Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 922 | 923 | (Page 924) | 925 | 926 | .... | 3272 | newer

  0 0

  KATIKA hali ya kukabiliana na changamoto nyingi kwenye sekta ya bodaboda, kampuni ya mawasiliano na matangazo ya Alternative Communication ya jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania na Jeshi la Polisi wametengeneza mfumo salama wa kumbukumbu kwa waendesha bodaboda ili kuwasaidia bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.

  Hatua hiyo inakuja kufuatia madai kuwa baadhi ya waendesha bodaboda wasiokuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.

  Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Edward Mgaya amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili boda boda 3,000 katika mfumo huo. Ameongeza kwamba wale waliosajiliwa pia watapata faida ya kupewa huduma ya bima, mafunzo ya usalama barabarani na Ujasiriamali.

  Bw. Mgaya alisema wale wanaosajiliwa katika mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili mbele na nyuma ya koti, Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipiki pia kwenye kofia zao (helmet) itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha Waendesha Boda boda husika.

  “Mtu yoyote akiipiga namba ya chama cha waendesha boda boda na akataja namba ya usajili wa dereva wa bodaboda, mfumo utamtambua dereva huyo mara moja.

  Bw. Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Boda boda wa Kanda ya Tabata, ameelezea kufurahishwa na utaratibu huo mpya wenye faida kubwa kwao, na kwamba mfumo huo utaboresha usalama katika eneo lake.
  Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya Alternative Communication Bw. Edward Mgaya akizungumza na vyombo vya habari katika tukio la kuwakabidhi sare (Reflactors), waendesha boda boda zitakazosaidia kuwatambua katika mfumo maalum wa kompyuta. Mradi huu unaendeshwa na kampuni hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Vodacom na jeshi la polisi.
  Bw. Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Boda boda wa Kanda ya Tabata, akizungumza na waandishi wa habari namna alivyoupokea kwa furaha utaratibu huo.
  Waendesha boda boda wa Kanda ya Tabata wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa zoezi la kugawiwa sare (Reflactors) kwa ajili ya utambuzi.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisaini kitabu cha maombolezi katika ofisi za Ubalozi mdogo wa India Zanzibar, kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India, Avul Pakir Abdul Kalam kilichotokea Julai 27. (Picha na Salmin Said).

  Na Khamis Haji (OMKR).
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa India kufuatia kifo cha mwanasayansi aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Dk. Avul Pakir Abdul Kalam kilichotokea Jumatatu iliyopita.

  Ametuma salamu hizo wakati alipozungumza na Balozi mdogo wa India hapa Zanzibar, Satendar Kumar huko katika ofisi za Ubalozi huo Migombani, ambapo Maalim Seif alifika kusaini kitabu cha maombolezi.

  Maalim Seif amesema Kiongozi huyo ni msomi aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa la India hasa kutokana na mchango wake katika uvumbuzi wa vyombo vya anga za juu, kwa ajili ya matumizi ya kiraia na Kijeshi.

  Maalim Seif amesema bila shaka kifo chake kimeacha pengo na masikitiko makubwa sio tu kwa wananchi wa India, bali kwa jamii ya wasomi Duniani, na amewataka wananchi wa India kuwa na subira katika wakati huu mgumu wa maombolezi. 

  Abdulkalam (83) ambaye alipewa jina la umaarufu ‘mtu wa misaili wa India’ alishika nafasi ya Urais wa India mwaka 2002 kwa muda wa miaka mitano.

  0 0

    Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai kushoto akimkabidhi Jezi ya Klabu ya Coastal Union winga mpya wa Kulia,Ibrahim Twaha "Messi"mara baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.
   winga wa kulia Mpya wa Coastal Union Ibrahim Twaha " Messi" akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Coastal Union kulia ni Katibu Mkuu,Kassim El Siagi kushoto ni Meneja wa timu ya Coastal Union Akida Machai
  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kufanya usajili wa nguvu ili  kujiimarisha vilivyo katika safu mbalimbali ambapo jana ilifanikiwa kuingia mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili aliyekuwa winga wa kulia wa Simba, Ibrahim Twaha “Messi”
  Utiliaji saini wa mkataba huo ulifanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mjini hapa na kushuhudiwa na viongozi waandamizi akiwemo Katibu Mkuu Kassim El Siagi na Meneja wa timu hiyo,Akida Machai.
  Akizugumza mara baada ya kumalizika utiaji saini huo,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao hasa anapokuwa uwanjani .
  Alisema kuwa winga huyo ana vitu adimu ambavyo akishirikiana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika timu hiyo itakuwa chachu ya kuipa maendeleo timu hiyo katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
    “Niseme tu safari hii tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara na hili tunalifanya kuhakikisha tunarudisha kombe mkoani hapa ambalo tulilichukua mwaka 1988 “Alisema El Siagi.
  Kwa upande wake,Ibrahim Twaha “Messi”mara baada ya kusaini mkataba huo alihaidi kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika safari za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
    “Sasa ni kama nimerudi nyumbani kwa sababu awali nilikuwa naitumikia timu hii hivyo najisikia faraja kubwa kurudi tena Coastal Union mi nihaidi kushirikiana nao kwa lengo la kuipa mafanikio “Alisema Messi.
  Awali akizungumza,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiri kufanya usajili nzuri ambao utaiwezesha kutwaa ubingwa na kurudisha makali yao ya miaka ya nyuma.


  0 0


  Mchekeshaji maarufu Eric Omondi na bendi ya muziki ya SARABI kutoka Kenya wataungana na wanamuziki wa Tanzania Grace Matata na Leo Mkanyia na bendi yake ya Swahilli Blues kukonga nyonyo za mashabiki wa muziki na vichekesho jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho la muziki jumamosi wiki hii.
  Onyesho hilo ambalo limeandaliwa na CDEA:“Culture and Development East Africa” kwa kushirikiana na Nafasi Art Space litafanyika jumamosi ya tarehe moja mwezi wa nane mwaka huu, kuanzia saa moja jioni mpaka asubuhi katika ukumbi wa Nafasi Art Space-Mikocheni.

  Mratibu wa onyesho hilo Naamala Samson alisema kuwa mbali na onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kemkem kutoka kwa maDJ wa Santuri Safari kutoka Kenya na Uganda ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 10,000/- kupata burudani za muziki wa bendi na kwa wale watakaoingia kwenye disco la kukesha ni shilingi 20,000/-, na tiketi za V.I.P zitauzwa kwa shilingi 40,000/-.

  “Wanamuziki wote wamefanya mazoezi ya kutosha na wamejiandaa kikamilifu kwa onyesho hili la kihistoria, ni siku hiyo watanzania watapata fursa ya kuonja ladha ya muziki wa Afrika Mashariki wenye vionjo vya nyumbani na kupata vichekesho vya mwaka kutoka kwa Omondi” alisema Naamala.

  Bendi ya Sarabi ni miongoni mwa bendi kubwa na zinazofanya vizuri nchini Kenya na kuwepo kwake kwenye tamasha hili kutanogesha mambo na kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani.

  Tamasha hilo limedhaminiwa na Regency Park Hotel, Vibe Magazine, Bongo5.com, Michuzi Blog, Goethe Institut, Midundo Online Radio, CEFA, Timeticket, Nafasi Art Space, Eco Sanaa Arts Space, Creative Infinity, Kenya Airways, Apex Media, Iris Media, Kumkichwa Entertainment, Santuri Safari DJs na Legendary Music.

  0 0


  0 0

  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donard Ngoma akiichambua ngome ya Timu ya Azama, wakati wa Mchezo wao wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Kagame, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penati 5-4, baada ya kutoshana nguvu kwa dakika 90 za mchezo.
  Mshambuliaji wa Timu ya Azam, John Bocco akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya  Yanga, wakati wa Mchezo wao wa robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Kagame, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam imeibuka mshindi kwa mikwaju ya penati 5-4, baada ya kutoshana nguvu kwa dakika 90 za mchezo.
  Beki hodari wa Timu ya Azam, Pascal Wawa akiruka juu kuwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donard Ngoma.
  Beki wa Yanga, Juma Abdul akichezewa rafu na Mchezaji wa Azam, Frank Domayo.
  Beki wa Timu ya Azam, Pascal Wawa akiangalia wa kumpatia mpira mbele ya Mshambuliaji wa Yanga.


  0 0


  Balozi wa India nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa kazi, Mhe.Debnath Shaw akitoa hotuba yake ya kuaga mbele ya wageni waalikwa wakiwemo  baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2015.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini ambaye pia ni mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.Juma Halfan Mpango wakifuatilia hotuba ya Mhe.Debnath Shaw (hayupo pichani).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Wachunguzi toka ofisi 27 za Mikoa za TAKUKURU wanapata ujuzi kupitia mafunzo yenye kugusa masuala ya utakatishaji wa fedha, kupata taarifa na mlolongo wa uhalifu kwa kutumia sheria za sasa za Tanzania. 

  Mafunzo haya yamefadhiliwa na DFID kama sehemu ya Mpango wa Kuimarisha Mapambano dhidi ya Rushwa Tanzania (STACA) na inasimamiwa na Afisa wa Uingereza toka kitengo cha NCA, Bwana Phill Jones.
   Wachunguzi toka ofisi 27 za Mikoa za TAKUKURU wakimsikiliza kwa makini, Afisa wa Uingereza toka kitengo cha NCA, Bwana Phill Jones (aliesimama) wakati akitoa mafunzo hayo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA, SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wafanyabiashara wa ECG na Al Kan kutoka nchini Misri, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa ECG AL Kan kutoka nchini Misri, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015. Picha na OMR.

  0 0

  Na. Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Mnamo tarehe 28.7.2015 majira ya jioni JOSEPH ELIAZA CHILONGANI alifika katika kituo cha Polisi Kibaigwa akilalalmika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na JOB YUSTOO NDUGAI (MB).

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamiz wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchaguzi wa madaktari na matibabu. Amelazwa na anaendelea na matibabu hadi sasa, hali yake anaendelea vizuri. 

  Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
    Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Rufaa  ni  hatua  ya   kisheria  ambayo  hufikiwa  na  mhusika  katika  shauri  fulani  iwapo  hakurushishwa  na  maamuzi. Rufaa  sio  mpaka  uwe  umeshindwa  kabisa,  hapana. Yawezekana  ukawa  umeshinda  kesi  lakini  hukuridhishwa  na kiwango   ulichoshinda.Kwa  mfano  uliomba  wavamizi  waondoke  katika  nyumba yako   na  hapohapo  wakulipe  fidia. Mahakama  ikatoa  hukumu  kuwa  umeshinda  wavamizi  waondoke  katika  nyumba  yako  lakini  ikasema wasikulipe  fidia.

  Mazingira  kama  haya  unakuwa  umeshinda  lakini  ukitaka  unaweza  kukata  rufaa  kulalamikia kutolipwa  fidia.  Kwa hoja  hii  tunaona  kuwa kumbe  kukata  rufaa  si  lazima  uwe  umeshindwa  badala  yake unaweza  kuwa umeshinda  lakini  ukawa  hukuridhishwa  na  vitu  fulani  katika  hukumu  ambavyo  unaweza  kuvikatia  rufaa  ili  navyo  uvipate. 

  1.AINA  ZA  RUFAA  KATIKA  MASHAURI  YA  ARDHI.

  Kisheria  rufaa  hutofautiana  kutokana   na  aina  ya  mgogoro  ulio  mbele. Mgogoro  wa  kimkataba  unazo  namna  zake   na  masharti yake  katika  rufaa, halikadhalika  migogoro  ya  kudai  fidia, migogoro  ya  kikazi, migogoro ya  kifamilia  na  talaka, migogoro  ya  jinai,  migogoro  ya  kibiashara n.k.  Hii  ina  maana  hata  migogoro  ya  ardhi  nayo  inazo  namna  zake  za  rufaa. Katika  mashauri  ya  ardhi   mara  nyingi  migogoro huanzia  baraza  la  ardhi  la  kata huenda  mabaraza  ya  ardhi  ya  wilaya, mahakama  kuu  ya  ardhi   hadi  mahakama  ya  rufaa.  

  Hizi  zote ni  mamlaka  zinazoweza  kuamua  mashauri  ya ardhi.  Aidha  aina  za  rufaa  huweza  kutokana  na  mpangilio huu  kimahakama. Ipo  rufaa  inayotoka  baraza  la ardhi  la  kata  kwenda  baraza  la  ardhi la wilaya. Ipo  rufaa  kutoka  baraza  la  ardhi  la  wilaya  mpaka  mahakama  kuu  ya  ardhi. Na  ipo  itokayo  mahakama  kuu  ya  ardhi  mpaka mahakama  ya  rufaa.  0 0

  Kwaya ya Gracias kutoka Korea ikitumbuiza katika kambi ya Vijana iliyomalizika jana katika viwanja vya mikutano vya Mlimani City.Kambi iyo mwaka huu imefanyika nchini ikijumuisha vijana elfu tatu duniani kote.
  Mkurugenzi msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Bi. Esther Riwa akiongea na Vijana mbalimbali baada ya Kuwapa somo kuhusu kuwa na Fikra Chanya ili kujiletea maendeleo na Stadi za Maisha.Vijana hao wameweka kambi katika Viwanja vya mikutano vya mlimani city jijini Dar es Salaam wakijifunza mambo mbalimbali.
  Naibu katibu mkuu kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Elisante Ole Gabriel akizungumza na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Vijana Duniani Bw Ock Soo Park katika Viwanja vya Mlimani city alipokuwa akifunga kambi ya Vijana yenye kauli mbiu Badilisha Fikra iliyoshirikisha vijana elfu tatu kutoka duniani kote.
  Naibu katibu mkuu kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akiwa katika majadiliano na viongozi wa mbalimbali wa Taasisi ya kimataifa ya Vijana Duniani,Kushoto kwake ni Mwanzilishi wa Taasisi iyo Bw Ock Soo Park na kulia kwake ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya maendeleo ya Vijana kutoka Wizara iyo Bi Esther Riwa.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
   Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akiwasili ofisi za Makao makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar,akiwa ameambatana na Mh Lowassa (hayupo pichani),kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.
    Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
  Rabsha za hapa na pale zilikuwepo kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya CHADEMA  yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
   Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 
   Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Raia wa kigeni wajaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wafikia 2040 kwa mikoa ya  mikoa ya Kagera watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65. 
  Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao  jijini Dar es Salaam leo.

   Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa.

  Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.
    
   Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale.

  Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na wahamiaji haramu wanayo jiandikisha katika  Daftari la wapiga kura katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
  Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa uhamiaji wilaya ya Iala, Safina Muhindi,katikati ni Afisa  uhamiaji wilaya ya Temeke, Jaffari Kisesa na Afisa Mdhibiti wa Paspoti, Cripin Ngonyani wakimsikiliza Kaimu kamishina wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Da es Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya jijin Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  It is true that for more than a century, Africa's best natural resources have found their way to Europe and America, under various circumstances, some positive, and others not. These include minerals resources in Africa's spoil, and human talent, who were nourished from food grown on Africa's soil.
  Today, many Africans are distinguishing themselves in various fields in the new world of Europe, Africa, Australia and Asia. One of such, who has made regional and global headlines throughout most of the last 20 months is 12 year old Nigerian girl - Zuriel Oduwole.
  She is the youngest person in the world to be featured in Forbes Magazine at age 10 in 2013, the youngest person in the world to meet and interview more than 15 World leaders [Presidents & Prime  Ministers], the youngest person in the world to be featured in ELLE Magazines Global 33 Women's List, the youngest person in the world to self produce and show their Film in commercial cinema chains, the only African to make Business Insiders Global Powerful 100 list, the youngest person in the world to address more than 23,000 children in 9 countries on Education issues, the youngest business and feature guest on global networks CNBC, CNN African Voices, BBC Africa andBloomberg TV, and now comes her newest new accolade.
  Zuriel has now made her film Directorial debut in Hollywood, calling the shots for a project made on the Disney Studios in California [see attached picture]. At 12 years old, she is the youngest African to accomplish this. She then went on to direct a new Girls Confidence documentary for Procter & Gamble's Always brand in New York a few days ago, and spoke also at the new #LikeAGirl Global Conference in New York.


  With youths like Zuriel, Africa truly Rises!!

  0 0


   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza    warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti 


   mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari
   Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao.

  0 0

  Wakazi wa Kata ya Kimbiji,Wilaya Temeke mkoani Dar-es-Salaam wamefunguka tena kwa kumpendekeza na kumtaka Diwani wao Mheshimiwa Muhidini Bunaya Sanya kugombea tena nafasi ya udiwani wa Kata hiyo ya Kimbiji hiliyopo wilaya Temeke. Wananchi wa wamemtaja Diwani wao huyo kijana Muhidini Bunaya Sanya kuwa ni mchapa kazi,mbunifu na mpenda maendeleo mwenye uchungu na Kimbiji. 

  Wakazi wa Kata ya Kimbiji wanawaomba wananchi wote kusimama bega kwa bega kwa kumpa kura zote za maoni Bwana Muhidini Bunaya Sanya ili aweze kututumikia tena katika nafasi ya udiwani na kutuwakilisha katika baraza la madiwani la wilaya ya Temeke. Pendekezo la kata ya Kimbiji Muhidini Bunaya Sanya aka Jembe La Pini wa Chuma Usikose kuungana na wanakimbiji at www.facebook.com/wanakijiji.kimbiji

older | 1 | .... | 922 | 923 | (Page 924) | 925 | 926 | .... | 3272 | newer