Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 928 | 929 | (Page 930) | 931 | 932 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii Cosato David Chumi ambaye ni afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akielekea jukwaani kuwashukuru wapiga kura wake baada ya kuibuka kidedea katika kura za maoni katika kugombea Ubunge jimbo jipya la Mafinga mjini mkoani Iringa kwenye hafla iliyofanyika katika uwanja wa Changarawe.  Jimbo hilo limemegwea kutoka iliyokuwa Mufindi Kaskazini na kata moja ya Bumilayinga toka Mufindi Kusini na kuwa Mafinga mjini
   Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii Cosato David Chumi akimwaga sera na kushukuru wapiga kura wake
  Matokeo rasmi katika kura za maoni Mafinga mjini

  0 0

  Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam.Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akizunguka kulibariki jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Francis Raphael Kitime kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi. Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akizunguka kulibariki jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Francis Raphael Kitime kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi.Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu. Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu.Mwanamuziki mkongwe na nguli nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime akitoa historia fupia ya marehemu baba yake mara baada ya ibada. Mwanamuziki mkongwe na nguli nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime akitoa historia fupia ya marehemu baba yake mara baada ya ibada. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (wa kwanza kushoto) akimsikiza Afisa Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu (UTTPID) Kilave Atenaka (wa pili kulia) wakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
  Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Masasi (kushoto) akimsikiliza Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla (katikati) wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambayo yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”. Wa kwanza kulia ni Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha Prosper Fivawo.
  Afisa wa hali ya Hewa kutoka Pemba Suleiman Ali Juma akiwafafanulia wanafunzi kutoka shule ya Masingi Tulieni kata ya Mnazi Mmoja Mkoani Lindi namna mamlaka ya hewa inavyofanya kazi zake kwa manufaa ya Wanzania kujua masuala ya hali ya hewa kila siku. Wwakati mkuu huyo wa wilaya alipotembelea banda la taasisi hiyo leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. Kauli mbiu ya Manesho ya Nane Nane mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.


  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifafanua jambo kwa umakini mbele ya waandishi wa habari  kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 
   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. 

   Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

   MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli, leo Jumanne Agosti 4, 2015  atawasili Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.
  Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, msafara wa Dk. Magufuli  kwenda kuchukua fomu hiyo, utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
  Nape amesema, msafara ambao utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshila Polisi.
  Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombeamwenza wake, Mhe. Samia Suluhu, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Dk. Magufuli alichaguliwa na Mkutano  Mku wa CCM uliofanyika Oktoba 11, 2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ally. 

  0 0

  Baada ya kura kutotosha kumfanya apite katika kura za maoni kugombea Ubunge kwa viti vya Vijana mkoani Tabora, Zahara Muhidin Issa Michuzi (pichani) amepokea matokeo kwa moyo mkunjufu na kumpongeza mshindi Irene Uwoya na kumuahidi ushirikiano katika mambo yote mema ya kuendeleza vijana mkoani humo.
  Zahara ambaye sasa ataelekeza nguvu zake katika kusaka digrii ya pili ya uchumi, amesema kwamba anawashukuru wajumbe wa mkutano wa uchaguzi, baba yake, mama walezi, kaka Mkala Fundikira wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kanda ya Magharibi na wana TBN wote wa ndani na nje ya nchi akiwemo kaka Jeff Msangi wa Canada na Mubelwa Bandio na DJ Luke wa Marekani, wanahabari wote wa makundi ya Whatsapp chini ya Francis Godwin na walimu wake pamoja  na wananchi wote kwa ujumla kwa kumpa heshima ya kumuunga mkono kwa kujitokeza kujaribu kuomba nafasi hiyo.
  Amesema kushindwa kwake hakumaanishi lolote zaidi ya kwamba demokrasia imechukua mkondo wake na aliyehitajika kuendeleza mapambano amepita na yeye hana kinyongo naye na ataendelea kuutumikia mkoa wa Tabora  katika nafasi yake ya mtu ambaye si kiongozi.
  Zahara ametoa mwito kwa wagombea wa nafasi zote kwamba kushindwa ni moja ya matokeo katika ushindani wowote hivyo ipo haja ya kujenga utamaduni wa kukubali matokeo bila ya hasira ama kinyongo kwani dunia i duara, na kwamba mlango mmoja ukifungwa kuna mwingine utafunguka.
  Amesema hana mpango wa kuhama CCM ambayo anaiamini kuwa ni chama ambacho kitaenzi na kutunza hadhi na mustakabali wa Taifa la Tanzania kuliko chama chochote.
  "Kushindwa kwangu kupata kura za kutosha sio mwisho wa dunia. Nina imani kwamba wapiga kura walijua wanachokifanya. Mimi ni nani kuwaoneshea kidole?  Maisha yaendelee kama kawaida na Mola awajaalie wote kwa yote" alisema.


  0 0

   Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik.
   Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik.
   Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.

   KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kusini, Ndandavala akipewa maelezo na Ofisa Uhusiano  Muandamizi  Salim Kimaro alipotembelea Banda la NSSF kwenye maonyesho ya Nananane.
  Afisa Uendeshaji Muandamizi Bi. Kabona Kandoro akitoa Maelezo ya faida mbambali kwa mmoja wa wakazi wa Lindi waliotembelea kwenye banda la NSSF.
  Mmoja wa watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakati wa maonyesho ya Nanenane mkoani Lindi.
  Wakazi wa Mkoa wa Lindi wakipata maelezo kuhusu mafao yanayotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea banda la NSSF kwenye Maonyesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.

  0 0

   Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Tanesco akitembelea miradi ya umeme wa gesi alisilia iliyogunduliwa Mtwala, katika kituo lilichojengwa na Kampuni ya mafuta ya Tanzania Petrolium Development Corpolation (TPDC) hii ni sehemu iliyojengwa ni kituo kikubwa cha kutunzia gesi ya kutengenezea umeme katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo. Ikiwa mhandisi wa kituo hicho amesema kuwa kituo hicho kipo tarari kutoa gesi asilia kwa Tanesco ili iweze kutengenezwa umeme.
   Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari katika katika ziara ya waziri wa nishati na madini George Simbachawene, kukagua miradi ya umeme wa gesi asilia katika kituo kikubwa cha kufikia gesi asilia kilichopo kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha kufikia gesi asilia inayotoka Mtwala ili iweze kutengeneza umeme kutokana na umeme wa maji kupungua kutokana na vyanzo vya maji vya mto Mtera na Kihansi kupungua maji kwaajili ya mabadiliko ya hali ya hewa.Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio.

   Meneja wa Kituo cha Umeme cha wa gesi asilia wa Tanesco, Mhandisi John Mageni akizungumza katika kituo cha umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelewa na waziri wa Nishati na madini,George Simbachawene.
  Baadhi ya mafundi wa kituo cha umeme wa asilia cha Tanesco akiendelea kufanya matengenezo katika kituo cha kufua umeme wa gesi asilia cha Kinyerezi jinini Dar es Salaam.
   Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


  0 0

  Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesikitishwa na kuhuzunishwa mno na kifo cha mmoja wa wanasiasa wa kongwe nchini, Mzee Peter Kisumo ambaye alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhaminiwa Chama cha CCM naaliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

  “Nimepokeakwamasikitikomakubwanahuzuninyingitaarifayakifo cha Mzee Peter Kisumoambayenimejulishwaaliagaduniajana, Jumatatu, Agosti 3, 2015, katikaHospitaliyaTaifaMuhimbili, Dar es Salaam, 
  ambakoalikuwaanapatiwamatibabuyafigo,”amesemaRaisKikwetekatikasalamuzakezarambirambikwafamiliayaMzeeKisumo. AmesemaRaisKikwete: “Kwahakika, kamataifa letu limeondokewa nakiongozi wa kupigwa mfano katika utumishi uliotukuka wa umma na Chama chetu cha Mapinduzi, na kabla ya hapo Chama cha TANU,ni MzeePeter Kisumo.

   Alikuwa mzalendo wa kweli. Alikuwa Mtanzania halisi ambaye hakusita kutetea maslahi ya taifa lake. Katika nafasi zote za uongozi wa taifa letu alizozishikilia – Ubunge, UkuuwaMkoa, Uwaziri, Udhaminiwa Chama Chetu – daimaalionyeshauongoziwakiwango cha juu. 

  Alikuwa mwadilifu na mwaminifu na wala hakusita kuyasemea kwanguvu zake zote na kuyatetea yale aliyoyaamini na yale yaliyohusu ustawi wanchiyetu.” Ameongeza Rais Kikwete: “Mzee Kisumo ametuacha wakiwa. 

  Tumeondokewa na Mzee hodaria mbaye busara zake na ulezi wake vilikuwa bado vinahitajika sana katika taifa letu kwanyakati za sasa. Tutamkumbuka daima.” 

  Katika salamu hizo kwa familia, Rais Kikwete amesema: “Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Mzee wetu.

   Huyu alikuwa Mzee wenu kama alivyokuwa Mzee wangu na Mzee wa taifa letu na hivyo msiba huu ni wakwetu sote. 

  Naungana nanyi katika majonzi na maombolezo. Kwapa moja tuna mwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

   Aidha, tunamwomba Mungu aiwe kapeponi roho ya Marehemu Mzee Peter Kisumo. Amen” 

  Imetolewana: KurugenziyaMawasilianoyaRais, Ikulu,
   DAR ES SALAAM. 4 Agosti, 2015

  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (wa nne kulia) akiwa ameshikana mikono na Mgombea wa Urais alieteuliwa na chama hicho, Mh. Edward Lowassa (wa tatu kulia) pamoja na Mgombea Mwenza wake, Mh. Dkt. Juma Haji Duni (mwenye suti nyeusi) pamoja na wanachama wapya wa Chama hicho, wakati wakitambulishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais alieteuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akimpongeza Mgombea wa Urais wa CHADEMA, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kupitishwa bila kupingwa na Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuwa Mgombea wa Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Katikati ni Mgombea Mwenza, Mh. Dkt. Juma Haji Duni.
   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
  0 0

   Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto)
  akichuana na mchezaji wa timu ya Simba Queens Mwanaidi Hamisi katika
  michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
  Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.
   Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Ilala Fatuma Salumu (Kushoto)
  akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Simba Queens Asha Abdul katika
  michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
  Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0.

  Mchezaji timu ya soka ya wasichana ya Simba Queens Eva Charles
  (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Ilala Fatuma Salumu katika
  michuano ya Airtel Rising Stars kwenye kiwanja cha kumbukumbu ya
  Karume jijini Dar es Salaam jana. Simba Queens walishinda 2 – 0
   
  Timu ya wasichana ya Simba Queens jana iliibuka na ushindi wa 2 – 0
  dhidi ya timu ya Ilala katika michuano ya vijana ya U-17 ya Airtel
  Rising Stars kwa mkoa wa kisoka wa Ilala. Mchezo huo ulipigwa katika
  uwanja wa kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam jana.

  Timu zilianza mchezo huo kwa kujihami na kushambuliana kwa kushtukiza.
  Simba Queens walifanikiwa kupata goli la mapema baada ya Zainab
  Mahmoud kuifungia timu yake katika dakika ya tano.

  Timu ya Ilala ilibadilika baada ya kuwa nyuma kwa goli moja na kuanza
  kushambulia kwa kasi. Lakini juhuhudi hizo hazikuzaa matunda na hadi
  mapumziko timu ya Simba Queens walikua wanaongoza kwa goli moja.

  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikicheza kwa
  umakini wa hali ya juu. Simba Queens waliongeza kasi na kufanikiwa
  kupata goli la pili katika dakika ya 46 kupitia kwa Khadija Ally baada
  ya kuachia shuti kali lililotinga wavuni moja kwa moja.

  Katika kiwanja cha Tanganyika Packers, Mburahati Queens iliichakaza
  Lulu Queens kwa magoli 2 -1. Wafungaji wa Mburahati Queens walikua ni
  Anne Adrea dakika ya 56 na Janeth Christopher dakika ya 90. 
  Wakati kwa upande wa Lulu walipata goli lao kupitia kwaOpah Clement dakika ya 46.Katika kiwanja cha Makangarawe Yombo Timu ya wavulana ya Wakati Ujaoilipata ushindi wa 2 -1 dhidi ya Dubu. 

  Kwa upande wa wasichana timu za
  Evergreen Queens na Temeke Queens zilienda sare ya bila kufungana.
  Michuano hii ya vijana ambayo kwa jiji la Dar es Salaam imeshaanza kwa
  takriban katika mikoa yake yote ya kimichezo, inafuatiliwa kwa karibu
  na jopo la makocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
  bila kusahau timu mbalimbali ambazo zinawanyatia kwa karibu vijana
  wenye vipaji kutoka michuano hiyo.

  Huu ni mwaka wa tano kwa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
  kuanzisha na kudhamini michuano hiyo ya Airtel Rising Stars yenye
  lengo la kutafuta na kuendeleza vipaji.

  Mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka huu yanajumuisha mikoa ya
  Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha ambapo
  fainali za taifa za michezo hiyo zimepagwa kupigwa jijini Dar es
  Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21.

  0 0

   Mwanachama akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Bi Rehema Mkamba
   Banda la Mfuko wa Pesheni wa LAPF ambalo lipo kwenye jengo la Ofisi ya waziri Mkuu, uwanja wa Nanenane, Dodoma
  Wanachama wakipata maelezo kuhusu bidhaa zinatolewa na LAPF ambazo ni uwezo wa kujichangia katika mfumo wa hiari, mkopo wa elimu, mkopo wa kujikimu, mkopo wa nyumba na fao la uzazi. 

  LAPF ni mfuko bora wa pensheni Tanzania pia umeshiriki Maonesho haya ya Nanenane 2015.LAPF ipo banda la ofisi za Waziri Mkuu TAMISEMI
  Katika banda hilo, LAPF tunatoa huduma zote za hifadhi ya jamii,kuu zikiwa ni;
  Elimu kwa umma kuhusu hifadhi ya jamii Tanzania yaani tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi.

  Tunaandikisha wanachama wapya wa hiari, wa kisheria na waajiri na kutoa vitambulisho hapohapo kwenye banda la LAPF
  Wanachama wanapata fursa ya kuona michango yao na ya mwajairi na kupata nakala inayo onyesha michango yao
  Tunajibu maswali ya wanachama, kupokea maoni ya wanachama na wananchi wote kwa ujumla.

  LAPF inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lao kujifunza kuhusu hifadhi ya jamii, kujiunga na kujionea huduma bora zilizo pelekea  LAPF kuzawadia tuzo ya mfuko bora na msimamizi na mdhibiti wa sekta  ya hifadhi ya jamii pia kupata tuzo ya kuwa mshindi wa kwanza kwa miaka mitano kwa utunzaji bora wa mahesabu ya mfuko
  Karibu sana banda la LAPF.

  0 0

    

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt  John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan wakionesha fomu zao za kuomba kugombea urais mara baada ya kuchukua kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es salaam leo, ambapo walisindikizwa na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla wakiwa wamepanda kwenye gari maalum.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan wakionesha mkoba wenye fomu za Kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho mbele ya wananchi  na wanachama wao nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais  leo agosti 4, 2015.
    Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wananchi na Wanachama wa chama hicho walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwashukuru Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM walioshiriki shughuli nzima ya kumsindikiza Dkt John Pombe Magufuli ya kuchukua fomu ya kuwania kiti cha Uraisi kupitia chama hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar leo.
   Mhe Samia Suluhu Hassan akiwashukuru Wananchi na Wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi nje ya ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi  leo agosti 4, 2015.
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan nwakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Uraisi leo agosti 4, 2015.
  Picha ya pamoja
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Taifa Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam,Ndugu Ramadhan Madabiba pamoja na pichani shoto Ndugu Januari Makamba aliyeshinda kura za maoni CCM jimbo la Bumbuli kwa pamoja wakimsindikiza Dkt Jonh Pombe Magufuli kuchukua fomu za kuwania Uraisi mapema leo jijini Dar. 
  Wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi Ndogo ya Makao ya CCM mtaa Lumbumba wakishangwekwa wakati Mgombea Mteule wa Urais kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akienda kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),jijini Dar leo.


  0 0  0 0

  Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias wakitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Australia Julai 29, 2015. 

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, akiwa na Mabalozi Macharia Kamau wa Kenya na David Donoghue wa Ireland wakati walipozungumza na waandishi wa habari kuelezea namna mchakato wa majadiliano yaliyokamilisha na hatimaye kupitishwa nan chi wanachama Tamko kuhusu Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015. Tamko hilo lilipitishwa jumapili usiku. Mabalozi wao ndio waliosimamia mchakato mzima wa majadiliano hayo.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, muda mfupi baada ya kuahirishwa mkutano kwa mapunziko mafupi hapo siku ya ijumaa usiku na kisha mkutano kuendelea tena hadi alfajiri ya Jumamosi, wakarejea tena mchana na kuendelea tena hadi usiku wa kuamkia jumapili na kuendelea jumpily mchana hadi usiku walilopitisha tamko hilo. Pamoja na naye Mkurungenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestin Mushy.
  Afisa Mkuu Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Bw.Songelael Shilla ambaye amekuwa akisimamia mchakato wa majadiliano yaliyopelekea kupatika kwa ajenda mpya za maendeleo endelevu baada ya 2015, aliyeketi nyuma ni Dk. Lorah Madete kutoka Tume ya Mipango hii ilikuwa ni Ijumaa usiku.

  Baaada ya  majadiliano  makali yaliyodumu kwa wiki mbili  na wakati mwingine wajumbe  kulazimika kukesha hadi asubuhi. Hatimaye nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa,     Jumapili   usiku (Agosti mbili), wamepitisha kwa kauli moja,  rasimu ya  tamko kuhusu  Agenda ya  Malengo ya Maendeleo  Endelevu  2015.

   Katika kuhakikisha kwamba  ilikuwa ni lazima  tamko hilo likamilike na kupitishwa,  wajumbe walilazimika kukesha ndani ya  ukumbi wa mkutano  kulikokuwa kukifanyika  mkutano huo,  wakipimzika  kwa saa chache na kurejea tena na hatimaye kufanikisha kukamilishwa kwa raslimu hiyo siku ya jumapili majira ya usiku.

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na  Mwakilishi wa Kudumu Balozi Tuvako  Manongi na Afisa Mkuu  Bw. Shilla,  kwa kushirikiana  na    wataalamu  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,   wakiongozwa na Mkurugenzi wa  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Celestin Mushy,  Wataalamu kutoka  Tume ya  Rais Mipango,  Tanzania   Bara na Visiwani,   Wizara ya Fedha na  Asasi zisizo za Kiserikali,  imeshiriki kikamilifu katika  kipindi chote  miaka miwili  tangu kuanza kwa  mchakato wa majadiliano  hayo.

  Tamko lilolopitishwa  i   Jumapili,   itawasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika  tarehe  itakayopangwa   kupitishwa   rasmi.

  Viongozi Wakuu wa Nchi na  Serikali watapokea na  kupitisha tamko hilo katika mkutano wao   wa Kihistoria utakaofanyika mwezi  ujao (  25-27Septemba) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

  Akionyesha kufurahishwa na kuridhika kwake baada ya  wajumbe  kupitisha tamko hilo  , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, licha ya kuwapongeza wajumbe kwa kazi kubwa , kujituma kwao na zaidi kupitisha  rasimu hiyo kwa kauli moja,  amesema  anasubiri kwa hamu kuungana na Viongozi  Wakuu wa  Nchi na Serikali  zaidi ya 150 na  wawakilishi wengine katika mkutano  wa kilele utakaopitisha  za ajenda hizo za maendeleo endelevu kwa miaka 15 ijayo.

  Akasema   mchakato mzima wa majadiliano ya maandalizi ya  tamko hilo ambao umedumu  kwa miaka miwili   umefanyika kwa   mshikamano,  weledi na ulikuwa shirikishi , ambapo hata makundi mbalimbali ya kijamii,  yalishiriki kwa ukamilifu.

  Ban Ki  Moon, amesema,  ajenda mpya za maendeleo endelevu ambazo zinachukua nafasi ya  Malengo ya  Maendeleo ya Millenia  yanayofikia ukingoni mwaka huu, zinalenga katika kuwaondoa watu kutoka  katika  lindi la umaskini  pasipo kumwacha  yeyote.

  “Napenda kuwapongeza nchi wanachama kwa uongozi wenu na kujituma kwenu, nawashukuru pia Mabalozi   Macharia Kamau  wa Kenya na   David Donoghue wa Ireland  kwa namna   walivyoendesha na kuusimamia mchakato huo bila  kuchoka na kwa kuonyesha  ufundi mkubwa  wa  kidiplomasia ” amesema Ban  Ki Moon.

   Na kuongeza kwamba Ajenda hiyo iitwayo: "kubadili dunia yetu: ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu" inajumuisha masuala yanayowahusu wote ikilenga pia kuhakikisha Amani, ufanisi na kubuni ubia unaojali watu na sayari duni.

  0 0

  WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami,hayo yalisemwa Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha Mlata (Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba.

  Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.

  Hata hivyo ahadi ya Magufuli imetekelezwa kwa kuwa sasa barabara yote kuanzia Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.

  Serikali ya awamu ya nne imetimiza ahadi ya wananchi ya kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Bukoba imetekelezwa kwa asilimia mia moja (100%).

  0 0


  Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

older | 1 | .... | 928 | 929 | (Page 930) | 931 | 932 | .... | 3272 | newer