Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MBEYA CITY YABUGIZA JKT RUVU GOLI 3-0 MJINI MBEYA

$
0
0
Kocha wa Timu ya Mbeya City fc a.k.a Wakoma Kumwanya ndugu, Juma Mwambusi akizungumza jambo na baadhi ya Vyombo vya Habari mara baada ya Mtanange huo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika katika Uwanja wa kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya, Ambapo Mbeya City FC  waliibuka kidedea kwa kuichalaza Jkt Ruvu goli 3-0, ambapo Dakika ya 23 mchezaji Joseph Mahundi kuipatia Mbeya City Goli la Kwanza na Goli la Pili toka kwa Temy Felix Dakika ya 57 kwa mkwaju wa Penati, huku Goli la Tatu kufungwa na David Kabole Dakika ya 71.
kiungo wa Mbeya City fc Geofrey Mlawa akiteleza na Mpira katika Mtanange huo uliochezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kamati ya Ufundi..
Baadhi ya Mashabiki Kinazi wa Timu ya Mbeya City FC wakishangilia katika Mtanange huo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambapo Mbeya City waliibuka mshindi kwa goli 3-0...

KUMBUKUMBU

$
0
0
                                                    KUNDASAI ROBERT TERRY
 16-09-1964 mpaka 16-09-1998

Mume wangu mpendwa, leo umetimiza miaka kumi na saba(17) tangu ulipoitwa mbinguni kwa Baba.

Hatuna cha kusema, tumebaki kushukuru tuu maana imeandikwa tushukuru kwa kila jambo. Kweli ua zuri limerudi kwenye bustani ya Eden.


Tunakumbuka sana upendo wako na utanashati uliokuwa nao. Kundasai, tupo kama ulivyotuacha kama familia. Imani yetu kuwa ipo siku wote tutakutana tena paradiso.


 Unakumbukwa  sana na mimi mkeo  mpendwa Elizabeth, wanao Harrison na Diana, nduguzo Martha, Hellen, pacha mwenzio Luwera, Alice, Glad, Vivian na Aida, wajomba wa kwa Terry wote wa mamba kwa Kiria, wa- Kweka wote wa narumu, majirani wa Temeke- mikoroshini na mtoni kijichi- DSM, ndugu, jamaa na marafiki wote.



“ RAHA YA MILELE UMPE EEE BWANA............”

Kipindi cha JUKWAA LANGU

$
0
0
Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dr Magufuli
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla
Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dr Patrick N'higula na Arthur

MASK YA ASALI, NDIZI MBIVU na NDIMU kwa WALE WENYE USO WA MAFUTA

$
0
0


Kama mlivyoomba wadau kwa wale wenye USO wenye MAFUTA mengi hii ni MASK unayoweza kutumia ukiwa nyumbani na ikakuaaidia.
Nini cha kufanya:-
1. Ponda ponda NDIZI MBIVU MOJA mpaka iwe laini kabisa
2. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA ASALI
3. Chukua KIJIKO KIMOJA CHA NDIMU
4. Changanya kwa pamoja vitu hivyo vizuri.
5. Paka mchanganyiko huo kwenye uso msafi kama inavyoonekana kwenye picha na kaa nao kuanzia dakika 15 hadi 30 kisha osha na maji ya uvuguvugu.
Unaweza tumia mask hii mara moja kwa siku.

Imeandaliwa na Honey Spring kwa kushirikiana na Jamiimojablog, Kwa mahitaji yako ya ASALI wasiliana nasi 0683370065 au 0769129351, karibuni sana 

Mhe. Amos Makalla AAGA RASMI WIZARA YA MAJI

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo mchana ameaga rasmi watumishi wa Wizara ya Maji na kwenda kuanza majukumu mapya kama Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
 Mhe. Makalla ambaye alifika Wizarani hapo, akitokea Ikulu alikoapishwa rasmi na Mhe. Rais, Jakaya Mrisho Kikwete, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 
Mhe. Makalla ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji kwa zaidi ya mwaka mmoja, aliweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa licha kuwa mgeni kwenye Sekta hiyo, ambapo aliweza kuzunguka karibu mikoa yote na kutembelea karibu Mamlaka zote za Maji nchini katika kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji.
 Mhe. Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Maji waliompokea mara baada ya kuwasili Wizarani, pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Gideon Manambo.
 Mhe. Amos Makalla akiwa ofisini kwake, alipofika kuaga Wizara ya Maji.
 Mhe. Amos Makalla akipokea shada la maua kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Beatrice Patrick.
 Mhe. Amos Makalla akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji, wakati akiaga wizarani hapo.
Mhe. Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara ya Maji.

ULIPAJI WA MAKOSA YA BARABARANI KWA NJIA YA KIELETRONIKI KUANZA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
KIKOSI cha Usalama Barabarani kimeanzisha mbinu mpya za ulipaji wa makosa ya barabarani kwa njia ya Mtandao kupitia kampuni ya Max Malipo pamoja na baadhi ya benki. 
Kuazishwa kwa mashine hizo imetokana na kuwepo kwa malalamiko ya madereva juu ya kupata risti ambazo si halali. 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP,Mohamed Mpinga amesema kuwa kwa kuanzia majaribio kwa Mkoa wa Dar es Salaam wataanza na mashine 300 pamoja na kamera 12. 
Kamanda Mpinga amesema zoezi hilo linaanza kesho kwa kuingiza mashine 150 na baaada ya majaribio wataingia katika mikoa mingine. 
Amesema gari ikiwa na kosa inaingizwa katika mfumo hivyo watu wanatakiwa kulipa kutokana na kosa kuchelewa zaidi ya siku saba za faini itatozwa kwa asilimia 25 baada ya siku 14 asilimia 50 kushindwa kabisha mtu atafunguliwa mashitaka ya kifungo cha miezi miwili au faini pamoja na kufungia leseni kwa miezi sita. 
Mashine za kutolea risti pamoja na kamaera 12 zimetolewa na Kampuni ya Max Malipo ili kuweza kushirikiana na jeshi la polisi katika kudhibiti fedha zinazolipwa. 
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Max Malipo, Bw. Ahmed Lussasi amesema kuwa wameangalia mazingira yote katika uendeshaji wa mashine hizo katika ulipaji makosa ya usalama barabarani. Lussassi amesema kuwa wataendelea kushirikiana kutokana na kutoa huduma kwa muda mrefu na kuwa na mafanikio.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, DCP Mohamed  Mpinga akizungumza na waandishi wa habari juu ya ulipaji wa makosa ya barabarani kwa njia kieletroniki iliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP,Mohamed  Mpinga akionyesha mfano wa risti iliyotoka katika mashine  baada ya ulipaji wa kosa la usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Max Malipo,Ahmed Lussasi akizungumza na waandishi juu walivyojipanga katika kutoa huduma ya usalama barabarani ,leo jijini Dar es Salaam.kushoto 02.Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed  Mpinga
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda Mpinga  leo jijini Dar es Salaam.

MKUTANO WA UIMARISHAJI NA UHAKIKI WA MIPAKA KATI YA TANZANIA NA KENYA

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inafanya mkutano wa siku tano kati ya Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Kenya ili kuimarisha na kuhakiki mipaka kati ya nchi hizo. Kikao hicho cha wajumbe maalumu kutoka nchi hizo mbili kinafanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 14 hadi 18 septemba 2015.
 Mkurugenzi Idara ya upimaji na Ramani Bw. Justo Lyamuya, Mkurugenzi wa Nyumba Bw. Charles Mafuru kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Chirua Ali wakiwa katika kikao hicho.
 Wajumbe kutoka Tanzania na Kenya wakiwa katika kikao hicho
 Washiriki wa mkutano wakiwa katika picha ya pamoja, hoteli ya  Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Picha na Hassan mabuye.


LOWASSA ATIKISA CHATO, MKOANI GEITA

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnaji Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato, Dkt. Benedicto Lukanima, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Mh. Tundu Lissu akiwasalimia wananchi wa Jimbo la Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Zamani ya Chato, Wilayani Chato, Mkoani Geita leo Septemba 16, 2015.


MAGUFULI APOKELEWA KAMA MFALME KIGOMA,WANANCHI WAKIRI WAZI ATOSHA KUWA RAIS

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo.

 Dkt Mafuli amewaabia wananchi wa Kigoma kwenye mkutano wa kampeni leo jioni kwenye uwanja wa kawawa kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema,amesema kuwa Serikali yake haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo hovyo,amesema kuwa ataimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yake, lakini pia atawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi

Magufuli amewataka Wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyika katika uwanja wa Kawawa,mkoani Kigoma jioni ya leo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Nguruka kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara mapema leo mchana.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya chama cha CCM kwa Mgombea Ubunge wa Kigoma Kusini,Hasna Mwilima na pia kummwombea kura kwa wananchi mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Nguruka mkoani Kigoma.
Wananchi wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi ya Wananchi wa Uvinza wakiwa wamefunga barabara wakitaka wasikilizwe kero zao na Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjni humo akielekea Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Peter Selukamba akiwahutubia wananchi wa Kalinzi,mkoani Kigoma kweny mkutano wa kampeni za Uraisi jioni ya leo.
Wananchi wakishangilia jambo kweye mkutano wa kampeni za Urais
Kada maarufu na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa CCM,Mh Yusuph Makamba akiwahutubia wananchi wa Kigoma na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais,uliofanyka katika uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma.

PICHA NA MICHUZI JR-KIGOMA

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Taarifa kwa Umma kutoka kwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi

$
0
0
Angellah Jasmine Kairuki

Tarehe 14 Septemba 2015 ulisambazwa ujumbe kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ukidai kuonyesha mawasiliano ya Makada wa Chama cha Mapinduzi nikiwamo mimi (Angellah Kairuki), Nd. January Makamba, Nd.Mwigu Nchemba na Nd.Livingstone Lusinde.  
Wakati ujumbe huo umeanza kusambazwa nilikuwa kwenye mikutano ya Kampeni ya Mgombea Mwenza wa CCM Mhe.Samia Suluhu Hassan Wilayani Nachingwea na Liwale hivyo kupelekea kuchelewa kutoa taarifa yangu hii.

Napenda kuufahamisha umma kwamba ujumbe huo uliosambazwa ni wa uwongo na hapajawahi kuwepo mawasiliano hayo popote.  Ni ujumbe uliotengenezwa kuupotosha umma kwa manufaa ya kisiasa ya walioutunga na kuusambaza.
Vilevile, napenda kuujulisha umma kwamba Mimi  binafsi situmii njia ya mawasiliano ya whatsapp na wala sijawahi kuitumia wakati wowote ule, hivyo siwezi kuwa kwenye group lolote lile  kama ujumbe uliosambazwa ulivyotaka kuuhadaa umma.
Ni vema ikaeleweka kuwa ni kosa la Jinai kujifanya wewe ni mtu fulani wakati siyo.  Hivyo naviomba vyombo vya sheria kuwasaka wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria waliotunga na kusambaza ujumbe ule kwa kutumia majina ya watu wengine.  


Natumaini TCRA nao watafuatilia chanzo cha taarifa hizo za uwongo ili washughulike na wahusika kupitia sheria ya makosa ya mtandao.

Ninawapa pole wale wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizo za uwongo.



MWENENDO WA KAMPENI ZA CCM

$
0
0
HADI  tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. 

Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720.
 Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. 

Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.
 

JK azindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo

$
0
0

 Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi majengo majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi majengo pacha ya PSPF TOWERS.


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa kadi yake baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka alama ya dole kwenye fomu yake ya uanmachama baada ya kujiunga mfuko wa pensheni wa PSPF kwenye sherehe hizo. Kulia ni Naibu waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Malima. Kulia kwa Rais ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF Mhe. George Yambesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw. Adam Mayingu 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na  na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau  na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio kwenye sherehe zsa  kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.


Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika 
Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.


PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.
Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.

Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake uliofanywa na makandarasi wazalendo ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika. 


Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mwanza yaiadhibu Morogoro katika michuano ya Airtel Rising Stars

$
0
0
Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa, imeendelea kutimua vumbi katika dimba la Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam, ambapo timu za Temeke na Mwanza zilipepetana kwa upande wa wasichana huku Mwanza na Morogoro walitifuana vikali kwa upande wa wavulana. 
Kwa kuanzia na mchezo ambao ulizikutanisha timu za wavulana, Mwanza waliwasambaratisha vibaya Morogoro kwa kuwashindilia magoli 3-1. Mwanza ambao walionekana kutakata kila idara, walijipatia bao la uongozi mnamo dakika ya 30 kupitia Lazaro Richard, baada ya kuitokea pasi nzuri iliyopigwa na David Richard na kumchambua vizuri kipa wa Morogoro kisha kuukwamisha mpira huo kimiani. 
Morogoro ambao katika mchezo wa Jumatatu wiki hii, waliitandika Kinondoni mabao 2-1, waliamka kutoka usingizi na kufanya mashambulizi kadhaa ambayo hata hivyo hayakuzaa matunda. Alikuwa ni David Richard ambaye aliandikia Mwanza bao la pili mnamo dakika ya 54, kutokana na krosi safi iliyochongwa kutoka mashariki mwa uwanja na kuusindikiza kwa uzuri kabisa mpira huo langoni mwa Morogoro. 
Baada ya goli hilo, Morogoro waliamka na kupeleka mashambuliza ya mara kwa mara langoni mwa Mwanza, na ndipo mshambuliaji wao hatari Evidence Kiongozi alipofunga goli dakika ya 63 na kuamsha matumaini ya walau kusawazisha na hatimaye kutafuta goli la ushindi. Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa upande wa Morogoro, baada ya David Richard kwa mara nyingine tena, kuifungia Mwanza bao la tatu na mwisho katika mchezo huo mnamo dakika ya 68 na kuhitimisha karamu ya magoli kwa upande wa timu yake. Katika mchezo mwingine, wasichana wa Temeke waliwaadabisha vikali Mwanza kwa kuwafumua magoli 3-0.
Temeke ambao katika mchezo wao wa kwanza walitaoa kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 8-0 dhdi ya Arusha, walianza kupata bao mnamo dakika ya 11 baada ya Shamimu Khamisi kufunga goli maridhawa, baada ya kutokea rapsha langoni mwa Mwanza na kuipa timu yake goli la uongozi. Iliwachukua takribani dakika takraibani 28, Temeke wakapata bao la pili kupitia kwa Rose Mpoma baada ya kuachia shuti kali la mbali na kuzama moja kwa moja wavuni, na kumwacha mlinda mlango wa Mwanza asijue la kufanya langoni mwake. Mpaka timu hizo zinakwenda mapumzikoni, Temeke walikuwa mbele kwa magoli 2-0. 
 Temeke waliendeleza kilio kwa wapinzani wao, katika kipindi cha pili kwa kushindilia msumari wa tatu na wa mwisho mnamo dakika ya 56, baada ya Oppah Masoud kugongeana mpira vizuri na Rose Mpoma na hatimaye kuusukumiza moja kwa moja mpira kimiani. 
Baada ya kupata goli la tatu, Temeke walionekana kuridhika na kucheza kwa kijiamini huku wakisubiri kipenga cha mwisho cha mwamuzi, huku wakiwa wamejikunyajia pointi tatu kibindoni.
Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa,
Patashika ya michuano ya vijana chini ya miaka 12 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa baina ya Mwanza na Morogoro

CNN Finalists Release- Mtanzania yupo kwenye 30 bora

Mhe. Rais Kikwete awaapisha rasmi Balozi Mwakasege, Bundala, Kilima, Luvanda, Mbega na Shiyo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Bi. Victoria Richard Mwakasege aliyekuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Balozi Victoria R. Mwakasege anaiwakilisha Tanzania nchini Malawi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 September, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Samweli Shelukindo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent E. Shiyo kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara hiyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman, Bw. Abdallah Kilima kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda Bi. Anisa Mbega kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Bw. Baraka H. Luvanda kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITEKA KIGOMA UWANJA WA KAWAWA

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI KIWANDA CHA TBL, WAFANYABIASHARA NCHINI WAPEWA WITO.

$
0
0

  Mkuu wa usalama wa mahali pa kazi wa TBL Mbeya, Godfrey Kisulilo akiwaonesha waandishi wa habari namna ya kutunza maji.
  Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na uomgozi wa tbl.
Waandishi wa habari Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara katika kiwanda cha bia cha TBL Mbeya.
WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
 Meneja wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.
Alisema TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Alisema licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la uhakika.
Katika shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe aliibuka mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa aliyeshika nafasi ya pili.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

JK KUELEZEA UMOJA WA MATAIFA MAENDELEO YA KAZI YA JOPO ANALOLIONGOZA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jopo  la Ngazi ya  Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa Ijumaa wiki hii  kuwasilisha mbele ya  wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja  wa Mataifa  maendeleo ya kazi ya  Jopo   tangu lilipoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki  Moon,  mwezi  April  mwaka huu.  
Na  Mwandishi Maalum, New York


Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya  Juu kuhusu  Mwitikio wa Kimataifa wa   Majanga ya Kiafya, anatarajiwa Ijumaa wiki hii, kueleza mbele ya  wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya kazi  ya jopo  hilo tangu kuundwa kwake.


Jopo la Ngazi ya juu kuhusu mwitiko wa Kimataifa wa majanga ya kiafya  liliundwa mwezi wa  nne mwaka huu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki  Moon, ambapo  Rais Kikwete  amepewa jukumu  la  kuongoza jopo hilo. 
Taarifa ambazo zimeufikia  Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa, zimebainisha kuwa  Mhe. Rais atawazungumza  wajumbe wa  nchi  wanachama wa Umoja wa Mataifa  mara  baada ya kumalizika  kwa  mkutano wa tatu wa jopo  hilo  unaofanyika hapa  Makao Makuu ya Umoja wa  Mataifa. 
Wajumbe  wengine  wa Jopo hili   ni  Bw.    Celso Amorim ( Brazil), Micheline Calmy ( Switzerland), Marty Natalegawa  ( Indonesia) Joy Phumapi ( Botswana) na  Rajav Shah ( USA). 
Jukumu  kubwa ya  jopo hilo  kwa mujibu wa hadidu za rejea,  pamoja na mambo mengine,  ni kutoa mapendekezo ya  namna ya  kuimarisha mifumo  ya kitaifa na kimataifa katika   kuzuia na kukabiliana na  majanga ya kiafya ikiwa ni pamoja na  kujifunza   kuhusu   mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa kufuatia  kuibuka kwa   janga la ugonjwa wa Ebola. 
Katika utekelezaji wa majukumu yake  Jopo limekuwa likikutana na kufanya majadiliano ya kina na makundi mbalimbali yakiwamo ya  wataalamu,   wawakilishi wa  nchi tatu ambazo  zimeathirika sana na ugonjwa wa ebola (  Liberia,  Siera Leone na Guinea),Mashirika ya Kimataifa na Kikanda , Taasisi za Fedha za kimataifa, wahudumu wa Afya, Wasomi , Watafiti,  Sekta Binafsi na wataalam wa  fani  na kada mbalimbali. 
Pamoja na kuhudhuria na kuongoza mikutano ya  Jopo, Mhe,  Rais   Kikwete  akiwa hapa  Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa, pia atahudhuria  Mikutano Mikubwa  miwili ambayo  ni,  Mkutano wa Kilele wa Kisiasa, ambao Wakuu wa Nchi na Serikali watapisha  Malengo  ya  Maendeleo Endelevu ( SDGs). Mhe. Rais atazungumza  katika  mkutano huu muhimu  kwa mstakabali wa maendeleo na ustawi wa binadamu kwa miaka 15 ijayo. 
Malengo Mapya ya Maendeleo yanachukua nafasi ya   Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayomaliza muda wake   mwishoni mwa mwaka. 
 Aidha Mhe. Rais atashiriki na kuhudhuria Mkutano wa  70 wa  Baraza Kuu la   Umoja wa  Mataifa.  Na anaratajiwa kulizungumza  Baraza Kuu na hii itakuwa ni hotuba yake ya   mwisho akiwa ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Vile vile Mhe. Rais atahudhuria mikutano  mingine  kadhaa.   Baadhi ya mikutano hiyo ni  ule  ambao umeandaliwa kwa pamoja  baina ya   Kansela wa Ujerumani  Mhe. Angela Merkel ,  Waziri Mkuu wa  Norway   Mhe. Erna Solberg na Rais wa Ghana Mhe.   John Dramani Mahama. 
Mhe Rais anahudhuria mkutano  huu kwa mwaliko rasmi aliopewa na Kansela Angela Markel. Washirika  na waandaji  wengine wa mkutano huu ni  Mfuko wa Bill na Melinda Gates, Shirika la  Afya Dunia ( WHO) na Bank ya Dunia. 

Mkutano huu unatarajiwa  kuzindua  misingi  na  hatua muhimu ambazo kwayo   zitaratibu  ufanisi na   upimaji  wa matokeo ya juhudi  za  kuimarisha mifumo ya afya.

SIKU DKT. DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOVAMIA JUKWAA LA WANAUME TMK

ARUSHA YAONGOZA MICHUANO YA WAZI TENISI KWA VIJANA.

$
0
0
 
Na Woinde Shizza,Arusha
Jiji la Arusha limeendelea kuwa kinara katika mchezo wa tenisi baada ya wachezaji wake kuibuka kidedea kwa kutwaa ushindi katika umri tofauti tofauti ,mashindano yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Arusha Tenisi gymkhana klabu.

Mashindano hayo yalidhaminiwa na Jubilee tyres ikiwa ni mwaka wa tatu sasa, yalishirikisha jumla ya wachezaji 90 ambao 28 kati yao ni wasichana kutoka Dar es salaam gymkhana klabu,Kijitonyama tenisi klabu kutoka Dar es salaam,Morogoro tenisi klabu, ISM –Moshi campus, AICC klabu –Arusha pamoja na Arusha tenis gymkhana klabu.

Katika umri wa miaka 6 kwa wasichana Schaefer Swantje kutoka ISM Moshi campus alifuatiwa na Suhana  Patel kutoka Arusha gymkhana klabu,huku kwa  upande wa wavulana wa umri huo Sahil Shah kutoka ISM moshi campus na kufuatiwa na Yuvraj Sidhu kutoka Arusha gymkhana klabu.
Kusoma zaidi bofya HAPA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images