Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 942 | 943 | (Page 944) | 945 | 946 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0
 • 08/15/15--23:06: WIZARA YA UJENZI YAMUAGA JK
 •  Rais Jakaya Kikwete akihutubia wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi wakati wa hafla maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
   Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye hafla ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.


   Wahandisi mbali mbali wa Wizara na wasiokuwa wa Wizara walijumuika pamoja kwenye hafla ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
   Wageni waalikwa kutoka taasisina mashirika mbali mbali walishiriki kikamilifu. 
   Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa ufunguo wa trekta lake alilopewa zawadi kwenye hafla ya kumuaga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikweteakiwa kwenye picha ya pamoja na wahandisi wanaogombea ubunge kwenye majimbo mbali mbali.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanamuziki wa Bendi ya Sikinde ambao walikuwa wakitumbuiza kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Askofu Charles Gadi akitoa historia yake katika ibada yake ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Good News for All baada ya kusimikwa rasmi katika kanisa hilo la Mapinga Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani hivi karibuni.
  Wazee wa kiroho wa Askofu Gadi wakiwasalimia waumini katika ibada hiyo.
  Rais wa Makanisa ya Kipentekosti Afrika, Dk.Athar Gitonga (kushoto), akimkabdidhi fimbo ya Uaskofu, Askofu Gadi wakati wa ibada hiyo ya kuzimikwa kuwa Askofu wa Makanisa hayo.
  Hapa akikabidhiwa Biblia Takatifu. Kushoto ni Askofu Joshua Lwele.
  Askofu Gadi akikabidhiwa cheti cha kutawazwa kuwa Askofu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Msanii wa muziki  wa Rap toka Kikosi cha Mizinga, Karama Masoud aka Kalapina (kushoto) akipokea fomu za kugombea udiwani kata ya Kinondoni kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo toka kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi Bibi Ikunda Lyimo siku ya Ijumaa jioni. Kala Pina aligombea udiwani kwa tiketi ya chama cha CUF katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo alishindwa na mgombea wa CCM. 
  Karama akipokea fomu za kugombea udiwani toka kwa Bibi Ikunda Lyimo,  anayetazama kulia ni katibu kata tawi la Kinondoni wa ACT Bw Johnson Kapi.
   Akiwa ameambatana na wapambe wake waliokuwa wamepanda bodaboda.
  HABARI ZAIDI INGIA HAPA


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya Uuzaji wa Hisa Stahili, ambapo benki hiyo ilianza rasmi kuuza hisa stahili milioni 435.3 kwa bei ya sh. 350 kwa kila hisa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya Uuzaji wa Hisa Stahili, ambapo benki hiyo ilianza rasmi kuuza hisa stahili milioni 435.3 kwa bei ya sh. 350 kwa kila hisa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya Uuzaji wa Hisa Stahili, ambapo benki hiyo ilianza rasmi kuuza hisa stahili milioni 435.3 kwa bei ya sh. 350 kwa kila hisa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 


   Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza katika hafla hiyo.

  Naibu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishiwa Benki ya CRDB, Ester Kitoka (katikati) akiwa na Naibu Mkurugenzi MtendajiwaBenki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay. 
   Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa (kulia) akiwa katika hafla hiyo.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba.
  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na mgombea uwakilishi wa CUF Jimbo la Ole baada ya kutambulishwa kwa wagombea rasmi wa Ubunge na Uwakilishi.
  Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba.
  Na: Hassan Hamad (OMKR)
  Chama Cha Wananchi CUF kimesema kimejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinapata taarifa za kuwaeleza wananchi kuhusiana na chama hicho kuanzia ngazi za majimbo.
  Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kupitia timu za ushindi wa chama hicho kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu ujao, chama hicho kitatoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ngazi zote kuanzia ngazi ya majimbo, Wilaya hadi Taifa.
  Amesema lengo la hatua hiyo ni kuondosha urasimu wa upatikanaji wa habari ndani ya chama hicho, ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa zinazokwenda na wakati kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi.
  Maalim Seif ameeleza hayo katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro kisiwani Pemba, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho kwa majimbo 18 ya Pemba.
  Amefahamisha kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na chama hicho, kamati tendaji za Taifa, Wilaya na Majimbo sasa zinageuka kuwa timu za ushindi, na kuwataka wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuhakikisha kuwa wanakipatia ushindi mkubwa chama hicho.
  Amefafanua kuwa Chama hicho hakitokuwa na muhali kwa mtendaji yeyote atakayekiuka maadili ya Chama, na kuwaagiza viongozi wa Wilaya na Majimbo  kuwa makini na kuwawajibisha watendaji watakao zembea.
  Wakati huo huo Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema wakati chama hicho kikijiandaa kuchukua fomu za uteuzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, hakitotoa barua kwa mgombea yeyote aliyeshindwa kulipa madeni yake ndani ya chama hicho.
  Amesema Chama hicho hakitokuwa na muhali na jambo hilo, na iwapo mgombea atashindwa kulipa madeni hayo, Kamati tendaji Taifa inaweza kuteua mgombea mwengine wakati wowote.
  Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kudumisha nidhamu ndani ya chama hicho na kuwafanya wanachama kuwa na imani na viongozi wao.
  Chama hicho tayari kimetangaza timu yake ya kampeni kwa upande wa Zanzibar inayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akisaidiwa na Mansoor Yussuf Himid, ambapo kwa upande wa Pemba kampeni za Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho zitaratibiwa na Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa Mhe. Hamad Massoud Hamad akisaidiwa na Waziri wa Habari Mhe. Said Ali Mbarouk.
  Aidha chama hicho cha CUF kimekabidhi seti 40 za jezi na mipira 120 kwa kila jimbo kati ya majimbo 18 ya Pemba na kukamilisha utaratibu wake wa kutoa vifaa kama hivyo kwa majimbo yote 54 ya Zanzibar.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye Baraza la Vijana wa CCM.

   Wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli. 

   Wajumbe wa Baraza la Vijana wakiwa kwenye hamasa ya hali ya juu.
   Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Sixtus Mapunda wakihimiza vijana kuwa imara.

   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiteta jambo na Dk. Emmanuel Nchimbi.

   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa NEC Vijana mara baada ya kufungua na kumaliza kuhutubia Baraza la Vijana wa CCM.


  0 0

    EAC Secretary General Amb. Dr Richard Sezibera with members of Kansas Department of Agriculture after a meeting the SG held with the Department.
   Amb Sezibera stresses a point during the meeting with Kansas State Governor Sam Brownback.

  East African Community Secretariat, Kansas City, USA, August 17, 2015: The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera, concluded a three-day visit to the State of Kansas, United States of America.

  During the visit, the Secretary General met and held talks with the Governor of the State of Kansas, Mr. Sam Brownback, as well as the Kansas Department of Agriculture. Amb. Sezibera and his counterparts held discussions on how EAC can work together with Kansas State in areas of Trade and Investment, Agriculture, Education and Pharmaceutical industries.

  Speaking during the meeting with the Governor, Amb. Sezibera described the progress registered in various regional infrastructure projects, noting that while these projects were negotiated at regional level, implementation was often done by the Partner States.

  The EAC Secretary General informed the Governor that the EAC is open to more structured discussions with the State of Kansas on improving business environment in the region, adding that a bilateral investment agreement framework between both parties was welcome.

  In his remarks, Governor Brownback commended the Secretary General for his leadership and commitment in the East African integration. He said the State of Kansas was elated with the developments within the EAC and would continue keeping tabs on progress of the integration.

  Meanwhile, Amb Sezibera also met the team from Kansas Department of Agriculture and held discussions with the department on various issues including how the EAC Partner States and the State of Kansas can work together towards the introduction of a Smart Agriculture Programme in East Africa.

  0 0

                                            


  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo la Miss Tanzania baada ya mwandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.

  Itakumbukwa kuwa mnano tarehe 22/12/2014 BASATA liliwaandikia barua LINO International Agency Limited ya kulisimamisha shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili (Mwaka 2015 na 2016) na kuwaagiza kujipanga upya na kurekebisha kasoro ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.


  Mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na; mosi, kutokufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa nchini, pili kutokuwasilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake hususan mikataba ya washiriki. Tatu kutumia mawakala wasiosajiliwa na kupewa vibali vya BASATA.


  Miongoni mjwa mapungufu ambayo Kampuni ya LINO imeyafanyia kazi ni kuanza mchakato wa usajili wa mawakala – BASATA na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za uendeshaji wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania. Aidha, LINO imewasilisha muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.


  Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote husika.


  BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote wa Sanaa hususan wale wa shindano la urembo la Miss Tanzania kwamba Kampuni ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa kama masharti ya kufunguliwa. Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.


  Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa yatakayopelekea kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na kuzua sintofahamu katika jamii.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini


  Godfrey Mngereza

  KATIBU MTENDAJI
  0 0   Kadi za NMB Mastercard: Tanzanite, Titanium na World Reward sasa ziko sokoni kwa ajili ya wateja wa NMB.Kwa maelezo zaidi tembelea tawi la NMB lililo karibu yako.
   sehemu ya wageni waalikwa waliokuja kushuhudia uzinduzi huo katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Gold Crest-Mwanza.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Baraka Konisaga(pili kushoto) na Mhazini wa NMB - Aziz Chacha wakipongezana baada ya kuzindua NMB MasterCard kwa Mkoa wa Mwanza na Kanda nzima ya Ziwa katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.Aina tatu za Kadi za NMB Mastercard zilizozinduliwa ni: Tanzanite kwa ajili ya wateja wa kawaida,Titanium kwa ajili ya wateja wa kati na NMB World Reward MasterCard  kwa ajili ya wateja wa kipato cha juu.Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa-Abraham Augustino na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB-Getrude Mallya.

  0 0  Jimmy Jiam akiwa na washindi wa Muzuki Mnene Bango  eneo la Kisarawe,Washindi hao walitokana na kuwenga bango la EFM katika sehemu zao mbalimbali  na kama wanavyoonekana tayari wamekabidhiwa zawadi zao.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikagua timu wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza jana.
   Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza jana.

  MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga jana Jumapili (Agosti 15) alifungua mashindano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza na kuwambia vijana kuwa wanalo jukumu la kubadilisha matokeo ya timu za Tanzania hasa katika mashindano ya kimataifa ambapo Tanzania imekuwa haifanyi vizuri.


  Akifungua mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa Mwanza, Konisaga alisema anaamini kuwa mkoa wa Mwanza umejaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya soka na ndio maana mwaka juzi uliibuka bingwa wa Airtel Rising Stars kwa upande wa wavulana. Amekitaka chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) kutumia mashindano ya Airtel Rising Stars kubaina wachezaji wazuri na kuwaendeleza.


  Mkoa wa Mwanza ulivuma sana miaka ya themanini kupitia timu ya Pamba ambayo wachezaji wake kama vile Joram Mwakatika, Madata Lubigisa, John Mhina, Beya Simba, Raphael Paul na wengine wengi walikuwa moto wa kuotea mbali.


  Mheshimiwa Konisaga ameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza sehemu ya raslimali yao kwenye maendeleo ya mchezo wa soka kwa vijana. “Mashindano ya Airtel Rising Stars ni fursa nzuri. Ni vema timu mbalimbali za soka zikayatumia kupata vijana wenye vipaji na kuwaendeleza”, alisema.


  Alisema mbali ya kuwa jukwaa la kutumia kubaini wachezaji wenye vipaji, Airtel Rising Stars pia yanawahamasisha vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwa na afya njema na kuhudhuria darasani kama kawaida.


  Konisaga aliwaambia vijana kwamba kwa dunia ya leo mpira ni chanzo cha ajira ya kutumainiwa kwa mamilioni ya vijana ambao wanaishi maisha mazuri kwa kuwa wanalipwa mishahara mizuri.


  Aliwataka viongozi wa chama cha soka mkoa wa Mwanza kuchagua wachezaji wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa itakayoshiriki kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam ambazo zinatarajia kuanza mwezi ujao.


  Naye mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana (TFF) Ayoub Nyenzi aliwataka viongozi wa soka kuzingatia kanuni za mashindano hayo has suala la umri.  Mwenyekiti wa MZFA Jackson Songora amejinasibu kwamba mkoa wake una vijana wenye vipaji ambao bila shaka watatwaa ubingwa wa taifa mwaka huu.


  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Ofisa Masoka wa Airtel Tanzania Mkoa wa Mwanza Emmanuel Raphael amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili.

  0 0

  SWAHILI culture is one that is unique. It is the product of the influence of the Middle East, India and Persia on the coastal region . The coast of East Africa had a long history of trade that involved exchange of ideas and commodities. Also mixed marriages between of African women and Middle Eastern men created and cemented a rich Swahili culture.

  Thus the diversity of Swahili culture was a result of the interaction of the coastal people with foreigners in ancient times around the small coastal strip in Dar es Salaam, Lamu, Zanzibar and Mombasa. It is very interesting for travelers and tourists since their uniqueness cannot be compared to other cultures in Africa. Jovago Tanzania mentions some peculiar features which make it distinctive.

  Language - Swahili people use “Kiswahili” as their common language, it’s the language that binds people together. The interactions during the coastal trade and colonialism made the language grow by borrowing words from other languages.

  Artifacts and crafts - Swahili people use various skills to express themselves in artistic forms which include furniture and architecture. The designs are said to be in form of geometry and the crafts specifically Kanga is quite enchanting. It is not just a rectangular piece of cloth but also an artifact of the Swahili culture.

  Women with a khanga
  Music - The outstanding emblematic music genre of the Swahili culture is taarab or taarab, which is mostly sung in the language. The melodies and orchestration have Arab and Indian influences.

  During the 20th century,  several musical  styles have emerged in the Swahili world. A good example is the infusion of ‘Dansi’ derived from Congolese soukous (rumba) and some elements of  Afro-pop
  Old taarab in Zanzibar

  Food; Ugali and chips yai are the very popular food in most of tribes, Ugali can be eaten with stewed or roasted meat especially at home but chips yai is the easiest food to buy at restaurants.
  Ugali

  Recreation - Holiday celebrations are the most important forms of leisure, at the end of the year most people like to travel to their local village for the purpose of greeting their relatives and ancestors

  But also, nowadays some families like to plan for tour instead of going to the village, popular places like Zanzibar, Arusha, Tanga, and Morogoro are great historical sites, and  Dar es Salaam for beaches and enjoying big hotels in town.

  Time - This is very interesting, Swahili time can’t be compared with others, most tourists may get confused  by this, when Swahili people say it is 3 am that means it is actually 9am.

  Greetings - The general greeting is ‘mambo, jambo, and habari’ and the reply is Salama, but for the Muslims like to use the Arabic world “Asalaam Aleikhum”. Nevertheless, children are supposed to greet their elders with respect by touching the forehead or kissing the elder’s hand.

  Transport; Many people use bajaji , motorcycle or dalala for the public transport in Dar es Salaam, but also Tanga and Zanzibar like to use bicycle, and few of them use daladala .

  Bajaji in Dar es Salaam.


  0 0

   Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga akimkaribisha Meneja Mipango  wa Kimataifa wa  Idara ya uya uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle  wakati wa Warsha ya uongozaji  wa ndega  barani afrika  iliyoandaliwa na  Idara ya Anga ya Marekani  .Washa hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara  ya Uongozaji  wa Ndege ya Marekani (FAA) Tony Ferrante.
   Baadhi ya washiriki wa Warsha ya uongozaji wa Ndega  barani afrika  iliyoandaliwa na  Idara ya Anga ya Marekani (FAA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)leo  jijini Dar es Salaam wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa katika warsha hiyo.
   Mkurugenzi wa Idara  ya Uongozaji  wa Ndege  nchini  Marekani (FAA) Tony Ferrante akitoa mafunzo ya uongozaji wa ndege wakati wa warsha iliyowashirikisha waoungozaji ndege kutoka barani afrika ,wakati wa warsha iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa Ndege ya Marekani  na  TCAA ,leo jijini Dar es Salaam.  Wanao msikiliza kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Wa Anga Tanzania (TCAA) Varrely Chanmlunga, Meneja Mipango  wa Kimataifa wa  Idara ya uya uongozaji wa Ndege wa Marekani (FAA) Michele Cappelle  na  mtaalamu  wa mipango  wa idara ya uongozaji wa ndege  wa Marekani FAA,Rebecca Barthe
  Washiriki wa warsha ya uongozaji wa ndege barani afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na Idara ya uongozaji wa ndege ya Marekani FAA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali

  Iddi akikabidhiwa Fomu za kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
  Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Mahonda kutoka kwa Afisa wa Uchaguzi
  Wilaya ya Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis.

   Afisa wa Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B Nd. Makame

  Pandu Khamis akitoa maelezo kumpatia Balozi Seif ya namna ya ujazaji
  wa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda Ofisini kwake Mahonda
  Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unaguja.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
  akisalimiana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi mara baadaya kuchukuwa fomu za kuwania Uwakilishi Jimbo la Mahonda hapo Ofisi yaTume ya Uchaguzi Wilaya ya Kaskazini B iliyopo Mahonda.

  WANACHAMA mbali mbali wa Vyama vya Siasa Nchini walioomba na
  kuthibitishwa na vyama vyao kuwania nafasi mbali mbali za uongozi
  wameanza rasmi kujitokeza kuchukuwa fomu za kuwania kugombea nafasi
  walizoomba katika  Ofisi za Tume ya Uchaguzi za Wilaya.

  Zoezi hilo litalowashirikisha wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na
  Udiwani linatarajiwa kuendelea hadi Tarehe 6 Septemba 2015 ambapo
  wanaochukuwa fomu hizo watalazimika kujaza vipengele vyote vinne
  vilivyomo kwenye Fomu hizo.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa
  miongoni mwa wanachama kadhaa wa Chama cha Mapinduzi waliojitokeza
  kuchukuwa Fomu hizo ambapo yeye ameamuwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa
  Baraza la Wawakilishgi Jimbo la Mahonda.
  Balozi Seif alikabidhiwa fomu hizo mapema asubuhi na Afisa wa Tume ya
  Uchaguzi Zanzibar {ZEC } Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Makame Pandu
  Khamis hapo ilipo ofisi hiyo Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa
  Kaskazini Unguja.

  Akikabidhi fomu hizo Afisa huyo wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya
  Kaskazini B Ndugu Makame Pandu Khamis amethibitisha kwamba Balozi Seif
  Ali Iddi ni Mgombea  halali wa kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la
  Wawakilishi Jimbo la Mahonda kupitia CCM.

  Nd. Makame alisema kwamba uhalali huo unatokana na Ofisi yake kupokea
  barua rasmi kutoka Chama cha Mapinduzi { CCM } iliyoainisha na
  kuthibitisha kwamba Balozi Seif Ali Iddi ameteuliwa na chama hicho
  kuwania nafasi hiyo ya Uwakilishi kwenye Jimbo la Mahonda.

  Afisa Uchaguzi huyo wa Wilaya ya Kakaskazini B alifafanua na kuwataka
  wagombea wote watakaochukuwa fomu za kuwania nafasi hizo kutumia fursa 
  ya kufika kwenye Ofisi hiyo kwa kupata ushauri zaidi wa namna ya
  kujaza vyema fomu hizo licha ya kupatiwa maelezo ya awali wakati
  wanapokabidhiwa.

  Alisema hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itatoa fursa pana ya kutatua
  changamoyo zinazoweza kujitokeza  na  kuepukwa mapema ili kukidhi
  matarahio yaliyopangwa na tume hiyo.

  Balozi Seif Ali Iddi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kitope kupitia chama
  cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ambapo kutokana na
  mabadiliko yaliyofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  jimbo hilo

  limevunjwa na kuzaliwa majimbo mawili ya Mahonda na Kiwengwa.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu maalum kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama ,Ofisi Ndogo Lumumba,kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakatiwa na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakati wa kikao hicho.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana wakipitia baadhi ya ajenda kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za mahudhurio ya kikao kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika kwenye ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.
   Wajumbe wa Kamati Kuu wakipitia makabrasha yenye ajenda za kikao muda mfupi kabla kikao hakijaanza.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi wa semina ya mafunzo ya madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es salaam,  juu ya kuanza kwa kipindi cha mpito cha mradi huo Oktoba mwaka huu, Semina itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu jijini Dar es salaam.
   Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya madereva wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) waliokaa mbele, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki na kulia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi.
   Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia aliyeshika mkasi akikata utepe kuzindua mafunzo madereva wa mabasi yaendayo haraka (BRT) jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mafunzo yayo ya madereva.
   Baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi hapa nchini  wakiwa na abiria katika basi la mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam leo.
   Mgeni rasmi na Waziri Mkuu, tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na mgeni rasmi  Hawa Ghasia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi katika mradi wa mafunzo ya madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka (BRT) jijini Dar es Salaam leo.
  Moja ya mabasi yaendayo mwendo wa haraka yakiwa barabarani katikati ya jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii. 

  Na Mwandishi wetu.

  SERIKALI imewataka madereva walioanza kupata mafunzo ya kuendesha mabasi yatakayotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) kuzingatia mafunzo hayo ya kihistoria hapa nchini.


  Mafunzo hayo yaliyoanza jana ni moja ya matayarisho ya kuanza kwa mradi huo katika kipindi cha mpito mwezi Oktoba mwaka huu.


  Akifungua rasmi mafunzo hayo jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia aliwataka madereva hao kuyapokea kwa bidii na umakini mkubwa.


  “Mafunzo haya yatawapa fursa ya kuweza kufanya kazi kwenye miradi mingine ya BRT kwani vigezo na mtaala wake ni wa kimataifa,” alisema wakati wa maadhimisho hayo katika eneo la Ubungo.


  Waziri Ghasia aliieleza kwamba mafunzo hayo ni ya kihistoria hapa nchini kwani kwa mara ya kwanza watapatikana madereva wenye leseni za kimataifa na kuwa mafunzo hayo yatahusu pia namna ya kuhudumia wateja.


  “Madereva hawa watajengewa weledi na nidhamu katika kazi yao ambayo kwa sasa inalalamikiwa sana na wananchi wakilalamikiwa kwa utovu wa nidhamu na kutotii sheria za barabarani,” alisema.


  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiki alisema kuzinduliwa kwa mafunzo hayo ni ushahidi wa dhamira ya serikali kutatua kero ya usafiri na msongamano wa magari jijini humo kupitia mradi wa BRT.


  “Mradi huu wa aina yake nchini na barani Afrika utatoa fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara kwa sekta binafsi ambayo ndio msingi wa maendeleo ya nchi,” alisema.


  Mafunzo hayo kwa madereva wazalendo yanafanyika baada ya kushinda usaili ulio endeshwa na wataalamu kutoka chuo cha ufundi stadi na mafunzo (VETA).


  Jumapili iliyopita kampuni ya watoa huduma wa ndani wa mradi huo, UDA-RT iliendesha semina ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na huduma za kipindi cha mpito za mradi huo.


  Mradi huo wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa kilometa 20.9 za barabara maalum kutoka Kimara hadi Kivukoni; barabara ya Msimbazi kutoka Faya hadi Kariakoo-Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni hadi eneo la makutano ya Morocco.

  0 0


  0 0

   Hon. Bernard Kamilius Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation receives Copies of Letters of Credence of H.E. Ambassador Sandeep Arya, the new High Commissioner of India to the United Republic of Tanzania.The Ceremony took place today in the Minister's Office in Dar es Salaam.
  Hon. Membe (right) exchanges views with H.E. Arya.
  Officials of the Ministry of Foreign Affairs take notes during the meeting. They are, from left: Thobias Makoba, Mkumbwa Ally and Emmanuel Luhangisa.
  conversation in progress
  Photo By Reuben Mchome.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  akifungua kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji wa  uchumi Tanzania
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Consolata Mgimba akizungumza katika kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania. 
  Washiriki wa kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 
   Baadhi ya washiriki katika kikao kazi cha wadau cha kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa kujenga na kuimarisha Stadi za kazi katika Sekta zinazochochea ukuaji Uchumi Tanzania.

older | 1 | .... | 942 | 943 | (Page 944) | 945 | 946 | .... | 3278 | newer