lissu akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions na litakafanyika Oktoba 4 kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni mwimbaji Christopher Mwahangila na Upendo Nkone.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Jesca Honore 'BM' akiimba wimbo wa 'Napokea' Jesca ni mmoja wa waimbaji watakaopamba tamasha la Amani la kuombea Uchaguzi Mkuu na Taifa.

WAIMBAJI  mahiri wa nyimbo za injili nchini waliotajwa kushiriki Tamasha la Uchaguzi Mkuu litakalofanyika Oktoba 4, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wameelezea walivyojipanga kufanikisha malengo ya tukio hilola kihistoria.
Wakizungumzia Tamasha hilo kwa nyakati tofauti katika mkutano wa utambulisho wao, baadhi ya waimbaji waliothibitishwa, wameelezea kufurahia kuwa miongoni mwa waimbaji watakaotumbuiza maelfu katika tamasha hilo la kuombea amani na utulivu Uchaguzi Mkuu.


Kwa upande wake Upendo Nkone, alisema ni faraja kwake kuwa miongoni mwao waimbaji katika tukio hilola kumsihi Mungu ajalie hali ya amani na utulivu wakati na baada ya uchaguzi mkuu kwani amani ndio msingi wa mafanikio ya kila kitu.
“Nafarijika kuwemo katika orodha ya waimbaji katika Tamasha hilo. Watanzania tukumbuke taifa linahitaji maombi kwani linapita katika kipindi kigumu ambacho bila msaada wa Mungu, ni mtihani mgumu ambao katika nchi nyingi tu, umekuwa chanzo cha mifarakano,” alisema Upendo.


Naye Christopher Mwangila, mbali ya kushukuru kupata nafasi hiyo, pia amewasihi wapendwa katika Kristio Yesu, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya kupaza sauti kwa Mungu autangulie uchaguzi huo uwe wa amani.
Kauli hiyo iliungwa mkono na mwimbaji mwingine, John Lissu ambaye pamoja na shukrani kupata nafasi ya kushiriki, pia ametumia fursa hiyo kuwasihi wapenzi na mashabiki wa muziki wa njili na wote wenye upendo kwa nchi yaokujitokeza siku hiyo.
Naye Matha Mwaipaja, alisema anamshukuru Mungu kupata fursa na kumjalia kipaji cha uimbaji, hivyo ana kila sababu kushiriki tukio muhimu kama hilo la kuombea amani ya nchi kwa kuzingatia kuwa, viongozi hutoka kwa Mungu.

Mwimbaji mwingine aliyetoa neno kuelekea Tamasha hilo, ni Jesca Boniface Magupa ‘BM’ akisema amejiandaa vizuri kuipamba siku hiyo akishirikiana na wengine mahiri wa ndani na nje ya nchi akiamini sauti za kumsihi Mungu uchaguzi uwe wa amani, hazitapotea bure.

Coventry Muslim Swahili Association (COMSWA) washerehekea Eid el Hajj kwa mafanikio makubwa.

0
0
 Ni neema kubwa ambayo imepatikana kwa juhudi kubwa zilizofanywa na viongozi wakishirikiana na wana jamii pamoja na mambo mengine lakini kuhakikisha jamii inakuwa pamoja.

Kipaumbele cha mwanzo ikiwa kuwafundisha vijana na wazee maadili mazuri, aidha kujenga moyo wa kushirikiana na kuhakikisha umoja wenye afya. Ni bahati kubwa kwa watu wa ughaibuni kuweza kukutana ktk mji mmoja wakiwa wanazugumza lugha moja, utamaduni wao mmoja na wana maadili yanayofanana. 
Ili kuona kwamba hayo yanafanikiwa wameandaa sherehe ya siku mbili tarehe 24 na 26/09/2015 kuanzia saa nane mchana hadi saa nne usiku. Vyakula vya ki-asili kama vile urojo,mishikaki na vinginevyo vitauzwa kwa malengo ya kuiingizia jumuiya mapato ili kufanikisha malengo wanayo yakusudia. 
Kutakua na kiingilio £ 10 kwa familia moja na £5 kwa wasio hudhuria na familia. Tunawatakiwa Eid njema na tunasema: Eid Mubaarak.


Kwa kutaka kuifahamu vizuri COMSWA na kazi zake tembelea www.comswa.com

MSAADA TUTANI: DADA WA NYUMBANI ATOWEKA NA MTOTO LOVENESS COLETHA JULLLU, FAMILIA YAMSAKA

0
0
Picha ya hivi karibuni ya mtoto Loveness C. Jullu
Familia ya Jullu ya Wazo Hill kwa Msabaha jijini Dar es Salaam inaomba msaada kutoka kwa raia wema ili kufanikisha kumpata mtoto wao Loveness Coletha Jullu aliyepotea nyumbani na msichana aliyekuwa akimlea na kusaidia shughuli za nyumbani.
Wawili hao hawajaonekana tangu juzi Jumanne. Taarifa zimefikishwa katika kituo cha polisi na RPC wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni amekiri kupata taarifa za tukio hilo.
Ikiwa una taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwao tafadhali zitoa kupitia namba hizi:0715797920 na 0786977615.

Asante.

Binti msaidizi wa kazi za nyumbani (house-girl)
Picha ya awali ya mtoto

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

MKOANI MARA KATIKA FAMILIA ZA KIKURYA, SHEREHE ZA KUCHINJA MBUZI KWA AJILI YA SUPU BADO ZINA THAMANI KUBWA.

0
0
Kutoka kushoto ni Professor Lyoyd Binagi (Manamba) James Binagi, Bi.Luise Binagi, Ghati Isanchu na wanandugu wengine wakiwa katika sherehe ya kifamilia iliyofanyika jana Septemba 24,2015 katika Kijiji cha Kenyamanyori ambapo Professor Binagi aliandaa sherehe hiyo kwa ajili ya kumchinjia mbuzi wa supu shemeji yake aitwae Bi.Nyamhanga Samo.

Na:George GB Pazzo
Kwa kabila la Wakurya sherehe ya kumchinjia mtu mbuzi kwa ajili ya supu huchukuliwa kama heshima kubwa miongoni mwa alieandaa sherehe hiyo na yule alieandaliwa sherehe ambapo ndugu, jamaa, marafiki na majirani hualikwa kwa ajili ya kushiriki pamoja katika sherehe hiyo.
Kushoto ndie Bi.Nyamhanga Samo ambae sherehe iliandaliwa kwa ajili yake na hapa akiwa pamoja na mke mwenzie wakipata chakula
Kushoto ni Hezekia Binagi (Maina) akipokea Supu kutoka kwa Professor Lloyd Binagi
Bi.Luise Binagi akimpatia Supu mhusika Mkuu wa sherehe Bi.Nyamhanga Samo
James Binagi (Chacha) akimpatia supu Shemeji yake

Geban Winani akimpatia Supu Bi.Otaigo Mohabe
Bi.Luise Binagi akimpatia Supu Bi.Sophia Binagi
Supu hii huandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu ni inafaa kunyweka kwa wazee, mwanawake alidjifungua siku za karibuni au mgonjwa kwa kuwa huufanya mwili kuwa imara zaidi.
Wazee wakipata supu
Tamaduni hii ilikuwepo miaka mingi iliyopita na bado inaendelea kuenziwa na familia nyingi katika kabila la Wakurya
Nyama huchomwa kwa ustadi mzuri pia
Waandaaji wa Nyama
Hapa pia Kichuri huandaliwa
Pia vyakula mbalimbali huandaliwa
Baada ya watu kunywa supu na kula chakula, hufuata zawadi kwa mlengwa wa sherehe  ambapo alieandaa sherehe huanza kumtuza zawadi za blanketi, vitenge na pesa yule alieandaliwa sherehe
Mzee Maina akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
Mzee Chacha akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Wazee katika picha ya pamoja
Wazee wakibadilishana mawazo baada ya chakula
Baada ya Chakula na kubadilishana mawazo
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanandugu
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanafamilia
Watoto nao hufurahia sherehe za kuchinja supu
Hatimae sherehe ikafikia tamati na Muandaaji wake ambae ni Professor Lloyd Binagi akaingia ndani ya gari na safari ya kurejea nyumbani kwake Bomani Mjini Tarime kutoka Kijijini alikozaliwa Kenyamanyori ambapo sherehe ilifanyikia ikawadia

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, ALIHUTUBIA TAIFA KWENYE BARAZA LA EID EL HAJJ MUSOMA LEO

0
0
 Injinia Mkuu wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Wilaya ya Musoma Suleiman Bishanga, akimuonesha Makamu wa Rais Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal ramani ya ujenzi wa msikiti huo hadi utakapokamilika wakati Makamu wa Rais alipotembelea kuangalia ujenzi huo leo Sept 24,2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Himid Jongo kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika kitaifa leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara.
 Waumini wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akihutubia Taifa kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Taifa kwenye Baraza la eid el Hajj iliyofanyika leo Sept 24, 1015 katika ukumbi wa MCC Musoma Mkoani Mara. (Picha na OMR)
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images