Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 974 | 975 | (Page 976) | 977 | 978 | .... | 3278 | newer

  0 0

  http://www.aitvapp.com/

  0 0

   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa  Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote. 

   Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
    Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
   Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.


   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.

   Wananchi wakishangilia .
    Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.   0 0


  0 0

  Msaada wako kaka Issa Michuzi nisaidie kuitoa kwenye blog yako hiyo picha ni ndugu yetu tunamtafuta Alikuwa south Africa tangu 1998 ila kwa sasa hatuji alipo. 
  Ni zaidi ya miaka 15 hatuna mawasiliano nae ,watu wa south Africa wanasema hayupo south Africa ila hawajui alipo. Jina lake anaitwa PAULO DASTAN NYANGUSI.
  Mwenye taarifa zake tafadhali sana awasiliane na email hii ernestkinyashi@gmail.com

  Ahsante

  Ernest

  0 0

  Wimbo maalum wa kuhimiza amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu, utawekwa rasmi hadharani mbele ya waandishi wa habari Jumanne hii.

   Wimbo huo uliopewa jina la “Amani Kwanza” utapigwa ‘live’ kwa mara ya kwanza mbele ya wana habari ndani ya ukumbi wa nyuma wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana. 
  “Amani Kwanza” ni ngoma iliyopigwa katika miondoko ya rhumba ikiwa imeshirikisha nyota wengi wa muziki wa dansi chini ya umoja  wa muda wa wanamuziki wa dansi na taarab. 
  Mgeni rasmi katika tukio hilo anatarijiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni bwana Paul Makonda. 
  Mratibu wa ‘project’ hiyo Juma Mbizo alisema umoja huo haufungamani na dini, kabila wala chama chochote na kwamba lengo la ni moja tu – kusumbaza ‘mahubiri’ ya amani, umoja na mshikamano kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu. 
  Mbizo amefafanua kuwa wimbo huo umerekodiwa katika studio za Sound Crafters chini ya producer Enrico huku video ikiwa imefanywa na King Dodoo. 
  Wanamuziki waliotengeneza wimbo huo wako chini ya kamati inayoongozwa na Kanku Kelly ambaye ni mwenyekiti, katibu Omar Teggo, wajumbe ni Mafumu Bilal, King Dodoo na King Kiki huku Juma Mbizo akiwa mjumbe na mratibu. 
  Mbizo amesema baada ya utambulisho huo, kila mwanahabari atapatiwa CD na DVD moja ya wimbo huo. 
  “Lengo letu ni kutaka wanahabari wawatambue wasanii wote walioshiriki kutengeneza wimbo huo ikiwa ni pamoja na kuusikiliza ‘live’ hivyo naomba waandishi wa habari na wadau wa muziki waje kwa vingi Mango Garden Jumanne mchana,” alisema Juma Mbizo.

  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. 
  Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga. 
  Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia. 
  Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma. 
  Ndugu Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.

   Uteuzi na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho kutwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.
  Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali. 
  Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano, Septemba 9, 2015. 
  Kabla ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.

  Vile vile, Rais Kikwete amemteua Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Uteuzi huo ulianza Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
  Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni mwanasheria kwa taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita ambako ametumikia katika nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji Mkuu.

  Ndugu Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

  Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.
  Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

   14 Septemba, 2015  0 0

  .

  Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi viwanja vya Mnazi Mmoja.


  Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
  Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
  Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete akizungumza na umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho uliokuwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Na  Bashir  Yakub

  Kama  ilivyo  makubaliano  katika  shughuli  nyingine  za  kijamii  ajira  nayo  huwa  na  makubaliano  maalum  wakati   inapoingiwa. 
  Makubaliano  haya ndiyo  huitwa  mkataba na  yumkini  huingiwa  kati  ya  wahusika  wawili  yaani  muajiriwa  na  muajiri. 
  Aina  ya  mahusiano  wanayoingia  wahusika  ndiyo  huibua  aina za haki  na   wajibu  kwa  pande  zote  mbili. Mwenye  haki  hutakiwa  kutoa  haki  hiyo  kwa  mwenzake  naye  mwenye  wajibu  huwa  hana hiari  isipokuwa  kutekeleza  wajibu  huo  kwa  mujibu  wa  makubaliano.  
  Hapa  Tanzania  taratibu   za  ajira  na  mahusiano  kazini  huongozwa  na  Sheria  namba 6  ya  ajira  na  mahusiano  kazini 2004.  Sheria   hii  hueleza  wajibu,  haki,  stahili,  kuacha  na  kuachishwa  kazi   na  kila  kitu  kinachohusu  ajira  na  kazi  kwa  ujumla  wake. Kusoma zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa(National Housing Corporation) NHC Lumumba Complex mjini Kigoma leo .Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,(watatu kushoto), Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Lukuvi,(wanne kushoto), Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya,(Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemia Mchechu(kulia), na kushoto ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe katika jiwe kuashiria kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Shirika la Nyumba la Taifa National Housing Lumumba Business Complex mjini Kigoma leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na watatu kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu..


  Jengo la Kitega uchumi Lumumba Business Complex, lililofunguliwa na Rais Kikwete mjini Kigoma leo

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi mradi wa nyumba za bei nafuu NHC eneo la Mlole mjini Kigoma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na  maendeleio ya Makazi Mh.William Lukuvi,Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bwana Nehemia Mchechu
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za bei nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC eneo la Mlole mjini Kigoma leo. Wengine katika picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi(wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya(wapili kulia), Mbunge mstaafu wa Kigoma mjini Mh.Peter Selukamba(wanne kjshoto), Mkurugenzi mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu kulia na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndugu Walid Kabouru.
   Jengo jipya la NSSF Kigoma
   .Uzinduzi wa jengo jipya la NSSF Kigoma
   Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa jengo la NSSF 
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa mji wa kigoma wakati akingia katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika ambnapo alihutubia Mkutano wahadhara na kuwaaga rasmi wananchi wa mkoa wa Kigoma. Picha na Freddy Maro
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa mji wa kigoma wakati akingia katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika ambnapo alihutubia Mkutano wahadhara na kuwaaga rasmi wananchi wa mkoa wa Kigoma(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Kampuni ya TICTS yakabidhi mchango wa Tshs 3,000,000/= kufanikisha shughuli za wiki ya Nenda kwa usalama barabarini kwa Mkoa wa Kipolisi Temeke Kanda maalum ya Dar-es-salaam.Pichani Mkurugenzi wa Shughuli za maendele0 (TICTS) Bw Donald Talawa akikabidhi hundi kwa Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Temeke SP R.T Shemndolwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani.
   Viongozi wa Kampuni ya TICTS.Bi Carol Owenya,Bw Donald Talawa na Bw John Masasi wakimsikiliza Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Kipolisi Temeke  Kamanda  R,T Shemdolwa akielezea mikakati ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke katika usimamizi wa Shughuli za usalama Barabarani Wakati wa wiki hiyo.
   Mkurugenzi wa Shughuli za maendele0 (TICTS) Bw Donald Talawa akiongea baada ya kukabidhi hundi kwa Kamanda wa Trafiki Mkoa wa Temeke SP R.T Shemndolwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani.

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Serikali ya Awamu ya nne inayomaliza muda wake mwezi Octoba mwaka huu, imeyashughulikia matatizo yaliyokuwepo kwa kiasi kikubwa na yale ambayo bado kukamilika, utekelezaji wake unaendelea na mengine mipango imekwisha anza.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jana mjini Kigoma katika uwanja wa Tanganyika, kwenye mkutano wa hadhara kwa madhumuni ya kuagana na wananchi wa Kigoma.

  "Mlinichagua, mlinipa imani yenu, sikusahau kwa sababu nilikua naifahamu Kigoma, kilio chenu nilikuwa nakifahamu".  Rais amewaambia wananchi waliofurika uwanjani hapo.

  Matatizo yaliyokuwepo Mkoani Kigoma wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 ni pamoja na tatizo la umeme ambapo serikali ilinunua jenereta na kulifunga Mkoani Kigoma.

  Jenereta hilo lilitatua matatizo ya umeme katika miji ya Kasulu, Kibondo na Kigoma Ujiji.

  Awamu ya pili ya utatuaji wa matatizo ya Umeme, yanatatuliwa chini ya Mradi wa Umeme Vijijini, maarufu kama Rural Electrification Agency (REA), ambao umekua na lengo la kuunganisha vijiji vilivyobakia.

  Tayari vijiji 92 vimeunganishwa  na hatimaye vijiji 306 vya Mkoa mzima vitaunganishwa. Awamu hii itahusisha Ujenzi wa kituo cha kuongeza nguvu ya umeme na hatimaye umeme kufika Wilaya zingine za Uvinza, Buhigwe na Kakonko.

  Tatizo lingine lilokuwepo ni Maji ambapo Rais Kikwete amesema Mradi mkubwa unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya unatarajia kukamilika mapema mwakani

  Mkoa wa Kigoma pia umekua na tatizo la Mawasiliano ambapo, mwaka 2005 wakati Rais Kikwete anaingia madarakani, Mkoa ulikua na barabara moja ya lami yenye urefu wa kilomita 7.36, Hivi sasa kuna barabara za lami zenye kilomita 28.7 Kigoma mjini, Kasulu kilomita 1.5 na Kibondo kilomita 2.7.

  Mbali na barabara za mjini, serikali ya awamu ya nne imeunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoa jirani kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami. Barabara hizo ni za Kigoma-Kidahwe km 28.2, Mwadiga-Manyovu km 60 na Kidahwe Uvinza km 76.6 na ujenzi ukiwa bado unaendelea kwa barabara za Kidahwe-Kasulu km 50, Nyakanazi- Kakonko-Kabingo km 75.

  Leo tarehe 15 Septemba, Rais Kikwete anatarajia kuzindua daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye urefu mita 275 na barabara zake unganishi zenye urefu wa km 48. Rais pia atazindua barabara ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa km 76.6 ambayo  imejengwa kwa kiwango cha lami.

  Imetolewa na :
  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
  Ikulu-Kigoma
  15 Septemba, 2015

  0 0
 • 09/15/15--02:45: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Na Ally Daud –MAELEZO
  Idadi ya mauzo katika soko la hisa la Dar es salaam DSE limeshuka kwa asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 6.4 hadi kufikia shilingi bilioni 2.4 ambapo zimeuzwa na kununuliwa katika soko zimeshuka kutoka milioni 4.3 hadi kufikia milioni 2.7.

  Akiongea na waandishi wa habari Meneja Miradi na Biashara waDar es salaam Stock Exchange  Bw. Patrick  Mususa alisema kuwa hata hvyo idadi ya mtaji katika soko umekuwa kutoka tilioni 21.9 hadi tilioni 22.3 ikiwa pia na idadi ya mtaji wa makampuni ya ndani imekua tilioni 9.9.

  AidhaBw. Mususa ameitaja benki ya CRDB kuwa ndiyo imeongoza kwa kuuza hisa zake katika soko ikiwa na asilimia 92 ziki fuatiwa na Kampuni ya Swissport yenye asilimia 4 na Twiga Cement ambayo ina asilimia 1.

  “Kampuni ambazo zimeongoza kwa ongezeko la bei katika soko la hisa ni Kenya Airways yenye asilimia 9 pamoja na Kampuni ya bia ya East Africa Breweries ambayo ina asilimia 6 pamoja na Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia yenye asilimia 3”,alisema Bw.Mususa.

  0 0

  Mashindano ya maarufu ya urembo duniani, Miss Universe, sasa yatakuwa chini ya kampuni ya kusaka, kuendeleza vipaji na masoko ijulikanayo kwa jina la WME/IMG. 
  Awali mashindano hayo yalikuwa yakiendeshwa kwa ushirika baina ya kampuni hiyo na kampuni inayojishughulisha na masuala ya habari na burudani ya NBCUniversal na mtangazaji maarufu wa vipindi vya televisheni, mwanasiasa na mfanyabiashara, Donald J Trump. 
  Akizungumza jijini jana, Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamepokea taarifa kuhusiana na kampuni mpya hiyo ambayo pia inaandaa mashindano ya Miss USA na Miss Teen Usa. 
  Maria ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Compass Communications alisema kuwa wamepokea mabadiliko hayo na wataendelea kufanykazi na mmiliki huyo mpya ili kuendeleza vipaji vya wasichana nchini. 
  Alisema kuwa mashindano ya Miss Universe ni moja kati ya matukio makubwa ya burudani duniani ambayo usaidia wasichana kutoka nchi zaidi ya 190 zinazoshiriki kila mwaka na watu zaidi ya nusu bilioni kufuatilia mashindano hayo kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao na televisheni. 
  “Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kufanya mashindano ya Miss Universe Tanzania, tunaamini kuwa mabadiliko haya yatatupa changamoto zaidi kwa lengo la kufika mbali na zaidi kuhakikisha tunatwaa taji baada ya matokeo mazuri ya Flaviana Matata ya mwaka 2007 ambapo aliingia hatua ya 10 bora,” alisema Maria. 
  Afisa Mkuu wa kampuni ya WME/IMG, Mark Shapiro ameahidi kuyaendeleza mashindano hayo kufika ngazi ya juu kabisa ikiwa pamija na washindano bora. 
  "Najisikia faraja kuendshs mashindano haya, tutayaendeleza kwa kiwango kikubwa na kuhakikisha umaarufu wake unaongezeka, naamini mashabiki wengi zaidi kwa sasa watafuatilia mashindano yetu kwa njia ya mbalimbali,” alisema Shapiro.
  Maria Mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai alizungumza katika mashindano yaliyopita.
  Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard akitoa elimu ya afya kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto

  0 0

   Mwalimu wa masomo ya Sayansi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam, Elibariki John akiwaelekeza wanafunzi wa kidato cha pili, Jacqueline James(kushoto) na Ibrahim Juma  wa shule hiyo jinsi ya kutafuta  taarifa za maarifa ya masomo  ya sayansi kwa njia ya kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
  Mariam Mwishaha na Khairat Massoud - wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam wakimsikiliza kwa umakini Mwalimu wa masomo ya Sayansi wa shule hiyo,Elibariki John(kushoto) wakati akiwafundisha masomo hayo kupitia kompyuta mpakato walizopatiwa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
  Wanafunzi wa kidato cha pili wa  shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza mwalimu wao wa masomo ya Sayansi Elibariki John,akiwafundisha somo hilo kwa vitendo kupitia kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.


  0 0

  Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu. Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Sabasaba Mjini Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu kwenye Uwanja wa Nangwanda Jimbo la Liwale.
  AKIZUNGUMZA na wananchi katika mikutano hiyo mgombea mwenza Bi. Samia Suluhu alisema licha ya ilaya ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuonesha kulenga kuboresha maisha ya wananchi haswa akinamama na vijana kupitia vikundi anuai, alisema Serikali itakayoundwa na CCM endapo ikifanikiwa kurudi madarakani itahakikisha inaweka utaratibu wa kupima ardhi na kuigawa kwa wananchi ili kuwaandalia hati za kawaida na zile za kimila kwa vijijini. 

  Alisema utaratibu huu utawawezesha wananchi kuwa na dhamana katika mikopo na kuweza kujiendeleza kwa shughuli zao za kiuchumi. Aliongeza licha ya zoezi la upimaji na utoaji hati kuwa na manufaa kwa wananchi aliongeza kuwa litapunguza migogoro ya ardhi kati ya pande anuai na matumizi tofauti jambo ambalo lilikuwa kikwazo hapo awali. "...

  Tutapima maeneo na kutoa hati za kimila na Serikali ili wananchi waweze kutumia kama dhamana katika mikopo, hizi zitasaidia wananchi kupata fedha za kujiendeleza," alisema. Akizungumzia soko la korosho alisema Serikali imekisikia kilio cha wananchi juu ya utaratibu wa stakabadhi ghalani hivyo kuwaahidi kulifanyia kazi suala hilo. 

  Mambo mengine ambayo Bi. Samia Suluhu aliahidi kuyashughulikia ni pamoja na huduma za maji safi na salama kuzijenga barabara za kuingia na kutoka katika Wilaya hizo za Nachingwea na Liwale kwa kiwango cha lami kwa awamu na kuboresha elimu. Bi. Samia anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Lindi na anatarajia kuanza ziara hiyo mkoa wa Mtwara leo jioni, kuendelea kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi. 
  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  TAMASHA la Amani linatarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali wamepania kutoa burudani ya nguvu kwa mashabiki watakaojitokeza.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa wiki hii na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa wasanii hao wamesema kuna mambo mazuri watayafanya siku hiyo.

  Baadhi ya wasanii waliotajwa kwamba watatumbuiza siku hiyo ni Sarah K, John Lissu, Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Boniface Mwaitege.

  Taarifa hiyo inawakariri wasanii mbalimbali wakizungumzia tamasha hilo, huku wakitamba kwamba mambo yatakuwa mazuri.

  “Nimedhamiria kuwapa mambo mazuri mashabiki wangu, najua watafurahi sana, watakaokuja hawatajuta,” ni kauli ya Rose Muhando.

  Naye msanii Upendo Nkone, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi na kuwa wana imani kubwa litakuwa tamasha zuri.

  0 0

  Wananchi wakiwa katika viwanja vya Ulyankulu wilayani Kaliua
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli leo katika viwanja vya Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani  Tabora  leo katika kampeni za kuwania nafasi hiyo mkoani humo.

  0 0

    Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali la READ International, Rob Wilson (katikati) akizungumza katikasherehe za miaka 10 ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya wanachama wa shirika hilo la kujitolea nchini Tanzania. READ International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa ikisihirikiana na Realising Education for Development pamoja na wahisani wengine imeweza kusaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote.
   Mjumbe wa Bodi ya READ International, Faraja Kotta Nyalandu (kulia), mwanzilishi wa READ, Tom Wilson (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Makumbusho ya jijini Dar es Salaam wakikata keki kusherehekea miaka 10 ya shirika hilo.
    Muasisi wa Shirika lisilo la kiserikali la READ International, Rob Wilson (kulia) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho alipotembelea maktaba ya shule hiyo iliyowezeshwa kwa ufadhili wa shirika hilo kwa kushirikiana na Realising Education for Developmentpamoja na wahisani  wengine. READ International inatimiza miaka 10 tokea kuanzishwa huku ikisaidia ujenzi wa maktaba 72 na kutoa vitabu zaidi ya milioni 1.4 nchini kote. Wengine pichani ni baadhi ya walimu wa shule hiyo.


  0 0


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa unahusu masuala ya Lishe na Chakula uliofanyika jijini Arusha.
  Mhe. Pinda akihutubia
  Mfalme wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo  akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika mkutano huo (hawapo pichani).

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 


older | 1 | .... | 974 | 975 | (Page 976) | 977 | 978 | .... | 3278 | newer