Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Tanzania Association in Switzerland (TAS) Fundraising Dinner and Dance - 10 October 2015


Maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu Rufaa za Wabunge

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea jumla ya rufaa 54 za madiwani kupinga Maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini. Pia jumla ya rufaa 198 za madiwani kutoka Halmashauri mbalimbali.
Tume imeanzakupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Wagombea (warufani) na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka majimboni. Imeanza kuzitolewa maamuzi rufaa za Wabunge.  Leo tarehe 31/82015 zimejadiliwa na kuamuliwa rufaa 38. Zilizobaki mawasiliano yanaendelea kati ya Tume na Wasimamizi wa Uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika kuisaidia Tume kufikia maamuzi ya kisheria na haki kwa wagombea na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi.  
Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa na Wasimamizi wa Uchaguzi ni 16 na Tume imerudisha wagombea 13 kati ya hao, waliobaki ni 3 ambao Tume imeridhia maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ni kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa kutoonesha makosa ya kisheria au kiufundi.
-- 
+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/focusradiotz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq 
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML, WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA.

$
0
0
 Moja kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.
 Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. 

MAASKOFU, WACHUNGAJI KUBARIKI TAMASHA LA AMANI

$
0
0
kushoto Mwenyekiti wa kamati ya tamasha la kuombea Amani hapa nchini,Alex Msama .

Na Mwandishi Wetu
MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali na Wachungaji wanatarajiwa kushiriki kwenye Tamasha la Amani linalotarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu Dar es Salaam.

Tamasha la Amani ambalo litahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ni maalum kwa ajili ya kuombea amani katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi muhimu yanaenda vizuri.

“Niseme kwamba Maaskofu na Wachungaji mbalimbali wamekubali kujumuika nasi siku hiyo katika tukio muhimu, ambapo baada ya tamasha la Dar es Salaam tutaelekea pia mikoani,” alisema Msama.

Alisema wasanii mbalimbali wanaendelea kuomba kushiriki katika tamasha hilo alilosema litakuwa la aina yake.

 “Tunaandelea na mazungumzo na wasanii mbalimbali, ambapo tayari Rose Muhando ameshakubali kutumbuiza na wengine tuliowatangaza,” alisema Msama.

Baadhi ya wasanii maarufu ambao wamewahi kushiriki matamasha yanayoandaliwa na Msama ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sohly Mahlangu.

KIMBISA AMNADI MAGUFULI KWA NGUVU, MAMA PINDA ANOGESHA...!

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma.'...Na wapigwe tu maana hamna namna nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma. '.
Na wapigwe tu maana hamna namna nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa ameweka kando msimamo aliyokuwa nao awali na kuanza kumnadi kwa nguvu mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli huku akiahidi atafanya hivyo nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka hadi shuka. 

Kimbisa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa kwenye mkutano na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) walipokuwa wakizungumza na mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma. 

Tukio la Kimbisa kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Bi. Suluhu linaonesha tayari kimbisa amefunga ukurasa wa kutokubaliana ambao aliuonesha mapema mjini hapo wakati wa mchakato wa chama hicho kutafuta mgombea mmoja wa urais atakaye peperusha bendera ya CCM. 

TANGAZO LA KIFO CHA MICHAEL JAPHET MBAGA NA JOHN JAPHET MBAGA

$
0
0
FAMILIA ya marehemu mzee Japhet Mbaga, wa Dar es Salaam kwa masikitiko makubwa inatangaza vifo vya kaka zao wapendwa, MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA, vilivyotokea hapa Dar es slaam  siku ya Jumapili na Jumatatu zilizopita.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, siku ya Alhamisi tarehe 3 Septemba, 2015 saa 10.00 jioni. 

Ratiba ya kutoa heshima za mwisho itafanyika siku hiyo hiyo, saa 7.00 mchana nyumbani kwa Mary Rusimbi (Mkurugenzi Mkuu, WOMEN FUND TANZANIA) eneo la Tabata - shule, nyumba za TAZARA.

 Baadaye saa 9.00 Ibada ya kuwaaga wapendwa wetu itafanyika Kanisa la KKKT Kijitonyama.


Marehemu MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA ni kaka wa MARY RUSIMBI, HILLARY MBAGA, ROSE MSHANA (ROZELLA) NA STELLA MBAGA.



"Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe."
AMINA

VYOMBO VYA HABARI VINAWAJIBU WA KUELIMISHA JUU YA MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Vyombo vya habari vimetakiwa kushiriki katika maendeleo endendelevu ya yenye malengo 17 yanayoanza 2016 hadi 2030 ili kuweza wananchi kufahamu kila lengo na kuweza kufikia mabadiliko chanya.

Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu yanatokana na kuisha kwa malengo ya milenia ambayo yamekamilika mwaka huu na kufanya nchi 88 duniani kukaa pamoja na kuja malengo hayo lengo likiwa ni kukamilisha malengo ya milenia ambayo yamekamilika mwaka huu pamoja na kuboresha sekta mbalimbali kupitia malengo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa na Hope Foundation for Social  Interprenuership, Mhadhiri wa Shule  Kuu ya Uandishi wa Habari  ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk.Ayub Rioba  amesema kuwa waandishi  wanawajibu kuelimisha wananchi kwa kila hatua ya melengo 17 ya maendeleo endelevu.

Rioba anasema baadhi ya nchi ikiwemo Singapore na Malaysia zimepiga hatua kubwa katika kutimiza malengo ya milenia inayokamilika kutokana na kuwashirikisha wananchi wake kupitia vyombo vya habari hivyo serikali na wadau wa masuala ya maendeleo wanatakiwa kufanya hivyo.

Mratibu  wa  Kanda ya Afrika  ya 2015,Steven Chacha amesema kama taasisi wamejipanga katika kuhakikisha wanashirikisha waandishi katika kuhakikisha malengo hayo yanayoangaliwa  katika kuleta mabadiliko yenye tija kwa wanananchi ambao wanatokana na changamoto.

Nae Afisa wa Takwimu wa  Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS),Emilian Karugendo amesema kuwa NBS watafanya tathmini kutokana na viashiria hivyo katika kwenda katika malengo 17  ya maendeleo endelevu.
 Afisa wa Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango Lorah Madete akizungumza na waandishi wa habari juu ya jinsi ya mipango inavyotekelezwa na serikali katika kuelekea malengo 17 ya maendeleo endelevu iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari pamoja na  viongozi wa Taasisi ya Hope Foundation for Social  Interprenuership iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

 KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI WA KIDINI KUTOKA NCHI 17 ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KUJADILI MIKAKATI YA KUMALIZAMA AMBUKIZI MAPYA YA VVU/UKIMWI

$
0
0
Mshereheshaji wa mkutano huo Prof. Venant Nantulya akiwa katika hatua ya uendeshaji wa mkutano wa Viongozi wa ngazi ya juu wa dini katika kupambana na kuweka mikakati ya 

kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.Picha na Geofrey Adroph

Mufti mkuu wa Zambia, Sheikh Assadullah Mwale akifungua kwa dua katika mkutano wa viongozi wa dini wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika uliofanyika leo jijini Dar.
Bi. Vanessa Anyoti kutoka YWCA Tanzania(kushoto) akizungumza kuhusiana masuala ya kijinsia  pamoja na maendeleo ambayo yanaweza kupunguza maabukuzi ya virusi vya UKIMWI. Kulia ni 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues

Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI na waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela akizungumza na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrikawakati wa mkutano ulioanza leo jijini Dar. Picha zaidi BOFYA HAPA


MKUTANO WA KAMPENI WA LOWASSA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma, Septemba 1, 2015, ambako kulifanyika Mkutano wa Kampeni na kunadi sera za Ilani ya Chama chake, anazoendelea nazo kwa nchi nzima
Mh. Lowassa na Mh. Sumaye wakiutazama Umati wa watu uliofurika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma wakati wa Mkutano mkubwa wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 02/09/2015

Mashehe wa Tanzania waliotekwa nchini Congo DRC waachiwa huru

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya kuachiwa huru kwa Mashekhe wa Tanzania waliotekwa nchini Congo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Haji Kombo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) wakimsikiliza Balozi Mulamula wakati akizungumza na Waandishi wa Habari. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI KWENYE MAZISHI YA MDHAMINI WA TAASISI YA WAMA MAREHEMU HULDA KIBACHA

$
0
0
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akipokewa na Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa WAMA wakati alipowasili nyumbani kwa Marehemu Mama Hulda Kibacha, Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA aliyefariki dunia tarehe 28.8.2015.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye ibada ya kumwombea Marehemu Hulda Kibacha, Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA iliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Ada Estate tarehe 2.9.2015. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Zakhia Meghji na kulia ni binti wa marehemu Nampombe Kibacha.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mdhamini wa Taasisi ya WAMA Mama Hulda Kibacha aliyefariki dunia tarehe 28.8.2015 hapa Dar Es Salaam. Marehemu Kibacha aliwahi kufanya kazi Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).  
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka udongo kaburini ulimolazwa mwili wa Mama Hulda Kibacha aliyekuwa Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA. Marehemu Hulda Kikbacha alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni tarehe 2.9.2015.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) kwa kushirikiana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro (kushoto) na Mama Zakhia Meghji (kulia) wakiweka shada la maua kwenye kaburi LA Marehemu Hulda Kibacha aliyezikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 2.9.2015.
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Hulda Kibacha.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, Ndugu Zakhia Meghji akitoa salamu maalum za Taasisi hiyo wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mdhamini na Mjumbe wa Bodi hiyo Marehemu Hulda Kibacha.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Binti wa Marehemu Nampombe Kibacha mara baada ya Mazishi ya Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA, Mama Hulda Kibacha.
PICHA NA JOHN LUKUWI. 

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MABANDA KWENYE MKUTANO WA MAMLAKA YA MANUNUZI(PPRA)JIJINI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini(SSRA)  baada ya kufungua kongamano la Mamlaka ya Ununuzi ya Umma(PPRA)jijini Arusha leo,kulia ni Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bi. Sarah Kibonde.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Mohamed Gharib Bilal (kushoto)akimsikiliza Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo  Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini(SSRA)   ,Sarah Kibonde wakati akimweleza utendaji kazi wa Mamlaka hiyo  baada ya kufungua kongamano la Mamlaka ya Ununuzi ya Umma(PPRA)jijini Arusha .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa  Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini(SSRA), Bi. Sarah Kibonde.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Mohamed Gharib Bilal (kushoto)akizungumza wa wafanyakazi wa UTT Asset Management and Investor Services PLC,  Afisa Mafunzo,Hilda Lyimo(katikati) na  Afisa Masoko na Mahusiano kwa Umma,Rahim Mwanga

Makamu wa Rais,Dk Mohamed Gharib Bilal akimsikiliza Mratibu wa Biashara Kanda ya Kaskazini wa Shirika la Simu nchini(TTCL)Thomas Lemunge(kulia)alipotembelea banda  kuona utendaji wa shirikan hilo.

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM ALHAMISI SEPTEMBER 3, 2015 KUANZIA SAA 12

Mazishi ya kiongozi wa kikosi cha wataalamu wa China katika mpango wa ushirikiano wa ujenzi wa uwanja wa taifa na uwanja wa Uhuru

$
0
0
 Mke wa marehemu Eng. QI XIN wa pili kutoka kulia akitoa heshima zake za mwisho katika mazishi ya mume wake ambaye alikuwa Kiongozi wa Kikosi cha Wataalam wa kichina katika mpango wa Ushirikiano katika ujenzi wa Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru akiuaga mwili wa mpendwa wake katika mazishi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
 
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga wa kwanza kushoto akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Eng. QI XIN ambaye alikuwa Kiongozi wa Kikosi cha Wataalam wa kichina katika mpango wa Ushirikiano katika ujenzi wa Uwanja wa Taifa katika mazishi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Leornad Thadeo akitoa heshima zake za mwisho kwa Kiongozi wa Kikosi cha Wataalam wa Kichina katika mpango wa Ushirikiano katika ujenzi wa Uwanja wa Taifa Eng. QI XIN wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene wa kwanza kushoto  akitoa heshima zake za mwisho kwa Kiongozi wa Kikosi cha Wataalam wa Kichina katika mpango wa Ushirikiano katika ujenzi wa Uwanja wa Taifa Eng. QI XIN wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

mwanasheria wa chadema Tundu Lissu amjibu Slaa

TMA yatangaza Utabiri wa msimu wa vuli

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa utabiri wa msimu kwa miezi ya Septemba hadi Desemba 2015 kwa wanahabari.kushoto kwa Dkt, Kijazi ni mkurugenzi wa huduma za utabiri, Dkt. Hamza Kabelwa.
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa iliyopo na inayotarajiwa, mvua za vuli zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)     Mvua za vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)

Msimu wa mvua wa miezi ya Oktoba hadi Disemba (vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. 

Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani kwa maeneo mengi. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki mbili za mwisho za mwezi Septemba 2015 katika  kanda ya ziwa Victoria na katika maeneo machache ya Pwani ya kaskazini. 

IMETOSHA Music and Laughter Night

$
0
0

Na Henry Mdimu

Ndugu zangu,
Nawasalimu katika jina la bwana,
Assalam Aleykum!


Nikianza na neno la shukrani, naomba nizitoe za dhati kwa kunivumilia, na kufanya nami kampeni ya Imetosha katika mazingira magumu sana katika awamu ya kwanza. Hii ni kutokana na ugeni katika uendeshwaji wa taasisi pamoja na uhalisia wa safari za kiharakati, mara nyingi wanaofika safari huwa ni wachache, lakini nyie hamkuwahi kukata tamaa katika kuniunga mkono.



Awamu ya kwanza ya kutambulisha taasisi na misimamo yake imefanikiwa, na sasa tunaenda katika awamu ya pili, ambapo baada ya kufanya matembezi, na kampeni mbali mbali ndogondogo, tulifanikiwa kwa kuungwa mkono na taasisi rafiki na azma ya kwanza ilikuwa ni kukiunga mkono kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga.



Lakini baada ya mimi binafsi kama muasisi na mwenye wazo, kufikiri kwa kina kuhusiana na Shinyanga, ambako kiukweli mazingira yake hayajathibitika kuwa salama, na pili kuwa ni kituo cha serikali, nilikuja na wazo la Taasisi kuwa na kijiji cha mfano ambacho, pamoja na kuhifadhi watu wenye ualbino na wasio na ualbino bali pia kiwe kituo cha uzalishaji mali, ambacho kitawakomboa watu wenye ualbino katika ile dhana na kuomba omba, na kuwa wachangiaji rasmi wa pato la taifa kwa kufanya biashara ya kilimo na ufugaji.



Hivi ninavyoongea tayari tumeshatoa malipo ya awali kwa Mzee idd Shemdoe wa huko Bumbuli, Lushoto, mkoani Tanga ambaye amekubali kuiuzia taasisi shamba la Mikahawa lenye ukubwa wa ekari 50. Hapo taasisi ina mpango wa kufungua kituo kitakachoitwa Santa Lucia, Safe House and Estate.



Eneo litatumika kwa kilimo, ufugaji, pamoja na elimu, kwa maana ya shule kubwa inayofundisha kwa mtaala wa kimataifa, lengo likiwa ni kuwawekea watu wenye ualbino vitega uchumi ambacho vitasababisha wao na taasisi yao kutowapigia wafadhili magoti mara kwa mara na badala yake kuwa sehemu ya watatuzi wa matatizo ya kijamii yanayoiklumba nchi.



Kaka na dada zangu, kuwa na eneo tu haitoshi, na safari ya kuifikia ndoto hii ni ndefu inayochukua muda mrefu kuikamilisha. Mimi naiamini kwa sababu tu nina nia na nimedhamiria kuifanya kama sehemu ya ndoto zangu za kimaisha.



Nachukua nafasi hii kuwaomba kunisaidia kushiriki katika shughuli mbali mbali nitakazokuwa nazifanya katika kutunisha mfuko wa taasisi, na hapa naileta kwenu shughuli ya Music and laughetrs, ambayo Orijino Komedi wamekubali kuwa wenyeji huku muziki nao ukichukua sehemu kubwa ya shughuli.



Hii itakuwa Septemba 11, naomba muwahimize wadau kadri muwezavyo wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono kwa umoja wetu.


Mungu ibariki Tanzania,
 Mungu aubariki umoja wetu

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA WASAIDIZI WA KISHERIA MAGEREZANI MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
 Meza Kuu wakimsikiliza Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani - Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi(hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bw. Joseph Ndunguru(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza baada ya kukabidhi  cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro. 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) walioketi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria kutoka Mikoa Mitano ya Magereza Tanzania Bara(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunula(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Joseph Ndunguru(wa kwanza kushoto) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi, Emmy Mkonyi(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MWIGULU NCHEMBA ALIPUA UKAWA KWA KUNUKUU MANENO YA BABA WA TAIFA

$
0
0
Mwigulu Nchemba akiwasili eneo la Mkutano nje kidogo na Mji wa Babati hii leo alipofika kwaajili ya Mkutano wa kampeni wa kuinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015.Pia kuwanadi wagombea Udiwani na Ubunge kwa Babati Mjini.Kutoka Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara Ndg.Ndekubali,Katikani ni Mwigulu Nchemba na Mwisho kulia ni Mh.Chambili ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Babati hii leo,Katika hotuba yake amesisitiza Wananchi waachane na maigizo yanayofanywa na baadhi ya wagombea Urais bali waamue moja la Kuchagua Rais Mchapa Kazi,.Mweigulu amesisitiza Zaidi kuwa rekodi za wagombea Urais zipo wazi kila kona na kwa rika zote.Hivyo watanzania watumie fursa hii kuhakikisha Taifa linapata kiongozi Mchapa kazi ambaye ni J.Pombe Magufuli wa CCM.Sehemu ya mamia ya Wananchi waliofika kusikiliza Ilani ya chama cha Mapinduzi wakishangilia namna Ilani ya chama hicho ilivyoweka bayana namna ya Kutekekeleza shughuli za maendeleo katika Jimbo la Babati Mjini,Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini Ndg.chambili wakiagana na Wananchi mara baada ya Mkutano huo wa kampeni wa CCM."CCM ni Ile Ile"
Picha na Sanga Jr.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images