Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 926 | 927 | (Page 928) | 929 | 930 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) inashiriki kwenye maonesho ya Nananane ambayo Kitaifa yanafanyika kwenye viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
  Katika maonesho hayo ambayo yanabebwa na Kauli Mbiu ya Matokeo Makubwa Sasa: Tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya  kilimo na ufugaji , NSSF itakuwa ikitoa huduma mbalimbali zikiwemo elimu juu ya scheme zake za Wakulima na Wavuvi, kuandikisha wanachama wapya, kutoa taarifa za michango  na kutoa elimu ya mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF kama vile matibabu, kuumia kazini, uzazi, pensheni ya uzee,ulemavu na urithi.


  Kauli mbiu ya mwaka huu inaendana sana na azma ya NSSF kuwafikia wakulima,wafugaji na watu wengine wasio katika ajira rasmi kujiunga na mfuko huo na kupata mafao yote saba sawa na walio katika ajira rasmi.Aidha Shirika limeshaandikisha wanachama zaidi ya elfu sabini kutoka katika sekta isiyo rasmi na malengo ni kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.

  NSSF inawakaribisha wakazi wa Lindi na Mtwara kwenye Banda lao ili waweze kupata huduma hizi kwa ajili ya kuboresha maisha yao na familia zao.

  Kaimu Meneja wa Mkoa wa Lindi Kabonwa Kandoro (kulia) akimpa maelezo mwanachama juu ya mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF wakati Afisa Uandikishaji  Tuli Mwaipopo akichukua taarifa za mwanachama mwengine kwa Lengo la Kumtengenezea kadi mpya ya NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi. 
  Kaimu Meneja Mkoa wa Lindi Kabonwa Kandoro akitoa maelezo kwa mmoja wa wanachama wa NSSF waliotembelea kwenye Banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane.

   Afisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro akimpa maelezo mmoja wa watu waliofika kwenye Banda la NSSF kwenye maonesho ya Nanenane Lindi.

  Afisa Teknohama, Rukia Penza akimpata taarifa za michango yake mmoja wa wanachama aliyetembelea kwenye Banda la NSSF.

  Afisa Uandikishaji wa NSSF Mkoa wa Lindi Tuli Mwaipopo akichukua taarifa za Mwanachama kwa ajili ya kutengeneza kadi mpya ya mwanachama huyo.


  0 0

  Je wafahamu dondoo za uchaguzi ndani ya CCM baada ya kura za maoni kufanyika hapo jana? Tazama hapa uhabarike.http://youtu.be/DbBqKA5GXSg
  JE kimejiri nini kura za maoni ndani ya CCM? Furahia habari hizo na nyingine nyingi kupitia uchambuzi wa magazeti asubuhi ya leo.https://youtu.be/jzv-j7hplpM
  Je wafamu ni habari gani za michezo zimepewa kipaumbele katika magazeti ya leo? Furahia uchambuzi hapa.http://youtu.be/ODCb6JtJHAQ 

  0 0

  Vijana mkoani Dar es Salaam na nchini kwa ujumla wametakiwa kujiamini na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kupiga vita tatizo la ajira ili kukukuza vipato vyao na kuchangia ukuaji wa pato la taifa. 
   Akizindua Programu ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake ijulikanayo kama Kijana Jiajiri, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiq amesema vijana hawana budi kuonyesha juhudi na hamu ya kufanikiwa katika nyanja tofauti. 
   Kijana Jiajiri ni program ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania wenye umri wa miaka 18-35. Inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). 
   “Msikubali kuona ndoto zenu zinatoweka…mpambane huku mkijituma na kutumia fursa zilizopo kukuza vipato vyenu,” alisema katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Paul Makonda mwishoni mwa juma. 
   Aliwataka vijana hao kujitambua na kuyafanyia kazi mafunzo watakayopata kupitia program hiyo. Aliwasisitiza vijana kutokubali historia ya umasikini wa familia zao, bali wajitume na kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na hali hiyo. Akifafanua kuhusu mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa alisema mafunzo hayo ya wiki sita yanawalenga vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake ili kuwaptia elimu ya ujasiriamali. “Hii ni programu ya kitaifa na mafunzo haya ni ya bure,” alisema na kueleza kuwa inaanza na mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam na kuwa baada ya mwaka mmoja mpango huu utapanuka kufikia mikoa mingine. 
   Program hiyo inadhaminiwa kwa ushirikiano wa makampuni matano ya kimataifa yanayojishughulisha na mafuta na gesi asilia hapa nchini ambayo ni BG, Statoil, ExxonMobil, Ophir na Pavilion Energy. 
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda akifafanua jambo alipokuwa akizindua Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki.  Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa na Meneja wa Maswala ya Nje wa Tanzania LNG Plant Project, Bi. Patricia Mhondo ambao ndio wafadhili wa programu hiyo.  Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.

   Baadhi ya vijana wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki. Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki.  Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda na Meneja wa Maswala ya Nje wa Tanzania LNG Plant Project, Bi. Patricia Mhondo ambao ndio wafadhili wa programu hiyo.  Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.


  0 0

  Watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam wametakiwa kuongeza kasi ya utumiaji wa mifumo wa kiiletroniki kulipia huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuondoa usheleweshaji wa uondoaji wa mizigo. Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga amesema matumizi sahihi ya njia za kielektroniki yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza ufanisi wa kazi katika bandari hiyo. 
   Akiongeana na waandishi wa habari baada mkutano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wake jijini hapa mwishoni mwa wiki, Bw. Mhanga alisema wakati sasa umefika kwa wadau wa bandari kuzoea matumizi ya kielektroniki hasa katika malipo. 
   “Hapo ndipo tulipofika, dunia iko hapo...lazima tuendane na mabadiliko haya na kuleta tija katika kazi zetu wote,” alisema. 
   Akisisitiza matumizi ya kielektroniki alisema mbali ya kuleta ufanisi, kazi zinafanyikakwa uwazi zaidi na kuziba mianya ya ubadhirifu. 
   “Kwa sasa wateja wetu wanaweza kufanya malipo kupitia taratibu zilizoelezwa kwenye tovuti ya TPA na pia wanaweza kulipia kwa njia ya mitandao ya simu,” alisema. 
   Alifafanua kuwa kwa sasa hakuna sababu ya mteja kwenda bandarini kufanya malipo, bali mifumo hiyo inawezesha kulipia mahali mteja alipo na kwenda moja kwa moja eneo la kutolewa mzigo. Akizungumzia hatua nyingine za kuboresha utendaji kazi bandarini hapo alisema swala la kufanya kazi masaa 24 linazidi kuimarika. 
   “Kulikuwa na tatizo kwa baadhi ya benki lakini sasa wapo tayari kufanya kazi kwa muda huo,” aliongeza kusema. 
   Akitoamfano alisema benki ya NMB wapo tayari kufanya kazi kwa masaa hayo na kuwa benki nyingine wameongeza muda wa kazi hadi saa mbili usiku na hata kuongeza muda zaidi kulingana na mahitaji ya wateja. 
   Kwa upande wake, meneja wa forodha bandarini hapo, Bw. Wolfgang Salia alisema upo umuhimu wa haraka wakuwa na miundombinu bora ya barabara na reli ili kuimarisha zaidi huduma. 
   Mkurugenzi wa huduma za meli na bandari wa taasisi ya Intergovernmental Standing Committee on Shipping (ISCOS), Bw. Clement William alisema ufanisi pekee ndilo jambo litakaloifanya bandari ya Dar es Salaam kuvutia wateja. Bandari ipo katika mkakati mkubwa wa kupanua huduma na kuleta ufanisi na mikutano hiyo ya wadau imekuwa nimoja ya njia za kufanikisha azma hiyo.
   Baadhi ya wadau wa bandari ya Dar es Salaam wakiwa katika kikao cha pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kujadili maswala mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za bandari hapa nchini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam (kushoto), Bw.Hebel Mhanga akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wadau wa mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kulia ni mkuu wa Usafiri na Miundombinu, Ofisi ya Rais, Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Joy Mwalugaja.

  Mkuu wa Usafiri na Miundombinu, Ofisi ya Rais, Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Joy  Mwalugaja akiongea katika kikao hicho

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumbani kwake Segerea mwisho, wakati akitangaza kujiondoa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumapili Agosti 2, 2015.

  0 0

   MCHAKATO wa kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa CCM Zanzibar watakaowania nafasi za  Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawawakilishi (BLW) na Udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, uliofanyhika jana (Agosti 01, 2015) mikoani mote.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Afisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, imesema kuwa matokeo ya kinyang’anyiro hicho, yameoonyesha baadhi ya vigogo waliokuwa wakitegemewa kuibuka na ushindi wameanguka vibaya katika kura hizo za maoni zilizofanyika katika matawi mbali mbali ya majimbo yote 50 ya Zanzibar.

  Vigogo walioibuka na ushindi na kuwa na nafasi nzuri  ya kuwa Wabunge au Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na waziri Kiongozi (Mst.) wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mhe. Shamsi Vuai Nahodha.

  Wengine wa nafasi ya Ubunge na Majimbo yao kwenye mabano ni Waziri wa Fedha wa SMT Mhe. Saada Mkuya, (jimbo jipya) la Welezo, Waziri wa Nchi (AR) Ikulu na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Mhe. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi (AR) Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman na Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Mhe. Issa Haji Ussi Gavu,(hakuwa na mpinzani) pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, ambaye ni Mkuu wa Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa (SUKI) CCM Zanzibar Mhe. Hamad Yussuf Masauni.

  Sambamba na hilo, aliyewahi kuwa Mwakilishi na Mbunge katika vipindi viwili tofauti (2000 na 2005) kupitia Jimbo la Dimani, Mkoa uliyokuwa Mjini Magharibi Unguja, Hafidh Ali Tahir, amemshinda  aliyekuwa akishikilia kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo Abdullah Sheria na hivyo kulipiza kisasi cha kupinduliwa katika Uchaguzi wa mwaka 2010.
   
  Miongoni mwa vigogo walioanguka katika mchakato huo ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Uzini, ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya NEC wa Idara ya Organaizesheni (CCM Makao Makuu) Mhe. Mohamed Seif Khatib, aliyepata kura 1,333 sawa (23.0 %) baada ya mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani kuibuka kidedea kwa kupata kura 1,521 sawa 26.0.

  Pia, Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Kusini Unguja na Naibu Waziri wa Nchi za Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mahadh Juma Mahadhi, aliyepata kura 1,785.

  Wengine ni pamoja na aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe na Naibu Waziri wa Biashara na Masoko wa SMZ Mhe. Thuwaybah Edington Kissasi, Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu (aliyeangushwa na Ibrahim Raza), Naibu Waziri wa Fedha wa SMT  Mhe. Ame Silima na Mbunge wa Jimbo la Koani sasa (Tunguu) Mhe. Amina Andrew Clement.

  Katika  mchakato huo, ndani ya  majimbo mbali mbali kumejichomoza sura mpya kadhaa zinazotaka kugombea  nafasi za Ubunge na Uwakilishi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  Miongoni mwao ni pamoja na Khalifa Salum Suleiman (Tunguu), Salum Mwinyi Rehani (Uzini) na Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Mjini Mansuriyya Bagwanj (Chwaka) wanaogombea Ubunge, wakati  mjumbe wa NEC (W) Kaskazini “B” Mtumwa Peya, Afisa Mwandamizi wa CCM wa Idara ya SUKI (AKZ) Mohamed Ahmada Salum (Malindi), Simai Mohamed Said (Tunguu) na Yussuf Suleiman (Uzini) wanaowania Uwakilishi.

  0 0

  Kamati ya maandalizi ya tamasha la ‘Kandanda Day 2015’, inatarajia kufanya tamasha lake la kila mwaka,litakalofanyika katika Viwanja vya TCC Oktoba 17
  mwaka huu,Chang’ombe, Dar es Salaam.


  Katika tamasha la mwaka huu,mbali na kuwepo kwa mechi kati ya Timu DizoMoja na Timu Ismail, lakini pia kutakuwa na matukio mbalimbali ya kimichezo na kijamii
  yatakayoendelea.
   
  Mratibu wa tamasha hilo Patrick Dumulinyi,alitanabaisha kuwa siku hiyo, kutakuwepo na mchezo wa utangulizi ambao utahusisha kituo cha kulea watoto yatima kinachojulikana kama House of Blue Hope, kilichoko Mabibo. 
  “Katika tamasha la mwaka huu ambalo litabeba kauli ya Tukapige Kura, kwa makini,Tuisaidie jamii, wanakandanda wote tunapenda kuwahakikishia kutakuwepo kwa mambo mbalimbali mazuri na yataacha kumbukumbu kwa
  wanasoka watakaohudhuria siku hiyo,”alisema Dumulinyi na kuongeza. 
   
  “Mbali na kucheza soka,lakini tutacheza pamoja na watoto yatima pamoja na kula nao chakula cha pamoja,pia katika kuelekea siku hiyo tutakuwa tunauza T-Shirt
  maalumu,ambazo tunatarajia fedha tutakazozipata tutatoa asilimia kumi ya mapato kwa ajili ya kuchangia kitu hicho, kama mwanzo wa kampeni ya tovuti ya kandanda
  ya #OneBallOneTxtBook, kampeni ambayo lengo lake ni Kutoa mpira na madaftari kwa vituo na shule za msingi”


  Dumulinyi,alisema kwamba kamati ya maandalizi imejipanga kikamilifu kufanya tamasha hilo kuwa bora na liwe mfano kwa makundi ya wadau wote wa soka
  nchini. 
   
  “Kikubwa tunachopigana nacho kwasasa ni uwezeshaji wa tamasha hilo,kwani licha ya kamati kujiandaa pamoja na kujitokeza kwa baadhi ya wadau kuunga mkono
  tunachokifanya,lakini tunahitaji nguvu zaidi kutoka kwa makampuni,taasisi, mashirika na wadau binafsi,ambao tunaamini nguvu yao itasaidia kufanikisha
  tamasha hilo kuwa bora zaidi,”
   
  Alisema tamasha la mwaka huu ni muendelezo wa tamasha bora la mwaka jana, ambalo lilipata udhamini mbalimbali ukiwemo ule wa kampuni ya matairi nchini ya
  Binslum, ambayo tayari imeshakubali kudhamini pia mwaka huu.
   
  Imetolewa na Kamati ya Kandanda Day 2015
  Mohamed Mkangara  0 0

  Aina mpya Oil ya magari na mitambo ya NEXTOIL imeingia nchini na kesho inazinduliwa rasmi chini ya duka la F-ZONE (T) LIMITED lililopo jijini Dar es salaam Mtaa wa Kariakoo na Msimbazi. Wasiliana nao kwa simu +255 757222480
  Sehemu ya shehena ya NextOil kutoka Triton kama inavyoonekana kwenye duka la F-Zone (T) Limited lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo, Dar.

  0 0


  Wachezaji wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es salaam wakisherehekea ubingwa wao wa Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, mara baada ya kuitungua timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya Bao 2-0, katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.
  Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,Mhe. Eugene Segore Kayihura (wa pili kulia) akikabidhi kitita cha Dola za Kimarekani eflu 30 kwa Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" ikiwa ni zawadi ya ushindi wa kwanza iliyotolewa na Mdhamini Mkuu wa Mashindao hayo ambaye ni Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame. Wengine pichani toka kushoto ni Rais wa Cecafa, Leodger Tenga, Mgeni Rasmi kwenye Mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick, Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
  Mgeni Rasmi kwenye Mchezo fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup 2015, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia) akishirikiana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Nchini Kenya, Mh. Raila Odinga wakimkabidhi Kombe la Ubingwa huo, Nahodha wa Timu ya Azam FC, John Bocco "Adebayor" baada ya kuichapa bao 2-0 timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo.
   Kiungo hodari wa Timu ya Azam FC, Ammy Ali akiondika na mpira huku Mabeki wa Timu ya Gor Mahia wakiangalia namna ya kumdhibiti, katika mtanange wa fainali ya Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame Cup 2015, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo. Azam FC imeshinda Bao 2-0 na kutwaa ubingwa huo.
   kiungo wa timu ya Gor Mahia ya Kenya, Karim Nizigiyimana akiachua shuti kuelekea lakongoni mwa timu ya Azam FC.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0

  Mh January amepewa tena ridhaa ya kuendelea kugombea Jimbo la Bumbuli na wana CCM katika uchaguzi uliofanyika ndani ya chama na Kuibuka kinara kwa kura nyingi na zakishindo dhidi ya wagombea wenzake.
  Hivi Ndivyo Matokeo yalivyokuwa.....

  0 0

  Kutoka Kushoto: Dkt.Abel Minani, Dkt.John P.J Magufuli na Dkt.John Kyaruzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam muhula wa mwaka 1985/1986.

  0 0
  0 0
 • 08/02/15--20:00: Article 17
 • 0 0

  Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.
  Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.

  Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.
  1- moja
  Pia filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.

  Filamu ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.

  Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.

  Filamu hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.

  AISHA imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la UZIKWASA.

  Filamu ya aisha ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.
  8- nane
  Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, nae alipata nafasi ya kutoa hotuba yake.
  6- sita
  Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.
  7- saba
  Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipeke ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali, Ilipendeza sana.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  IMG_0282
  Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euprasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.

  Na Mwandishi wetu, Kibaha
  MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita wa Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

  Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.

  Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.
  IMG_0335
  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi akimpa mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.
  IMG_0341
  Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.


  0 0

  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano waNHC, Bi Suzan Omari akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo waliokuwa wakisimamia michezo mbalimbali wakati wa tamasha la NHC Family Day lililofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach mwishoni mwa wiki likishirikisha wafanyakazi wa shirika hilo jijini Dar es salaam na familia zao na kufahamiana ikiwani pamoja na kubadilishana mawazo.
  ????????????????????????????????????
  Wafanyakazi hao wakishindana katika mbio ufukweni.
  ????????????????????????????????????
  Mmoja wa wafanyakazi wa NHC akiwa amejishindia Jogoo katika shindano la kufukuza kuku.


  0 0

  Muonekano mpya wa Barabara ya Morogoro Rodi jijini Dar baada ya kupigwa sop sop kufuatia mradi wa mabasi yaendayo kasi.


  0 0
 • 08/03/15--00:40: Kumbukumbu
 • Kumbukumbu ya Miaka Mitatu (1955-2012)
  Mpendwa Baba yetu, Joseph Mturi Mahemba
  Hatimaye siku, Miezi imepita hadi hii leo ambapo imetimia Miaka mitatu (3) tangu ulipotutoka ghafla usiku ule wa siku ya jumatano ya tarehe moja ya Mwezi Agosti, 2012 na kutuachia huzuni kubwa.

   Japokuwa haupo nasi hapa duniani lakini tupo nawe kiroho kwa kuendeleza mema yote uliyotufundisha na kutuasa. 

  Tunakukumbuka kwa Upole, Upendo, Busara na Ukarimu uliokuwa nao kwa familia na Marafiki. Mwongozo na matendo yako yataendelea kuwa dira kwetu

  Daima unakumbukwa sana na Mkeo Rose Joseph, dada  zako Theresia, Karaghita, Wankuru na Mnaga, wanao wapendwa Michael, Mkami, Niwa, Sagana, Mary, Geofrey, Nyakaho, Lecardia na Pricilla, na wajukuu zako wote .

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake libalikiwe.

  0 0

  Mkuu wa masuala ya ufumbuzi na ushauri wa Huawei Afrika mashariki na kusini Dr. Bello Moussa, akizungumza wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa ulipewa jina la Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano na teknolojia kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika. Mkutano ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
  Meneja Uhusiano Huawei Tanzania Bw. Jimmy Nlinguo akipokea tuzo ya uongozi bora kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Selina M. Lyimo kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam kujadili changamoto za mawasiliano pamoja na jinsi ya kuongeza ukuaji wa broadband katika nchi za Afrika.
  Meneja Uhusiano wa Huawei Tanzania akisema maneno machache ya shukrani kwa wadau wa sekta ya mawasiliano na teknolojia mara baada ya kampuni yake kutunikiwa tuzo ya uongozi bora na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kutokana na mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Connect to Connect (C2C) ulioandaliwa na wizara hiyo katika hoteli ya kimataifa ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.


older | 1 | .... | 926 | 927 | (Page 928) | 929 | 930 | .... | 3284 | newer