Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MGOMBEA MWENZA CCM SAMIA SULUHU HASSAN AANZA KAMPENI KILIMANJARO LEO

$
0
0

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan akilakiwa na wananchi baada ya kuwasili Ofsi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro leo.
 Mbombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCMSamia Suluhu Hassan, akimtazama mtoto, alipokagua Kituo cha Afya cha Hedalu wilayani Same mkoani Kilimanjaro leo
 Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na Kijana wa CCM baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro leo
 Mama Suluhu Hassan akisani kitabu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro. Kulia ni Mohammed Juma, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro
Mama Samia Suluhu akiwasili uwanja wa mikutano Shule ya Msingi Hedalu
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Hedaru, wilayani Same mkoani Kilimanjaro. Picha zote na Bashir Nkoromo, Same

WANAFUNZI 94 WAHITIMU ELIMU YA MSINGI SHINNING SCHOOL SONGWE MBEYA

$
0
0

Wahitimu wa elimu ya msingi katika shule ya kimataifa ya Shinning School  Songwe Mbeya wakiwa katika maandamano ikiwa ni sehemu ya kufurahia tukio hilo mwishoni mwa wiki mkoani Mbeya.

Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya kimataifa ya Shinning School iliyopo nje kidogo ya mji wa mbeya eneo la songwe kiwandani Amani Kajuna ambaye pia ni Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya akizungumza katika hafla hiyo.
Mmoja wa wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi  2015  shule ya kimataifa ya Shinning School  akionesha ushahidi  wa cheti chake mara baada ya kutunukiwa na uongozi wa shule hiyo katika mahafali hayo ambayo yamefanyika shuleni hapo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


UFAFANUZI KWA KUHUSU KASORO ZA BVR NA UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

$
0
0
Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) ulikamilika tarehe 04/08/2015 katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.
 
Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata (processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Mfumo wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR Kit yoyote. Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
Kwa kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062 Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa taarifa.
Baadhi ya vituo kutokuwa na Wapiga kura.
Tatizo hili linasababishwa na maombi ya kuanzishwa kwa vituo wakati zoezi la Uandikishaji limeanza, baadhi ya vituo hivyo havikutumika wakati wa Uandikishaji kama ilivyokusudiwa kwa sasa Tume inafanyika kazi ya kuhamisha Wapiga Kura na kuwapeleka katika vituo hivyo ili kuwapunguzia umbali mrefu kutoka kwenye vituo walivyojiandikisha wakati wa zoezi la Uandikishaji, kazi hii Tume inaendelea kuifanya kwa kushirikiana na watendaji wa Kata katika Halmashauri husika.
Baadhi ya Vituo kuwa na Wapiga Kura wachache au Wengi katika Vituo vya Uandikishaji.
Tatizo hili pia lilisababishwa na vituo kuongezwa wakati zoezi la Uandikishaji limeanza. Kabla ya kuongezwa vituo katika BVR kutokana na hamasa ya Wapiga Kura Kujiandikisha Wapiga Kura hao walianza kujiandikisha katika vituo vingine na baada ya kuongeza vituo katika BVR vituo vilivyoongezwa viliendelea kufanya Uandikishaji kwa siku mbili au tatu za mwisho hivyo kuonekana kama vina Wapiga Kura wachache, kasoro hiyo inarekebishwa pia kwa kusaidiana na watendaji wa Kata husika ili kuwahamisha Wapiga Kura waliojiandikisha katika vituo kabla ya kuongeza kwenye BVR vituo vilivyoombwa kuongezwa na kupelekwa kwenye vituo karibu na maeneo wanayoishi.
Wapiga kura kuandikishiwa katika Mfumo wa Mafunzo.
Katika taarifa zilizochakatwa imebainika kuwa baadhi ya Wapiga Kura waliandikishwa kwa kutumia mfumo wa mafunzo uliowekwa katika katika BVR kit iliyotakiwa kutumika wakati wa mafunzo tu, Usahihi wa taarifa za Biometric za Wapiga Kura hao kuwa sahihi lakini baadhi ya taarifa nyingine kuhitaji marekebisho kutoka katika fomu za Uandikishaji zilikizojazwa. Kazi hiyo inaendelea kufanyika katika kitu cha maandalizi ya Daftari kwa kuwa fomu zote za uandikishaji zimeishafika. Marekebisho hayo yalichelewesha kidogo baadhi ya taarifa katika madaftari yaliyowekwa wazi. Kazi ya Kurekebisha kasoro hizo zimeendelea kurekebishjwa na kabla ya tarehe 05/09/2015 kasoro zote zitakuwa zimerekebishwa.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura kutochukuliwa taarifa zao katika BVR Kit.
Tatizo hili lilisababisha baadhi Wapiga kura kutoonekana katika vituo walivyojiandikisha, zipo baadhi ya BVR Kit ziliibiwa na zikafanyika jitihada za kung’oa baadhi ya vifaa katika BVR kama vile Laptop na vifaa vingine. Zipo BVR mbili (2) kati ya BVR Kit 8000 ziliibiwa na walioiba walifanya jitihada za kuiba baadhi ya vifaa katika BVR kit hizo, BVR Kit hizo zilipatikana lakini zikiwa katika hali mbaya ya Uaribifu hivyo kushidwa kuondoa taarifa za Wapiga Kura mara moja, kwa kuwa Tume iliweka vifaa mahususi inapojitokeza changamoto kama hiyo kutopoteza taarifa za Wapiga Kura, chombo hicho kinachohifadhi taarifa za Wapiga Kura mara inapotokea uaribifu mbukbwa hususan wa kompyuta kuweza kupata taarifa za Wapiga Kura bila tatizo, Tume tayari imekwisha pata vifaa vilivyokuwa vimeifadhi taarifa za Wapiga kura na tayari taarifa hizo zinaingizwa katika mfumo wa kuchakata taarifa za Wapiga Kura.
Kata Mpya.
Kwa mujibu wa sheria OWM ­ TAMISEMI ndiyo yenye hadhi ya kupandisha na kugawa maeneo ya kiutawala ili kuchochea maendeleo ya haraka kwa wananchi wake. Mabadiliko hayo ya mipaka ya kiutawala yanahitaji kuhuishwa na Tume katika Mifumo yake ili kuwezesha chaguzi kufanyika na hasa chaguzi za madiwani, hivyo yanafanyika marekebisho ya kuhamisha kuweka vituo na Wapiga Kura katika maeneo mapya ya kiutawala yaliyoanzishwa, ikiwa ni pamoja na:­ Vitongoji, Mitaa,Vijiji, Kata na Halmashauri.
Baadhi ya Taarifa za Wapiga Kura taarifa zao kukosewa na BVR Kit Opereta wakati wa Uandikishaji.
Baadhi ya Wapiga kura taarifa zao zilikosewa na BVR Opereta wakati wa Uandikishaji hivyo kuhitaji marekesho na kupatiwa kadi mpya. Tume ilipeleka BVR Kit katika Halmashauri zote wakati wa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura, ili kufanya marekebisho ya taarifa za Wapiga kura pale panapohitajika. Marekebisho yamefanyika Tume inategemea Taarifa hizo zitafika na kuingizwa katika mifumo ili kupata taarifa sahihi.
Wapiga Kura Kujiandikishia katika maeneo tofauti na maneo wanayoishi.
Baadhi ya Wapiga Kura walijiandikisha katika maeneo tafauti na maeneo wanyaoishi, hivyo kuhitaji kuhamisha taarifa zao, tatizo hili limebainika katika maeneo mengi ya mjini, hasa kwa Wapiga Kura kutaka kuwahi kupata kadi za Mpiga kura, kasoro hii imeendelea kurekebishwa wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.
Uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
Uwekaji wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ni takwa la kisheria, kifungu cha 11a cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 kinaitaka Tume kuweka wazi Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uhakiki wa Taarifa na kurekebisha kasoro zozote zinalizojitokeza.
Ili kuhakiki taarifa katika Daftari la Awali la Wapiga Kura wananchi wanatakiwa kufika katika Ofisi za kata ili kuweza kuangalia kama majina yao yapo katika Daftari, na ikiwa Taarifa zao ni sahihi mfano Jina, Jinsia, Tarehe ya kuzaliwa na Kituo chake cha kujiandikishia, Aidha, kwa Wapiga kura waliohama kata au jimbo moja kwenda kata au jimbo lingine wanatakiwa kuhamisha taarifa zao.
Zoezi hili la uhakiki lilianza rasmi tarehe 07/08/2015 katika Mikoa mbali mbali na limekuwa likiendelea hadi sasa ili kuhakikisha kila Mpiga kura aliyeandikishwa kupiga kura anaweza kupiga kura bila usumbufu wowote.
Katika zoezi hili Tume imeweka utaratibu wa kuwaondoa watu wote waliojiandikisha katika Daftari ambao siyo raia wa Tanzania, ambapo mchakato huo unaishia katika mahakama ya wilaya. Ili kasoro hii iweze kuondolewa Tume inahitaji kwa kiasi kikubwa Ushirikiano na wananchi wanaoishi nao ili kuwawekea pingamizi na waweze kuondolewa katika Daftari, ni ukweli kwamba iwapo wananchi watawaficha na kutowawekea pingamizi tatizo hili litakuwa gumu kwa Tume kulitatua.
Kasoro mbalimbali zilizobainika wakati wa Uandikishaji Tume itahakikisha inazirekebisha ili kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na Daftari sahihi na la kuaminika.
Imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

BBC DIRA YA DUNIA

TANZIA: Jaji Mkuu afiwa na Mwanawe

$
0
0

Mheshimiwa Mohamed Chande Othman,Jaji Mkuu wa Tanzania anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mkubwa, Said Mohamed Chande Othman (24), kilichotokea katika hospitali ya Aga Khan jijini DAr es salaam tarehe 24 Agosti,2015.


Marehemu Said Othman alikuwa ni mfanyakazi katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).



Mazishi yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 25 Agosti,2015 saa kumi jioni huko Chumbageni, Tanga.



Inna lillahi wainna ilayhi raajiun.

NHIF yateta na NIDA kuhusu vitambulisho

$
0
0
Na Grace Michael

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekutana na Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na changamoto katika suala la utambuzi wa watumiaji wa huduma za vitambulisho.

Hatua hiyo ya NHIF kukutana na uongozi huo inakusudia kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wake ambao tayari wana vitambulisho vya Taifa.

Akizungumzia hatua hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando, amesema Mfuko wake umeona kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu na rasilimali chache zilizopo katika eneo hilo kwa manufaa ya wote.

“Tumeona ni vyema tutakakutana na wenzetu wa NIDA ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wetu kupitia vitambulisho vya Taifa lakini pia kubadilishana uzoefu katika uandaaji wa vitambulisho ambavyo ni vya kisasa zaidi,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Mifumo Habari wa NHIF, Bw. Ali Othman amesema kuwa hatua hiyo ni fursa kubwa kutokana na ukweli kwamba kitambulisho cha Taifav kitamuwezesha mwananchi kutumia huduma mbalimbali.

“Kitambulisho cha Taifa kinajibu nani ni nani, anakaa wapi, anamiliki nini na anafanya nini taarifa ambazo ni za muhimu sana katika kuuwezesha Mfuko kutambua kila kundi na namna ya kuhamasisha kuwa na Mfumo wa bima ya afya kulingana na kundi husika,” anasema.

Ametumia mwanya huo kuushukuru uongozi wa NIDA KWA KUUSHIRIKISHA Mfuko katika hatua za awali za uandaaji na ubunifu wa vitambulisho vya Taifa jambo ambalo litarahisisha sana utekelezaji wa hatua hii ya sasa.

Bw. Othman amesema kuwa kwa kutumia teknolojia ya Mifumo Habari kuna uwezekano mkubwa wa wanachama wa NHIF kutumia vitambulisho vya Taifa sanjari na NHIF katika upatikanaji wa huduma ikiwemo udhibiti wa mianya ya udanganyifu hivyo Mfuko unatarajia kwa kila hali kuanza kutumia vitambulisho vya NIDA katika utambuzi wa wanachama wake.

MKUU WA MKOA WA ARUSHA FELIX NTIBENDA KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA 10 LA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 10 la vyombo vya habari  vya mkoa wa Arusha. ambalo litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.

Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli jana  mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar  na Katibu wa TASWA Arusha,  Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

Omar alisema Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo ni kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na   timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira wa pete.

Alisema mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T) Ltd.

Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.

Akizungumzia tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL itaendelea kushirikiana na wanahabari.

Awali Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio ,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.

 Alisema kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha vile vile  kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi  mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo
Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma

JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 - JUMATANO AUGUST 26, 2015


Balozi mteule wa Switzerland awasilisha nakala za Hati za Utambulisho

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, leo Tarehe 25-08-2015 ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Bernard Membe akizungumza na Balozi Mteule wa Switzerland hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MASHINDANO YA KUTUNISHA MISULI KUFANYIKA AGOSTI 29, 2015 JIJINI DAR

$
0
0
Washindi wa mwaka jana wa Mashindano ya kutunisha misuli (The Most Musicular Man Tanzania 2014) wa kwanza kutoka kushoto ni msindi wa pili, Omary Lyombe, mshindi wa kwanza Mohamed Nouma (katikati) na mshindi wa tatu, Erick Majura wakionyesha utunishaji misuli wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Gymkana jijini Dar es Salaam leo. Mbele yao (walioketi) ni waandaaji pamoja na wadhamini wa shindano hilo
 Mratibu wa mashindano ya kutunisha misuli, Mohamed Ali akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) moja tuzo ya heshima atakayopewa mshindi wa kwanza wa mashindano hayo yatakalofanyika Agosti 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere mjini Posta.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Torque Tyres, Mohamed Dewji, ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo ya kutunisha misuli akizungumza na waandishi wa habari.

WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM AZINDUA BODI YA PPF NA MAFAO MAPYA YA MFUKO

$
0
0

 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja, mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Sara Haule ikiwa ni malipo ya fao la uzazi wakatinwa uzinduzi wa bodi mpya ya PPF, sambamba na uzinduzi wa fao hilo la uzazi, Jumanne Agosti 25, 2015.

 Waziri Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya uzinduzi
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ukaribisho na utambulisho nwakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mfuko, sambamba na uzinduzi wa Fao la Uzazi, ambapo wanachama wawili wa Mfuko, Sara Haule na Caroline Kiswaga, walilipwa shilingi milioni 1 kila mmoja kama malipo ya fao hilo.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, akitoa hotuba yake
 Waziri Saada Mkuya Salum, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Ramadhan Kijjah, na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya PPF



 Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za PPF, na Mamenejawaliohudhuria hafla hiyo, 
 Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku, akielezea namna fao hilo lilivyozingatia Mwanachama na Mwenza wake
 Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF
 Waziri Saada Mkuya akimpongeza Mwanachama wa PPF, Caroline Kiswaga, baada ya kumkabidhi shilingi milioni moja ikiwa ni malipo ya fao la uzazi
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah, (kushoto), akimkabidi kadi mpya ya uanachama wa Mfuko nhuo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya SDalum, wakati wa uzinduzi wa bodi na fao la uzazi, hafla iliyofanyika makao makuu ya PPF jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2015.

 Waziri Saada Mkuya, (kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, 
 Waziri Mkuya akiteta jambo na Erio wakati wa hafla hiyo
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,  Elihuruma Ngowi, (kulia), akifurahia jambo wakati waziri wa fedha Saada Mkuya Salum, (kushoto), akimtania Mwanachama wa PPF, Sara Haule, baada ya kupatiwa malipo ya shilingi milioni moja kama fao la uzazi

TANZIA

$
0
0

Ndugu T'shombe Gilbert Abwao anasikitika sana kutangaza kifo cha Binti yake wa kwanza Marsella Gilbert Abwao, mkuu wa George na Chiku Abwao ,Dada wa Pauline, Pendo na Issac kilichotokea jana saa 9 mchana huko Shinyanga.
Kwa kweli tuna huzuni kubwa na hakuna maneno ya kuelezea ni jinsi gani tulivyo na huzuni ila ni mioyo yetu tu ndo yaweza kuelezea.
TWAMSHUKURU  MWENYEZI Mungu kwa yote kwanni HAWAZI KUKUPA  MSALABA USIOWEZA KUUBEBA.
Na kwa KWAKE BWANA  hakuna kilichoharibika.
Tunaomba aiweke ROHO YAKE mahali pema PEPONI.
AMINA.

TANGAZO LA KIFO TOKA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

$
0
0
  





































Bodi  ya Ushauri, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanasikitika  kutangaza kifo cha  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA,   Mhandisi Lambert W. Ndiwaita  kilichotokea   tarehe 20/08/2015  katika  Hospitali  ya Nairobi,  Kenya.  
Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake mjini Bukoba  tarehe 25/08/2015.
Mhandisi  Lambert Ndiwaita (64)  alikuwa ni mmoja wa wataalamu waliobobea katika masuala ya  usafiri wa anga  kitaifa na kimataifa. Katika kipindi cha uhai wake ametoa mchango mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na nchi  nyingine duniani.
Alianza shughuli zinazohusiana na  usafiri wa anga mwaka 19971  alipoajiriwa na iliyokuwa  Wizara ya  Ujenzi  kama  Mhandisi  Msaidizi na baadaye alipanda hadi   kufikia cheo cha  Mhandisi Mkuu  (Chief Engineer) akishughulikia masuala ya barabara na  viwanja vya ndege.
 Mwaka 1993 alikwenda kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini Botswana kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mwaka 1994 aliajiriwa na  Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga  International Civil Aviation Organization (ICAO)  kusimamia  masuala ya  viwanja vya ndege (Aerodrome & Ground Aids) kwa eneo  la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika ofisi za ICAO  zilizopo jijini Nairobi, Kenya.
Mhandisi Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya Uhandisi (Bsc Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978 alihitimu  masomo Shahada ya Uzamili (Msc in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha Califonia, Berkley, nchini Marekani akijitikita zaidi katika masuala uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.

Marehemu Lambert Ndiwaita atakumbukwa  na  wadau wa usafiri wa anga nchini na duniani kwa  mchango  mkubwa katika  maendeleo ya sekta hiyo  ambapo  kwa hapa nchini akiwa  Mwenyekiti wa Bodi  ya TAA  amechangia   kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa viwanja  kadhaa  vikiwemo Mwanza, Tabora, Kigoma, Songwe,Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere  (JNIA).

Mungu ailaze roho ya marehemu  mahala pema peponi.


AMINA

Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi 
Mkuu-TAA.

24th AUGUST, 2015

Final Report of General Purpose on the Eac Creative and Cultural Industries Bill 2015

$
0
0
Hon Shyrose Bhanji takes the floor in support of the Bill on Creative and Cultural Industries Bill, 2015
Hon Judy Pareno contributes to the debate this afternoon
Uganda's EAC Minister, Hon Shem Bageine during debate today

Hon Dr. James Ndahiro, mover of the Private members Bill on EAC Creative and Cultural Industries Bill, 2015


Rais Kikwete ashiriki mazishi ya Mtoto wa Jaji Mkuu mjini Tanga

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande wakati Rais alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria mazishi ya marehemu.
 Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni Tanga leo jioni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said Mohamed Chande wakati ya mazishi yaliyofanyika katika eneo la Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman.
 Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo katika kaburi la mrehemu Said Mohamed Chande wakati wa mazishi yaliyofanyika huko Chumbageni Tanga.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya marehemu Said Mohamed Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofanyika katika makaburi ya familia huko Chumbageni Tanga leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman(aliyesimama pembeni ya Rais) kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande mjini Tanga. Picha na Freddy Maro

MGOMBEA URAIS DR MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA KAMPENI RUVUMA KUANZIA AUGUST 30

$
0
0
Picha kutoka maktaba

MGOMBEA Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dr. John Magufuli anatarajiwa kupokelewa na mamia ya wananchi wakiwemo wanachama wa chama cha mapinduzi katika kijiji cha Igawisenga wilayani Songea mkoa wa Ruvuma akitokea mkoa wa Njombe  tayari kuanza kampeni mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama cha mapinduuzi mkoani Ruvuma Mwenyekiti wa  kamati ya maandilizi ya kampeni mkoani Ruvuma ya mgombea uraisi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani Ramadhani Kayombo alisema kuwa Dr. Magufuli na msafara wake unatarajiwa kupokelewa Agost 30 mwaka huu majira ya asubuhi huko katika kijiji cha Igawisenga.

Kayombo alieleza kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani wanafanyiwa kampeni za kistaarabu katika kipindi chote cha kampeni ambapo mgombea uraisi Dr. Magufuli anatalajia kufanya ziara za kampeni katika wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru ambako atamaliza ziara septemba 02 mwaka huu na kuendelea na ziara mkoani Mtwara.

Alisema kwa kuwa wananchi wengi wana imani na chama cha mapinduzi ambao wanahitaji kumuona na kumsikiliza  hivyo amewataka wajitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni itakayofanyika wakati Dr. Magufuli akiwa mkoani Ruvuma na amewaomba kuwa na mshikamano wa pamoja katika kuhakikisha kuwa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu kinapata ushindi wa kishindo kwa mgombea uraisi, wabunge na madiwani na si vinginevyo.
 Na Jamvi la Habari Songea.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VYAMA VYA SIASA KUZINGATIA RATIBA YA KAMPENI YA UCHAGUZI WA RAIS KWA KUFANYA MIKUTANO KWA TAREHE, SEHEMU NA MAHALA KWA MUJIBU WA RATIBA

BBC DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI

Dkt. Shein afanya ziara Pemba

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Karume katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa majisafi na salama katika kijiji cha Taif wete kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuifungua miradi mbalimbali ya Serikali kisiwani humo, mradi uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha Ndoo ya Maji Mwajuma Ahmed Abdalla baada ya kufungua Mradi wa Maji safi na Salama katika kijiji cha Taif Wete Pemba Mkoa wa Kaskazini leo akiwa katika ziara ya kuifungua miradi mbalimbali ya Maendeleo, mradi ambao uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua mfereji kama ishara ya uzinduzi wa Mradi wa majisafi na salama katika kijiji cha Taif wete kaskazini Pemba leo akiwa katika ziara ya kuifungua miradi mbalimbali ya Serikali kisiwani humo,mradi uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika ADB. Picha na ikulu, Zanzibar.

TAASISI YA BILL NA MELINDA GATE YAANGALIA UWEZEKANO WA KUSAIDIA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA KILIMO NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Aron Msigwa

Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gate imekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)kuangalia namna ya inavyoweza kusaidia  upatikanaji wa Takwimu Bora za Kilimo nchini Tanzania.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanyika kwa  mazungumzo hayo jijini Dar es salaam, Afisa Mwandamizi wa Taasisi hiyo anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo Bw. Stanley Wood amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali Barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika  zilizopewa kipaumbele na kunufaika na taasisi hiyo.

Amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya, taasisi hiyo inaangalia uwezekano wa kusaidia upatikanaji wa takwimu bora za kilimo.

" Juhudi kubwa imefanywa na Tanzania katika kufanikisha mambo mbalimbali, kwa upande wetu tumeona vipaumbele vilivyopo ili tuweze kuona namna  tunavyoweza kutoa mchango wetu kusaidia ukusanyaji wa takwimu Bora za kilimo , kikubwa ni kuendelea  kujenga ushirikiano wa kuwezesha ufanisi wa tafiti mbalimbali" Amesema.

Wood ameeleza kuwa taasisi ya Bill na Melinda Gates imekuwa ikichangia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo Barani Afrika kupitia mashirika ya kimataifa yanayohusika na utoaji wa huduma kwa umma na kuitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika  zinazonufaika na miradi  hiyo.

Amesema taasisi ya Bill na Melinda Gate kwa kipindi kirefu imekuwa ikitoa kipaumbele kusaidia miradi ya afya hasa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi, kusaidia huduma za Afya ya mama na mtoto  pamoja na kuweka mkazo  katika kuimarisha huduma za maji safi na maji Taka Barani Afrika.
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia Sera na maendeleo ya kilimo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates Bw. Stanley Wood akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam mara baada ya kufanyika kwa kikao cha mazungumzo na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) nchini Tanzania kuangalia uwezekano wa taasisi hiyo kusaidia miradi ya ukusanyaji wa Takwimu za kilimo nchini Tanzania.Kushoto kwake ni Mratibu wa miradi wa Taasisi hiyo Bi.Bhramar Dey.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu umuhimu wa takwimu za Kilimo nchini Tanzania na mikakati ya Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha upatikanaji wa Takwimu za kilimo nchini.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi hiyo Bw.Morrice Oyuke.
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof.Innocent Ngalinda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya chuo anachokiongoza katika kutoa elimu kwa watakwimu wa kilimo nchini Tanzania na mpango wa chuo hicho kuimarisha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za kilimo kwa kutumia wataalam wanaozalishwa.
Mtakwimu mwandamizi kutoka Benki ya Dunia Bi.Elizabeth Talbert( kulia) na Meneja wa Idara ya Viwanda na Ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Joy Sawe wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wawakilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Bill na Melinda Gates jijini Dar es salaam. Picha na Veronica Kazimoto.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images