Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 927 | 928 | (Page 929) | 930 | 931 | .... | 3284 | newer

  0 0


  ????????????????????????????????????
  Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT pamoja na maaskofu wenzake wakiombea albam hizo kabla ya kuzizindua rasmi kushoto ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kamuni ya Msama Promotion.
  ????????????????????????????????????
  Askofu na Dokta Mwakibolwa wa EAGT akizindua rasmi albam hizo kushoto Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
  ????????????????????????????????????
  Maaskofu na wachungaji wakiwa wameshikilia albam zao mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion.

  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya maaskofu na wachungaji waliohudhuria katika uzinduzi huo wakifuatilia wakati mwimbaji huyo akiimba jukwaani.
  ????????????????????????????????????
  Mwimbaji nguli wa muziki wa injili Bonny Mwaitege akiimba katika uzinduzi wa albam zake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na maelefu ya wapenzi wa muziki wa ijini akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa muziki huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya kwaya kutoka katika baadhi ya makanisa ya jijini Dar es salaam, Bonny Mwaitege alikonga nyoyo za mashabiki wake kwa ikwango kikubwa huku akiwa amevalia vazi la Kinigeria wakati akiwa jukwaani, wapenzi wa muziki waliohudhuria katika uzinduzi huo walijikuta kila mmoja akijitikisa pale alipo kutokana na kuvutiwa na nyimbo za mwimbaji huyo kutoka mkoani mbeya
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya wapenzi wa muziki wa injili wakiwa katika uzinduzi huo.


  0 0

  Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
  Wanafunzi shule Darasa la nne Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
  Wahitimu wa masomo ya awali shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wa Shule wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam
  Wanafunzi wa Darasa la awali Shule ya Kimataifa ya Joyland, wakiimba wimbo wakati wa mahafali ya pili ya shule hiyo iliyopo Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam


  0 0

  Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akisikiliza kwa makini taarifa fupi iliyosomwa mbele yake na Afisa mkuu wa ubalozi wa Ghana hapa Tanzania Dr. Ken Kwaku kuhusiana na utendaji kazi wa Ecobank nchini Ghana na bara la Afrika kwa ujumla na kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa kibiashara kati ya Ghana na Tanzania. (Katikati) ni Balozi wa Ghana nchini Kenya Mhe. Karim. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
  (Wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa Ecobank nchini Tanzania Mr. Enoch Osei-Safo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea kuhusiana na mikakati ya kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania kupitia benki hiyo. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
  Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwaalika katika siku tatu za mkutano wa uamsho utakaofanyika hapa Washington DC.
  Ni kati ya Agosti 14-16 2015

  Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji alipohudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya Jumapili 07/07/2013 katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES

  0 0

  The U.S. Agency for International Development (USAID) recently announced support of the Government of Tanzania’s Results Based Financing (RBF) Initiative in the health sector through a $49 million grant. 

  Through a single donor trust fund administered by the World Bank, Tanzania will receive $49 million over the next five years. Tanzania’s RBF Initiative aims to improve the quality of primary health care services in Tanzania, with a focus on maternal, neonatal, and child health services. 

  RBF priorities in achieving results, greater value for money, and efficiencies, will help secure Tanzania’s domestic resources and ensure long-term security in the country’s health sector. 

  As a result of the $49 million USAID grant, the Ministry of Finance increased its loan allocation to the health sector by an additional $100 million. In response to this financial commitment from the Government of Tanzania, U.S. Ambassador Mark B. Childress stated, “In alignment with Big Results Now, this initiative will strengthen the quality and sustainability of health services in Tanzania.” 

  The $49 million will support the Government of Tanzania’s plans to increase access to high quality health care services, which includes rolling out a facility accreditation scheme, improving the distribution of skilled health care workers to regions with critical shortages, and enhancing community-based health interventions. 

  As part of this scheme, the Medical Stores Department will also receive performance-based payments to increase the availability of essential medicines. USAID will also support its partners to provide technical assistance at national, district, and facility levels.

  To request more information about this announcement, please email Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Senior Information Specialist at U.S. Embassy Dar es Salaam.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Saud Arabia, Hemed Mgaza, wakati alipofika kumuaga Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 3, 2015. Balozi Mgaza anakwenda nchini Saud Arabia, kuanza kazi rasmi baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete. Picha na OMR.

  0 0
 • 08/03/15--05:47: FOD YAPANIA MAKUBWA
 • Kundi linaloundwa na wasanii wa filamu,wanamuziki na wanamichezo kwa ajili ya kusukuma gurudumu la  maendeleo yao na taifa kiujumla la Friends of Developments(F.O.D), limepania kufanya mengi makubwa kulisimamia jina lao la “Rafiki wa Maendeleo” kwa kufanya kazi za kijamii zikiwemo kusaidia wasiojiweza, kwa kujitolea na kufanya matamasha mbalimbali mfululizo na hasa kipindi hiki cha uchaguzi.

  Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa FOD na pia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE “Bigright” amesema – FOD inayoongozwa na Rashid Nasor “chidy mzee wa mbele” recho na Crama tayari imeshajikusanyia wanachama zaidi ya milioni tatu  wengi wakiwemo,wanafunzi wa vyuo,  viongozi wa chama na serikali wazee kwa vijana.

  Kwa kuwa FOD yenyewe ina simamia zaidi maendeleo , na kipindi hiki ni cha uchaguzi  ikaweka muswada wa kumsapoti kiongozi wanayeona atawaletea maendeleo na ambaye tayari amekwisha fanya mengi yaliyoonekana ambaye ni John Pombe Magufuli.

  FOD  imedhamiria kwa dhati itajituma kila kona ya Tanzania kuhakikisha magufuli anakuwa madarakani washirikiane nae katika kulisukuma hilo gurudumu la kuleta maendeleo .

  0 0

  Mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya akifanya manjonjo yake wakati wa onyesho la East Africa Vibes Concert (EAVC) 2015 lililofanyika siku ya Jumamosi pale Nafasi Art Space, jijini Da res Salaam
  Mshairi Neema Komba, kutoka La poetista akifannya ushairi wake wakati wa onyesho la East Africa Vibes Concert (EAVC) 2015, lililofanyika siku ya Jumamosi pale Nafasi Art Space, jijini Da res Salaam
  Grace Matata, akitumbuiza wakati wa onyesho la East Africa Vibes Concert (EAVC) 2015, lililofanyika siku ya Jumamosi pale Nafasi Art Space, jijini Da res Salaam.


  0 0

  Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akipokea fomu ya kugombea urais kutoka kwa Afisa Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adam Nyando katika ofisi za NEC leo jijini Dar es Salaam.
  Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA nje ya ofisi NEC leo jijini Dar es Salaam. (Pichana Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)  Na Chalila Kibuda, Globuya Jamii.
   MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe amechukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema watanzania kama wanahitaji maendeleo wachague chama hicho na sio kuchagua watu wanaotaka kutumikia matumbo yao. Amesema zoezi la kuchukua fomu za urais ziko wazi na kutufanya wagombea kuwa huru katika zoezi zima kutoka na maandalizi yalifanywa na tume ys Taifs ys Uchaguzi.

  Rungwe amesema mwaka 2015 aligombea kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi lakini kura hazikutosha na kufanikiwa kupata wabunge wawili kwa tiketi kwa chama hicho. Amesema ana uwezo wa kuwatumikia watanzania na sio kwenda Ikulu kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kujinufaisha na kuwaacha watu walionipa ridhaa ya kuwaletea maendeleo.

  Aidha amesema nafasi ya urais sio ya mchezo kutoka na na kuwa majukumu makubwa ya kuwatumikia watu katika kuwapa maendeleo yatayotokana nafasi hiyo.

   “Nina imani watanzania wataichaugua CHAUMA katika kuperusha bendera katika kuweza kupata maendeleo kama kauli mbiu ya chama kutaka ukombozi” anasema Rungwe. Vyama vilivyochukua fomu ya urais vimefikia vinnea mbavyo ni, Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), UPDP, Chama cha Democratic Party (DP), pamoja na Chauma.

  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli anatarajia kuchukua fomu kesho katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dar es Salaam. mwisho

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Injini Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao na wafanyabiashara hao kilichokuwa na lengo la kuwapatia ufahamu juu ya masuala ya manunuzi.
  Bwana Nixson Mlumba – AfisaManunuzi wa ACACIA akifafanua jambo wakati wa Kikao hicho
  Baadhi ya Wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini maelezo ya kutoka kwa Uongozi wa Kampuni ya Acacia wakati wa Kikao hicho.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Na Jeff Msangi 
  wa TBN Ughaibuni
  Nyota njema huonekana asubuhi. Bila shaka umewahi kusikia msemo huu. Kwa Zahara Muhidini Issa Michuzi, nyota yake njema ni tunu ya uongozi. Tangu alipoweza kutambua maana na tofauti ya jambo jema na baya, amekuwa kiongozi.
  Muhtasari wa maisha yake unaonyesha alizaliwa mnano tarehe 2 Septemba mwaka 1987 Nzega mkoani Tabora. Amesomea katika shule zifuatazo;

  *Shule Ya Msingi Rufita, Tabora- 1995-2001

  *Shule Ya Sekondari Kazima, Tabora-2002-2005

  *Shule Ya Sekondari Ya Juu Emma, Kampala-Uganda 2007-2009

  *Chuo Kikuu Cha Dodoma, Dodoma,Tanzania 2011-2014.


  Zahara Muhidini Issa Michuzi, ambaye ni binti wa Ankal, ni mhitimu wa Shahada ya Sanaa katika masuala ya Uchumi. Mpaka kufikia hapa alipo, nyota yake ya uongozi imejidhihirisha katika sehemu mbalimbali alizopitia hususani shule.

  Amekuwa kiranja, msimamizi  wa shughuli na miradi mbalimbali shuleni na alipokuwa Chuo Kikuu Dodoma alikuwa kiongozi katika Jumuiya ya Wanafunzi- University of  Dodoma Students Organization (UDOSO) akiwa kama Mbunge wa Baraza La Wanafunzi.

  Mbali ya uzoefu wa kiuongozi alionao, Zahara anazo sifa zifuatazo ambazo ni nadra na tunu kubwa katika uongozi;

  Anajitambua- Zahara anajitambua vilivyo. Anatambua kwamba uongozi ni heshima na utumishi uliotukuka.

  Ana Ari Ya Kuongoza na 
  Kujifunza- Zahara anaamini kwamba kiongozi bora lazima awe ana ari ya kuongoza na kutumikia wananchi anaowaongoza. Mbali ya kuongoza,kiongozi lazima awe tayari kujifunza kutokana na hali halisi na kukabiliana na mabadiliko ya aina yoyote yanayoweza kujitokeza.

  Ni Msikivu Na Ana uwezo Mkubwa wa Kufanya Kazi na Watu- Hili Zahara amelithibitisha katika ngazi zote za kiuongozi ambazo amepitia. Usikivu wake umekuwa chachu ya kumwezesha kutatua matatizo mbalimbali ambayo amekabiliana nayo huku yeye kama kiongozi akitarajiwa kuyatatua.

  Ana Uwezo Wa Kuongoza Mabadiliko Ya Kijamii- Zahara anaamini kwa vitendo kwamba jamii yoyote lazima isonge mbele ili kwenda sambamba na mabadiliko mbalimbali ya kijamii. Anaamini kwa vitendo kwamba uongozi thabiti unahitajika ili kuleta mabadiliko chanya ambayo jamii yoyote inahitaji. 
  Zahara Muhidini Issa Michuzi hivi sasa anagombea kuwa mwakilishi wa vijana Bungeni kupitia Viti Maalumu Vijana (Youth Seats) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)- Tabora. Anaomba Kura na Ushirikiano Wako.


   Ankal akifurahi na binti yake Zahara siku ya Maulid maalumu ya kusherehekea kuhitimu digrii ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka jana. Hii ndiyo siku ambayo Zahara aliweka nia hadharani kwamba angependa kugombea Ubunge mkoani TABORA  ili kumuenzi marehemu mama yake kwa kuwatumikia wananchi wa mkoa huo kwa moyo wake wote.
  Zahara akifurahi na Mama yake mlezi
   Zahara akiwa na dada zake
   Zahara akiwa na familia yake
   Zahara akiwa na baba yake mzazi, Ankal
   Zahara akiwa na baba yake na Mama yake Mlezi ambaye ni dada wa marehemu mama yake, Bi Rehema Saidi
  Zahara akiwa na baba na wadogo zake.


         


  0 0


  0 0
 • 08/03/15--12:37: introducing bona productions
 • KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO TUMEKUWA TUNA VIDEO MOVIES, CONFERENCE NA DOCUMENTARY, SASA TUNAPANUA BIASHARA MPAKA KWENYE SHEREHE.
  KWA MAHITAJI YAKO YA VIDEO SHOOTING YA HARUSI, SEND-OFF, KITCHEN PARTY, GRADUATION, WASILIANA NASI, TEL - NOELA 0715 432 310
  KARIBUNI SANA.

  0 0


  Zahara Muhidin Michuzi akiwa nje ya ukumbi wa uchaguzi mapema leo.
  Na Mkala Fundikira wa 
  TBN kanda ya Magharibi
  Leo hii mchana binti ya mpiga picha na blogger maarufu nchini Muhidin Issa Michuzi Bi Zahara Michuzi alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

  Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo  na kusema :
  "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote. Pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha kwani mgombea  mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. 
  Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

  Awali mgeni rasmi wa mkitano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. 
  Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea? 
  Waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? 
  Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. 
  Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.
  Zahara Michuzi akiwa na wagombea wenzie Mariam katikati na Irene kulia
  Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
  Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3
  Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.
  Bi Mariam Amir katibu wa UVCCM mkoa wa Tabora akisoma tamko la kuunga mkono na kupongeza kuchaguliwa Bw John Magufuli kuwa mgombea urais wa Jamhuhuri ya muungano wa Tanzania.
  Katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tabora Bibi Janeth Kayanda akisalimia wajumbe leo hii mapema.
  Mwenyekiti mstaafu UVCCM wilaya ya Tabora mjini Nassor Wazambi akifuatilia mchakato.
  Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
  Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora Bw Seif Gulama (Kazuge) akitoa yake machache.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Mzee Hassan Wakasuvi akihutubia mkutano huo.
  Sunday Kabaye akiwa amebeba sanduku la kura mara baada ya kura hizo kuhesabiwa nyuma akifuatiwa na Irene Uwoya na Zahara Michuzi.
  Irene Uwoya akitokwa machozi kabla ya kutangazwa mshindi
  Kada wa CCM Jaha Kaducha kushoto akiwa na Mwalimu Nassoro Wazambi.
  Msimamizi wa uchaguzi Bw Mwambeleko akisoma matokeo ya uchguzi huo leo mchana mijini Tabora
  Team Irene wakifuatilia mchakato


  0 0

  Na Profesa Mbele
  Jana, tarehe 1 Agosti, tamasha la Afrifest lilifanyika mjini Brooklyn Park, Minnesota. 
  Hili ni tamasha ambalo huandaliwa mara moja kwa mwaka na bodi ya Afrifest Foundation ambayo mimi ni mwenyekiti wake. ili kuwakutanisha wa-Afrika, watu wenye asili ya Afrika waishio Marekani ya Kaskazini, Kati, na Kusini, pamoja na Caribbean, na pia watu wa mataifa mengine. Lengo kubwa ni kufahamiana, kuelimisha, na kuuenzi mchango wa watu weusi duniani kote, katika nyanja mbali mbali. 

  Hiyo jana ilikuwa ni mara ya kwanza kwa bendera ya Tanzania kupepea kwenye tamasha la Afrifest. Baada ya kushiriki matamasha na kujionea wenzetu wanavyotumia fursa kuzitangaza nchi zao, nilijiuliza kwa nini nisitafute bendera ya Tanzania, kama nilivyoeleza katika blogu hii.

  Hatimaye, nilifanya uamuzi wa kununua bendera, niwe ninaipeperusha kwenye matamasha ninayoshiriki, maadam fursa zipo. Hapo kushoto naonekana na binti zangu Assumpta na Zawadi kwenye meza yetu, hiyo jana.

  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Wapendwa Watanzania na marafiki popote pale duniani,

  Kwa niaba ya uongozi wa Tanzania Global Prayer Movement (TGPM) natoa shukrani za dhati kwa wale wote waliojiunga nasi kwenye maombi ya Jumapili hii na siku zote kuanzia Jumapili July 26 tukiombea utakaso wa kiti cha Raisi, Ikulu, viti vya wabunge na madiwani pamoja na amani wakati vyama vinajipanga sawa sawa na uchaguzi.

  Yafuatayo ndiyo tunayoendelea kuombea mpaka siku ya Jumapili Agosti 9 ambapo itakuwa hitimisho la wiki tatu kuombea haya maswala. Endelea kuinua jina la Bwana.

  1)   Omba Mungu akupe mzigo wa kuombea nchi yako ya Tanzania.
  2)   Ombea amani nchini wakati vyama vinakamilisha uchaguzi wa wagombea wao wa nafasi ya Raisi.
  3)   Ombea utakaso wa Kiti cha Uraisi wa Tanzania.
  4)   Ombea utakaso wa Ikulu ikiwa ni mahali anapofanyia kazi Raisi wa Tanzania, pamoja na ikulu ndogo mikoani.
  5)   Ombea utakaso wa viti vya wabunge na madiwani nchi nzima.
  6)   Ombea mgombea Uraisi wa UKAWA kama jina litakuwa limetoka. Kama bado, tutaendelea kuombea amani huku mchakachuo ukiendelea.


  Please join us via a prayer conference call this Sunday. To join the conference call every Sunday, please dial (218) 895 9661 and passcode is 222555.  The prayer starts at 9pm Eastern, 8pm central, 7pm Mountain or 6pm Pacific time.

  For more information about Tanzania Global Prayer Movement (TGPM), please visit our website at:

  0 0

   Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama
  FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
  Bendi hiyo yenye makao yake nchini Ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki mahiri Ebrahim Makunja aka  Kamanda Ras Makunja,imejizolea umaarufu wa kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa "Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.
  Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo"
  yenye mbili za kumuaga Rais JK.
  Unaweza kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au uungana nao at www.facebook.com/ngomaafricaband
   Gwaride limenoga Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
   Mashabiki wa Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 
   Mambo ya Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. 


  0 0

   Wananchi wa Jimbo la Ukonga wakiwa nyumbani kwa mgombea ubunge wa jimbo hilo aliyeibuka kidedea, Jerry Silaa.
  Mgombea Jerry Silaa akishukuru wapiga kura baada ya kuibuka kidedea kwa kupata kura 10,382 huku mshindani wake PATEL Ramesh akipata kura 7355. 
  Mgombea ubunge huyo aliwashukuru wananchi na wanaCCM waliokwenda nyumbani kumpongeza na kuwapongeza wagombea wenzake wote,na kuongeza kuwa wiki moja waliyokuwa pamoja amejifunza mengi, anaamini watashirikiana kufanikisha Ushindi wa CCM October 25.

  0 0

  Na Bashir Yakub
  Sheria  ya  Uwekezaji  ya  Mwaka  1977 imehamasisha  uwekezaji  kwa  wazawa  na  wasio  wazawa  kwa  kuweka  mazingira  rafiki  kwa  wajasiriamali katika  nyanja  zote.  Wapo  ambao  wanajua fursa hizi  na wamezitumia   kujipatia  maendeleo  na  wapo  ambao  hawajatumia  fursa  hizi.  Nataka  niseme  kitu  kimoja  kuwa  wazawa  wengi  wameshindwa  kufanikiwa  kwa  kutojua  uwepo wa fursa. Wengi  wangependa  kutumia  fursa   kama  zipo  lakini  hawajui ziko  wapi na  zinapatikana vipi.
  Badala  yake  wageni  na  watu  wengine  ambao  si  wenye  asili  halisi  ya  Tanzania  ndio  wamekuwa  wakihabarishana  kuhusu  fursa  hizi  wanazitumia  na  wanafanikiwa sana.  Wenyeji  halisi   wa  nchi  hii  wanabaki  kutazama  mafanikio  ya  watu  hawa  wasijue  yanapatikanaje. 
  Ziko  fursa  ambazo  zimetolewa  na  serikali  na  kuainishwa  na  sheria  mbalimbali  mojawapo  ikiwa  hii  ya  kusamehewa  kodi  kwa bidhaa  zinazoingizwa  nchini  kutoka  nje  ya  nchi. 
  Wafanyabiashara  watakubaliana  na  mimi  kuwa  ikiwa  utapata  msamaha mzuri  wa  kodi bandarini  basi  unayo  nafasi  kubwa  ya  kutengeneza  faida  kubwa  katika  biashara  yoyote  utakayoamua  kufanya.


  Mara  zote  kodi  ndio  huwa  tatizo. Makala  haya yataeleza  namna  ya  kupata  msamaha  wa  kodi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia mamia ya wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza katika mkutano mkubwa wa hadhara ambapo aliwaaga rasmi na kumpa zawadi mbalimbali jana  jioni 

   Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoa wa Tanga wakiandamana wakati wa sherehe za maadhimisho  ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua stika maalumu zing’aazo zitakazosaidia kupunguza ajali kwakuwa magari makubwa yataonekana kwa mbali na waendesha gari wengine hivyo kuepisha magari kugongana.kulia ni Kamanda Mkuu wa Usalma Barabarani kitaifa Mohamed Mpinga.
   Askari wa kikosi cha usalama barabarani akimuonesha Rais Kikwete kidhibiti mwendo cha magari maarufu kama tochi wakati Rais liapotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa wiki ya usalama barabarani ilkiyofanyika kitaifa mkoani Tanga
  Mtoto wa shule ya msingi mjini Tanga Doreen John akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya barabara kwa Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipotembelea mabanda kadhaa ya maonyesho katika viwanja vya Tangamano,mjini Tanga wakati wa maadhimisho ya sherehe ya wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika mkoani Tanga.Picha na Freddy Maro

older | 1 | .... | 927 | 928 | (Page 929) | 930 | 931 | .... | 3284 | newer