Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 983 | 984 | (Page 985) | 986 | 987 | .... | 3282 | newer

  0 0


  0 0

  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi leo Mjini Korogwe ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwapokea baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Korogwe. Jumla ya wanachama 25 walijiunga na CCM katika mkutano huo.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
  Baadhi ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia wasanii.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mratibu wa Veta kanda ya Dar es Salaam Bi. Frorence Kapinga akiwakaribisha wakuu wa vyuo vya ufundi vyenye usajili wa awali wa VETA kanda ya Dar es Salaam kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam. Bw.Habibu Bukko akizungumza jambo wakati wa mkutano la wakuu wa vyuo vya ufundi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa kutano huo. 
   Mgeni rasmi Mwalimu Charles Philemon akizungumza na wakuu wa vyuo na wawakirishi wao(hawapo pichani) wakati alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar.
  Bw. Asanterabi Kanza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya Mashariki akiwasilisha mada kwa wakuu wa vyuo pamoja na wawakilishi wao(hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano huo ili kukumbushana mmbo ya msingi kwenye uendeshaji wa vyuo hivyo vya ufundi.

  Mkutano ukiendelea
   
  Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano huo
   
   Picha ya Pamoja

  Na Mwandishi wetu

  KONGAMANO la wakuu wa vyuo pamoja na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajiri ya  kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo pata usajiri wa awali  ili waweze kupata usajiri wa kudumu vilevile kupewa hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu ili kupata usajiri huo wa kudumu.

  Mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam Mwalimu Charles Philemon  akiongea na wamiliki na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata usajili wa kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki ya kupata hisibati inayoonyesha aina ya kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza, kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili  wao waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.

  Kwani watu mbalimbali hupimwa kutokana na stadi zao mbalimbali wanazozipata  katika vyuo vyetu na kwenda nazo katika kuzitekeleza  maeneo tofauti , watu hao ambao wamepita  kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi  VETA ndio watu wenye stadi za kazi kwani hutenda kazi kutokana na elimu na utashi  mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao kupitia vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA, anasema  “kutokana na semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia kuna watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi kwa umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za utoaji mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika mamlaka ya VETA”

  Pia aliweza kusisitiza fursa ya kujengana kwa kutembeleana baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya kupata ufanisi zaidi  katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani familia inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana ndani ya VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda mwingi  huwa tunakutana mara moja katika maonesho mbalimbali lakini familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo mbalimbali.


  Naye mkurugenzi wa VETA  kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa pamoja na kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza kusema baada ya kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila chuo kiwe kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo ya ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI ni kutambua zile fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo kwenye fani zipi.

  0 0

  Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akifanunua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu, wakati wa maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA wakichukua vipeperushi mbalimbali vya SSRA katika monyesho hayo.
  Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
  Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
  Naibu Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi wa Zanzibar, Issa Ussi Gavu akizungumza wakati alipotembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Juma Malik Akil.  
  Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimsalimu Ofisa wa SSRA, Ally Masaninga, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
   (Picha zote na mpigapicha wetu)

  0 0

  Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
   Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.

  0 0

  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 16 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

  Na:Binagi Media Group
  Semina hiyo imeratibiwa na Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya Shirika la TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao unafanya tathmini ya Kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kwa wanafunzi walio na umri wa miaka Saba hadi 16 katika kujua kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu.

  Baada ya Semina hiyo, Washiriki hao watatembelea shule za Msingi pamoja na Kaya mbalimbali kwa ajili ya utafiti huo na baadae kuwasilisha taarifa yao kwa SHIMATA na baadae TWAWEZA kwa ajili ya kupata tathimini ya hali ya elimu ilivyo Wilayani Tarime. Nchini Tanzania Mradi huo wa UWEZO unajumuisha Wilaya 159.

  Akifungua Semna hiyo, Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara amewataka washiriki hao kuja na tathimi ya hali halisi ya kielimu Wilayani Tarime na namna ya kufanya ili kupandisha kiwango cha ufaulu kwa kuwa tafiti zilizopita zinaonyesha kuwa hali ya ufaulu kwa shule za msingi siyo nzuri huku akisikitishwa wanafunzi kumaliza darasa la saba na kuijiunga na kidato cha kwanza huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 
  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe akizungumza wakati semina
  Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara
  Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara akifungua Semna
  Seemina ikiendelea
  Washirki wa Semina
  Wshiriki wa Semina
  Washiriki wa Semina
  Washiriki wa Semina
  Chai
  Chai
  Chai
  Muda wa Chai
  Mapumziko kwa ajili ya chai
  Washiriki wa Semina Wakitokelezea na kamera ya BMG
  Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya Mahojiano na Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO unaosimamiwa na Taasisi ya TWAWEZA Wilayani Tarime
  Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe (Kulia)
  Baita Matinyi ambae ni Mratibu kutoka Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA

  0 0


  0 0
 • 09/22/15--19:23: KIPINDI CHA JUKWAA LANGU
 • Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York.
  Kutoka Tanzania tuliungana na Richard Kasesela
  Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 21, 2015 ambapo mbali na waongozaji Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio, pia walikuwepo Georgina Lema, NY Ibra na Dr Temba toka New York. Kutoka Tanzania tuliungana na Blogger Mr Verbs wa www.habarika24.blogspot.com, pia kulikuwa na Dr Patrick Nhigula, Hajji Khamis na Emil Mutta na Kennedy

  0 0


  0 0


  Wa pili Kulia waliokaa ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahari ya fedha kwa ajili ya kumuoza binti wa Kaka yake aitwae Milika Daniel Marwa Binagi kutoka kwa Mzee Samweli Chacha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
  Mahari ikihesabiwa
  Kushoto ni Professor Lloyd Binagi (Manamba) na Kulia ni Mzee Chaha Binagi wakihesabu pesa kwa jili ya Mahari ya binti yao
  Baada ya Mahali kukamilika hatua iliyofuata ni familia ya mme na mke kusaini mkataba wa Makubaliano chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa. Taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent school  ya jijini Dar es salaam
  iliyodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969 . Na Forodhani Sekondari  ilyokuwapo kati ya 1970 hadi 2008 ( ilipotaifishwa na serikali) na baada ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurudishwa kwa kanisa Katoliki)  hadi leo, tumeungana  na kuitwa  St. Joseph & Forodhani  ALUMNI .

  St Joseph &Forodhani ALUMNI imeandaa “reunion” mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi tarehe 26 September kwa wanafunzi wote waliosoma shule hizo tajwa hapo juu bila kujali umri, jinsi, dini au kabila.


  Habari njema, kuna wanafunzi waliosoma shule hii maarufu, wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka Canada, Australia, New Zealand Uingereza na Seychelles wanahudhuria mkutano huu wa kishitoria.  Kuna wengine hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30.  Wanarudi kuona shule iliowalea.

  Jumamosi tarehe 26 September 2015 kuanzia saa 3 asubuhi kwa shughuli mbali mbali hadi saa 7 mchana katika viwanja vya St Joseph Cathedral High School.

  Katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles  ambae alisoma hapo na kumaliza kidato cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo  kuendelea na masomo ya juu.


  Richard Rugimbana                                        Sr Theodora Faustine 

  Mwenyekiti wa kamati                                         Mkuu wa Shule  0 0

  Juma Pinto Mwenyekiti Miss Tanzania
  Kamati ya Miss Tanzania inapenda kuwatangazia wadau wote wanaotaka kuandaa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30 Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi hayo.
   
  Mashindano yatakayo fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika ngazi ya kitongoji, wilaya wala Kanda.
   
  Sifa za kuwa Wakala wa Miss Tanzania ni pamoja na
   
  1)      Uwe na Kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali.
  2)      Uwe na mtaji wa kutosha.
  3)      Uwe na uwezo wa kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa.
  4)      Uwe mstari wa mbele katika kukuza sanaa za utamaduni nchini.
   
  Wakala atakaye pitishwa na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa shindano.
   
  Wilaya za Mkoa wa D’salaam, Ilala, Kinodoni na Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Elimu ya Juu.
   
  Ada ya Uwakala ni shilingi milioni moja(1,000,000/-). Ada ya Uwakala italipwa kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na kupitishwa.
   
  Maombi yatumwe kwa barue pepe  misstanzania2015@yahoo.com
  Kwa mawasiliano na ufafanuzi zaidi piga namba zifuatazo:-
   
  0673 521037  Katibu wa Kamati
  0754 337043 Msemaji wa Kamati
  0755 019288 Sekretariet.
   
  Imetolewa na:
   
  JUMA PINTO.
  MWENYEKITI
  KAMATI YA  MISS TANZANIA.

  0 0

   Meneja Malipo ya Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya wateja 50,000 wa zamani na wapya walishiriki na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa hadi asilimia 50 ya mishahara yao na huduma za bure katika baadhi ya miamala kupitia akaunti hizo. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GMT), Mrisho Millao, Meneja Akaunti za Mishahara, Deogratius Kibodya na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo.
   Meneja Malipo ya Mishahara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Amos Lyimo (wa tatu kushoto), akibonyesha kompyuta ili kupata washindi wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya akaunti za mishahara ya NBC iitwayo ‘Mcheza Kwao’ jijini Dar es Salaam leo ambapo zaidi ya wateja 50,000 wa zamani na wapya walishiriki na kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa hadi asilimia 50 ya mishahara yao na huduma za bure katika baadhi ya miamala kupitia akaunti hizo. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GMT), Mrisho Millao, Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo na Meneja Akaunti za Mishahara wa benki hiyo, Deogratius Kibodya.
  Meneja Akaunti za Mishahara wa NBC, Deogratius Kibodya (kulia) akijibu moja ya maswali  ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya mwisho ya kampeni ya Mcheza Kwao ya benki ya NBC ambayo wateja wa zamani na wapya wenye akaunti za mishahara katika benki hiyo walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo nyongeza ya pesa katika mishahara yao na pia waliweza kupata zawadi ya kuondolewa ada watumiapo huduma za mobile banking za NBC kupitia akaunti zao za mishahara. Kushoto Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao na katikati ni Meneja Malipo ya Mishahara wa benki hiyo, Amos Lyimo.

  0 0

  Image result for HIFADHI YA JAMII             
  Na Bashir Yakub

  Hela  ya  mifuko  ya  hifadhi ya jamii  ni  hela  ambayo  mwajiriwa  hukatwa  kiasi  kadhaa katika  mshahara  wake na  mwajiri  hutoa  kiasi  kadhaa  na  kuhifadhiwa  katika  mfuko uitwao  mfuko  wa hifadhi ya  jamii. Mfuko  wa  hifadhi  ya jamiii ni  kama NSSF, PSPF, LAPF, GEPF  n.k. Hii ndio  mifuko  ya  hifadhi  ya   jamii. Ipo  mifuko  ya  hifadhi  ya jamii  ambayo  huhudumia  mashirika  ya  umma  na  ipo  mingine  ambayo  huhudumia  mashirika  binafsi, makampuni  binafsi  na  sasa  ipo  inayohudumia  hata wajasiriamali  wadogo  ambao  sio  kampuni  wala  shirika.
  Lengo  kuu  ni  kumpunguzia  mtumishi  au  mfanyakazi  machungu  ya  maisha pindi  anapostaafu  au  kuacha   kazi.  Ni  kumwezesha  mtu   kuweza  kukabiliana  na  maisha  yake  baada  ya  kutokuwa  na  kazi  iliyokuwa  ikimwingizia  kipato. Ni  kumfanya  asikose  hata  matumizi  ya  kawaida  kama  chakula, malazi, mavazi   na  hata  matumizi  kama  ada  za  shule  ,matibabu  n.k. Mifuko    hii  haipo  Tanzania tu  bali  ni  ajenda  ya  dunia.  Ukienda  ulaya, Amerika, Asia  na  kote  Afrika utaikuta.

  0 0

   Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria (kushoto) akimkabidhi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawii wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando (kulia) tuzo ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya wanafunzi nane na walimu wanne bora wa masomo ya biolojia na kemia.  

  Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita katika hafla ya utoaji tuzo.  

   Afisa Mauzo wa NMB, Joseph Mang’ongo akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Aya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando kadi ya akaunti ya chapchap wakati wa maonesho yaliyokwepo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa.

   Wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa katika hafla ya kuwakabidhi tuzo kwa kuibuka vinara iliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 

  Picha ya pamoja ya meza kuu, Uongozi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wanafunzi na walimu katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita jijini Dar es Salaam.
  ----------------------------------
  Katika kutambua jitihada za wanafunzi na walimu nchini, Benki ya NMB imewatunukia tuzo wanafunzi nane waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya biolojia na kemia kitaifa na walimu wanne waliowawezesha wanafunzi hao kuwa vinara katika masomo hayo tuzo ya jumla ya shilingi milioni 10  mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  Kila mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi kwenye masomo hayo mawili amejishindia jumla ya shilingi milioni 1 na kila mwalimu shilingi laki 5.

  Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Upande wa Taasisi - Noelina Kivaria alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.

  Bi.Kivaria aliwapongeza wanafunzi hao kwa jitihada zao shuleni na kuwaasa wanafunzi wengine wachukulie hiyo kuwa ni sehemu ya changamoto kwao hivyo wakaze kamba ili nao waweze kuwa vinara katika masomo yao.

  Benki ya NMB imekuwa ikiipa sekta ya elimu nchini kipaumbele cha hali ya juu kwa kushirikiana na shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es Salaam ikitoa misaada mbalimbali kama madawati.


  Wanafunzi waliotunukiwa tuzo hizo ni:

  1.      Samwel Felician-Nyamanoro Secondary School

  2.      Jenipher Naali-St. Francis Secondary School

  3.      Joshua Zumba-Uwata Secondary School

  4.      Monica Mtei-Marian Girls Secondary School

  5.      Felister Silvester-Ifunda Tech. School

  6.      Mariam Mzingi-Feza Girls Secondary School

  7.      Elisha Mmari-St. Mary Goreti Secondary School

  8.      Innocent Yusufu-Feza Boys Secondary School

  Walimu waliotunukiwa tuzo ni:

  1.      Halima Tajiri-Feza Girls Secondary School

  2.      Rogasian Fisso-Uwata Secondary School

  3.      Grolius Rwabutomize-St. Mary Goreti Secondary School


  4.      Jane Lalika-Marian Girls Secondary School


  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser (Kushoto )Akimkabidhi Cheti Mshiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali Hafla iliyofanyika Katika Ukumbi wa Parokia ya Yombo Dovya, Temeke Yalio chini ya Taasisi "Sauti ya Mama na Mtoto.".Mama Shekha Nasser ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Shuguli hiyo Kutokana na Juhudi zake za Kupambana Kama mwanamke Mzalendo wa Kiafrika na Mtanzania Pekee anayemiliki Bidhaa yake ya Vipodozi Ijulukanayo Luv Touch Manjano.Pia anahangaika usiku na Mchana kuwasaidia Wanawake wengine wa Kitanzania Kuondokana na tatizo la Ajira na kuwawezesha wanawake Kudhubutu na Kujikita kwenye biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi Ambapo Ameweza kusidia zaidi ya wanawake 30 Kwa kuanzisha Taasisi ya Manjanio Foundation.
       Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser Akiwa kwenye Picha pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya "Sauti ya Mama na Mtoto."Ndugu  David Mwandele wa Pili kutoka Kushoto,Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi Hiyo..Shughuli ilikuwa ni kutoa vyeti kwa kina mama 50 waliopewa mafunzo ya ujasiriamali na taasisi hiyo  ili kuwejengea uwezo wanawake hao wanaoishi katika mazingira magumu ili kuona kwamba wanapata elimu ya kuwawezesha kujikimu na mahitaji yao msingi, yaani waweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa watoto wao, kwa kupitia elimu ya ujasiriamali waliopata.
   Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali wakimpokea kwa Furaha  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser kwenye Halfa hiyo. Easter Lukindo ni mwanamke aliye Dhubutu na kuanza Biashara kwa Kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano chini ya Taasisi ya Manjano Foundation akizungumza Machache kwenye halfa hiyo ambapo aliwaasa washiriki wa Mafunzo hayo Kuacha woga na kujiamini kwamba nao wanaweza,Pia aliwataka Washiriki hao nkuanza Kuchangamkia Fursa zilizopo haraka mara baada ya Kupata elimu ya Ujasiriamali.Alitumia Muda huo Pia Kumshukuru Mama Shekha Nasse Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambayo imempa nafasi ya Yeye Kuongeza Kipato kwa  kujikita kwenye Biashara,
     
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali.

  0 0

   Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia), Bw. Clement Mshana pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes, Bi. Guo Ziqi (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vyombo vya Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Luninga,  kulia) Bw. Clement Mshana wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
   Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing (katikati) akifurahia jambo na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Filamu na Tamthiliya za Beijing kupitia kwenye Luninga ya mwaka 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni jitihada za kukuza filamu pamoja na uhusiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC- wa kwanza kulia) Bw. Clement Mshana (kulia), akikabidhiwa zawadi ya kinyago.

  0 0

  Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower( kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku msanii mwenzake Sony Masamba akiendelea kuzirundi ngoma ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar. Usikose leo siku ya Jumatano kwenye mkesha wa EID maana kuna vitu vingi vipya.
  Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha pamoja na mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight yenye uwezo mkubwa wa katika uimbaji.
  Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake.
  Sam Mapenzi pamoja (kulia) akiimba pamoja na Ashura Kitenge wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika siku ya Jumapili kwenye kiota cha Escape One Mikocheni na leo sio ya kukosa njoo tukeshe pamoja tukifurahi na mziki mzuri kutoka katika bendi hiyo.
  Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower  akiimba huku mashabiki wa bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako uje kuona vitu vipya kutka kwenye bendi hiyo.

  0 0

  IMG-20150919-WA068
  UBA Tanzania staff during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.
  IMG_0311
  UBA Tanzania staffs participate engaged in  aerobics session during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015
  IMG_0330
  UBA Tanzania staffs participate in the aerobics session during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.
  IMG_0358
  A cross section of UBA Tanzania staff in a group selfie  after the exercises during the jogging to bond event which took place on Saturday September 19, 2015.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akutana na wananchi wa Dar es salaam na kupokea malalamiko ya migogoro inayohusu ardhi katika mkoa wa Dar es salaam tarehe 22 na 23, septemba, 2015 kuanzia saa 4.00 asubuhi makao makuu ya Wizara hiyo. 
  Katika siku ya jana tarehe 22 septemba 2015 Mhe. Waziri amepokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Kinondoni na leo tarehe 23 septemba 2015 atapokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Temeke na Ilala.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa Dar es salaam waliokuja kuwasilisha malalamiko yao kuhusu migogoro ya ardhi, kulia ni naibu wake Mhe. Angela Kairuki na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Methew Nhonge, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt.  Selasie Mayunga na Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  naibu wake Mhe. Angela Kairuki na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Methew Nhonge, wakipokea malalamiko ya wananchi wenye migogoro ya ardhi katika mkoa wa Dar es salaam.
   Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.
   Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.
  Wananchi wa manispaa ya Kinondoni wakiwa katika mkutano huo.

older | 1 | .... | 983 | 984 | (Page 985) | 986 | 987 | .... | 3282 | newer