Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
(kushoto), Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi
(kulia) na Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks wakionyesha bango
kama ishara ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa
Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya
akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni
Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks, Kamishna Msaidizi wa Wizara
ya Fedha, Ridhiwan Masudi na Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel
Tanzania, Arindam Chakrabarty.
3) Afisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Arindam Chakrabarty
akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo kwa mawakala wa Airtel Money ijulikanayo kama ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni
Mkurugenzi wa Afb Tanzania, Wayne Stocks na Kamishna Msaidizi wa
Wizara ya Fedha, Ridhiwan Masudi.
Baadhi ya mawakala wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
uzinduzi wa huduma ya Timiza Mkopo kwa wakala, huduma itakayowawezesha
kupata mikopo isiyo ya dhamana kupitia huduma ya Airtel Money.
Airtel yatoa Mikopo kwa Mawakala wa Airtel Money
* Mikopo isiyo na dhamana
* Zaidi ya mawakala 20,000 kunufaika
KAMPUNI ya simu za mkononi
ya Airtel kwa kushirikiana na Afb Tanzania imezindua huduma ya mikopo
kwa wateja wa Airtel Money ijulikanayo kama "Timiza Mkopo kwa Wakala",
itakayowawezesha mawakala wa Airtel Money nchini nzima kupata mikopo
isiyo na dhamana ya kuanzia shilingi 50,000 hadi 500,000.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mkuu wa Biashara Airtel , Bwana
Arindam Chakrabary alisema" Airtel inatambua kuwa mawakala wetu
wanatafuta fursa ya kukuza biashara zao na kuongeza mitaji. Na leo
tunayo furaha kuzindua huduma ya kwanza Tanzania na Afrika "Timiza
Mkopo kwa Wakala" mikopo isiyo na masharti mahususi kwa mawakala wetu.
Huduma hii ya mikopo kwa mawakala itawanufaisha mawakala zaidi ya
20,000 nchi nzima, na tunaamini mikopo hii itasaidia kukuza biashara
za mawakala wetu , kuwaongezea faida zaidi na hatimaye kuboresha
upatikanaji wa huduma za kifedha"
Chakrabarty aliongeza kwa kusema" Mwaka jana tulizindua huduma ya
Timiza kwa wateja wetu nchini nzima, ambayo kwa sasa ina zaidi ya
wateja milioni 7 wanaoweza kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti
kwa urahisi , mikopo ambayo inawasaidia kutatua changamoto za kijamii
na kiuchumi.
"Timiza Mkopo kwa Wakala" itatoa kwa mawakala wetu wa
Airtel Money uhuru wa kupata mikopo ya haraka isiyo na masharti bila
kupitia njia ndefu zakupata mikopo katika mfumo wa kawaida. Tunaamini
huduma hii inatasaidia na kuwawezesha mawakala wa Airtel Money kupata
fedha za kutatua mahitaji yao ya muda mfupi na mrefu wakati wote.
AliongezaNaye Msimamizi Mkuu Afb Tanzania, Rwebu Mutahaba, amesema " Mawakalawanapata mikopo kulingana na matumizi yao ya simu ndo mana tumeweza kuwaamini na kuwapatia mikopo isiyo na masharti. Lengo kubwa ni kuwapatia watu fulsa ya kupata huduma ya kisasa na kibunifu ambayoa haijawahi kutolewa kabla.
Afb Tanzania tunajivunia ushirika huu na Airtel ambao umetuwezesha kutoa suluhisho kwa wateja wa Airtel , mikopo kwa mawakala ni moja ya huduma nyingi za kibunifu tulizonazo na tunazopanga kuzindua katika mienzi ijayo nchini Tanzania".
Timiza Mkopo kwa Wakala" ina viwango na riba tofauti zenye marejesho
ya ndani ya siku saba, wiki mbili au mwezi mmoja.
Kiasi cha kukopa
kitategemeana na matumizi simu ya wakala na jinsi anavyorudisha mkopo
wake kwa wakati. Mteja atakapo rudisha mkopo wake ndani ya siku 7,14
au 28 mojakwamoja atawezeshwa kupata mkopo mwingine.
Inachukua dakika moja kwa mteja kujaza fomu ya kuomba mkopo kupitia simu yake na kisha mara baada ya kujaza pesa zinawekwa kwenye akaunti yake ya Airtel Money hapohapo".
alisema Mutahaba Kwa upande wake, kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna Msaidizi Wizara ya
Fedha, Bwana Ridhiwan Masudi alisema" sisi kama Serikali tumefurahishwa na hatua walioichukua Airtel katika kuboresha mfumo rasmi wa kifedha kupitia huduma ya Airtel Money. Tunafurahi kuona huduma ya Airtel Money ikikuwa kwa haraka na kuwafaidisha watanzania wakawaida hususani wanaoishi katika maeneo ya pembe zoni mwa nchi.
Napenda kuchukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kuleta bidhaa na
huduma za kibunifu ili kuweza kuipatia jamii huduma bora za
mawasiliano na kukuza zaidi huduma za kifedha."
Mawakala wa Airtel Money wanaweza kujipatia mikopo kwa kupiga
*150*60#, na kuchagua 4 ili kupata orodha ya mikopo kwa wakala , na
kisha kuingiza namba ya simu na namba ya siri na baada ya hapo
wataunganishwa kwenye orodha ya mikopo ya Timiza.