Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 941 | 942 | (Page 943) | 944 | 945 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014. Mh. Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa wananchi.
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
  Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini  Mbeya leo Agosti 14, 2014.

  KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  DSC_0016Mwenyekiti wa Kamati kuu wa tamasha la 34 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Bw. John Mponda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika ukumbi wa MAELEZO mapema leo 8.14.2015. Wengine ni Mwalimu Christa Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa Maonyesho (kulia) na kushoto ni Bw. Frank Sika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Majukwaa na Ufundi wa tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu (Picha zote na Andrew Chale wa modewjiblog)
  TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
  (TaSUBa)
  945988442748510035_tangazo_html_mb1ecfee
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU .TAMASHA LA 34 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO.

  Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Lengo kuu la Tamasha kwa wakati huo ilikuwa ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, baada ya Tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa chuo uliamua tamasha hilo lifanyike kila mwaka kwa kushirikisha Vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana Uzoefu na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.


  0 0

  The Defence Forces of the EAC Partner States (Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda and Tanzania) will hold the 9th Edition of the East African Military Games and Cultural Event from 15 to 26 August 2015 at the Mandela National Stadium in Kampala, Mukono and Jinja in the Republic of Uganda.

  The event, themed One People One Destiny through EAC Military Games and Cultural Event 2015, will involve over 500 participants representing the various services of the Defence Forces of the EAC Partner States.

  The games will involve the disciplines of Athletics (Cross-country Race), Boxing, Football, Netball and Handball. The event is expected to have high profile participation intended not only to popularize the event but also to raise the sporting competitive levels thereby contributing to the highest standards within the East African region commensurate with international standards.

  The East African Military Games and Cultural Week is an annual event instituted since 2005 when the first edition was held Kampala, Uganda. The second edition of the games was held in Nairobi Kenya in 2006. The objective of the Military Games is to contribute to building confidence among the EAC Defence Forces under the EAC Memorandum of Understanding on Co-operation in Defence Matters.


  0 0

  The East African Secretariat has received a donation of various essential medicines and health supplies from the Federation of East African Pharmaceutical Manufacturers (FEAPM) for emergency humanitarian assistance to Burundi refugees’ camps in Kigoma region of Tanzania and Eastern Province of Rwanda.

  Dr. Dhirendra Shah, FEAPM Chairman, accompanied by Dr. Ashvin Pandya, Member of the Board of the Federation, handed over the first consignment of medical supplies to Hon. Jesca Eriyo, EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors. The handing over ceremony took place at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania, on the sidelines of the ongoing 32nd meeting of the Council of Ministers-the EAC Policy Organ. 

  “We are very grateful to FEAPM for today’s donation, as these medicines are badly needed over at the refugee camps in Tanzania and Rwanda,” said Hon. Eriyo, adding that “This is a good partnership we have started, and through this relationship we will encourage citizens to purchase medicines locally so as to boost the East African Pharmaceutical sector”. 

  The emergency medical support came from a team effort of fourteen pharmaceutical manufacturing companies from Kenya, Uganda, Rwanda and Tanzania.

  The medical supplies will go towards treating Burundi refugees suffering from cholera outbreaks and other outbreaks of various communicable diseases at camps in Kigoma, Tanzania and the Eastern Province of Rwanda. 

  “We are very pleased to have donated medicines for a good cause as we are always there whenever there is a crisis; in the past we come to the aide of the crisis in Rwanda, South Sudan, Somalia, and now Burundi,” said Dr. Shah. “We promise to continue providing humanitarian assistance for the people of East Africa,” he said.  
  Dr. Dhirendra Shah, FEAPM Chairman (3rd left), handingover medical supplies to Hon. Jesca Eriyo, EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors. Also present in the ceremonial handing over are Dr. Ashvin Pandya, Board Member of FEAPM (2nd left); Hon. Philemon Mateke, Uganda’s Minister of State for Regional Cooperation (grey suit); Hon. Amantus Msole, Deputy Permanent Secretary for MEACA Tanzania (2nd right); Commissioner Rona from MEACA Uganda and EAC senior staff members Dr. Stanley Sonoiya, Principal Health Officer (3rd right) and Jennifer Gache, Senior Industrial Engineer (far left).

  0 0


  0 0

  Akiendelea na ziara katika Mamlaka zinazohusu udhibiti wa huduma za kiuchumi na za kijamii,Waziri wa Nchi(Kazi Maalum), Ofisi ya Rais,Profesa Mark Mwandosya ametembelea makao makuu ya Tume ya Ushindani wa Haki kibiashara, na Baraza la Ushindani, Ubungo, Dar es Salaam. 

  Tume ya Ushindani(Fair Competition Commission-FCC) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003. Madhumuni makubwa ya uwepo wa Tume ni kukuza na kulinda ushindani wa haki katika biashara na kumlinda mtumiaji wa bidhaa na huduma dhidi ya mwenendo usiofaa katika soko. Baraza la Ushindani,ambalo ni baraza la rufaa nalo limeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 ili kusikiliza na kutoa maamuzi ya kesi zinazohusu masuala ya ushindani.

  Akiongozana na maafisa waandamizi kutoka vyombo vya udhibiti vya kisekta, SUMATRA, TCAA, TIRA, na EWURA, Waziri Mwandosya alipata taarifa za utendaji na kuzungumza na watendaji wa FCC na FCT kuhusu mafanikio na changamoto, namna ya kukabili changamoto hizo ili kuzifanya taasisi za udhibiti zichangie vilivyo katika kukuza uchumi.

  Katika picha ya kwanza waliokaa, kushoto ni Dr Frederick Ringo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani. Katikati ni Waziri Mwandosya, na kulia ni Ndugu Paul Ngwembe,Mkurugenzi wa Sheria, Mamlaka ya Udhibiti wa sekta ya Bima. Wengine ni maafisa wa Tume,na wawakilishi wa mamlaka za udhibiti za kisekta.

  Katika picha ya pili, Profesa Mwandosya ,katikati,akiwa na Ndugu Kunda Mkenda,Kaimu Msajili wa Baraza la Ushindani,kulia kwake, pamoja na maafisa watendaji wa Baraza na kutoka mamlaka za udhibiti za kisekta.

  0 0
  0 0  0 0

  Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
   Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
  Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.
   Baadhi ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
  Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.

  Na Mwandishi Wetu.
  Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
  Wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.
  Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.
  Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.
  Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi wanayemtaka.
  “Tumejiandaa vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema Professa J.
  Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.
  Akizungumza katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.
  “Hii siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature.

  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi baada ya kuweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
   Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi zikioneshwa huku zikishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam
   Mwenyekiti wa Business Roundtable Ali Mufuruki na Mkuu wa Brela wakisaini kwa niaba ya sekta binafsi na za umma Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam. 


  0 0

  SIMUTV: Mbowe adaiwa kuuza chama bei chee, fahamu mengi kuhusu hili na mengine mengi kupitia dondoo za magazeti hapa Simu.tv . https://youtu.be/4sKlAHoa_QM   
  SIMUTV: Daktari feki atibu watu 20,abainika kuwa na elimu ya darasa la saba,fuatilia hili na mengine mengi kupitia Uchambuzi wa magazeti ya leo ; https://youtu.be/dnRNQ0D1Iqs
  SIMUTV: Jeshi la wananchi  Tanzania JWTZ lawaonya wanasiasa nchini. Ni moja kati ya habari zilizopewa kipaumbele magazetini leo; Bofya hapa; https://youtu.be/U2_lcOA7Uc0 
  SIMUTV: Shaaban Kisiga atamba kuirejesha shooting ligi kuu.Pata habari motomoto  za michezo   katika magazeti ya leo hapa Simu.tv; https://youtu.be/RAu00vxOU5E

  0 0
 • 08/15/15--02:00: Scania P420 inauzwa
 •  Scania P420 ya Mwaka 2005 na iko katika hali nzuri kabisa. Bei mil 85 majadiliano yapo, ila dalali hatakiwi kabisa. Gari iko Dar es salaam tayari  na imeshalipiwa kila kitu. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0754396519.
   Ubavu wa kushoto
   Ubavu wa kulia
  Mbele kulia

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin wakati alipowasili hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria hafla ya Kongamano la pili la Diaspora. Kushoto mwenye kanzu ni Mhe Ali Mzee Ali, Mjumbe wa Bodi ya AICC
  Rais Kikwete akiwa meza kuu na viongozi wengine katika  hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakati wa hafla ya Kongamano la pili la Diaspora. Wengine kutoka kulia ni Mhe Ali Mzee Ali, Mjumbe wa Bodi ya AICC, Bw. Matheu Lamolle Mtafiti wa Massoko wa Taasisi ya International Trade Centre (ITC) ya Uswisi ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu  Zanzibar (Utawala Bora)  Mhe Dk Mwinyihaji Makame, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania DMV Marekani  Bw. Iddi Sandaly, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula na Bi Mariam Mungula wa Diapora London
  MC wa hafla hiyo ambaye ni Mratibu wa Dawati la Diaspora katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bi Suzana Mzee akiwa kazini
  Wadau wa Diaspora kutoka nchi mbalimbali na Tanzania  katika  hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakati wa hafla ya Kongamano la pili la Diaspora.

  0 0

  Umati wa Wakazi wa mji wa Tengeru, ukiwa umefurika kwa wingi barabarani kumlaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa alipopita eneo hilo, wakati akielekea Jijini Arusha kwenye Mkutano wa hadhara wa kutambulishwa kwa Mgombea huyo kwa wananchi wa Arusha,uliofanyika kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa wamesimama pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha walifurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, wakati wa kuimba wimbo wa Taifa.
  Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa kumtambulisha.
  Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na kutambulishwa kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kimandolu, leo Agosti 15, 2015.
  Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.

  KUONA PICHA ZAIDI
  BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

  0 0

  Curious on Tanzania is an organization and a platform that promotes Tanzanian tourism in the United States of America. Its founder and CEO, Justa Lujangwana is determined to make Americans and the people of other nationalities taste what she describes as a "Tanzanian Flavor". By this, she means whatever that is Tanzanian in terms of music, cuisine, history, tourism and even beauty. The aim of her organization is to  make Americans be aware of what Tanzania has to offer be it culturally, socially or economically, but everybody is invited.
  On September 5th, 2015 Justa and her organization will be organizing the first Tanzanian Fest ever in New York City at Punta Space 325 West 38th Street. You are  invited to attend this special event. In this interview, Justa explains what you should expect from the Curious on Tanzania Fest 2015.
  You are welcome to watch this show on Friday August 21th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 60 Minutes. The above video has only 36 minutes of the 60 minutes. To watch the entire 60 minutes of the show please see the details below.

  Provider Channel
  Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998
  FiOS 36
  RCN 85

  To stream online tune to channel 4 @ www.mnn.org/4-culture-channel%20 every friday from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time).

  Thank You and Stay Tuned.

  0 0
 • 08/15/15--16:00: Article 12
 • Na: Hassan Hamad (OMKR) 
  Chama Cha Wananchi CUF kimesema kimejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinapata taarifa za kuwaeleza wananchi kuhusiana na chama hicho kuanzia ngazi za majimbo. Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kupitia timu za ushindi wa chama hicho kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu ujao, chama hicho kitatoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ngazi zote kuanzia ngazi ya majimbo, Wilaya hadi Taifa. 
  Amesema lengo la hatua hiyo ni kuondosha urasimu wa upatikanaji wa habari ndani ya chama hicho, ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa zinazokwenda na wakati kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi. Maalim Seif ameeleza hayo katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro kisiwani Pemba, wakati akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho kwa majimbo 18 ya Pemba. 
  Amefahamisha kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na chama hicho, kamati tendaji za Taifa, Wilaya na Majimbo sasa zinageuka kuwa timu za ushindi, na kuwataka wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuhakikisha kuwa wanakipatia ushindi mkubwa chama hicho. Amefafanua kuwa Chama hicho hakitokuwa na muhali kwa mtendaji yeyote atakayekiuka maadili ya Chama, na kuwaagiza viongozi wa Wilaya na Majimbo kuwa makini na kuwawajibisha watendaji watakao zembea. Wakati huo huo Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema wakati chama hicho kikijiandaa kuchukua fomu za uteuzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, hakitotoa barua kwa mgombea yeyote aliyeshindwa kulipa madeni yake ndani ya chama hicho. 
  Amesema Chama hicho hakitokuwa na muhali na jambo hilo, na iwapo mgombea atashindwa kulipa madeni hayo, Kamati tendaji Taifa inaweza kuteua mgombea mwengine wakati wowote. Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kudumisha nidhamu ndani ya chama hicho na kuwafanya wanachama kuwa na imani na viongozi wao. 
  Chama hicho tayari kimetangaza timu yake ya kampeni kwa upande wa Zanzibar inayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akisaidiwa na Mansoor Yussuf Himid, ambapo kwa upande wa Pemba kampeni za Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho zitaratibiwa na Mjumbe wa Kamati Tendaji Taifa Mhe. Hamad Massoud Hamad akisaidiwa na Waziri wa Habari Mhe. Said Ali Mbarouk. Aidha chama hicho cha CUF kimekabidhi seti 40 za jezi na mipira 120 kwa kila jimbo kati ya majimbo 18 ya Pemba na kukamilisha utaratibu wake wa kutoa vifaa kama hivyo kwa majimbo yote 54 ya Zanzibar.
   Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na mgombea uwakilishi wa CUF Jimbo la Ole baada ya kutambulishwa kwa wagombea rasmi wa Ubunge na Uwakilishi.
   Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Ismail Jussa Ladhu, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba.
  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi pamoja na wagombea wa chama hicho katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Kisiwani Pemba. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

   Rais wa VICOBA Endelevu, Devota Likokola, (Watatu kushoto), akinyanyua juu, mfano wa ATM kadi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo itakayotumiwa na wanachama wa VICOBA Endelevu kota nchini. Uzinduzi huo ulifanyika leo Agosti 15, 2015 kwenye bustani ya kumbukumbu ya mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, Mwenyekiti wa Bodi wa Wadhamini ya Benki hiyo, Profesa Lettic Rutashobya, na Katimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, Beng’ Issa.(Picha na Habari na K-VIS MEDIA)

  BENKI ya Posta Tanzania, TPB, imezindua rasmi kadi maalum ya ATM kwa ajili ya wanachama wa kikundi cha, VICOBA Endelevu.

  Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika kwenye bustani ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2015, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TPB, Profesa Lettic Rutashobya, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Beng’ Issa, walishuhudia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, akimkabidhi mfano wa kadi hiyo ya ATM, Rais wa Vicoba Endelevu, Devota Likokola mbele ya mamia ya wanachama wa Vicoba Endelevu kutoka sehemu mbalimbali nchini.

  Benki ya Posta Tanzania, imeingia mkataba na Vicoba Endelevu, wa kuwapatia mikopo midogomidogo wananchama hao chini ya udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, ili kukuza mitaji na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.


   Wana VICOBA Endelevu wakiingia kwenye bustani hiyo kwa maandamano. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kwamba ujenzi wa Nyumba  1,500 zinazotarajiwa kujengwa katika eneo Huru la uwekezaji Vitega Uchumi katika ukanda wa Fumba utasaidia kupunguza ufinyua wa makaazi kwa Wananchi wazalendo pamoja na wawekezji wanaoamua kuanzisha miradi yao hapa Zanzibar. 
  Alisema ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya CPS Live ya Nchini Ujerumani ambayo tayari imeshasajiliwa hapa Zanzibar utaenda sambamba na kutoa ajira kwa kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo yao. 
  Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizindua rasmi matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba hizo kwa njia ya fedha taslimu na mkopo uliotayarishwa na Kampuni hiyo hapo katika eneo linalotarajiwa kujengwa nyumba hizo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”. 
  Alisema Wawekezaji wengi pamoja na baadhi ya wananchi watapata fursa ya kuondokana na tabia ya kukodi nyumba jambo ambalo huwapa gharama kubwa kulitekeleza. Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarajika kuona kwamba Wawekezaji wameanza kuitikia wito wa Serikali wa kuanza kuonyesha ishara ya kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa uchumi wa Taifa. 
  “ Nyumba hizo kwa mujibu wa nilivyoziona ni nzuri zikiwa katika eneo safi na kiwango kijnachokubalika kimataifa na itategemea mhusika mwenyewe hadhi na thamani ya nyumba atayohitaji kununua au kukopeshwa “. Alisema Balozi Seif. 
  Aliwaomba Wananchi wenye uwezo na wale wawekezaji wenye miradi ya kudumu hapa Nchini kuunga mkono katika ununuzi au ukopaji wa nyumba hizo ili kuondokana na matatizo ya makazi. Akimkaguza Balozi Seif kuona sampuli ya nyumba za mfano zilizojengwa kwenye mradi huo Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live Bwana Sebastian Dietzold alisema ujenzi huo utaanza na Nyumba 416 katika awamu ya kwanza. Bwana Sebastian alisema sehemu hiyo iliyopimwa kitaalamu kwa kuzingatia mipango miji itagaiwa kwa kujengwa nyumba kumi kwa kila kipande kimoja ambapo suala la mazingira itazingatiwa katika hali inayokubalika. 
  Alifahamisha kwamba utunzaji wa mazingira ni suala litakalotiliwa mkazo kwa kuandaliwa taratibu maalum wa kutolewa elimu utakaohusisha wanafunzi maskulini. Bwana Sebastian alieleza kwamba huduma za lazima zitazingatiwa kwa kupatikana kwenye nyumba zote zitakazojengwa eneo hilo sambamba na ujenzi wa Kituo cha Polisi, Hospitali viwanja wa michezo mbali mbali pamoja na maeneo ya mapumziko. 
  Mapema Mkurugenzi wa Huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Ndugu Sharif Ali Sharif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitangaza kwamba Fumba ni eneo Tengefu la Uwekezaji mwaka 1992. 
  Nd. Sharif alisema Fumba sasa imefumbuka kutokana na mwanzo mzuri wa uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi unaoanza kutekelezwa na baadhi ya wawekezaji ndani ya eneo hilo. Mradi wa ujenzi wa Nyumba za kuuzwa kwa fedha taslimu na Mkopo uliopo eneo huru la Uchumi Fumba unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni Mia Moja na Ishirini { U$ Dollar 120,000,000 }.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live inayotarajiwa kujenga Nyumba za Mkopo katia Eneo Huru la Uwekezaji Fumba Bwana Sebastian Dietzold akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipowasili eneo hilo kuzindua matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba hizo.
  Nyuma ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Ndugu Sharif  Ali Sharif.
   Baadhi ya sehemu za ndani za Nyumba za mfano zilizojengwa kwenye  eneo Huru la Uwekezaji liliopo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.
   Baadhi ya sehemu za ndani za Nyumba za mfano zilizojengwa kwenye  eneo Huru la Uwekezaji liliopo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.
   Baadhi ya sehemu za ndani za Nyumba za mfano zilizojengwa kwenye  eneo Huru la Uwekezaji liliopo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live Bwana Sebastian Dietzold akimueleza Balozi Seif taaluma inayotumika katika ujenzi wa Nyumba za Mkopo ambapo asilimia kubwa wanatumia mali ghafi za hapa Zanzibar. Picha na OMPR,  ZNZ.


  0 0

  Naibu waziri wa maji Amos G Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Sengerema kwa kukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika na serikali ya Tanzania.
   Mradi huu unagharimu shilingi bilioni 20 na utanufaisha watu wapatao 108,000 hadi kufikia mwaka 2025 
  Naibu Waziri wa maji ametembelea chanzo cha maji ziwa victoria kijiji cha Nyamazugo, ujenzi wa matanki maeneo ya Mwabaluhi na Igogo na kuwataka wakandarasi kampuni ya Kichina Ya CCECC ltd na mhandisi mshauri kampuni ya COWI kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha ujenzi wa mradi ifikapo Februari 2016.
   Aidha ameagiza mkandarasi kuanza ulazaji wa mabomba kutoka tanki la Nyamazugo kwenda tanki la Igogo ili kuharakisha upatikanaji wa maji.
  Amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati mradi huu unatekelezwa kwani kukamilika kwa mradi huo kutawanufaisha wao wananchi wa sengerema Amepongeza jitihada za mkuu wa wilaya ya sengerema na mamlaka ya Maji mkoa wa Mwanza kwa pamoja wamewezesha mradi kufikia hatua nzuri
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Amos Makalla akiongea na waandishi habari eneo la Igogo
  Mhe Makalla akiwa na  mhandisi mshauri wa kampuni ya COWI Bw. Michael Nyagabona


  Mhe Makalla akikagua mradi huo

  Mhe Makalla akiongea na Mkuu wa wilaya Sengerema bi Zainabu Taleck na wataalamu wa mradi


  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter  Pinda(katikati) akipokea Salaam kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kwa Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Daraja la kwanza akiongozwa na Kamanda wa Gwaride. Sherehe hizo zimefanyika leo Agosti 15, 2015 katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akitoa cheti cha sifa kwa Mwanafunzi Mhitimu wa Mafunzo hayo, Wdr. Raymond Mgosso ambaye amefanya vizuri masomo ya Darasani(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa jukwaani akifuatilia  kwa makini Onesho Maalum la zoezi la kujihami(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
   Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la kwanza likipita mbele ya Jukwaa kutoa heshima kwa Mgeni rasmi kwa mwendo wa haraka.
   Askari wa Kike ambao wamehitimu Mafunzo hayo wakionesha zoezi la kujihami(Self Defence).
   Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi. 
  Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza(wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

older | 1 | .... | 941 | 942 | (Page 943) | 944 | 945 | .... | 3278 | newer