Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 965 | 966 | (Page 967) | 968 | 969 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia 'Wazee wa Ngwasuma' wakitoa burudani kwa mashabiki wao siku ya uzinduzi wa Hotel ya Mfikemo Sae jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.Picha Elvis Kimambo Jamiimojablog
  Mashabiki na wadau wa Fm Academia wakiserebuka katika onyesho hilo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  RAIS Jakaya Kikwete amesema madai kuwa elimu inayotolewa Tanzania ni duni ni potofu kwani wahitimu wake wanakubalika duniani.

  Akihutubia Mkutano Mkuu wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema badala yake, tatizo liko kwenye kuwaandaa wahitimu kukidhi matakwa ya soko la ajira la ndani na la kimataifa.

  “Elimu yetu ni bora na inakubalika popote duniani...wahitimu wanaweza kufanya kazi katika nchi yoyote, kinachotakiwa ni kuwapatia ujuzi wa kutosha kukidhi matakwa ya soko la ajira,” Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo aliwaambia wadau wa mkutano huo toka sekta ya umma na binafasi ambao hutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo.

  Takwimu zinaonyesha kwamba vijana wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka nchini ni kati ya 800,000 hadi 1,000,000 na wanapigania nafasi za ajira zisizozidi 60,000 katika sekta ya umma na nafasi takribani 300,000 katika sekta binafsi.

  Dkt. Kikwete alisema serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji na kuomba mchango wa kila mdau kutumia fursa na raslimali zilizopo nchini kuzalisha mali na kuongeza ajira katika sekta ya umma na sekta binafsi.

  Rais aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kila anayestahili kulipa kodi afanye hivyo na kusisitiza kuwa “serikali haiko tayari kuona watu wanakwepa kulipa kodi.”

  Akitoa mfano alisema kama wadau wa sekta ya usafiri wa ndege wanaona kodi wanazotozwa ni kubwa ni vyema wakakaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakubaliane lakini siyo kuchukua uamuzi wa kutolipa kodi.

  Kuhusiana na mapambano ya rushwa alisema Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB) ijidhatiti vya kutosha kwa weledi na kwa mujibu wa sheria ili uwepo ushahidi wa kuiridhisha mahakama kumtia hatiani mshitakiwa.

  “Mnapokwenda mahakamani mkashidwa mara kwa mara, zoezi hili la kupambana na kuzuia rushwa halitofanikiwa,” alieleza.

  Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mali Asili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru alisema ingawa utalii unazidi kuimarika na kuchangia pato la taifa,  unakumbwa na tatizo la ujangili unaoangamiza tembo na faru.

  Katika kukabiliana na tatizo hilo, alisema vifaa na askari vitaongezwa na kuwa patajengwa minara ya kuimarisha ulinzi katika mbuga za Serengeti na Ruaha.

  Aliwataka wananchi kutochunga mifugo katika mbuga hizo kwani serikali haitoruhusu vurugu na uharibifu unaofanywa katika mbuga za wanyama uendelee.

  0 0

   Wananchi wakiangalia ajali ya daladala lenye namba za usajili T 456 BVT lililoacha njia kutokana na mwendokasi na kuparamia genge na bajaj yenye namba MC 611 ADC, maeneo ya Kitunda relini barabara ya Mombasa kwenda Moshi Baa Dar es Salaam leo asubuhi. Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa daladala kukimbilia abiria. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
   wananchi wakiangalia ajali hiyo.
   Daladala hilo likiwa ndani ya genge baada ya kuacha njia.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akiwaonesha ilani ya chama hicho na kuainisha mipango mizuri ambayo imewekwa katika kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali.Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Meya wa Ilala Jerry Slaa ambaye pia ni mgombea ubunge CCM Jimbo la Ukonga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam jana.

   MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema Serikali watakayoiunda endapo watapewa ridhaa ya kuongoza nchi watahakikisha wanadhibiti wizi wa dawa kwenye hospitali za Serikali ambazo zimekuwa zikiuziwa wananchi katika maduka ya dawa mitaani. Bi. Suluhu katoa kauli hiyo jana alipokuwa akihutubia katika mikutano ya anuai ya hadhara Jimbo la Ilala kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo amebainisha kuwa dawa zote zitakuwa zinaingizwa katika mtandao maalum na kuzifuatilia na endapo zitatumika nje ya utaratibu itabainika na hatua kuchukuliwa. 

  Alisema mtandao huo utafanikiwa kukabiliana na kero ya ukosefu wa dawa katika hospitali za serikali kwani dawa hizo zimekuwa zikiibwa kwenye hospitali za Serikali na kuuzwa nje katika maduka ya dawa binafsi na hospitali binafsi. "...Tunaamini mfumo huu utatusaidia kukabiliana na wizi wa dawa na rushwa hospitalini...unakuta daktari anakuandikia dawa alafu anakuelekeza duka la kwenda kununua sasa unajiuliza huyu mtu kajuaje kama sio yeye kapeleka pale," alisema Bi. Suluhu.
   
   Pamoja na hayo mgombea huyo mwenza, aliwashauri wananchi kuukubali utaratibu wa kutumia mfumo wa bima ya afya kwa matibabu ambao umekuwa ukimlazimu mwananchi kuchangia kiasi kidogo cha fedha na kutibiwa mwaka mzima bure katika hospitali zote zinazotumia utaratibu huo, kwani alidai utawasaidia wengi. "...Unajua ugonjwa unampata mtu ghafla na muda wowote haijalishi una fedha za kujitibu au la, lakini kama unabima ya afya waweza kutibiwa muda wowote hata kama hauna fedha wakati huo," alisisitiza Bi. Suluhu.

   Aidha, Bi. Suluhu alisema serikali watakayoiunda itajitahidi kupima maeneo mengi ya ardhi na kuyatoa kwa wananchi ili kukabiliana na migogoro ya ardhi.

   Alisema Serikali yao pia imekamilisha utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni ambao wanadai fidia na itawalipa wananchi hao kwa thamani ya sasa ya ardhi kwani 2004 hadi sasa ni muda mrefu na ardhi imepanda thamani. 

  Akizungumzia kero ya foleni, alisema ili kumaliza kero hiyo na msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, Serikali imepanga kujenga miji mipya maalum na ya kisasa pembezoni wa jiji hili na kwa kuanzia itajenga mjini huo eneo la Kibaha ili shughuli nyingine ziwe zikifanyika katika mji huo na Dar es Salaam kupunguza msongamano, zoezi litakaloenda sambamba na ujenzi wa barabara ndogondogo za mitaani ambao utapunguza msongamano na foleni katika barabara kubwa. 

   Aidha Bi. Suluhu alisema zitajengwa barabara za juu katika makutano ya barabara ikiwa pamoja na kuzijenga barabara ndogondogo zikiwemo za Mbezi Morogoro-Malamba Mawili-Tangi Bovu-Kimara Baruti-Goba na nyinginezo ili kupunguza msongamano katika barabara kubwa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com


  0 0

   Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
   Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
   Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume  ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiongea na  Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza.


  0 0

  Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Nature leo alikua akiongea na Waandishi wa Habari juu ya Ufanyaji kazi wake katika kipindi hiki cha kampeni Ambapo aliongozana na Mgombea Ubunge jimbo la Mbagala ambaye ni rafiki mkubwa na jirani wa msanii huyo Ndg Issa Mangungu. Juma nature kwa sasa amerudi kufanya kampeni na chama cha mapinduzi CCM na ameamua kuelezea nia ya kurudi CCM baada ya mashabiki kumuona katika Majukwaa mengine ya vyama vya kisiasa. 
   Nature amesema kuwa mziki ambao anaufanya ni Biashara lakini pia anafanya kwa ajili ya Jamii yake ambayo inamzuuka na pia anaangalia sehem ambayo anakubalika ivyo akiitwa sehem yeyote kufanya kazi anaenda anafanya kazi maana mziki ndio ajira yake. Sikilize hapa Juma Nature akiongea.......

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Dr. Binadamu Hellen Bisimba   akizungumza na wananchi waliofika kwenye uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya Azaki Tanzania  katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyam leo Jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Tume ya Haki za binadamu na utawara bora,Bahame Nyanduga akizindua ilani ya uchaguzi ya Azaki Tanzania katika ukumbi wa Milleniamu Towers Kijitonyama leo Jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Hellen Bisimba na wakulia Mratibu wa Mtandao wa watetea wa haki za Binadamu Onesmo Ngurumwa.
  (Picha na Emmanuel Massaka)

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
   VYAMA vya Siasa vimeaswa kuachana na lugha ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani na badala yake vimetakiwa kunadi sera zao kwa wananchi waweze kupewa ridhaa inayotokana na kura.

  Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Tume ya Haki ya binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga wakati wa uzinduzi wa ilani ya Asasi za Kiraia iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Nyanduga amesema wakati wa sasa ni kunadi sera kwa vyama vya siasa na sio kutumia lugha ambazo haziendani na Demokrasia wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

  Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  alitaja baadhi ya lugha zinazotumika ni pamoja na Tutashinda saa Nne Asubuhi, Goli la Mkono zote ni lugha ambazo hazitakiwi katika kuelekea katika uchaguzi mkuu.

  Amesema kuwa vyombo vya dola ikiwemo jeshi la Polisi kuhakikisha linasimamia wananchi katika mchakato wa kuelekea katika uchaguzi pasipo kutumia nguvu ili wananchi waweze kusikiliza sera za vyama vyote kupitia wagombea wake.

  Hata hivyo amesema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zilizosaini kuwepo kwa Mahakama ya ICC hivyo wale wote ambao watashiriki kuvunja amani wakati wa uchaguzi mkuu watahusika na mahakama hiyo kutokana na kufanya uchochezi na kuvuruga amani.

  Aidha amesema kuwa wananchi nao wametakiwa kuvumiliana katika kipindi hiki pasipo kudharau chama cha mwenzake, uchanaji wa mabango  ya wagombea kwani hiyo sio demokrasia.

  0 0

   Meneja Mshauri wa Zantel, Charles Jutta akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya usafi kwa  mkoa wa Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Magalula Said Magalula.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdula Lutavi akiteta jambo na Meneja Mshauri wa Zantel, Charles Jutta(Kushoto) mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya usafi baina ya Zantel na jiji la Tanga anayeshudia katikati ni meneja mauzo wa Zantel Tanga. 
  Mkuu wa mkoa wa Tanga Magalula Said Magalula (kulia) akishiriki zoezi la usafi katika eneo la Mwembe Mawazo jijini Tanga muda mfupi baada ya kupokea vifaa vya kufanyia usafi kutoka kampuni ya Zantel kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mheshimiwa Abdula Lutavi.

  TANGA:Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imetoa msaada wa vifaa vya usafi kwa halmashauri ya jiji la Tanga venye lengo la kusaidia shughuli za usafi katika jiji hilo.


  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa Zantel, Bwana Charles Jutta alisema msaada huo ni sehemu ya juhudi za kampuni yake kuziunga mkono jitihada zinazofanywa na halmashauri ya jiji la Tanga katika kutunza na kuweka mazingira safi na salama kwa wakazi wake.


  ‘Kampuni ya Zantel inaamini katika kushirikiana na serikali ili kuhakikisha jamii yetu inaishi katika mazingira safi na salama, na vifaa hivi tulivyotoa leo vitasaidia swala la usafi jijini hapa kama sehemu ya wajibu wetu kwa jamii’ alisema Jutta.  Kusoma zaidi bofya HAPA

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
  Iddi akifungua Pazia kuashirika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
  Nyumba ya Kuishi Askari Polisi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
  Kaskazini Pemba.
   Balozi Seif akikagua moja ya vyumba Kumi vilivyomo
  ndani ya jengo linalojengwa kwa ajili ya makaazi ya Askari Polisi
  Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
   Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
  Kaskazini Pemba wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani
  ambapo wa kwanza kutoka kulia ni OCD Wilaya ya Micheweni Kamanda HajiMiraji na anayefuatia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba RPCMoh’d  Shehani.


  0 0

   Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Elias Kasikila, (kushoto), akiagana na baadhi ya vijana wanaokwenda kuhudhuria mafunzo ya ufundi chini ya mpango wa IMTT unafadhiliwa na mgodi huo, wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye eneo la mgodi, huko Msalala mmoani Shinyanga. Mgodi huo umetuamia kiasi cha zaidi ya  nusu bilioni kila mwaka kufadhili mpango huo

  Na K-VIS MEDIA
  MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini ya Acacia, umetumia kiasi cha zaidi ya shilingi nusu bilioni kila mwaka, kufadhili mafunzo ya ufundi kwa vijana, chini ya mpango wa IMTT.

  Mpango wa kufadhili mafunzo ya IMTT, (Integrated Mining Technical Training), ulianzishwa mnamo mwaka 2009, ambapo mgodi huo hutoa fedha kufadhili elimu hiyo kwa vijana wenye elimu ya kidato cha nne ambao walisoma kwenye shule zilizoko vijiji 14 vinavyozunguka mgodi huo na kushindwa kuendelea na kidato cha sita kwa sababu mbalimbali lakini wawe na umri usioozidi miaka 25.

  Akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga vijana 20 kutoka vijiji hivyo kwenye mgodi huo, mwishoni mwa wiki ambao wameenda kuanza mafunzo hayo yanayochukua muda wa miaka kati ya mitatu na miwili kwenye chuo cha VETA-Moshi, Menenja Ufanisi (OE),wa BGML, Elias Kasikila, alisema, ufadhili huo ni utekelezaji wa sera ya mgodi kushirikiana na wenyeji wao, (wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi), katika kujenga mahusiano mema.

  Akielezea utaratibu wa kuwapata vijana hao, Kasikila alisema, waombaji hupeleka maombi yao kwenye ofisi za serikali za vijijina kisha maombi hayo kukabidhiwa kwa uongozi wa mgodi ambao huyaachuja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

  “Sharti muombaji awe amefaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati, lakini kupitia kitengo chetu cha usalama, vijana hao huchunguzwa tabia zao huko walikotoka, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya kiafya na wanaokidhi vigezo hivyo huchaguliwa.” Alifafanua

  Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na ufundi umeme kwa miaka mitatu, fitting na uchomeleaji vyuma, kwa miaka miwili, Diesel mechanic and Instrument, kwa miaka mitatu.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0
  0 0

  Mwigulu Nchemba na Mwakalebela wakiwa kwenye Gari ya wazi wakielekea Uwanja wa Mwembetogwa hapa Iringa Mjini tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge.

  Mwigulu Nchemba akiwambia Wananchi wa Iringa kuwa mambo yapo POA kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.Hisia za Wananchi kwa chama chao,Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba (katikati),Mbunge mtarajiwa Mwakalebela(kushoto) na Kampeni Meneja wa Mwakalebela Ndg.Mahiga(Kulia) wakiwaaga wananchi wa Iringa mjini na kuwashukuru kwa Mafuriko waliyoyaleta Uwanja wa Mwembetogwa.
  Picha na Sanga Festo Jr.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
  Rais Jakaya Kikwete (Pichani)ameridhishwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua iliyofikiwa ya kuweza kusajili jina la biashara kwa njia ya mtandao na kupata cheti ndani ya saa moja.

  “Hatua hii ya BRELA ni nzuri, wanastahili pongezi na wengine waige,” alisema Dkt. Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  Pongezi za Dkt. Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi.
   
  Akithibitisha maendeleo hayo mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka VIBINDO alisema hivi karibuni aliweza kufanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja tu.
   
  BRELA imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka huu.
   
  Mteja wa BRELA anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza, anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya kuzaliwa.
   
  Mteja anatakiwa kuingia katika mtandao wa BRELA ambao ni www.brela.go.tz kisha ataingiza jina na baada ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.
   
  Baada ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia mchakato huo wa kimtandao.

  0 0

  Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, watu kupitia fani na kazi mbalimbali wamekuwa wakijaribu kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya maamuzi yatakayolipeleka taifa letu mbele.
  Innocent Galinoma(Pichani juu)ni msanii mkongwe wa Reggae anayefanya kazi zake nchini Tanzania.

  Naye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya uchaguzi huu mkuu. Akisisitiza kuhusu kusikiliza na kuwahoji wagombea ili kujua fika wanalotaka kutufanyia katika kutatua kero zetu
  Karibu usikilize kibao....UCHAGUZI

  0 0  0 0

   Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
   Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara  katika kambi hiyo.
  Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
  (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

  0 0

  Wahitimu wa darasa la saba Fredrick Robert (kulia) na Rania Hante kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakisoma risala yao kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo. Waliopo meza kuu ni Wakurugenzi wa shule hiyo, kwanza kulia ni Mkurugenzi Imelda Philip akifuatiwa na Machage Kisyeri. Na wa kwanza kushoto ni Julius Rutabanja.
  Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo cha M-Pesa wa Vodacom Tanzania, George Kagaruki akitoa mafunzo kwa Mawakala wa M-Pesa wa kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wakati wa Semina iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma  za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja wa kampuni hiyo kwa kutumia huduma ya M-Pawa.
   Wakufunzi wa Semina ya Mawakala wa Vodacom Tanzania, kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye Semina iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja katika huduma ya M-Pawa.
   Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam, akifafanua jambo kwa Mawakala wa kampuni hiyo waliohudhuria katika Semina  iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja katika huduma ya M-Pawa.

older | 1 | .... | 965 | 966 | (Page 967) | 968 | 969 | .... | 3353 | newer