Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUWASAIDIA WAKIMBIZI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,  akizungumza wakati wa  Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu dhana ya wajibu wa kuwalinda raia, ambapo alisema licha ya kuasisiwa kwa dhana hiyo dunia bado imeendelea kushuhudia  maisha ya watu wasiokuwa na hatia yakiendelea kupotea  kwa sababu tu Jumuiya ya Kimataifa inashindwa kutumiza wajibu wake kwa wakati.
 Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa Majadiliano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu  dhana ya kuwalinda raia (R2P) majadiliano yaliyojielekeza katika kutathimini mafanikio na changamoto za utekelezi wa dhana hiyo ikiwa ni miaka kumi tangu kuasisiwa  kwake.
 Picha hii  ya maktaba ni ya  wakimbizi  katika kambi moja nchini Tanzania,  ambao jana  jumanne akizungumza katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UN Balozi Tuvako Manongi amesema kutoka na wimbi kubwa linaloendelea la wakimbizi  kukimbilia mataifa mengine kutafuta usalama wao. Jumuiya ya kimataifa haina budi kushirikiana na bila  kubagua katika  kuwalinda na  utoaji wa huduma na misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi.

Na Mwandishi Maalum,  New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imetoa wito kwa   Jumuiya ya Kimataifa wa kushirikiana katika  wajibu wa kuwalinda na kuwapatia misaada ya kibinadamu,  wakimbizi wanaokimbia machafuko, vita na  migogoro katika nchi zao.
Wito huo  umetolewa   siku  ya jumanne na Balozi Tuvako Manongi,Mwakilishi wa  Kudumu  wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,   wakati  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  lilipokutana  kwa majadiliano  ya  siku moja kuhusu utekelezaji wa dhana juu ya wajibu wa kulinda raia (R2P) mafanikio na changamoto zake.

Dhana  ya wajibu wa kuwalinda raia  dhidi ya  mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita,  mauaji ya kikabila na uhalifu dhidi ya  binadamu   ilianzishwa mwaka 2005 wakati  wa mkutano wa Kimataifa  uliofanyika mwaka huu, ambapo viongozi wakuu  wa  nchi na serikali walikubaliana kwamba wajibu wa kwanza wa kuwalinda raia  dhidi ya udhalimu wa aina yoyote ile ni wa serikali yenyewe husika.


UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA

$
0
0
Raymond Richmond, Meneja wa kampuni ya Bia (TBL) Mwanza,akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), mapumba ya mchele,yanayotumika kuzalisha nishati ya umeme wa kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari, Daniel Mkate (kushoto) akiwauliza maswali, Meneja wa  Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na Meneja wa Maji na Nishati wa kampuni hiyo, Sunday Kidolezi, kuhusu  changamoto ya upatikanaji wa mali ghafi hiyo na madhara yake katika kuzalisha nishati na athari za mazingira.
Meneja wa Maji na Nishati wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Sunday Kidolezi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhudu mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,unaotumika kuendesha mitambo ya kiwanda cha kampuni hiyo kwa kutumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa kiwanda cha kampuni hiyo,Raymond Richmond.

MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA ND.JABU KHAMIS MTWANA YALIYOFANYIKA JANA KIJINI KWAO WILAYA YA MICHEWENI

$
0
0
 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu.
 Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishiriki katika mazishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Micheweni Pemba.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 08/09/2015

SHUKRANI TOKA KWA MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU

$
0
0
New Picture

Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wa Ukonga Dar es salaam wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nao na kuwafariji kwa hali na mali katika kumuuguza na mpaka kumlaza katika nyumba ya milele mpendwa baba yao Dr. John Edward Mchechu aliyefariki tarehe 21/07/2015 nyumbani kwake Ukonga na kuzikwa tarehe 26/07/2015 Muheza, Tanga.
Shukrani za pekee zimfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. JakayaMrishoKikwete,MakamuwaRais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, WaziriMkuu, Mh. Mizengo Peter Pinda, Mawaziri, Wabunge, WakuuwaMashirikanaWafanyakaziwaSerikalikwakutufarijikipindichote cha kuumwa kwake mpaka alipotwaliwa kutoka ulimwengu huu.
Shukrani za pekee pia ziwafikie wafanyakazi na wajumbe wa bodi ya NHC, Serengeti Breweries, DAWASCO, KCB, Rafiki Club, Soul Sisters, New Millenium Women Group, Beach Ladies, Sisters Club, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Muhimbili, Hindu Mandal, Apollo Hydrabadna Dispensary yaArafa.
Mapadri na wachungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Mbezi Beach, Makanisa ya Anglikana ya Mtakatifu Paulo la Ukonga, Dar es Salaam na Mtakatifu Petro la Mkuzi,Tanga, kwaya mbalimbali na vikundi vya maombi kwa msaada wao wa kiroho.
Tunawakushukuru mtu mmoja mmoja lakini haiwezekani kwani watu ni wengi sana, tunaomba tu mpokee shukrani zetu za dhati kutoka moyoni mwetu kwajinsi mlivyotufariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu.
Misa ya Shukrani Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wanapenda kuwakaribisha wote katika misa ya shukrani itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 12/09/2015 kuanzia saa mbili asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Petro Mkuzi, Tanga. Karibuni sana mjumuike nasi.
Raha ya milele umpeeeh Bwana wamilele umwangazie apumzike kwa amani, Amina
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU.

SHUKURANI

$
0
0
Familia ya Bwana na Bibi Charles Yanga ya Tabata Chang'ombe, Dar es salaam, inakukaribisha kwenye Misa ya shukrani kwa ajili ya marehemu mtoto wao mpendwa Abel Charles Yanga. Misa itakuwa Jumamosi tarehe 12 Sep. 2015 saa  5.00 asubuhi nyumbani Tabata Chang'ombe. Baada ya Misa tutashirikiana chakula cha mchana. Karibuni sana. 
Kwa mawasiliano zaidi  Kiduma Yanga 0653 013 211 

Bei ya Madafu leo

AIRTEL YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa (
Kushoto) akimkabithi kikombe Afisa masoko na biashara wa Airtel ,
Emmanuel Raphael mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel
kuibuka mshindi wa pili  katika maonyesho ya Biashara ya Afrika
Mashariki ya mwaka huu.  Katika maonyesho hayo Airtel ilipata makombe
manne katika vipengele mbalimbali ikiwemo, Mtoa huduma bora , Mtoa
huduma bora katika sekta ya mawasiliano,  ubora katika mawasiliano ya
habari na tecknologia  pamoja na mshindi wa pili wa maonyesho kwa
mwaka huu. Akishuhudia (katikati) ni mwenyekiti wa Tanzania Chamber of
Commerce , Industrial and Agriculture Elibariki Mmari
Afisa masoko na biashara wa Airtel, Emmanuel Raphael katika picha na
makombe mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya
Afrika Mashariki ya mwaka huu

Wafanyakazi wa Airtel kwa pamoja wakiwa na makombe yao mara baada ya
kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi
Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya
Afrika Mashariki ya mwaka huu


·         Yazawadiwa vikombe vinne vya ubora wa huduma na bidhaa.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imepokea
vikombe vinne katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kufatia
ubora wake katika kutoa huduma na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake.

Maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mashariki ni maarufu kwa
kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo bidhaa za matumizi ya
kawaida na ya viwanda, huduma, mashine na teknologia.  Na maonyesho
haya yametoa fulsa ya kukutanisha wadau pamoja na kubadilishana uzoefu
wa kibiashara na kuwawezesha ushirikiano wa biashara  katika nchini za
ukanda wa mashariki.

Akiongea wakati wa halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Uledi Abbas Musa alisema” Maonyesho haya yana lengo la
kuwapatia makampuni yaliyoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki
fulsa ya kujitangaza na kukuza biashara zao lakini pia kuwapatia
nafasi ya kuboresha mahusiano ya kudumu na wateja wao. Leo najisikia
furaha kuwazawadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  kwa kuonyesha
ubora wake katika huduma, bidhaa, tecknologia za kibunifu na kwa kuwa
washindi wapili katika maonyesho  ya mwaka huu”
Aliongeza kwa kusema” Airtel imedhihirisha dhamira yake ya kutoa
huduma za kibunifu na za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na
kutokana na hilo tumeona ni muhimu kuwapongeza na kuwazawadia kwa
jitihada zao”

Kwa upande wake Afisa Masoko na bidhaa wa Airtel , Bwana Emmanuel
Raphael alisema” huu ni mwaka watano mfululizo sasa kwa Airtel
kushiriki katika maonyesho haya tukuwa na lengo la kufikia wateja wetu
, kutoa elimu ya huduma na bidhaa tunazotoa pamoja na kuboresha
mahusiano nao. Maonyesho haya pia yamekuwa ni fulsa muhimu kwetu
kuonyesha bidhaa na huduma zetu za kibunifu na za kisasa na pia ni
nafasi pekee ya kushikiana na makampuni mengine yanayoshiriki kila
mwaka”.

“Napenda kuwashukuru waandaaji wa maonyesho haya kwa kutambua na kuona mchango wetu na tunahaidi kuendelea na dhamira yetu ya kutoa hudumabora na za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu.” 

AliongezaRaphael Katika halfa hiyo, Airtel ilipokea makombe manne ya ubora katikavipengele vya  namba moja kwenye kutoa huduma, namba moja katika sektaya mawasiliano, namba moja katika teknologia ya mawasiliano ya habarina namba mbili katika maonyesho ya mwaka huu. 

Nchi zilizo shirikikatika maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda,Rwanda and Burundi

SAMY COOL PRODUCTION WAENDELEZA KUTOWA HUDUMA YA MAZOEZI JIJINI DAR

$
0
0
 Mwalimu Hasani Gigoro akitoa mafunzo ya Dance kwa ajili ya mazoezi ya kupunguza kitambi na kupunguza unene  mazoezi hayo ambayohufanyika kila siku ya juma tatu kuazia saa kumi na mbili jioni, mpaka saa mbili usiku  kujiunga na mazoezi hayo ya dance kiingilio ni Tsh 5000/=  mazoeo hufanyika katika viwanja vya Mzalendo Pub Kijitonyama leo Jijini Dar es Salaam.


Mazoezi ya viungo ya kudensi yakiendelea kwa umakini wa hali ya juu.

WANANCHI WA KATA YA BARAY KARATU WAKABIDHIWA MIRADI MINNE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha Omary Kwaang’ (katikati mwenye kaunda suti) akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo, akikagua lambo la maji eneo la Endesh, linalotumiwa na mifugo na binadamu, lililogharimu sh169 milioni kwa ufadhili wa shirika la World Vision. 
 Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha Omary Kwaang’ (kushoto) akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo, akikagua lambo la maji eneo la Endesh, linalotumiwa na mifugo na binadamu, lililogharimu sh169 milioni kwa ufadhili wa shirika la World Vision.
WANANCHI 12,082 wa Kata ya Baray Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamekabidhiwa miradi nane ya elimu na afya ambayo imegharimu sh447.8 milioni kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la World Vision Korea.
Mratibu wa mradi wa World vision Karatu John Massenza akikabidhi jana miradi hiyo kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo John Mabula alisema  itawanufaika wakazi wa vijiji vitatu vya Dumbachang, Mbuga Nyekundu na Jobaj.

DANGA CHEE: Mahojiano na Zahir Ally Zorro -

A DECADE LONG OF BLOGGING: 6 IMPORTANT LESSONS FROM MICHUZI BLOG

$
0
0
By Mdau wa globu ya jamii

Every niche has a name. And when it comes to blogging in Tanzania you cannot miss the name of Muhidin Issa Michuzi. His blog, dubbed as Globu ya Jamii (societal blog) , with a slogan “The most read swahili blog on earth”, is unquestionably one of the most informative and most authoritative Swahili blog on earth. I know he has come a long way to deserve all this, and he is still going strong.
With Collins Mtita, author of this note, in Paris
It was on the 8thSeptember of 2005 when Michuzi wrote his first post (see below) for what would become one of the most famous Swahili blogs. Today this very platform marks the first day into another decade. Many have come and many have gone, a few have persistently stood the test of time, and he is one of them.

It is rather uncustomary to find such articles on Michuzi Blog, (taking into slide his rather down-to-earth attitude) but this being a mark to celebrating  his decade long blogging career; I thought he deserves a  pat on the shoulder. And I dare take this opportunity to do just that. I know strong people never get this all the time, but once in a while it does more good than harm.

Michuzi was certainly a household name before blogging. He was, and still is, one of the most prominent photojournalists in Tanzania, since way long back in the days when print media ruled. When blogging started, Michuzi found an opportunity to express his burning passion in a more tangible way to reaching more people. The rest is history.

I am aware that he was not the first (but he was the pioneering blogger in Tanzania as then all Tanzanian bloggers were in the Diaspora), but he has made blogging famous. He is not the only one, but he has created a career for many to follow through. He may not be the last, but his name will be engraved in the minds of those who think of blogging as an opportunity to express oneself, as a source of income and a channel to let others shine as well.

If I had to sum up the last decade, here are a few things that I have managed to learn from Michuzi though his long and amusing career of blogging.



1. Love what you do

Falling in love with that you do is perhaps one of the most precious thing I have learnt though my constant encounters with Michuzi. Through chats with him I could easily tell that he does not stress for what he does, simply because he is having fun doing it. When you love what you do, that love becomes expressed in what you do. People can see and they will get to love it too.

At Finlandia hall in Helsinki, Finland
Loving what you do is doing it every day. Loving what you do is doing it with the best of your abilities. Loving what you do is to think about it almost all the time. And Michuzi cannot be overstated in this, because he still loves what he does.

2. Timely provide what people want with standards

Blogging is a hard work, but it rewards handsomely. This can be well understood by those in this niche. What is even harder is to provide what people want while maintaining standards.

When Michuzi started blogging, there was hardly any media outlet that entertained the idea of instantly publishing news or events within a short period of time of it breaking, not even Television. Michuzi saw this opportunity and seized it. In effect, he helped shape news reporting in Tanzania by proving almost real-time updates on main events – on politics, sports, entertainment, and lifestyle. With time, this habit built trust among daily visitors and they became permanent audiences.

It goes without saying that this blog has been so resourceful to the people in the Diaspora. A few years back when social media was  still in its infancy, and not so many people blogging, Michuzi blog was the only way to get updates from Tanzania, and that still continues today.

3. Be simple

Simplicity is the key to brilliance, a simple quote in itself with such a powerful meaning. Simplicity is the power to attract audience and it can never be explained any easier.

Success comes when you think beyond today and trivial challenges. Think at a very higher level, make big decisions but act simple so that more people understand you. That is the recipe for success.

4. Do not be predictable

Predictability is a weakness. If people can tell what you will do next, then you are in the wrong path. The best way is to become so unpredictable that people will keep coming back for more. For so long Michuzi blog has been a homepages for many. These people understood that within a very small span of time there will be something new on Michuzi blog, but they could hardly tell, hence they kept coming back for more hot updates from all walks of life.

5. Become a trendsetter

With Fidelis Tungaraza in Helsinki
The leader is visionary and never distracted by petty issues. He is more focused on solving perennial issues and create path for others to follow. Trendsetting is not easy if you are not focused or do not know what you want, but it is left for a few who have the courage to follow through their ideas even if none believes in them yet.

6. Never give up, enjoy the journey

I once asked Michuzi on how he finds blogging after being in the niche for nearly a decade, his reply was “The journey through blogging has not been easy, but for me it was more fun. I have faced my a share of obstacles on the way, but the best thing about challenges whenever you have fun is that they have a tendency to propelling  you forward. I can say it is magic in disguise.

As we celebrate 10 years of Michuzi blog, I sincerely wish Michuzi Media Group a lot more success and more wonderful opportunities ahead. May you reach and touch more people as they go through their own battles through life. You are inspiration to many.

Thanks a lot Ankal  Muhidin Issa Michuzi. You have been a force to reckon with and an inspiration to me, and hopefully many more.

Wako,


Mdau wa globu ya jamii, Diaspora


PS: Nashukuru sana mdau wa Diaspora ambaye si mwingine ila huyo hapo juu, Collins Mtita, ambaye ndiye webmaster wangu. Picha inayofuata ni mimi nikiwa Finlandia Hall mwaka huu, miaka 10 baada ya kuanzisha Michuzi Blog mahali hapo Septemba 8, 2005. Fidelis Tunaraza ambaye niko naye katika picha ya mwisho ndiye aliyenishawishi kuanza ku-blog. Picha ya mwisho (ambayo ndito ya kwanza kuweka katika Michuzi Blog) niko na Ndesanjo Macha aliyenifungulia blog na namna ya kuiendesha siku ya kwanza kabisa) . Hawa watu watatu ni muhimu mno katika maisha yangu ya blogging. Nilipanga kufanya sherehe kubwa kuadhimisha siku hii adhimu lakini nikaona haitonoga sana kwa kuwa kuna mambo ya kampeni kila kona. Sherehe nitaifanya mwezi Desemba mwaka huu.

Muhidin Issa Michuzi
Septemba 8, 2015


“HATUSAMBAZI MAJI YENYE UCHAFU BUGURUNI”- DAWASCO

$
0
0
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wananchi kuepuka taarifa za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya usambazaji maji machafu kwenye line za mabomba ya wateja wa Dawasco.

Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro alisema taarifa hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili kuchafua taswira ya shirika hilo na pia  kuihusisha Dawasco moja kwa moja na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.

“Tunawatahadharisha wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo vyote kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji yenye kuleta madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu kufanya hivyo ” alisema Lyaro.

‘Ukweli wa maeneo yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na Buguruni ni kuwa kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini kama ni ya watu binafsi au za manispaa. 

Wao walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja walio na line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea mabomba ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu yaliyokatwa kutoka kwenye mifereji” aliongezea lyaro.

Alisema kuwa Baada ya kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni kuchukua sampuli za Maji hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji hayo yasiendelee kutoka.  Na baada ya upimaji sampuli ile na kukuta sio salama tulitenga line(isolate) ya majisafi ya sharif shamba hadi hapo tatizo litakapotatuliwa na mamlaka husika.

Tuhuma za Dawasco kusambaza Maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku zikihusishwa zaidi na athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kushika kasi jijini dar.

NBC LAUNCHES SMS ALERT

$
0
0
NBC has today launched SMS alert service that enables NBC customers to receive instant SMS notifications on their registered mobile phone numbers of transactions carried out on their accounts. The SMS notifications enable NBC customers to instantly keep track of transactions happening on their accounts. 
“In addition, this service will allow our customers to identify if their accounts have carried out any unauthorized transaction enabling them to take immediate action”, said Musa Jallow, the bank’s Head of Retail Banking
The SMS notifications will be sent out for all ATM and POS transactions carried out by a customer’s debit card. This service is free of charge, and hence NBC customers will not be charged for receiving SMS notifications.
NBC customers are not required to register for this service as SMS notifications are sent to customers’ mobile phone numbers which are registered in the NBC database. All customers with valid registered phone numbers automatically receive SMS notifications every time they carry out ATM or POS transactions with their debit card.
“If any of our customers does not receive SMS notification, it’s mostly likely that we do not have their phone number registered in our database or the phone number registered is incorrect. If that happens, we urgently advise the customers to visit any of the nearest NBC branch to update their information and start enjoying this service”, stressed Musa Jallow
NBC is one of the most represented retail bank in the country with over 45 years experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself with an expanded branch network and footprint. NBC has 52 branches, 242 Visa enabled ATMs, and over 173 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC has employed over 1200 staff

BENKI YA NMB YAIPA MKONO JAMII YA GEITA

$
0
0
 Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino (kulia) akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita - Manzie Mangochie (kushoto) kwa niaba ya Shule za Msingi Nyamkumbu na Ukombozi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka Benki ya NMB katika hafla fupi iliyofanyika mjini Geita jana ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
 Wanafunzi wa Shule za Msingi Nyankumbu wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 na Benki ya NMB jana wilayani Geita.NMB ilisaidia madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni 10 katika shule mbili za msingi za Nyamkumbu na Ukombozi ambapo kila shule ilipata madawati 50
BENKI ya NMB jana ilikabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shule za Msingi Nyankumbu na Ukombozi zilizopo mkoani Geita ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.

Msaada huo umekabidhiwa na meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino ambapo mkuu wa wilaya ya geita alipokea madawati hayo kwa niaba ya shule hizo mbili za msingi.

“Madawati haya tunayoyakabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema Augustino.

EXPRESSION OF INTEREST JOINT DEVELOPMENT OF PLOT NUMBER 552 IN UPANGA AND PLOTS NUMBER 296 - 299 IN MIKOCHENI, DAR ES SALAAM

$
0
0

EXPRESSION OF INTEREST
JOINT DEVELOPMENT OF PLOT NUMBER 552 IN UPANGA AND PLOTS NUMBER 296 - 299 IN MIKOCHENI, DAR ES SALAAM

The ELCT-ECD Investment Trust is a commercial entity of the Registered Trustees of The Evangelical Lutheran Church in Tanzania (ELCT) - Eastern and Coastal Diocese (ECD). The core objectives of the Trust are:-To be the vehicle that will be used to achieve greater investment by the ELCT-ECD for its well being so as to support itself financially, to advice the  ELCT-ECD where and when to invest and how much to invest, To mobilize financial resources from the general public and in certain specific communities and groups in society, locally and internationally, in order to meet the costs of implementing development programmes and activities and  to cooperate with relevant national and international institutions in order to participate jointly in eradicating poverty.

The Investment Trust is offering an investment opportunity to develop its plots which are located in Dar es Salaam - Central District Business area.

The first release of joint development is proposed to be at plot number 552 in Upanga just opposite Muhimbili National Hospital, Mindu Street.  The plot is 2,878.59 square meters. The other plots are number 296 - 299 at Mikocheni close to Mwalimu Nyerere bus station, these plot are 3,960 square meters. The plots are prime for commercial, residential, diplomatic residences, and offices. In addition, the plots are surrounded by all basic infrastructure including electricity, water and tarmac roads.
 
In that regard, the Board of Trustees of ELCT - ECD INVESTMENT TRUST invites expression of interest from different investors/partners under the following clusters; A: Embassies, International Organizations/Agencies B: Social Security Funds, International Financial Agencies C: Real estate developer Companies/organizations. Individual are strongly discouraged to apply. For further information please call Mr. Godfrey Benjamin, Telephone No. 0719 367 002

Please note that the Board of Trustees can correct and re-design or reject the project proposal. All interested investors/partners are advised to send their profile/project ideas through the under mentioned address or e-mail:  info@elctecd.org before 30thSeptember 2015.

The Secretary to the Board of Trustees
ELCT - ECD Investment Trust
15 Soikoine Drive
Luther House Building near Azania Front Cathedral
First Floor
P.O.BOX 837
DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA, MJINI KIGOMA LEO.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya jiwe lenye Madini huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aifola Investiment Co. Ltd, Zubery Mabie, kuhusu upatikanaji wa madini na utengenezaji wa Unga wa 'Lime Powder', wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika leo Sept 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
 Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika leo Sept 9, 2015. Picha na OMR

RATIBA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA RAIS 2015

LOWASSA, DUNI WAHUDHURIA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CHAMA ZA CUF, ZANZIBAR LEO

$
0
0


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, Nassor Mazrui, wakati akiwasili katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Mgombea Urais wa Ukawa wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CUF, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI

BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

MICHUZI BLOG YAADHIMISHA MIAKA KUMI YA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
Maadhimisho ya Miaka 10 ya uanzishwaji wa MICHUZI BLOG hapa nchini, chini ya Mmiliki wake Ankal  iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Keki  ya maadhimisho ya miaka  1o ya MICHUZI BLOG ikiwa na keki ndogo zenye majina ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
 Mr na Mrs Ankal  na watoto wao wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 10 ya MICHUZI BLOG, wakishuhudiwa na baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
Mkurugezi Mtendaji wa MICHUZI MEDIA GROUP,Ankal akilishwa keki na mkewe  katika hafra fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mpiga picha wa Michuzi Blog, Avila Kakingo akifungua shampeini katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA  
GROUP wakiwa katika picha ya pamoja.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images