Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

cheka kuzipiga uingereza Sept 19

0
0
Na Mwandishi wetu

Bondia nyota nchini wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka atapigana na bondia wa Uingereza, Martin Murray katika pambano maalum lisilo la ubingwa la uzito wa Super Middle.

Pambano hilo limepangwa kufanyika mjini Manchester Septemba 19 na maandalizi yake yamekwisha kamilika.
Meneja mpya wa bondai huyo, Juma Ndambile alisema kuwa Cheka ataondoka hapa nchini Septemba 15 kwenda Uingereza kwa ajili ya pambano hilo la raundi 10.

Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security alisema kuwa ameamua kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Cheka ili kuresha heshima yake katika mchezo huo na pambano la Uingereza ni la mtoano kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Dunia.

Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa. Alisema kuwa endapo atashinda pambano hilo, atasaini mkataba mwengine za zaidi ya dola 25,000 ili kupigana pambano la tatu.

“Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.

Cheka alisema kuwa amefurahi sana kupata meneja mpya ambaye tayari amemtafutia pambano nje ya nchi na sasa imebakia kwake ni kufanya kazi tu. “Ndambile amenilipia kambi ya zaidi ya  Sh  milioni 2 hapa jijini, nakaa mimi na kocha wangu, naahidi kufanya vyema kwenye pambano hilo,” alisema Cheka.

RAIS KIKWETE AWASILI MKOANI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA SEKTA YA BARABARA

0
0
 Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Arusha wakimkaribisha kwa shangwe Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ttayari kufungua Mkutano wa nne wa mwaka wa wadau wa sekta ya barabara chini ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa unaofanyka katika hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha.
 Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi alipowasili kata ya Ngurdoto Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Barabara wa TAMISEMI uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto wilayni Arumeru Mkoani Arusha leo jioni.(picha na Freddy Maro).

mzinga: Daladala laingia mtaroni

0
0
Kamera yetu, leo imeinasa taswira hii ya Daladala likiwa limepiga mweleka na kuingia mtaroni, lilipokuwa likijarimu kulikwepa gari lingine lililokuwa likipita eneo hilo la Mbagala Charambe, Jijini Dar, Hakuna aliejeruhiwa katika ajali hiyo.

Zaidi ya vijana 1000 wapata mafunzo bora ya Kilimo

0
0
Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture” iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Kushoto ni Doris Chaula na Faraja Alex ambao ni washiriki wa semina hiyo.
Mkulima wa Mkoa wa Arusha Faraja Alex(kulia)aliyeshiriki katika semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture”akisalimiana na Maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(katikati)wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Anayeshuhudia kushoto ni mshiriki wa semina hiyo Doris Chaula.
MWenyekiti wa Taasisi ya AMSHA,Biubwa Ibrahimu(katikati)akimsikiliza jambo maneja wa Mradi wa Kilimo Klabu wa Vodacom Tanzania, Frank Madebwe(kushoto) wakati wa Semina ya Vijana iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam iliyohusu masuala ya Kilimo na biashara ”Youth and Agriculture” iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya kilimo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya kilimo klabu,Kulia ni mshiriki wa semina hiyo Faraja Alex.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

TANGA CEMENT YATOA SOMO LA UPANDAJI MITI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA ROSMINI

0
0
 Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Nje  wa Tanga Cement,Bi. Mtanga Noor (kulia) akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Rosmini ya mjini Tanga wakishiriki zoezi la kupanda miti katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na elimu kwa vitendo kuhusu namna bora ya kupanda miti. Miti 316 ilipandwa katika hafla hiyo iliyofanyika Pongwe mkoani Tanga jana.
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Rosmini ya mjini Tanga wakimwagilia maji miti waliyoipanda katika hafla ya upandaji miti iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na elimu kwa vitendo kuhusu namna bora ya kupanda miti. Miti 316 ilipandwa katika hafla hiyo iliyofanyika Pongwe mkoani Tanga jana.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Rosmini ya mjini Tanga wakishiriki zoezi la kupanda miti katika hafla ya upandaji miti iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na elimu kwa vitendo kuhusu namna bora ya kupanda miti. Miti 316 ilipandwa katika hafla hiyo iliyofanyika Pongwe mkoani Tanga jana.

FILIKUNJOMBE NJIA NYEUPE UBUNGE WAPINZANI WAKE WAINGIA MITINI

0
0
Deo  Filikunjombe (CCM)

Na  matukiodaimaBlog Ludewa 
ALIYEKUWA  mbunge   wa  jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe (CCM)  amepita  bila kupingwa  baada ya  mgombea  wa chama  cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Barthomew Mkinga  kushindwa  kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Bw  Wiliam Waziri alisema  jana   kuwa Mgombea wa Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge hivyo  kumkabidhi  barua  rasmi Filikunjombe   ya kupita  bila  kupingwa
Waziri alisema   kwamba Kati ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni Mgombea wa CCM, Bw. Filikunjombe pekee;

Kuwa Wagombea wa DP na TLP walishindwa  kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi. 

Mgombea   huyo  wa Chadema  aliyereja  fomu  ya  wadhamini  bila  kujaza tarehe  ,mwezi  wala mwaka ambao uchaguzi  mkuu utafanyika .

DK.SHEIN ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR

0
0
 Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akiwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mkewe Mama Mwanamwema  Shein wakisalimiana na Viongozi walipofika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupata baraka za Wazee wa Chama  kabla ya kuelekea kuelekea katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ZEC  Bwawani Hotel Mjini Unguja kuchukua fomu  leo.


Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akiwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi walipofika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupata baraka za Wazee wa Chama  kabla ya kuelekea kuelekea katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ZEC  Bwawani Hotel Mjini Unguja kuchukua fomu  leo.
[Picha na Ikulu.]


MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA JIJINI DAR YAZINDULIWA

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn  Mworia akiongea  na waandishi wa habari kuhusiana na  utoaji wa semina  mbalimbali wanazozifanya kama wadhamini wakuu  kwa waendesha badabado  wakati wa  maadhimisho ya wiki ya Usalama barabaranijijini dar es Salaam yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Kulia kwake ni Mwenyekiti wa  waendesha bodaboda Wilaya ya Kipolisi Buguruni Kanda ya Tabata, Ramia Mazwela.
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova ( watatu kutoka kulia)  akiwa ameambatana  na Maofisa wa jeshi hilo kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya nenda kwa Usalama ikidhaminiwa na Vodacom Tanzania.


PSPF YATOA MSAADA WA MAGODORO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

0
0
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David Mfinanga, (Watatu kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (watatu kulia), wakati akipokea msaada wa magodoro 118 yaliyotolea wan Mfuko huo kwenye hafla fupi iliyofanyika chuon I hapo, Agosti 24, 2015. Magodoro hayo ni kwa ajili ya wanafunzi walioathiriwa na mogto uliozuka kwenye bweni kitalu B kule hosteli za Mabibo, Aprili mwaka huu 2015.

NA K-VIS MEDIA

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, leo Agosti 24, 2015, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa wanachuo walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli ya chuo hicho Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.

Akikabidhi msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David A. Mfinanga, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na ajali hiyo ya moto ambayo iliyotokea  kwenye bweni kitalu namba B na kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.

“Kwa kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni wanachama watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili wanafunzi waweze kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.

Akitoa shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF, kwa msaada huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo yatapelekwa kwa walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu waliyoyapata kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.

Kwa mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jingo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo 788, wakati linawaka moto.


 Profesa mfinanga (wapili kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya chuo mbele ya maafisa wa PSPF,  viongozi wa wanachuo na wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa hafla hiyo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

NMB MASTERCARD YAZINDULIWA RASMI KWA MKOA WA ARUSHA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Felix Tibenda (Pili kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker kwa uzinduzi wa NMB Mastercard kwa Mkoa wa Arusha na Kanda nzima ya Kaskazini.Wakishuhudia ni Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bw.Salie Mlay(kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Bw.Abdulmajid Nsekela.

LOWASSA APANDA DALADALA KUTOKA GONGO LA MBOTO MPAKA PUGU KAJIUNGENI JIJINI DAR LEO

0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi. 

MUZIKI MNENE BANGO MBEZI

0
0
Bwana E Mr Jimmy Jiam akiwa na swaga za hali ya juu wakati anampa zawadi  mshindi wa EFM Muziki Mnene Bango baada yakuona kuwa ameweka stika kwenye eneo lake la biashara  eneo la Mbezi Jijini Dar es salaam. 

 Mshindi mwingine wa EFM Muziki Mnene Bango na washabiki wa EFM wakipozi kidogo na kupiga picha na bwana E Mr Jimmy Jiam. Mshindi huyo alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye taksi  yake alikabidhiwa zawadi yake na bwana E.

 Bwana E akipozi na mashabiki wa EFM. mashabiki hao walikutwa wanasikiliza 97.3 EFM na wakamjulisha bwana E jinsi wanavyo ipenda EFM na ndio hapo wakapewa zawadi za t-shirt za EFM.

DK. SHEIN ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA URAIS WA ZANZIBAR LEO

0
0
Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk.Ali Mohamed Shein akiwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea fomu hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ZEC Jecha Salum Jecha katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo.

Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Ali Mohamed Shein akiwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akiwapungia mikono wananchi katika Gari maalum akitokea katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi ZEC Bwawani Hotel Mjini Unguja kuchukua fomu leo.[Picha na Ikulu.]

CHUO KIKUKU DODOMA KUMUENZI RAIS KIKWETE

0
0
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula akimkabidhi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi nakala ya kitambu kinachoelezea kwa kina historia ya Chuo Kikuu cha Dodoma.  Katika Maelezo yake,  Prof. Kikula amesema UDOM  imeamua kuweka katika maandishi historia nzima ya  Chuo hili ili kuepusha upotoshaji na upindishaji wa  ukweli na kwamba UDOM  inapanga kumuenzi Mhe. Rais Jakaya Kikwete  ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuanzishwa na hatimaye ujenzi wa UDOM. wengine katika picha kutoka kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Prof. Shaaban Mlacha anayesimamia masuala ya  mipango, fedha na utawala, Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi Ramadhan Mwinyi na Bi. Christina Silvester, Katibu wa Baraza.
Makamu Mkuu wa UDOM Prof. Kikula akimkabidhi nakala ya kitambu cha historia ya UDOM,  Prof. Estomih Mtui, M.D  anayefanya kazi  Weill Cornel Medical Collage, Prof. Mtui  ni moja kati ya  wana-Diaspora ambaye  amekuwa  kiungo kikubwa katika utafutaji na upatikanaji wa vifaa tiba ,vitabu na wataalam wa fani mbalimbali kwaajili ya kusaidia nchini Tanzania. baadhi ya  vifaa na vitabu ambavyo  Ujumbe wa   Makamu Mkuu wa UDOM wamevikagua vimepatikana kwa  juhudi za Prof. Mtui

Na Mwandishi Maalum, New York
Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM), kinatarajia kufanya hafla ya  aina yake ya kumuenzi Rais  wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa hali na mali uliopelekea kuanzishwa kwa Chuo   Kikuu hicho cha aina yake 

Tanzania na nje ya Tanzania.
Taarifa ya kusudio la  Chuo hicho kumuenzi Mh. Rais Kikwete imetolewa mwishoni mwa wiki na Makamu Mkuu wa  UDOM, Prof. Idris Kikula wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na   Mabalozi na Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika 

Umoja wa Mataifa.Profesa Kikula   na ujumbe wake   yuko  katika ziara ya kikazi nchini Marekani,  ziara iliyomfikisha  Jijini New York, ambapo   ujumbe ulipata fursa ya kukagua vifaa tiba na vitabu  vya kiada na ziada ambavyo vimetolewa na  wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na Tanzania.

JOTO LA ASUBUHI LA RADIO 93.7 EFM


NSSF, NEEC zaingia makubaliano ya ushirikiano leo Jijini Dar

0
0
MKURUGENZI wa Shirika Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Ramadhan Dau amewataka  madereva na wamiliki wa pikipiki za Bodaboda kuwa na utamaduni wa kurudisha mikopo wanayopata kupitia Zao ili iweze kuzungushwa kwa bodaboda wengine.

Dau ametoa rai hiyo leo wakati alipokuwa akitia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano kati NSSF na  Baraza la Taifa  la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).

“Hamkufanya makosa kujiunga Saccos, kwa kuwa nina imani mtapata nafasi ya kukopeshwa na mtapata maendeleo, hivyo ni matarajio yangu kuona kwamba yule bodaboda aliyepata mkopo siku moja nije kusikia anamiliki ndege,” alisema Dau.

Makubaliano hayo ya mkopo wenye thamani ya Shilingi bilioni moja yalitiwa saini na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa, huku akishuhudiwa na  wanachama wa Chama Cha Ushirika wa Akiba  na Mikopo Cha Wendesha Bodaboda Jijini Dar es Salaam.

Mkataba huo uliotiwa saini jana una lengo la kuisaidia serikali kutimiza wajibu wake kwa kuwasaidia vijana kutambua fursa na nafasi yao katika maendeo ya taifa, kama sehemu ya jitihada  za kuchangia  katika  kukabiliana  na tatizo la kuzalisha mali  kwa ajili ua ujenzi wa uchumi.

“Mkataba tunao saini leo ni moja  ya jitihada za kuchangia katika kukabiliana na tatizo hili. Kuanzishwa kwa programu hii kutasaidia vijana katika sekta hii ndogo ya usafirishaji kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kununua pikipiki zao wenyewe, kuanzisha au kuendeleza biashara nyingine na pia kupata huduma za matibabu na huduma nyingine zilizotolewa na NSSF,” alisema.

Fedha za  dhamana kwa ajili ya programu hiyo zitawekwa katika Benki ya Posta na NSSF itatumia  fedha zake kukopesha vijana kwa ajili ya kununulia pikipiki kwa lengo  la kufikia hesabu walizokubaliana na waajiri wao, matokeo yake kusababisha ajali mara kwa mara.

Akiweka wazi sifa na mashari ya wanachama ambao wataweza kukopesha ni wale ambao  watakuwa wako kwenye vyama kuweka na kukopa, Saccos ambavyo vimesajiliwa kisheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kulia) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (kushoto) wakitia saini hati ya mkataba wa utekelezaji wa program ya NSSF Boda Boda katika hafla iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa NSSF Water Front, Jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto), ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji wa NEEC, Edwin Chrisant, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Omari Issah, Mwenyekiti wa Dar es Salaam Bodaboda Saccos (DABOSA), Saidy Kagomba na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau wakibadilishana hati baada ya kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa programu ya NSSF Boda Boda katika hafla iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa NSSF Water Front, Jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Omari Issah.

Nyomi katika uzinduzi wa kampeni wa CCM Jangwani jijini Dar es salaam Jumapili Agosti 23, 2015

Uzinduzi wa Kampeni za CCM Jumapili viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam

0
0
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mhe Benjamin William Mkapa wakimnadi mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa hadhara uliovutia umati uliovunja rekodi kwa wingi katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es alaam Jumapili
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Kikwete na Rais Shein pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji joseph Sinde Warioba akimnadi mgombea wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiozungumza Jangwani 
Rais Mstaafu Mhe Benjamin William Mkapa akiunguruma Jangwani
 Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
Makongoro Nyerere akipiga saluti baada ya kusalimia umati huo
Kwa Picha zaidi BOFYA HAPA

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITEKA KATAVI LEO

MAGUFULI AITIKISA KATAVI,WAZIRI MKUU PINDA AMNADI KWA KISHINDO.

0
0
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akihutubia wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimtambulisha Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM, Dkt John  Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni  katika kata ya  Mishamo,wilayani Mpanda mkoani Katavi.
 Waziri Mkuu MizengO Pinda akimtambulisha Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli mbele ya umati wa watu waliofurika jioni ya leo kwenye uwanja wa Azimio mjini MPanda mkoani Katavi wakati wa muendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani humo leo.Chama cha CCM kimezindua kampeni zake jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho cha CCM
 Wananchi wakishangilia wakati  Waziri Mkuu Pinda alipokuwa akimnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa  Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi.
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wamefurika leo katika uwanja wa Azimio mjini MPanda wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jonh Pombe Magufuli kupitia chama cha CCM,mkoani Katavi.

Wananchi wa kata ya Katumba wilayani Nsimbo wakiwa wamekusanyika kwa wingi kumsikiliza Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata hiyo, wilayani Nsimbo mkoani Katavi 
Waziri Mkuu Pinda akimuelekeza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokwenda kuwahutubia wananchi wa Mpanda mjini kwenye kutano wa kampeni  mkoani Katavi.
   Sehemu ya umati wa Wananchi wa kata ya Mishamo,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni,wilayani Mpanda mkoani Katavi.

PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

NA  HAPA
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images