Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

PEDIATRIC NURSE REQUIRED

$
0
0

An exciting career opportunity for a Certified Registered Nurse to work for private pediatric clinic located in downtown Dar es Salaam. The individual should have some pediatric nurse experience and be able to communicate well and appropriately with children and their parents or guardians.
He/She should be:
  • Registered with Tanzanian Nursing Council
  • Have excellent planning and organization skills
  • Have time and record keeping management skills
  • Must be computer proficient specifically with MS Office, Word and Excel
  • Must be able to read, write and speak fluently in Kiswahili and English
  • Additional language will be of an added advantage
  • A quick learner and who is customer care oriented
  • Not be more than forty (40) years of age
  • Pediatric nursing experience will be of an added advantage

NB: All interested candidates are required to apply by sending their current Curriculum Vitae with full communication addresses [including contact phone numbers] of three referees who can testify to the applicant’s academic abilities, working experience and character.

Please reply to this advertisement with your detailed CV to darchildclinic@gmail.com no later than April 15th, 2013. Only Short listed candidates will be contacted. 

TASWIRA ZA WATANI WA JADI WAKATI WA KUAPISHWA RAIS UHURU KENYATTA

$
0
0
 Biashara ilikubali
 Madheee wanakwambia leo hakuna kulia....
 Ulinzi ulikuwa mkali na makini
 Kila aina ya tamaduni ziliwakilishwa
 Wengi walikuwa kizazi kipya
 Maji yakiwahishwa 
 Vuvuzela ndani
 Kila barabara ilielekea Moi Centre
 Mambo yalikuwa live kutwa nzima
 KTN ndani ya nyumba
wadau wakisubiri muda

Mh. Lowassa atoa msaada wa sh. mil. 5 kwa Baraza la Misikiti Tanzania

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa kukabidhi msaada wa sh. mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana,katika makabidhiano yaliyofanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.
Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

UZINDUZI WA MPANGO KAZI WA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO

MUNGU IBARIKI AFRIKA WARINDIMA KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA NNE WA KENYA UHURU KENYATTA

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU KAMATI MAALUM YA KATIBA

$
0
0
Prof Yash Ghai kutoka Kenya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kamati maalum ya katiba ya kituo cha sheria na haki za binadamu.
wanakamati wakisikiliza salamu za ukaribisho na ufunguzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Maboresho na Ushawishi wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu,wakili Harold Sungusia.
Wanakamati wakipiga makofi kushangilia uzinduzi huo rasmi wa kamati maalum ya katiba ya kituo cha sheria na haki za binadamu.
Baadhi ya wanakamati wakiwa nje ya ofisi za Kituo cha sheria na haki za binadamu.

FILAMU YA LOVE AND POWER YA KANUMBA KUINGIA MTAANI RASMI IJUMAA TAREHE 12th APRIL 2013.

$
0
0

Pichani kati ni mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa akizungumza na Wanahabari Mapema leo jijini dar.

Dar es Salaam, 10th April 2013

Imetayarishwa na Kanumba the Great Film , ikiongozwa na Steven C. Kanumba imeandikwa na  Ally Yakuti.


Ile filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa filamu hatimaye mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa tarehe 12th April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na kusambazwa nchi nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment Ltd.


Akizingumza na waandishi wa wanahabari mratibu wa filamu ya Love & Power Bwana Myovela Mfwaisa amesema kuwa  “Filamu ya Love & Power  ni filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu The Great Kanumba  inaingia sokoni na kuwafikia watanzania wote siku ya ijumaa,”


Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu Tanzania.


Akizungumzia kwa ufupi juu ya filamu ya Love & Power Bwana Myovela, “Filamu ya Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na marehemu  kuongozwa na Steven Kanumba, Watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd imetengenezwa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo  tofauti tofauti.


Lugha iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya kiingereza imetumika  kama ‘Subtitles’. Umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16 ni filamu nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na familia, iliyopewa kibali cha ukaguzi  Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza Tanzania.


Katika kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao tunaomba kila mdau wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za kitanzania kwa kupambana na Maharamia wa kazi za Wasanii wa filamu, pia tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua filamu ya Love & Power halali.


Unaweza kupata filamu ya Love & Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa namba hizi:  0716 788 805, 0713 570 581

Asanteni.

sophia simba azindua tovuti ya kupaza sauti ya mwanamke mjini dodoma leo.

$
0
0
 Mhe. Sophia Simba akipewa maelezo na Bill Marwa kuhusiana na  tovuti rasmi iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kupaza sauti ya mwanamke (www.sautiyamwanamke.org) baada ya kuizinduwa kwenye uzinduzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika Dodoma.  Waliosimama kushoto kwa waziri ni Teresa Yates na Hilda Mashauri viongozi wa mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) waandaaji wa mdahalo huo.Tovuti hiyo itatumika kutoa taarifa za kila siku za mdahalo na kuendelea kupaza sauti ya mwanamke baada ya mdahalo kwa kuandika habari mbalimbali zinazohusu mwanamke. 
Teresa Yates, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania akikabidhi zawadi kwa Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto  na kwa Dr. Rose Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. 
 Mwanahamisi Salim, Meneja wa Kampeni, Ushawishi na Utekelezaji wa Haki za Kiuchumi kutoka shirika la Oxfam akiendesha zoezi la ufunguzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma. 
 Dr. Rehema Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto kwa ajili ya kufungua rasmi mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. 
  Mshiriki kutoka Unguja akizungumza kwa niaba ya wanawake takribani 300 wanaoshiriki mdahalo wa kitaifa wa wanawake uliozinduliwa leo Dodoma na Mhe. Sophia Simba (MB) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto. 
  Baadhi ya Wanawake wanaoshiriki Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake. Mdahalo wa Kitaifa wa wanawake ni tukio linalofanyika kwa hisani ya mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia (CSO Gender Coalition) kuanzia tarehe 10-14 April, 2013 mkoani Dodoma.

jijini dar leo

$
0
0
Ujenzi wa upanuzi wa barabara wa mwendo kasi katika ya barabara ya Morogoro ukiendelea katika eneo la Magomeni Mapipa, ujenzi huo utakapomalizika utarahisisha usafiri katika jiji la Dar es Salaam na kupunguza msongamano wa magari.
Ujasiramali upo wa aina nyingi ili kujisaidia katika kupata kipato na kuweza kujikimu . Pichani kijana akiwa amejiajiri kwa kazi ya kufuta vioo vya magari katika eneo la barabara ya Morocco jijini Dar es Salaam kama kamera yangu ilivyomnasa hivi karibuni.

DKT. SHEIN AFANYA UZINDUZI WA MRADI WA UMEME KILOWAT 100 ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akikata utepe na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, kama ishara ya uzinduzi mradi wa Umeme wa Njia ya Pili ,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuzindua mradi wa Njia ya Pili ya Umeme,kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,hafla hiyo ilifanyika jana katika kituo kikuu cha Umeme Mtoni Mjini Zanzibar.
Hiki ni Kituo kikuu cha Umeme cha Mtoni Unguja.ambacho tayari Mradi wake uliofadhiliwa na MCC Marekani umezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kwa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo, pia Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt, alihudhuria katika uzinduzi huo,utakaochukua Ukubwa wa Kilowati 100.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la ‘Millennium Challenge’ MCC,Daniel Yohannes Ceo,(katikati) na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania ALfonso Lenhardt,wakipata maelezo ya kiutendaji kazi katika kituo kikuu cha umeme kutoka Ubungo Dar es Salaam mpaka Mtoni,ukiwa umefadhiliwa na Shirika la Misaada la MCC la Marekani,kwa Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali,(kushoto) baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Norway yaisaidia Tanzania Sh. bilioni 200 kwa ajili ya umeme vijijini

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akiwa na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas, muda mfupi kabla ya kusaini Mkataba wa Krona 700 (sawa na sh. bilioni 200 za Tanzania) uliotolewa na Serikali ya Norway kwa Watanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akitiliana saini na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas kuhusu msaada wa Krona 700 (sawa na sh. Bilioni 200 za kitanzania) kutoka Serikali ya Norway kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya miradi ya umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto), akipeana mkono na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Bw. Heikki Holmas, baada ya kusaini mkataba wa Krona 700 (sawa na sh. Bilioni 200 za Tanzania) uliotolewa na Serikali ya Norway kwa Watanzania kwa ajili ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini.

President Kikwete mourns Thatcher, Signs a Condolence book

$
0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence book at British High Commissioner's Office in Dar es Salaam following the death of former British Prime Minister Margareth Thatcher who died of stroke on Monday at the age of 87.Photo by Freddy Maro

Mh. CHIKAWE AUNGURUMA GAMBIA

WAKE WA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI TANZANIA WAWATAKA WANAWAKE WABUNIFU KUIGA MFANO WA ENJIPAI

$
0
0
Mwenyekiti wa kundi la wake wa mabalozi nchini (DSG) Juliana Parroni akifungua mkutano wa wake wa mabalozi nchini "Coffee meeting" uliyofanyika katika ukumbi wa Synergy Grill Oysterbay jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Mke wa Balozi wa Japani nchini Tanzania Bi. Keiko Okada (kulia) akimtambulisha aliyewahi kuwa Miss Tanzania (2008) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Duka la bidhaa za Kiutamaduni zinazotengenezwa kwa Mikono na wanawake wa Kimasai - ENJIPAI Nasreen Karim aliyepata fursa ya kuonyesha kazi za mikono zinazotengenezwa na wanawake wa Kimasai walioko katika kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim (wa pili kulia) lilipo barabara ya Kaunda Drive Oysterbay jijini Dar es Salaam akielezea namna anavyofanya kazi zake za ubunifu wa bidhaa za shanga na kinamama wa Kimasai.Zaidi Bofya HAPA chini

Sehemu ya wake wa Mabalozi nchini na wageni waalikwa wakipiga makofi baada ya kusikia Utambulisho wa kazi anazofanya Nasreen Karim Mkurugenzi Mkuu wa Duka la ENJIPAI.
Picha juu na chini wake wa mabalozi nchini katika Coffee meeting yao.
Nasreen Karim akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa kutoka Umoja wa Ulaya.
Nasreen Karim akimvisha moja ya bidhaa za Shanga mmoja wa wageni waalikwa kutoka World Bank Bi. Sharon Mitchell aliyetokea kuvutiwa na kazi za mikono ya kinamama wa Kimasai wa duka la ENJIPAI.
Mkurugenzi Mkuu wa Duka la ENJIPAI Nasreen Karim akimvisha mkufu wa shanga mmoja wa wake wa mabalozi wakati wa maonyesho ya bidhaa zake kwenye Coffee meeting ya wake wa mabalozi nchini.
Mke wa Balozi wa Nigeria Bi. Naomi Majnabu (kushoto) na Mke wa Balozi wa Rwanda nchini Bi. Mary Rugangazi (katikati) wakimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim kwa kazi nzuri ya ujasiriamali anayofanya.
Nasreen Karim akifurahi jambo na Mke wa Balozi wa Misri wakati wa maonyesho ya bidhaa za duka la ENJIPAI yakiendelea.
Nasreen Karim katika picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mkuu wa duka la ENJIPAI Nasreen Karim katika picha ya pamoja na baadhi ya kinamama wa Kimasai anaofanya nao kazi za kutengeneza bidhaa za shanga mara baada ya maonyesho hayo wakati wa Coffee meeting ya wake wa mabalozi.
**************************************
Na. Mwandishi wetu
Wanawake wajasiria mali haswa wa fani ya vifaa vya urembo vya asili kama vile mikufu ya shanga na vinginevyo nchini Tanzania wametakiwa kujitangaza zaidi kimataifa kwa kushiriki maonyesho mbalimbali ili kuonyesha uwezo wao.

Akitoa rai hiyo wakati akimtambulisha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya inayotengeneza bidhaa hizo ya Enjipai Bi. Nasreen Karim kwa niaba ya wake wa mabalozi hao, Mke wa Balozi wa Japan hapa Tanzania Keiko Okada amesema bidhaa hizo zinazo tengenezwa kwa shanga zinapendwa na zinahitaji kutangazwa kimataifa.

Wake wa mabalozi hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mikutano yao ya kila mwezi maarufu kama ‘Coffe Meeting’, kuzungumzia miradi wanayoifanya ambapo kila wakati huwa wanaalika wajasiria mali tofauti na kwa wakati huu wamealika kampuni iliyokusanya akimama wa kimasai wanaotengeneza bidhaa tofauti za shanga ya’Enjipai’.

Enjipai ni kikundi kilichoanzishwa miaka miwili iliyopita chini ya Bi. Nasreen Karim na leo kupata mualiko kutoka kwa wake za mabalozi kuonyesha bidhaa wanazozitengeneza.

Akizungumza Mimi niko Nasreen Karim kama unavyojua kazi zetu ni kwa wawezesha wanawake kwa namna hiyo hivyo nitazungumza na wageni hawa kuwaonyesha bidhaa zetu na baadae tukimaliza watatambua wapi tunataka kuelekea na kudhibitisha kuwa tukiwezeshwa tunaweza.

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI

$
0
0



GOOD NEWS FOR KENYA
AIR CARGO TO NAIROBI 
£2.80 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN KENYA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA TU KENDA HOUSE
TOM MBOYA STREET NAIROBI
FLIGHTS EVERY WEEK
WE COLLECT FROM ANY ADDRESS IN UK FROM £40 
MINIMUM WEIGHT IS 35KG

  CONTAINER PRICE CUT!
40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950
20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
THIS IS MORE THAN £300 DISCOUNT!
THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE

www.serengetifreight.co.uk


NB: TUNAHITAJI MTU MWENYE UZOEFU WA KUFANYA CUSTOMS ENTRY FOR EXPORT
MSHAHARA NI £11.50 KWA SAA



SALIM ALI MTOKO NEW COLLECTION

$
0
0
To be launched on 17th april at Alliance francaise in Dar es salaam.
 Entrance is  free.

HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHESHIMIWA MIZENGO PETER PINDA (MB), KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA BUNGE KWA MWAKA 2013/2014

$
0
0

       Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja kwamba kutokana na Taarifa zilizowasilishwa leo na Wenyeviti wa Kamati za Katiba, Sheria na Utawala; Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; na Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara na Kamati ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya ndani ya Bunge lako Tukufu ambazo zimechambua Bajeti ya Mafungu ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2012/2013 na Mwelekeo kwa mwaka 2013/2014. 

Vilevile, naliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2013/2014.


introducing Libeneke la Pangani Information Alliance

$
0
0

Habari Ankal,

Natumai umzima na unaendelea na majukumu yako kama kawaida ya kuliendeleza hili libeneke la globu yetu ya jamii.

Sisi ni vijana ambao tumeanzisha maktaba hapa Pangani, Tanga. tuliwahi kuweka post yetu kwenye globu ya jamii na tukapata muitikio mzuri. Baada ya post ile Prof Mbele kutoka Marekani alituchangia vitabu na
Mr. Rodrick Maro kutoka kituo cha msaada wa sheria naye pia ametupatia vitabu.

Bado tunahitaji vitabu zaidi na tunatoa wito kwa Watanzania waliopo ndani ya nchi na nje ya nchi kutuunga mkono katika hili, kwa kuchangia moja kwa moja au kutuunganisha na anayeweza kutuchangia akiwa ni mtu au shirika, taasisi au kampuni.

Leo naileta habari moja ya mafanikio, tumeweza kuanzisha blog yetu ambayo tutakuwa tukipost mambo yetu na kupokea ushauri na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau wote watakaounga mkono jitihada zetu.

Tunapatikana katika www.panganiia.blogspot.com

Karibuni wote.

Kamburuta, Ally Said
Mratibu

Article 7

kanyaboya ya kujiepusha nayo, jamaa keshalambwa email yake hapa

$
0
0
Hi I just arrived in Greece and I am in a fix. Can I get a loan of to 2950 Euros or whatever amount if not all. You'll have it as soon as I get back. It's really urgent, please get back to me asap if you can. I will advise on how you can get it to me.

Regard

Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa, Middle East, Arabian Gulf & Persian Gulf
Registered as Societies (Application for Registration) Rules 5, 1954, by United Republic of TANZANIA
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Registered as Societies (Application for Registration) Rules 5, 1954, by United Republic of TANZANIA
President, East & Central Africa Professional Boxing Association (ECAPBA)
Registered as not for profit entity No. 93291, by the United Republic of TANZANIA
Member of the Board of Directors, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Registered as not for profit entity No. 3401556 in England and Wales, UK

Benjamin William Mkapa Pension Towers
Tower B, Mezzanine Floor, Azikiwe Street
Dar-Es-Salaam - Tanzania

Technology House, 35-38 Ghalla Road,
P.O BOX 1106, Moshi - Tanzania
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>