Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM ZANZIBAR CHATOA TAMKO JUU YA KUJITOA KWENYE CHAMA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASA.

$
0
0

 Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga akitoa taarifa ya Chama hicho kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa ndani ya Chama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa katika mkutano uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
 
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar.


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir/Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar   

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni Chama  kikubwa chenye wafuasi  na wanachama wengi  pamoja na  Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na uadilifu mkubwa.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga  wakati alipokuwa akitoa taarifa  kwa Waandishi wa Habari  kuhusu kujitoa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na Chama cha upinzani  huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui 

Amesema CCM ni Chama  kinacho aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa Tanzania  hivyo  kujitoa kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama haiwezi kukiathiri  chama hicho.

Nyawenga ameongeza kuwa wingi wa wanachama wa chama hicho  haujaletwa na utajiri wa vingozi wake bali umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi yake.

Alisema CCM haina hasara kumpoteza mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na itikadi ya Chama  kwa maslahi yake binafsi na marafiki zake hata kama utajiri  wake ni mkubwa wa kupindukia.

Ameongeza kuwa uwamuzi wa Lowassa kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la kukishituwa chama, viongozi, pamoja na wanachama wake na hakiwezi kudhoofika wala kutetereka.

Alisema hii sio mara ya kwanzi kwa Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi  mwandamizi  na kujiunga na  vyama vya upinzani na bado kinaendelea kuimarika.

“Mwaka 1989, CCM iliwafukuza uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino Lyatonga Mrema  na mwaka jana CCM ilimfukuza uanachama aliyekua Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,” alikumbusha Katibu wa Chama Mkoa.

Nyawenga aliweka wazi kuwa  umaarufu alionao  Lowassa inawezekana umejengwa kutokana na CCM lakini haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa kutokana na yeye.

Alisema wanachama wa Zanzibar  waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma  ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani ya Chama na sasa  baada ya kuhama wameamua kujitenga  na hawako pamoja naye.
 
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib Borafia Silima amesema kwamba Tanzania inaheshimika kuwa  ni  nchi yeye amani, na mshikamano na Chama cha Mapinduzi  kinafuata utaratibu wa katiba iliyowekwa.


Amesema kila Mwanachama anayo haki  na uhuru wa kuchaguwa kiongozi anayemtaka na yeye  kuchaguliwa na mtu yeyote ikiwa ni Demokrasia iliyotandikwa na Chama hicho.    

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na ujumbe Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar michoro iliyotengenezwa na Wataalamu wa ECG ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kuwa katika mazingira ya Biashara ya Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri waliopo Tanzania kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuwekeza miradi ya Kiuchumi.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana Mohammed Alef Sherief wa kwanza kutoka kushoto akimfahamisha Balozi Seif hayupo pichani fursa zinazotolewa na Taasisi yake katika kuwajengea Vijana uwezo wa kufanya Biashara.
Balozi Seif katika Picha ya pamoja na Wafanyabiashara na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba na Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohammed Hamza. Kulia ya Balozi Seif ni Mtaalamu wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji ya ECG Mhandisi Sherif Meurad pamoja na Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana Mohammed Alef Sherief.

TAKUKURU YAKANUSHA TUHUMA ZA RUSHWA DHIDI YA NAPE

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MUHIMBILI 1988 WAIKUMBUKA SHULE YAO.

$
0
0
Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, akikata utepe ili kufungua Ofisi ya walimu wa shule ya msingi Muhimbili, iliyokarabatiwa na kuweka viti 29 na meza 8 na wanafuzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo Mwaka 1988, pamoja na kiti na meza ya kisasa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo katika hafra fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao ikiwa imehudhuliwa na walimu wa shule hiyo wa tangu mwaka 1978.
 Walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi waliohitimu katika shule hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo.Kutoka kulia ni Mhitimu wa shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi muhimbili,Usia Nkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na  Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu wa shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimmbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafra fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dra es Salaam.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

LOWASSA ARUDISHA FOMU ZA KUWANIA URAIS KUPITIA CHADEMA, ADHAMINIWA NA ZAIDI YA WATANZANIA MIL. 1.6

$
0
0
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mh. Godluck Ole Medeye alieambatana nae.
 Mkurugeni wa Oganaizesheni na Uratibu wa Kanda wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila akionyesha fomu zenye idadi ya wananchi waliomdhani Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa. ambapo jumla ya wananchi 1,662,397 walijitokea katika maeneo mbali mbali kumdhamini Mgombea huyo.
 Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akikabidhi fomu hizo kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Prof. Abdalaah Safari wakati wa hafla fupi ya kurudisha fomu hizo, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Wadhamini wa CHADEMA, Mh. Arcado Ntagazwa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.

GULIO LA VODACOM KUFIKIA TAMATI KESHO

$
0
0
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Jessam Jeremia akiwapa maelekezo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika kwenye gurio la “Vodacom expo” lilioandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwauzia bidhaa mbalimbali za mawasiliano kwa bei nafuu.Gurio hilo linafanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam waliofika kwenye viwanja vya Kijitonyama kwenye gurio la Vodacom Expo wakionyeshwa baadhi ya simu na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania ambazo zinauzwa kwa bei nafuu zaidi, Gurio hilo limeandaliwa na Vodacom Tanzania kwa siku mbili mfululizo kwa ajili ya kuwauzia wakazi wa jiji bidhaa za mawasiliano kwa gharama nafuu.
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wakinunua bidhaa mbalimbali za mawasiliano kwa bei nafuu kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama wakati wa Gurio la Vodacom Expo linalofanyika kwa siku mbili mfululizo.
Meneja bidhaa wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga akifanyiwa mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika Gulio(Vodacom Expo)lililoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kununua bidhaa mbalimbali za mawasiliano kwa bei nafuu na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Posta kijitonyama jijini.

LORI LAPIGA MWELEKEKA ENEO LA UKONGA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Lori la Migizo lenye namba za usalili T 567 BQW ambalo tela lake limepiga mwenyeka jioni hii eneo la Ukonga jijini Dar es salaam na kusababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo. Chanzo mweleka huo bado hakijafahamika.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika barabara hiyo baada ya tela la Lori hilo kupiga mweleka.
Magari mengine yanayoitumia barabara hiyo yakipita kwa taabu kando kando ya barabara hiyo.
Muonekano wa tela hilo.

MBIO ZA URAIS 2015: MCHUNGAJI MTIKILA WA DP, FAHMI DOVUTWA WA UPDP,MAXMILLIAN LYIMO WA TLP WACHUKUA FOMU ZA UTEUZI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC

$
0
0
MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, akikabidhiwa fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, kutoka kwa afisa uchaguzi mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Agosti 1, 2015.
MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015, za Tume hya Taifa ya Uchaguzi, (NEC), kutoka kwa afisa mwandamizi wa tume hiyo, makao makuu ya NEC, jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi Agosti 1, 2015. Dovutwa amekuwa mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo na kazi iliyo mbele yake ni kutafuta wadhamini 200 ambao ni raia wa Tanzania wenye shahada za kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo. Dovutwa alifuatana na mgombea mwenza wake, Hamad Mohammed UIbrahim na wanachama wachache wa chama hicho
Mgombea kiti cha Urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, (kulia), akipokea mkoba wenye fomu za uteuzi wa kuwania kiti hicho za Tume ya Taifa ya Uchaguzi .
Mgombea kiti cha urais kupitia TLP, Maxmillian Lyimo, akionyesha mkoba wenye fomu za uteuzi za tume ya taifa ya uchaguzi, NEC, baada ya kukabidhiwa.PICHA NA K-VIS BLOG.

NHIF YAWAFUNDA WAANDISHI HABARI PAMOJA NA JUMUIYA YA MASHEIKH WA JUMUIYA YA ZAWIYATUL QADIRIA

$
0
0
Mkurungenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athumani Rehani (katikati) akizungumza na waanshi wa habari (hawapo pichani) juu ya kujiuga na mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Media Car Wash for Cancer,Benjamin Thomson na kulia ni Afisa Matekelezo Mkuu wa NHIF,Hance Mwankenja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Media Car Wash for Cancer,Benjamin Thomson akizungumza na waanshi wa habari juu ya kujiuga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wa NHIF ,Uegene Mikongoti akizungumza na masheikh wa Jumuiya ya Zawiyatul Qadiria wakati wa kuwajengea uwezo wa kujiunga na bima ya afya leo jijini Dar es Salaam.

Mwigulu Nchemba Ashinda kwa 99% kura za maoni Ubunge jimbo la Iramba

$
0
0





Mwigulu Nchemba Ashinda kwa 99 % kura za maoni Ubunge jimbo la Iramba

 Masimba         
Mwigulu 88
Jairo 1
Kilimba 0
Amon 0

Mlandala
Mwigulu 50
Jairo 0
Kilimba 3
Amon
0

Mang'ole 
Mwigulu 173
Jairo 6
Kilimba 0
Amon 0

MSAI
Mwigulu 294
Jairo 35
Kilimba 59

MALUGA
Mwigulu 322
Kilimba 5
Jailo 0

 UWANZA
Mwigulu 172
Jairo 8
Kirimba 23
Amon 2

 Nganguri
Mwigulu 727
kilimba 2
jairo 2
Amon 0Mwigulu kashinda

UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE NI KESHO UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, WAIMBAJI WATAKAO MSINDIKIZA WATAMBULISHWA

$
0
0
 Mwimbaji wa nyimbo za injili, Boniface Mwaitege (katikati), akiimbaji sanjari na waimbaji wenzake wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi. Waimbaji hao kesho watatoa burudani wakati wakimsindikiza mwimbaji mwenzao Boniface Mwaitege katika uzinduzi wa albamu zake tatu za Utanitambuaje, Mama ni mama na Tunapendwa na Mungu utakaofanyika kesho ukumbi wa Diamond Jubilee saa nane mchana kesho. Kutoka kulia ni Faustine Mnishi, Upendo Kilahiro, Jesca Magupa (BN) na Atosha Kissava.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi huo.
Msama (katikati), akiwa na waimbaji watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

MWANAMUZIKI wa Injili, Boniface Mwaitege kesho mchana anatarajiwa kuzindua albamu zake tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mkurugenzi wa Kapuni ya Msama Promotion alisema kuwa maandalizi yote muhimu ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia saa nane mchana yamekamilika, Mwaitege atatambulisha albamu hizo kwa kusindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili.

Alisema mashabiki wa muziki wa Injili watarajie burudani ya nguvu kutokana na maandalizi ya nguvu na ya kipekee aliyofanya mwanamuziki huyo ikiwemo kurekodi albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Nairobi na Kenya.

"Maandalizi yote ya uzinduzi wa albamu za Mwaitege yamekamilika, mashabiki watarajie burudani ya nguvu, pamoja na ujumbe kutoka katika nyimbo hizo pamoja na mwanamuziki wengine watakamsindikiza," alisema Msama.

Alisema sehemu ya mapato katika uzinduzi huo ambao pia utafanyika katika mikoa mingine, itapelekwa kwa kwenye vitu vya watoto yatima.

Msama alizitaja albamu hizo ni pamoja na 'Tunapendwa na Mungu' yenye nyimbo za 'Tukiimba Mungu anashuka', 'Mtoto wa mwenzio ni wako', 'Safari Bado', 'Tumekuja Kukuchukua (Bibi harusi)', 'Tuko Salama', 'Moyo wa Shukrani', 'Hakuna Ridhiki', albamu nyingine ni Utanitambuaje na Mama ni Mama.

Baadhi ya wanamuziki watakaopanda jukwaani kusindikiza uzinduzi wa albamu za Mwaitege waliotambulishwa kwa waandishi wa habari na baadhi ya nyimbo zao zilizotamba katika mabano ni Upendo Kilahiro (Baba Ninakuabudu), Jesca  Magupa (Napokea), Mchungaji Faustine Munishi (Malebo) na Atosha Kisava (Umwema).

Akizungumzia utambulisho wa albamu zake tatu, Mwaitege alisema amejiandaa vizuri kwa uzinduzi huo, ambapo mashabiki wataweza kupata burudani nzuri na ujumbe, pia albamu hizo zitakuwepo ukumbini.

Aliwataka mashabiki kufika kwa wingi katika onesho hilo ili kumpa hamasa yeye na waimbaji wengine ambao watamsindikiza.

Awali wasanii wengine waliotajwa kusindikiza uzinduzi huo ni  pamoja na John Lisu, Martha Mwaipaja, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Eiphraim Sekereti, Atosha Kisava, Mess Chengula,  Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe na Joshua Mlelwa.

Onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini.


Kiingilio katika onesho hilo kitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti maalumu, sh. 5,000 na sh.2,000 kwa watoto. 

Mchezo wa Kirafiki Kati ya Simba na Polisi Usiku Huu Uwanja wa Amaan Simba Ikiwa mbele kwa bao 2--0

$
0
0
Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
Kikosi cha timu ya Polisi Zanzibar kilichokubali kipigo cha bao 2--0 kutoka kwa timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Simba kilichotowa kipigo cha mabao 2--0 dhidi ya timu ya Polisi Zanzibar wakati wa mchezo wao wa kujipima nguvu wa tatu kisiwani Zanzibar ikiwa imeshinda michezo yake yote
Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo huo.

WATANZANIA CALIFORNIA WAMUAGA BALOZI LIBERATA MULAMULA

$
0
0
 Watanzania California wakiongozwa na Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa walijumuika pamoja siku ya Ijumaa na kumuaga Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na kurudi nyumbani kwenda kulitumikia taifa kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Watanzania wa California wakipiga picha ya pamoja na Mhe. Balozi Libarata Mulamula (wapili toka kushoto) siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomuaga rasmi.
 Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi yake Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme mara tu baada ya kukabidhiwa na Watanzania California siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomualika rasmi kwa ajili ya kumuaga.
 Balozi Liberata Mulamula akicheza na kuburudika kwenye moja ya nyimbo zilizopigwa kwenye tafrija hiyo.
 Balozi Liberata akipiga makofi
Moja wa kikundi maarufu cha ngomma ya asili kikitoa burudani

MSIKILIZE OLE SENDEKA ALIPOKANUSHA UVUMI KUHUSU YEYE KUHAMIA CHADEMA

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0

TAARIFA YA KAMATI YA UTENDAJI
Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichokutana leo kimepitia na kutoa maamuzi yafuatayo:

(i)           Kila mkoa utakua na kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto (Regional Sports Centre). Mapato ya mchezo wa Ngao ya Hisani msimu huu yatatumika kuagiza kontena la vifaa (mipira size 3, 4, bips na cones) ambavyo vitasambazwa katika vituo vyote vya michezo vya mikoa.

(ii)         Ubovu wa viwanja – Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretariat kuwaandikia barua wamiliki wa viwanja vyenye mapungufu, kufanyia kazi marekebisho hayo haraka kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi nchini. Kiwanja ambacho hakitafanyiwa marekebisho hakitatumika kwa michezo ya ligi msimu huu.

(iii)       Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu nchini Tanzania (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini tarehe 04 Agosti kisiwani Zanzibar kwa gharama za TFF kujiandaa na Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo Brazaville mwezi Septemba mwaka huu. Aidha Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretariet kuwasiliana na Kamati ya Olympic nchini (TOC) kuweza kujua mchango wao katika maandilizi hayo ya michezo ya Afrika.

(iv)        Kamati ya Utendaji imeipongeza Kamati ya ndani ya Uendeshaji wa Michuano ya Kombe la Kagame (LOC) kwa kuandaa michuano hiyo vizuri kuanzia mwanzo mpaka sasa inapoelekea mwishoni kesho kwa mchezo wa Fainali.  Aidha Kamati inaipongeza klabu ya Azam FC kwa kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo na kuitakia kila la kheri katika mchezo wa kesho ili iweze kulibakisha kombe hilo nyumbani. Kamati hiyo pia imeipongeza klabu ya Yanga kwa kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

(v)          Aidha Kamati ya utendaji imeiagiza sekretariat kuandika barua kwenda kwa uongozi wa CECAFA juu ya masikitiko na mapungufu yaliyoenekana katika michuano hiyo. Timu ya Gor Mahia pamoja na washabiki wake wamekuwa wakifanya vitendo vya utovu wa nidhamu huku CECAFA ikiwatazama pasipo kuwapa adhabu yoyote.

(vi)        Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji pia kimepitia na kupitisha mapendekezo ya rasimu ya kanuni za uendeshaji wa Bodi ya ligi nchini (TPLB), yaliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji Wakili, Idd Mandi.

 FAINALI KAGAME KIINGILIO  BUKU TATU
Michuano ya Vilabu Bingwa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kufika tamati kesho jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa mchezo wa Fainali utakaozikutanisha timu ya Azam FC dhidi ya Gor Mahia. 
Viingilio vingine vya mchezo huo wa kesho wa fainali ke ni VIP A ni shilingi elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000) na sehemu nyingine ya uwanja  iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000) kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa. 
Katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika jana, Gor Mahia iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya Khartoum mabao yaliyofungwa na Michael Olunga, Innocent Wafula na Kagere Meddie na kukata tiketi ya kucheza fainali. 
Gor Mahia chini ya kocha wake Frank Nuttal mpaka kufikia hatua ya fainali, imecheza jumla ya michezo sita, ikiwemo michezo minne katika hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali, ambapo imeweza kushinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja. 
Mshambuliaji wa Gor Mahia,Michael Olunga anaongoza kwa ufungaji, akiwa amepachika mabao matano, akifuatiwa na nahodha wa Khartoum Salehdin Osman na msadizi wake Amin Ibrahim wote wenye mabao manne kila mmoja.

Kwa uapnde wa Azam chini ya kocha wake Stewart Hall, imefanikiwa kufika hatua ya fainali bila ya kuruhusu nyavu zake kutikisika, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imepachika mabao tisa (9) katika michezo mitano iliyocheza kuanzia hatua ya makundi. 
Kuelekea mchezo wa Fainali, Azam FC iliziondosha Yanga SC kwa mikwaju ya penati (5-4) hatua ya robo fainali, na kasha kuindoa KCCA hatua ya nusu fainali kwa kuifunga kwa bao 1- 0, bao lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Farid Musa.
Mshambuliaji Kipre Tchetche ana mabao matatu kwa upande wa washambuliaji wa Azam FC, akifuatiwa na nahodha John Bocco na Farid Musa wenye mabao mawili kila mmoja.

Katika fainali hiyo ya kesho, inatarajiwa kuwa ya vuta ni kuvute kutokana na makocha wa timu hizo, Frank Nuttal wa Gor Mahia kutaka kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 tangu Gor Mahia kushinda kombe hilo mara ya mwisho mwaka 1985 walipotwaa kwa mara ya tano (5). 
Huku Stewart Hall akiwania kuweka historia ya kwanza kwa klabu ya Azam FC kuweza kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo miaka tisa iliyopita, baada ya kusindwa kutwaa taji hilo ilipotinga fainali mwaka 2012 kwa kufungwa na Yanga SC mabao 2-0.

Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuanza saa 9:45  alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, huku mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ukitarajiwa kuanza saa 7:30 mchana ukizikutanisha timu za Khartoum ya Sudan dhidi ya KCCA kutoka nchini Uganda. 
Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa kitita cha Dola za Kimarekani Elfu Thelathini (U$ 30,000), mshindi wa pili Dola za Kimarekani Elfu Ishirini (U$ 20,000) huku mshindi wa tatu akizawadiwa Dola za Kimarekani Elfu Kumi (U$ 10,000).

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini Mkoa wa Temeke, linawashikilia watu watatu kutoka nchini Kenya kufuatia kufanya kosa la shambulio katika mchezo wa nusu wa fainali kati ya Gor Mahia dhidi ya Khartoum katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
Raia hao wa Kenya walifanya shambulio kwa mlinzi wa TFF uwanja wa Taifa, Omary Mayai wakiwa katika jukwaa la VIP A ambapo askari polisi walijaribu kuwaonya na kuwaomba kuwa wastaarabu, lakini walishidwa kutii amri ya polisi na kuendelea kufanya vurugu kabla ya mmoja wao kukimbilia ndani ya uwanja na kuketi katika benchi la ufundi la Gor Mahia. 
Namba ya jarada la kesi iliyofunguliwa kituo cha Polisi cha Chang’ombe ni CHA/RB6265/2015, na wanaoshikiliwa kituoni hapo ni mshabiki wa Gor Mahia Jackson Mjidie (Jaro Soja), pamoja na waandishi wa habari wawili kutoka kituo cha Citizen, Okinyi Mike na Jariri Otieno.
  
DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA AGOSTI 6
Dirisha la Usajili kwa Vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (RCL) linatarajiwa kufungwa tarehe 06 Agosti, 2015. 
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linavikumbusha vilabu vyote kufanya usajili wa wachezaji wao mapema kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo, ili kuondokana na usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho. 
Pindi dirisha hilo litakapofungwa Agosti 06, hakuna klabu au timu yoyote itakayoweza kufanya tena usajili wake, hivyo ni vyema vilabu vitahakikisha vinamaliza mausala ya usajili mapema kabla ya siku ya mwisho.
  
U15 KUJIPIMA LEO ZANZIBAR
Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinatarajiwa kushuka dimbani kisiwani Zanzibar kucheza michezo wa kirafiki na kombani ya kisiwani humo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017. 
Timu ya vijana ya Taifa wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imekua ikiingia kambini kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu, na kocha kupata nafasi ya kuona maendeleo ya vijana na kuongeza wachezaji wengine wanaonekana katika kuboresha kikosi hicho. 
Kikosi hicho cha Vijana cha U-15 kilichopo chini ya kocha mzawa Bakari Shime, kinajumuisha wachezaji 22 waliopo kambini, na kinatarajiwa kucheza michezo miwili kisiwani Zanzibari leo jumamosi na jumapili, kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WIZI WA FEDHA KWA KUTUMIA MTANDAO TISHIO DUNIANI

$
0
0
Jitihada za serikali katika kupambana na uhalifu wa mitandao imeungwa mkono kutokana na baadhi ya vyuo kuanzisha mitaala yenye somo la ulinzi wa  mitandao. 
Moja ya jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ni kupeleka muswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa mtandao ya mwaka 2015  katika mkutano wa 19 wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ulipitishwa na bunge hilo. 
Taarifa ya waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknologia , Profesa Makame Mbarawa kuhusu sheria hiyo inasema kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habarina Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio ya kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii. 
Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi

katika jamii ikiwemo  kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia


mbinu mpya za kutenda makosa ya zamani. 

Angalia kipindi cha Nyumbani Na Diaspora cha wiki hii

introducing Filamu ya Maisha ni Siasa

Taswa FC yashinda 5-3 Morogoro, yaomba udhamini toka kwa wadau

$
0
0
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imeendelea kutamba katika mechi zake za kirafiki baada ya kuisambaratisha timu ya Warioba Veterans mabao 5-3 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama. 
Taswa FC ambayo inadhaminiwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ilianza mchezo huo polepole huku wapinzani wao wakiongozwa na Barnaba Emilio na Jerry Mtetema kutawala dakika 10 za mwanzo na kukosa mabao kadhaa. Taswa FC chini ya Ali Mkongwe, Majuto “Ronaldo” Omary, Salum Jaba, Julius Kihampa, Athuman Jabir na Khatimu Naheka walianza kulishambulia lango la wapinzani wao na kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 kupitia kwa Julius Kihampa baada ya pasi safi ya Mkongwe. 
Bao hilo halikudumu sana na dakika mbili baadaye, Warioba Veterans walisawazisha kupitia wa Barnaba Emilio kwa njia ya penati baada ya Fred “Chuji” Mbembela kucheza faulo ndani ya eneo la hatari. 
Bao hilo liliwafanya Taswa FC kuongeza mashambulizi na kufuanga bao la pili kupitia kwa Kihampa tena baada ya pasi ya Majuto. Warioba ilisawazisha kupitia kwa Mtetema kabla ya Kihampa kufunga bao la tatu kwa Taswa FC na Stanley Abasirim kufunga la nne kufuatia pasi ya Tito Jonathan na Kihampa kufunga la tano dakika ya 78 ya mchezo baada ya pasi safi ya Jabir Johnson. 
Mtetema alifunga bao la tatu kwa timu yake katika dakika ya 85 ya mchezo. Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo ambao ni chachu kwao kuelekea kushiriki katika bonanza la waandishi wa habari mkoa Arusha Agosti 29 mwaka huu. 
Majuto alisema Taswa FC inahitaji msaada wa kifedha na vifaa ili kuweza kufika Arusha na kufanya vyema katika mashindano hayo ya kila mwaka. 
“Tuna timu nzuri sana ya mpira wa miguu na mpira wa pete, mwanzoni mwa mwaka huu kupitia udhamini wa benki ya Posta Tanzania tulimaliza katika nafasi ya pili mkoani Iringa, tunawaomba wadhamini watusaidie kufikia malengo yetu,” alisema Majuto.
Mchezaji wa Taswa FC, Shadrack Kilasi akimiliki mpira katika moja ya mechi za timu hiyo mkoani Iringa.
Wilbert Molandi wa Taswa FC akimpiga chenga mchezaji wa Mkwawa veterans katika bonanza la mkoa wa Iringa
Mchezaji wa Taswa FC, Zahoro Mlanzi akimtoka mchezaji wa Mkwawa veterans katika bonanza la wadau wa michezo mkoani Iringa

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0
Azam tv
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini Takukuru,yawatia mbaroni makada wa CCm kwa tuhuma za kutoa rushwa jijini Dar es salaam. https://youtu.be/S5m9N27VKBQ
Wakati kazi ya uandikishaji ikielendelea kwa siku 4 zilizo ongezwa baadhi ya waandikishaji wa BVR wagoma kwa  kutolipwa mafao yao. https://youtu.be/QfITiVLbDZI
 TBC NEWS
Wizara ya afya na ustawi wa jamii yaombwa kuweka kipaumbele kutibu magonjwa nyemelezi nay ale yasio ambukizwa kwani yamekuwa yakiwasumbua sana wazee na kupelekea vifo. https://youtu.be/P-kzlF3qgfw
Watu wenye ulemavu mkoani Iringa wawaomba wananchi kuwaunga mkono mara wajitokezapo kuwania nafasi mbalimbali za uongozi nchini. https://youtu.be/O4bsAUBrghU
Waandishi wa habari pamoja na wananchi wengine waaswa kujiunga na mfuko wa bima ya afya kufuatia changamoto nyingi katika kazi zao. https://youtu.be/bVwgPmOv0YU
 STAR TV NEWS
Katika hali ya kusikitisha Mwanamke mmoja wilayani Geita atengwa na familia yake kwa zaidi miaka 2 kwa tuhuma za uchawi huku akikosa huduma muhimu kwa mtoto wake. https://youtu.be/SeLDKlEhdoc
Wahitimu wa mafunzo ya awali ya kijeshi waaswa kutumia mafunzo waliyopata katika kulinda amani,nchi na jamii na kuacha na vitendo vya kihalifu,pamoja na matumizi ya dawa za kulevya. https://youtu.be/wg9o3ZGtLuA
Wizara ya uhamiaji nchini inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa watumishi, vitendea kazi na mazingira duni ya utendaji kazi. https://youtu.be/KfHWlm2R0po
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images