Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

MUDA WA KUJISAJILI KWENDA HIJJA WASOGEZWA MBELE TOKA JUNI 15 HADI AGOSTI 25, 2015

$
0
0
 Naibu Mwenyekiti Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania (BIITHA), Yusuf Musun (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kusogezwa mbele muda wa kujisajili kwenda Hijja kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Habari wa Biitha, Hamisi Tembo na Mratibu wa Biitha, Abdallah Khalid.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MAHUJAJI nchini wametakiwa kujitokeza kujisajili katika taasisi zilizosajiliwa kisheria ili kujiandaa kwenda katika ibada ya hija itakayofanyika nchini Saud Arabia Septemba 16 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Naibu Mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania Bara na Zanzibar,  Yusuf Musun  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusogeza muda huo kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu,

Alisema kusogeza mbele kwa muda wa usajili ni kutoa fursa kwa wanaotarajia kwenda kuhiji ili waendelee kujitokeza kwa wingi kujisajili katika taasisi zilizo rasmi.

Alisema  wananchi  wenye nia ya kwenda hijja lakini hawana fedha za kulipa kwa mkupuo wanaweza kwenda kulipia kidogo kidogo kwenye ofisi husika.

Musun alisema lengo la kutoa mwito huo ni kuhimiza watu wanaolipa fedha zao binafsi na wale wanaolipiwa na mashirika mbalimbali kujisajili kwa wakati ili usajili uweze kumalizika katika muda uliopangwa.

"Waislamu wengi hawatoe hela zao kutoka mfukoni wengi wao wanaolipiwa na mashirika mbalimbali hivyo tunawahimiza wajisajili kwa wakati kwa ajili ya safari hiyo ya hijja.












MASHIRIKA MATANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA(FOS) YAUNGANA KWA PAMOJA KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

$
0
0
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo.

Umoja wa Mashirika Matano yanaounda ushirika wa Fahamu,Ongea Sikilizwa(FOS) ambayo ni Oxfam,BBC Media Auction, Legal and Human Rights Centre, Restless Development, and VSO leo wamekutana na waandishi wa Habari kwa ajili ya kuzungumzia mambo Mbalimbali yanayohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015 na kueleza malengo ya muungano huo.

Akizungumza Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Bi. Jane Foster ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo na waandishi wa Habari alisema kuwa Lengo kubwa la Umoja huo ni kusisitiza na kuwaelimisha wananchi wote kwa ujumlan juu ya Uchaguzi mkuu 2015 ambapo Oxfam wao jukumu lao kubwa ni kuwahimiza wanawake na wasichana wadogo  kuelekea uchaguzi Mkuu kama wapiga kura, na ili kuyafikia makundi yote haya waliandaa na wanaendesha Midaharo mbalimbali, kuunda makundi ya wanawake na zaidi wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kuwapa taarifa juu ya uchaguzi.

BBC kwa upande wao wanajukumu la kusimamia mashirika mbalimbali ya utangazaji Nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kanuni za uandishi bora wa Habari za uchaguzi Mkuu 2015 

Nao kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao walikuwa na jukumu la Kusimamia zoezi zima la uasdikishaji wa wapiga Kura ambapo walikuwa na watu 165 nchi nzima wakiangalia na kuangalia makosa yaliyojiokeza na kupeleka Maoni yao sehemu husika, na pia katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 wameandaa kitengo maalumu cha Teknolojia ambacho kitasimamia uchaguzi wote.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

MAZISHI YA KAMISHINA MSAIDIZI WA MAGEREZA(SACP), ANNETHY LAURENT

$
0
0
 Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Magereza (SACP) Annethy Laurent.
 Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili katika Kanisa Katoliki Parokiani Segerea. Walio mbele ni Pamela  (mtoto wa dada yake na Marehemu) na aliyebeba picha ni mtoto wa Pamela ( Mjukuu wa Marehemu). Walioshika jeneza kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dk.Kato Rugainunura, kulia ni Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Rajab Nyange
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati wa ibada ya kumuombea Marehemu.
 Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya akitoka salaam za Jeshi la Magereza kwa wafiwa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa  Magereza John C. Minja.

Picha zote na Mkaguzi wa Magereza Moses Sebastian
Makao Makuu ya Magereza.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

SINA ACCOUNT YEYOTE YA MITANDAO YA KIJAMII - DAVIS MOSHA

$
0
0
Napenda kuwajulisha wananchi wote kumetokea tabia ambayo sio nzuri kwa jamii watu kutengeneza maneno na kuanzisha post kwenye mitandao ya jamii isiyokuwa tija ili kumchafua mtu. 

Naomba ieleweke kuwa mimi binafsi sina account yoyote ya mtandao wowote wa jamii na wala sina mpango wakuwa nayo maana ninajua madhara yake watu wanatumia visivyo kupotosha jamii ukweli utabaki kuwa ukweli pamoja kwa maendeleo - 

Davis Moshi

BREAKING NEWZZZZZZ.....: PROF. LIPUMBA ABWAGA MANYANGA UWENYEKITI WA CUF

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.

Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.

TAARIFA KAMILI 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania  katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba (UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akilini.
Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia kiasi hata kabambikiziwa  kesi ya kufanya maandamano bila kibali.

Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu  pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani  pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu  ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

RAIS KIKWETE AAGA RASMI IDARA YA MAHAKAMA, YAMPA TUZO KWA MAKUBWA ALIYOFANYA KATIKA MIAKA 10

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutokana na mambo makubwa liyoifanyia idara hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi. PICHA ZOTE NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha  tuzo maalumu aliyoipokea kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.

  wadau wa mahakama na sheria wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
  Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu wakimsikiliza  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TCRA YAWAPIGA MSASA WASANII JUU YA MATUMIZI YA MITANDAO YA MAWASILIANO

$
0
0
Naibu Mkurungenzi wa Masuala ya watumiaji Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Issac Mruma akizungumza na Baadhi ya wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongofleva) (hawapo pichani) juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii, huku akiwataka kujilinda dhidi ya Mbinu za kitapeli,wizi na udanganyifu kupitia mitandao ya Mawasiliano, wakati wa semima ya siku moja iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jiji Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akizungumza na Baadhi ya wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongofleva) (hawapo pichani) wakati wa semima ya siku moja iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jiji Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo leo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) Tanzania Jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.

TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA BABA WA JERRY MURO

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Muro, kufutia kifo cha Mzee Cornel Muro kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika Machame mkoani Kilimanjaro.

Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Muro, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa

Marehemu Cornel Muro ni baba mzazi wa Afisa Habari wa klabu ya Young Africans, Jerry Muro.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TAARIFA YA CHAMA CHA CUF KUFUATIA MWENYEKITI WAO KUTANGAZA KUJIUZULU LEO JIJINI DAR

$
0
0
Leo tarehe 6 Agosti, 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na kutangaza kwamba amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF).


Sisi kama Chama tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake. Ni haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi kwake.

Bila shaka, Profesa Ibrahim Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu katika miaka 16 ambayo alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe kiongozi wetu mkuu. Kwa nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na tutaendelea kumheshimu kwa utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi yetu. Tunamtakia kila la kheri katika mipango yake ya baadaye.

Chama Cha Wananchi (CUF) ni taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana maamuzi yake yote yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa Profesa Lipumba katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia wanachama na wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba Chama hichi hakitayumba.

Katika historia yake, CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi lakini mara zote kimeonesha uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba na misukosuko hiyo na kukabiliana na athari zake. Hatuna chembe ya wasiwasi kwamba hata mtihani huu tutauvuka na tunaamini tutaibuka tukiwa Chama imara zaidi.

Katibu Mkuu ameagiza kuitishwa kwa vikao vya dharura vya Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa siku ya Jumapili, tarehe 9 Agosti, 2015 ili kujadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.

Katika kipindi hiki, Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa watulivu na wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya kitaifa vya Chama.

Mwisho kabisa, tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika katika UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake. Tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu, uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM. 

Tunatambua kwamba kuna njama na mbinu kubwa na nyingi zinazofanywa na watawala kutaka kuuvuruga na kuuhujumu UKAWA wakidhani kwamba watapata manusura. Tumesema na tunaendelea kusema CCM mwaka huu hawana manusura. Watanzania wameamua kuwan’goa, na watan’goka Tanzania Bara na Zanzibar kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015. Wimbi hili kubwa la mabadiliko halizuiliki tena.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA
06 AGOSTI, 2015

MSAADA WA MATIBABU KWA NDUGU SELEMANI RASHIDI MKAZI WA KITONGOJI CHA LUGONGONI (A) NGURUKA MKOA WA KIGOMA

$
0
0
Selemani Rashidi (kushoto), akiwa na mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia mkasa mzima wa mwanaye, alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa Degedege na alimpeleka kwa mganga wa kienyeji na kupona matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi na kikawa kinakuwa na kushikana na sikio, kutokuwa na uwezo wa kipesa hakuweza mpeleka popote, Baba yake yapata Miaka kumi na tano toka afariki na ukizingatia ni pesa inayo hitajika, hayo yalisemwa na mama yake mzazi ambaye anaitwa Zamda  Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya kitongoji cha  Lugongoni, (A)  Kataa ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma, Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota kinyama hicho, kauli kutoka ni kwa shida, akijibu maramoja harudii tena kuongea na chooni anakwenda mwenyewe na kula anakula kama kawaida, mama anaomba kwa mtu yoyote mwenye kuona na kusia anaomba msaada wa hali na mali ili mwanaye apate matibabu, kwa mawasiliano mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti, Nguruka kigoma. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa blog.
 Selemani Rashidi,  Namba msaada  kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu kwa kinyama kilicho jitokeza kichwani mwangu toka nilipo zaliwa.

 Selemani Rashidi, anapoishi na mama yake mzazi

TCAA watoa Elimu ya Usafiri wa Anga kwa wananchi waliofika kwenye maonesho ya Nanena yanayofanyika Ngongo, Lindi

$
0
0
Afisa Mtoa Leseni Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Christopher Sabuni akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Tulieni iliyopo kata ya Mnazi Mmoja leo katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Ngongo yanayoendelea mkoani Lindi.
Afisa Habari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akiongea na baadhi ya wageni waliotembelea banda la mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Mwongoza Mdege Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Tuju Shalali akiwaonesha watoto waliotembelea banda mamlaka hiyo namna ndege vinavyorushwa angani kwa kutumia mfumo wa kompyuta wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Mwongoza Mdege Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Tuju Shalali akiongea na baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la Wizara ya Uchukuzi wakati Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Habari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila akiongea na baadhi ya wageni waliotembelea banda la mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Kilimo ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi. (Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Lindi)

JK APOKEA KOMBE LA KAGAME TOKA KWA AZAM FC IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho kikwete pozi na mabingwa Kombe la Kagame na mabingwa wa Tanzania Azam FC walipofika Ikulu jijini Dar es salaam kumkabidhi kombe hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015. Azam ambao pia ni mabingwa wa soka wa Tanzania Bara walishinda kombe hilo katika michuano ya Shirikisho la soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati yaani CECAFA hivi karibuni

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI AGOSTI 6, 2015

UMOJA WA WASANII WA FANI MBALIMBALI WAMUGA JK,WAMTANGAZA KUWA SHUJAA WA SANAA YA MUZIKI NCHINI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo  na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia akishiriki tukio hilo.Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dk.Jakaya Kikwete.
 Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City usiku huu.
 Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom,Kelvin Twisa
 Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa bongofleva
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city usiku huu.
Wanauziki wakongwe pia walikuwepo kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki. 

PICHA NA MICHUZI JR.

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

$
0
0

SIMUtv: Lipumba afanya maamuzi magumu , ajivua rasmi uenyekiti CUF na kuituhumu UKAWA. Tazama zaidi uchambuzi wa habari za Magazeti. https://youtu.be/KdEMeaxaBA8
SIMUtv: Maamuzi magumu ya Lowassa yahamia kwa Lipumba. Aukosoa UKAWA na kujiuzuru. Mengi yaandikwa katika Magazeti ya Leo. https://youtu.be/EsToWBi9JVg
SIMUtv:UKAWA hali tete,mwamba mmoja wavunjika,wahaha na vikao kumjadili Lipumba kuachia ngazi. Jionee habari hizo katika Magazeti ya Leo.  https://youtu.be/iECu-SGN5Kk
SIMUtv: Klabu ya Mwadui FC imetamba kuingia 4 bora msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kujihakikishia kusajili wachezaji machachari. https://youtu.be/PPEZQbRGA8E

WENGI WAJIUNGA NA NSSF MAONYESHO YA NANENANE

$
0
0
 Meneja Kiongozi wa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akiwaelezea faidaza kujiunga na mfuko huo wakazi wa Mkoa wa Lindi waliofika kwenye banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani humo.
 Meneja Kiongozi wa Masoko Na Uhusiano Eunice Chiume akiwapa Maelezo ya Faida za kuwa Mwanachama wa NSSF wanachama waliotembelea banda la NSSF mkoani Lindi.
 Mwanachama wa Hiari, Mrisho Mpoto akilipia michango yake kwenye maonesho ya Nanenane Mkoani Lindi.
Afisa Uendeshaji Muandamizi Kabona Kandoro akimkabidhi zawadi mmoja wa wanachama waliotembelea banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane mkoani Lindi.
Mwanachama mpya wa NSSF akipigwa picha kwa ajili ya kadi ya uanachama baada ya kujiunga na mfuko huo.

ZAWADI MASHINDANO YA JIMBO LA VUNJO (MBATIA CUP 2015) HADHARANI

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi.

KAMATI ya Mashindano ya Kombe la jimbo la Vunjo maarufu kama Mbatia Cup 2015 imetenga zaidi ya kiasi cha sh Mil 6 kama zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yanayoingia hatua ya nusu fainali pili leo.

Zawadi zilizotengwa ni pamoja na sh Mil 2,Kombe kubwa,Medali za Dhahabu na mipira mitatu kwa mshindi wa kwanza,Sh Mil 1,Kombe la kati,Medali za fedha na Mipira miwili kwa mshindi wa Pili huku mshindi wa tatu akipata Sh 500,000,Ngao,Medali za Shaba na Mpira mmoja.

Mwenyekiti wa kamati hiyo,Danielson Shayo alisema mbali na zawadi hizo kwa washindi,kamati pia imepanga kutoa zawadi za Jezi kwa timu nane ambazo zitafanikiwa kuigia hatua ya nane bora.

“Mshindi wan ne pia tumemuandalia zawadi ya Mpira ,mbali na jezi ambazo itakuwa imepata wakati wa kufanikiwa kuingia hatua ya Nane bora,lakini pia kuna zawadi kwa Mchezaji bora,Mfungaji bora,mlinda mlango bora,timu yenye nidhamu na kocha bora”alisema Shayo.

Shayo alisema mashindano hayo yatakayotumia viwanja vitano vya Chuo cha Ualimu,Marangu,Njia Panda,Kahe Magharibi ,Himo Polisi na Ifati yamepangwa kuchezwa kwa mtindo wa mtoano .
Baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo akiwa katika hafla fupi ya kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mbatia Cup 2015.
Mmoja wa Waratibu wa Mashindano ya Mbatia Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Vunjo,Danielson Shayo akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa washindi.

U.S. Government Awards $61Million to Help Strengthen Public Sector

$
0
0
The U.S. Agency for International Development (USAID) recently announced the award of a contract for $61 million to Abt Associates, Inc. for the Public Sector System Strengthening (PS3) project.  Through this award, USAID aims to support the Government of Tanzania to strengthen the public system to promote the delivery, quality, and use of government services, particularly for underserved populations.  

In commenting about the award, U.S. Ambassador Mark B. Childress stated, “The U.S. Government is committed to helping the Government of Tanzania build a strong and sustainable public sector that has the capacity to deliver quality services to all its citizens.”

The purpose of PS3 is to strengthen existing Government of Tanzania systems at both national and local levels to improve service delivery across sectors.  To reach the goal of improved government service delivery, PS3 will focus on four major systems components: governance and citizen engagement, human resources, financial management, and information systems.

At the national level, the project will focus on the development and operationalization of key strategies and policies.  At the local government-level, the project’s emphasis will be on helping to translate national guidance into action on the ground, while also informing the national level dialogue of the realities at the local government levels.  

PS3 will accommodate the multi-sectoral nature of local government authorities and assist in promoting inclusive and evidenced-based planning, management, and implementation of government services pertinent to health, education, agriculture, rural roads, and water and sanitation sectors.

By the end of the five year period the Government of Tanzania will be able to better distribute their workforce so that teachers, agriculture extension agents and health workers are available in rural areas, local governments will have increased tax revenue to better serve the needs of the public, local governments will better utilize data for decision making, and citizens will have increased influence over how local government budgets are planned and executed.
USAID’s Public Sector Systems Strengthening (PS3) project will work with the Government of Tanzania to strengthen the public system to promote the delivery, quality, and use of government services. For example, it will help ensure health facilities in underserved areas have skilled health workers, such as the technician pictured above at the Nyamagana Hospital in Mwanza. Photo Credit: Sala Lewis/Verve.

NMB MasterCard yazinduliwa Mkoa wa Mbeya.

$
0
0
Mkaguzi Mkuu wa ndani wa NMB Bw. Augustino Mbogella (pili kushoto) akimpa mkono Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw. Nyirembe Sabi baada ya uzinduzi rasmi wa familia ya kadi za NMB MasterCard kwa Mkoa wa Mbeya na Kanda nzima ya Nyanda za Juu. kadi hizo zikiwa ni :Tanzanite, Titanium na World Reward MasterCard. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyada za Juu Bi.Lucresia Makiriye na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NMB Bw. Filbert Mponzi.
Sehemu ya Wageni waalikwa.
Shurkani kwa wateja wetu waliopo Mkoa wa Mbeya kwa kutuunga mkono katika uzinduzi huu.

MBUNIFU WA MITINDO AMINA PLUMMER ATOA MADA NAMNA YA KUJITAMBUA KWENYE SEMINA YA KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

$
0
0
   
Mbunifu na Mmiliki wa Maduka ya Amina Design  Ambaye pia ni   Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Amina Plummer Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao. Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi  ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser (Katikati) Akiwa na Mbunifu Amina Plummer (Kushoto ) Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth  Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images