Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WATANZANIA WANAIPENDA TANZANIA-NCHEMBA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari juu ya Watanzania wanaoipenda Tanzania wakisha maliza kutimiza wajibu wake wawapishe waendelee kutimiza haki zao za msingi za kupiga kura, ameyasema katika Hoteli ya Serena leo Jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkurugenzi wa (NEC) Jaji Mustafu  Hamad M. Hamid akizungumza na ziongozi mbalimbali wadini pamoja na viongozi wa Siasa juu ya zoezi la uchaguzi kuwa la amani na utulivu leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo  Dk Ayub Rioba.
 (Picha na Emmanuel Massaka)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

                     

Benki ya Exim yatoa msaada wa vitabu sekondari Mbeya.

$
0
0
Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Mbeya, Bw Iddy Mwacha(kushoto) akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo kwa mmoja wa wanafunzi aliewawakilisha wanafunzi wenzie na uongozi wa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya katika kupokea msaada huo ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, uongozi wa shule pamoja na wanafunzi.
BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitabu vya masomo vyenye thamani ya sh mil. 8/- kwa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu hivyo iliyofanyika kwenye viunga vya shule hiyo mwishoni mwa juma lililopita, Meneja wa benki hiyo tawi la Mbeya Bw Iddy Mwacha alisema msaada huo ni sehemu ya uthibitisho wa namna benki hiyo imekuwa ikipambana kuhakikisha uwepo wake hapa nchini unaleta tija zaidi kwa jamii.

BALOZI WA LUVTOUCH MANJANO ATEMBELEA WASHIRIKI WA SEMINA YA UJASIRIAMALI

$
0
0
  
 Balozi wa Luv touch Manjano Irene Pul Katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Semina ya ujasiriamlai ya wanawake kwa kupitia Vipodozi vya Luv Touch manjano iliyochini ya Manjano foundation.

Lengo la Mradi huo ni kuona kwamba wanawake hawa wanajisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara zao kwa lengo la kumuongezea ajira mwanamama na kuondoa dhana za ukosefu wa ajira kuwa chungu ya yeye kujiwezesha katika kujikimu mahitaji yake ya msingi, yaani aweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa kupitia ujasiriamali.Balozi huyo amewashauri Washiri hao kwanza kupenda ujasiriamali na kufanya kazi kwa bidii lazima watafanikiwa.

Pili kila mshiriki kuwa mbunifu kwenye biashara na kuja na kitu cha kipekee ambacho kitawafanya watumiaji wa luv Toch manjano pamoja na wateja wengine kushawishika kuwaunga mKono washiriki hao katika biashara yao pamoja na kuwatangaza kwa watu wengine wengi zaidi. 
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAZINDUA KAMPENI WILAYA YA DIMANI ZANZIBAR

$
0
0
 Zuhura Seif Hassan akighani utenzi katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Wilaya ya Dimani zilizofanyika uwanja wa shinyanga karibu na Baraza la Wawakilishi Chukwani nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Baadhi ya wanachama wa CCM wakisikiliza Mgeni rasmin Mhe. Shamsi Vuai Nahodha (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia katika Mkutano uliofanyika kiwanja cha shinyanga karibu na Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Ibrahim Raza akiwatambulisha wagombea uwakilishi wa Jimbo hilo, (kulia) mgombea Uwakilishi jimbo la Chukwani Bi. Mwanasha Khamis na (kushoto) mgombea Uwakilishi jimbo la Kiembe samaki. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MARA (MARA DAY) BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasha Mshumaa katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la Maua katika Kaburi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kama ishara ya Kumbukumbu wakati alipofika katika Jumba la makumbusho Butiama mkoani Mara leo Sept 15, 2015 baadda ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mara (Mara Day) iliyofanyika Butiama. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Kenya, Eugene Wamalwa.  

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 15/09/2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

TFF YABAINISHA KATIBA NA KANUNI ZA LIGI KUU WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
Baraka Kizuguto - Msemaji wa TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limebaini kuwepo kwa vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kujihusisha na masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za vilabu na wadhamini wa Ligi.
Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of politics and religion. Discrimination of any kind against a country, private person or group of people on account race, skin colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion, political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”
Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.
TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na FIFA.

MKUTANO WA KILELE WA DUNIA KUHUSU CHAKULA NA LISHE WAFUNGULIWA ARUSHA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa unahusu masuala ya Lishe na Chakula uliofanyika Arusha. .
Mhe. Pinda akihutubia 
Mfalme wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo  akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika mkutano huo (hawapo pichani).
 Wadau mablimbali wakifuatilia hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na viongozi ho
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe naye alitoa Hotuba yake wakati wa Hafla hiyo
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na wadau mbalimbali katika meza kuu.  Picha zote na Reginald philip .
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

TFF: RUKSA WACHEZAJI KUTUMIKA KATIKA KAMPENI ZA SIASA, LAKINI WASIVAE JEZI

$
0
0

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halizuii mchezaji kufanya kampeni za siasa, isipokuwa wasitumie sare za kimichezo hususan zenye nembo za wadhamini.
Hatua hiyo inafuatia TFF kubaini kuwepo kwa vitendo vya wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania kujihusisha na masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za klabu na wadhamini wa Ligi.
Taarifa ya TFF imesema kwamba Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of politics and religion. Discrimination of any kind against a country, private person or group of people on account race, skin colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion, political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”
Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.
TFF imesema inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa Stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.
Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao haukiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na FIFA.
Tamko la TFF linakuja baada ya kuvuja picha ya Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa kwenye bango la kumpigia debe mgombea Urais wa CCM, John Pombe Magufuli ambaye hata hivyo anaungwa mkono na Watanzania wengi akifuatiwa kwa mbali na Edward Lowassa wa CHADEMA.
Kwa tamko hilo la TFF, sasa Cannavaro au mchezaji mwingine yeyote anaweza kutokea kwenye bango la kampeni za siasa akiwa na maavazi ya kawaida.
Source:Bin Zubeiry

JK amteua Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Casmir Kyuki kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Kabla ya uteuzi huu, ndugu Kyuki alikuwa Mwandishi Kufuatia uteuzi huu, Rais amemteua Bibi Sarah Barahomoka kuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na ndugu Kyuki.
Kabla ya uteuzi huu, Bibi Barahomoka alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya uandishi wa Sheria. Uteuzi huu unaanza mara moja.


Wateule hawa wataapishwa Tarehe 16 Septemba, 2015, Ikulu Dar-es-Salaam leo saa 3 asubuhi.


Imetolewa na:

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari, Msaidizi,

Ikulu-DSM
15 Septemba, 2015





MAGUFULI AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI WILAYA YA SIKONGE,KALIUA,ULYANKULU NA URAMBO MKOANI TABORA

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa kaliua alipokuwa akiwahutubia wakazi hao katika uwanja wa Kolimba,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
  Wakazi wa mji wa Kaliua wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Kaliua kupitia chama cha CCM Prof.Juma Kapuya
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Urambo kupitia chama cha CCM,Mh.Magret Sitta,kulia kwake ni Mh.Samweli Sitta kwa pamoja wakimkaribisha Dkt Magufuli alipowasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Urambo jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Urambo jioni ya leo mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Urambo jioni ya leo mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mjini Urambo mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
Wananchi wakiwa wamekusanyika mjini Urambo kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM,Dkt Magufuli.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sikonge mapema leo mchana mjini humo,kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora,kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba abaye amerejesha kadi yake kwa Dkt Magufuli,shoto ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George John.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba akipeana mikono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George John,mbele ya Wananchi wa Sikonge kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia aliyekuwa Mbunge wa Sikonge ambaye alijiunga na chama cha CHADEMA mara baada ya kuondolewa kwenye kura za maoni ya chama cha CCM,Ndugu Said Nkumba akipeana mikono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Sikonge Ndugu George John,mbele ya Wananchi wa Sikonge kwenye mkutano wa kampeni mkoani Tabora.


KAMPUNI YA UNIGLOBE SKYLINK TRAVEL & TOURS YATANGAZA WASHINDI WA DROO YAO

$
0
0
 Bw. Moustafa H. Khataw, Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Uniglove Skylink Travel & Tours akiwakaribisha waandishi wa habari pamoja na wageni waliofika katika droo ya kuwapata washindi wanne  kwa wateja wote wa kampuni hiyo  ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Bw. Husain AlSafi, Mkurugenzi Mkuu wa tawi la Shirika la ndege la Emirates Tanzania ambao walikuwa ni wadhamini wa shindano hilo akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Skylink.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akizichanganya vipeperushi ili kuwapata washindi wa droo hiyo.
Mwandishi wa habari kutoka TBC akiwa ameshika moja ya kipeperushi cha mteja wa Skylink aliyeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Uniglobe Skylink Travel & Tours Bw. Solomon Mwale akiwatangaza washindi waliopatikana kwenye droo iliyofanywa na kampuni ya Skylink leo.
Wafanyakazi wa kampuni ya Uniglobe Skylink Travel & Tours wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Hyundai Tanzania ambao walikuwa ni wadhamini wakuu kwenye shindano hilo

Hassan Taliki mkazi wa  Jijini Dar es Salaam leo ameibuka mshindi na kushinda gari mpya aina Hyundai ix35   katika droo iliyochezeshwa  kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.
Mshindi huyo amepatikana kutokana na kukata tiketi ya ndege katika Kampuni hiyo hivyo ili aweze kupata zawadi hiyo ametakiwa kwenda na kipeperushi Skylink cha tiketi aliyokana na kitambulisho chake kwa maelekezo zaidi.
Washindi wengine walioshinda kwenye droo hiyo ni  Mohamed Swala ambaye  ameshinda safari ya kwenda Mahinra  kwenda na kurudi huku Issa Nassoro ambaye amekuwa mshindi wa tatu  amepata tiketi ya kwenda na kurudi Dubai ambako atapelekwa na Kampuni hiyo .
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  Ofisa wa Skylink Solomon Mwale  alisema kwamba wamepanga kufanya hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao ili umma uweze kuamini kwamba hawabahatishi na droo ikichezeshwa inakuwa  ni kweli.
Droo hii ni sehemu ya motisha inayotolewa na Kampuni yetu  kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Droo hiyo imedhaminiwa na Skylink, Hyundai, Emirates, Exim Bank na Club Mahindra.

JK azindua rasmi daraja la Kikwete juu ya Mto Malagarasi mkoani Kigoma

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea Kusini Mhe. Chung II, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Korea Kusini uliojenga Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi mara baada ya kulifungua rasmi Daraja hilo lenye urefu wa mita 275 na barabara unganishi zenye urefu wa Km. 48.

Muonekano wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye uwezo wa kubeba tani 180 na kudumu kwa miaka 100 kama likilindwa na kupitisha mizigo isiyozidi uzito.
Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii mjini Dodoma Bw. Gama akifurahia kukamilika na hatimaye kuzinduliwa kwa Daraja la Kikwete juu ya mto Malagarasi mkoani Kigoma. Anasema Mnyonge Mnyongeni, haki yake mpeni. Jk ameifanyia makubwa nchi ya Tanzania katika utawala wake wa awamu ya nne hata kama wapinzani watajifanya vipofu na kutoona maendeleo haya aliyoleta JK na ambayo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli amepania kuchukua baton na kuendeleza kwa kasi kubwa mbio za Maendeleo na Maisha bora kwa kila mtu.

COPA COCA COLA KUFANYIKA MWAKANI

$
0
0
MASHINDANO ya Copa Coca Cola yanayodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Coca Cola yaliyokuwa yafanyike katikati ya mwaka huu, sasa yatafanyika mapema mwakani mwezi Februari kuanzia ngazi ya Wilaya na fainali zake kufanyika mwezi Juni na Julai 2016.

Michuano hiyo ambayo hushirikisha timu za mikoa yote Tanzania kuanzia katka ngazi ya Wilaya, hufanyika kila mwaka kwa kuwashirkisha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Taarifa ya Idara ya Masoko ya Coca Cola imesema kampuni hiyo imeahirisha kufanyika kwa michuano hiyo wa mwaka huu, na sasa itafanyika mwakani ili waweze kupata nafasi ya kuandaa vizuri mashindano hayo.

Tuna uzoefu na mashindano hayo, ni vyema tukaifanya wakati wa likizo wakati vijana wakiwa mapumziko, sababu wachezaji wote wa michuano ya Copa Coca Cola ni wanafunzi hivyo ni vizuri tukaandaa mashindano hayo wakati wanafunzi wakiwa likizo.

Michuano ya Copa Coca Cola ilianza mwaka 2007 kwa kushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U17) na baadae mwaka 2012 kubadilishwa na kuwa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15).

Baadhi ya wachezaji waliopatikana katika mashindano hayo kwa sasa wanacheza katika vilabu vikubwa vya Ligi Kuu ya Vodacom nchini na wengine wamepata naafasi ya kucheza soka nje ya nchi.

ZAIDI YA WATU 500 WANATARAJIWA KUSHIRIKI KATIKA BONANZA LA KUSHEREKEA MIAKA 17 TANGU KUANZISHWA KITUO CHA MAZOEZI CHA HOME GYM

$
0
0
 ZAIDI ya watu 500 wanatarajiwa kushiriki katika bonanza la kusherehekea miaka 17 tangu kuanzishwa kituo cha mazoezi cha home gym kilichopo mwenge jijini dar es salaa litakalofanyika juma pili hii ya septemba 20 katika viwanja vya Escape One.

Andrew Mangomango ni mkurugenzi wa kityuo hicho ametanabaisha kuwa maandalizi yote yamekamalika na kusema kuwa miongoni mwa watu watakaoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na vikundi vya Joging vya jijini DSM, vutio vya gym na yeyote atakayehitaji kushiriki katika bonanza hilo.

Miongonui mwa mambo yatakayoshamirisha bonanza hilo ni pamoja na kutembelea hospitali ya palestina  ya sinza jijini DSM na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa sanjari na kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Bonanza hilo litakalofanyika katika viwanja vya Escape One litaanza Mlimani City majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki kukimbia kwa mwendo wa taratibu pamoja na kutembea kwa kundi linguine.


MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, AMOSI MAKALLA APITA OFISI ZA MICHUZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makalla alipopita kusalimia katika Ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya kutoka kuapishwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Watatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amosi Makalla  akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya MICHUZI MEDIA GROUP jijini Dar es Salaam leo.

JK AFUNGUA TERMINAL YA MBOLEA YA KAMPUNI YA YARA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi terminal ya mbole ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.   Kulia ni  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu   Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa YARA nchini Bw. Alexandre Macedo na Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka kukagua terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.   Kulia ni  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu   Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa YARA nchini Bw. Alexandre Macedo na Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether
 Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway akihutubua katika sherehe hizo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu  akimkaribisha Rais Kikwete kuhutubia
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati anafungua rasmi terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia sanamu ya meli aliyozawadiwa baada ya kufungua rasmi terminal ya mbolea ya kampuni ya Norwaya ya YARA Kurasini jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kushoto ni  Mama Monica Maeland, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway. Kutoka na katikati ni Rais na Mtendaji Mkuu wa YARA  Bw. Svein Tore Holsether.
PICHA NA IKULU

JK AKAGUA MAENDELEO YA KITUO CHA MICHEZO KWA VIJANA CHA KIDONGO CHEKUNDU DAR ES SALAAM

$
0
0
  Kituo cha Michezo kwa vija na cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam kinavyoonekana kutoka angani.
 Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland  ya Uingereza na kampuni ya symbion
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitambulishwa na Mkurugenzi wa kampuni  ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wakituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland  ya Uingereza na kampuni ya symbion
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitambulishwa na Mkurugenzi wa kampuni  ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa kocha wa vija na kutoka Uingereza anayetambuliw3a na FIFA ambaye atakuwa mkufunzi Mkuu katika kituo hicho  wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wakituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland 
ya Uingereza na kampuni ya symbion.

Wafanyakazi wa Kujitolea wa Kimarekani kufanya kazi katika sekta ya elimu katika wilaya 31 nchini Tanzania

$
0
0
Dar es Salaam, TANZANIA.  Leo asubuhi, Balozi wa Tanzania nchini Tanzania Mark Childress amewaapisha wafanyakazi wa kujitolewa wa Kimarekani (Peace Corps Volunteers) wapatao 59 ili kuanza huduma yao ya miaka miwili nchini Tanzania. Hafla ya kuwaapisha wafanyakazi hao ilifanyika katika viwanja vya Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukaguzi wa Shule ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Edicome Cornel Shirima, Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps nchini Tanzania Dk. Elizabeth O’Malley, watu waliowahi kuwa wafanyakazi wa kujitolea wa Peace Corps katika sehemu mbalimbali duniani na maafisa wa taasisi wabia wa kiserikali na taasisi nyingine za kujitolea.

Katika hotuba yake, Balozi Childress aliwaambia wafanyakazi hawa wapya wa kujitolea wa Peace Corps kuwa “Mojawapo ya maneno yanayonivutia sana ninayoyasikia mara kwa mara nchini Tanzania ni neno pamoja. Neno hili linawasilisha moyo wa ushirikiano baina ya nchi zetu mbili na miongoni mwa Watanzania. Na hivi sasa mnapoanza safari na rafiki na wabia wenu wa Kitanzania, ninachoweza kuwaambia kuwa kwa pamoja mtakuwa na safari yenye kusisimua sana.”

Katika hotuba yake kwa wafanyakazi wapya wa kujitolea Dk. Shirima alirejelea maoni ya Balozi, akiwaasa kuwa “fanyeni kazi kwa bidii, fanyeni yaliyo mema, yafanyeni hayo kwa moyo wote, enzini uzoefu mtakaoupata na kuhusiana vyema na watu wa Tanzania. Kwani mtakuwa mkiishi na kufanya nao kazi  bega kwa bega katika shida na raha. Furahieni muda wenu mtakaokuwa hapa Tanzania.”

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Dk. Elizabeth O’Malley alisema “Kwa niaba ya Peace Corps Tanzania, ninapenda kutambua na kushukuru kwa ushirikiano mkubwa tunaoendelea kuupata kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa upande wa Zanzibar na Bara, hususan kutoka kwa Wizara za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Afya.  Aidha, napenda kuwashukuru Maafisa Elimu wa Wilaya na Wakuu wa Shule wanaotoa msaada mkubwa kwa watendaji wetu na wafanyakazi wetu wa kujitolea.”

Wafanyakazi wa hawa 59 wa kujitolewa walioapishwa leo watapangiwa kufanyakazi katika wilaya za Karatu, Kongwa, Chamwino, Mufindi, Iringa Vijijini, Hai, Rombo, Lushoto, Wete na  Nzega. Wengina watapangiwa katika wilaya za  Moshi Vijijini, Same, Ruangwa, Nachingwea, Hanang, Babati, Kiteto, Tukuyu, Kyela, Chunya, Mbarali, Masasi, Newala na Mtwara Vijijini. Wengine watakwenda katika wilaya za Mbinga, Shinyanga, Kishapu, Maswa, Singida vijijini, Iramba, Nzega na Lushoto.

Wafanyakazi hawa wa kujitolea wa kimarekani watatoa huduma kwa wanafunzi wao, shule na jamii watakazokuwa wakiishi kwa kufundisha masomo darasani pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya kijamii mathalan ile inayohusu lishe bora, stadi za maisha, afya bora, mazingira na mafunzo ya kusoma na kuandika.  Aidha, kwa miaka miwili ya kuwepo kwao hapa nchini, wafanyakazi hawa watachangia katika jitihada za Tanzania za kuongeza idadi ya walimu wa hisabati, Sayansi na Kiingereza hususan katika maeneo ya vijijini.


Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 8,000 katika zaidi ya nchi 75 duniani. Kwa miaka 48, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini.  Jumla ya wafanyakazi wa kujitolewa wapatao 189,000 wamehudumu katika nchi zipatazo 138. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:

·         Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao;

·         Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;

·         Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

 Zaidi ya Wafanyakazi wa Kujitolea wa Peace Corps wapatao 2,000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1962. Peace Corps hutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani wanao fanyakazi katika jamii katika Nyanja za elimu ya sekondari (wakifundisha hisabati, sayansi na teknolojia ya mawasilianoa), afya na elimu ya mazingira.


Kwa taarifa Zaidi, tafadhali wasiliana na Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images