Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

TCRA YATOA ELIMU KWA WANANCHI KWENYE MAONESHO YA KILIMO ARUSHA

$
0
0
Gari maalumu la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) likiwa kwenye uwanja wa maonesho ya Nanenane Njiro jijini Arusha,wananchi wanaotembelea banda la TCRA hupata elimu namna gari hilo linavyofanya kazi. 

Mmoja wa wananchi akipata maelezo kwenye banda la TCRA kwenye uwanja wa Taso ,Njiro jijini Arusha.
Afisa wa TCRA,Oswald Octavian(kulia)akimweleza jambo namna taasisi hiyo inavyofanya kazi ya kusimamia mawasiliano nchini.

NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.

Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.

Waziri Mkuu aitaka NHIF kuongeza bidii katika kutoa elimu ya Afya kwa Jamii

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipatiwa maelezo ya huduma zinazotolewa katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko huo, Rehani Athumani, wakati alipotembelea Banda lao kwenye Maonyesho ya Nane nane, mkoani Lindi.
Waziri Mkuu akitoa maagizo kwa uongozi wa Mfuko wa kuongeza elimu hususan katika magonjwa ya unyanyapaa ndani ya jamii.
Mwanachama wa Mfuko akipata maelezo ya huduma zinazotolewa bandani hapo.

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini Malawi ambaye pia ni Kiongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini humo, Maepheson Matowe. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga.
Mtoa mada wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Usalama Barabarani ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samweli Manyele akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Prof. Manyele alitoa elimu ya jinsi ya kusafirisha salama kemikali. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati meza kuu) akijadili jambo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wengine katika picha ni wajumbe wa mkutano huo. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE PETER KISUMO

$
0
0

 Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dk.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mwanasiasa Mkongwe nchini Mzee Peter Kisumo aliyefariki dunia jioni ya tarehe 3 Agosti katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi,Dk.John Pombe Magufuli akizungumza na mjane wa marehemu Pater Kisumo, Hosiana Kisumo nyumbani kwa marehemu mtaa wa Isevya ,Upanga,Dar es Salaam.(Picha na Adam Mzee) BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

Rais Kikwete kuzindua benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Thomas Samkyi, (pichani kati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Benki hiyo,Kinondoni kuhusu uzinduzi wa benki hiyo utakaofanyika Agosti 8, 2015,jijini Dar. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki, Bi Rosebud Violet Kurwijila.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bi Rosebud Violet Kurwijila akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),katika ofisi za Benki hiyo jijini Dar mapema leo kuhusu uzinduzi wa benki hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Thomas Samkyi, na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Sera, Bwana Francis Assenga.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema asubuhi ya leo

 Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua rasmi benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, ambayo inalenga kuanzisha mtizamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali, kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo. Benki hiyo inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa sekta ya kilimo ambayo imeajiri zaidi ya aslimia 70 ya Watanzania.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kwa ngazi mbili: ngazi ya kwanza itahusisha uzinduzi wa Makao Makuu ya TADB jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 7 ya mwezi huu; ambapo ngazi ya pili itahusisha uzinduzi rasmi wa TADB mbele ya wadau wake wakuu ambao ni Wakulima, kwenye Maonesho ya Nane Nane Mkoani Lindi, katika kilele cha Siku Kuu ya Wakulima hapo tarehe 8 Agosti 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya benki hiyo yaliyoko Barabara ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa benki, Bwana Thomas Samkyi, alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa benki hiyo ni kuboresha tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali ili kuwezesha uendelezaji wa miundombinu ya kilimo kama miradi ya umwagiliaji, usafirishaji, uhifadhi, mindombinu ya masoko, n.k. ambayo inachangia maendeleo ya sekta ya kilimo.

‘Uanzishwaji wa benki hii unalenga kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo ambayo inaachwa na benki za biashara, ili kuchochea kukua kwa sekta ya kilimo, kwa kutoa mikopo na huduma nyingizezo za uwezeshaji wa kilimo kwa wakulima, ambao wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za kibenki’ alisema Bw. Samkyi.

Akieleza zaidi kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo, Bwana Samkyi alisema Benki ya Wakulima itakuwa msitari wa mbele katika kusukuma shughuli za kilimo pamoja na kuchagiza benki na taasisi nyingine za kifedha kushiriki katika kuwezesha shughuli za kilimo.

‘Benki hii imeundwa ili kutoa mikopo kwa masharti nafuu, pamoja na kutoa huduma nyinginezo zitakazoongeza uwezo wa wakulima kukopa na kuzalisha. Ili kufanikisha haya, benki inabidi iwe na vyanzo endelevu vya fedha za kutosha kwani nchi hii ni kubwa na wadau wa benki ni wengi sana. Lengo kuu ni kubadili kilimo cha Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara’ alisema Bw. Samkyi.

Benki hii pia inatarajiwa kuwa ni kiungo muhimu cha utekelezaji wa mageuzi ya awamu ya pili ya sekta ya kifedha, na vile vile kuboresha maendeleo ya kilimo nchini ikizingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo ya miaka mitano mitano, Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo, na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA), pamoja na sera mbali mbali za Serikali zinazohusu sekta ya kilimo.
  
Kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania

Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (katika kuanzishwa kwake) ni taasisi mpya ya kifedha iliyoanzishwa na serikali kwa madhumuni ya kuboresha huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na huduma nyinginezo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Benki hii imeanzishwa ili kufikia malengo ya taifa yaliyoafikiwa katika Tanzania Vision 2025, kusudio likiwa ni kuwezesha na kutosheleza upatikanaji wa chakula, kuchochea kilimo cha biashara, pamoja na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umasikini.




KAMATI YA UTENDAJI YA CHAMA CHA HABARI ZA MICHEZO (TASWA) KUKUTANA AGOSTI 7 2015 JIJINI DAR

$
0
0

A; KIKAO KAMATI YA UTENDAJI

KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), inatarajiwa kukutana Ijumaa Agosti 7, 2015, Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yahusiyo michezo na waandishi wa habari za michezo hapa nchini.


Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili namna bora ambayo chama kinaweza kushiriki kwa kuangalia jinsi ya kuwaunganisha wanamichezo kwa namna mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa maslahi ya michezo nchini.


Moja ya madhumuni ya TASWA wakati inaanzishwa ni kuwaunganisha waandishi wa habari za michezo nchini, kushirikiana katika kukuza na kupromoti michezo na wanamichezo kwa njia ya kalamu na njia nyingine za kupashana habari.

Kwa msingi huo tunaamini kikao kitatoa muongozo mzuri, ambao unaweza ukasaidia wanamichezo hapa nchini kufahamu sera za michezo kwa wagombea mbalimbali na hivyo kufanya uamuzi sahihi wakati ukifika.


Pia kikao kinatarajiwa kufanya uteuzi wa washiriki wa semina mbili zinazotarajiwa  kufanyika hivi karibuni, zikihusisha waandishi wa habari za michezo wa kada ya kati na wale wazoefu.


Tunaamini tumetoka mbali na tunajua safari yetu ya kuchangia kukuza michezo nchini bado ni ndefu na ina mabonde, mabwawa na utelezi. Sisi hatujiulizi ,  Jee tutafika? Bali hujiambia juhudi zetu zitatufikisha tunapotaka kufika.


B; PONGEZI AZAM

Tunatoa pongezi kwa timu ya soka ya Azam FC kwa kuibuka bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ mwaka 2015.


Tunaungana na Watanzania wengine katika kufurahia ubingwa huu, baada ya Jumapili Azam kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo tunawaomba wachezaji watumie ubingwa wa Kagame kama changamoto ya kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani.


Azam wasibweteke na kuona tayari wamemaliza kazi, bali waendelee na jitihada za kutafuta mafanikio makubwa zaidi.


C: UTOAJI WA VITAMBULISHO

TASWA ilisitisha kutoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake kwa muda kwa sababu ilikuwa ikifanya utaratibu wa kubadili vile vya awali na kuwa na vitambulisho vya kisasa zaidi, ambapo suala hilo lipo hatua za mwisho kukamilika na hivi karibuni wanachama wote wapya watapatiwa vitambulisho vyao.


Nawasilisha,

Amir Mhando,

Katibu Mkuu TASWA

05/08/2015

MOJA YA KIPAUMBELE CHETU NI KUIGEUZA TTB KUWA MAMLAKA - DK MERU

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (Mwenye miwani) kuzungumza na wafanyakazi alipotembelea bodi hiyo jana.
Mmoja wa wafanyakazi wa TTB Bw. Geofrey Tengeneza ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano akielezea jambo kwa Katibu Mkuu alipotembelea ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuzungumza na wafanyakazi.  
 Baadhi ya wanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania wakimsikiliza kwa makini  Katibu Mkuu Dk Meru alipokuwa akizungumza nao.

 Na: Geofrey Tengeneza
Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kuupa kipaumbele mchakato wa kuifanya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) kuwa Mamlaka ya Utalii Tanzania (TTA) kwa lengo la kuiwezesha Bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Aidha Wizara hiyo imeitaka TTB  kuangalia ni maeneo gani yanaweza kuwa ni vyanzo vya mapato vitakavyoiwezesha Bodi kujiingizia fedha.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru  alipotembelea Makao makuu ya Bodi ya Utalii yaliyoko katika jengo la IPS jijini Dar es salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bodi hiyo.
Dkt Meru ameipongeza   Bodi ya Utalii kwa kuendelea kufanya kazi vizuri katika mazingira yenye changamoto nyingi hasa za kifedha zinazoikabili. Amesema TTB ndiyo chombo chenye dhamana ya kutangaza vivutio vya utalii kwa ujumla wake, hivyo kinapaswa kuwezeshwa kutimiza jukumu hilo kwa niaba ya nchi badala ya kila taasisi kutangaza vivutio inavyosimamia.
“Tunawajibu wa kuwawezesha TTB mtekeleze majukumu yenu vizuri kwa kuwa ninyi ndio hasa mliokabidhiwa jukumu la kutangaza vivutio vyetu vyote vya utalii kama vile vya kihistoria, fukwe, wanyama, milima na kadhalika” alisema.


Hii ni ziara ya kwanza ya Dk Meru kutembelea Makao Makuu ya ofisi za Bodi tangu kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo. Bodi ya Utalii Tanzania ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara yake yenye jukumu la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

TAZAMA SHAMRA SHAMRA ZA MAGUFULI ALIVYOCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA CCM

STAMICO KUANZISHA MTANDAO WA KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico), Zena Kangoi akizungumza na waandishi wahabari juu mafanikio ya stamico yaliyofanywa katika katika Ofisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuuwa Stamigold, Mhandisi Dennis Sibugwao akizungumza na waandishi wahabari juu Stamico inavyosimamia mgodiwa STAMIGOLD, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Stamico,jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Stamico, Rehema MwakajubeBeatrice akizungumza na waandishi wahabari juu ya mipango mikakati ya uwekezaji wa StamicoiliyofanyikaMakao Makuu ya Stamico jijini  Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Deusdedith Magala, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchongaji ,Alex Rutagwelela.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico, Zena Kangoi akiwa na baadhi ya wakurugenzi wakati akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika makao Makuu jijini Dar es Salaam.

 Na ChalilaKibuda,GlobuyaJamii 
 SHIRIKA la Taifa la Madini(Stamico) limesema linatarajia kuzindua mtandao utaosaidia kupata taarifa mbalimbali za kuweza kuchimba kisasa. 

Akizungumza na waandishiwa habari jijini Dar esSalaam, Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji, Zena Kongoi amesema kuwa kuanzishwa kwa mtandao kwawachimbaji wadogo kutawafanya kuweza kukua kiuchumi kuliko ilivyosasa kwa uchimbaji duni. 

Amesema kuwa mtandao utasaidia jinsi ya kuweza kupata vifaa vya kuchimbia madini kutokana na taarifa zitazowekwa katika mtandao. 

“Lengo letu ni kuwa saidia watanzania wenzetu katika uchimbaji wamadini kuweza kwenda kisasa zaidi nasio uchimbaji duni ambao unarudisha maendeleo yao”amesema Zena. 

Amesema Stamico imeongeza mapato yake kutokana na uwekezaji wakupitia kampuni tanzu za utoaji wa huduma za kibiashara kutoka Sh.Milioni 281 kwa mwaka fedha 2014 /2015 hadi kufikia Sh.Bilioni 3.17 kwa fedha 2014 /2015. 

Zena amesema wanatarajia kuzalisha umeme wamakaa yamawe ya Kiwira ambapo watazalisha megawati 400 za umeme hali ambayo itapunguza tatizo la umeme kwashirika  licha yakuweka miradi yakusaidia wachimbaji wadogo lakini wameweza kuwekeza uchimbaji wamadini kwakushirikiana na makampuni mengine kutokana shariaziliwekwa baada ya mabaoresho ya shirika hilo. 

Amesema baadhi yamiradi ya uzalishaji wa  madini imeanza kuzalisha na kuwezasha shirika kutoka hatua moja kwenda nyingine katika utoaji huduma pamoja ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kuongeza ajira nchini kutokana na miradi ya uzalishaji wa dhahabu. 

Zena amesema kuwa shirika limeanzisha miradi kuendeleza wachimbaji wadogo kitaalamu na ufundi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu (SMMRP) katika kuwaondoa katika uduni. 

Amesema katika mradi wa Stamigold umesafirisha na kuuza dhahabu katika nchi ya Switzerland kwa kiasi cha Wakia 12,923.35 na kuingizia shirika la Taifa la Madini (Stamico) na taifa kwa ujumla Dola za marekani Milioni 15.6. na kuaza kurejesha mrabaha wa asilimia 4.0 ya mauzo sawa na sh.1.3 milioni za serikali na Wizara ya Nishati na Madini na kulipa ushuru sh.milioni 40.

Aidha amesema shirika limeweza kuanzisha mradi wa ununuzi wa madini ghafi ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa maeneo ya vijiji vya Kabingo,Murongo ,Syndicate na Rugasha katika Wilaya Kyerw,mkoani Kagera na kuyauza madini hayo kwenye soko la nje ya nchi ikiwa na lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo . 

Zena amesema wako katika mazungumzo na Benkiya TIB kuweza kukopa Dola za Marekani700,00090000 kwaajili ya kununua mitambo hali ambayo shirika litaweza kukua katika kuendesha miradi mbalimbali. 

Airtel yakabithi pesa kwa washindi wa promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”

$
0
0
Gabriel Ferdinand (kulia) mwanafunzi wa Musoma Mara
akikabidhiwa fedha na Meneja wa Airtel Musoma, Emmanuel Rafael
(Kushoto) baada ya kuibuka mshindi wa droo ya pili ya promosheni ya
“Jiongeze na Mshiko”.
Wakazi wawili wa Tabora na Musoma wameeleza furaha yao mara baada ya Kampuni ya mawasiliano ya Airtel kuendelea kukonga nyoyo za wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwa kuwatangaza na kuwakabithi pesa zao baada ya kuibuka washindi wa wiki ya pili ya promosheni inayoendelea ya “Jiongeze na Mshiko”.

Washindi hao ni pamoja na , Gabriel Fernandis(18) mwanafunzi na mkazi wa wa Mkoa wa Musoma mkoani Mara, yeye amejishindi shilingi milioni 1 , na mshindi wa pili ni Hamis Rashid(52)na mkazi wa Sikonge mkoa waTabora yeye amejishindi shilingi milioni 3.

Sambamba na kukabithi zawadi hizo , Airtel imeendesha droo ya wiki ya tatu ya “Jiongeze na Mshiko” katika ofisi ya makao makuu ya kampuni ya Airtel iliyopo Morocco jijini Dar Es Salaam ilihudhuriwa na waandishi wa habari na wasimamizi kutoka bodi ya bahati nasibu Tanzania.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi yake , Grabriel Fernandisi alisema”nimefurahi sana kuibuka mshindi katika promoshenii hii ambayo nimeshiriki bure , bila gharama yoyote na kujibu maswali na kujiongezea points zilizoniwezesha kushinda.

Nafurahia ushindi huu kwasababu pesa hizi zitanisaidia kujiendeleza kwenye masomo yangu” Akiongea na waandishi wa habari, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki, amesema kwamba tunayofuraha kuwazawadia washindi wa wiki ya kwanza na ya pili ya promosheni “Jiongeze na Mshiko” ni matumaini yetu kuwa pesa hizi zitawawezesha kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi nakutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

Hamisi Rashid (kulia) mkulima wa Sikonge, Tabora akikabidhiwa
fedha na Meneja wa Airtel Tabora, Phidelis Lugangila (Kushoto) baada
ya kuibuka mshindi wa droo ya pili ya shindano la “Jiongeze na
Mshiko”.
Tutaendelea kuwazawadia wateja wetu kila wiki kwa muda wa wiki 16 hivyo natoa wito kwa watanzania kuendelea kujiunga na kushiriki katika promosheni hii bila gharama yoyote na kupata nafasi ya kujishindia.

Pamoja na kuwazawadia wateja wetu, leo pia tunaendesha droo ya wiki ya tatu na kutangaza washindi wengine wawili ambao wameibuka washindi. Katika droo ya leo tumebahatika kuwapata washindi wawili ambao ni pamoja na Afrillious Kapinaa (21) mwanafunzi, Mkazi wa Dar es Saalam amejishindia shilingi milioni moja pamoja na Shangai Rodger (53) mfanyakazi wa TRA na mkazi wa Tanga amejishindia shilingi milioni 3"

“Tunawashukuru wateja wetu na Watanzania wote walioshiriki na wenye sifa za kushiriki katika promosheni hii ya aina yake waendelee kushirikiIli kwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

WAZIRI MKUU: WANAOHITIMU JKT WAPEWE NYENZO

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itapaswa itafute njia za kuwawezesha vijana wanaohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili waweze kutekeleza kwa vitendo mafunzo wanayoyapata na waweze kujiajiri.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Agosti 4, 2015), wakati akizungumza na wananchi na washiriki wa maonyesho waliohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya 22 ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) ambayo mwaka huu yanafanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.

Akizingumza mara baada ya kutembelea mabanda zaidi ya 10, Waziri Mkuu Pinda alisema kuna haja ya kuwatafutia fursa za kujiajiri vijana wanaohitimu mafunzo hayo ili wasibweteke.

“JKT ndiyo inayofundisha vijana wetu katika fani mbalimbali… tuwatafutie fursa za kujiajiri mara wanapohitimu mafunzo ili wasitoke huko na kubweteka eti hawana kazi,” alisema.

Alisema kuna haja ya kuweka mfumo maalum kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT ambao utawatambua vijana wachache wanaotoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini ambao hupatiwa mafunzo ya ujasiriamali kama vile kutengeneza batiki, sabuni, samani, mabanda ya kuku, kufuga mbuzi, ng’ombe, samaki na kuku na kilimo cha bustani za mboga za majani.

“Mtu akishapatiwa ujuzi huu akaachwa arudi kijijini hawezi kufanya chochote… lazima atakaa kijiweni na kudai hana ajira. Tutafute mfumo wa kuwasaidia ili wapate mtaji wa kuanzia, wajiajiri kupitia kile walichofundishwa na baadaye iwe ni mfumo wa kuzungusha ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika,” alisema huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kukipongeza kituo cha utafiiti cha Naliendele kwa kuibua aina mpya 16 za mbegu za korosho ambazo zimesaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo hadi kufikia tani 200,000 kwa mwaka ikilinganishwa na tani 16,000 miaka michache iliyopita.

“Ninawasihi ndugu zangu wa Lindi na Mtwara tusikilize wataalamu wanatuambia nini kwa sababu utafiti ndiyo mkombozi mkubwa wa kilimo cha Tanzania. Tufuate maelekezo wanayotuelekeza na hii si kwa korosho tu, iwe ni karanga, ufuta au alizeti kwani ni mazao yanayokubali vizuri katika ukanda huu wa Kusini,” alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo imekuwa ikitekeleza mipango ya Kitaifa ikiwemo shughuli za kuendeleza kilimo kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) ambayo imefikia ukomo. “Hivi sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Awamu ya Pili ya Programu hiyo yaani ASDP II. Programu hiyo  imekuwa ikitekeleza Kilimo Kwanza na miradi mbalimbali ya kilimo na imekuwa muhimili muhimu katika kuendeleza kilimo chetu nchini,” alisema.

Waziri Mkuu Pinda amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Wilaya wabadili mitazamo yao kama kweli wana nia ya kuwasaidia wananchi.

“Viongozi hatuna budi tuwe karibu na wananchi na hasa maafisa ugani. Hawa wanapaswa kujituma ili waweze kweli kubadili wananchi kwani asilimia 70 ya Watanzania ni wakulima, wafugaji na wavuvi,” alisisitiza.

Maadhimisho hayo ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) yanatarajiwa kufungwa Jumamosi, Agosti 8, mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete.

WANARIADHA WA POLISI WAREJEA KUTOKA SWAZILAND

$
0
0
Wanamichezo wa Polisi Tanzania waliokuwa wakishiriki Michezo ya Umoja wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mji wa Mbabane Swaziland wakiwa katika uwanja wa ndege wa Swaziland baada ya kumalizika kwa michezo hiyo ambapo walifanikiwa kujipatia jumla ya medali kumi na moja .(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Swaziland)

BANDA LA JESHI LA MAGEREZA KUWANUFAISHA WANANCHI WA LINDI NJIA BORA ZA KISASA ZA UFUGAJI MIFUGO, MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KITAIFA

$
0
0
Na Lucas Mboje, Lindi

Wananchi mbalimbali wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wanaotembelea katika Banda la Jeshi la Magereza Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa wananufaika na elimu inayotolewa bure na Maafisa Mifugo wa Jeshi hilo kuhusiana na njia bora na za Kisasa za Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyama.

Akizungumza umuhimu wa elimu hiyo kwa Wananchi, Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Mlasani Kimaro amesema lengo kubwa la kutoa elimu hiyo kwa Wananchi ni kusaidia kuboresha vipato vyao sambamba na kuondokana na Ufugaji wa kizamani usiokuwa na tija.

"Tunatoa elimu hiyo bure kwa Wananchi wote wanaotembelea katika Banda letu ili waweze kuzitumia mbinu hizo za kisasa kufuga kisasa hususani kupitia teknolojia hii ya Uhamilishaji Mifugo hivyo kuboresha vipato vyao na kujiletea Maendeleo katika jamii zao". Alisema Kamanda Kimaro.

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kutumia fursa hiyo kutembelea Banda la Jeshi la Magereza, lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi ambalo Mwaka huu limejielekeza kwenye elimu ya Ufugaji wa kisasa.

Jeshi la Magereza nchini lina mashamba makubwa yanayofuga ng'ombe wa nyama na maziwa ambapo kwa upande wa ng'ombe wa nyama ni aina ya "Tanzania Shorthorn Zebu" na Boran.

Miongoni mwa mashamba makubwa yanayofuga ng'ombe wa nyama na maziwa ni pamoja na Gereza la Ubena - Pwani, Mbigiri - Morogoro, Mgumu - Mara, Kitengule - Kagera, Kingurungundwa - Lindi, Namajani - Mtwara, Majimaji - Ruvuma na King'ang'a - Dodoma.

Ng'ombe wa maziwa ni Magereza ya Kingolwira - Morogoro, Isupilo - Iringa, Mugumu - Mara, Arusha, Songwe - Mbeya, Mollo - Rukwa na Kitengule - Kagera ni miongoni mwa mashamba makubwa yanayomilikiwa na Jeshi la Magereza yanayohusika na Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Aidha, Mikoa yote nchini kuna magereza yanafuga idadi ndogo ya ng'ombe wa nyama kwa ajili ya nyama ya kulisha wafungwa, ziada huuziwa Askari na Wananchi wengine.

Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yamefunguliwa Agosti 04, 2015 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Matokeo Makubwa Sasa" - Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Wakulima na Wafugaji.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza(wa pili kulia) akipata maelezo ya Kitaalam kuhusu Ufugaji wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa kutoka kwa Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(wa kwanza kulia). Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wakulima Kitaifa, Bw. Engelbert Moyo.
Ng'ombe Dume aina ya Boran ambaye hutumika kuboresha vinasaba vya ng'ombe bora wa nyama. Ng'ombe huyu amekuwa kivutio kikubwa kwa Wananchi wengi wanapotembelea katika Banda hili la Jeshi la Magereza ili kujifunza Stadi za Ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa na nyama kupitia teknolojia ya Uhamilishaji wa Mifugo.
Ng'ombe wa maziwa kutoka Gereza Kingolwira, Morogoro katika Banda la Jeshi la Magereza ambalo linatoa elimu ya Ufugaji wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa kwa Wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wanapotembelea Banda hilo. Maziwa yanayozalishwa katika Mashamba ya Mifugo ya Jeshi la Magereza hutumika kwa ajili ya Lishe ya Wafungwa, watoto wa Wafungwa na kuuzwa kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza na Wananchi wengine.
Mshiriki wa Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi, Mtaalamu wa Mifugo Koplo wa Magereza, Henry akiandaa vifaa vya teknolojia ya Uhamilishaji wa Mifugo kabla ya kuanza kutoa elimu hiyo kwa Wananchi mbalimbali wanapotembelea katika Banda la Jeshi la Magereza.

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI WA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI

$
0
0
 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .
 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.


YST YAENDESHA MAONYESHO YA 5 YA SAYANSI, JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gosbert Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku tatu ya miradi na ubunifu wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi kutoka shule 120 nchini. Maonyesho hayo yatafikia kilele Ijumaa Agosti 7, 2015. (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).

Mwanzilishi Mwenza wa YST, Joseph Clowry, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii. 
Makamu wa Rais wa kampuni ya kuchakata mafuta na gesi ya BG Tanzania, John Ulanga, akizungumzia udhamini wao katika maonyesho hayo ya YST. Kampuni hiyo imetoa kiasi cha Dola 200,000 kudhamini maonyesho ya mwaka huu. 

LUTALOSA YEMBA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA ADC

$
0
0
 Wanachama wa chama cha ADC wakishangilia mara baada ya kumtangaza mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa chama cha ADC wakipata urudani kutioka kwa kijana wao wa burudani katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kumtangaza mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,mgombea urais wa Zanzibar na mgombea mweza katika nafasi hiyo, katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Katibu mkuu wa chama cha ADC, Lidia Bendela akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ADC ambao walikuwa wanawatangaza wagombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wa Zanzibar pamoja na Mgomea mwezakatika mkutano uliofanyika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Chifu Lutalosa Yemba akigombea nafasi ya uraiskupitia chama cha ADC akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwania nafasi hiyo leo katika mkutano wa kamati kuu wa chama cha ADC  uliofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa chama cha ADC na Mgombea wa urais kupitia chama cha ADC, Said Miraji Abdala akizungumza mara mbaada ya kutangazwa kugombea nafasi ya mombea mweza kupitia chama hicho leo katika mkutano wa kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano watanzania kupitia chama cha ADC, Chifu Lutalosa Yemba na Mgombea wa urais wa Zanzibar,Hamad Rashid Mohamed wakipunga bendera za chama chao kuashiria ushindi wa kuwania nafasi za juu uongozi katika chama hicho, katika mkutano wa Kamati kuu uliofanyika katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Blogu ya Jamii.

Meno ya Tembo yakamatwa Zurich yakitokea Tanzania kwenda China

$
0
0
Confiscated Ivory displayed at Zurich Airport in Kloten on Tuesday, Aug. 4 , 2015. Swiss authorities say customs officials at Zurich airport have seized 262 kilograms (578 pounds) of ivory that three Chinese men had dispatched from Tanzania. Switzerland's customs authority said Tuesday that the ivory — found during a security check on July 6 and packed in eight suitcases — had an estimated black market value of about 400,000 francs (US $413,000). (Walter Bieri/Keystone via AP)

BERLIN (AP) — Customs officials at Zurich airport have seized 262 kilograms (578 pounds) of ivory that three Chinese men had dispatched from Tanzania, contraband that may have come from up to 50 elephants, Swiss authorities said Tuesday.

The ivory was found during a security check on July 6 and packed in eight suitcases, Switzerland's customs authority said. It put the estimated black market value at about 400,000 francs ($413,000).

The elephant tusks had been sawed into 172 pieces to fit into the luggage, which was being transported from Tanzania's capital, Dar es Salaam, to Beijing via Zurich. The head of the customs operation at the airport, Heinz Widmer, said officials estimate that the pieces came from 40 to 50 elephants.

Demand from China's rising middle class has been fueling elephant poaching in Africa and illegal trade in ivory, which is turned into jewelry and other decorative items.

The Chinese men were temporarily detained in Zurich and questioned, Widmer said. They could face large fines for violating customs and animal protection rules.
Heinz Widmer, Chief of the custom at Zurich Airport, shows confiscated Ivory at Zurich Airport

They could be used as jewelry or talismans, or as a symbol for strength in Chinese traditional medicine, Widmer said.

The ivory haul, while sizeable, is below the 500-kilogram (1,100-pound) threshold considered to be a large-scale seizure that indicates the likely involvement of organized crime, according to TRAFFIC, a wildlife trade monitoring organization.

Vast haul: The ivory was found during a security check on July 6 and packed in eight suitcases, Switzerland's customs authority said. It put the estimated black market value at about £265,000.

The group, which said that it doesn't speculate on the black-market value of ivory as a matter of policy, said the frequency of large-scale seizures has increased greatly since 2000, with 18 such hauls reported in 2013.

In May, a senior Chinese official made an unexpected pledge to halt the ivory trade inside the country, though it isn't clear how and when that ban might take effect.
Source: AP

WAZIRI MEMBE AMUAGA RASMI BALOZI WA HISPANIA ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza mbele ya Mabalazi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Hispania aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Luis Manuel Cuesta Civis.  Katika hotuba yake Mhe. Membe alimshukuru Balozi Luis kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Hispania. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Agosti, 2015.
Balozi Luis (kulia) kwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia ni Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (wa pili kulia), Balozi wa Zimbabwe na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kushoto) wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Balozi Luis akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiririkiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.

 KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

UVCCM SINGIDA YAMCHAGUA MSOMI FANCY NKUHI UBUNGE VITI MAALUM KUPITIA VIJANA

$
0
0
Na Hillary Shoo, SINGIDA.

MKUTANO Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida umemchagua, Fancy Nkuhi kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Viti maalum kupitia vijana.

Katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Singida Fancy mwenye Shahada ya pili ya mahusiano ya Kimataifa alipata jumla ya kura 21 huku mpinzani wake Jamila Kitila akiambulia kura 8.

Kwa mujibu wa Katibu wa UVCCM, Mkoa wa Singida Ramadhan Kapeto alisema umoja huo una jumla ya wajumbe 45 lakini waliohidhuria mkutano huo ni wajumbe 29 tu.

Hata hivyo Fancy atawakilisha Mkoa huo kwenye kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa kuwa Mbunge kupitia umoja huo na kupambana na wagombea kutoka mikoa mingine.

Kapeto alisema nafasi 10 zimegawanywa  kwa Zanzibar kuwa na  nafasi nne na Bara nafasi sita  za kuwakilisha Ubunge kupitia umoja huo.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku akisaidiwa na mchumi wa CCM Mkoa huo Ahmed Kaburu.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa singida kabla ya uchaguzi huo.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images