Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 953 | 954 | (Page 955) | 956 | 957 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Binagi Media Group George Marwa Binagi-GB Pazzo akionyesha Kitambulisho chake cha Kupigia Kura ikiwa ni katika Uzinduzi wa Kampeni yake ya KUHAMASISHA WATANZANIA WOTE kujitokeza Kupiga Kura 0ctoba 25 Mwaka huu kwa ajili ya Kuwachagua Viongozi watakaowatumikia. 
  Kampeni hiyo inafahamika kwa jina la "MTANZANIA PIGA KURA, EPUKA KULA KWA AJILI YA MAENDELEO YAKO".

  Katika Kampeni hiyo ambayo inaanza leo Agost 26, 2015 Wasomaji wa Mtandao huu pamoja na Wadau mbalimbali watapata fursa ya kutuma picha zao kwa ajili ya kuhamasisha zoezi zima la upigaji wa Kura pamoja na kuwa na uchaguzi wa Amani. Tuma picha yako kupitia Whatsupp namba +255 (0) 757 342 694 au Email binagimediagroup@gmail.com ukiambatanisha na ujumbe mfupi.

  Huu ndio ujumbe wa GB Pazzo juu ya Kampeni hii ya Piga Kura, Epuka Kura "Kwangu mimi Piga Kura, Epuka Kula ina maana kwamba mimi ambae ni mpiga kura napaswa kuweka maslahi yangu binafsi pembeni na kupiga kura kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote maana nikiendekeza kula leo kuna uwezekano wa kushinda njaa kwa miaka mitano ijayo".
  Binagi Media Group; Mtanzania Epuka Kula, Piga Kura Kwa Ajili Ya Maendeleo Yako"

  0 0


  Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.
  Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.
  Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa muda mrefu maishani bila matatizo.  0 0

  Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha Akifurahia Jambo na Wakili  Peter kibatala
  (wa kwanza kulia)   na Albart Msando (wa pili kushoto)
   Masha aliyevaa tisheti jeusi suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu akifurahia jambo  na mawakili na marafiki zake  muda mfupi baada ya kupata dhamana
  --
   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
  Masha alifikishwa mahakamani hapo jana nyakati za saa 6:49 mchana na kuhifadhiwa mahabusu na ilipofika saa 9:31 alasiri alipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi  Mkuu, Waliarwande Lema kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.
  Masha aliachiwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuithibitishia mahakama kuwa nyalaka hizo ni halali.
  Kufanyika kwa uthibisho huo wa nyaraka za wadhamini ndio uliopelekea juzi Masha kupelekwa mahabusu katika gereza la Segerea.
  Baada ya kumaliza kukamilisha taratibu hizo za dhamana ilipofika saa 9:46 alasiri Masha, mkewe, mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo, Peter kibatala na Albart Msando pamoja na ndugu zao wengine waliondoka mahakamani hapo kwenda nyumbani.
  Awali Agosti 25, 2015 Masha alipandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha ya matusi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi.
  Masha aliyekuwa amevaa tisheti jeusi, suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu na viatu aina Sendo anadaiwa kuwa Agosti 24,2015  katika kituo cha polisi cha Osterbay alitoa lugha ya matusi kwa maofisa wa jeshi la polisi.
  Chanzo: Mwananchi

  0 0

  The East African Legislative Assembly sitting in Kampala, Uganda,  yesterday adjourned debate on the EAC Electronic Transactions Bill 2014 to pave way for stakeholders to make additional input. 

   The adjournment came after a request for deferment of the debate by the Chair of Council of Ministers, Hon Dr. Abdallah Saadaala was approved. 

   In his ruling, the Speaker, Rt Hon Daniel F Kidega directed that the Bill be brought back to the Order paper during the next Plenary in Nairobi, Kenya. 
   The Chair of Council of Ministers reiterated total support of the Bill but added there was need for more time for the consolidation of further inputs and comments by stakeholders. 

   At the same time, consultations are been called to allow for enrichment of the Report of the Committee of Communication, Trade and Investment. 


   The Chair of Council of Ministers, Hon Dr. Abdalla Saadaala moved for deferment of debate
   Hon Mukasa Mbidde, Chair of the Communication, Trade and Investment Committee reads the Report on the Electronic Transactions Bill
   Hon Isabelle Ndahayo makes her contribution on the floor
  Hon Susan Nakawuki takes the floor to contribute to the debate

  0 0

   Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa imemuwezesha mjasiriamali Prisca George Chillumba ambaye ni mmiliki wa biashara ya saluni mkoani Mtwara. 
  Prisca amenufaika na mradi huu kwa kupatiwa vitendeakazi mbalimbali vitakavyomuwezezesha kupanua wigo wa idadi ya huduma zitatakopatikana katika saluni yake. 
   Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi amesema, sambamba na kuongeza idadi ya huduma zitakazopatikana katika saluni ya Prisca, vifaa hivi vitamuwezesha kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja, jambo ambalo litamuwezesha Prisca kuajiri vijana wenzie ili kuendeleza biashara na kukuza kipato chake. 
  Bi Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali unawapatia vitendeakazi vijana wajasiriamali ili kuwaongezea kasi ya maendeleo ya kibiashara vijana hawa ambao tayari wameshachukua hatua na kuanza kujishughulisha na biashara ndogondogo. 
  Lengo likiwa ni kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii katika njia inayoleta tija. 
  “Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo. 
  Awali akipokea msaada huo Bi Prisca ameshukuru kwa vifaa hivyo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa. 
  “Siamini kama naweza kufikia malengo yangu katika biashra hii, naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu lakini pia nitatoa fursa kwa viajana wenzangu” alisema Priscar. 
  Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili waweze kukuza mitaji yao.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto) na rafiki wa Prisca. 
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akimkabidhi kijana Prisca George Chilumba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, kwa kijana Prisca George Chilumba (kulia), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia), akimpongeza kijana Prisca George Chilumba, baada ya kumkabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Ligula, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Airtel.

  0 0

  Mgombea mwenza wa nafasi ya urais  kwa tiketi ya CCM Bi. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa mkoa wa Arusha katika viwanja vya Samunge jijini humo.
   Sehemu ya wananchi waliohudhuria  katika mkutano huo hii leo
   Mgombea mwenza wa nafasi ya urais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa anacheza ngoma  iliyokuwa inapigwa na wakina mama waliohudhuria mkutano huo
  Mgombea mwenza wa nafasi ya urais Mhe Samia Suluhu Hassan akisaini vitabu vya wageni kabla ya kuanza mkutano huo viwanja vya Samunge jijini Arusha.Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Wakati  nilipoandika kuhusu  talaka  na  mambo  yanayokubalika  kisheria  kama  sababu  za  talaka  nilipata   maoni  na  maswali  mengi kutoka kwa  wasomaji wetu.  Kati  ya  hao  ni mmoja  ambaye  alijitambulisha  kwa  jina   na  kuwa  ni  mkazi  wa  kinondoni  Dar es  salaam. Huyu  aliuliza  swali  lake  ambalo  ndilo  kichwa  cha  makala  haya.  Alisema  ameziona  sababu  nilizoeleza  ambazo  zinapelekea   mtu  kupewa  talaka  lakini  sababu  inayohusu  tatizo  lake  hakuiona  na  hivyo  aliomba  nimpatie   ufafanuzi. Maelezo  yake  kwa  ufupi  yalikuwa  hivi:


  1.KUPATA  MIMBA  NJE  YA  NDOA.


  Ndugu  huyu  alichoeleza  ni  kuwa  yeye ni  muajiriwa  katika jeshi  la  Wananchi  wa  Tanzania.  Na  kuwa  mwaka  jana   alipangiwa  safari  ya kikazi   kwenda  Congo  kwa  ajili  misheni  maalum  ya  jeshi  kwa  kipindi  cha  miezi  sita.  Anasema  alikwenda  na kumuacha  mke  wake  nyumbani  kwake  ambapo  amerudi   mwaka  huu . 
  Anasema   ndani  ya  wiki  moja  tangu  arudi  hakuielewa  hali  ya  mke  wake kitu  kilichomfanya  achukue  maamuzi  ya  kumpeleka  hospitalini  kwa  ajili  ya  vipimo.  Alifanyiwa  vipimo  vyote  na  hatimaye  kugundulika  ana  mimba  ya  mwezi mmoja.  Swali  la  ndugu  huyu  lilikuwa  ni  sheria  inasemaje  katika  hali  kama  hiyo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mlemavu wa miguu ndugu Joseph,mkazi wa kijiji cha Lwasho wilaya ya Momba,ambapo alimuahidi kumletea baiskeli ya kutembelea.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akiombewa na Watawa wa kijiji cha Lwasho,mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba.


  Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
  Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
   Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya.


     Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandolo alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nzoka Wilaya ya Momba mkoani humo,pichani kati ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbozi Mh Godfrey Zambi.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ileje Mh.Janet Mbene,mara baada ya kuwasili wilayani humo kuhutubia mkutano wa kampeni.
  Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
  Wananchi wa wilaya ya Ileje wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Ileje mjini wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wilayani humo.

  PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Ndg.Robert Gondwe wa Dar es Salaam,anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Geoffrey Boardington Gondwe kilichotokea jana(25.08.2015).

  Ataangwa kesho(27.08.2015) kwake Kunduchi saa 6 mchana. Mazishi yatafanyika katika   makaburi ya Kinondoni saa kumi jioni.

  Sisi tulimpenda, lakini BWANA alipenda zaidi. Jina lake BWANA na lihimidiwe...
  AMINA!

  0 0  0 0


  0 0

  Mdau wa Globu ya Jamii Leticia Mutaki (kati) wa SUMATRA Dar es salaam akifurahia na wadau baada ya kulamba nondozzzz yake ya Master of Law in Martime International huko nchini MALTA hivi karibuni. Hongera sana mdau Leticia.

  0 0

  Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gate imekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)kuangalia namna ya inavyoweza kusaidia upatikanaji wa Takwimu Bora za Kilimo nchini Tanzania. 
   Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa mazungumzo hayo jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Taasisi hiyo anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo Bw. Stanley Wood amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali Barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizopewa kipaumbele na kunufaika na taasisi hiyo. 
   Amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya, taasisi hiyo inaangalia uwezekano wa kusaidia upatikanaji wa takwimu bora za kilimo. 
   " Juhudi kubwa imefanywa na Tanzania katika kufanikisha mambo mbalimbali, kwa upande wetu tumeona vipaumbele vilivyopo ili tuweze kuona namna tunavyoweza kutoa mchango wetu kusaidia ukusanyaji wa takwimu Bora za kilimo , kikubwa ni kuendelea kujenga ushirikiano wa kuwezesha ufanisi wa tafiti mbalimbali" Amesema. 
   Wood ameeleza kuwa taasisi ya Bill na Melinda Gates imekuwa ikichangia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika kupitia mashirika ya kimataifa yanayohusika na utoaji wa huduma kwa umma na kuitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika zinazonufaika na miradi hiyo. Amesema taasisi ya Bill na Melinda Gate kwa kipindi kirefu imekuwa ikitoa kipaumbele kusaidia miradi ya afya hasa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi, kusaidia huduma za Afya ya mama na mtoto pamoja na kuweka mkazo katika kuimarisha huduma za maji safi na maji Taka Barani Afrika.
   Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.

   Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za  kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
  Mtakwimu mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam. Picha na Veronica Kazimoto.

  0 0


  0 0

  Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka mtandao wa matapeli wanaojipatia fedha kutoka kwa wananchi kwa udanganyifu kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi hasa katika kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi lipo katika mchakato wa ajira.

  Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linatoa tahadhari kwa  wananchi wote kuwa makini na mtandao wa matapeli hao na kwamba, mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na unafuata taratibu na kanuni za Jeshi la Polisi, hivyo, Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi hilo wafuate maelekezo yaliyoainishwa katika matangazo ya ajira yaliyotolewa kupitia vyombo vya habari pamoja na tovuti ya Polisi ya www.policeforce.go.tzili kuepuka usumbufu na utapeli wa  wahalifu hao. 
  Tunawakumbusha vijana wote waliochaguliwa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa kabla hawajaripoti shule ya Polisi Moshi. Hivyo, yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa kamanda wa mkoa anakotoka hatapokelewa chuoni.

  Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

  Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.


  Imetolewa na:

  Advera John Bulimba-SSP

  Msemaji wa Jeshi la Polisi.


  Makao Makuu ya Polisi.         


  0 0

  Baadhi ya wanafunzi waliopata vyandarua katika  programu ya Rais ya uhamasishaji wa matumizi ya vyandarua kuzuia malaria kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na ugawaji wa vyandarua bure kupitia mashuleni imeanzia katika  mikoa ya Lindi , Mtwara na Ruvuma mwezi huu.
  Waalimu wakijiandaa kugawa vyandarua katika shule mkoani Lindi
  Wanafunzi wakichukua vyandarua kwa zamu
  Wanafunzi wakifurahi kwa kupatiwa vyandarua vya bure

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini anayemaliza muda wake Mhe Ali Davutoglu aliyefika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 27,2015
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini anayemaliza muda wake Mhe Ali Davutoglu aliyefika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 27,2015

  0 0

   Mhe. Jaji Lawrence Gidudu, Rais wa Chama cha Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) (wa tatu kushoto) akiendesha Mkutano wa Waheshimiwa Majaji na Mahakimu wa Jumuiya hiyo, Mkutano huo unahitishwa leo baada ya wajumbe hao kukubaliana kwa pamoja kuoresha huduma ya utoaji haki kwa umma. Wengine ni Wajumbe wa Mkutano huo kutoka Tanzania, Kenya na Uganda
   Baadhi ya kundi la Washiriki wa Mkutano wakiwa katika mkutano huo mapema leo, Mkuano huo uanatarajiwa kumalizika leo
   Mhe. Robert Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza (wa kwanza kushoto) pamoja na Washiriki wengine wa Mkutano wakiwa katika Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Malaika uliopo jijini Mwanza.
   
  Wajumbe wa Mkutano wakiwa nje ya banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Hoteli ya Malaika, lengo la kuwepo kwa banda hilo la Maonesho ni kuwaeleza washiriki wa Mkutano huo juu ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama ya Tanzania lenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. Picha na Mahakama. 

older | 1 | .... | 953 | 954 | (Page 955) | 956 | 957 | .... | 3272 | newer