Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 977 | 978 | (Page 979) | 980 | 981 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Balozi wa China nchini Tanzania Dr. Lu Younq ing akiongea na baadhi ya wasanii wa sanaa ya uchoraji  wa Tingatinga katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China. Tuzo hizo zimetolewa kwa  ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea  katika hafla ya utoaji wa  Tuzo  la Mashindano ya Kimataifa ya Uchoraji wa Tingatinga Tanzania iliyofanyika leo (jana) jijini Dar es Salaam.Tuzo hizo zimetolewa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China ambapo washindi wawili wataelekea nchini China kwa ajili ya kubadilishana utamaduni
    (Picha na Benjamin Sawe- WHVUM)  0 0

  _MG_1920
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiingia katika ukumbi wa mkutano hoteli ya Double Tree by Hilton kwa ajili ya warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.

  Na Mwandishi wetu
  VIJANA nchini Tanzania wanatakiwa kujitambua, kuacha kuwa kigeugeu na kufanya papara ya kupata fedha kama wanataka kuendelea na kufanikiwa kibinafsi na kiuchumi.

  Kauli hiyo imetolewea jana na Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga kwenye warsha ya wadau wa kitaifa ya kujadili suala la ajira kwa vijana Tanzania .

  Kauli yake hiyo kwa vijana hao waliojumuika katika hoteli ya DoubleTree by Hilton, Dar es salaam, ilitokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini ambazo zinaonesha kwamba vijana wengi hawana msimamo wa maisha, hawana maono, hawana malengo binafsi wala kutambua matarajio.
  Amesema: “ Usipojitambua, leo nikija nikakueleza habari za kuanzisha biashara ya matofali utachangamkia. Kesho akija mtu mwingine akakueleza kuhusu uchimbaji wa madini utaacha kutengeneza tofali na kukimbilia machimboni”.


  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha
  TIMU ya panone FC ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro maarufu kama matajiri wa mafuta ,inatarajia kuanza kutupa karata yake ya mchezo wa kwanza wa ligi daraja la kwanza(FDL) dhidi ya maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha.
  Mchezo  huo utafanyika septemba 19 mwaka huu, katika uwanja wa Ushirika mjini moshi mkoani kilimanjaro,ambapo  baada ya mchezo huo pia wataikaribisha timu ya Polisi Tabora semptemba  26.

  Katibu wa timu ya Panone FC  Augstino mwakatumbula alisema kuwa msimu  huu  wanaenda kuanza ligi daraja la kwanza  ambapo kila mchezo kwao ni fainali na watahakikisha wanatinga kucheza ligi kuu msimu wa 2016-2017.

  “Tulifanya usajili mzuri wa wachezaji 7  ambao wameungana na wachezaji wetu tuliokuwa nao msimu uliopita na  tunaimani wataisaidia timu hii na tuna jumla ya wachezaji 27 wanaounda kikosi cha timu pia hatukuweza kuwasajili wote waliokuwepo hapo mwanzo na  ni kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo wengine  kutokuwa na nidhamu,uwezo wao umeshuka kimchezo.”alisema Mwakatumbula .

  Aliwataja wachezaji hao saba  ambao wamefanikiwa kusajiliwa na matajiri hao wa mafuta kuwa ni pamoja na Ally Mseja ambaye ni mchezaji huru na Abdallah Shauri ‘Machopa’ aliyetokea timu ya Lipuli –Iringa wote wakiwa ni washambuliaji, Florence  Haure kutoka academy ya Kitayosce ya mkoani Kilimanjaro, Frank Kijoti aliyetokea AFC Arusha Rashid Gumbo kutoka  Kinondoni Manispaa ambaao wote ni Kiungo,Maulid Khalid kutoka  Singida United ambaye ni winga,Mansoul Mansoul  kutoka Coastal Union ya Tanga ambaye ni golikipa.

  Timu hiyo ya Panone FC ipo kambini miezi miwili sasa ikijiweka tayari kwa ajili ya michuano hiyo ya ligi Daraja la kwanza ambapo inatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki mapema wiki hii  na timu za  African sports,Magambo JKT na Coastal Union zote za Tanga .

  Matajiri hao wa mafuta wananolewa na kocha Atuga  Manyundo akisaidiwa na msaidizi wake Azizi Nyoni .

  Ligi daraja la kwanza ina shirikisha jumla ya timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu ambapo timu ya Panone ipo katika kundi ‘C’ na timu za JKT Olojro- Arusha,Polisi Mara –Mara,Rhino Rangers –Tabora,Mbao fc –Mwanza,Polisi Tabora  -Tabora,Geita Gold –

  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini.
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.

  KUONA PICHA ZAIDI
  BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Tamasha la 34 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni, John Mponda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 21 hadi 27, 2015 katika Kumbi na Viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), mkoani Pwani. Kulia ni Katibu wa Tamasha hilo na Ofisa Biashara, Benjamini Malimbali na Ofisa Habari, Sophia Mtakajimbo.
    Hapa Mwenyekiti wa Tamasha hilo, John Mponda (kulia) akisisitiza jambo kuhusu tamasha hilo. Kushoto ni Ofisa Habari wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha
  Wanafunzi wametakiwa kuwekeza katika elimu, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha ya sasa na ya baadaye ikiwemo kufanya kazi kwa vitendo ,na mashiko vitavyowasaidia kwenye maisha yao ya sasa na baadae sanjari na kulijenga taifa lao.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa utawala na uongozi wa chuo cha Habari maalum,Mr Ernest Karata wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha Full Bright college kilichopo Ngaramtoni,wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. 

  Katika mahafali hayo wanafunzi  wanane walihitimu mafunzo ya ukatibu muhtasi ualimu wa shule za awali (chekechea) ambapo wote watapata ajira katika shule na vyuo mbalimbali vilivyopo ndani na nje ya nchi.

  Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi mtendaji  wa chuo cha Full Bright College  Mr.Julius Matiko amewaasa wahitimu wajiongeze na wazidisshe bidii katika elimukwani chuo hicho kina vifaa vya kutosha vikiwemo vifaa vya kompyuta,uhazini ambavyo vipo na hotel management .Chuo hicho kimesajiliwa na VETA ambapo pia wanatoa mafunzo ya NABE(National Business Examination)

  Mku wa chuo hicho Rose Mapunda  amewasihi na kuwashauri wazazi wawalete  wanafunzi chuoni hapo wajipatie elimu na maarifa ya kutosha  zikiwemo stadi za kazi mbalimbali iliwatakapotoka chuoni hapo waweze kupata ajira na kujiajiri.

  Mkurugenzi wa chuo hicho cha Full Bright Mr .Julius Matiko ameiomba serikali itoe ruzuku kwa vyuo binafsi ikiwezekana itoe usafiri pamoja na kutoa vifafa mbalimbali vya kujifunzia  na kujisomea katika chuo hicho.

  Akitaja Changamoto zinazokabili chuo hicho ni uhaba wa ardhi ,wa kujenga nyumba za walimu nyumba za kulala wanafunzi, maktaba za kujifunzia  na viwanja vya michezo kwa wanafunzi  na wahitimu wa chuo hicho cha Full Bright

  0 0

   Organisers tell how Julio Ludago (centre) a professional mountain guide at Mt. Kilimanjaro will attempt  beat world record on September 27th 2015 when he ascends and descends Mt Kilimanjaro via Umbwe route – Western breach in less than 6 hours, 56 minutes and 24 seconds which is the current world record held by Swiss-Ecuadorian climber Karl Egloff. To read more CLICK HERE.  


  0 0

   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
  Sintofahamu imeibuka ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi ambapo viongozi wake wamedai kuwa taratibu zilizo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zimekiukwa na kufanya chama hicho kuingia katika mgogoro wa majimbo. 
   Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho,Leticia Ghati Mosore amesema  kuwa NCCR-Mageuzi wamezidiwa idadi ya majimbo kutokana na taratibu nyingi kukiukwa kuanzia serikali ya Mtaa na sasa uchaguzi Mkuu.
   Mama Mosore amesema baada ya kuona mambo hayaendi sawa, na ingawa wataendelea kuwa UKAWA, lakini sasa wameamua kupambana wenyewe kama NCCR-Mageuzi katika kugombea viti vya ubunge pamoja na udiwani katika mgawanyo huo ambao amedai chama hicho kimepata majimbo pungufu ndani ya umoja wa vyama vinavyounda Ukawa. 
  Amesema kuwa ili kukamilisha ushirikishwaji kulitakiwa kuundwa kamati zitakazoendesha uchaguzi ndani ya UKAWA na mambo mengine mengi ikiwemo uwazi wa matumizi ya fedha, lakini hayajaweza kufanyika hivyo . 
  “Mchakato wa kumpata mgombea Urais haukufuta utaratibu katika ushirikishwaji wa vyama vyote vitakavyoweza kutambua mgombea gani anaweza kusimama katika kupeprusha bendera ya UKAWA”, amesema Mama Mosore.
  Mama Masore pia ametaka Mwenyekiti wao Mhe. James Mbatia asiwe msemaji wa CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi) kinadhoofika, akidai kwamba wananchi wanashindwa kututoufautisha UKAWA na CCM na wataamua kuchagua zimwi walijualo. “Tunasisitiza upinzani wa kweli nchini hauwezi kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia, tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na kuwasaidia” alisema. 
  Mama Masore amesema”Tunamshauri Mwenyekiti James Mbatia aitishe vikao vya kikatiba haraka  ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya Chama chetu.Upinzani wa kweli haujengwi kwa kuweka mbele tamaa na maslahi binafsi kuliko taifa, na kwa kutegemea propaganda. 
   “Tangu UKAWA ianze, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa Chama chetu cha NCCR”, amesema mama Masore. 
   Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho,Bw. Mosena Nyambabe amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ndio kinafanya uandaji wa masuala yote bila kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi licha kuwa na udogo katika muungano huo. 
   Bw. Nyambabe amewataka wanachama wote wa NCCR-Mageuzi kushikamana katika uchaguzi mkuu ili kupata majimbo hayo licha ya kuwepo kwa changamoto ya kufanyiwa vurugu na Chadema. Bw. Nyambabe amehoji juu ya hatima ya NCCR-MAGEUZI baada ya uchaguzi na UKAWA wakiwa madarakani huku changamoto zikiwa bado hazijamalizika, akitolea mfano itakuwaje kwenye mgawanyo wa wakuu wa mikoa ,pamoja na wakuu wa Wilaya. 
   Amesema NCCR-Mageuzi imepoteza matumaini katika muungano huo ya kupata wabunge wengi, na kusisitiza kuwa chama hicho kitakuwa na wakati mgumu bila kutafuta ufumbuzi kukiwa bado mapema 
  Mgawanyo wa majimbo ambao unaleta mkanganyiko katika UKAWA ni Chadema –Majimbo 148; CUF (Majimbo 99) ,NCCR-Mageuzi (Majimbo 12) na NLD - Majimbo matatu.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI,Reticia Ghati Mosore akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam  muda huu kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu katika umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutangaza kuendelea na mapambano nje ya umoja huo wa vyama pinzani. 
  Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, Mosena Nyambabe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatima yao ya kupambana kama wenyewe NCCR-MAGEUZI bila ya UKAWAna  kuwa  chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  kuwa inavibana  vyama vishiriki vya UKAWA  katika wagombea wa Ubunge majimboni na wagombea wa udiwani katika kata.

  Kwa taarifa rasmi ya NCCR-Mageuzi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akiwapungia mkono wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa uliofanyika katika kata ya Katolo jimbo la  Busanda mkoani Geita.
   Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.
   Mgombea mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Haji Duni akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Busanda mkoani Geita.

  0 0
 • 09/17/15--10:48: Najivunia DMV Allstars PROMO

 • 0 0

    Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akipanda ngazi kwa kukimbia kwenda jukwaani kujinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Kibondo, Kigoma
  Wananchi wa Kasulua wakifuatilia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dk Magufuli aliwahutubia.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kibondo ndani ya uwanja wa Taifa mkoani Kigoma jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
   Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Taifa,  Kibondo, Kigoma.Akihutubia kwa nyakati tofauti, katika mikutano ya  kampeni zake mkoani Kigoma, amekuwa akihimiza kudumisha amani nchini ambapo pia aliwataka viongozi wa kisiasa  kuhubili suala hilo katika mikutano yao.
   Dk Magufuli akiwanadi Daniel Nsanzugwako (kulia) anayegombea ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Kasulu Mjini na Agustino Zuma Ole anayewania ubunge jimbo la Kasulu Kusini kupitia chama hicho
    Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma
  Wananchi wa Kasulu wakimshangilia  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye mkutano wa kampeni  uliofanyika kwenye Uwanja wa Umoja  Kasulu, Kigoma. 

  PICHA NA MICHUZI JR-KIBONDO-KIGOMA

  0 0  0 0


  Gazeti la Mwananchi la Tarehe 14/9/2015 toleo namba 5529 ukurasa wa 25 liliandika habari kuhusu Mwenge wa Uhuru chini ya kichwa cha Habari “Anayeumba Mwenge wa Uhuru” huyu hapa


  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM) ambayo ndiyo yenye dhamana ya Mwenge wa Uhuru inapenda kuufahamisha umma kwamba habari hiyo sio ya kweli na ni ya upotoshaji.


  Mwenge wa Uhuru ni Chombo maalum na moja ya alama nyeti za Taifa la Tanzania. Mwenge wa Uhuru ni chombo chenye hadhi ya pekee na hivyo dhamana ya kukitengeneza haiwezi kupewa mtu binafsi kama alivyodai Ndugu Shaban Mwinchumu na kuandikwa kwenye gazeti la Mwananchi. Kwa sababu hiyo, kitendo cha kutengeneza au kuigiza chombo chenye dhana na falsafa ya Mwenge wa Uhuru ni ukiukwaji wa sheria za nchi.


  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ingependa kuufahamisha umma kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianzishwa rasmi mwaka 1964  na sio mwaka 1961 kama ilivyoandikwa katika toleo lililotajwa. Ieleweke kwamba, Mbio za Mwenge wa Uhuru tangu kuanzishwa kwake zimekuwa zikitumika katika kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kuendelea kujenga upendo, umoja na mshikamano wa Kitaifa bila ya kubaguana kwa misingi ya kidini,rangi, jinsia, ukabila na itikadi za kisiasa.


  Vilevile, Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikitumika kuhamasisha na kuchochea  shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi kiuchumi na kijamii kupitia kwenye ujumbe maalum unaotolewa kila mwaka na miradi ya maendeleo inayobuniwa .


  Wizara pia, inapenda kuufahamisha  umma wa Watanzania kuwa michango ya fedha inayotolewa na wananchi kwa ajili ya Mbio za Mwenge wa Uhuru si kwa ajili ya kugharamia mafuta ya Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa kama ilivyodaiwa na gazeti la Mwananchi. Fedha zinazochangwa ni kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo hubuniwa na wananchi wenyewe. Aidha,  michango hiyo hutolewa  kwa hiari kutoka kwa mwananchi mmojammoja, Vikundi, Taasisi za Umma na Binafsi, Wadau wa Maendeleo, Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya.


  Kwa Taarifa hii Wizara inasisitiza kuwa madai ya Ndugu Shaban Mwinchumu ni ya upotoshaji na hayana uhusiano wowote na masuala ya Mwenge wa Uhuru. Pia, Ndugu Shaban Mwinchumu hajawahi kupewa kazi ya kutengeneza Mwenge wa Uhuru anayodai kuifanya kwa muda mrefu kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Manendeleo ya Vijana kwani hakuna Wizara hiyo kwenye orodha ya Wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Mwisho kabisa Wizara inawataka waandishi wa habari na wahariri wa vyombo vya habari  kuandika habari kwa usahihi  zenye kujenga Umoja wa Kitaifa kwa kupata ufafanuzi wa kila upande ili habari itoe picha halisi badala ya kuegemea upande mmoja kwani kwa kuegemea upande mmoja hupotosha jamii na si maadili ya taaluma ya habari.  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


  0 0


  Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
  Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:

  *Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, 
  Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;

  *Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo 
  Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;

  *Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, 
  Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;

  *Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali 
  kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na

  *Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja 
  nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.

  Makundi yote haya hugharamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.
  Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya  kujenga chuki dhidi ya Serikali.  Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.
  Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
  17 Septemba 2015

  0 0


  0 0
    Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba
     Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba katika ubora wake
     Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba kama baba yake Sunday Manara 'Computer'
   Rais wa Simba Mhe. Evans Aveva akitoa 
  maelekezo toka benchi la ufundi kama Mourinho vile...  Kwa niaba ya Rais wa klabu yenu pendwa Simba SC Mhe. Evans Aveva na uongozi mzima wa klabu napenda kuwashukuru wanachama na wapenzi wetu wote waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi.kwenda mkoani Tanga kwa ajili ya kuishangilia klabu yenu kwenye mechi zetu za ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya timu za African sports na Mgambo


  Rais na uongozi mzima wa Simba wamefarijika sana na support yenu mliyoionyesha Tanga na kupelekea kuwa na mwanzo mzuri wa ligi kwa kuzifunga timu zote mbili zinazotumia uwanja wa Mkwakwani  Pia uongozi unawashkuru sana washabiki wetu ambao hawakujaaliwa kufika Tanga kwa sala na dua zao ambazo bila shaka zilisaidia kutupa nguvu kubwa zilizofanikisha ushindi huo muhimu kwa klabu  Ni matarajio ya uongozi.support na dua zenu zitaendelea kwenye msimu mzima wa ligi hadi tutakaporejesha kombe letu.ambalo Simba ndio klabu ya kwanza nchini kulitwaa.  RECLAIMING OUR GLORY  Imetolewa na Hajj S Manara
  Mkuu wa habari wa Simba  17-9-2015
  Simba sports club

  0 0


  0 0

  SISI, viongozi wa dini pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi (NEC, TAKUKURU, Polisi pamoja na Msajili wa vyama vya siasa)  tuliokutana leo tarehe 17/9/2015, tumepata nafasi ya kujadili kwa kina suala la uhuru,haki na amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika 25/10/2015 na wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa uhuru,haki na amani vinalindwa kipindi hiki.Suala la uhuru haki na amani ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na watanzania wote kwa ujumla na halina mjadala.Kila mmoja achukuwe nafasi yake kulinda uhuru,haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vya siasa.

  Viongozi wa dini wamepata nafasi ya kujadili na vyombo hivi masuala ya msingi kama kuhakikisha kuwa maadili ya uchaguzi yanazingatiwa kwa wote, muda wa kutangaza matokeo ya kura unazingatiwa , haki ya wananchi kupata matokeo haraka ili kuepuka fujo wakati wa kusubiri na kutangazwa kwa matokeo. Jeshi la polisi kutokutumia nguvu kupita kiasi, wajibu wa Msajili kuhakikisha vyama vyote vinapata fursa sawa na pia tumejadili suala la kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya jukwaa la siasa.

  Viongozi wa dini tumekubaliana kwa pamoja kuepuka kutumia nyumba za ibada kuonyesha ushabiki wa aina yoyote kwa chama chochote cha siasa.
  Baada ya kujadili kwa kina masuala hayo viongozi wa dini wanatoa wito ufuatao;
  1. Vyombo vya habari vifanye kazi kwa ueledi bila upendeleo na pia kuhakikisha kuwa inatoa taarifa ya kutosha kuelimisha umma.
  2. Tunaishauri NEC kwenye chaguzi zijazo  iweke utaratibu maalum wa kuruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha pamoja na watu wote waliojiandikisha/watakaojiandikisha waweze kupiga kura.
  3. Tunaishauri  NEC    kwenye chaguzi zijazo  siku ya kupiga kura isiwe siku ya ibada.
  4. NEC iendelee kutoa elimu ya uraia  kuhusu haki ya raia kupiga kura na haki yao ya  kukaa mita mia moja kusubiri matokeo yatangazwe kwa utulivu kama ambavyo NEC imehakikishia viongozi wa dini kuwa kila kituo itabandika matokeo yote (Urais,Ubunge na Udiwani)
  5.  Pamoja na kutimiza wajibu wake wa msingi wa kulinda raia na mali zao Jeshi la polisi wakati huu wa uchaguzi  liendelee kutimiza wajibu wake wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.

  6. Wagombea,wafuasi   na wanaowanadi,  wanaaswa waache mara moja lugha za matusi,vitisho,kejeli na kukashifiana vinavyoweza kuchochea fujo na kuleta uvunjifu wa amani wajikite kunadi sera za vyama vyao.
  7.Tunawahimiza wananchi kuwa makini katika kufuatilia kampeni na sera mbalimbali za wagombea, kuzipima kwa hali ya juu sera hizo, kutokuuza kadi zao za kupigia kura, kutokununuliwa na kujitokeza kwa wingi kutumia uhuru na haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka kwa hiari na  amani.
   8. Viongozi wa dini wanawahimiza Watanzania wote kuendelea kuombea nchi hii kuendelea kuwa  taifa lililojengwa   katika misingi ya uhuru , haki na amani.

  9. Viongozi wa dini tutabaki kuwa manabii na wahubiri wa uhuru,haki na amani wakati huu , wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi
  Sisi viongozi wa dini Tunawashukuru Inspekta generali wa polisi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya siasa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kwa ufafanuzi makini na wa kina juu ya nafasi na utayari wao wa kushirikiana na viongozi wa dini kuhakikisha uhuru, haki na amani vinaendelea nchini.Maelezo yao na mafafanuzi  yao tumeyasikia  na tutaendeleza kwa kuwa  hiki ni kikao cha mwanzo na tutaendelea kuwa na vikao vingine pamoja nao kuelekea uchaguzi mkuu ili kufuatilia utekelezaji na kuendeleza makubaliano yetu katika kuhakikisha uhuru,haki na amani.

  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akimfariji Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kuhosto) ambaye alifiwa na Mama yake , Hajjat Pili Mlolwa Rehani, nyumbani wa marehemu, Tanata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015. Kuliani  Mama Hasina Kawawa.
   Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani   ambaye ni mama wa Mama Tunu, aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu  kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
    Makamu wa Rais Mohammed Bilal akishiki kubeba jeneza  lenye mwili wa Hajjat Pili  Mlolwa Rehani,mama yake Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika sala ilitofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salam Septemba 17,2015.

older | 1 | .... | 977 | 978 | (Page 979) | 980 | 981 | .... | 3272 | newer