Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

FOMU ZA WAGOMBEA URAIS ,UBUNGE PAMOJA NA UDIWANI KESHO-LUBUVA

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu juu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi,Clothilde Komba.
 Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu juu  jeshi la polisi lilivyojipanga katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia wa taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii) 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti 21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu,Damian Lubuva  amesema wakati wa uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoa na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.
Lubuva a amesema kuwa wakati wa kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu na kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watu wengine.
Amesema kwa fomu za ubunge ni sh.50,000  na udiwani sh.5000 ambapo wanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa  wanasiasa wanatakiwa  na lugha za kistaarabu katika mikutano yao katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata hivyo amesema kuna baadhi ya vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo.
Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana  na usalama hivyo jeshi limejipanga katika ulinzi katika kipindi hiki.
Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha uchaguzi.

USIKOSE KUANGALIA GEMU LA NGAO YA HISANI JUMAPILI HII KATI YA CHELSEA NA ARSENAL KUPITIA DSTV

AZAM YAINGIA FAINALI YA KAGAME 2015, KUCHEZA NA GOR MAHIA

0
0
 Beki wa Azam FC, Abbas  Mudathir Yahya akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa timu ya KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akichuana na beki wa KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Beki wa Azam FC, Agrey Morris akichuana na beki wa KCCA, Hassan Wasswa katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia) akimtoka beki wa KCCA, Ochaya Joseph katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Azam FC, Agrey Morris akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa KCCA, Habib Kavuma katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

TANZIA- MKUU WA MAGEREZA MKOA WA SHINYANGA AFARIKI DUNIA

0
0

                                                Marehemu SACP Aneth Laurent  enzi za uhai wake

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza - SACP Aneth Laurent kilichotokea jana Julai 30, 2015 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.
Kamishna Jenerali wa Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba ambapo mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwa ndege kutoka Mwanza kuja Jijini Dar es Salaam na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
                    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya 
Marehemu mahali pema peponi Amina.

Rished Bade:Sheria mpya ya kodi kuwanufaisha wafanyabiashara

Simba Imeshinda katika mchezo wake wa Pili wa Mazoezi dhidi ya Timu ya Black Sailor kwa mabao 4--0

0
0
Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Black Sailor, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 4--0
Mchezaji wa timu ya Black Sailor akiwapita wachezaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki.
                    Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

USIKU WA HERIETH PALLANGYO ULIVYOFANA

0
0
 Biharusi mtarajiwa Herieth Charles Pallangyo akiwa kwenye pozi muda mfupi kabla ya kuanza tafrija yake maalum ya kugana na familia yake kbla ya kufunga ndoa. Tafrija ya kumpongeza na kumuaga iliyofanyika ukumbi wa Giraffe Sunset, Mbezi Beach Dar es Salaam. Production by: MD Digital Company +255 717002303, +255 755 373999.
 Herieth akiwa katika pozi la picha na mama yake
 Wazaa chema Bwana na Bibi Charles Pallangyo wakiwa katika pozi.
 Wageni waalikwa wakiwa ukumbini hapo. PICHA ZAIDI HAPA

CHAGUA AMANI RAI KATIKA KURA ZA MAONI SINGIDA MJINI

0
0
Chagua Amani Rai Jimbo la Singida Mjini.

MKURUGENZI MTENDAJI WA 8020 FASHIONS SHAMIM MWASHA ATOA MADA NAMNA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA MANUFAA KWENYE SEMINA YATAASISI YA MANJANO

0
0
Mkurugenzi Mtendaji   8020 Fashion na  Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Shamim Mwasha Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha  Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake  Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao.Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekhar Nasser
Washiriki wakimsikiliza Kwa Makini Mentor Shamim Mwasha aliyetoa Mada kwenye semina hiyo Namna ya Kutumia Mitandao ya Kijamii kwa Manufaa ya Maisha yetu ya Kila siku na Kucha Kupoteza Muda Kwenye Mitandao ya Kijamii Bila Manufaa yoyote. 
 Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi  ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii  limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd  Mama Shekhar Nasser AkitoaMafunzo  kwa njia Vitendo kwa Washiriki wa Semina hiyo yenye lengo la Kumsaidia Mwanamke wa Kitanzania Kudhubutu Kujikita Kwenye Biasha ra hususani Kwa Kutumia Vipodozi Pekee  vinavyozalishwa na Shear Illusion vya Luv Touch Manjano.
Washiri Wakiwa Pamoja Mra baada ya Kumaliza Mafunzo kwa Njia ya Vitendo. Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania



WAZIRI WA UJENZI AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA TENGERU-SAKINA (KM 14.1) ITAKAYOJENGWA KWA NJIA NNE MKOANI ARUSHA

0
0
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Patandi wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya kukagua ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akizungumza na wakaazi wa Patandi, Sangis na Tengeru kuhusu ujenzi wa barabara ya lami ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km 14.1 itakayojengwa kwa njia nne pamoja na madaraja makubwa mawili.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini TANROADS  Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa barabara hiyo pamoja na Barabara ya Arusha bypass km 42.2
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akizungumza na wakazi wa Patandi mkoani Arusha kuhusu ujenzi wa barabara ya Tengeru-Sakina utakaojengwa kwa njia nne.
 Wakaazi wa Patandi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla hiyo. 

Sehemu ya barabara ya Tengeru-Sakina katika eneo la Patandi ikiwa imeanza kufanyiwa ukarabati utakaohusisha ujengwaji wa njia nne kwa kiwango cha lami.Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi

BBC DIRA YA DUNIA KUTOKA LONDON - IJUMAA

SHUKURANI NA MISA YA KUMALIZA MSIBA

0
0
MAREHEMU RICHARD AZZA MGAYA 
04. 04 , 1939 - 22. 05,  2015. 

Familia ya Marehemu Mzee Richard Azza Mgaya inawaarifu ndugu, jamaa, marafiki na jirani kwamba shughuli ya kumaliza msiba itafanyika Jumapili hii ya tarehe 02 agosti, 2015 nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha.
Misa ya shukurani na sadaka itaanza saa tatu za asubuhi na baadaye chakula cha mchana.
Familia inatoa shukurani kwa wote walioshiriki kikamilifu katika shughuli za mazishi toka mwanzo hadi mwisho wa kumuweka kwenye nyumba yake ya milele. Familia inasema haina cha kuwalipa zaidi ya kusema AHSANTE SANA kwa yote na Mola awajaalie afya na uzima zaidi.

SISI TULIMPENDA, LAKINI BWANA ALIMPENDA ZAIDI.
HIVYO JINA LAKE BWANA NA LIHIMIDIWE - AMINA

Marehemu Mgaya atakumbukwa daima kama  Mfanyabiashara maarufu aliyekuwa akimiliki duka pekee lilikokuwa linauza bidhaa zitokanazo na maliasili za wanyama pori  kama vile pembe na ngozi pamoja na vinyago. Duka lake lilikua mtaa wa Samora wakati huo ukiitwa  Independence Avenue na duka lake likiitwa National Trophy and Carvings Co Ltd. 

KUMBUKUMBU

0
0
Mpendwa Mama Rhoda Cleopa Msuya
Daima tutakupenda kamwe hatutokusahau.
Ni Miaka kumi tangu ulipotangulia

Tumebaki na kumbukumbu za mapenzi yako ya dhati na wema wako
Tumekukumbuka leo, jana, juzi na siku kabla yake

Tunakukumbuka moyoni na kila tunapotaja jina lako

Kumbukumbu zetu kwako haziwezi kuelezeka

Tumebaki na kumbukumbu ya tabasamu lako na picha yako

Ni kumbukumbu za upendo wako ndio zinatupa nguvu ya kuendelea mbele

Daima utabaki katika mioyo yetu

Uko Katika Ufalme wa Mungu, Tunakuombea upumzike kwa amani.


Unakumbukwa daima na mume wako Cleopa, watoto wako George,John,Joyce, Job, Naanjela.
Wakwe, Onesmo, Khadija,Mercy,Mary na Yoko, wajukuu, ndugu na marafiki.

Misa maalum ya kumbukumbu ya wapendwa wetu Mama Rhoda Cleopa Msuya na Geoffrey Cleopa Msuya itafanyika Tarehe 9 August 2015 kwenye kanisa la Azania Front Cathedral saa tatu na nusu asubuhi,
Wote mnakaribishwa.

“kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka” Mithali 10:7

MGOMBEA UBUNGE ARUSHA ,MUSTAFA PANJU APANDIKIZA MBEGU YA UPENDO,AMANI NA MSHIKAMANO

0
0
SAM_4682Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akiwaonyesha kadi ya CCM inayoonyesha imani ya mwanachamana kwa wanahabari pamoja na wadau mbalimbali jijini Arusha, pia alizungumzia kuhusu mchakato wa ndani ya chama kumpata mgombea wa Ubunge wa jimbo la Arusha kupitia CCM siku moja baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuzunguka katika kata 25 za kuomba kura kwa wanachama wa chama hicho,aliwataka wananchi kumchagua mwanachama watakaoonyeshwa na Mungu na siyo kwa kushawishiwa kwa pesa,pia alionyesha furaha yake kwa kuweza  kupandikiza mbegu bora ya Upendo,Amani na Mshikamano kwa wagombea wenzake pamoja na Wanaarusha kwa ujumla(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4659Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali jijini Arusha ,ambapo aliwashukuru wagombea wenzake 12 wanaowania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Arusha kwa kumaliza mchakato wa kuzunguka katika kata 25 jimbo la Arusha kwa Amani,Upendo na mshikamano na pia alionyesha furaha yake kwa kupandikiza mbegu bora ya Upendo,Amani na Mshikamano
SAM_4665Sehemu ya wadau wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM .

Nipitisheni nilirejeshe Jimbo la Kawe- Pijei

0
0
MTIA nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kawe, Jumaa Mhina 'Pijei', amewaomba wananchi wa Kawe kumpa kura ili aweze kulirejesha jimbo mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika kampeni zake za mwishoni jimboni humo, Pijei, alisema mbali ya kujitokeza makada 21 kulitaka jimbo hilo, wananchi ndiyo wenye uwezo wa kuamua nani wa kumpa nafasi hiyo.

"Wanachama sehemu zote tulizopita watakuwa tayari wamemwona anayefaa kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Kawe, nami naamini nafasi hiyo ninaiweza kwani vijana, akina mama na hata akina baba wanajua kazi zangu za maendeleo nilizozifanya jimboni kwetu," alisema.

Pijei katika kata zaidi ya tano za jimbo hilo, amekuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na jinsi alivyokuwa akijinadi katika mikutano ya kampeni ya kura za maoni.

Jimbo la Kawe limekuwa likishikiliwa na upinzani tangu mwaka 2010, likiwa chini ya Halima Mdee,hivyo CCM wamejipanga kuhakikisha wanalirejesha mikononi mwao, lakini kama likimpitisha mtu sahihi anayependwa na wengi.

Baadhi ya waliojitokeza ni Mtiti Butiku, Yusuph Nassoro, John Mayanja, Dickson Muze, Dk. Wilson Babyebonela, Kippi Warioba, Colman Masawe, Elias Nawera, Abdallah Majura na Jerry Muro.

MGOMBEA URAIS WA CHADEMA KUREJESHA FOMU LEO

0
0
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU MGOMBEA URAIS KUREJESHA FOMU



Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kuwa baada ya hatua ya kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa ndani ya chama kugombea nafasi ya urais, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa kesho (LEO) Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.


Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu  yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara ikayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.


Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.


Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.



Imetolewa leo Julai 31, 2015 na;


Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano – CHADEMA

TREKTA LINAKODISHWA

0
0
"Kwa wale wakulima wenye ekari za kutosha maeneo kuanzia Mkuranga, Mwarusembe, Kimanzichana ya Mkiu, Mkamba nk hadi maeneo ya Ikwiriri na Rufiji.... mkombozi kapatikana sasa. Ile hofu ya kulima kwa muda muafaka imepata jawabu!!
Tumeleta trekta linalofaa kupambana kwa kazi maeneo hayo, hili FORD 7500.
Bei zetu ni nzuri zipo baina ya Tshs. 40,000/= hadi 60,000/= kulingana na umbali.

Kwa mawasiliano:
1. 0787519910 na 0767519910... Tutakujibu kwa simu na sms!!
2. Kwa 0787519910 tutakujibu kwa whatsapp
3. Email: moddyguyz@yahoo.com
 Sisi tupo Kimanzichana ya Mkwechembe; kama kilometa tatu kutoka Kimanzichana getini...."

Statment by the Director General - Tfda - Steering Committee

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA 4 LAANZA RASMI, WAFANYIWA SHEREHE YA UKARIBISHO KIJIJI CHA MAKUMBUSHO DAR

0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri , Shindano hili litaruka katika  Runinga ya ITV Kila siku kuanzia 2.08.2015 -21.08.2015 saa 12 Jioni akicheza ngoma ya kwao wakati wakitambulishwa
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa hapo jana katika kijiji cha Makumbusho

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Angalia kipindi cha Nyumbani Na Diaspora cha wiki hii

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images