Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

IMPORTANT: THE BROADCASTING SERVICES (CONTENT) (THE POLITICAL PARTY ELECTIONS BROADCASTS) CODE, 2015


MKUTANO WA BARAZA KUU LA VIJANA WA CCM (UVCCM) JIJINI DAR ES SALAAM

Anthony Mavunde achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Dodoma MJINI

$
0
0
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma,Antony Mavunde akionesha fomu alizochukua za kugombea Ubunge katika jimbo hilo nje ya ofisi za Halmashauri ya Dodoma. 
 Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Antony Mavunde akipungia mamia ya mashabiki wakati akielekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Dodoma kwekuchukua fomu.
 Mavunde akifurahia jambo na Wafuasi wake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Dodoma Elizabeth Gumbo jana Mjini Dodoma.
MGOMBEA wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Anthony Mavunde amechukua fomu na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha analinda haki za wakazi wa mji wa Dodoma katika masuala ya ardhi.
 
Akizungumza na wanachi mara baada ya kuchukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Mavunde amesema akipata nafasi ya kuwa mbunge kupitia nafasi hiyo atakuwa mjumbe wa bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA),hivyo atahakikisha mamlaka hiyo inaboresha maisha ya watu na sio kuyadidimiza.

Aidha ameahidi kuimarisha sekta ya michezo ambayo imepewa kisogo katika Mkoa wa Dodoma.Michezo hiyo ni Pamoja na Mpira wa pete,Kikapu,Mpira wa mikono na Riadha,Mavunde alisema kama akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi suala la michezo kwake litakuwa ni la lazima na inapiga hatua.

"Mimi ni muumini wa michezo hivyo tofauti na soka nitatoa nafasi pia kwa michezo mingine ambayo imekuwa ikiipa sifa mkoa wa Dodoma ili vijana waweze kujikwamua na kuondokana na tatizo la ajira, "alisema

Alisema akipata nafasi ya kuwa Mbunge wa Dodoma basi cha kwanza atakachofanya ni kukutana na viongozi wote wa vyama vya michezo mkoani hapa ili kuweka kalenda za kisasa ambazo zitaendeleza michezo.

Mavunde alisema lengo lake lingine ni kuanzisha academic ya michezo ambayo itakuwa ikiwaandaa vijana jinsi ya kuwa wachezaji wa kulipwa katika miaka ya baadae pamoja na kuwatafutia soko la kwenda kuonyesha vipaji vyao nje ya Tanzania.

Wasanii kuipigia debe CCM na tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015.

$
0
0
Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda).Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo. Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya tamasha hilo.Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli). Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli).Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo. Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa katika mkutano huo.Baadhi ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari. Baadhi ya wasanii na makada wa CCM ambao watajumuika katika tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.

NEC YAWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUTOKUWA NA UPANDE WAKATI WA KUWAELIMISHA WANANCHI KUHUSU UCHAGUZI MKUU UJAO.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada leo jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutanoni .
 Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC leo jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.
 Wanasekretarieti ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali  na baadhi ya waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akiteta jambo na mmoja  wa makamishna wa Tume hiyo Prof Amon Chaligha leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi na hatua zilizofikiwa hadi sasa leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini.


MWANDISHI WETU -MAELEZO-DAR ES SALAAM

Tume ya Taifa ya uchaguzi  NEC  imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea  ili waweze kufanya maamuzi sahihi  wakati wa uchaguzi Mkuuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti   wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa  taasisi za kidini zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na kuwaacha watanzania wakiwa  na umoja na mshikamano licha ya tofauti za kiimani zilizopo miongoni mwao.

“Tume inawataka, nyinyi  viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema chama au mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT-Mikocheni -A ameiasa Tume  hiyo  kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo  ili kuivusha nchi ikiwa  salama.

Mshiriki mwingine kutoka Kanisa la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati  huu wa uchaguzi maana amani inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

MTANDAO WA WAANDISHI WA MASUALA YA HAKI YA AFYA YA UZAZI NA JINSIA WAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0

Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akizungumza na waandishi wa habari za masuala ya haki jinsia na uzazi katika mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,Siyovelwa Hussein akizungumza na waandishi wa habari wa wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR leo jijini Dar  es Salaam.
Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa, Dk. Koheleth Winani akionyesha katiba ya chama hicho kuashiria uzinduzi wa chama cha TAMENET–SRHR leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa mradi wa TMEP ,Eugnia Msasanuri akizungumza na wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya wadau wa Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR.
Wadau wa  Mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa imefikia lengo la nne la millenia ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano  kwa kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000.

Hayo ameyasema leo Mratibu wa Uzazi Salama Kitaifa,Dk. Koheleth Winani wakati wa uzinduzi  wa mtandao wa waandishi wa habari wa Haki na Afya  ya  Jinsia na Uzazi TAMENET–SRHR nchini,amesema kuazishwa kwa mtandao kutasaidia kusukuma harakati za kupunguza vifo hivyo.

Amesema anatambua mchango wa waandishi habari  katika mapambano dhidi ya Afya ya Uzazi na ukatili wa kijinsi  pamoja na ukatili dhidi ya watoto.

Dk. Winani katika kuboresha afya ya uzazi ,kutokomeza ukatili wa wa kijinsia  na ukatili dhidi ya watoto katika kupunguza vifo vya vitokanavyo na uzazi  pamoja na  watoto chini ya miaka mitano.

Aidha amesema waandishi katika  kwa kuazisha wametambua majukumu yao katika taifa  katika harakati za masuala ya afya hususani uzazi.

Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao huo,Siyovelwa Hussein amesema kuwa kuazishwa kw amtandao huo inatokana na mafunzo mbalimbali pamoja na kujionea hali halisi  katika maeneo ambayo yako nyuma katika masuala ya afya ya uzazi.


Siyovelwa amesema kuzinduliwa kwake na kuaza kufanya kazi katika kuweza kujiimarisha kifedha katika kuelimisha wananchi katika masuala ya afya.

OFISI YA WAZIRI MKUU NA WADAU WA MABADILIKO TABIA NCHI WAJADILI UBORESHAJI WA MIFUMO YA UTOAJI TAHADHARI ZA AWALI

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya akieleza jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali leo, tarehe, 20 Agosti, 2015, Jijini Dar esalam.
Mtaalam wa Mabadiliko ya Tabia nchi UNDP, Abbas Kitogo akieleza jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali leo, tarehe, 20 Agosti, 2015, Jijini Dar esalam, kushoto kwake ni Mratibu wa mradi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Alfei Daniel.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Wadau wa Mabadiliko ya Tabia nchi na Uboreshaji wa Mifumo ya utolewaji Tahadhari za awali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig.Jen, Mbazi Msuya (wapili kushoto waliokaa), baada ya ufunguzi wa warsha hiyo leo, tarehe, 20 Agosti, 2015 Jijini Dar esalam.

TPDC YAANZA KUZALISHA GESI YA KWANZA HUKO MNAZI BAY, MTWARA

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na kampuni za Maurel and Prom na Wentworth Resources, leo hii wameendelea na zoezi nyeti la kutoa gesi asilia katika kisima namba 3 kilichopo Mnazi Bay (MB3) kwenda katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba, Mtwara. 

Zoezi hili ni muendelezo wa ukamilishaji wa mradi mkubwa wa Serikali wa kuzalisha gesi asilia kwa madhumuni ya kuzalisha umeme hapa nchini.

Akiongea wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema “ ni furaha kubwa leo kuanza kuzalisha gesi asilia ya Mnazi Bay ambayo itaenda kuchakatwa katika mitambo yetu iliyopo Madimba na kisha kusafirishwa hadi Kinyerezi, Dar es Salaam ambapo wenzetu wa Tanesco wataitumia kuzalisha umeme”. 

 Dkt. Mataragio aliongeza kuwa kisima namba 3 (MB3) kina uwezo wa kuzalisha gesi asilia takribani futi za ujazo milioni 20 hadi 30 kwa siku (20-30mmscfd). Visima vingine vitakavyounganishwa ni pamoja na MX1, MB2, MB4 na MB1 hapo baadae na kufanya uzalishaji kufikia futi za ujazo milioni 130 kwa siku (130mmscfd).

Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Mafuta (TPDC) limetekeleza mradi huu wa kipekee kwa madhumuni ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa umeme hapa nchini. Hata hivyo, gesi asilia pia inatarajiwa kutumika viwandani kama nishati na pia malighafi, majumbani kupikia na katika magari. 

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuwa na miundombinu mikubwa ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuuza gesi hata kwa nchi majirani hapo baadae.
Kisima namba 3 au MB 3 kama kijulikanavyo kimeanza kuzalisha gesi asilia leo hii ikiwa ni mojawapo ya visima ambavyo vitapeleka gesi asilia katika mitambo ya kuchakata gesi iliyopo Madimba. Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (aliyeshika valvu) akifungulia gesi ya kwanza katika kisima namba 3 au MB 3 kama kijulikanavyo kuruhusu gesi kuanza kupita kuelekea katika mitambo ya kuichakata iliyopo Madimba, Mtwara.

Diamond Motors rolls out the new Fuso FZ in ‘Ndiyo Fuso niFaida’ campaign

$
0
0
                
         Transport sector is an important component of the economy and a common tool used for development because of its intensive use of infrastructures. This is even more so in Tanzania’s economy where economic opportunities are increasingly related to the mobility of people, goods and service. It is with this factors in mind that Diamond Motors (Hansa Group) has introduceda NewFuso heavy-duty truck range of Fuso FZ which offers more benefits in terms of efficiency, operation costs and suitable for the nature of Tanzania’s infrastructures.

Diamond Motors Limitedhas been playing a major role in the transportation sector since 1980 in Tanzania by the distribution of Mitsubishi Fuso trucks and Bus Corporation.A new range of Fuso FJ and Fuso FZ encompasses exceptional functionality, durability, and comfort, giving customers an entirely new breed of trucking technology.  Fuso heavy- duty trucks delivers lower operating costs, making them the best choice for smart businesses. Trucks ideal for long distance and heavy loads with high torque engines optimized for power andmaintain being economy to provide profitable transportation facility.

The ongoing campaign of “Ndiyo Fuso niFaida” in various regions in Tanzaniaaims at bringing awareness to stakeholders of different sectors of the economy on the benefits by the use of new Fuso truck which are of latest technology, in terms of capability, reliability, economy and long distance travelling as well as characteristics from the in-built specifications which are beneficial to the user. The 170kW/810Nm engine is more fuel efficient, for better mileage and lower costs and other long-haul applications.

Diamond Motors Limited has been servicing this sector through Mitsubishi Canters and Light trucks over the past few decades. Backed with after sales and spares support, the product portfolio is amply suited and tailored to meet the requirement and demands for this sector, and become the total transport solution provider in Tanzania.

With Fuso Value Parts, you are assured of authentic parts of the highest precision manufacturing guaranteed by Mitsubishi Fuso, without having to pay a premium. For excellent value at approachable prices, Diamond Motors Limited has made the choice easy. The availability of the required genuine parts determines the downtime of your vehicle. Turn to your Mitsubishi Fuso dealer for quick supply of the genuine parts needed to keep your truck running, reliable consultation and the quality of the service network determine how well and how long your truck performs while a trust to our trained technicians ensures high quality.

Umoja wa Mataifa waanza maadhimisho ya miaka 70 kwa kupanda miti Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira,  Mhe. Binilith Mahenge  akiwahutubia wananchi (hawapo pichani) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed  Gharib Bilal wakati wa tukio la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 70 ya Ummoja wa Mataifa lilofanyika katika Kijiji cha Marua, Mkoani Kilimanjaro. Mhe. Waziri aliwaasa wananchi waliojitokeza na Watanzania kwa ujumla kulinda na kuhifadhi mazingira
Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mahenge (hayupo pichani).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, naye akizungumza katika maadhimisho hayo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MIAKA MIAMOJA YA SKAUTI NCHINI UGANDA

$
0
0
Rais wa Uganda Yoweri Museni akiongea na Waziri mkuu Mizengo Pinda katika sherehe ya Skauti kwakutimiza miaka miamoja nchini Uganda kulia  Waziri  wa Jinsia kazi namaendeleo ya Jamii Hajati Rukia Isanga Nakadama Waziri mkuu alimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete  Picha na Chris Mfinanga.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa anateta jambo na Makamu wa Raisi wa Sudani Kusini H.E James Wani Igga ambaye aliwakilisha nchi yake katika sherehe ya Skauti kutimiza miaka miamoja nchini Uganda kulia kwa waziri mkuu ni Naibu Mkuu wa Itafaki Bw. James Bwana .

Picha na Chris Mfinanga.

Tamasha la muziki la sauti za busara Zanzibar 2016 halitokuwepo

$
0
0
Kutokana na uhaba wa fedha, Busara Promotions inasikitika kutangaza kuwa tamasha la Sauti za Busara mwaka 2016 halitakuwepo, hii itakuwa ni mara ya kwanza ndani ya miaka kumi na tatu Zanzibar kulikosa Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara lifanyikalo kila wiki ya pili ya mwezi Februari.

Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions, amesema leo "Uamuzi huu haukuchukuliwa kwa wepesi”. Kawaida huwa tunatangaza tarehe za tamasha mwaka mmoja kabla. Lakini baada ya kufanya tamasha lililopita kwa mafanikio, tumekuwa katika hali ya ukosefu wa fedha kwa toleo lijalo la 2016. 
 
Tulijiwekea  malengo ya kukusanya dola za kimarekani  200,000 kabla ya Julai, wakati tulipokuwa na matumaini ya kutangaza tarehe za Sauti za Busara 2016. Baada ya mikutano mingi na wadau, tulisogeza muda wetu wa kutafuta fedha hadi usiku wa Agosti 19. Kiasi ambacho tuna uhakika wa kukipata kuandaa tamasha lijayo kwa sasa kinasimamia kwenye dola za kimarekani 42,000, hivyo basi bado tuna safari ndefu mbele yetu.
 
Kawaida wakati kama huu, tunakuwa tumeshafika mbali kwenye makubaliano ya mikataba mbalimbali kama ya kukodi ukumbi, ukodishaji wa vifaa, wasanii na mameneja, tunaanza kupanga ratiba, maandalizi ya usafiri na malazi kwa wasanii mapema iwezekanavyo. Shinikizo zaidi, tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa watu mbalimbali duniani kote wakitaka kujua tarehe za tamasha ili waweze kufanya mipango yao ya safari. Mauzo ya tiketi za Sauti za Busara haijawahi kuwa tatizo, lakini hii inasaidia kulipa 30% ya gharama za tamasha ".

Yusuf ameendelea , "Matamasha yanahamasisha vijana kupenda utamaduni wao, hutoa fursa kwa wasanii na wataalamu wa muziki kukutana na kujifunza , yanashawishi uhai wa tamaduni, pia yanatoa nafasi za ajira kwa watu wa ndani na kutoa mifano ya utalii ambayo inathamini na kuheshimu utamaduni wa ndani. Hata hivyo, tangu mwaka  2004 hatuna msaada wowote wa kifedha kutoka serikali ya  Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na jitihada nyingi, msaada kutoka kwa wahisani, balozi na wafanyabiashara unazidi kupungua siku hadi siku. Busara Promotions ni shirika lisilo la kiserikali; tamasha haliko kibiashara. 
 
Wengine walipendekeza tujaribu kuomba pesa kupitia mitandao. Hata hivyo, kwa kweli ili kuwa endelevu zaidi, kipaumbele chetu kabla ya toleo la 2017  kitakuwa ni kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu na wadhamini na wafadhili ambao wanakubaliana na  mtazamo wetu. Mtu yeyote anaesoma ujumbe huu na ana nia ya kusaidia kuiweka Sauti za Busara hai, kukuza ajira nchini, wakati tunaendelea kuung’arisha muziki wetu wenye utajiri wa mila na kukuza utalii wa kiutamaduni Zanzibar na Tanzania, tafadhali awasiliana nami kupitia Busara Promotions."

Katika kipindi cha miaka kumi na mbili iliyopita, Busara imewavutia maelfu ya wageni kutoka kila pembe ya dunia  kuja Zanzibar , wakati ambayo hakuwa msimu wa wageni wengi . Ndege zote zinazokuja Zanzibar kipindi cha tamasha zinajaa, hoteli na migahawa vinajaa, maduka yaliyopo maeneo ya Mji Mkongwe yanapata wateja wengi zaidi. 
 
Hata makadirio yanaonyesha tangu mwaka 2004 tamasha limekiingizia kisiwa mapato ya kiasi dola za kimarekami milioni 70. Wakati huo huo, Shirika la utangazaji la BBC limeiweka Sauti za Busara kama moja ya "matamasha ya muziki bora na ya kuheshimika  zaidi Afrika ". Pia limeingizwa kwenye CNN "matamasha 7 ya muziki ya kiAfrika unayotakiwa kuyaona" na kileleni kwenye orodha ya AfroTourism ya "Matamasha bora ya Muziki  ”

Yusuf Mahmoud hatimaye alisema " Wakati mwingine ni muhimu kupiga hatua moja nyuma, kabla ya kusonga mbele. Bodi na uongozi wa Busara itafanya kazi kwa bidii zaidi miezi ijayo, ili kuhakikisha  kuanzia mwaka 2017 tamasha linarudi kuwa na nguvu zaid
i. Inawezekana itamaanisha kuhama  eneo, au kulifanya kila baada ya miaka miwili . Hakika vipaumbele vyetu vitakuwa kulifanya tamasha litoe nafasi zaidi kwa  wananchi  , wakati tunaelendea kuomba  kujenga ushirikiano wa muda mrefu , na sekta za umma na binafsi".

Wakati tamasha likiwa kwenye mapumziko, Busara Promotions itaendelea na shughuli zake za kawaida za kukuza muziki wa kiAfrika, kuimarisha uelewa wa watu na kuboresha sekta ya muziki. Kwa mwaka mzima, Busara itahakikisha wasanii wa Afrika Mashariki wanapata mialiko kwenye matamasha mengine ya  kimataifa na kuwezesha kujenga ujuzi kwa wasanii wa ndani na wafanyakazi wa tamasha, kwa njia ya kubadilishana na mafunzo ya uongozi wa  sanaa, masoko, habari na ujuzi wa kiufundi . Kazi hii , ambayo inadhaniniwa na Ubalozi wa Norway , Dar es Salaam , haitotetereshwa  na uamuzi wa kufuta Sauti za Busara 2016 .

Rais Kikwete atembelea na kuaga rasmi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake kwa viongozi na wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika ukumbi wa mikutano wa Haki House makao makuu ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bwana Tom Nyanduga wakati Rais alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Tom Nyanduga akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kuboresha haki za binadamu na Utawala Bora nchini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuhutubia na kuagana rasmi na wafanyakazi wa Tume hiyo jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serkali Mh.George Masaju.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Bwana Tom Nyanduga pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro baada ya Rais Kuwahutubi na kuagana na wafnyakazi wa tume hiyo leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati alipotembelea makao makuu ya Tume hiyo na kuzungumza na viongozi na wafanyakazi na kuwaaga rasmi leo.(picha na Freddy Maro)

MATUKIO MBALIMBALI YAENDELEA KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 70 YA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwa pamoja na  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakichanganya saruji, kokoto na mchanga ili kupata zege kwa ajili ya kuweka Jiwe la  Msingi ikiwa ni uzinduzi wa kuanza kwa ujenzi wa vyoo 22 kwenye Shule ya Msingi Kiboriloni, Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi huo ni tukio mojawapo kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa  Ujenzi huo umedhaminiwa na UNDP. 
Bw. Alvaro akiweka jiwe la msingi  kuzindua kuanza kwa ujenzi wa  Vyoo hivyo
Balozi Mushy naye akiweka tofali katika msingi huo 
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem naye akimpatia fundi tofali la ujenzi wa vyoo hive
Picha na Reginald Phili.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA


TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika sherehe ya kumuaga mara baada ya kumaliza uongozi wake katika Serikali ya awamu ya nne.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga katika Sherehe iliyoandaliwa na Tume ya kumuaga mara baada ya kumaliza Uongozi wake.
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Tom Nyanduga akizungumza katika sherehe ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza  utawala  wake katika serikali ya  awamu ya nne ,ndani ya  ofisi za tume hiyo.
 Baadhi ya viongozi wa Serikali pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Sherehe ya kumuaga baada ya kumaliza uongozi wake katika serikali ya awamu ya nne.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora mara baada ya kuwasili katika ofisi yao.

NEC YATOA RATIBA YA KUREJESHA FORM NA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS.

STARS KWENDA UTURUKI MOJA KWA MOJA

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro sasa itaondoka nchini siku ya jumapili usiku kuelekea Istambul nchini Uturuki kwa kambi ya siku nane kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria Septemba 05, 2015.

Awali Taifa Stars ilikua ipitie Muscat nchini Oman kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo, lakini kutokana na shirkikisho la Soka la Oman kushindwa kukidhi mahitaji ya Kanuni za FIFA za uuandaaji wa mechi ya kimataifa ya kirafiki sasa mchezo huo hautakuwepo tena.

Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili Istambul (Ataturk Airport) siku ya jumatatu majira ya saa 5 kamili asubuhi, kisha kuelekea Kocael katika hoteli ya Green Park Kartepe ambapo ndio itakua kambi yake ya wiki moja.

UCHAGUZI WA TEFA WAAHIRISHWA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Aloyce Komba imeitisha majalada ya kamati ya uchaguzi ya TEFA na kamati ya uchaguzi ya DRFA baada ya kupokea malalamiko na rufaa kutoka kwa wagombea.

Kamati ya Uchaguz ya TFF imeyaomba majalada hayo ili ijiridhishe na kuona haki inatendeka kwa wagombea wote na baadae tarehe mpya ya uchaguzi itatolewa.

SAANYA KUCHEZESHA AZAM NA YANGA

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii jumamosi, badala ya mwamuzi Israle Nkongo aliyekua amepangwa awali.

Mwamuzi Israel Nkongo anasumbuliwa na matatizo ya misuli ya paja, ambayo itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa takribani siku kumi, hali iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea kwenye mchezo huo wa jumamosi.

Mkutano wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi na Viongozi wa Dini

$
0
0
Tume ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, hapo kesho inatarajiwa kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu. 
 Akizungumza katika mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wawakilishi kutoka katika madhehebu ya dini hapa nchini katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani alisema uchaguzi mkuu wa Mwaka huu utahusisha majimbo mapya 25 na kata 620 ambazo zimeongezeka kutokana na sababu za kiutawala na kuongezeka kwa Idadi ya watu. 
 Aidha Jaji Lubuva alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imeandaa mkakati na mongozo wa kutumia radio na televisheni za kijamii zikiwemo zile za dini kutoa elimu kwa wapiga kura katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu ili kuelimisha wapiga kura kuhusiana na uchaguzi huo. Katika mkutano huo, Jaji Lubuva amewataka viongozi wa dini kutoonyesha hisia za kuegemea upande wowote au kutowashawishi waumini wao kuegemea upande wowote hasa wanapoto elimu ya mpiga kura ili uchaguzi ufanyike kwa uhuru na Amani. 
 “Tume inawataka mnapotoa mafundisho kutoonyesha hisia za kuwa upande wowote wa chama chochote cha siasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegemea upande wowote au mgombea” alisema Jaji Msaafu Lubuva na kuongeza kuwa Tume ya Taifa ya uchaguzi inawaomba viongozi wa dini kuyatumia majukwaa yao kuwaelimisha waumini waweze kufanya kufanya maamuzi sahihi. 
 Akiwaslisha mada katika mkutano huo,Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani alisema kuwa azma ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuhakikisha kwamba kila raia mwenye sifa na aliyejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura anapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa wa wazi, huru na haki ili kujenga demokrasia na kukuza uatwala bora hapa nchini. 
 Ramadhani aliongeza kuwa, hadi sasa,Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha mambo kadhaa katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. 
Baadhi ya mambo ambayo yamekamilika hadi sasa ni pamoja na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, na kuweka wazi daftari la awali la wapiga kura. Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu nchini Tanzania utashirikisha jumla ya majimbo 264 na kata 3,957 kutoka Tanzania Bara. 

+255(0)772 55 55 53
LISTEN LIVE
http://myradiostream.com/focusradiotz
Tume ya Taifa Ya Uchaguzi Tanzania
FACEBOOK
http://bitly.com/1zIiIkq 
TWITTER
http://bit.ly/1678Vq2




MKUTANO MKUU WA 15 WA MWAKA WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

MKUTANO UTAHUDHURIWA NA MAJAJI NA MAHAKIMU KUTOKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,MHE. DR. JAKAYA MRISHO KIKWETENDIYE MGENI RASMI ATAKAYEFUNGUA MKUTANO HUO.

KAULIMBIU YA MKUTANO NI:

KUIMARISHA IMANI YA UMMA KWA MAHAKAMA

WAKATI WA MKUTANO KUTAKUWA NA MAONYESHO JUU YA HUDUMA MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA. WOTE MNAKARIBISHWA

AIDHA MKUTANO HUO UTAFUATIWA NA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WA TANZANIA(JMAT) UTAKAOFANYIKA TAREHE 29 AGOSTI HADI TAREHE 30 AGOSTI,2015 KATIKA HOTELI HIYO .


IMETOLEWA NA:

RAIS


CHAMA CHA MAJAJI NA 
MAHAKIMU TANZANIA (JMAT)

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images