Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 95 | 96 | (Page 97) | 98 | 99 | .... | 3286 | newer

  0 0
 • 04/09/13--01:26: SHUKRANI
 • Familia ya Mzee George P. Mapango na Marehemu Mwashaban A. Liganja tunatoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kwa kutufariji katika msiba wa mpendwa wetu MARIA G. MAPANGO aliyefariki tarehe 04 Machi, 2013 na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni hapa Dar es Salaam tarehe 06 Machi, 2013.

  Shukrani za pekee ziwafikie wafuatao, Mke wa Rais wa Awamu ya Pili, Bibi Siti Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, Mkurugenzi na Wafanyakazi wa Inter-Consult Ltd., Bwana Jonas Masabala, Katibu Mkuu Kiongozi, (Mstaafu),Bwana Phillemon L. Luhanjo na Mama Luhanjo, Katibu Mkuu, Ikulu, Naibu Katibu Mkuu, Ikulu, Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu, Wafanyakazi Ofisi ya Rais, Mapadre wa Kanisa la ST. JOSEPH, Marafiki wa Marehemu Mwashaban A. Liganja, Majirani Ocean Road Flats, Madaktari na Manesi Wote waliokuwa wanamhudumia Maria (IA) katika Hospitali ya Emilio Mzena, Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi J.K. Nyerere, Shaaban Robert High School, Al-Muntazir High School, Jumuiya ya Ocean Road na Ndugu, Jamaa na Marafiki

  Tarehe 13 Aprili, 2013 kutakuwa na mkesha wa Kisomo na tarehe 14 Aprili, 2013 saa 04.00 Asubuhi kutakuwa na misa ya Shukrani ambapo shughuli zote zitafanyika nyumbani kwao Ocean Road Flats. Karibuni

  “RAHA YA MILELE UMPEE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI - AMINA.

  0 0

  Waziri Mkuu Mtaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdurahaman Kinana wakati walipo kutana katika eneo la ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam hivi karibuni.Picha na Chris Mfinanga.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambao walikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali baada ya uzinduzi wa mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up). Kushoto Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Magari matatu ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  On April 8, 2013 President Jakaya Kikwete (third from right) met with the Millennium Challenge Corporation (MCC) CEO Daniel W. Yohannes (third from left) at the State House in Dar es Salaam. President Kikwete and Mr. Yohannes discussed the ongoing partnership between MCC and Tanzania, which was deemed eligible to develop a second compact in December of 2012. Mr Yohannes is currently visiting the country to mark the upcoming completion of MCC’s $698 million compact, which invested in roads, water and energy sectors in both Tanzania mainland and Zanzibar. Others in the picture are Ambassador Alfonso E. Lenhardt (second from right), MCC Managing Director for Public Affairs Nasserie Carew (right), MCC's Resident Country Director Karl Fickenscher (second from left) and U.S Embassy's Political and Economic Affairs Counselor, Elizabeth Pelletreau (left).

  0 0

  Habari yako Mdau Michuzi!

  Leo asubuhi katika mchakato wa kwenda mzigoni town, maeneo ya selander bridge, nilikutana na staili mpya iliyo nikosha roho ya kutoka kwa jeshi la polisi (traffic) ama kama wanavyo julikana 'wazee feva' wakitoa uhamasishaji wa usalama barabarani kwa kutumia bajaj na kipaza sauti kwa madereva barabani.

  Hii ni safi sana hasa ukizingatia kuwa inasaidia madereva wote kuhamasishwa na kuwa makini muda wote sababu wanaambiwa wasifanye baadhi ya faulo za barabani kama kutanua kwa kipasa sauti.

  nilifanikiwa kuwadaka kwa picha na nimeziambatanisha. Warushie wadau katika blog yako waweze kuona juhudi za jeshi letu likifanaya kazi na big up kwa aliyetoa donation ya bajaj hii amabye ni 'DSM ROAD SAFETY COMITEE' kama inavyoonekana nyuma ya bajaj hiyo.

  Asante

  Mdau Jerry


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini China,Philip Marmo (katikati) akizungumza na Ujumbe wa Bodi ya Utalii Tanzania uliyopo nchini China kwa kazi maalum ya kutangaza Utalii wa Tanzania nchini humo.
  Maafisa kutoka Ujumbe wa Tanzania walioko nchini China kwa kazi maalum ya kutangaza utalii wa Tanzania.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii nchini Balozi Charles Sanga akisani kitabu cha wageni katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini China.Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China,Philip Marmo.

  0 0
 • 04/09/13--06:06: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi akitoa Malekezo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA),jana jioni alipotembelea eneo hilo ambapo crane iliyokuwa inanyanyua mabehewa yaliyoanguka ilipata ajali ya kuangukia mwishoni mwa wiki hii katika neon la Mzenga kisarawe.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, (Mwenye tai nyeusi), akimsikiliza Meneja wa Usalama wa TAZARA, Bw. Elisha Mhoka, wakati akitoa maelezo ya namna ambavyo Crane hiyo ilianguka na njia zinazotumika kuhakikisha inasimama. Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walitembelea eneo hilo jana jioni kuangalia kasi ya kuisimamisha crane iliyoanguka aidha Katibu Mkuu huyo ameiagiza TAZARA kuhakikisha kazi hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo.
  Crane (yenye rangi ya njano) ya shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA) ambayo ilikuwa inainua mabehewa yaliyopata ajali ikijaribu kuinuliwa na Crane nyingine ya Shirika hilo jana jioni katika eneo la Mzenga Kisarawe.
  Crane inayosaidia kuiinua Crane iliyoanguka mwishoni mwa wiki wakati ikijaribu kuinua mabehewa yaliyopata ajali katika eneo la Mzenga Kisarawe kama yalivyokutwa jana jioni,wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.PIcha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam. Katika Harambee hiyo zilikusanywa fedha taslimu shilingi milioni 71 na ahadi ya fedha za Kitanzania shilingi milioni 658.
  Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi sarafu Dkt. Charles Kimei, baada ya kuinunua sarafu hiyo kwa Sh. milioni 19 katika mnada wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi, baada ya kununua sarafu kwa Sh. milioni 20, wakati wa Harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha moja ya Sarafu iliyopigwa mnada katika harambee ya Mfuko wa Udhamini wa Elimu ya Juu wa Mwalimu Nyerere, iliyofanyika jana Aprili 8, 2013 katika Ukumbi wa Benki Kuu (BOT) jijini Dar es Salaam, ambayo ilinunuliwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi kwa Sh. milioni 20. Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa. Harambee hiyo ilifanyika jana April 8, 2013 katika Ukumbi wa BOT.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa harambee hiyo. Picha na OMR

  0 0

  Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi na watu wengine mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.
  Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake, mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika ndani ya uwanja wa Kasarani,Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais wa nchi mbalimbali ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria.
   Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta
  Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
   Rais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.
   Rais wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma hotuba yake fupi wakati wa kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.

  0 0

  Mrurugenzi Mkuu wa Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew akizungumza mapema leo asubuhi wakati akifungua warsha ya uzinduzi wa huduma mpya ya "free* mobile travel itinerary app for iPhone and Android" inayomuwezesha mteja kupata huduma ya kununua tiketi ya ndege kwa kutumia simu ya mkononi.Warsha hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Towers jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mipango wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Robert Maina akiwasilisha mada kwa wadau  na Mawakala wa kuuza tiketi za Ndege nchini wakati wa warsha iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo wa Travelport Tanzania,Rehema Issa akitoa mafunzo kwa Wadau na Mawakala wa kuuza tiketi za Ndege nchini juu ya huduma mpya ya "free* mobile travel itinerary app for iPhone and Android" iliyozinduliwa leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam.
  MC wa Shughuli hiyo,Khadija Kellow akionyesha moja ya vipengele vya huduma hiyo mpya kwenye tangazo lililokuwepo kwenye ukumbi huo.
  Katibu wa Chama cha TASOTA,Shamim Kermali akitoa neno kutoka kwenye chama hicho.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,( kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.Picha na RamadhanOthman,Ikulu.

  0 0

  Katika kuendelea kuboresha mahusiano bora kati ya Benki na wateja wake, Tawi la Benki ya CRDB Meru liliandaa siku maalum kwa ajili ya watoto iliyoitwa Junior Jumbo Day. 

  Siku hiyo ilikua ni kwa ajili ya kuwakutanisha wazazi, watoto na wafanyakazi wa Benki katika mazingira tofauti na ya kiofisi ambapo michezo mbalimbali iliandaliwa kwa ajili ya watoto huku pia zawadi mbalimbali zikitolewa kwa watoto. 

  Pamoja na hayo vyakula na vinywaji mbalimbali viliandaliwa kwa ajili ya watoto na wazazi/walezi wao. Yafuatayo ni baadhi ya matukio ya picha zilizochukuliwa kwenye tukio hilo.
  Afisa masoko wa Benki ya CRDB akihudumia watoto waliofika katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha kwenye siku maalumu ya Junir Jumbo Day.
  Watoto wakifurahia michezo mbalimbali ya iliyoandaliwa katika siku maalumu ya watoto (Junior Jumbo Day ) katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
  Watoto wa shule za msingi Hady,Kilimani,St Patrick,Green Acres na watoto wa wateja wakisherehekea siku maalum ya watoto iliyoandaliwa na Benki ya CRDB,tawi la Meru kwa ajili ya watoto iliyofanyika tarehe 6/06/2013 jijini Arusha katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
  Watoto wakishindana kwenye mchezo wa kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
  Mmoja ya watoto walioshinda moja ya michezo iliyoandaliwa na kukabidhiwa zawadi na Meneja wa tawil la Meru Bi. Loyce Kapaliswa katika viwanja vya Olasiva Park Garden jijini Arusha.
  Watoto wakijiandaa kushindana mchezo wa kukimbia na magunia katika viwanja vya Olasiva Park Garden.

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimshukuru Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose kutokana na ubalozi huo kutoa mafunzo ya mitandao ya kijamii (Social Media) kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake yaliyofanyika mwezi wa tatu mwaka huu. Balozi huyo alimtembelea waziri Dk. Mukangara ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kuimarisha mahusiano baina ya Wizara hiyo na Uingereza.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akibadilishana kadi ya mawasiliano (Business Card) na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Ubalozi wa Uingereza umeahidi kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akisalimiana na Joseph Paync ambaye ni afisa miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose. Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

  0 0

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,
   Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahimu Kilongo 
  akionyesha bastola iliyokutwa toka kwa watuhumiwa watatu 
  waliokamatwa kwenye moja ya nyumba ya kulala 
  wageni iliyopo eneo la Sombetini jijini Arusha.
  Mahmoud Ahmad Arusha

  Jeshi la polisi mkoani hapa limefanikiwa kuwatia mbaroni majambazi watatu wakiwa na bastola aina ya browning yenye no.016080 pamoja na risasi zake 41 huko maeneo ya Shamsi kata ya Elerai jijini hapa.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Ibrahim Kilongo alisema kuwa huko maeneo ya shamsi kwenye bar ya Tarakea walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na bastola hiyo iliyokuwa na risasi 13 kwenye magazine na baada ya kwenda kuwapekuwa kwenye nyumba ya wageni ya Honolulu waliwakuta na risasi zingine 28.

  Kilongo aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kwenye tukio hilo kuwa ni Hashimu Abdallah 59 mkazi wa KIhonda mkoani morogoro na mwingine ni Omari Husein Ludanga 40 mkazi wa Morogoro na mwingine ni Gibson Ngosi 56 mkazi wa Gairo.

  Kaimu Kamanda alisema kutokana na upelelezi uliofanyika matukio mawili tofauti waliwabaini watuhumuwa hao wakishirikiana na mwenzao Raphael Robert walishiriki kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye matukio mawili yaliofanyika tarehe tofauti 13,16 ya mwezi wa 3 mwaka huu jijini hapa.

  Alisema kuwa mtuhumiwa Raphael yeye alikamatwa pekee yake akiwa na simu iliyoibiwa kwenye tukio la kwanza maeneo ya Kijenge majira ya saa 1:30 usiku baada ya kumpiga risasi ya paja Vicky Maglan 50 na kumpora kiasi cha tsh.700,000 na simu ya mkononi akiwa anatokea dukani kwake maeneo hayo ya kijenge.

  Aidha katika tukio lengine Kilongo alisema kuwa watuhumiwa hao walishiriki katika tukio la kuiba kwenye shule ya Notre Dame iliopo kwenye eneo la Njiro na kumpiga risasi Sister Mary Shobana 79 mkazi wa Njiro na kasha kunyang’anya fedha taslimu kiasi cha tsh.30 milioni ambazo alitoka kuchukuwa kwenye Benki ya Exim tawi la shoprite.

  Kaimu kamanda alisema baada ya mahojiano watuhumiwa walikiri kushiriki katika matukio hayo na kuwa jeshi hili linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine walioshirikiana nao kwenye matukio hayo huku watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara upelelezi wa awali kukamilika.

  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo (MB) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta mpakato (laptop) kuashiria uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
  Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo (MB) akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyarandu (MB) akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
  Mratibu Mwanzilishi wa Kampeni ya ShuleDirect, Faraja Kotta Nyalandu akifafanua jambo wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Faraja alisema kuwa ili malengo ya nchi yetu hasa kwenye elimu bora yafikiwe, ni muhimu kila mtu katika Nyanja na maisha yake atimize wajibu wake, na hata wakati mwingine achukue wajibu ambao si wake na aliendelea kusema kuwa inatupasa wote tuchanganye uzoefu, maarifa, ujuzi, miundombinu, rasilimali za wengi ili kufikia malengo ya nchi yetu. 
  Mratibu Mwanzilishi wa Kampeni ya ShuleDirect, Faraja Kotta Nyalandu (pili kushoto) akiwa na Jacqueline Ntuyebaliwe,Ally Remtullah na Mdau.
  Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo akifurahi jambo na baadi ya wanafunzi wa shule za sekondari waliokuwepo kwenye uzinduzi huo wakati akiwaonyesha kitu kutoka kwenye kompyuta.

  0 0


  AFRICAN Barrick Gold (ABG) has appointed Janet Reuben-Lekashingo (pictured) as the Organizational Effectiveness Director of ABG.

  Janet assumed her position effectively from 1 April, 2013, making her one of the most senior Tanzanians in the mining company.

  Her main duties will be to work with the team to lead evolution of the human resources function to Employee Effectiveness Management, ensuring that ABG has all organizational conditions required to utilise the available workforce at their full potential and effectively ensure all the control mechanisms for monitoring the effectiveness of the employee utilisation are in place.

  Her last appointment in ABG was Corporate Human Resources Manager, where her main responsibilities included Talent Management and Learning & Development and advising ABG's mine sites on Human Resources related processes.

  Janet joined ABG as the Human Resources Manager for the Dar es Salaam office and working with specific projects with the mine sites in October 2008. She has worked in different capacities within the Human Resources Function in the company.

  Prior to joining ABG, she was the Human Resources Manager for AngloGold Ashanti’s Geita Gold Mine where she started her mining industry career after spending 5 years in the aviation industry.

  Janet has a Masters Degree in Arts from the University of Dar es Salaam and a Post Graduate Diploma in Management from the Graduate School of Business at the University of Cape Town.

  She is a member of the Society for Human Resource Management (SHRM) as well as an affiliate member of the Chartered Institute of Personnel and Development (CIPD).

  Janet was a Board member of the Association of Tanzanian Employers (ATE) for the past six years and is currently a Board Member of the Tanzanian Wage Board. 

  0 0

  Dk. Bitrina Dyamett, akifungua mkutano uliowakutanisha wanasayansi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam, leo
  Dk. Bitrina Dyamett akimkaribisha Ktibu Mkuu wa Wiazara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Frorence Turuka, katika mkutano wa STIPRO.

  NCHI wa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetakiwa kuwa na ushirikiano mathubuti na Taasisi zinojihusisha na tafiti mbalimbali za kisayansi kama njia ya kuwasaidia wananchi wa nchi zao ili kujua matokeo ya tafiti zilizofanywa.

  Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Taasisi utafiti ya STIPRO, Britrina Diyamett kwenye mkutano wa wadau wa tafiti za kisayansi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.

  Alisema sehemu kubwa ya wananchi katika Jumuiya hii wamekuwa hawapati matokeo ya tafiti kwa wakati na hivyo kushindwa kuyatekeleza katika majukumu yao ya kimaendeleo.

  “kuna mambo mengi ya kuyaangalia , kwanza tunaanza na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zishirikiane kwa kiasi kikubwa ili taarifa zetu za tafiti ziweze kuwafikia wananchi kwa haraka,” alisema Diyamett.

  Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dk Florens Turuka, alipongeza mpango wa mpadirishano wa sera za kitafiti ambao umewekwa na Taasisi hizo.

  “ Hali hii inaonyesha kwa sasa watafiti wanaongezeka na hii itatusaidia kujidhatiti kutafuta majibu na njia za kufanya kutatua matatizo katika jamii,” alisema Dk. Turuka.

  0 0

  Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa kupita eneo hilo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara,Masasi,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Liwale,Nanyumbu na Tunduru kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii Kufuatia hali hiyo.

   baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa salama ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.Picha na Mdau Abdulaziz Lindi.


  0 0


  Rais Mpya wa Kenya,Mh. Uhuru Kenyatta akiwahutubia wananchi wake.


older | 1 | .... | 95 | 96 | (Page 97) | 98 | 99 | .... | 3286 | newer