Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 930 | 931 | (Page 932) | 933 | 934 | .... | 3282 | newer

  0 0

  LIP1
  Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam,na kuwaambia kuwa CUF ni Taasisi,hivyo wanachama wote wanatakiwa kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni kukijenga chama cha CUF,Pro Lipumba aliyasema maneno hayo bila kutoa ufafanuzi wa kina.

  Profesa Lipumba alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho,lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake alikuwa na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na wanachama,aidha wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
  LIP2
  Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam
  LIP3
  Baadhi ya wanachama wa chama cha CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
  LIP4
  Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba 
  LIP5
  Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho Buguruni.PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG.
   
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
   
  MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),amewataka wanachama wa  chama hicho kukijenga kwa nafasi walizonazo iwe kiongozi au mwanachama wa kawaida.
   
  Lipumba ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama waliofika katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho wakitaka kauli ya yake juu ya chama na taarifa zilizopo katika mitandao juu ya kutaka kuachia nafasi yake uenyekiti wa chama hicho.
   
  Lipumba  amesema kuwa chama ni taasisi sio chama mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu hivyo wanachama tambueni hivyo.
   
  Aidha amewataka wanachama waisome katiba ya chama hicho kwa sababu zipo ili kuweza kujua chama jinsi kinavyoendeshwa kutokana na katiba ambayo inapitishwa na wanachama.
   
  Wakati huo huo  mkutano ulitishwa na chama hicho kwa lengo la Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa,Ibrahim Lipumba umearishwa kutokana na wazee wa chama hicho kuvamia Ofisi hiyo na kwenda kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho.
   
  Akizungumza wakati kuarisha Mkutano huo Mwenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Bara,Magdalena Sakaya amesema kuwa mkutano huo ulikuwa wa mwenyekiti Lipumba lakini wazee wa chama wamevamia hivyo hawezi kuzungumza tena.
   
  Sakaya amesema kitu ambacho alikuwa anataka kuzungumza anajua mwenyewe hivyo haiwezekani mtu mwingine azungumze kitu cha mwenyekiti.
   

  “Jamani tunaahirisha mkutano wetu ambao ulitakiwa kuzungumzwa na mwenyekiti lakini wazee wa chama wamevamia ofisi na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti”amesema Sakaya Naibu Katibu Mkuu Bara.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi Mhe Shaaban Ally Lilla na Katibu Mkuu kiongozi katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu 13 na Jaji wa Mahakama ya Rufaa mmoja aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2015.

  0 0

  SAM_4795Wafanyakazi wa Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,wakiwa katika banda lao la matangazo katika viwanja vya nane nane Themi njiro jijini Arusha (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_4802Mtangazaji maarufu ndani na nje ya Arusha Semio Sonyo wa kituo cha Redio 5 akirusha matangazo moja kwa moja katika maonyesho ya nane nane,kushoto Meneja masoko wa kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha, Bi.Sarah Keiya
  SAM_4789
  Taswira katika banda la kituo cha Redio 5 wakirusha matangazo yao moja kwa moja katika maonyesho ya nane nane Themi njiro jijini Arusha

  Meneja masoko wa ampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha, Bi.Sarah Keiya amesema kuwa kila wanaposhiriki maonyesho ya nane nane kila mwaka kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha wanawafikia wakulima,wafugaji na wafanyabiashara katika maonyesho hayo ya nane nane

  Pia alisema kwa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya kila aina ikiwemo la shindano la kuimba,kurup,kula na kunywa,vipaji vya danadana huku akiweka wazi kuwa zawadi zipo kwa washindi wa shindano hilo.

  0 0

   Watanzania walioshiriki kongamano la Young African Leadership watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC na kupokelewa na mwenyeji wa Balozi Liberata Mulamula.
   Pichani ni baadhi ya washiriki wa kongamano hilo walipokua wakijitambulisha kwa Mhe, Balozi kwani wote wametoka kwenye Nyanja mbalimbali za kitaaluma.
   Washiriki wa Kongamano ambao walikiri kujifunza mengi kutoka upande wa Marekani ambapo wamepata mwanga wa kuweza kuleta mabadiliko nchini Tanzania kutoka na taaluma walizopata.
   Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano hilo wakimsikiliza Mhe Balozi  na yake ya kusema.
  Picha ya pamoja washiriki wa kongamano hilo pamoja na Mhe Balozi Liberata Mulamula
  Picha na Ubalozi

  0 0  0 0

  IMG_1853Aliyevalia shati la blue ni Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia akiondoka katika banda la kampuni yaSimba Cement mara baada ya kutembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kenya plant helth inspectorate service Bi.Esther Kimani(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  IMG_1863Wananchi wakipata elimu katika banda la Simba Cement katika maonyesho ya nane nane ya kandaele ya kaskazini yanayoendelea katika viwanja vya njiro Themi jijini Arusha
  IMG_1851(1)Ugeni kutoka kenya wakiongozwa na Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia wakipata maelezo katika banda la Simba Cement 
  SAM_4855Afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement Leslie Massawe kushoto akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda lao katika maonyesho ya nane nane
  SAM_4853
  Tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya watumiaji wa saruji hapa nchini hawafati viwango vilivyowekwa na hivyo hupelekea kupata bidhaa isiyo bora kwa watumiaji wa bidhaa hiyo

  Hayo yamebainishwa na afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement ambao ni watengenezaji wa Saruji  ,Leslie Massawe wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembea banda lao katika maonyesho ya nane nane ,kanda ya kaskazini  jijini Arusha

  Massawe alisema kuwa utafiti uliofanywa na kampuni yao ya saruji inaonyesha kuwa baadhi ya wajenzi hawafuati  mchanganyiko unaokubalika baina ya saruji,mchanga,kokoto hivyo inapelekea kupata matofali yaliyochini ya kiwango 

  “Bidhaa zetu ni matokeo ya utafiti wa kina na uboreshaji makini unaofanywa na wataalumu wetu kupitia ujuzi wao wenye sifa zinazozingatia viwango vya ubora wa simenti Tanzania”alisema Massawe

  Aidha alisema kuwa wanautarabu wa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wateja wao pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya saruji ,katika ujenzi wa sekta mbalimbali sanjari na uzalishaji wa viwandani hali itakayosaidia upatikaniji wa ujenzi wa nyumba imara na miundombinu bora

  Alitoa wito kwa wananchi kupata elimu ya matumizi bora ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi kabla ya kuanza ujenzi,huku akiwataka mafundi ujenzi  na watengenezaji wa matofali kutenga muda wa kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na kampuni za saruji.

  0 0


  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Stamina akiwaburudisha mashabiki wake ambao ni wakazi wa Morogoro kwenye tamasha lililoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu ya huduma ya M-Pawa kupitia kampeni yake ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma hiyo inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi. Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya soko la mawenzi mkoani morogoro jana.
  Mtoto Salumu Mussa(15) ambaye ni mkazi wa Morogoro akiimba wimbo wa Stamina jukwaani kwa ujasiri kwenye tamasha lililoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu ya huduma ya M-Pawa kupitia kampeni yake ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma hiyo inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi. Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya soko la mawenzi mkoani morogoro jana.
  Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamefurika kwenye tamasha lililoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kutoa elimu ya huduma ya M-Pawa kupitia kampeni yake ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma hiyo inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi. Tamasha hilo lilifanyika katika viwanja vya soko la mawenzi mkoani morogoro jana.

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi – jeshi la Polisi

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, amewataka Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa na Wilaya, kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuzitatua changamoto zinazojitokeza katika jamii yetu hatua ambayo itasaidia kuutokomeza uhalifu na wahalifu.

  Kauli hiyo ameitoa mjini Dodoma, jana wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya, mafunzo ambayo yatawajengea uwezo wa kiutendaji katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.

  Hata hivyo, IGP Mangu, amesema kuwa, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ni wazi kuwa, kasi ya utendaji kazi iongezeke ili kujenga taswira bora ya kiutendaji ya Jeshi la Polisi na kwamba suala la utoaji wa huduma bora kwa mteja ni la lazima hususan katika Nyanja ya upelelezi, alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, amesema kuwa, mafunzo haya ya siku mbili yatasaidia kuongeza kasi ya utendaji na kwamba Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini imeandaa mafunzo haya ili kuongeza tija katika masuala ya upelezi.

  Ameongeza kuwa, jumla ya Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya 205 wanashiriki katika mafunzo haya na kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi hatua ambayo kwa pamoja itasaidia kuzuia makosa ya uhalifu na wahalifu.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakatia akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mjini Dodoma.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu, akizungumza na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya, wakatia akifungua mafunzo ya siku mbili yenyelengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji yanayofanyika mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Diwani Athumani, akitoa neno kwa Wakuu wa Upelelezi wa mikoa na wilaya (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili inayofanyika mjini Dodoma. (Picha na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi).

  0 0

  Timu ya Moro Kids imeukwaa uchampioni wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro baada ya kuwafunga Kihonda 2-1 katika mchezo wa funga dimba uliopigwa jana kwenye uwanja wa Shujaa mjini Morogoro.

  Ushindi huo kwenye mchezo wa jana uliohudhuriwa na mashabiki wengi uliwawezesha Moro Kids kufikisha pointi sita wakifuatiwa na timu ya Tecfort iliyohitimisha mashindano hayo ya mkoa ikiwa na pointi tatu.

  Wakati huo huo chama cha soka mkoani Morogoro (MOREFA) kimetangaza kikosi cha wachezaji 20 kitakacho uwakilisha mkoa huo katika mashindano ya taifa yaliyopangwa kuanza kutimua vumbia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Septamba 11 hadi 21.

  Katibu Mkuu wa MOREFA Emmanuel Kimbawala amesema kikosi hicho kilichochaguliuwa wakati wa michuano hiyo mkoani Morogoro kimeundwa na wachezaji wenye vipaji na ku0nyedha dhamira ya dhati ya kuweza kutwaa tena ubingwa wa Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu.

  Lengo la mashindano ya Airtel Rising Stars ni kuwapa fursa wachezaji chipukizi wa soka, wasichana na wavulana, kuonyesha vipaji vyao na hatimaye kuweza kuonekana na kuchaguliwa kuchezea timu mbalimbali. matunda ya Airtel Rising Stars yanaonekana katika timu za taifa za vijana na Twiga Stars.

  Mwaka huu mashindano ya Airtel Rising Stars yanajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke, Ilala Mbeya na Mwanza kwa timu za wasichana na wavulana huku mkoa wa Morogoro ukishirikisha wavulana peke yake wakati Arusha ni wasichana tu.
  Naodha wa timu ya Moro Kids Dissy Job akinyanyua kombe la ubingwa la Airtel Rising Stars baada ya kutawazwa mabingwa wa mkoa wa Morogoro.
  Timu ya Moro Kids waki pozi na kombe la ubingwa baada ya kutawazwa mabingwa wa mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Airtel Rising Stars.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (alieketi katikati mstari wa juu) akifatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Jaji Mohamed Othman Chande (aliesimama) wakati alipokwenda kuaga Mahakama. Hafla hiyo inafanyika hivi sasa ndani ya Ukumbi wa Mahakama Kuu Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni baadhi ya majaji pamoja Waziri wa Katiba na Sheria, Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro.
  Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu wakifatilia hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Jaji Mohamed Othman Chande, wakati Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kuaga Mahakama.
  Sehemu ya Maafisa wa Mahakama.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu, (aliyevaa koti jeusi) akikagua ujenzi wa jengo la kisasa la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.(Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)


  0 0

   Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.
  Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.
   Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
  Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.


  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF. Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada katika semina hiyo leo ofisi za WLF,Mikochini Jijini Dar.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani,akifafanua jambo.Waandishi wa Mitandao ya Kijamii Wapewa Elimu ya Afya na UzaziMeneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.

  BAADHI ya wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze kuelimisha zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo. 

  Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa  wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na  mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao.

   Alisema kazi ya kupunguza vifo vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au hospitali pekee lakini jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo, alisema vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za kuonesha mapungufu na kueleza changamoto katika huduma za afya zinazotolewa kwa lengo la kuboresha zaidi huduma hizo.

   Alisema tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni kubwa nchini kwani takwimu zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama anayepoteza maisha kutokana na  matatizo ya uzaziSerikali. "...Kila siku kuna akinamama takribani 24 wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi nchini," alisema Dk. Mwakatundu. 

  Awali akizungumzia hali halisi ya uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa WLF, Victoria Marijani alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa Mpango kwani ni uwekezaji wenye faida na endelevu ambao unachangia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44. 

  Aliongeza kuwa uwekezaji huo wa ziada katika afya, elimu, usawa wa kijinsia na uwepo wa sera wezeshi za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata manufaa yatokanayo na ukuaji wa haraka wa uchumi. Alisema familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa na uwezo wa kuwatimizia watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu, mavazi, huduma za afya na makazi. 

  "...Atapata muda wa kushiriki katika shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo kwa familia yake. Alisema kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (vifo 81 kwa vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia 27 tu ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za kisasa za Uzazi wa Mpango. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Na Frank Shija, WHVUM

  Vijana watakiwa kujitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa yatafanyika tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Ushiriki wa Vijana katika masuala ya Kiraia”

  Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

  Bibi Sihaba amesema kuwa maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ikiwa ni kutambua mchango wa Vijana katika kuleta maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla kwa kuwa ndiyo kundi kubwa la nguvu kazi yenye kuleta chachu ya maendeleo kupitia ubunifu.

  “Natoa wito kwa vijana wote nchini kushiriki katika kuadhimisha Siku hii muhimu kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao, kwa wale wa Dar es Salaam ni vyema wakajitokeza na kushiriki maadhimishio hayo ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hapa” Alisema Sihaba.

  Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwayatafikia kilele siku ya Jumatano ya tarehe 12 Agosti yatatanguliwa na Kongamano litakalofanyika mnamo tarehe 10 mwezi huu katika ukumbi wa Karimjee nakushirikisha zaidi ya Vijana 150 watakao jadiliana mada mbalimbali ikiwemo ushiriki wa vijana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Aliongeza kuwa sambamba na maadhimisho hayo siku ya kilele kutakuwa vijana watapata fursa ya kutoa na kupata burudani mbalimbali kupitia matamasha na michezo, pia siku nhiyo itatumika kwa vijana kuonyesha kazi zao zikiwemo za ubunifu.

  Katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyikiwa Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika mikakati na uendelezaji wa Vijana nchini amjbapo baadhi ya wadau hao ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), AMREF,ILO, PSI, IYF, Restless Development na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha na vijana.

  Siku ya Kimataifa ya Vijana ilianza tangu mwaka 1991 nchini Australia ikiwa na lengo la jumuiya ya Kimataifa na jamii kwa ujumla kupata fursa ya kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi zao, na mwaka 1998 ilikubaliwa na jopo Mawaziri wanaoshughulikia Vijana na hatimaye Umoja wa Mataifa uliridhia rasmi kuitambua siku hiyo kuwa ya maadhimisho Kimataifa ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Baraza la Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania walianza kuadhimsha siku hiyo muhimu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na waandishi wa habari wa wa Kituo cha Redio cha TBC Taifa walipomtembelea ofisini kwake jana.Waliosimama kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wa wizara hiyo Bw. James Kajugusi na wa mwisho kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bibi. Concilia Niyibitanga.Waandishi hao walifika ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kwaajili ya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifanya mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani na mwandishi wa habari kutoka Redio ya Taifa TBC Taifa Bibi. Betty Tesha. Maadhimisho hayo kitaifa yanaadhimishwa tarehe 12 Agosti jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM

  0 0


  0 0

  Mhandisi Kisaka kutoka TCRA makao makuu akitoa somo kwa viongozi wa vyombo vya habari kanda ya Nyanda za juu kusini.

  Na Edwin Moshi, Mbeya
  Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuwa makini na kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufuata maadili na weledi wa taaluma hiyo ili kufanikisha uchaguzi huo kwa amani

  Hayo yamesemwa leo jijini Mbeya na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wakati wakiwapa semina mameneja na wamiliki wa vyombo vya habari vilivyopo kanda ya nyanda za juu kusini semina iliyofanyika jijini Mbeya

  Akizungumza katika semina hiyo wakati wa hotuba ya kufungua semina hiyo Naibu Mkurugenzi idara ya utangazaji TCRA makao makuu Bw. Fredrick Ntobi amewasisitiza waandishi wa habari kote nchini kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao ili kuepuka madhara yatakayoweza kujitokeza pindi watakapotoa taarifa potofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi nyingine zitakazofuata baada ya uchaguzi huo

  "Naomba muwe makini na uandishi wenu wa habari maana ninyi ninyi ndio mtakaofikishwa mahakamani, ninyi ndio mtakaofikishwa The Heag, ajirini watu wenye professional (taaluma) ya habari, hii itasaidia kuepuka kauli za uchochezi, zitawamaliza na niwahakikishie sisi kama mamlaka tupo makini na tutafuatilia vyombo vyote vya habari" amesema Ntobi

  Kwa upande wake Mhandisi mkuu idara ya Utangazaji TCRA makao makuu Mhandisi Andrew Kisaka amewataka washiriki kuhakikisha wanazingatia usawa katika kutoa taarifa za uchaguzi na kuepuka upendeleo wa baadhi ya vyama

  "Unakuta CHADEMA mnawapa dakia mbili kujieleza halafu CUF mnawapa dakika 20 hili sio sawa, hakikisha mnatoa kipindi kilichowapa fursa sawa wagombea wote bila upendeleo

  Aidha Kisaka amewaonya waandishi wa habari kuacha kujiingiza kwenye siasa kwa kushabikia wagombea fulani na kuingiza itikadi zao katika kuripoti habari za uchaguzi kwa kuwa itasababisha kuwagawa wananchi na kuona kituo chako kina upendeleo jambo ambalo halitakiwi

  Katika semina hiyo washiriki wamepewa nafasi ya kuuliza ma swali na kutoa ushauri wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa mambo hayo katika vyombo vyao vya habari wanavyofanyia kazi
   Semina ikiendelea
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika semina hiyo

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Ndugu Augustino Ngonyani, anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi Mzee Joachim A. Ngonyani kilichotokea alfajiri ya tarehe 6.8.2015, Dar Es Salaam. 
  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Sinza Makaburini. 
  Mwili wa marehemu utaagwa tarehe 8.8.2015 Jumamosi saa 3 asubuhi katika kanisa la Mt.. Petro Oysterbay na baada ya hapo kusafirishwa siku hiyo hiyo kwenda Songea kwa Mazishi. 
  Mazishi ya Mzee Ngonyani yanatarajia kufanyika siku ya Jumatatu 10.08.2015, Kijijini Kwake Parangu, Songea.

  Bwana alitoa, Bwana Ametwaa na Jina lake lihimidiwe. 
  Amen

  0 0
 • 08/06/15--06:00: MKWASA ATANGAZA 29 STARS

 • 0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa kituo cha kufundishia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua Bibi Meagan  Garnahan wakati aliposawasili katika uzinduzi wa kituo hicho katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Bw.Abdul Barwan Abdalla kuhusu ufugaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa wakati alipotembelea maonesho ya kazi mbali mbali za ujasiria mali kabla ya kukifungua kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kazija Gharib Issa akiwa ni miongozi mwa wanawake waliopata mafunzo ya kutengeza vifaa ya kutumia umeme wa jua nchini India wakati alipotembelea maonesho ya kazi mbali mbali za ujasiria mali kabla ya kukifungua kituo cha kuwafunzia Wanawake utengenezaji wa vifa vya Umeme wa jua na kazi mbali mbali za ujasiriamali katika kijiji cha Kibokwa Wilaya ya kaskazini A Unguja leo (katikati) Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana Wanawake na Watoto Bi Zainab Omar Mohamed.  [Picha na Ikulu.]

   KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


older | 1 | .... | 930 | 931 | (Page 932) | 933 | 934 | .... | 3282 | newer