Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 944 | 945 | (Page 946) | 947 | 948 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Afisa  Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Tanzania akizingumza na baadhi ya wafanyakazi  pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo  wakifurahia kwa pamoja wakati wa hafla fupi iliyoaandaliwa na benki hiyo  kuadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita
   Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
  Meneja Mwandamizi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Exim Tower, Bi Rose Kanijo (wa tano kulia) akiwaongoza wawakilishi wa wateja wa benki hiyo Bw. Geofrey Mihaambo (wan ne kulia) na Bi. Usha Kakad (wa tatu kulia) kukata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 18 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa juma lililopita.Wanaoshuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.


  Exim Bank imeadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwake huku uongozi wa benki hiyo ukiahidi kuboresha zaidi huduma zake hasa katika kipindi hiki ambacho sekta benki imetawaliwa na ushindani mkubwa.

  Benki hiyo iliyoanza kutoa huduma zake mwezi Agosti,1997 ikiwa na tawi moja jijini Dar es Salaam kwa sasa ina jumla ya matawi 30 hapa nchini  na matawi saba nje ya nchi huku pia rasilimali yake ikitajwa kuwa na thamani ya sh. trilioni 1.1 hadi kufikia mwezi juni mwaka huu.

  Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha baadhi ya waafanyakazi na wateja wa benki hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ukweli kuwa benki hiyo inafanya kazi chini ya bodi ya wakurugenzi iliyo imara.

  “Siku kama ya leo miaka 18 iliyopita ndio benki yetu ilianzishwa. Leo benki ya Exim imesaidia ukuaji wa biashara  ndani na nje ya nchi na tunashukuru kuona kwamba baadhi ya wateja wetu wameweza kuhudhuria hafla hii ili tusherehekee pamoja siku hii muhimu,’’ alisema.

  Kwa mujibu wa Bw. Selemani mbali ya kuwa na idadi kubwa ya matawi ndani na nje ya nchi pia imefanikiwa kuwa na mashine za kutolea fedha 57 hapa nchini, vituo vya mauzo zaidi 250 na kwa sasa ina matawi kwenye mikoa 16 hapa nchini ambayo yanahudumia takribani wateja 180,000.

  “Miaka yote tumekuwa tukiitumia siku hii pia kutathmini ubora wa huduma zetu kwa wateja na ndio maana tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri kila siku. Uhodari wa wafanyakazi wetu imekuwa pia imekuwa ni chachu kwenye mafanikio haya,’’ alibainisha bw. Ponda.

  Kwa mujibu wa Bw. Ponda, benki hiyo ndio benki ya kwanza hapa nchini kufungua matawi yake nje nchi ambapo kwa sasa imefungua matawi yake visiwa vya Comoro na nchini Djibouti.


  0 0  0 0


   Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea Mwanza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya majiji hayo mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
   Abiria wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kuelekea jijini Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
  Abiria wakipanda kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ-200 tayari kuelekea jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni baada ya shirika hilo kurejesha safari zake kati ya Dar es Salaam na Mwanza baada ya kusimamisha safari hizo tangu mwezi Agosti mwaka jana. Shirika hilo litafanya safari zake kati majiji haya mawili mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

   SHIRIKA  la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma  kwa wateja wake hapa nchini.

  Safari ya kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.

  “Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’ alibainisha Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake  mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

  Alisema ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.

  Akizungumzia na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza mmoja wa abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa kwa huduma hiyo pia alionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa na wahudumu wa shirika hilo.

  “Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.

  Pamoja na kurejesha safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100.

  “Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam,’’ aliongeza Fungamtama.

  0 0

  Mratibu wa Bima kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, katikati akizungumza katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na Bajaj kwa kushirikiana na Kampuni ya NIKO Insurance. Kulia ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Niko, Mannaseh Kawoloka.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamTAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, imezindua huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj, ikiwa na lengo la kurahisisha masuala ya usafiri kwa wateja wao ili kukwamua zaidi. Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetajwa kuwa kutachangia kwa kiasi kikubwa wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri waliokuwa wakishindwa kulipa bima kwa wakati na wakati mwingine mteja kupata ajali hali ya kuwa hana huduma ya bima inayoweza kumlinda.
  Oparesheni Meneja wa Bayport Financial Services, Charles Mgeta, kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Magari, pikipiki na bajaj. Anayefuata ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka.
  1. Afisa Mtendaji Mkuu wa NIKO Insurance, Mannaseh Kawoloka katikati akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj inayoendeshwa na Taasisi ya Bayport Financial Services. Kulia kwake ni Mratibu wa bima hiyo, Ruth Buran a kushoto kwake ni Meneja Oparesheni wa Bayport, Charles Mgeta. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 
  Wakati shughuli ya uzinduzi wa huduma mpya ya bima ya magari, pikipiki na bajaj kutoka Bayport Financial Services kwa kushirikiana na NIKO Insurance ukiendelea Makao Makuu ya Bayport leo asubuhi.
  Meneja Madai wa Niko Insurance, David Mshuza, akiafuatiwa na Cecilia Peter na Lester Chinyang'anya. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

  Akizungumza leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima hiyo kutoka Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema huduma yao wanayoshirikiana na NIKO Insurance ina lengo kubwa la kumrudisha mteja wao (mkata bima), katika hali aliyokuwa nayo kabla ya kupata ajali hiyo.

  Alisema mara kadhaa baadhi ya Watanzania wamekuwa wakikimbizana na askari wa usalama barabarani kwa sababu hawana bima kwenye vyombo vyao vya usafiri, ila kwa kupitia huduma yao mpya, sasa kila mtu anaweza kujiunga na bima kwa njia rahisi, wakiamini kuwa ni sehemu yao ya kuhakikisha wateja wao wanakuwa kwenye usalama ili watimize wajibu wao kufanya kazi na kukuza uchumi wao na wa Tanzania kwa ujumla.

  “Ili mtu aweze kujiunga na huduma yetu ya Bima kutoka Bayport Financial Services, kwanza anatakiwa kujaza fomu yetu ya mkopo na ile fomu ya udhibitisho wa bima, bila kusahau nyaraka za umiliki wa gari lake ili tujiridhishe na umiliki wake.

  “Baada ya hapo, gari lake litapigwa picha tano kila pembe, ikiwa ni nyuma na mbele na kwenye injini na tukimaliza hatua hiyo, mteja wetu atapatiwa mkataba wa bima pamoja na ‘sticker’ kuonyesha kuwa yupo kwenye bima, huku huduma hiyo ikiwa ni rahisi kwa sababu gharama za bima kwa mwaka ni kuanzia Sh 354,000 pamoja na VAT,” Alisema.

  “NIKO tunajisikia faraja kubwa kushirikiana na wenzetu Bayport Financial Services kutoa huduma bora na kiwango cha juu, hususan kwa kupitia huduma hii mpya ya bima ya magari, tukiamini kuwa itawafanya Watanzania wote watembee kifua mbele, maana ile presha ya kukimbiana na watu wa usalama barabarani itakuwa imepatiwa ufumbuzi,” alisema Kigoda.

  Bayport Financial Services ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa, bila kusahau mradi wa mikopo ya viwanja vya Vikuruti unaoendelea na kuwafanya Watanzania watembee kifua mbele, huku taasisi hiyo ikifanikiwa kuwa na matawi 80 Tanzania Bara, hivyo kutoa huduma bora na kwa njia rahisi kwa kupitia matawi yao au mtandao wao wa www.kopabayport.co.tz.

  Naye Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NIKO Insurance, Jabir Kigoda, alisema kuwa huduma hiyo ni nzuri na rahisi inayoweza kuwanufaisha wateja na Watanzania wote, hivyo wanapaswa kuichangamkia ili kuwaweka katika usalama wao na wa vyombo vyao vya usafiri.

  0 0


  0 0

  WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Arusha juzi wameungana na familia zao katika tamasha la familia( Family Day),zilizofanyika katika viwanja vya TGT, vilivyopo eneo la Kisongo,nje kidogo ya Arusha.

  Aidha katika tamasha hilo wafanyakazi hao na familia zao walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu,kuvuta kamba,mpira wa mezani,kucheza muziki pamoja na michezo mbalimbali ya watoto.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo Optaty Minja,alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuonyesha jinsi kampuni hiyo ya bia inavyothamini familia za wafanyakazi wake.

  Minja ambaye pia ni Mhasibu wa TBL katika upande wa mashamba,alisema kuwa kuwakutanisha wafanyakazi hao na familia zao kunawasaidia kuweza kufahamiana , na kusaidia kujenga mahusiano mazuri baina ya familia zao,kwani mara nyingi hukutana wakiwa kazini lakini watoto, wake na waume zao hawafahamiani hivyo kupitia siku ya familia husaidia kujenga uhusiano na kufanya kuwa familia moja.

  “Kama kampuni tumeona ni jambo zuri familia zetu kukutana leo ili kuonyesha jinsi gani kampuni inathamini familia za wafanyakazi wake ambapo pia tunazidi kufahamiana,kujenga mahusiano mazuri kati yetu na familia zetu kwa ujumla”alisema Minja
  Baadhi ya familia za wafanyakazi wa TBL Arusha, wakipata chakula cha mchana katika viwanja vya TGT,vilivyopo eneo la Kisongo,nje kidogo ya Jiji la Arusha,juzi katika sherehe ya familia (family day) ya kampuni hiyo.
  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya TBL mkoa wa Arusha, wakipewa zawadi baada ya kushinda katika michezo mbalimbali iliyofanyika katika sherehe ya familia (family day) ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,juzi,jijini Arusha.

  0 0


  0 0

  ..Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade  Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la  10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.
   
  habari na libeneke la kaskazini blog
  Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.


  Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.


  "tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema


  Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuwakaribisha nchini wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kabla ya kufungua kikao cha wajumbe hao kinachofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar. Lengo la kikao hicho ni  kujadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania.
   Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan ya Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo, hata hivyo katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia meza kuu) anamuwakilisha katika kikao hicho. 
   Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini, Pereira Ame Silima (kulia) akiwa na  Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Uganda ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi James Baba (katikati) na Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani nchini Rwanda, Balozi Munyabagisha Valeus, wakisoma taarifa za masuala mbalimbali ya jinsi ya Kupambana ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Baraza hilo limekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.
  Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi nchini, Pereira Ame Silima (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo ambalo nchi zake wanachama ni Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Seychelles, Afrika ya Kati, Somalia na Tanzania. Wajumbe hao wamekutana katika Hoteli ya Sea Cliff, Zanzibar leo.

  Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

   Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akikagua mradi wa majisafi katika Kituo cha Majisafi cha Capri Point, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa MWAUWASA, Inj. Anthony Sanga.
   Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiwa kwenye mradi wa majitaka katika Kituo cha Kusukuma Majitaka cha Makongoro.
   Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiambatana na Meneja Msaidizi wa Operesheni ya Tiba ya Maji (Sanitation Operation), Inj. Salim Lossindilo katika mradi wa tiba ya maji (sanitation) Butuja, unaopokea majitaka kutoka Makongoro na kuyatibu na kutumika kwa ajili ya matumizi mengine.
  Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla akiwa pamoja na Bodi ya MWAUWASA, wafanyakazi wa MWAUWASA na maafisa wa Wizara ya Maji alipotembelea ofisi ya MWAUWASA, Capri Point.


  Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Amos Makalla leo ameendelea na ziara yake Kanda ya Ziwa kwa kutembelea miradi ya Mamlaka ya Majisafi na Mazingira, jijini Mwanza (MWAUWASA) na kukagua utekelezaji na maendeleo ya miradi ya maji mkoani Mwanza.


  Aidha, Mhe. Makalla aliweza kujionea ujenzi wa jengo jipya la MWAUWASA, Isamilo na kuzungumza na wafanyakazi wa MWAUWASA katika hafla fupi ya kuwazawadia wafanyakazi waliofanya kazi kwa uaminifu kwa zaidi ya miaka 15 katika ofisi za MWAUWASA zilizopo Capri Point.

  0 0

  Afisa habari wa TFF,Baraka Kizuguto.
  TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumamosi usiku kuelekea Muscat Oman, kucheza mchezo wa kirafiki kabla ya kuunganisha kuelekea Istambul Uturuki kwa kambi ya wiki moja.
  Taifa Stars imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Oman tarehe 24 Agosti, 2015 usiku, ambapo baada ya mchezo huo timu itasafiri kuelekea nchini Uturuki katika jiji la Istambul.
  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Oman (OFA) liliomba kucheza mchezo wa kirafiki na Taifa Star kabla ya kuwavaa Turkemebistan katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia Septemba 03, 2015 kwa bara la Asia, ambapo kocha wake mkuu Mfaransa Paul Leguen aliomba kucheza na vijana wa Charles Mkwasa kujiandaa na mechi hiyo.
  Mara baada ya mchezo huo Taifa Stars itaelekea Istambul katika mji wa Kocael hoteli ya Kartepe kwa kambi ya wiki moja, ikiwa nchini Uturuki Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki kabla ya kurejea nchini kucheza na Nigeria Septemba 05, 2015 mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika.
  Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa anatarajiwa kutoa orodha ya kikosi chake cha wachezaji 22 mwishono mwa wiki watakaosafiri kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya hiyo ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.
  Mshambuliaji Adi Yussuf anayechezea klabu ya Mansfield Towny ya Uingereza alitarajiwa kujiunga na timu nchini Uturuki, lakini kutokana na majeruhi aliyoyapata hivi karibuni katika michezo ya ligi, uongozi wa Mansfield umeomba mchezaji huyo kutojiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya kupata mataibabu zaidi.
  Adi aliumia wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Nottingham Forest ambapo kwa sasa anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa klabu hiyo, na pindi atapokuwa fit atapata nafasi ya kujumuika na kuitumika timu ya Taifa ya Tanzania.

  0 0

  Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
  Baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

  Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo wilayani Moshi, Kilimanjaro. 

  (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

  NA VERONICA KAZIMOTO.
  Wito umetolewa kwa viongozi wote wa Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.


   Wito huo uletolewa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.


  "Ninawaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na Wahariri watakaoshiriki zoezi la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya katika nchi yetu, amesema Makuwani".


  Dkt. Makuwani amesema kuwa taarifa zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya  utafiti huo zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu na wala hazina uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.


  kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015  unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.


  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.

  0 0

                   Ni katika suala la uanzishaji viwanda ili kukuza uchumi.
    
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda (Pichani)amesema Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) haina kuweka mkakati utakaohakikisha kuwa nchi wanachama zinakuwa na mpango mahsusi wa kuendeleza viwanda kama ambavyo imekubaliwa kwenye kikao chao kilichomalizika leo.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 18, 2015), wakati akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mkutano wa 35 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika jijini Gaborone, Botswana.

  “Jumuiya ya SADC kupitia sekretarieti yake itabidi iweke mkakati maamlu wa kufuatilia kama nchi wananchama imeandaa mapango wa kuendeleza viwanda kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kwenye kikao cha leo,” alisema Waziri Mkuu ambaye ameshiriki kikao hicho kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete.

  Alisema yeye binafsi amefurahishwa na kupitishwa kwa azimio la uendelezaji wa viwanda katika nchi za SADC kwani unaendana na juhudi za Serikali ya Tanzania za kukuza uchumi kupitia uendelezaji wa viwanda vya usindikaji.

  “Nimefurahi kwa sababu azimio hili linaendana na mpango wetu wa kuendeleza viwanda wa mwaka 2015/2016 hadi 2020/2021. Sisi tumelenga viwanda vya kusindika mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji… kwa hiyo naamnini tutaenda vizuri na mpango mzima wa Jumuiya hii,” alisema.

  Kuhusu madeni ya michango kutoka kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema Tanzania iko kwenye hatua nzuri ya ulipaji michango hiyo. “Jana nilipofika niliulizia suala hilo, nikaambiwa kwamba Tanzania imekwishalipa kwa kiwango cha kuridhisha. Nilitoa wito wakamilishe kulipa hiyo michango iliyobakia kwenye maeneo husika,” aliongeza.

  Mapema, Waziri Mkuu Pinda alisoma salamu maalumu mbele ya wakuu wa nchi na washiriki wa mkutano huo zaidi ya 500, zikiwa ni salamu maalum za kuwaaga zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete. Rais Kikwete anamaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu na hatapata nafasi nyingine ya kushiriki kikao cha wakuu wa nchi.

  Kikao kijacho kimepangwa kufanyika Agosti, 2016 nchini Lesotho ambapo Mfalme Letsie Mswati wa III alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakuu wa nchi wanachama kwenye mkutano huo.

  Katika hatua nyingine, wakuu wa nchi  za Jumuiya ya SADC wamechangua Rais Ian Khama Seretse Khama kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo.

  Katika kikao hicho waliazimia kuendeleza mapambano dhidi ya magonjwa ya Kifua Kikuu, Malaria na kuazimia kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwenye nchi wanachama.

  Mbali na kusisitiza utunzaji na uhifadhi wa mazingira, waliazimia pia kila nchi itekeleze mpango wake wa kilimo ili kuwa na akiba ya kutosha hasa ikizingatiwa hali ya ukame ambayo imezikumba nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na kuashiria uhaba mkubwa wa chakula.

  Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea nchini leo jioni.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, AGOSTI 18, 2015.

  0 0


  al4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifunguaMfereji ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katikaviwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja (katikati) Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hamad Yusuf Masauni.
  al5
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimtwisha ndoo ya maji Fathiya Khamis Husein (Suza)baada ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja.

  al1

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja leo alipofika kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni
  al2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua  Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika  Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja,(kutoka kushoto) Nd,Abdalla Suleiman  Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni  Hmad Yusuf Masauni.
  al3
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji ZAWA wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja.

  0 0

  JESHI  la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatarajia kuzindua mashindano ya michezo mbalimbali kwa lengo la kuwashirikisha wananchi  wa  rika zote  na  itikadi  mbalimbali 
  yatakayojulikana“KAMISHNA KOVA CUP”.

   Madhumini ya mashindano haya ni  ni  Kuwaunganisha wananchi wenye itikadi mbalimbali ili kupitia mashindano  haya  watakaoshiriki  watajifunza  masuala  ya usalama, uzalendo  na kuzingatia utaifa kwa madhumuni ya kuwashirikisha kikamilifu katika ulinzi wa nchi na kudumisha amani  na  utulivu  katika  jiji  la  Dar  es  Salaam  na  mikoa mingine.

  Lengo lingine ni  Kuishirikisha jamii  kuondokana na dhana ya kutenda uhalifu wa aina mbalimbali kama vile ujambazi, matumizi ya aina mbalimbali ya  madawa ya kulevya,  wizi katika mitandao,uzururaji, na kukaa katika vijiwe bila kazi.

  Pia  Kupitia michezo mbalimbali, jamii itafaidika kupata elimu juu ya umuhimu wa jukumu la msingi la kushiriki katika ulinzi na usalama  wa  nchi  hii,  itakuwa  ni  fursa  nzuri  kujua madhara ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

  Katika michezo watajifunza kujenga au kuimarisha mahusiano mema baina ya Jeshi la Polisi na  jamii  kwa  ujumla  kupitia  dhana  ya  Polisi  Jamii itatekelezwa kwa vitendo.

  0 0

   WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, (anayeshughulikia masuala ya Muungano), Samia sSuluhu Hassan,(wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi, (wakwanza kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Property International Ltd, (PIL), Abdulkarim Haleem, (watatu kulia), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Gabriel Silayo, (wane kulia), wakiwa wamekamata mwamvuli ikiwa ni ishara ya umoja, kwenye uzinduzi wa mpango wa kukopesha viwanja wanachama wa PSPF ambapo TPB itaratibu ukopeshwaji huo kwa kutoa fedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Jumanne Agosti 18, 2015.

   Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano), Samia Suluhu Hassan, akitoa hotuba.

   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Gabriel Silayo, akitoa hotuba yake

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake

   Msanii wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, ambaye pia ni balozi wa PSPF, akitoa burudani kwenye hafla hiyo.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi,katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni  kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Wajumbe

  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

  Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

  Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-
  1.
  KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
  1. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mwenyekiti
  2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara
  3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar
  4. Ndugu Sofia Simba
  5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
  6. Ndugu Asha-Rose Migiro
  7. Ndugu Samwel Sitta
  8. Ndugu Nape Nnauye
  9. Ndugu Mwigulu Nchemba
  10. Ndugu Harrison Mwakyembe
  11. Ndugu January Makamba
  12. Ndugu Amina Makillagi
  13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
  14. Ndugu Stephen Wasira
  15. Ndugu Abdallah Bulembo
  16. Ndugu Hadija Aboud
  17. Ndugu Mohamed Aboud
  18. Ndugu Lazaro Nyalandu
  19. Ndugu Issa Haji Ussi
  20. Ndugu Waride Bakari Jabu
  21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
  22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
  23. Ndugu Maua Daftari
  24. Ndugu Stephen Masele
  25. Ndugu Pindi Chana
  26. Ndugu Shaka Shaka
  27. Ndugu Makongoro Nyerere
  28. Ndugu Bernard Membe
  29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
  30. Ndugu Antony Diallo
  31. Ndugu Livingston Lusinde
  32 . Ndugu Ummy Mwalimu


  Imetolewa na:-
  Nape Moses Nnauye,

  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
  ITIKADI NA UENEZI

  18/08/2015

  0 0

  Daktari Hafidh Ameir toka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) akitoa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya kwa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Semina iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marcelina Henry akichukuliwa vipimo vya shinikizo la damu na Muuguzi toka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Asma Msimbe wakati wa zoezi la kupima afya kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
  Bwana Ponela John wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa Timu ya Wataalamu waliofika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili ya kupima afya za wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mfanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. Radhia Said akichukuliwa vipimo vya urefu na Bwana John Joseph wa Timu ya Wataalamu waliofika Wizara hapo kwa ajili ya kuendesha zoezi la kupima afya za wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na.Aron Msigwa - MAELEZO,ARUSHA

  Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu.

  Kauli hiyo imetolewa jana jijini Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA,Rasilimali watu,Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini.

  Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuondoa wizi na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu.

  Ameeleza kuwa utendaji wa Serikali na taasisi zake umerahisishwa kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
  Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw.Adorf Mapunda akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali mtandao kwa Maafisa TEHAMA,Rasilimali Watu,Utawala na Maafisa habari kutoka maeneo mbalimbali nchini jana jijini Arusha.

  0 0
 • 08/19/15--02:40: Bei ya Madafu leo


older | 1 | .... | 944 | 945 | (Page 946) | 947 | 948 | .... | 3278 | newer