Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

wanafunzi madaktari wa KCMC walivyoadhimisha Siku ya Afya Duniani

$
0
0
Dr Anzibert Rugakingira (mwanafunzi wa udaktari KCMC) akiwahutumia wananchi wa usharika Mamba Kotera katika kuadhimisha siku ya AFYA DUNIANI.
Dr. Diana akipima shinikizo la damu kwa mmoja kati wananchi waliofika katika zoezi la Upimaji wa presha na viashilia hatari vya magonjwa ya moyo.
Dr. Sabina mtweve wa Idara wa Tiba ya Jamii akitoa ushauri kwa mmoja kati ya wananchi waliofika katika zoezi la Upimaji wa presha na utoaji wa huduma ya kupima presa na viashilia hatari vya magonjwa ya moyo.

Dr Mbishi Matumbo akimpima mmoja wa wananchi waliojitokeza kupima presha yake.

Dr Sabina mtweve wa Community Medicine akiongoza jopo la wanafunzi madaktari wa KCMC waliofika katika kuazimisha siku ya afya duniani ambapo walifanya zoezi la Upimaji wa presha na viashilia hatari vya magonjwa ya moyo.

DR. SALIM AHMED SALIM AONGOZA MAADHIMISHO YA 19 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA YALIYOFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa maashimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.
Katika mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

usiku wa kumbu kumbu ya steven kanumba ulivyofana jijini dar.

$
0
0


Pichani kushoto ni aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye usiku wakumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Yusuph Mwenda akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwa niaba ya Mh Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanumba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.


Pichani kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko,Steven Kanumba.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanimba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.

Mwakilishi kutoka Kampuni ya Clouds Media Group,Zamaradi Mketema akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya kampuni hiyo iliyotoa mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu hapa nchini,kutoka kwa Mama yake,Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho ya kumbu kumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu afarikii nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko,Steven Kanumba.


Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama yake Marehemu Kanumba,kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwenye tasnia ya Filamu hapa nchini.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

BEI YA MADAFU LEO

Mtaalam wa masuala ya majanga,Mdau Ruger Kahwa akiwajibika

$
0
0
Mdau Ruger Kahwa ambaye ni mtaalam mkongwe wa masuala ya kukabiliana na majanga na mkuu wa ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulika na uratibu wa majanga na maafa ( United Nations Office for the Coordination of Humanitarian Affairs) nchini Papua New Guinea wa kwanza kulia akiweka shada la maua kwenye eneo ambalo Meli iliyozama na kuuwa watu 300 nchini Papua new Guinea ilipoanzia safari mwaka 2012. Hii ilikuwa wakati wa kuwakumbuka wahanga wa ajali hiyo katika jimbo la West New Britain.

BREAKING NYUZZZZZZ: Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher Afaraiki Dunia

$
0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi. Margaret Thatcher maarufu kama "Iron Lady" amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 87. 

Watoto wa marehemu Sir. Mark na Bint Carol wamethibitisha kuwa mama yao Margaret (Baroness) Thatcher amefariki leo asubuhi na alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa "Stroke". 

Marehem Margaret Thatcher alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia 1979-1990, katika kipindi cha utawala wake alikuwa akilumbana sana na nchi changa zinazoendelea kwa ajili ya kuvutia maslahi ya Uingereza,kitu ambacho viongozi wa nchi nyingi za jumuiya ya madola hawakukubaliana naye.

Lakini kwa nchi yake atakumbukwa kuwa ni kiongozi aleyesaidia sana kunyanyuka kwa uchumi wa Uingereza katika enzi za utawala wake. 

Habari zaidi zitafuata baadaye

Tanzania na Japan zasaini makubaliano ya ujenzi wa Barabara nchini

$
0
0
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa wa kwanza kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye riba nafuu kwajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kulia ni Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada akitia saini pia makubaliano hayo.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akibadilishana hati za makubaliano ya mkataba na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada, mkataba huo utaiwezesha Tanzania kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akisisitiza jambo wakati akiwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bwana. Masaki Okada mara baada ya kukamilika kwa shughuli za utiliaji saini wa makubaliaono ya mkopo wa riba nafuu.

taarifa kutoka shirikisho la soka nchini (TFF) leo


MKUTANO WA WADAU KUHUSUKANUNI ZA MATUMIZI SALAMA YA BAIOTOKNOLOJIA YA KISASA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Kikao cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa, kikao kilihusisha wanasanyansi, wanasheria, Mtandao wa wakilishi wa wakulima na Taasisi za Mbegu.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia mjadala, katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamuwa Rais Mtaa wa Luthuli JijiniDar es Salaam.Picha na Ali Meja.

Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC ikulu jijini Dar leo,Pia apongeza walioshiriki Zoeazi la Uokozi Ajali ya Jengo la Ghorofa Dar

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC Bwana Daniel Yohannes ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akioongea na makundi mbalimbali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoshiriki katika zoezi la uokozi wakati wa ajali ambapo jengo la ghorofa liliporomoka , kuuwa na kujeruhi watu kadhaa katikati ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibun.Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa Sabasaba katik viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova kwa uendeshaji wa Zoezi la uokoaji katika ajali ya Jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kijana mlemavu Shabani Selemani Mohamed katika ukumbi Sabasaba katuka viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa ,wakati wa hafla fupi ya kupongeza makundi mbalimbali yaliyoshiri katika kazi ya kuokoa watu na kuopoa miili wakati wa ajali ya kuanguka kwa ghorofa katikati ya Jiji la Dar e Salaam hivi karibuni.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ walishiriki katika kazi ya kuokoa watu wakati wa ajali ya kupomoka kwa jengo katikati ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.picha na Freddy Maro

Article 6

Mshindi wa Tshs 10,000,000 za DStv apatikana

$
0
0
Meneja wa Fedha wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Francis Senguji (kushoto) akimkabidhi Bw. Masoud Said (38), mkazi wa jiji la Mbeya kitita cha Tshs 10,000,000 alizoshinda kutokana na bahati nasibu ya DStv Rewards inayochezeshwa na kampuni hiyo ya MultiChoice Tanzania Kila wiki, DStv wamekuwa wakitoa kitita cha Tshs 5,000,000 kwenye droo maalum ya DStv Rewards kwa wateja wake wanaofanya malipo kabla ya akaunti zao kukatika. Kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo,Furaha Samalu.
Bw. Masoud Said akiweka kitita chake hicho kwenye mfuko mara baada ya kukabidhiwa.

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma lakamata Mikia 10 ya Tembo waliouwawa

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Deusdedit Nsimek akionyesha nyara za serikali (mikia ya tembo) zilizokamatwa na Jeshi la Polisi MKoani humo.
Nyara za Serikali ambazo zimekamatwa(mikia kumi ya tembo)

Na Demasho Blog.

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikiria kijana ambaye anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa eneo la Mbalikiwa kata ya Ligunga Wilayani Tunduru kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali (mikia ya tembo).

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma,Deusidedit Nsimeki ameyasema hayo leo mapema wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la Mbalikiwa mnamo tarehe Aprili 5, 2013 majira ya saa:7 usiku ambapo jumla ya idadi hiyo ya mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20 yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15 sawa na zaidi ya milioni 245 kwa fedha za kitanzania.

Mtuhumiwa Bakari Said leo alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara hiyo haramu ya nyara za serikali ambapo taharifa ya tukio hilo la uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wao wa dhati ili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.

Rais Kikwete aomboleza kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza,Margaret Thacher

Balozi Dr. Diodorus Kamala akutana na watanzania wanaosoma Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubelgiji

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai ya bendera ya taifa) akiwa katika picha ya Pamoja na Wanachuo kutoka Tanzania wanaosoma Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubelgiji. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kikazi ya kukutana na Watanzania katika eneo lake la uwakilishi.

RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI JIONI HII TAYARI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS WA NNE WA KENYA MHE UHURU MUIGAI KENYATTA KESHO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wakipozi na wasichana waliowazawadia mashada ya maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni na wenyeji wao. PICHA NA IKULU.

DK.SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WIZARA YA BIASHARA VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara  ya Biashara,Viwanda na Masoko,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. Kkushoto ni Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,

Baadhi ya Watendaji na maafisa wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko,wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,katika kikao cha Uongozi wa Wizara
hiyo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ikiwa katika mpangilio  wa Rais, kuzungumzia utekelezaji wa kazi za kila Wizara. Picha na
RamadhanOthman,Ikulu

Uhuru Kenyatta on Zuku Road to Statehouse

UPEO MDOGO WA WANANCHI JUU YA SUALA LA USAFI WA JIJI NI CHANGAMOTO KWA KAMPUNI ZILIZOPEWA ZABUNI YA KUSAFISHA JIJI

$
0
0
Baadhi ya Dust bin zinazomilikiwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd. zilizowekwa katika baadhi ya mitaa ya Manispaa ya Ilala ambazo pia mteja yoyote anapohitaji huuzwa.

Wananchi wa jiji la Dar es Salaam hususan wakazi wa manispaa ya Ilala wametakiwa kutambua kuwa suala la usafi na kutunza mazingira ni jukumu la watu wote na sio tu la kampuni zilizopewa kandarasi ya kukusanya taka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd iliyopewa dhamana ya kufanya usafi katika manispaa ya Ilala Vidah Fammie amesema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku wanakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo watu kutochangia katika ulipaji wa ada ya taka na pia kutolipa kwa muda muafaka.

Akiendelea kuzitaja changamoto hizo amesema pia wangependa wananchi watambua kuwa suala la dust bin, watu wamekuwa wakielewa vibaya kuwa wao ndio wanaopaswa kuzimbaza jambo ambalo sio kweli, kampuni ya usafi ya Green Waste Pro wanaziuza na hawamlazimishi mteja wao yeyote kununua, ila anaruhusiwa kununua pale anapopenda, na kuwa zile dust bin zinazowekwa mitaani wao wanapata usaidizi kutoka manispaa.

Pia ameshauri kwa wale ambao hawana dust bin watumie mifuko maalum ya kuweka taka na gari litakapopita litachukuwa kama ulivyo utaratibu wa suala la usafi.

Bi. Vidah Fammie ameongeza kuwa tatizo jingine wanalokabiliana nalo ni suala la upeo mdogo wa wananchi kuhusu suala la usafi.

Mwandishi wa habari hizi alipotaka ufafanuzi kuhusu suala hilo, amesema inaonekana wapo wananchi wanaoelewa suala zima la usafi lakini wanapuuzia na kuna wale wasio elewa kabisa hivyo mtu akiwa na taka anatupa tu kwa kuwa anajua kuna mkandarasi wa kufanya usafi kitu ambacho si sawa.

Kingine amesema ni miundo mbinu mibovu na hali ya hewa hivyo wakati mwingine kwa mfano gari maalum la kusafisha barabara linashindwa kufika hivyo inabidi kutumika nguvu za ziada kama vile vibajaji na vitu vingine.

DoubleTree by Hilton HAS PARTNERED WITH SOBER HOUSE WITH THE AIM TO EDUCATE THE CHILDREN OF ZANZIBAR ON DRUG AWARENESS AND PREVENTION

$
0
0
First Vice-President of Zanzibar Seif Sharif Hamad, DoubleTree by Hilton Regional Director Mr.Judd Lehmann, Director of Sales, DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata in a group photo with Sober House Members.

DoubleTree by Hilton Resort in Zanzibar announced their partnership with Sober House, a grass roots organisation in Zanzibar that supports the recovery of drug addicts and conducts community awareness and prevention.

DoubleTree by Hilton has partnered with Sober House with the aim to educate the children of Zanzibar on drug awareness and prevention.

The Sober House volunteers (many former drug addicts) will visit schools every month for the next two years and facilitate a workshop that allows the children to learn about the facts and ask questions in a safe, supported space.

Each child will receive a booklet that features a comic written by the Sober House residence as well as factual information that was approved earlier this year during a workshop hosted by DoubleTree with the Ministry of Education, The Drug Commission of Zanzibar and representatives from The Ministry of Health.

Director of Sales, DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata said Sober House Founder Members, Suleiman Mauly and Fatma Juma should be applauded for their dedication and efforts.

Added that we are proud to empower Sober House by building their capacity to make a larger impact in the community.

DoubleTree by Hilton Regional Director Mr Judd Lehmann insisted that “we hope that our campaign throughout schools will encourage the children to say NO to drugs because they understand the consequences.”
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live


Latest Images