Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

SERIKALI IJAYO YAOMBWA KUREKEBISHA SHERIA KULINDA MAKUNDI MAALUM


MAMA SAMIA AITEKA AUNGURUMA JIMBO LA UKONGA JIONI YA LEO

0
0
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi atika mutano wa kampeni uliofanyika leo, katika eneo la kwa Warioba, jimbo la Ukonga, Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo.
Wasanii waliopo katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao mpigie kura Dk. Magufuli, wakiwa kwenye mkutano huo

MSANII WA KENYA SARA K KUSHIRIKI TAMASHA LA KUOMBE AMANI HAPA NCHINI

0
0
 Mwenyekiti wa kamati  Maandalizi ya Tamasha la Amani, Alex Msama amesema  washiriki wa tamasha hilo ni waimbaji mbalimbali wa injili kama SolomonMkubwa, Rose Mhando, Upendo Nkone, Boniface Mwaitege, kwaya ya  KKT ya  Dar es Salaam pamoja na kwaya mojawapo kutoka Iringa, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Kulia niKatibu mkuu wa makanisa ya Kipendekote Askofu, David Mwasota akizungumza kuhusiana na tamasha hilo kuwa wananchi wakitokeze kwa wingi bila kujali itikadi zai za dini wala chama ili kuombea uchaguzi mkuu uwe wa amani utakaofanyika Oktoba 4 mwaka huu.Mwenyekiti wa kamati  Maandalizi ya Tamasha la Amani, Alex Msama
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.

UZINDUZI WA KAVASHA CLUB NA KITABU CHA JIFUNZE LINGALA MTUNZI TCHIMANGA ASSOSSA

0
0
Uzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza. Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani  kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.
Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA, GAUDENSIA KABAKA, AZINDUA BODI YA WADHAMINI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF

0
0
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, (kulia), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, wakati wakichukua nafasi zao kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2015. Waziri Kabaka alizindua bodi hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti wake,   Bw. Emmanuel Humba


 Waziri Kabaka akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAZINDULIWA LEO DAR ES SALAAM

0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiangalia kibao cha taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyozinduliwa leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiogea na mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo
 Muuguzi akiwa na mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo
 Picha ya pamoja baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid  kuizindua  Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam  
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid  akizindua Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam  
 Taasisi ya Moyo ambayo itajulikana kwa jina la  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( The Jakaya  Kikwete Cardiac Institute ) imefunguliwa  rasmi leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salam.
Taasisi hiyo itatoa mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya Upasuaji wa Moyo , dawa ya usingizi na Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili( MUHAS).
            Akizindua Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid  amesema taasisi hiyo  imeleta ahueni  kwa wagonjwa  wa moyo nchini ambapo kati ya Januari hadi Agosti mwaka huu imehudumia wagonjwa wa nje 14, 257 ,wagonjwa waliolazwa ni 912 na imefanya upasuaji kwa wagonjwa 148.
            Kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji ,wagonjwa watano tu ndio waliofariki Dunia ambao ni Asilimia 3. 4 , kiwango ambacho ni kidogo kuliko wastani uliokisiwa na wataalam wa asilimia 13.
            Akifafanua amesema huduma zilizotolewa na taasisi hiyo  zimeokoa kiasi cha Shilingi 1, 915,440,000  iwapo wagonjwa hao  wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi.

PPF, NHIF WAFANYA BONANZA LA PAMOJA KUONYESHA USHIRIKIANO

0
0

 Kipa wa timu ya soka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akichupa kuzuia mpira wa penati bila mafanikio wakati timu hiyo ilipomenyana na ile ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wakati wa bonanza la pamoja la taasisi hizo mbili lililoandaliwa na PPF na kufanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo Septemba 5, 2015. Katika bonanza hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi wa michezo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia, soka na mpira wa wavu. (Volleyball)

NA K-VIS MEDIA

MFUKO wa Pensheni wa PPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wamefanya bonanza la michezo kwenye uwanja wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Septemba 5, 2015 ili kuonyesha ushirikiano.



Akizungumza kwenye bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, amesema, bonanza hilo limewakutanisha pamoja wafanyakazi wa taasisi hizo mbili za umma, ili kuonyesha mshikamano na ushirikiano sio tu katika Nyanja ya kazi bali pia katika Nyanja ya michezo na burudani.

Bonanza hilo lilishirikisha michezo ya kuvuta kamba, soka, mpira wa wafu (Volleyball), mbio za magunia, na kufukuza kuku, ambapo washindi walijinyakulia zawadi mbalimbali. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


 Mazoezi ya viongo kwa wote
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MTANDAO WA WANAWAKE WAHITIMISHA TAMASHA LA UZINDUZI WA ILANI YA UCHAGUZI LEO JIJINI DAR

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na wananchi juu ya kutambua michango ya kimaendeleo inayofanywa na wanawake kwa kuwawekea kumbukumbu kama ilivyo kwa wanaume, ili kuleta uwiano wa kijinsia leo Jiji Dar es Salaam katika kilele cha tamasha la Jinsia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akiteta jambo na Ruth Meena.
 Wanawake wakitaja baadhi ya matatizo ambayo yanayowakabili ni pamaoja na suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama maeneo mbalimbali nchini.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

KATIBU MKUU OFISI YA RAISI ZANZIBAR, MHE. SALUM MAULID AFUNGA MKUTANO WA TANZANIA DIASPORA BUSINESS CONVENTION 2015 NCHINI UINGEREZA

0
0
Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula (kati), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, Uingereza, Peter Kallaghe (pili kushoto), Mheshimiwa Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Zanzibar, Bwana Salum Maulid (kushoto), Mwenyekiti wa Watanzania waishio Birmingham, Prince Katega (pili kulia), dada Gradys Katega (MC) wakiwa pamoja na Kamati ya Mkutano wa Tanzania Diaspora Business Convention 2015.
Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula (kati), Mheshimiwa Salum Maulid ,Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Zanzibar (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe na mama Joyce Kallaghe, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Watanzania, unaoendelea hivi sasa Birmingham, Uingereza.

Mheshimiwa Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula akimpongeza mwanahabari masahuhuri Bwana Ayoub Mzee mara baada ya kufungua rasmi huduma ya Television (Mobile application - Apps). Bwana Ayoub ni mwakilishi wa AITV Application hapa nchini Uingereza.

DK.SHEIN AREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi fedha tasilim Shilingi za Kitanzania Millioni mbili Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe,Jecha Salim Jecha wakati  aliporejesha fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar   katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Wananchi waliofika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja baada ya kurejesha  fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar   katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Wananchi waliofika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja baada ya kurejesha  fomu  za kugombea Urais  wa Zanzibar   katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi iliyopo Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]

Wanawake wanateseka sana duniani - Spika Anne Makinda

0
0

Picha: Joseph Msami
Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema wanawake bado wanateseka takribani kote duniani, wengine wakiambulia vipigo na kadhia mbalimbali.
Kandoni mwa mkutano wa Nne wa maspika wa mabunge duniani jijini New York spika Makinda amemueleza Joseph Msami wa idhaa hii, spika huyo wa kwanza mwanamke nchini Tanzania anasema lazima wanaume na jamii kwa ujumla wamkomboe mwanamke. Kwanza anaanza kueleza maudhui ya mkutano.
KUSIKILIZA BOFYA HAPA

A+E NETWORKS(R) KURUSHA DOKUMENTARI YA OJ SIMPSON

0
0
A&E_0005
Mkuu wa vipindi channel ya A & E Networks, Racheal Job akizungumza na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice nchini Mauritius. Katikati ni Mkurugenzi wa Kanda channel ya A & E Networks, Anthea Petersen na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins.
A&E_0038
Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins akifafanua jambo kwenye jukwaa lililowakutanisha waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika nchini Mauritius.
A&E_0045
Ebenezer Donkoh kutoka YFM Ghana akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa habari ulionadaliwa na MultiChoice Africa.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

REGGAE TIME YA PRIDE FM......JUSTIN KALIKAWE

0
0

Na Mubelwa Bandio
Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.
Kwangu ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu,ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).

Na nakumbuka tulipanga kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji.
 Ni katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi. 
Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.

Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. 

Huo ndio ukawa mwisho wa ushiriki wake katika mkakati huo.
Lakini wakati anafariki, nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.
Lakini….
Justin Kalikawe ni nani?

SITOKUWA TAYARI KUTOA MATUMAINI HEWA KWA WANANCHI AMBAYO HAYATEKELEZEKI-DKT MAGUFULI

0
0

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.

  Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero,wakimshangilia kwa shangwe Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la ilombero Ndugu Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha baadhi ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais waliomtangulia,amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.

Akizungumza kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk.Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi waliomtangulia kuongoza nchi.

Alisema sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.

“Iwapo nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo mzee Ali Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete,Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.

“Huu ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua msimamo wangu na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena kwangu mimi ni kazi tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.


Alisema kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.

Dk.Magufuli ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara Mkoa wa Morogoro.

 Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  ukikatiza kwenye dara la muda la Mto Kilombero,ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  akikagua daraja la Mto kilombero ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  akipata maelezo mafupi kuhusia na maendeleo ya ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kilombero,litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa kiasi kikibwa.

 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya kumaliza kuhutubia  jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni ya leo.


HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA MJINI IFAKARA JIONI YA LEO


WANANCHI WAFUNGA BARABARA KIJIJI CHA LUPIRO-IFAKARA WAKITAKA KUMUONA MAGUFULI

MICHUZI BLOG EXCLUSIVE: JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA AFANYIWA SHEREHE YA KUSTUKIZWA YA MIAKA 75 YA KUZALIWA KWAKE NA WATOTO NA WAJUKUU WAKE

0
0
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ijumaa usiku alijikuta anapigwa  butwaa baada ya kurudi nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam na kukuta bango hilo mbele yake ambapo  watoto na wajukuu wake walikuwa wamemuandalia sherehe ya kuzaliwa kwake ya miaka 75 (suprise Birthday Party) bila ya yeye mwenyewe kujua
 Jaji Warioba na mkewe walijikuta wanashangaa zaidi kukuta kumbe watoto na wajukuu sio tu wameandaa Birthday party yake bali pia sala maalumu ya kushukuru kwa kufikisha miaka 75 akiwa buheri wa afya
 Jaji Warioba akiwa na marafiki wake wa karibu walioaloikwa kwenye hafla hiyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Paul Rupia akifuatiwa na mama Janeth Kahama na mumewe Sir George Kahama
 Jaji Warioba akikata keki akiwa amezungukwa na wajukuu 
 Jaji Warioba akilishwa keki na mkewe
 Jaji Warioba akimlisha keki mkewe
 Jaji Warioba akiongea katika hafla hiyo ya kustukiza
 Jaji Warioba akiendelea kuongea

 Jaji Warioba na mkewe na wajukuu wao
 Jaji Warioba na mkewe wakiwa na watoto na wenza wa watoto wao

MAMBO 10 MUHIMU ILI SHERIA YA MAKOSA YA KIMTANDAO YASIKUKAMATE.

0
0
Sheria ya mitandao iliyoaanza kutumika rasmi tarehe 1 septemba 2015. 
 1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao

3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)

4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii

5. Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea ) itakugharimu

6. Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu

7. Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu

8. Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu

9. Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini

10. Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia 'brand' ama jina la mtu itakugharimu

Hukumu
Ni kifungo cha miaka kadhaa gerezani ama faini ya fedha isiyopungua milioni 5 kulingana na kosa lililofanyika (au vyote!)

WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WAPATIWA MAFUNZO YA UREMBO NA MSHAURI WA KITAALAMU WA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA MARY KAY

0
0
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakichagua vipodozi mbalimbali vya kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo (Mary Kay) wakati wa mafunzo mafupi  ya jinsi ya kujiremba kwa kutumia vipodozi hivyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya kampuni hiyo mahususi kwa wafanyakazi wake. 
Jacqueline Macha ambaye ni mshauri wa kitaalamu wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya Mary Kay akiwaonesha wafanyakazi wa Vodacom Tanzania moja ya picha iliyorembwa kwa kutumia vipodozi vya kampuni hiyo wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi hivyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania  mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam. 
   Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Vodacom Tanzania,Joan Makwai (kulia) akimsikiliza kwa makini Jacqueline Macha ambaye ni mshauri wa kitaalamu  wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya Mary Kay akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati wa mafunzo mafupi  ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo .Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya kampuni hiyo mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyaka wa Vodacom Tanzania walioshiriki katika mafunzo mafupi  ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo  ya Mary Kay,wakimsikiliza Mshauri wa kitaalamu  wa kampuni hiyo Jacqueline Macha,wakati wa mafunzo  mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania,mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Vipodozi vya urembo kwa wanawake vya kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo  ya Mary Kay.
Mshauri wa kitaalamu  wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya (Mary Kay) Jacqueline Macha(kulia)akimremba Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Vodacom Tanzania,Joan Makwai,wakati wa mafunzo  mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania,mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Edna Mtema (kushoto) akirembwa na Mshauri wa kitaalamu  wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya (Mary Kay) Jacqueline Macha kwa kutumia vipodozi vya kampuni hiyo wakati wa mafunzo  mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania,mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.

VIONGOZI WA TAASISI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI MTAALA WA KUFUNDISHIA ‘UJASIRIAMALI USIOATHIRI MAZINGIRA’

0
0
Viongozi wa taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini Bagamoyo kujadili na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana namna ya kufanya ujasiliamali usioathiri mazingira “Green Entrepreneurship”.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za vijana kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji Tanzania walipata fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati mbadala isiyoathiri mazingira.
Shukuru Meena, Mratibu wa miradi ya nishati kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO).
 Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live


Latest Images