Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 978 | 979 | (Page 980) | 981 | 982 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Ndege aina ya Super Bat DA-50

  us.
  Imetengenezwa Ufaransa na kampuni ya Delair Tech. Hii ni kubwa kidogo, ina uwezo mkubwa na inatumia viwango vya satelaiti za kijeshi vya mawasiliano kutumana kupokeataarifa pamoja na namna ya kuongozwa kwake.
  Superbat DA 50 – Imejaribiwa Mkomazi.
  Na Daniel Mbega, Mkomazi

  Ni majira ya saa tatu asubuhi Jumatano, Septemba 16, 2015 wakati tunawasili kwenye uwanja mdogo wa ndege (air strip) katika eneo la Kisima ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi inayotenganisha mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.

  Uwanja unaonekana mweupe, hakuna ndege! Nikashangaa kwa sababu wenyeji wetu kampuni ya Bathawk Recon wametuambia tunakuja kushuhudia uzinduzi wa ndege maalum zinazopambana na ujangili.
  Kilichoonekana mbele yetu ni hema kubwa ambalo mbele yake kulionekana minara midogo iliyosimikwa kama fimbo. Kwenye banda kubwa ikaonekana ndege ndogo aina ya Twin otter. Nikadhani ndiyo inayozinduliwa, lakini Idrisa Jaffary, mwenyei wetu tuliyekuwa naye kwenye gari akasema, hapa siyo hiyo.
  Mshangao ukanipata baada ya gari kusimama wakati nilipokiona kifaa mfano wa ndege kikiwa kimeegeshwa kwenye bomba maalum kana kwamba ndege inataka kupaa.

  Kama nisingekuwa nazifahamu ndege hizi maarufu kama drones, ningeweza kusema kwamba huo ni mdoli ambao mwanangu angefurahia kama ningempelekea akauchezea.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.  0 0

  Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.
  Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) Foluma Tuition Centre kilichopo Bomani-Tarime Mkoani Mara ni mkombozi kwa wanafunzi wa darasa la awali pamoja na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakati wa likizo.Kutana na Mwl.Hosea Daniel, Madam Elizabeth Daniel, Mwl.Evance Malaba pamoja na Mwl.Malima Mjinja kwa maendeleo ya mwanao kielimu.

  0 0

   HII NAFASI YA PEKEE NA ELEWA MAANA YA MABADILIKO WITO KWA WANAWAKE WOTE [WOMEN AS WINNERBREAD] ELISERENA KIMOLO MWENYEKITI UWT DMV NCHINI MAREKANI. 1.WITO KWA WANAWAKE WOTE.

  Tumepata nafasi ya pekee mwanamke kuwa Makamu wa Rais,Mama Samia anafahamu fika matatizo ya mwanamke ndani ya familia,hivyo kwa mara ya kwanza huu ni ukombozi kwa mwanamket .

  Tumepata mtetezi katika ngazi ya juu kwa sababu siku zote mwanamke ndie anayehusika zaidi na mambo ya familia , huku Nchini Marekani na nchi nyingine kama China au nchi zilizoendelea, Mwanamke anajulikana kama" WOMEN AS WINNERBREAD".Kwanini tunaitwa hivyo , Kwasababu ya jitihada zetu katika jamii.

  Jitihada zetu za kuhakikisha familia zetu zinasonga mbele zikiwa na maendeleo mazuri kuhakikisha hakuna mtoto atakae achwa nyuma katika maendeleo."NO CHILD LEFT BEHIND" .

  Hayo yote yatafanikiwa kwa kuwa na SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.MAENDELEO AU MABADILIKO HAYATOKEI KWA SIKU MOJA,JITIHADA ZETU TUKISHIRIKIANA NA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA Tutafika tunapotaka, Dr. Magufuli alishatutangazia kabisa katika kampeni yake kwamba mama NTILIE hatalipa tena kodi, mara atakapokuwa madarakani,hivi tunahesabu siku ifike. 

  0 0

   Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mikindani mkoani Mtwara
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la MafiaMbarak Dau katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoa wa Pwani
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia suluhu (Kushoto), akishiriki kucheza muziki wa taarab uliokuwa ukitumbuizwa na nguli wa muziki huo, Mzee mwishoni mwa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani.
   PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud (Wanne kushoto waliokaa), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Litice Rutashobya, (watatu kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanakijiji, mbele ya jengo la Kituo Cha Afya, Ungi, Shehia ya Msuka Mashariki, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya TPB kukabidhi jengo hilo kwenye hafla iliyofanyika Sptemba 17, 2015. Kituo hicho kimekamilishwa ujenzi wake na TPB.  0 0

  Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007)
  Mroki Mroki-Father Kidevu
  Sekunde, Dakika, Saa, Siku, Wiki, Mwezi, Mwaka na hatimaye mika nane sasa imetimia tangu Mzee Shauri Timoth Nathan (18/08/1925 – 18/09/2007) ututangulie Mbele za haki kama ulivyotutangulia kuja duniani.

  Nimajonzi sana kwetu hasa ukizingatia kuwa uliondoka katika tarehe ambayo kitinda mimba wako Mroki Mroki 'Father Kidevu' alizaliwa na ni siku kumi tu baada ya kufunga ndoa Mroki.

  Unakumbukwa na wengi sana maana ulikuwa ni mhimili mkuu katika familia, kipekee ni Mke wako Mary O Nathan  pamoja na watoto wako wote, wajukuu wako na vitukuu.

  Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakukumbuka sana na kukuombea kila lililo jema katika mapumziko yako. 

  Tunakumbuka maneno yako ya Mwisho uliotuachia watoto wako kuwa TUPENDANE, TUSAIDIANE na TUSHIRIKIANE, baba hakika hili linatendeka na tupo na umoja uliotujengea na tunajivunia hilo daima.

  Tunazidi kukuombea Baraka na pumziko jema maana sote uliotuacha tutakufuata kama tulivyo kufuata hapa duniani.

  Jina la Bwana Lihimidiwe Amina.

  0 0

  Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya mkutano vya Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba kwa ajili ya kampeni yake kwa wananchi wa Jimbo hilo la Mkoani.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Siasa jukwaa kuu baada ya kuwasili katikac viwanja hivyo kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni katika viwanja vya mpira Black Wizard Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
  Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Mkutano wake wa Kampeni Jimbo la Mkoani Pemba.
   Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot. zanzinews.com
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  0 0
 • 09/18/15--12:48: HABARI SEPTEMBER 18 | CH10

 • 0 0


  0 0

  WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe  za hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na  matumizi ya madawa ya kulevya.

  Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya kemia na biolojia kwa mwaka 2013-2014 iliyofanyika leo Ijumaa (Septemba 18, 2015), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Dkt Donan Mmbando alisema hatua hiyo ni mkakati wa serikali wa kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya nchini.

  Dkt Mmbando alisema  Wizara kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa mchango mkubwa wa uchunguzi wa kimaabara kuweza kutambua dawa za kulevya na pia kuwatambua waathirika wa dawa hizo.

  “Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa kazi zinazofanywa na wakala wa maabara na mkemia mkuu wa serikali katika kulinda afya na usalama wa watu na mazingira pamoja na kuleta uelewano katika jamii” alisema Dkt Mmbando.

  Aidha alisema serikali itaendelea kuitegemea Taasisi hususani katika utaalamu kwa utatuzi wa masuala yanayohusiana na kulinda afya na usalama wa jamii, hivyo itahakikisha inaiwezesha taasisi hiyo katika mahitaji ya rasilimalli watu na fedha.

  Aidha Dkt Mmbando aliwapongeza walimu na wanafunzi wote waliofanya vyema katika mitihani yao na kuwakumbusha juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambayo yanaweza kufuta ndoto ya kuwa nguvu kazi ya taifa.

  0 0
  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(kulia) akikata utepe
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(kulia)akisoma jiwe la Msingi kwenye hafla ya uzinduzi wa Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja. 
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi wakati wa kumkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha. 
  Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Magereza mbalimbali yaliyopo Mkoani Arusha wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbaraka Abdulwakil(hayupo pichani).
  Bidhaa za majumbani zinazopatikana katika Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Arusha waliosimama mara tu baada ya kuzindua Huduma za Duty free shop ya Magereza Mkoani Arusha(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Arusha, SACP. Hamis Nkubasi(wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, SACP. Venant Kayombo(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Mart LTD, Bw. Mohamed Panjwan
  Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja pamoja na Uongozi wote wa Jeshi hilo kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao ya kazi hususani huduma za "Duty free shops".
  Mhe. Mbarak Abdulwakil ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa "Duty free shop"ya Magereza Mkoani Arusha iliyofanyika leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha ambapo baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Binafsi wa Mkoa wa Arusha walihudhuria hafla hiyo.
  "Nampongeza kwa dhati Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja kwa jitihada hizi ambapo matunda yake yanaonekana na amethibitisha kwamba azma ya kusambaza huduma hii nchi nzima ipo pale pale na jitihada zinaonekana". Alisema Abdulwakil.
  Ameongeza kuwa lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya Maafisa na Askari wa Majeshi yote ya Ulinzi na Usalama unatekelezwa ipasavyo kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
  Aidha, Mhe. Abdulwakil amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha Maafisa, askari pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.
  Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar Mart LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.
  Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za "Duty Free Shop" na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenda kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.
  Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya "Duty Free Shops" tisa(09) ikiwemo Gereza Kuu Ukonga na Keko - Dar es Salaam, Gereza Isanga - Dodoma, Gereza Kuu Karanga - Moshi, Gereza Butimba - Mwanza, Gereza Ruanda - Mbeya, Gereza Lilungu - Mtwara, Gereza Uyui - Tabora, Chuo KPF - Morogoro na duka la tisa(09) ni Gereza Kuu Arusha.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa pili kushoto)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Huduma za Magereza Duty free shop Mkoani Arusha leo Septemba 18, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Arusha(wa kwanza kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dar Smart LTD, Bw. Mohamed Panjwani.

  0 0
 • 09/18/15--13:30: TAMKO LA AZAM TV
 •  
  Wadau, tunapenda kusahihisha baadhi ya taarifa zinazosambaa kuhusiana na urushaji wa mechi za VPL (Vodacom Premier League) na La Liga.


  Katika mkutano wetu na bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) tarehe 15 Septemba 2015, AzamTV iliiomba bodi kufikiria kubadili muda wa kuanza mechi za ligi katika siku za Jumamosi na Jumapili ili kuruhusu urushaji wa mechi nyingi zaidi za moja kwa moja (live). Hivi ndivyo jinsi ligi za nchi za barani Ulaya zinavyofanya ili kuhakikisha wapenzi wa soka wanashuhudia mechi kadhaa ndani ya siku moja. Kwa mfano, mechi tatu za EPL huruka muda tofauti katika siku moja.

  Kama hapa nyumbani Tanzania, mechi za ligi nazo zingepangwa kuanza muda tofauti kama wanavyofanya wenzetu, kwa mfano mechi zingeanza saa 8:00 mchana, Saa 10:00 alasiri na saa 12:00 jioni, basi wapenzi wa soka wasingepata shida kuchagua mechi gani ya kuangalia na badala yake kuangalia mechi zote 3. Kuliko ambavyo watakapokuwa na wakati mgumu wikiendi hii ambapo mechi zote zitaanza saa 10:00 alasiri.


  Hii ina maanisha, si wapenzi wa soka tu watakaofaidika na mabadiliko haya, bali fursa hii ya kuonekana moja kwa moja (live) kwenye TV itaongezeka maradufu kwa wachezaji, klabu zao, pamoja na wadhamini wao. Vile vile hii inamaanisha kwamba sio timu kubwa tu zitakazofaidika, bali timu zote kwenye ligi ya VPL zitapata nafasi ya kuonyesha ujuzi wao mbele ya wadau na wapenzi wa soka. 

  Hizi mechi zitaonyeshwa kupitia chaneli ya Azam One na Azam Two ambazo mbali ya kupatikana ndani ya Tanzania, pia huonekana katika ukanda wote wa Kusini wa jangwa la Sahara katika nchi ambazo AzamTV inapatikana. Kwa hiyo kuongeza fursa ya kuonekana ndani na nje ya Tanzania. Tumefurahishwa na bodi ya Ligi kuu Tanzania kuonyesha ushirikiano katika kuunga mkono hoja hii na wataendelea kulifanyia kazi pamoja nasi ili kufanikisha ratiba ya aina hii.

  Wateja wetu wa chaneli ya Azam Sports HD (ambayo inapatikana Tanzania tu) nao watapata fursa ya kuangalia baadhi ya mechi hizi katika ubora wa HD. Chaneli ya Azam Sports HD ni chaneli maalum inayoonyesha mechi za ligi ya Hispania (La Liga) ndani ya AzamTV. Hata hivyo taarifa za kizushi zilizoenezwa kwamba, tumependekeza ratiba hii ili kuitangaza zaidi La Liga kuliko VPL, hazina ukweli wowote. Mechi zote za Ligi kuu ya VPL zitarushwa kupitia chaneli zetu mbili za kimataifa – Azam One na Azam Two. Hii inamaanisha wateja wetu wote watapata nafasi ya muendelezo wa mechi kuanzia saa nane mchana mpaka saa sita za usiku kila mwisho wa wiki kwa kipindi chote cha msimu wa Tanzania, Afrika Mashariki na Hispania.  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI, Mohammed Tibanyendela akizungumza na waandishi wa habari juu ya maswala mbalimbali ikiwemo viongozi wa juu kufanya kikao kinyemela leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
   Kamishna wa Tanga wa NCCR-MAGEUZI, Ramadhan Manyeko akizungumza na waandishi wa habari juu ya kushiriki kikao cha jana cha utoaji taarifa nje ya utaratibu wa chama leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.

   Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI,Mohammed Tibanyendela katika ofis za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka

   Na Chalila Kibuda
  CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimesema mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Land Mark  jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho hawajajua lengo lake kutokana na kutokwepo kwa baraka ya vikao kwa mujibu wa chama hicho.
  Akizungumza leo  na waandishi habari jana Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chama hicho, Mohamed Tibanyendela amesema kuwa mkutano huo hujafanyika kwa kufuata taratibu hivyo wanaamini kuwa walikuwa wanazungumza  masuala yao wenyewe na sio masuala yanayohusiana na chama hicho.
  Amesema kuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu ndio watendaji katika uendeshaji wa vikao vya chama lakini hadi wanakwenda kuzungumza na waandishi wa habari hakuna taarifa ya maandishi katika ofisi hiyo.
  Tibanyendela amesema kama kumekuwepo na manung'uniko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kwamba suala hilo lingezungumzwa ndani ya vikao kutokana  na viongozi waliozungumza walikuwa wakishiriki katika vikao vya UKAWA.
  Amesema kuwa kikao kinachotambulika kilifanyika Septemba 16 katika ofisi ya chama lakini kufuatia na kikao cha jana hakikuwepo hivyo  watakwenda tafsri katiba juu ya viongozi kuzungumza masuala ya chama bila kuwepo kwa vikao vinavyotambuliwa kikatiba.
  Aidha amesema  kuwa katika harakati zozote lazima kutakuwa na milima na tambalale yote haya ni kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani.
  Kamishina wa Tanga wa Chama hicho, Ramadhan Mnyeko ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa yeye aliitwa na Mwenyekiti lakini alikuwa hajui anaitiwa nini katika hoteli ya Land Mark.
  Amesema gharama za kuja Dar es Salaam  amejilipia mwenyewe kwani na taarifa ya kufika alipigiwa simu na sio barua.

  0 0
 • 09/18/15--13:43: TANGAZO LA MSIBA
 • Mr and Mrs Nyango'oro wanasikitisha kutangaza msiba wa baba mzazi wa Julie Nyang'oro uliotokea 09/17/2015 huko nyumbani Moshi. 

  Mipango ya mazishi inafanyiwa na mfiwa anatarajiwa kusafiri kwenda hudhuria mazishi.

  Kwa taarifa Zaidi tafadhali wasiliana na Julie Nyang'oro 614 595 4896 na Metty Nyang'oro 614 226 4216.

  Wana mfuko na wasio wana mfuko tunaombwa kwenda nyumbani kwa wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

  BWANA AMETOA BWANA AMETWAA. 
  AMINA.

  0 0

  MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA),  imetoa Sh. 10, 486,000 kwa ajili ya kudhamini tuzo za Wanamichezo Bora waliofanya vizuri zaidi katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. 

  Tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA zinatarajiwa kufanyika Oktoba 8, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo pia TASWA itatoa Tuzo ya Heshima kwa Rais Kikwete ikiwa ni kuthamini mchango wake kwa sekta ya michezo katika uongozi wake. 

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo, alisema wameamua kusaidiana na TASWA kwa sababu Rais Kikwete ni mdau mkubwa wa michezo na pia wa masuala ya utalii. 
  ‘’Dk. Kikwete ni mdau mkubwa  wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwani kwa kipindi chote ambacho amekuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ametembelea hifadhi hii  mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa letu waliomtangulia. 
  ‘’Pia amekuwa mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika  kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya Ngorongoro katika mataifa mbalimbali duniani alikokwenda kwa ziara za kikazi. 
  ‘’Jambo hili limeleta watalii wengi nchini kutoka mataifa  mbalimbali dunini. Vile vile ziara zake za mapumziko hifadhini wakati wa sikukuu mbalimbali zimewahamasisha sana  Watanzania walio  wengi kutembelea  hifadhi hii kutoka kote nchini na hata nchi jirani,’’ alisema Akyoo. 
  Pia alisema waandishi wa habari ni wadau wakubwa na muhimu katika harakati za utalii na ndiyo sababu wameamua kuisaidia TASWA ifanikishe shughuli yake. 
  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru mamlaka ya hifadhi hiyo na kusema kuwa msaada huo ni mkubwa na kuomba wadau wengine waungane nao kufanikisha jambo hilo. 
  ‘’Kama tulivyosema bajeti yetu ni Sh milioni 130, juzi (Jumatano) tulipata watu wa GSM Foundation waliotupa Sh. Milioni 50, tunaomba na wengine tushirikiane nao katika hili,’’ alisema Mhando. 
  Alisema TASWA imeamua kuandaa hafla ya wanamichezo kumuaga Rais na pia kumpa tuzo kwa vile wakati wa uongozi wake amefanya mambo makubwa katika sekta ya michezo. 
  Kwa mujibu wa Mhando, wanamichezo pia watatumia tuzo hizo zilizoandaliwa na TASWA kumuaga Rais Kikwete anayemaliza muda wake kikatiba baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25, mwaka huu.

  0 0

  The Chairman of the UN High level panel on Global Response to Health Crises President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete leads a consultative session in New York. On his right  is the UN Deputy Secretary General Mr.Jan Eliason.  
  The Secretary-General has asked the Panel to make recommendations to strengthen national and international systems to prevent and manage future health crises, taking into account lessons learned from the response to the outbreak of Ebola virus disease.
  In carrying out its work, the Panel will undertake a wide range of consultations, including with representatives from the affected countries and communities, the United Nations system, multilateral and bilateral financial institutions and regional development banks, non-governmental organizations, countries supporting the response effort, other Member States, health-care providers, academic and research institutions, the private sector and other experts.  
  The Panel will be supported by a Resource Group of leading experts which is to provide advice to the Panel on technical and other issues.The Panel held its first meeting in early May 2015 and is expected to submit its final report to the Secretary-General at the end of December 2015.  
  The Secretary-General will make the report available to the General Assembly and undertake further action as appropriate.Other panel members include Celso Amorim from Brazil, Micheline Calmy Rey from Switzerland, Marty Natalegawa from Indonesia, Joy Pumaphi from Botswana and Rajiv Shah from the US.

  0 0


  MWENYEKITI  wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji (PICHANI) amenyakua tuzo ya kielelezo cha viongozi wa biashara wa Afrika kwa mwaka 2015.

  Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, aliwapiku wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo bilionea namba moja Afrika,  Aliko Dangote.
   Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi Quality Group, ilisema  tuzo hiyo ilimshtua 'bosi' wao kwani hakutarajia na kwamba itasaidia kuvutia wawekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii
  nchini.  Tuzo hizo zilitolewa Septemba 16 mwaka huu.
  Taarifa hiyo iliongeza ya Manji ni chachu kwa vijana kufanya vizuri kwenye sekta zao na  itasaidia nchi kusonga mbele katika kujikwamua na umasikini.  Tanzania inaendelea kujukulikana kimataifa na itasawaidia watanzania kwa ujumla kufanya kazi ama biashara katika nchi nyingine bila ya vikwazo visivyo na msingi kupitia tuzo hiyo.
  Baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Emirates Group, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege ya Emirates inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na
  nyingine kubwa.
  Wengine ni Mwenyekiti wa Emmar Properties, Mohammed Alabbar pia bilionea kutoka India, Ratan Tata anayemiliki kampuni kubwa yaEmeritus of Tata Sons Ltd.
  Pia bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri, Mukesh Ambani ambaye ni mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
  Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Manji, pia kampuni yake ya Quality Group imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa uhakika kwa bara la Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”

  0 0

   Mtendaji Mkuu katika Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa aliyekuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi.  

   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu wakionesha vipaji vya  kuimba na kucheza wakati wa mahafali ya 23 shuleni hapo
   Sehemu ya wahitimu wa kidato cha nne katika mahafali katika Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu wakifuatilia matukio katika sherehe hizo
    Mmoja wa wazazi aliyeshiriki mahafali ya 23 ya Shule ya Sekondari St. Mary’s Mazinde Juu akichangia ujenzi wa maabara ya sayansi shuleni hapo
    Mkuu wa Shule ya Sekondari St. Mary’s Mazinde Juu, Sister Evetha Kilamba akikata keki maalum ikiwa ni moja ya shamrashamra za mahafali shuleni hapo.  
  Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa akizindua maktaba mpya ikiwa ni sehemu ya sherehe za mahafali ya 23 katika Shule ya Sekondari ya St. Mary’s Mazinde Juu. (Picha Kwa Hisani ya PDB).


  0 0


older | 1 | .... | 978 | 979 | (Page 980) | 981 | 982 | .... | 3282 | newer