Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 963 | 964 | (Page 965) | 966 | 967 | .... | 3284 | newer

  0 0  Copyright © 2015 Jerry Silaa, All rights reserved.
  You are receiving this email as we have been communicating directly with me
  Our mailing address is:
  Jerry Silaa
  Ukonga Ilala
  Dar Es Salaam
  Tanzania

  Add us to your address book
  Email Marketing Powered by MailChimp


  0 0

  East African Community Secretariat, Kampala, Uganda, 3rd September, 2015: The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr Richard Sezibera, on Thursday paid a working visit to Roofings Group Uganda at its 2nd plant located in Namanve, Uganda's upcoming Industrial Area on the outskirts of the capital, Kampala.

  The Secretary General was accompanied by Hon. Dr. James Shinyabulo Mutende, Uganda's Minister of State for Industry; Mr. Dennis Karera, the Chair of the East African Business Council (EABC) and the Ag. CEO, Ms. Lilian Awinja; Mr. Hussein Omar, the EABC Uganda Chapter Chair; Dr. Samuel M. Nyantahe, Chairman of Confederation of Tanzania Industries; Amb. Jean Rigi, Burundi's Permanent Secretary for EAC Affairs, and; Commissioner Rona Sserwada from Uganda's Ministry of EAC Affairs.

  Welcoming the Secretary General to the Plant, the Chairman and Managing Director of the Roofings Group, Mr. Sikander Lalani, said it was gratifying that Amb. Sezibera's visit to the plant came immediately after the 1
  st East African Manufacturing Business Summit held from 1st to 2nd September, 2015 in the Ugandan capital.

  Lalani said the deliberations at the Summit were all geared towards job creation for the youth, increasing value addition, quality assurance, enhancing tax revenues, fair trade and. most importantly, boosting the region's economic standing in the world.

  Lalani told the Secretary General of various issues that must be addressed at the regional level in order to boost the growth of the steel sector, namely: the need to increase the EAC Common External Tariff (CET) on galvanized wire to 25% in the region, and; the Re-bars to have either a fixed import tax rate based on volume at $250 EAC CET per tonne or based on value at 25% CET, whichever is higher.

  The CEO also proposed removing cold rolled coils, galvanized coils and pre-painted coils removed from the duty remission schemes of Rwanda and Burundi. He also requested the region to put in place a robust quality assurance system by way of adopting regional standards in the steel sector as well as putting in place a level playing field in tax administration.

  He further urged Partner States' governments to prioritize and enhance local/regional content for infrastructural and donor funded projects as a way of promoting the Buy East African, Build East Africa campaign.

  Lalani disclosed that the Group was employing people from the region without any discrimination for as long as they have the required skills and ability to deliver.

  He also assured the Secretary General that the firm was keen on investing in the entire region depending on the enabling environment in terms of import duty policies, level of playing field and availability of markets.

  Minister of State for Industry Dr. Mutende assured the Secretary General and investors in the region that Uganda Government was working to address all the issues impacting on her business environment including a reduction in energy costs.  

  EABC Chair Mr. Karera called for an urgent meeting of steel producers and stakeholders before the end of September 2015 to address the issues impacting on business in the sector in the region, adding that a regional code of conduct was being developed and will be considered for adoption at the November EAC Heads of State Summit.

  In his remarks, Amb. Dr. Sezibera congratulated Mr. Lalani for the massive and quality investment in Uganda and the wider East African region, adding that some of the issues raised were already being addressed by the EAC Secretariat, the Council of Ministers and EABC.

  On the issue of standards, Amb. Sezibera urged the Roofings Group to work closely with the EABC and the EAC Secretariat to sort them out.


  0 0

   Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi (katikati), akiwaonesha wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi Umeme Nuru (Solar Power panels) ambazo hazina ubora zilizokamatwa zikiwa katika soko la Tanzania baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi hiyo, kufanya uchunguzi na kubaini kuwepo katika soko solar hizo. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe  na Ofisa Uhusiano, Roida Andusamile.
   Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew, akiwaonesha wanahabari Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko ambazo ni bora.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mkuu wa Maabara  ya Mikrobilojia wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini  (TFDA)Dk. Adelard Mtenga akitoa maelekezo juu ya kifaa  maalumu cha uchunguzi wa Vifaa tiba ikiwemo nyuzi za ushonaji pamoja na dawa za sindano  ambapo ni kifaa cha kwanza Katika  Nchi za Kusini ,Mashariki na Kati  Barani Afrika. leo Jiji Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  Sillo akikata utepe kufungua mtambo huo leo Jiji Dar es Salaam. Katiti ni mwakilishi mkazi wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Dk. Mohammed Ally Mohammed kuli ni Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly Hamblin.
   Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti  akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).


  0 0

  Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa (pichani) amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.
  Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Taifa Stars.
  “Tumefanya mazoezi kwa takribani siku kumi, vijana wako katika hali nzuri ya mchezo, uwezo waanaouonyesha mazoezini ni wa hali ya juu na unatupa matumaini ya kufanya vizuri” Alisema Mkwasa.
  Aidha Mkwasa amesema katika mpira hakuna kinachoshindakana, anatambua Nigeria ni timu kubwa Afrika, wameshatwaa ubingwa wa Afrika mara tatu, lakini mpira wa sasa lolote linaweza kutokea, hivyo sisi tumejiandaa vilivyo kufanya vizuri katika mchezo huo.
  Mwisho Mkwasa amesema wamejindaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuja kuwapa sapoti wachezaji uwanjani kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo, na kusema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi hata mmoja kuelekea kwa mechi hiyo.
  Mechi hiyo ya kesho jumamosi itachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) na kamisaaa wa mchezo ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda ambao wote tayari wameshawaili jijini Dar es salaam tangu jana jioni.

  0 0

  Na Hassan Hamad, OMKR 
  Waislamu mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo wamekusanyika katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kwa ajili ya kuomba dua ya kuiombea nchi amani na utulivu katika uchaguzi mkuu ujao. 
  Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar Sheikh Abdallah Talib, amesema mara nyingi amani ya Zanzibar hutoweka kutokana na sababu za kisiasa hasa inapofika wakati wa uchaguzi mkuu, hivyo juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa katika kuendeleza amani ya nchi wakati wote. 
  Amesema suala la kudumisha amani na utulivu ni mchakato unaopaswa kuendelezwa, ili kuinusuru nchi kuingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima, na kwamba kila mwananchi ana jukumu la kuhakikisha kuwa amani ya nchi haichezewi. 
  Naye Amir wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar Sheikh Ali Abdallah amesema dua hiyo ya kitaifa imefanyika nchi nzima katika viwanja mbali mbali Unguja na Pemba. 
  Dua hiyo iliyotanguliwa na sala ya Alasiri viwanjani hapo, imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini ya kiislamu, serikali na vyama vya siasa wakiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha ADC Mhe. Hamad Rashid Mohammed.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Bw. Hamad Rashid Mohamed, baada ya kushiriki kwenye dua ya kuiombea nchi amani wakati wa uchaguzi, iliyofanyika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, akisoma dua kabla ya kuanza kisomo maalum cha kuiombea nchi amani, katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga, baada ya dua hiyo. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma  kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, KIGOMA.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Kigoma Kusini, waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma  wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika leo Septemba 4, 2015.

  KUONA PICHA ZAIDI


  0 0

  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye hafla ya ufungaji wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
  Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Kongamano hilo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa neno la shukrani kwa Washiriki kabla ya kumkaribisha Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza kufunga Kongamano hilo.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kushoto) tayari kwa ufungaji rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria ambalo limefanyika Mkoani Morogoro kuanzia Septemba 02 - 04, 2015(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi iliyowasilishwa kwake na Mjumbe maalum Mhe.Eliseu Joachim Machava ambaye pia ni katibu Mkuu wa Chama Cha FRELIMO ikulu jijini Dar es Salaam leo.Baadaye viongozi hao wawili walifanya mazungumzo(picha na Freddy Maro)


  0 0

  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) imehitimisha rasmi Mradi wa Picture Afrika,tukio lililofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mjini Njombe
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dkt Dugushilu Mafunda akizungumza wakati wa kutamatisha Mradi wa Picyure Afrika.Pamoja naye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi(wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh Sara Dumba(wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Njombe Bw Noah Lameck

  Poverty and Information and Communication Technologies for Urban and Rural East African Coutries(PICTURE AFRICA) ni Mradi ulifadhiliwa na Shirika la la Kimataifa la Maendeleo ya Utafiti la nchini CANADA (IDRC) ukihusisha nchi Nne za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda.Nchini Tanzania Mradi huo ulihusisha wajasiriamali wa Njombe na Makambako.

  Akizungumza wakati wa kuhitimisha Mradi huo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Dugushilu Mafunda amesema kuwa mwaka 2008 COSTECH ilitekeleza Mradi wa Miaka Mitatu wa Kuondoa Umaskini kwa wajasiriamali wa mijini na vijijini kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(PICTURE AFRICA).
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa kuhitimisha Mradi wa Picture Africa.Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh Sara Dumba(wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dkt Dugushilu Mafunda(wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Njombe Bw Noah Lameck

  Dkt Mafunda anasema kuwa COSTECH yenye jukumu la kuratibu na kuendeleza Tafiti nchini iliamua kusaidia utafiti huo ili kuhawilisha teknolojia ya habari na mawasiliano kwa wajasiriamali wa Njombe na Makambako lakini pia kuweza kuishauri serikali umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara za wajasiriamali wadogo na wa kati maeneo ya Njombe na Makambako.
  Mtafiti Mkuu katika Mradi huo, Prof. Ophelia Mascarenhas anasema lengo la Mradi huo lilikuwa Kuondoa Umaskini mijini na vijijini kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Simu za Mikononi,Kompyuta na Mtandao wa Intaneti).

  Prof. Ophelia Mascarenhas anaongeza kuwa utafiti huo umeweza kuonyesha kwa kiwango kikubwa ushahidi wa kisayansi wa uhusiano kati ya utumiaji wa TEHAMA na ukuaji wa uchumi kwa maeneo ya Mijini na Vijijini.
  Picha ya Pamoja

  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi akihitimisha hafla ya kutamatisha Mradi huo,amesema Mradi huo umefanikiwa kuwapatia uwezo Wajasiriamali wa Njombe na Makambako kutokana na Sera nzuri za Serikali kutumia utafiti kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

  “Wajasiriamali wengi wa Njombe na Makambako walipatiwa Simu,Kompyuta na Mtandao wa Intaneti ili kurahisisha biashara zao.”Anaeleza Dkt Nchimbi na kuongeza TEHAMA imerahisisha kupunguza gharama ya usafiri na biashara kwa kuwa inaifanya Dunia kuwa ndogo kama kijiji.

  0 0
  0 0


  0 0


  0 0

   Mgombea Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kisarawe katika mkutano wa kampeni.

   Mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni. 

  Mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” 
   
   Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” wakati wa mkutano wa kampenzi uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kisarawe mkoa wa Pwani.
  Mgombea Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa wilayaya Bagamoyo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo.

  0 0

   The on-going construction of the main terminal building of Terminal III of Julius Nyerere International Airport in Dar es salaam to facilitate  3.5 million annual passengers – including parking lots, access roads, platforms and a taxiway. 
  The new terminal is designed (together with NACO, Netherlands Airport Consultants) for the anticipated growth of international air traffic, leaving the existing international Terminal 2 to cater for domestic flights. The design of the roof is inspired on the traditional sailing boats that can be found at the Dar es Salaam Coast.


  How it will look like after completion. For source and more CLICK HERE

  0 0


  0 0


  Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora) wametakiwa kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo ya biashara na uwekezaji katika nchi yao ili kuongeza pato la taifa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa kufungua kongamano la wafanyabiashara linalofanyika Birmingham, Uingereza tarehe 4 na 5 Septemba 2015. Aliwaasa washiriki wa kongamano hilo kulitumia kama jukwaa la kufanya majadiliano kwa madhumuni ya kubadilishana mawazo mapya ili kuibua fursa lukuki za uwekezaji nchini Tanzania. Aidha, aliwahimiza wanadiaspora kushirikiana na wajasiliamali wa nyumbani ili kuzitumia fursa hizo ipasavyo.

  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe
  Balozi Mulamula aliwahakikishia wnadiaspora waliohudhuria kongamano hilo, kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwashirikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni ili kuchangia maendeleo ya nchi yao. Hivyo, aliwahimiza kuja kuwekeza nyumbani kwa kuwa Serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwapatia ardhi kwa ajili ya kujenga makazi au kuwekeza.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
   

  0 0

   Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waiite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's yenye makao kule Ujerumani inatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Vechelde Festival nchini Ujerumani leo kuanzia saa 2:00 Usiku katika eneo la Bürgerzentrum Vechelde liliopo mtaa wa Hildesheimer Straße 5 mjini Vechelde jirani mji wa Braunschweig
  Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye sifa za kuwatia kiwewe washabiki wa muzikikatika maonyesho ya kimataifa kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi"made in Uswahilini ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kudumu kwa miaka 22 na kufanikiwa kukama soko la kutumbuiza katika maonyesho ya kimataifa. 
  Kwa sasa bendi hiyo inatamba na CD yake mpya ya"LA MGAMBO"yenye nyimbo mbili za kumuaga rais Jakaya Kikwete na CD hiyo utunzi wake Kiongozi wa bendi Ebrahim makunja aka Kamanda Ras Makunja imeshatua nchini Tanzania tayari kwa kutingisha anga katika vituo vya redio mbali mbali.
  wasikilize ffu-ughaibuni at www.reverbnation.com/ngomaafricaband


  0 0

  Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu katika viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam. Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba akizungumza katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu katika viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.


  0 0

   TAREHE 04 – 09 – 2015
   UKUMBI WA MIKUTANO WIZARA YA KAZI NA AJIRA

  WCF ni Taasisi ya Serikali  chini ya Wizara ya Kazi na Ajira iliyoundwa kwa Mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka 2008 ili kushughulikia masuala ya fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua au kufariki dunia wakiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Mwajiri.

  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeanzishwa kwa Madhumuni makuu yafuatayo;
  ·        Kutekeleza matakwa ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003 katika kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoikumba jamii ikiwamo ajali, magonjwa au vifo vinavyotokana na kazi;
  ·        Kutekeleza matakwa ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008;
  ·        Kulipa fidia stahiki pale mfanyakazi anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi;
  ·        Kuwasaidia wafanyakazi watakaoumia au kuugua kutokana na kazi ili waweze kurudi kazini au kushiriki katika shughuli nyingine zitakazowapatia kipato (ukarabati na ushauri nasaha);
  ·        Kuweka utaratibu utakaowezesha kuharakisha malipo ya fidia kwa wafanyakazi au wategemezi wao;
  ·        Kuweka utaratibu utakaowezesha Mfuko kupokea michango kutoka kwa waajiri na kufanya malipo;
  ·        Kukidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu fidia kwa wafanyakazi; na 
  ·        Kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa au vifo  katika maeneo ya kazi.older | 1 | .... | 963 | 964 | (Page 965) | 966 | 967 | .... | 3284 | newer