Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

SIMU TV: HABARI ZA USIKU HUU


TANZANIA KUWA MWENYEJI WA WARSHA YA MADINI- NCHI ZA MAZIWA MAKUU

PATASHIKA YA LIGI KUU YA UINGEREZA KUENDELEA WIKI HII, USIKAE MBALI NA DSTV YAKO

HOJA YA HAJA: Je kuna nia ya dhati ya kuwaondolea watanzania umaskini?

$
0
0

 Tunapoelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi wagombea urais watarajiwa wanajaribu kuwaeleza watu  mambo yenye mvuto kwao na kuonyesha  kuwa wataifanya Tanzania  iwe nchi ya maziwa na asali. Nafahamu watatupa ahadi nyingi zaidi wakati wa kampeni.
Lakini kinachonisikitisha  zaidi ni pale  wanasiasa  wanaposema  wanakerwa na umaskini wa watanzania na nia yao  ni kuondoa umaskini. 
Lakini hapo hapo anahamasisha maelfu ya  vijana na watu wengine kuacha kazi zao   kumsindikiza kwenda kuchukua fomu ya uteuzi na kuwafanya waache shughuli zao kwa siku nzima, wamesimamisha shughuli za kiuchumi mjini kwa zaidi ya masaa matano nk.  
Je kwa kufanya hivyo tumeongeza  umaskini au tumepunguza umaskini wa mtanzania?. kama kweli tunajali watanzania na tunataka kuwaondolea umaskini kwanini usiende kuchukua  fomu na viongozi na washabiki wako wachache   halafu uongee na watanzania kupitia vyombo vya habari. 
Hawa waheshimiwa wanajua ni kiasi gani cha pesa kimepotea kwa wao kufunga barabara na shughuli zote mjini kwa zaidi ya masaa matano. je wanajua hawa maelfu ya vijana na watu wengine waliokusanywa na kuandamana kwa siku nzima  kumsidikiza mgombea wamepoteza kipato kiasi gani?

 Naomba watanzania   kipindi hiki cha uchaguzi   tusikitumie  kuongeza umaskini na kutegemea  viongozi wetu watuondolee umaskini wakiingia  madarakani. Umaskini inabidi tujiondolee wenyewe. 
Kuna tafiti zilionyesha kiasi cha fedha kinachopotea kutokana na  foleni za magari  jijjini Dar es Salaam, watu kukaa muda mrefu barabarani na kuchelewa makazini. Ningefurahi kama wasomi wetu wangefanya utafiti na kubainisha  kiasi gani cha fedha kinachopotea kwa kusimamisha  shughuli za uchumi kwa misafara  isiyo na muhimu kama kusindikiza wanasiasa kwenda kuchukua  fomu za uchaguzi.


R. Kahwa  - Mtanzania 

Tanzania by Milca Kakete

MAKALA YA SHERIA: JE TRAFIKI ANARUHUSIWA KUKUNYANG”ANYA LESENI?

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.
Kumekuwepo  na  sintofahamu   nyingi  kwa  madereva  na  watumiaji  wengine  wa  vyombo  vya  usafiri. Sintofahamu  hii  imekuwa  ikiletwa  na   baadhi  ya  mambo  ambayo  hayaeleweki  sawasawa  katika  suala  zima  la  usalama  barabarani   na  sheria  zake. Wadau   wa  barabarani wamekuwa  wakilaumiana,  madereva  wakiwalaumu  askari  wa  barabarani  kwa  uonevu  huku  askari  wa  barabarani  wakiwalaumu  madereva  kwa  ukorofi   na  ukosefu  wa  utii  wa sheria  bila  shuruti. Lakini  swali  hapa  ni  kwanini  iwepo  mivutano  na  hali  kuna  sheria. Sheria  inasemaje  kwa  kila  jambo  ambalo  wadau  hawa  wanatofautiana?. 

1.UBABE  WA  ASKARI  WA  BARABARANI.

Baadhi  ya  askari  wa  barabarani  wamekuwa  ni  wababe  sana. Wanahoji  mambo  ambayo   si  wajibu  wao  kuyahoji  na  hawataki  dereva  aulize  lolote  kuhusu  kuhoji  kwao  mambo  hayo. Wanataka  kila  wanachosema  dereva atii  hata  kama anaona  hakipo  kwa  mujibu  wa  sheria. Matokeo  yake  mtu  anaandikiwa  faini  za  makosa  mengi  ilimradi  tu  kumkomoa. Askari wengine  wamefikia  hatua  ya  kuwapiga madereva  vibao.  Binafsi  nimewahi  kushuhudia  askari  wa  usalama  barabarani  akimnasa  kibao  dereva wa  daladala. Ni  ubabe  uliovuka  mipaka  na  hakika  ni  uvunjaji  wa  sheria  uliopitiliza .

2.  JE  TRAFIKI  ANARUHUSIWA  KUMNYANGANYA  DEREVA  LESENI.

Masuala ya usalama  barabarani   yanaainishwa  ndani  ya  Sheria  ya  Usalama barabarani ( The  Road  Traffic Act) ambayo  ndio  hueleza  wajibu   na  haki  za  kila  mdau  na  mtumiaji  wa  barabara. Katika  sheria  hii  hakuna  pahala pameandikwa  kuwa  trafiki  achukue  leseni  ya  dereva  kwa  kuwa  dereva  ametenda  kosa   fulani. Maana  fupi  ya hili  ni  kuwa  trafiki  haruhusiwi  kuchukua  leseni  ya  dereva.  Anachoweza kufanya  trafiki  ni  kile  kilichoainishwa  na  kifungu  cha  17  cha  sheria hiyo  ya  usalama  barabarani. Kifungu  hicho  kinampa  trafiki  mamlaka  ya  kukagua  na kujiridhisha   na  uhalali  wa  leseni  ya  dereva. Hakisemi  aichukue. Kinasema  aikague  basi.  Kukagua  na  kuchukua  ni  mambo  mawili  tofauti.  

Kama  hivyo  ndivyo  basi  yafaa  kueleweka  kuwa   kitendo  cha  askari  kumsimamisha  dereva  na  kisha  kumpokonya  leseni  yake  ni  kinyume  cha  sheria.  Dereva  anao  wajibu  wa  kulinda   haki  hii  kwa  kulikataa  hili na kuhakikisha trafiki  hamfanyii  kitendo  hiki.  Kumbuka  kuwa  wakati  askari  wa barabarani  akitekeleza  wajibu  wake  wa kisheria  na  wewe  dereva  unayo  haki  ya  kutetea  haki  zako  za  kisheria. Hakuna  aliye  juu  ya  mwingine kwani  anatekeleza  wajibu  nawe  unalinda  haki.

Simple Hope Foundation wamtembelea Balozi Mulamula Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Bi. Pamela A. Schwalbach, mmoja wa waanzilishi wa Shirika la (Simple Hope East Africa) linalo fanya kazi za kijamii na  wakina mama wa Kabila la Hadzabe, Mkoani Manyara.  
Bi. Pamela (katikati) na Bi Karen J. Puhl (Kushoto)  wakiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu Mambo ya Nje ambapo alipata wasaa wa kupokea taarifa ya kazi za shirika hilo lisilo la kiserikali la Marekani, Jimbo la Wisconsin. 
Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Pamela A. Schwalbach (wa pili kushoto), Bi. Karen J. Puhl (wa pili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje Bi. Felista Rugambwa.Picha na Reginald Philip

MODEWJI BLOG YARUDI HEWANI BAADA YA KWIKWI YA MASAA 4*

$
0
0
modewjiblog logo
Baada ya kwikwi ya saa takribani 48 wataalamu wa Modewji blog wanakurejeshea hewani Blog yako pendwa.
Watundu wanaovuruga mambo mtandaoni (hackers) walijaribu kuimiliki blog hii kwa kufanya majaribio zaidi ya mara 300 yaliyosababisha mifumo ya kiusalama, kufanyakazi ya ziada kuihami Modewjiblog.
Hata hivyo wataalamu wetu wameziba mianya iliyokuwa imesababisha hali hiyo na sasa tupo pamoja nanyi.
Tunashukuru kwa uvumilivu wenu, tuko pamoja na endelea kuperuzi nasi.
Kwa mawasiliano zaidi tutumie email: info@modewjiblog.com
Imetolewa na Operation Manager, Zainul Mzige.

VIJANA WALIOTIMIZA MIAKA 18 WAASWA KUPIGA KURA ILI KUCHAGUA VIONGOZI WANAO WATAKA.

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya jamii.
VIJANA waliotimiza miaka 18 kwa mwaka huu waaswa kupiga kura ili kumchagua kiongozi wanaemtaka na watambue mchango wao katika jamii kwa kupiga kura  kwaajili ya maendeleo ya taifa letu.

Nae Mwenyekiti wa  asasi isiyo ya kiserikaliTanzania People  with Disabilities Organization (TAPWAO), Michael  Mwanzalima ameomba tume ya uchaguzi  kutoa vipaumbele kwa  walemavu wa viungo mbalimbali siku ya kupiga kura ili isiwe kikwazo kwao katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili waweze kuwachagua viongozi wanao wafaa.

 Hayo yamesemwa na  vijana mbalimbali waliohudhuria katika mdahalo wa “ELEKEA UCHAGUZI 2015 NA VIJANA ”ulioandaliwa na  kampuni ya Tanzania Bora Initiative (TBI) ikiwa na nia ya kuadhimisha siku ya vijana dunia katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika Dar es Salaam leo.

Pia katika mdahalo uliohusisha vijana mbalimbali hapa nchini ikiwa na wacheza muvi,waimba mziki wa kizazi kipya (Bongo freva) na vijana kutoka makampuni mbalimbali wakijadiliana kuhusiana na UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25 MWAKA HUU, vijana watashiriki vipi ili kuchagua kiongozi wanae mtaka.

Pia katika mdahalo huo uliambatana na  uzinduzi rasmi wa kampeni ya njia ya mtandao ya habari ujulikanao kama  UCHAGUZI 2015# KURA YETU.
Mwenyekiti wa  asasi isiyo ya kiserikali hapa nchini ya Tanzania People  with Disabilities Organization (TAPWAO), Michael  Mwanzalima akizungumza katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afrika jijini Darr es salaam jana, yeye akiwakilisha walemavu akiomba rai kwa  Tume ya uchaguzi kuwawekea mazingira rafiki katikauchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 waweze kupiga kura bila  kikwazo chochote.
 wageni waalikwa wakiwa katika mdahalouliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.
Manzilishi wa kampuni ya Ekihya na mwenyekiti wa mdaholo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam.akizungumza na vijana waliohudhulia mdahalo huo.
 Hamfrey Pole pole akizungumza katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya New Afika jijini Dar es Salaam. akiwaasa vijana wajitokeze katika upigaji kura wa mwaka huu utakaofanyika Oktoba 25 ili kuwachagua viongozi bora na sio bora viongozi.

Maria Salungi akichangia maada kuhusiana na kijana anajitambuaje katika kuhamasika kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu ili waweze kumchagua kiongozi wanae mtaka, kwa kuwa baadhi ya vijana ni mara yao ya kwanza upiga kura.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 

JK Aongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu mjini Dodoma leo

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakipiga makofi pamoja na wajumbe wengine muda mfupi baada ya kuingia katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM leo jioni.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt.John Pombe Magufuli wakiteta muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo. 
Picha na Freddy Maro.

SHIWATA yakabidhi nyumba 16 Mkuranga

$
0
0
 Wasanii wakipata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (hayupo pichani) utaratibu wa kutunza nyumba walizogaiwa kwenye kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi .
 Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akitoa ufafanuzi wa makazi mapya ya kijiji cha M\Wasanii Mwanzega, Mkuranga baada ya kugawa nyumba 16 kwa wasanii hao.
Picha ya pamoja.
 

Na Peter Mwenda

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imegawa nyumba nyingine 16 kwa wanachama wake waliokamilisha ujenzi ambako mpaka sasa wanachama 120 wamekabidhiwa nyumba zao katika kijiji cha Wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.

Katika hafla ya kukabidhi nyumba hizo jana, Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba hizo ni endelevu mpaka hapo ekari 300 zilizotengwa kwa ujenzi zitajengwa nyumba kwa mpango wa kuchangiana.

Taalib alisema aina za nyumba zinazojengwa kwa sasa ni za matofali ya saruji ya chuma kimoja kwa sh. 750,000, nyumba za vyumba viwili na sebule kwa sh. 3.8 na nyumba kubwa ya sh. mil. 6.4.

Alisema kipa wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa, Hamisi Kinye anatarajia kukabidhiwa nyumba yake Desemba mwaka huu sambamba na wasanii wengine Lilian Ndelwa, Edson Mwela, Happyness Magere, Asheri Kazeba, Jaqueline Joseph na Suzan Moshi ambao wamebadilisha nyumba walizokuwa wakabidhiwe za udongo na sasa watachukua nyumba zilizojengwa kwa saruji.

Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeandaa mpango mkakati wa kuingiza umeme na maji katika kijiji hicho kabla ya Desemba na tayari kikundi cha wasanii kimepiga kambi ya kujiandaa kurekodi tamthilia ya maisha ya Bongo katika kijiji hicho.

Mmoja wa wasanii aliyekabidhiwa nyumba ya sh. mil. 6.4, Mwajuma Kisengo alisema ametimiza ndoto yake ya kushirikiana na wasanii wenzake kuishi katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.

WATHAMINI MADINI VITO WAASWA KUWA WABUNIFU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo (Kulia), akimwongoza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Ngosi Mwihava kuingia Ukumbi wa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika Agosti 12 na 13 katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT) Archard Kalugendo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Ngosi Mwihava, Kaimu Kamishna wa Madini nchini Mhandisi Ally Samaje na Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Mrimia Mchomvu, wakijadili jambo muda mfupi kabla ya kuanza kwa Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini, iliyofanyika Agosti 12 na 13, 2015 katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Meza Kuu – wakiwa katika Semina ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini. Semina ilifanyika Agosti 12 na 13, 2015 katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Mhandisi Ngosi Mwihava, Kaimu Kamishna wa Madini Ally Samaje na Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Mrimia Mchomvu.

WATHAMINI MADINI VITO WAASWA KUWA WABUNIFU

Na Veronica Simba - Mwanza


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava amewataka Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini kuendelea kuwa wabunifu ili kutafuta majibu na suluhisho kwa changamoto zinazoikabili tasnia ya vito nchini.


Aliyasema hayo alipokuwa akifungua Semina ya Nne ya Wathamini Madini ya Vito na Almasi nchini iliyofanyika Agosti 12 na 13, mwaka huu katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest, jijini Mwanza.


Mwihava alisema kuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo zitaweza kuondolewa endapo watumishi katika kada hiyo watajituma kufanya kazi kwa uaminifu, weledi na ubunifu wa hali juu. “Napenda kuwakumbusha kwamba Watanzania wanataka kuona faida stahiki kutoka katika sekta ya madini hasa itokanayo na almasi na vito vingine; kadhalika hata mimi nataka kuona matokeo yanayopimika na malengo hayo kutimia na hata kuzidi viwango wanavyotarajia,” alisema Kaimu Katibu Mkuu.

Akifafanua zaidi, Mwihava aliongeza kuwa angependa kuona Soko la uhakika kwa Madini yanayopatikana nchini hususan Almasi na Vito ili Watanzania wanaojishughulisha na biashara hiyo wajue utaratibu wote.


Alisema kuwa angependa kuona wataalam hao wakitumia ipasavyo mitandao iliyopo katika kuwavutia wafanyabiashara na wakataji wa vito kuja nchini kununua na kuwekeza katika tasnia husika.


Aidha, Mwihava aliongeza kuwa angependa kuona wataalamu hao wa Madini ya vito na almasi wakitumia ujuzi wao katika kuwasaidia wadau wa tasnia husika kupata tafsiri sahihi na kuzingatia Sheria ya Madini ya mwaka 2010 pamoja na Kanuni zake.


“Nawaagiza mzingatie maadili na miongozo ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yenu; msome na kuzingatia Sera ya Madini ya mwaka 2009, Sheria ya Madini ya mwaka 2010 pamoja na kanuni zake na Mkataba wa Huduma kwa Mteja,” alisisitiza Mwihava.


Vilevile, Kaimu Katibu Mkuu alitahadharisha kuwa yeyote atakayefanya kazi kinyume na matarajio, kwa kupokea rushwa, wizi au kufanya jambo jingine lolote kinyume na maadili ya utumishi wa Umma na kusababisha kuathiri juhudi zinazofanywa na Wizara, hatavumiliwa.


Akizungumzia mchango wa Serikali katika kuinua tasnia ya Madini ya vito na almasi, Mwihava alisema Wizara imeahidi kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya madini ili kuongeza uwezo kwa Serikali kujitegemea katika bajeti yake.


“Endapo azma hii itafanikiwa, uchumi wetu kama Taifa utakua, fursa za ajira zitaongezeka na kipato cha Watumishi kitaboreshwa. Aidha, wananchi watapata huduma stahiki, muingiliano wa biashara utakua na hivyo kuchochea ufikiaji wa malengo ya Dira ya Taifa, yaani kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapo 2025.”


Alisisitiza kuwa suala muhimu zaidi ni kuhakikisha Watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi wa watumishi wa Serikali hususan walioko katika kada husika na kuwaonyesha Watanzania kwamba wana uwezo wa kusimamia sekta husika kwa niaba yao na pia wananchi waone kwa maneno na vitendo kwamba kazi hiyo inafanyika vizuri.


Mwihava alihitimisha kwa kuwataka washiriki wa semina hiyo kuitumia kama fursa muhimu ya kujitathmini, kubadilishana uzoefu, kupeana mbinu za utendaji bora, kutafuta majibu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili na kukumbushana maadili mema ya kazi na utumishi wa umma.


Alitoa changamoto kuwa anatarajia baada ya semina husika, wataalam hao wa sekta ya Madini vito na almasi watakuja na mkakati wa kuboresha ukusanyaji mapato ya Serikali kutoka katika tasnia ya almasi na vito, ili kuisadia Wizara kufikia malengo ya makusanyo na kuboresha utendaji wao. 




Vijana nchini watakiwa kuzingatia upatikanaji wa taarifa sahihi kuelekea uchaguzi mkuu

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumaza na vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem (kulia) akisalimiana na mmoja wa vijana waliokua katika banda la familia wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani katikati) katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki maadhimisho ya siku kimataifa ya vijana duniani jana katika Viwanja ya Mnazi Mmoja.

 Baadhi ya vijana wakiandamana kuelekea katika Viwanja vya Mnazi Mnoja kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, kushoto mwenye tisheti ya bluu ni Mkurugenzi Msaidizi Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerosa Mtenga. Siku hiyo imeadhimishwa jana katika viwanja hivyo.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo


Na: Genofeva Matemu – Maelezo

Tarehe: 13/08/2015.


Vijana nchini wametakiwa kuwajibika kutafuta taarifa sahihi kutoka katika vyanzo sahihi na kuzingatia utoaji wa taarifa zilizo sahihi haswa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu.


Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya  vijana duniani jana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.Prof. Gabriel aliwataka vijana kuachana na taarifa za uchochezi zinazosambazwa katika mitandao mbalimbali zisizokua na ukweli ndani yake na kuzishikilia kwa kuhamasisha vijana wenzao kuamini mambo yasiyokua sahihi.

“Vijana wana haki ya kupata taarifa sahihi, haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi mwenye maslahi katika nchi, na kuheshimu sheria zilizopo kwa kuwa na maadili mema yatakayowawezesha kujengewa heshima na kuthaminiwa katika jamii” alisema prof. Gabriel.


Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mwakilishi Mkazi kutoka shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanema aliitaka jamii kuhakikisha kuwa vijana wanashirikishwa kutoa maamuzi katika masuala ya kifamilia,  kijamii na kitaifa.


Bibi. Kanema amesema kuwa vijana ni taifa la kesho, wanapaswa kushikilia ndoto zao na kujiongeza hivyo jamii iwakumbatie na kuwashirikisha katika maamuzi kuweza kujenga taifa lililokomaa na lenye weledi wa hali ya juu.


Aidha kijana Hesein Melele kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) amewataka vijana nchini kuondokana na dhana ya kulalamikia Serikali bali wajitokeze kushiriki katika masuala mbalimbali na kuachana na tabia ya kusubiri kushirikishwa. 

Bw. Melele aliwahasa vijana kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki katika uchaguzi kwa amani na utulivu ili kuweza kuchagua kiongozi mwenye maslahi katika jamii atakayeongoza nchi kwa amani.


Naye mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Jangwani Bi.Tatu Ahmed amewataka vijana wenzake nchini kuwa na maadili mema katika jamii na kutumia fursa mbalimbali walizonazo kujikwamua kiuchumi.

NHIF YATOA “DARASA” KWA BLOGGERS WA TANZANIA KUHUSU UCHAGIAJI WA BIMA YA AFYA CHINI YA MPANGO WA “KIKOA”

$
0
0
 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti
 MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akifafanua jambo wakati alipokuwa akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Bloggers wakimsikiliza  Mkurugenzi wa huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, alipokuwa akiwasisilisha mada iliyohusu mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
  MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti,akiwasilisha mada juu ya mpango wa uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 
 Baadhi ya Bloggers wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha hiyo
 Wadau wakifuatilia jambo
 Bloggers wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha hiyo 
  Baadhi ya Bloggers wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha hiyo
Blogger Mzee Kitime akichangia jambo katika semina hiyo ya iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NHIF na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN).Warsha hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI YAAFRICAN LIFE ASSURENCE YABADILISHA JINARSNI KUWA SANLAM LIFE

$
0
0
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda  Akiwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius Magabe Tayari kwa Uzinduzi wa  Kampuni ya Sanlan. 
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof Mkenda wa Pili Kushoto Akiwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam life Insurance Ndg.Julius Magabe, wa pili kulia Pamoja na 
Mtendaji Mkuu wa umoja wa makampuni ya Sanlam.Ndugu.Ian Kirk..Israel Kamuzora, Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) Mara baada Uzinduzi wa wa Kampuni ya Sanlan wakionyesha Mshikamano.Kampuni inayoongoza katika bima za maisha nchini, African life .

Assurance(Aflife) jana usiku wa Agosti 12, 2015 ilitangaza rasmi Kubadilisha jina lake la kibiashara na kuwa Sanlam Life Insurance ambayo ni Kampuni ya kimataifa ya huduma za kifedha yenye makao yake makuu Afrika ya Kusini, ambayo imekuwa na umiliki mkubwa zaidi wa hisa za kampuni hiyo tangu mwaka 2005.Badiliko hili ni kwa mujibu wa umoja wa makampuni ya Sanlam yenye lengo la kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini TanzanianaAfrika Mashariki kwa ujumla.Kwa upande wa wateja, wanahisa, mawakala na wafanyakazi, badiliko hili kuwa Sanlam Life Insurance litaimarisha faida za ushirika zilizojengwa kwa miaka 10 sasa.

Kwa mujibu wa Bw Magabe, Sanlam Group ni kampuni ya kuheshimiwa Afrika yenye matawi katika nchi 12. "Kwenye suala la wateja kuridhika na uaminifu, Sanlam imekuwa ikiipa sekta ya bima ya maisha kipaumbele kwa wakazi wa Afrika Kusini. 

Vile vile, kwa Tanzania Aflife daima imekuwa ikisifika kwa kuwa na huduma bora kwa wateja na kupewa alama za AA-na kampuni ya viwango ulimwenguni ya Global Credit Rating (GCR) kwa nguvu ya kifedha na ulipaji bora wa madai.”mabadiliko kutoka Aflife kuwa Sanlam Life Insurance yatachangia utendaji wa kibiashara kwa kampuni. "Kuna mipango ya kupanua soko la rejareja na kutoa huduma za ziada zilizo endelevu katika ukuzaji wa biashara, wateja wa Sanlam Life Insurance watapata bidhaa mpya zilizoboreshwa zaidi.”

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KONGAMANO LA VIJANA MKOANI MBEYA WAKATI WA KUAZIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI.

$
0
0

KATIKA maadhimisho ya siku ya Vijana duniani yaliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Vijana wamekumbushwa kuhusiana na afya ya uzazi kwa vijana pamoja na maendeleo yao.

Aidha katika kongamano hilo ambalo liliandaliwa na mashirika binafsi ya Restless Developmentna Young & alive initiative ambalo lilihudhuriwa na Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu na shule za Sekondari za Jiji la Mbeya.
Akizungumza katika kongamano hilo mwakilishi wa Shirika la Young & Alive Initiative, William Otuku, alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha vijana kuhusiana na maswala yanayohusu afya ya uzazi kwa vijana ili waweze kuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za maendeleo wakiwa salama.

Aliongeza kuwa kauli mbiu ya siku hiyo ni kuhakikisha vijana wanashirikishwa na kuhusishwa  katika kupanga maamuzi mbali mbali hivyo hayo yote yanaweza kutimia endapo wataelimishwa kuhusiana na afya ya Uzazi ili waliomashuleni waendelee kufanya vizuri na kusaidia kutoa elimu kwa ambao hawako mashuleni.

“Vijana tunawapa elimuya afya  ya uzazi ili waweze kuwa imara katika kushiriki shughuli za maendeleo za kijamii pamoja na kuwaepusha na vitendo ambavyo vitaweza kuwaondolea katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuepukika” alisema Otuku.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa  Shirika la Restless Development,Fadhili Mtanga, alisema lengo la kongamano hilo ni kujadiliana kwa pamoja kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabili vijana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya kuweza kutatua na kukabiliana na vikwazo vya maendeleo kwa vijana.

Alisema lengo la kuwahusisha wanafunzi ni kutokana na kuwa na kundi kubwa la vijana wanaoanzia umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao ni kundi kubwa katika jamii hivyo ni rahisi kwao kupeleka mabadiliko kwa wananchi wengine ambao hawakubahatika kuhudhuria kongamano hilo.

“Sisi tumewalenga zaidi vijana ambao ni wanafunzi kwa sababu tunaamini wanakubalika kaika jamii na nirahisi kwao kutoa elimu ambayo iaweza kuwafikia wahusika kwa haraka zaidi” alisema Mtanga.

Naye Mgeni rasmi katika Kongamano hilo, Afisa Vijana wa Jiji la Mbeya, Ona Temu kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Mbeya, alipongeza kwa wadau kujitokeza na kuandaa kongamano hilo kwa kutambua mchango wa vijana katika jamii.

Alisema vijana wanapaswa kuutumia vizuri umri kati ya miaka 18 hadi 40 kwa kujenga na kutafuta uchumi ili kipindi cha miaka 40 hadi 60 anabaki kuwa msimamizi wa shughuli ambazo alizifanyia kazi kipindi cha ujana wake.

Aliongeza kuwa kipindi cha umri wa zaidi ya miaka 60 ni muda wa kufaidi matunda na kupumzika kwani utakuwa tayari umeshafanya kazi ya kutafuta na kuzisimamia vizuri kwa malengo makubwa.

 Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Vijana Halmashauri jiji la Mbeya  Onah Temu  akitoa hotuba katika siku ya Vijana Duniani ambayo kwa Mkoa wa Mbeya ilifanyikia Ukumbi wa Chuo kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya.
 Maandamano kuelekea katika Ukumbi ambapo vijana wanakutana kwa ajili ya Sherehe yao
 Mratibu wa Mradi wa Restless Fadhiri Mtanga akitoa mada kuhusu Maendeleo ya Vijana .

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

LOWASSA KUJITAMBULISHA KESHO ARUSHA

$
0
0

Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi makubwa ikiwemo magari,pikipiki,katika uwanja wa ndege wa  kia hadi viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho

Akizungumza mapema jana na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya maandalizi hayo Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukiohilo ni la kihistoria 
Alisema kuwa  lengo la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji ,kwa kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha sambamba na kupata udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga kura
Pia alisema kuwa zoezi la udhamini umeshaanza Arusha na  uongozi wa Tume umaelekeza mgombea kupata wadhamini 300 na  jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini 300
Aidha aliwataka ,wakazi wa jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa wingi katika tukiohilo la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama hicho watahudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti wenza wa ukawa kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu katibu mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi
“Kwakushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi na Usalama vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo”Alisema Golugwa
Hata hivyo baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hilo
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu waTimu Lowassa for president  Ndama Jeuri alisema wamejiandaa vizuri kumpokea  na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa katika harakati zake za Urais
Katika msafara huo zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi katika uwanja wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Lowassa.
SAM_5047
Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais  Edward Lowassa kupitia  CHADEMA  yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15)(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_5049
Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari akizungumza na vyombo vya habari.

Airtel Fursa yaandaa semina ya Daraja la mafanikio kwa Vijana Mjini Mtwara.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
 Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu akitoa mada kuhusu fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua vijana kiuchumi, wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.
 Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Salum Ally (kulia), akijadiliana jambo na vijana walionufaika na fursa za Airtel (kutoka kushoto), Iddy Salum Chilumba, Godfrey Frank Manjavila na Prisca George Chilumba baada ya kufungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi VETA mjini Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kulia) na Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu.


Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kutumia fursa za uwepo wa nishati ya mafuta na gesi katika kukuza biashara zao na uchumi wa mkoa huo.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya ujasiriamali mkoani humo, baadhi ya vijana hao wamesema kuwa fursa zilzizopo mkoani humo ni lazima ziwanufaishe vijana ili waendane na ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Kampuni ya Airtel Tanzania, kupitia mradi wake wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha” imewapatia mafunzo na kuwawezesha mitaji baadhi ya vijana wa manispaa ya mtwara kwa lengo la kuwawezesha kumudu uendeshaji  biashara zao na kukuza mitaji yao.

Idd Abdallah ni mjasiriamali aliyenufaika na mafunzo hayo ambaye anasema kuwa kwa sasa amepata muongozo mzuri utakaokuza biashara zake na kuzifanya kwa weledi mkubwa zaidi.“Hii ni fursa ya kipekee kwangu kama kijana na ninaishukuru sana Airtel kwa mafunzo yenye manufaa kwangu na vijana wenzangu wa hapa mtwara” Alisema Abdallah.

Nae mkuu wa wilaya ya Mtwara bi.Fatuma Ally, alisema “mafunzo haya yatapanua wigo wa ufahamu kwa vijana hawa ambapo aliwataka kujituma kwani fursa zipo nyingi mkoani humo.
“Mtwara kuna maeneo mengi sana yenye fursa kwa vijana kujiendeleza hivyo nawataka vijana kutumia fursa na mafunzo haya kuhakikisha wanajiendeleza kiuchumi” alisema mkuu huyo wa wilaya.

Hawa Bayumi ni Meneja Maendeleo ya Jamii wa Airtel, alisema hiyo ni fursa inatolewa na Airtel kwa lengo la kusaidia vijana kupata fursa ya kujiajiri na kupata mitaji kupitia mpango huo.
“Kwetu sisi Airtel tunaona ni fahari kuwawezesha wajasiriamali kwa mafunzo na mitaji ili waweze kuendeleza biashara zao na kukuza mitaji pia. Alisema Bayumi.

Ugunduzi wa gesi na mafuta mkoani hapa, vijana wanapaswa kujituma kwa kuongeza elimu na mitaji ili waweze kuwa sehemu ya wanufaika na kuondoka na hali ya kuwa watazamani wa tunu hiyo.

BENKI YA EXIM TANZANIA YAFUNGUA TAWI JIPYA ZANZIBAR

$
0
0
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania Bw Selemani Ponda (wa pili kulia) akizundua tawi jipya la benki hiyo lililopo eneo la Mwanakwerekwe, Zanzibar wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika Zanzibar hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wageni waalikwa.

TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI KUFANYIKA SEPTEMBA 21-27, 2015 WILAYANI BAGAMOYO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, John Mponda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika kwa mara ya 34 kuanzia tarehe 21-27 Septemba katika ukumbi na viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe Tanzania. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho ya tamasha hilo, Christa Komba na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na Majukwaa, Frank Sika.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maonyesho ya tamasha hilo, Christa Komba (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi na Majukwaa, Frank Sika (kushoto), akizungumzia maonyesho yanavyofanyika katika majukwaa.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ikichukuliwa na wanahabari.


TAMASHA la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Lengo kuu la Tamasha kwa wakati huo ilikuwa ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cha sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, baada ya Tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa chuo uliamua tamasha hilo lifanyike kila mwaka kwa kushirikisha Vikundi mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana Uzoefu  na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya Tanzania.

Tamasha la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo mwaka huu litafanyika kwa mara ya 34 kuanzia tarehe 21-27 Septemba katika kumbi na viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambao ndio wenyeji na waandaaji wa tamasha hilo kongwe Tanzania.

Tamasha la mwaka huu linabeba Kauli mbiu isemayo ‘SANAA NA UTAMADUNI KATIKA UCHAGUZI HURU NA WA AMANI’  Aidha kutakuwa na mada ndogondogo zitakazotolewa kupitia kongamano na warsha zitakazohusu  Haki za binadamu, Rushwa na kupinga Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)

Tamasha la mwaka huu litahusisha Ngoma za Asili, Maigizo, Sarakasi, Mazingaombwe, Muziki wa kisasa na asili, Sanaa za Ufundi  na bidhaa mbalimbali.

Hadi sasa jumla ya vikundi 48 kutoka ndani na nje ya Tanzania vimethibitisha kushiriki,ambapo vikundi 43 ni kutoka ndani ya Tanzania na vikundi 5 kutoka nchi za Kenya, Namibia, Afrika Kusini, Korea na Congo.
Hadi kufikia sasa hakuna mdhamini yoyote aliyejitokeza kudhamini Tamasha hili na hii imepelekea vikundi kujigharamia na TaSUBa kugharamia Uendeshaji,hivyo Taasisi inatoa wito kwa wadau mbalimbali wa sanaa,Makampuni,Taasisi za serikali na zisizo za serikali kujitokeza kudhamini tamasha hili muhimu kwa mustakabali wa sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

Kwa yeyote anayehitaji kuchangia tamasha hili anaombwa awasiliane na Kamati ya maandalizi kwa mawasiliano hapo chini. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images