Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 984 | 985 | (Page 986) | 987 | 988 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akimnadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumapili Sept. 20.15. Kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Charles William Iteba.
  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akipongezwa na wanaCCM katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
   Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akihutubia  na wanaCCM na wananchi  katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
  Bando la Kippi Warioba likinuliwa juu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,  Utamaduni na Michezo, Mama Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tanzania Media Foundation - Mfuko wa Habari Tanzania - TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. Mfuko huu unachukua nafasi ya Tanzania Media Fund 
   Mwenyekiti wa Bodi ya TMF Mama Halima Shariff akitoa neno la shukurani baada ya bodi hiyo kuzinduliwa usiku wa kuamkia leo  katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. .
   Mkurugenzi wa TMF Bw. Ernest Sungura akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) uliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam
   Mkurugenzi wa TMF Bw. Ernest Sungura akimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la habari la Daraja Bw. Simon Mkina wakati wakati uzinduzi huo wa Mfuko wa Habari Tanzania 
   Mrisho Mpoto akitumbwiza wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyofanyika leo katika ukumbi wa Millenium Tower jijjini Dar Es Salaam.
   Wajumbe wapya wa Bodi  ya TMF katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana  Utamaduni na Michezo Mama Sihaba Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa Bodi ya TMF na  watendaji wa mfuko huo usiku wa kuamkia  leo katika ukumbi wa LAPF Millennium Tower jijini Dar es Salaam. 
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii 

  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa kwa shule ya msingi Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust, (kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere  (kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi wa moja ya darasa la shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya ambayo yametolewa kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust.
  Walimu wa shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
   Wanafunzi wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.

  WATOTO wa shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 10.Pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo ambayo pia inatoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili.


  Msaada huo umetolewa kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust,nayo ya jijini Dar es Salaam ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuboresha mazingira ya watoto kusomea kwa kutoa misaada ya madawati na vifaa vya kusomea mashuleni ikiwemo vitabu na tangu ianzishwe tayari imetoa misaada kwa shule mbalimbali nchini.


  Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mbuyuni Meneja wa Mawasiliano na matangazo wa Aggrey&Clifford  Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.


  “Kampuni yetu ambayo ina mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa imeajiri wataalamu wa Nyanja mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na ndio maana tumetoa msaada huu kuwawezesha watoto hawa wasome katika mazingira mazuri ili waje kuwa wataalamu wazuri katika siku zijazo na tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu nchini”.Alisema.


  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Hassan Maajar Trust   ZenaTenga, alisema ana imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi wengi katika shule ya Mbuyuni watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya kusomea ni jambo la muhimu katika kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea elimu bora wakati watoto wanasoma wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa wito kwa makampuni na taasisi zingine kulivalia njuga tatizo la upungufu wa madawati mashuleni na kulimaliza kabisa.


  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela alishukuru kwa msaada huo ambaye shule yake imepata na alitoa wito kwa wafadhili wengine kuendelea kujitokeza kusaidia jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika ufanikishaji wa kutoa elimu bora.

  0 0  1
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mpya jukwaani jana kwa kupiga Push Up kama kumi hivi ili kuwadhihirishia wananchi wa Mjini Karagwe mkoani Kagera  kuwa yuko fiti kiafya ili kuwatumikia watanzania mara watakapompa ridhaa ya kuwaongoza Watanzania ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani .

  Huku umati wa Wakazi wa Karagwe ukishangilia kwa mayowe,Dkt Magufulia alieleza kuwa  kazi ya kuwatumikia Watanzania siyo rahisi ni muhimu kuwa na afya njema ili kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na yuko tayari kuwatumikia Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana.
  2
   Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi. 
  PICHA NA MICHUZI JR-KAGERA
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya jana  kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya  zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
    Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema jana  mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema jana  mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Watoto wa shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 10.
  Pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo ambayo pia inatoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili. Msaada huo umetolewa kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust, nayo ya jijini Dar es Salaam ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuboresha mazingira ya watoto kusomea kwa kutoa misaada ya madawati na vifaa vya kusomea mashuleni ikiwemo vitabu na tangu ianzishwe tayari imetoa misaada kwa shule mbalimbali nchini. 
   Akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mbuyuni Meneja wa Mawasiliano na matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
  “Kampuni yetu ambayo ina mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa imeajiri wataalamu wa Nyanja mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na ndio maana tumetoa msaada huu kuwawezesha watoto hawa wasome katika mazingira mazuri ili waje kuwa wataalamu wazuri katika siku zijazo na tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuboresha elimu nchini”.Alisema. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi Hassan Maajar Trust ZenaTenga, alisema ana imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi wengi katika shule ya Mbuyuni watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya kusomea ni jambo la muhimu katika kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea elimu bora wakati watoto wanasoma wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa wito kwa makampuni na taasisi zingine kulivalia njuga tatizo la upungufu wa madawati mashuleni na kulimaliza kabisa. 
   Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela alishukuru kwa msaada huo ambaye shule yake imepata na alitoa wito kwa wafadhili wengine kuendelea kujitokeza kusaidia jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika ufanikishaji wa kutoa elimu bora.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa kwa shule ya msingi Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust, (kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere  (kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi wa moja ya darasa la shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya ambayo yametolewa kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust
  Walimu wa shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
  Wanafunzi wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.

  0 0


  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the U.S. Deputy Secretary of State Antony Blinken in Washington D.C. this morning and held bilateral talks on cementing further diplomatic and economic cooperation between the two countries. President Kikwete is in the US for a working visit whereby among other things he is expected to address the 70th session of the UN General Assembly in New York Photos by Freddy Maro


  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa chama cha ACT Wazalendo, Nixon Tugara akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya matokeo ya  utafiti wa Twaweza na nafasi ya Mgombea wa Urais wa chama cha (ACT)Wazalendo licha ya kuonesha hali hiyo sisi (ACT) wazalendo tunafarijika na matokeo ameyasema hayo katika mkutano huo uli0fanyika katika ukumbi wa makao makuu ya chama  hicho jijini Dar es Salaam  leo kulia ni Mjumbe wa kamati ya uchaguzi, Emmanuel Mvule.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa wa chama cha ACT Wazalendo, Nixon Tugara leo jijini Dar es Salam. Picha na Emmanuel Massaka

  0 0

  Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya ufadhiri wa Taasisi ya TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao umelenga kufanya kazi ya kutathimini hali ya kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda linatarajia kufanya tathimini kwa watoto (Wanafunzi na wasio wanafunzi) walio na umri kati ya miaka saba hadi 16 katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kwa lengo la kubaini hali ya kielimu na changamoto zake ilivyo wilayani humo.
  Na:Binagi Media Group
  Ili kufanikisha zoezi hilo, SHIMATA imetoa semina kwa wahojaji watakaofanya tathimini hiyo ambayo pia itawafikia wenyeviti wa Mitaa na Vijiji pamoja na Wanakaya pamoja na kupima kiwango cha madini joto katika kaya hizo.

  Akifunga semina hiyo iliyoanza juzi Septemba 22,2015 na kutamatika jana Septemba 23,2015 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka washiriki wa semina hiyo (wahojaji) kuhakikisha wanafanya tathimini hiyo kwa ukweli na uwazi ili kupata majibu sahihi ya kiwango cha elimu katika Wilaya hiyo.
  Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa
  Mwenyekiti wa SHIMATA Joseph Magabe akizungumza katika semina hiyo

  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina
  Mratibu wa Twaweza Wilayani Tarime akipokea Cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
  Mwenyekiti wa SHIMATA akipokea cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
  Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
  Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi
  Viongozi na Wajumbe wa SHIMATA

  0 0

  Mapema jana Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambao ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi waliweza kusafirisha wanafunzi wapatao 70 kwenda nchini China kwa ajili ya masoma. Akizungumza Mkurugeni wa GEL, Abdulmaliki Mollel alisema kuwa wanamshukru Mungu kwa kuendelea kuwafungulia milango ya kuendelea kupokea wanafunzi wanaopenda kusoma vyuo nje ya nchi. Pichani: inawaonyesha  wakiwa tayari katika mstari wa kukaguliwa ili waweze kuanza safari yao ya kwenda nchini China kimasomo.                                                             Mzazi kumuaga mwanae kwa bashasha.
   Mwandishi wa Mlimani Tv akifanya mahojiano na mmoja ya wanafunzi anyekwenda kusoma chuo kikuu nchini China.
  Mkurugenzi Msaidizi wa GEL, Zakia kulia akimhoji mwanafunzi endapo anavielelezo vyote vya kusafilia ikiwemo Passport na nyaraka nyingine za shule. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Much of the discussion in traditional media, on social media and elsewhere regarding our recently published opinion poll findings on Tanzanian politics has focussed on perceived errors in the brief. We want to correct three of the most common misunderstandings.
  1. “Totals do not add up to 100%.”
  2. “Totals for 2013 and 2014 add up to much less than 100%.”
  3. “A sample size of just 1,848 respondents is not sufficient.”
  It has been pointed out that several charts and tables in the brief include data that does not seem to add up to 100%. In some cases, the figures add up to 99%, 101% or 102%.
  This is purely as a result of rounding the figures to the nearest whole number, a standard practice in opinion poll research. We do this because presenting figures with one or even two decimal points suggests a level of precision in the findings that can be misleading.
  The examples below show how this happens, by presenting the unrounded figures alongside the rounded figures that were presented in the brief. 

  0 0


  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa Mashine mbili  ambazo zitatumika kufuatilia mapigo ya moyo ya mgonjwa mahututi akiwa kwenye tiba ( Patient Cardiac monitors). 
   Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mashine hizo ambazo zimetolewa na Mfuko wa Human Welfare Trust, Veena Joa,  amesema wataendelea kusaidia kutoa huduma mbalimbali kwakua Hopsitali ya Taifa Muhimbili inategemewa na wananchi wengi wana imani nayo. 
   Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Hussein Kidanto amewashukuru Human Welfare Trust kwa msaada wa mashine hizo ambazo zitatumika katika Kitengo cha magonjwa ya dharura hapa MNH na kueleza kwamba kitengo hicho ni sehemu muhimu kwani kinapokea wagonjwa wengi kabla ya kupelekwa Wodini. 
   Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura na ajali MNH ambaye pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa hayo Dkt Juma Mfinanga, kwa siku kitengo hicho hupokea wagonjwa 150 hadi 200 na kati ya hao asilimia 60 hadi 70 wanakuja wakiwa  mahututi.

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Hussein Kidanto akipokea msaada wa mashine za kufuatilia mapigo ya moyo kwa mgonjwa mahututi wakati akiendelea na tiba kwenye hospitali hiyo. Shughuli ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika hospitali hiyo.
  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga akipokea moja ya mashine za kufuatilia mapigo ya moyo ya mgonjwa mahututi wakati wakiwa kwenye tiba kwenye hospitali hiyo. 

   Baadhi ya wawakilishi wa mfuko wa Human Welfare Trust wakikabidhi mashine hizo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MNH, Hussein Kidanto. 
   Baadhi ya wawakilishi wa mfuko wa Human Welfare Trust.


  0 0

   Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akimkaribisha na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe Victoria Mwakasege, ofisini kwake jijini Dar es salaam. Balozi huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni, anaenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Patrick Tsere aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa sheria.
   Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege kabla ya mazunguzo yao ofisini kwake  jijini Dar es salaam 
  Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege ofisini kwake jijini Dar es salaam 

  0 0  0 0

                                                                       

  logo EACThe  Federal Republic of Germany has signed an intergovernmental agreement with the East African Community (EAC) to support regional health programmes. In total, 30 million euros (34 million USD) will be invested in vaccines and health supply chain management.
  EAC-Logo 
  German development cooperation will provide 20 million euros for the procurement of vaccines against different diseases for children in the EAC. The programme will be implemented in collaboration with GAVI. 

  This new commitment will bring Germany`s contribution to regional immunisation programmes with the EAC to 60 million euros since 2012. Earlier in 2015, Germany hosted the record replenishment of the global vaccination alliance GAVI. As a result, an additional 300 million children will receive live-saving vaccines, including in the EAC.

  Inappropriate cooling systems result in high volumes of vaccines being wasted before they reach the people that need them. This is why Germany also makes available a grant of 10 million euros to support the establishment of the EAC Regional Centre of Excellence for Health Supply Chain Management. 
  The Centre which will be hosted in Kigali will strengthen capacities and support the management of complex supply systems for health products, such as vaccines that need to be kept cool at all times. 
  Amb. Dr. Richard Sezibera, Secretary-General of the EAC, and Member of the GAVI Board said: “We are very happy with new and existing projects that are being financed by the Government of the Federal Republic of Germany. This assistance for the health sector in the EAC reaffirms Germany’s status as a true friend of the people of East Africa.” 
  HE Egon Kochanke, Ambassador at the German Embassy in Tanzania, said: "The new commitments underline that Germany continues to be a strong partner for the EAC, contributing to an integration process that puts the people in the centre." 
  GAVI, the Vaccine Alliance is a public-private global health partnership committed to increasing access to immunisation in poor countries.Gavi brings together developing country and donor governments, the World Health Organization, UNICEF, the World Bank, the vaccine industry in both industrialised and developing countries, research and technical agencies, civil society, the Bill & Melinda Gates Foundation and other private philanthropists. 
  Since as early as 1998, Germany's development cooperation, on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ), contributes to the capacity development of the Secretariat of the EAC and the regional integration in East Africa through a variety of programmes and projects. Germany's funding for Technical and Financial Cooperation with the EAC amounts to a total of 176 million Euros. Germany also provides substantial support for the health sectors in EAC member states.

  Accompanying Amb. Kochanke were Ms. Lena Thiede, Counsellor/Head of Regional Cooperation at the German Embassy in Dar es Salaam; Katrin Brandes of KFW, and; Bernd Multhaup, Programme Manager, GIZ.

  Others at the function were EAC Deputy Secretary General (Planning and Infrastructure) Dr. Enos Bukuku; Lake Victoria Basin Commission Deputy Executive Secretary Patrice Niyongabo; Counsel to the Community, Dr. Albert Kafumbe, and; theGAVI Special Adviser to the EAC Secretary General, Mr. Stephen Karengera.


  0 0

  Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya ufadhiri wa Taasisi ya TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao umelenga kufanya kazi ya kutathimini hali ya kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda linatarajia kufanya tathimini kwa watoto (Wanafunzi na wasio wanafunzi) walio na umri kati ya miaka saba hadi 16 katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kwa lengo la kubaini hali ya kielimu na changamoto zake ilivyo wilayani humo. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  Blogger mpiganaji wa Bukoba Faustine Ruta anapenda kumshukuru Mungu kwa kumfikisha leo hii Sept. 24, siku yake ya kuzaliwa. Anasema hakika Mungu ni mwema kwa kila jambo. Anaishukukuru familia yake, ndugu,  jamaa, marafiki na majirani kwa kumsindikiza vyema katika safari yake hii ya maisha.
  "Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema kubwa. Hakika napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana ambayo natakiwa niitumie kwa mambo mema", Faustine amesema katika mahojiano maalumu na Globu ya Jamii usiku huu.
  Akaongeza: "Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kunisapoti kwa mambo mbalimbali ili mradi nifikie pale ambapo waliamini ni sehemu bora zaidi katika maisha yangu mpaka sasa. 

  "Niwashukuru MABLOGGER wenzangu wote wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kwa ushirikiano tulionao", alimalizia.
  Globu ya Jamii, ambayo inafanya kazi kwa karibu sana na Faustine, inamtakia maisha mema na yenye mafanikio mpiganaji huyu mchapakazi na mbunifu. Tunajivunia kuwa naye pamoja...


  0 0

  “We have become aware that there is a page on Facebook impersonating the genuine Twaweza Tanzania page. To all our stakeholders and interested parties, please be aware that Twaweza has been in operation since 2010. The genuine Twaweza Facebook page contains content going all the way back to that time. 
  We take with utmost seriousness the impersonation of our organization in order to spread rumours and misinformation. It is clear that this has been brought about from our release of an opinion poll. While we welcome debate and discussion on all of our research (of which there is plenty) we are disappointed to note that elements of the discussion have degenerated into deliberate attempts to discredit Twaweza as an organization, to falsely represent us and to make personal attacks on our staff members and partners. 
  We invite all Tanzanians to visit Twaweza’s genuine online presence [insert Facebook, our website and Twitter handles] where we will be happy to engage in a robust, enlightening and respectful discussion.”


  0 0


older | 1 | .... | 984 | 985 | (Page 986) | 987 | 988 | .... | 3285 | newer