Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 962 | 963 | (Page 964) | 965 | 966 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015. 
  Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo
  Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo. 
  Waziri Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini. 
  Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0  0 0  0 0  0 0


  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa za Wabunge 55 na imeshatolea maamuzi rufaa 42  bado rufaa za Wabunge 13 ambazo vielelezo vyake vinasubiriwa kutoka kwenye Halmashauri husika. 
  Kulikuwa na Rufaa 16 za Wabunge waliokuwa wameenguliwa. Kati ya hizo Wabunge 13 wamerudishwa kuendelea na kampeni na rufaa 3 Tume ilikubaliana na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi hivyo hao hawatarudishwa kwenye orodha ya Wagombea. 
  Aidha, rufaa 24zimekataliwa na Tume ambapo maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yataendelea kubaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea. Pia kuna rufaa 2 ambazo Tume haijazijadili kwa kuwa hazikufuata utaratibu wa kuwasilisha Tume yaani kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo husika hivyo, maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi yatabaki kama yalivyo na wagombea wataendelea kugombea kama walivyoteuliwa. 


  0 0


  0 0

  Maisha ni Siasa - Supporting Actor

  MAISHA NI SIASA is a political film that tells a story of sacrifice, patriotism, loyalty, heroism, challenges and the role that bloggers and social media activists play in post-independent African politics and ongoing democratisation process. 
  But do you know who is who in 
  MAISHA NI SIASA This September?

  To know more about the movie please visit www.maishanisiasa.co.tz or our facebook pagewww.facebook.com/maishanisiasa or visit our page in You Tube (maisha ni siasa). 
  To know more about our past movie projects please visit www.onemonthdate.co.tz

  0 0


  0 0

  Na Aron Msigwa 
   Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuwatumia wahandisi wazalendo waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini. 
   Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Wahandisi kwa mwaka 2015 jana  jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Wahandisi wanao mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kwa kuifanya mipango iliyo kwenye karatasi kuwa katika uhalisia unaoonekana kwa macho. 
   Amesema fani ya uhandisi inagusa maisha ya watu moja kwa moja hasa sekta ya ujenzi wa miundombinu ya maji, umeme, majengo,miundombinu ya migodi, hospitali, barabara, viwanda na shughuli nyingine za kihandisi. 
   "Ni jambo lililowazi kuwa tuna kila sababu ya kujivunia maendeleo na mafanikio tuliyofikia, tuna kila sababu ya kuwatumia na kutoa kipaumbele kwa wahandisi wazalendo ,wahandisi wetu wanaweza" Amesisitiza Balozi Sefue. 
   Amewataka wahandisi hao kuendelea kuzingatia weledi pindi wanaposimamia utekelezaji wa miradi ya Serikali ili miradi hiyo iendane na thamani halisi ya fedha za wananchi kwa kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia miradi hiyo. 
   "Nawataka muendelee kuzingatia weledi,muwe waadilifu na mfanye kazi kwa bidii ili tufikie malengo ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025,mkumbuke kuwa kazi mnazofanya zinaonekana na watu wote, zikiwa mbaya au kuwa chini ya viwango watasema tu na mtaonekana hamzingatii taaluma wala viapo vyenu" Amesisitiza. 
   Amesema toka mwaka 2005 hadi 2015 Sekta ya Uhandisi nchini Tanzania imeweza kuwanufaisha watanzania kwa kuzalisha ajira 256,480 na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mzauri kwa kuboresha shule , vyuo na taasisi mbalimbali ili ziweze kuzalisha wahitimu bora wenye kuhimili ushindani soko. 
   Aidha, ameziagiza Halmashauri kote nchini kuhakikisha kuwa zinakuwa na wahandisi waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi kabla ya Juni 30, 2016 na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka msisitizo katika ubora wa wahandisi wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo katika sekta ya ujenzi baina Tanzania na nchi za jirani. 
   Awali akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuongea na washiriki wa maadhimisho hayo Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Ujenzi, Muhandisi Joseph Nyamhanga, amesema kuwa siku hiyo inatoa fursa kwa wahandisi kote nchini kukutana na kubadilishana uzoefu wa kitaalam katika kuleta maendeleo nchini. 
   Amesema Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imewezesha kufanyika kwa maadhimisho hayo nchini Tanzania lengo kubwa likiwa ni kuweka msukumo na msisitizo wa kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2015, kuangalia changamoto na mikakati ya kukabiliana nzao. 
   Ameongeza kuwa mkutano huo wa mwaka unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya 13 ukizishirikisha baadhi ya nchi za Afrika zikiwemo Nigeria,Afrika kusini,Malawi, Kenya na wawakilishi kutoka Norway.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Wahandisi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakati wa ufunguzi wa Siku ya Wahandisi nchini mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya Wahandisi wahitimu kutoka katika vyuo na taasisi mbalimbali wakiapa kiapo cha utii kwa Taaluma yao mbele ya Kamishna wa Viapo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wahandisi yanayoendelea jijini Dar es salaam.

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikabidhi vyeti na miongozo mbalimbali ya utendaji wa kazi kwa Wahandisi baada ya kuapishwa   jijini Dar es salaam
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikabidhi vyeti na miongozo mbalimbali ya utendaji wa kazi kwa Wahandisi baada ya kuapishwa  jijini Dar es salaam
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERB) Mara baada ya ufunguzi wa Siku ya Wahandisi 2015 leo  jijini Dar es salaam. 
  Picha na Lorietha Laurence Maelezo)


  0 0

  Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF profesa Fortunata makene akifungua warsha
  Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha.
  mwasilishaji wa mada Hosana Mpango akizungumza
  Mwasilishaji wa mada Hossana Mpango akizungumza na washiriki (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo.
  washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasirimali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha
  Washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasiriamali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).

  Na Mwandishi wetu
  SERIKALI imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kisera kuwezesha kukua kwa viwanda vidogo na vya kati  nchini.
  Kauli hiyo imo katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) kuhusu ukuaji wa sekta hiyo katika muktadha wa upatikanaji wa fedha.
  Akiwasilisha utafiti huo mmoja wa watafiti Hossana Mpango alisema kwamba kwenye utafiti wao wamebaini mgongano mkubwa wa kisera na utendaji, unaosababisha kukwama kwa maendeleo ya sekta hiyo.
  Alisema ingawa kuna tatizo kubwa la ajira ambalo limefanya watu wengi kukimbilia kujiajiri wenyewe, kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo hasa sera na uwapo wa mlolongo wa taasisi zinazopishana mamlaka na  huku wakiwa ndio wanatoa leseni.
  Alizitaja taasisi hizo zinazopishana mamlaka kama  Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mamlaka ya kodi (TRA) halmashauri  mbalimbali nakadhalika.
  Alisema mabadiliko ya kisera yatawezesha kutengeneza muundo unaojali ukuaji wa sekta hiyo hasa kwa kuangalia kodi zinazolipwa ambazo kwa sasa ni za aina moja bila kuangalia uwekezaji unaohusika.
  Sekta hiyo ya wajasirimali wadogo na wa kati yenye watu milioni 3 kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2012 inakabiliwa na tatizo la kutokua kutokana na vikwazo mbalimbali vikiwemo pia kukosekana kwa mafunzo ya ujasirimali na uwezo wa kupata fedha za mtaji.
  "Ni dhahiri upatikanaji wa fedha kutoka nje ili kuendeleza mtaji ni tatizo. Lakini tatizo hili linakuwagumu zaidi kutokana na riba kubwa, uchelewefu  wa kupata mikopo, rushwa katika utoaji na ukosefu wa nidhamu ya fedha kwa wakopaji” alisema Hossana.
  Alisema pamoja na mambo hayo kuna matatizo mengine makubwa yanayokwamisha ukuaji wa sekta hiyo. Matatizo hayo mengine ni gharama kubwa zinaootokana na haja ya kukidhi masharti ya uendeshaji wa viwanda hivyo vidogo na vya kati, tozo zinazojirudia, ukosefu wa soko na elimu ndogo ya wajasirimali.
  Alisema mabadiliko ya kisera yatasaidia kuimarisha sheria na kuweka sawa mwelekeo wa sekta hiyo kwa kuzingatia kwamba inahitaji mchango mkubwa wa nje ili kukua.
  Alisema mathalani ingawa kuna SACCOS, taasisi hizo zinashindwa kwenda kukopa kutokana na riba kubwa na kuwapo kwa mfumo wa kodi na makato mengine yakiwemo ya tozo usiokuwa na tija.
  Alisema suluhu nyingine inayostahili kufanywa ni kwa taasisi za kifedha kufuata tabia njema za kimataifa  za utoaji wa mikopo unaozingatia pamoja na mambo mengine ukubwa wa mikopo na malipo kwa kuangalia manufaa ya kiuchumi.
  "Ili viwanda hivi vya chini na kati kukua masuala ya kifedha na yasiyo ya kifedha ni lazima yaangaliwe na kushughulikiwa..." alisema.
  Matatizo mengine ni pamoja na sekta hiyo kukosa msaada huku taasisi mbalimbali zinazohitaji kushirikiana zikifanya vitu kila mmoja na wake.
  Taasisi hizo ni SIDO, TRA, WDF,  YDF,  BRELA  na pia miundombinu inayokera katika maeneo hasa ya vijijini.
  Pia ili kukuza sekta hiyo ni vyema serikali ikatengeneza miundombinu inayojkidhi haja ya ukuaji wa sekta hiyo kama maghala, masoko, barabara, maji, umeme kwa lengo la kupunguza gharama za kufanya biashara.
  Pia utafiti huo ulishauri kwamba serikali ni lazima kutenga fungu ambalo litatumiwa na  taasisi kama SIDO, NEEC  na hata maofisa biashara wa wilaya kwa ajili ya mafunzo ya ujasirimali na uendeshaji wa biashara.
  Mapema Mkuu wa idara ya utafiti na machapisho wa ESRF Profesa Fortunata Makene, aliwataka washiriki wa  warsha hiyo kutoa michango katika kuboresha uelewa ili serikali iweze kutatua kizungumkuti cha ukuaji wa sekta hiyo.

  0 0

  Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF profesa Fortunata makene akifungua warsha
  Mkuu wa utafiti na machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akifungua warsha.
  mwasilishaji wa mada Hosana Mpango akizungumza
  Mwasilishaji wa mada Hossana Mpango akizungumza na washiriki (hawapo pichani) kwenye warsha hiyo.
  washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasirimali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha
  Washiriki wa warsha ya siku moja ya ujasiriamali mdogo na wa kati katika muktadha wa fedha iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).

  Na Mwandishi wetu
  SERIKALI imetakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kisera kuwezesha kukua kwa viwanda vidogo na vya kati nchini.

  Kauli hiyo imo katika utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) kuhusu ukuaji wa sekta hiyo katika muktadha wa upatikanaji wa fedha.

  0 0

   Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi  jana jioni tayari kwa safari ya kuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), kushoto aliyevaa suti ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.
   
   Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni  tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwa ajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games
   Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni  tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwa ajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games
  Mkurugenzi  wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo kushoto akimkabidhi mmoja wa wanariadha Bendera ya Taifa tayari kwa safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), Timu hiyo iliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania.  Picha na Benjamin Sawe- WHVUM


  0 0

   Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia suluhu Hassam akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya jana, Septemba 3, 2015 katika Kata ya Buza jimbo la Temeke mkoani Dar es Salaam.
  Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia akishangiliwa na wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kata ya Buza jimbo la Temeke mkoani Dar es Salaam, Septemba 3, 2015.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhai Madabida akimkaribisha mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Buza, jimbo la Temeke katika mkoa huo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

    Na Yusef israel
  Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuweza kutufikisha hapa  toka tupate uhuru na toka nchi zetu mbili hizi zilizoweza kuungana na kuzaliwa taifa moja la jamhuri ya muungano  watu wa Tanzania,ni mambo mengi tumeshuudia mazuri  na mabaya natunapakaa na kuangalia nyuma  tunaona kweli kuna mazuri tumefanikiwa na kuna mambo ambayo tumeshindwa kuyatimiza au kuyatenda kwa sababu zetu wenyewe au makosa yetu wenyewe au sababu ya kutokuwa na uwezo wa kifedha.

  Tanzania ya leo ina  wananchi waliozaliwa wakati nchi ikiwa inaitwa Tanganyika  na ikiwa haijapata uhuru na watanzania wa baada ya uhuru  na Wa Tanzania wa waliozaliwa nchi ikiwa inaitwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Je,  wakati  nchi hizi zilizokuwa zinaungana Wazee wetu walifikiria nini au nini kilichowafanya wazee wetu hawa waamue nchi izi mbili ziungane  utakuta kuna mambo mengi yanayosemwa ,wengine ni kwa ajiri ya ulinzi wa visiwa hivyo visije vikachukuliwa tena na sultan wa oman wengine hiyo ni siri ya  Mwalimu na Mzee Karume kuna mambo mengi sana na baadhi ya viongozi wa siasa waliosomeshwa na serikali zilizokuwa zikiongozwa na wazee leo wamewaita majina mengi tu ya ajabu na kuwadharau.


  0 0

  Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli (aliyechuchumaa) akiwa kwenye maabara ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wakati akiwa mwanafunzi  mwaka 1985. Dkt Magufuli alisomea Kemia, Hisabati na Elimu. Kupata wasifu wake zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) wa Wilaya ya Lindi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini Ndugu Hassan Suleiman Kaunje wakiwapungia mikino mamia ya wananchi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi rasmi wa kampeni kwenye Jimbo kwenye uwanja wa Fisi uliopo Manispaa ya Lindi tarehe 3,9.2015.
   Baadhi ya wanachama na wananchi katika Manispaa ya Lindi wakishangilia wakati Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Manispaa hiyo Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiingia uwanjani hapo.
   Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Manispaa Mama Salma Kikwete akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mitandi Ndugu Laibu Kaisi aliyeamua kurejea Chama Cha Mapinduzi wakati wa sherehe za uzinduzi rami za kampeni za Chama hicho katika Manispaa hiyo.
   Kusoma zaidi bofya HAPA.

  0 0

  KUMBUKUMBU YA FLORA
  (MAPENDO YA FLORA)
  _________________________

  TUNAPOADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KUMBUKUMBU
  YA KIFO CHA MPENDWA WETU
  FLORA FLOWIN MKANULA
  (1993 – 2013)
  ___________________________________

  Tunaona ni vema kumshukuru MUNGU hasa kwa mapendo aliyotushirikisha kupitia maisha ya FLORA, nasi tukabakiwa kwa namna ya pekee tunamuenzi kwa matukio mbalimbali hasa kupitia Misa Takatifu katika kanisa kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Siku ya tarehe 10/09/2015, saa 12.30 asubuhi.  Baada ya hapo tunadhulu makaburi ya Kinondoni sote tuzidi kuyaenzi hayo.
  “Pendaneni kindugu Rum 12:10

  “APUMZIKE KWA AMANI”
  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katika Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ili aweze kuufungua mkutano huo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi umekuwa muhimu kwani unaleta uwazi pamoja na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wapili kulia meza kuu, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. Anayefuata ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.
   Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa makini wakati akitoa hotuba yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 barani Afrika unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani humo.
   Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini,  Jasem Ibrahim Al-Najem  kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait  na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Ibrahim Al-Najem  (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait  na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

older | 1 | .... | 962 | 963 | (Page 964) | 965 | 966 | .... | 3285 | newer