Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mkutano wa Masuala ya Serikali Mtandao kufanyika jijini Arusha Agosti 17

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo katika ukumbi wa Habari (MAELEZO) kuhusu mkutano wa Serikali Mtandao utakaowakutanisha Watendaji Wakuu na Maofisa wa Ngazi na Fani Mbalimbali kutoka Serikalini utakaofanyika jijini Arusha Agosti 17-20,2015. 

JWTZ YAKANUSHA KUWANYANG'ANYA KADI ZA KUPIGIA KURA MAOFISA NA ASKARI WAKE

$
0
0

Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akikanusha jeshi hilo kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na kiongozi mmoja wa chama cha siasa. Kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omari.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na  kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.

"Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa.
Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia. Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo.

"Wananchi na viongozi wa kisiasa mnaombwa mfanye kazi zenu za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa wananchi" alisema Kanali Lubinga.

Kanali Lubinga alisema jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani wananchi wanaimani na jeshi lao.
 Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lafanyika

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu akifungua mkutano wa  baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam mapema leo.
Baadhi ya Wajumbe wa  Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Dar es Salaam mapema leo. 

Watanzania walionufaika na Ufadhili wa Masomo nchini Japan waagwa

$
0
0
 Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo wa mpango wa ABE Initiative  wakati wa hafla fupi ya kuwaaga  iliyofanyika nyumbani kwake mapema jana
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa sita kutoka kulia) na Balozi wa Japan nchini Bw. Masaharu Yoshida (wa tano kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watanzania wakionufaika na ufadhili wa mpango wa ABE Intiative baada ya hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo mapema jana. Wengine ni Maofisa kutoka Utumishi na JICA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ateua wajumbe wa Bodi ya KADCO na RAHCO

Waziri Membe atembelea mabanda ya maonesho wakati wa Kongamano la Diaspora

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akipata maelezo kuhusu na matumizi ya Gesi Asilia, Miradi na manufaa yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. James Mataragio (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa Kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) .
Waziri Membe akionyeshwa na Bw. Mataragio eneo bomba la gesi asilia lilipopita kwenye Mchoro wa Ramani ya Tanzania uliopo mbele yao.
Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Dorcas Membe (kushoto), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Mataragio (Kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) na Watumishi kutoka katika shirika hilo.
Waziri Membe na Mkewe Mama Dorcas wakipata maelezo juu ya matumizi ya radio calls kutoka kwa  Bw. Sunji wa Kampuni ya Huawei nchini alipotembelea banda la Kampuni ya hiyo wakati wa Kongamano la Diaspora.
Waziri Membe (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) nchini, Bi. Matilda Nyallu. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Mulamula (katikati) akielezea jambo kwa Waziri Membe (kushoto).
Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa  Washiriki wa Kongamano la Pili la Diaspora,Bw. William Malecela. Kulia ni Balozi Mulamula na katikati ni Bi. Suzani Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa pili kutoka kushoto)na Maafisa Mambo ya Nje Bw. Batholomeo Jungu ( kulia) na Bw. Amosi Tengu ( kushoto). 
Picha na Reginald Philip

Bodi ya Mikopo kuendelea kutekeleza majukumu yake ili kuinua sekta ya elimu

Kongamano la Diaspora na Wajasiriamali likiendelea kwa siku ya pili jijini Dar es Salaam

$
0
0

Chukwu-Emeka Chikezie akiongoza moja ya mdahalo katika kongamano la Diaspora, Balozi wa Marekani nchini Mhe. Mark Childress kwa pamoja na Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Watendaji Wakuu nchini, Bw. Richard Miles, Mwakilishi wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Marekani nchini na Dkt. Silencer Mapuranga, Mchumi kutoka ITC.
Balozi wa Marekani nchini, mhe. Childress akichangia mada kuhusu mabadiliko ya kiuchumi Tanzania wakati wa Kongamano la Diaspora.
Bw. Miles nae akichangia wakati wa mjadala kuhusu mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na namna ya kuwashirikisha wafanyabiashara wadogo na wakati katika maendeleo ya nchi.
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa mjadala huo .
Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing akiwasilisha mada kuhusu Mapinduzi ya Viwanda nchini na wajibu wa Diaspora katika ukuaji wa SME's
Balozi Lu akiwasilisha mada yake

PICHA ZAID BOFYA HAPA

MGOMBEA WA CHAMA CHA WAKULIMA ACHUKUA FOMU YA URAIS LEO

$
0
0
  Afisa Uchanguzi Mwandamizi Deogratus Nsawagwanko akimkabidhi fomu Mngombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupiti chama cha wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi leo katika ofisi za Tume ya uchaguzi  jijini Dar es Salaam.
Afisa Uchanguzi Mwandamizi, Rafiki Kiravu akitoa  maelekezo kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi kabla ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo leo  katika ofisi za Tume ya uchaguzi (NEC) jijini Dar es Salaam.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia  chama cha wakuliama (AFP), Omari Mohamed Sombi akionesha fomu ya kuwania nafasi hiyo hapa nchini  akiwonesha waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi za tume ya uchanguzi (NEC) leo jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.)

JARIDA LA WIKI WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

IDADI YA WANAFUNZI WANAONUFAIKA NA MIKOPO YAZIDI KUONGEZEKA

$
0
0
Na Jenikisa Ndile
Idadi ya wanafunzi  wanaopata  mikopo kutoka   Bodi ya Mikopo  kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia kuongeza idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu.


Katika mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo kwa  wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh.  bilioni 56.1  na mwaka wa masomo wa 2014/2015 bodi ya mikopo ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000 iliyogharimu shilingi bilioni 345.


Hayo yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati akizungumza na waandishi wa  habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu mafanikio ya  bodi hiyo katika kipindi hicho.


Alisema kwa kipindi hicho chote  wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa wanufaika hadi pale bodi  ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006/2007.


Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa  na mafanikio makubwa kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi katika matumizi ya teknolojia  ya habari na mawasiliano (TEHAMA)  kwa lengo la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo  wa (OLAMS)

Aidha  bodi hiyo  imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.


Bodi hiyo imewawezesha wateja wake  kupata huduma katika maeneo manne ambayo ni  Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu zaidi.


Mwaisongwa   aliwahakikishia wateja  hao  wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua kuwa mikopo ya wanafunzi  wa elimu ya  juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha mfuko huo  kuwa endelevu.


Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba  9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa endelevu.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAJI AMOS MAKALLA MJINI GEITA

$
0
0
NAIBU waziri wa maji Amos Makalla leo ametembelea mradi  unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) wa uboreshaji huduma ya maji kwa mji wa Geita, Mradi huu unagharimu fedha sh 10 bilioni ambao kukamilika kwake kutaongeza huduma ya upatikanaji maji kutoka asilimia 13 iliopo sasa hadi  kufikia asilimia 57.

Kwa mujibu wa tathmini ya kazi iliyofanyika mradi huu unatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwezi august mwaka huu na naibu waziri wa maji ameagiza wahakikishe wananchi wanapata maji wiki ya kwanza mwezi ya mwezi septemba na si vinginevyo.
NAIBU waziri wa maji,Amos Makalla akikagua kazi za uchimbaji mitaro, ulazaji wa mabomba na ukaguzi wa tanki leo katika mji wa Geita
 NAIBU waziri wa maji Amos Makalla akitembele maeneo mbalimbali yaliyo na mabomba ya maji.

Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa akimpokea naibu waziri maji Amos Makalla.

SUGU, NATURE, PROFESSA J KUFANYA SHOO YA KUHAMASISHA MASHABIKI KUPIGA KURA OKTOBA 25, 2015

$
0
0

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule “Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. 
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

LAPF YAMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Manispaa ya Kinondoni. Vifaa vilivyotolewa na mfuko huo ni jezi seti 30, mipira 30 pamoja na viatu jozi 30. (Na Mpiga Picha Wetu)
Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 5 mjumbe wa bodi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni, Abbas Tarimba. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya timu hiyo, Yusuph Mwenda zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya timu hiyo. 
Meneja Masoko Kanda ya Pwani, Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Bodi ya timu soka ya Kinondoni, Yusuph Mwenda zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya timu hiyo. Wanaoshuhudia ni wajumbe wa Bodi ya timu hiyo, Abbas Tarimba (kulia) na Mtemi Ramadhani (wa pili kushoto).

SEKTA BINAFSI YASAINI HATI YA UADILIFU

$
0
0
Na Lilian Lundo, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete  (Pichani)amezipongeza sekta binafsi kwa kukubali kusaini hati  ya ahadi ya uadilifu  katika harakati za mapambano dhidi ya rushwa na utovu wa nidhamu.

 Rais alisema hayo katika wakati akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa hati hizo zinazojumuisha sekta ya Umma na  Binafsi katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Katika hafla hiyo,  Mhe. Rais alisaini hati tatu ambazo ni Hati ya ahadi ya uadilifu ya Viongozi wa Umma, hati ya ahadi ya uadilifu ya Utumishi wa Umma na hati ya uadilifu ya Sekta Binafsi. 

“Ushiriki wa sekta binafsi katika hati hii utasaidia kuleta mabadiliko ya kuwa na mwenendo wa kimaadili ya mapambano dhidi ya rushwa” alisema Mhe. Kikwete.

Rais Kikwete alisema kuwa badala ya wananchi na sekta binafsi kulalamika pembeni ni vyema kuwasilisha malalamiko yao katika sehemu husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

 Aidha, Rais aliongeza kuwa baadhi ya sekta binafsi  zimekuwa zikiombwa na kutoa rushwa ili kupewa  upendeleo wa kupata  tenda serikalini, hivyo kwa kusaini hati   hiyo ya ahadi ya uadilifu kutaondoa mianya ya  upokeaji na utoaji rushwa katika sekta hiyo.

Hati ya ahadi ya uadilifu inakumbusha Makampuni, Viongozi na Watumishi wa Umma juu ya wajibu wao wa kuzingatia kanuni za maadili na mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Wazo la kuwa na ahadi ya uadilifu liliibuliwa katika maabara ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambapo ilionekanakuwa rushwa bado ni tatizo katika uendeshaji wa shughuli za Umma na Binafsi hususani utoaji huduma kwa umma na biashara.

Article 2

MTOTO CHINI YA MIEZI SITA HAWATAKIWI KUPEWA MAZIWA YA NG'OMBE-TFNC

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

IMEELEZWA kuwa Mtoto chini ya mwezi hatakiwi kunywa maziwa yeyote isipokuwa ya mama yake, kutokana na maziwa ya ng’ombe  kuwa mazito na hayawezi kumsaidia mtoto katika kukua kwake.

Hayo ameyasema mtaalam wa lishe  wa Taasisi ya Chakula  lishe  nchini (TFNC),Neema Joshua wakati wa semina ya waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa masuala ya Lishe,amesema maziwa ya ng’ombe yanatumika tu pale hakuna namna ya kuweza kupata maziwa mengine.

Amesema watoto chini ya miezi sita wanahitaji maziwa kwa mama na anatakiwa kupewa kila muda katika kuweza kumjenga mtoto kiakili.

Neema amesema katika suala la utapiamlo liko katika viwango vya juu ambapo mwaka 2010 ilikuwa na asilimia 42 hadi sasa imefikia asilimia 34.7 kwa takwimu za mwaka 2014.

Aidha amesema kuwa wale ambao wananyonyesha wakapata mimba akiwa ananyonyesha anaweza  kuuendelea kunyonyesha mtoto na bila kuathiri mimba nyingine.

Amesema wakati akinyonyesha huku ana mimba nyingine anatakiwa karibu na kujifungua miezi miwili aache kwa ajili ya kuupa mwili nguvu kwa mtoto atakayezaliwa na baada ya hapo anaendelea kunyonyesha wote wawili kwa kwanza akifikisha miwili ndipo anaweza kukoma.

CCM YAKANUSHA UVUMI WA HABARI YA MGOMBEA WAKE WA URAIS DKT JOHN MAGUFULI KUAHIDI KUGAWA KOMPYUTA KWA WALIMU NCHINI

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Lumumba jijini Dar,kuhusiana na madai ya kauli inayodaiwa kutolewa na Mgombea wa Urais wa Chama hicho Dkt John Magufuli kuwa kupitia Ilani yake ya chama atatoa kompyuta kwa Walimu nchi nzima iwapo CCM itapita madarakani,habari ambazo Nape amezikunusha vikali na kusema hayo ni maneno ya uzusihi na kuwa Dkt Magufuli hajawahi kutamka maneno hayo popote pale.
 Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.Nape amefafanua kuwa kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani  ya chama cha CCM,siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.
  Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.


NA BAKARI ISSA WA GLOBU YA JAMII.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.

Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.

Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho,Nape amesema " Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzi,hiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.

TCRA Renews Licenses of Seven Broadcasting Stations.

$
0
0

The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director, Licensing Services  Mrs Elizabeth Nzagi issues a Renewed License to the East Africa Radio at the Mawasiliano Towers in Dar Es Salaam on 14 August 2015. Receiving the license is the Head of the East Africa  Radio, Mr Nasser Kingu. Looking (centre) Ag. Director Broadcasting Affairs Mr Frederick Ntobi and second left, TCRA Manager for Eastern Zone Eng. Deo Moyo. The Authority renewed licenses of Six Radio Stations and One TV station. Others issued with renewed license were Radio One, Times FM Radio, Upendo FM Radio, Wapo FM Radio, Capital FM Radio  and Tumaini Television.  Photo by  Courtesy of TCRA
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images