Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 90 | 91 | (Page 92) | 93 | 94 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na John Nditi, Morogoro

  JAJI Mstaafu Ernest Mwaipopo (63) amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Aprili 3, mwaka huu eneo la Kijiji cha Mkata , Kata ya Doma, Wilayani Mvomero katika barabara kuu ya Iringa – Morogoro anataeajiwa kuzikwa Jumamosi , Aprili 6, mwaka huu kijijini kwao Ibatu, wilayani Mifundi, Mkoa wa Iringa.

  Hata hivyo , Jaji Mstaafu huyo alikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa tume ya kurekebisha sheria. Mtoto wa pili wa Marehemu Jaji Mstaafu Mwipopo (63) , Angaza Mwipopo amesema hayo wakati wa kuagwa kwa mwili huo mjini Morogoro na kusafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa mwanae huyo, mwili wa marehemu utazikwa Jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu katika Kitongoji cha King’ola, Kijiji cha Ibatu, wilayani Mufindi, Mkoani Iringa.

  Mwanae huyo ambaye ni mwanasheria ,mwili wa marehemu umesafirishwa mchana wa leo kutoka Morogoro na ulipagwa kufikishwa Hospitali ya Jeshi la Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaliwa vyema na kupelekwa nyumbani kwake Ostabey kuangwa rasmi siku ya Ijumaa na kuondoka siku hiyo hiyo kwenda wilayani Mufindi kwa ajili ya maziko.

  Awali , Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa kifo cha Jaji Mstaafu huyo kilitokea Aprili 3, mwaka huu kuwa wakati akisafiri na gari lenye namba za usajili T 691 AUL aina ya Toyota Land Cruser iliyokuwa ikiendeshwa na Dereva Chafasi Mgohamwende ( 38) mkazi wa Kawe , Jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ajali hiyo ilitokea majira ya , saa 7:30 mchana , wakati akitokea Wilayani Mafinga Mkoa wa Iringa kuekeleza Jijini Dar es Salaam.

  Alisema ,chanzo cha ajali hiyo ni baada ya kupasuka matari mawili moja la nyuma kushoto na kuyumba na baadaye kupasuka jingine la mbele upande wa kulina na liliacha njia na kupiduka na kusababisha kifo cha Jaji Mstaafu mkazi wa Ostabey , Jijini Dar es Salaam ambaye alifarki dunia papo hapo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wakisaidiana na wananchi kuingiza mwili wa Jaji Mstaafu , Ernest Mwipopo kwenye gari tayari kwa kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.
  Akina mama wakijawa na huzuni juu ya kifo cha Jaji Mstaafu Mwipopo.
  Baadhi ya watumishi wa Idara ya Mahakama Mkoa wa Morogoro wakijumuika na watu wengine eneo la viwanja vya jengo la kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa,Morogoro.
  Dada wa Marehemu Jaji Mwipopo, Mrs Grace Mnyanyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera.
  Mtoto wa pili wa kiume wa Jaji Mstaafu Mwipopo , Angaza Mwipopo akizungumza na simu kuwafahamisha ndugu waliokuwa nje ya Morogoro kuhusu maendeleo ya maandalizi ya mazishi.
  Mwinjilisti Steven Banzi wa Kanisa kuu Bungo la KKKT Dayosisi ya Morogoro akiendesha sala kabla ya kuondoka na mwili wa Jaji Mstaafu Mwipopo kwenda Dar es Salaam.
  RC Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akizungumza na simu, anayemfuatia ni RPC Morogoro, Faustine Shilogile wakiwa nje ya viwanja vya jengo la kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa,Morogoro.

  0 0

  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kulia), akizungumza wakati mkutano na wanachama wa NMB Business Club, Kanda ya Temeke, uliofanyika leo, Mbagala, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ezekiel Gutti, Meneja wa Mikopo Midogo Midogo ya Biashara wa benki hiyo, Mashaga Changarawe na Loelia Kibassa ambaye ni Meneja wa Mikopo ya Kati ya Biashara. 
   Mwanachama wa NMB Business Club Kanda ya Temeke, Hermetus Urassa akichangia mada wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa NMB Business Club Kanda ya Temeke, Ezekiel Gutti akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wanachama wa club hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Mikopo Midogo Midogo ya Biashara wa benki hiyo, Mashaga Changarawe na Meneja wa Mikopo ya Kati ya Biashara,  Loelia Kibassa.
   Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika warsha hiyo.
   Mmoja wa wajasiriamali akichangia mada.
   Meneja wa NMB tawi la Temeke, Halord Lambileki akiwa maofisa wa NMB. 

  0 0

  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinasikitika kuwajulisha wadau wake kuwa bonanza la wanahabari lililopangwa kufanyika kesho viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe sasa litafanyika viwanja vya Leaders Klabu, Kinondoni Dar es Salaam siku hiyo hiyo ya Aprili 6,2013.

  Uamuzi huo wa kushtukiza umefikiwa kwenye kikao cha dharura kilichofanyika jana usiku kati ya TASWA ambao ni waandaaji na wadhamini wa bonanza hilo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutokana na kushindwa kuafikiana baadhi ya mambo na menejimenti ya viwanja hivyo.

  Tunawaomba sana radhi wanahabari kwa usumbufu mkubwa ambao wataupata kutokana na mabadiliko haya, lakini tunaamini yamefanyika kwa dhamira nzuri yenye nia ya kuboresha bonanza letu na kwa kiasi kikubwa litafana kwa asimilia 100.

  Dhamira ya TASWA ni kuona inakuwa na bonanza zuri lisilokuwa na aina yoyote ya kwikwi, hivyo tayari tumeshamalizana na menejimenti ya viwanja vya Leaders Klabu na kila kitu kitakuwa safi kuliko maelezo.

  Pia tunaishukuru menejimenti ya viwanja vya Sigara kwa ushirikiano iliotupa kwa nia ya kufanya bonanza hilo eneo lao, ingawa ndoto zetu hazikutumia, lakini tunaamini siku za usoni tunaweza kufanya nao kazi.

  Tunasisitiza lengo la bonanza letu ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.

  Awali bonanza letu ilikuwa lifanyike Leaders Klabu, lakini tulilihamishia viwanja vya Sigara kutokana na wadau wengi kuomba wapate nafasi ya kwenda kutazama mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers ya Liberia kesho. Hata hivyo tunaamini wahariri wa habari za michezo watajipanga vizuri kulingana na mabadiliko hayo na hakuna litakaloharibika.

  Pia katika kuboresha bonanza hilo litakalotumbuizwa na bendi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern, kutafanyika mchezo wa soka kati ya wanahabari ambao wameoa na wale ambao hawajaoa utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida baina ya vyombo vya habari kumalizika.

  Bonanza litaanza saa tatu asubuhi kwa washiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, wavu, kuruka kichura, aina mbalimbali za riadha, kuvuta kamba na kucheza muziki. Bonanza litamalizika saa moja usiku.

  Ahsanteni.

  Amir Mhando 
  Katibu Mkuu TASWA 
  05/04/2013

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo April 5, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji ndugu wa marehemu baada ya kutoa heshima za mwisho, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo April 5, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
  Picha ya Marehemu Jaji Mstaafu Ernest Mwipopo

  Majaji wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, wakishusha katika gari kwa ajili ya kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee, leo.
  Mmoja wa wanafamilia akibugujikwa machozi wakati wa shughuli hiyo ya kuaga.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee leo kushiriki kwenye shughuli za kuaga mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Jaji Mkuu Kiongozi na Jaji Mkuu wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga mwili.Picha na OMR

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama (Katikati) akipata maelezo ya Kituo cha Kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kutoka kwa Mtaalamu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Aliyesimama nyuma ya mkuu wa mkoa mwenye miwani ni mkuu wa chuo hicho Dk. Richard Masika.


  Na Mwandishi Wetu,Hai.

  Chuo cha Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na umeme mwingine kubaki.

  Ufafanuzi huo umetolewa na  mkuu wa Chuo hicho Dk Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)

  Alisema kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja na kuzalisha umeme.

  Dk Masika ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.

  “Kiasi hicho kitaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na kiasi kingine kubaki,”

  Akifafanua zaidi alisema kuwa kituo hicho ambacho kilijengwa mwaka 1930 kwa sasa kina mashine tatu ambazo zilikufa na kuacha kuzalisha umeme mwishoni mwa miaka ya Themanini zikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme kati ya megawati moja na moja na nusu.

  Dk Masika ameeleza kuwa mashine mbili kati ya hizo tatu chuo chake kina uwezo wa kuzifufua na kuanza kufua umeme utakaoingizwa katika gridi ya taifa wakati chuo chake kikiendelea na mkakati wa mpango mkubwa wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya kisasa

  Kwa upande wa mafunzo,Dk Masika ameeleza kuwa cuo hicho kimelenga kutoa idadi kubwa ya wataalamu wafanyakazi ambao wenye taalamu ya stashahada ambao kwa kawaida ndiyo wacahapa kazi ili kuzipa pengo la sasa la idadi kubwa kukimbilia katika shahada na baada ya kuhitimu kwa wasimamizi na si wachapa kazi

  Alisema kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na kuongezeka wakati wa kiangazi

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme.

  Alisema kuwa ni vyema sasa wakatambua kwamba taifa limewapa dhamana kubwa kwa kuwakabidhi raslimali kubwa ambayo inatakiwa kusimamiwa vyema kwa ajili ya manufaa ya watanzania na siyo ya watu binafsi.

  Gama aliwataka kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji yanayotumika katika mitambo hiyo vya Chemka kilichopo wilayani Hai na cha Mto Mbuguni ambacho kipo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

  Alisema kuwa uongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro unakiweka kituo hicho katika miradi yake mikubwa ya kimkoa na utakuwa tayari kikusaidia chuo hicho wakati wowote kitakapohitaji msaada wa hali na mali.

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.

  Alisema kuwa kutokana na mazingira yanayozunguka kituo hicho kutunzwa vizuri katika miaka yote tangu uzalishaji uliposiamama,mara nyingine wakati wa ukame mkali baadhi ya wenyeji ujaribu kuingiza mifugo kwa ajili ya kupata malisho na hivyo kusababisha vurugu.

  Makunga alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa nguvu

  0 0

   Mkurugenzi wa Hoteli ya Sapphire Court ya Jijini Dar es Salaam, Abdulfatah Salim (kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo, Nahodha wa timu ya wamiliki wa Magazeti 'Tando' Blogers Fc, Muhidin Sufiani, ambaye ni mmiliki wa mtanda wa www.sufianimafoto.com, kwa ajili ya kushiriki katika Bonanza maalum la waandishi Medi Day linalofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni kesho. Katikati ni Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki Mroki. Timu hiyo ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika michezo na bonanza kama hilo, inatarajia kushiriki katika michezo yote itakayo chezwa hiyo kesho, ikiwa ni pamoja na Soka, Netiboli, Kukimbiza Kuku, Kukimbia na Magunia, Kuvuta Kamba, Kucheza Pool, Kuimba na Kudansi 'Sebene' na mingineyo.
   Makabidhiano yakiendelea, hii ni Jezi ya Kipa.
  Nahodha wa timu hiyo Sufianimafoto (kushoto) akiwa na Meneja wa muda wa timu hiyo, Mroki Mroki, wakiwa na Vifaa vilivyokabidhiwa.
  *************************************** 
  HOTELI ya Sapphire Court iliyopo makutano ya mitaa ya Swahili na Lindi, Dar es Salaam leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya wamiliki wa magazeti tando (Blogers FC) kwa ajili ya Bonanza la Media Day, linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.


  Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Sapphire, hoteli iliyojizolea umaarufu mkubwa kwa sasa nchini, Abdulfatah Salim Saleh amesema ameamua kukabidhi vifaa hivyo ili kuunga mkono timu hiyo mpya inayoanzishwa katika tasniya ya michezo nchini.


  “Nilipopata ombi lenu, sikutaka hata kujifikiria, nilisema nitawasadia, na huu ni mwanzo tu. Naahidi kushirikiana nanyi zaidi na zaidi na ninawakaribisheni wakati wowote, mimi ni shabiki wa timu yenu kuanzia sasa,”alisema. Kwa upande wake, Meneja wa Muda wa Blogers FC, Mroky Mroky alisema kwamba wanashukuru kwa msaada huo na wanaahidi kudumisha uhusiano mzuri na Sapphire.

  “Wazo hili la kuanzisha timu ni la muda mrefu, lakini lilikuwa likisuasua, ila tukaamua kwa vyovyote lazima tutokee kwenye Media Day ya mwaka huu. Tulipofikiria suala la wapi tutapata vifaa vya michezo, vichwa vilituuma kidogo, lakini tunashukuru Sapphier wametuliza maumivu hayo,”alisema Mroky.


  Naye Nahodha wa Blogers FC, Muhiddin Sufiani amesema kwamba baada ya kupata vifaa hicyo kesho wanatarajia kuanza kuonyesha cheche zao kesho katika Bonanza la Media Day, lengo likiwa ni kubeba ubingwa upande wa soka na kutwaa pia mataji mengine madogo madogo. 
       

  Miongoni mwa wachezaji nyota wanaotarajiwa kuichezea Blogers FC kesho ni Issa Michuzi, Majjid Mjengwa, Sufiani mwenyewe, Majuto Omary, Joseph Lukaza, Shaffi Dauda, Saleh Ally, Mahmoud Zubeiry, Millard Ayo na John Bukuku.


  Bonanza la wanahabari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), litafanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders, chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Pamoja na wanahabari kuchuana katika michezo mbalimbali, lakini Bonanza hilo pia litapambwa na burudani ya bendi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern.

  Kutakuwa pia na mechi maalum baina ya wanahabari ambao wameoa na wale ambao hawajaoa utakaofanyika baada ya michezo ya kawaida baina ya vyombo vya habari kumalizika.


  Bonanza litaanza saa tatu asubuhi kwa washiriki kucheza michezo mbalimbali ikiwemo soka, netiboli, wavu, kuruka kichura, aina mbalimbali za riadha, kuvuta kamba na kucheza muziki. Bonanza litamalizika saa moja usiku.   


  0 0

  Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiongozwa na Askari polisi kuingia katika Mahakama Kuu ya Zanzibar  kusikiliza kesi inayomkabili.
   wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) kulia akizungumza na mawakili wake Abdalla Juma kushoto na Rajab Abdalla muda mfupi baada ya kutajwa kwa kesi yake Mahakamani hapo. 
   Mawakili wanaomtetea Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri , Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) wakili Abdalla Juma (kulia) na Rajab Abdalla wakiwa mezani pao  kabla ya kutajwa kwa kesi ya mteja wao katika mahakama Kuu Vuga mjini Zanzibar
  Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake kutajwa mahakamani hapo.
   Picha zote na Haroub Hussein

  0 0
  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Capt (Mstaafu) George Mkuchika akifungua semina ya siku moja kwa waheshimiwa wabunge wanachama wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Rushwa Tanzania (APNAC) iliyfanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa APNAC Tawi la Tanzania Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
  Mkurugenzi Mkuu wa Taaisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (PCCB) Dkt. Edward Hosea akiwasilisha mada kwa waheshimiwa Wabunge wakati wa Semina hiyo.
  Meza kuu na waheshhimiwa wabunge wakifuatilia mada
  Meza Kuu wakisikiliza kwa makini baadhi ya hoja kutoka kwa wabunge wakati wa semina hiyo


  0 0

  Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge, ( kushoto) akifuatilia mada moja wapo zilizowasilishwa na wataalamu wa Shirika la Tanapa ,( hawapo pichani) jana wakati wa mkutano wa wadau wa uhifadhi Kanda ya Mashariki ulioandaliwa na Shirika hilo na kufanyika Aprili 3 hadi 4 , mwaka huu mkoani Morogoro ( kati kati) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi , (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, mkutano huo wa siku mbili uliwashirikisha pia wakuu wengine wa mikoa, wilaya, wabunge na wakurugenzi watendaji wa Halmashauri kadhaa nchini.Mkutano huo wa kanda ya mashariki ulioitishwa na Tanapa uliwashirikisha wadau mbalimbali wa Mikoa inayounda Kanda hiyo ya Tanapa , ambayo ni Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe na Pwani sambamba na Wakuu wa Wilaya wa baadhi ya Mikoa hiyo , Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri hizo , wabunge na maofisa wingine wa Tanapa na ulilenga kuzungumzia masuala la ujirani mwema kati ya mamlaka za Serikali, Halmashauri na viongozi wa kisiasa katika kuboresha sekta ya Uhifadhi. ( Picha na John Nditi).
  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, mkoa wa Dodoma , Fatma Ally ( kulia) akiteja jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wakati wa mkutano wa ulioandakiwa na TANAPA uliofanyika Aprili 3, 2013.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahemed Kipozi akiwasikiliza wanataaluma wenzake wakati wa mkutano wa Tanapa.

  0 0

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shimo la Udongo Kata ya Kurasini Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Issa Chigona akizungumza na wananchi wa Mtaa huo kabla ya kufanyika kwa mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa ili kuwachagua wananchi watakaopendezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya leo.
  Wakazi wa Mtaa wa Buza, Kata ya Buza Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam wakifuatilia kwa makini kikao cha mkutano mkuu maalum wa Mtaa kwa ajili ya kuchagua wananchi watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya katika Mtaa huo leo.
  Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni Kata ya Kurasini Wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, aliyewania nafasi ya uwakilishi wa Vijana katika Mikutano wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Sophia Stephen akijinadi mbele ya wananchi wa mtaa huo kabla ya kufanyika kwa kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa ili kuwachagua wananchi watakaopendezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya katika Mtaa huo leo
  Wagombea wa nafasi za uwakilishi wa wanawake katika kikao cha Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa Mtaa wa Buza Kata ya Buza Wilayani Temeke Mkoani Dar e Salaam wakionyesha nambari zilizotumika kuwachagua wananchi waliopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kikao hicjo kilifanyika katika shule ya Msingi Buza leo.
  Wananchi wa Mtaa wa Buza Kata ya Buza Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam wakipiga kura za kuwachagua wananchi watakaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa huo uliofanyika katika Shule ya Msingi Buza leo.

  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Mohammed baada ya kuwasilili jioni hii kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo mjini Moshi. Kesho Nape anatarajiwa kufungua semina ya Halmashauri Kuu ya Mkoa huo ya CCM na baadaye kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Moshi.
   Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi (wapili kushoto) akimtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo, Frederick Mushi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Elizabeth Minde.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akivishwa skafu na Kijana wa CCM baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanajro mjini Moshi jioni hii.
   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kucharaza ngoma, iliyokuwa inapigwa na kundi la sanaa la CCM, baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro jini Moshi jioni hii.
   Katika ziara hiyo Nape ameambatana na Vijana waliojiengua hivi karibu kutoka Chadema, Mtela Mwampanga na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Juliana Shonza. Pichani, Mwampamba na Shonza wakisalimiana na vijana wenzao ambao pia wamehamia CCm hivi karibuni kutoka Chadema mkoani Kilimanjaro, David Waryoba (kushoto) na Yona Makwaya (wapili kushoto)
  Vijana wakimsubiri Nape kwa shauku alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii.
  Nape akitia saini kwenye kitabu cha wageni, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Iddi Mohammed.Picha zote na Bashir Nkoromo.

  0 0

  Jengo moja la ghorofa nane linalosemekana lilikuwa likijengwa kinyume cha sheria limeporomoka na kuua watu 47 na kujeruhi wengine 70 jijini Mumbai, India siku ya Alhamisi jioni. 

  Waokoaji wakiwa na nyundo, misumeno, jeki na bulldozer zipatazo sita walikuwa wakijitahidi kunasua walionasa kwenye jengo hilo lililo maeneo yam situ liiltwalo Thane.

   “Kuna uwezekano kuna watu wamenasa katika kifusi” Kamishna wa Polisi wa eneo hilo Bw. K.P. Raghuyanshi amesema leo mchana. 

  Wakati linaporomoka inasemekana ndani ya jengo hilo mlikuwa na watu kati ya 100 na 150, wengi wakiwa ni wakazi wa humo mjengoni na wengine wajenzi. Zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo hadi sasa, kwa mujibu wa Bw. R.S. Rajesh, afusa wa kitengo cha majanga na uokoaji. Waliokufa ni pamoja na watoto 17. 

  Ghorofa nne za jengo hilo zilikuwa zimeshamalizika kujengwa na watu walikuwa wanaishi humo, ambapo wajenzi walikuwa wakimalizia ghorofa zingine tatu na walikuwa katika kuongezea ya nane ndipo lilipobumburuka.
  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Dkt Narriman Jiddawi juu ya Utunzaji wa Samaki Aquarium wakati wa Ziara ya waziri huko Zanzibar
  Kaimu Mkurugemzi waTaasisi ya Sayansi ya Bahari ya chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt Christopher Muhando akimtembeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Jengo la Taasisi ya Sayansi ya Bahari huko Chukwani Mjini Unguja wakati wa Ziara yakutembelea taasisi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mhadhiri Mwandamizi wa Tasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chua Kikuu cha Dar es Salaam Dkt NarrimanJiddawi akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan aina ya Kasa katika chumba cha Kutunzia samaki[AQUARIUM}wakati wa Ziara ya Kutembelea Tasisi za jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizopo Unguja.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo juu ya Ujenzi wa Kituo cha tasisi ya Sayansi za Bahari kilichopo Chukwani Unguja kwa Kaimu Mkurugenzi Dkt Christophet Muhando wakati waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Tasisi za Jamhuri za Muungano wa Tanzania zilizopo Unguja.PIcha na Ali Meja.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa sensa ya watu na makazi Waziri Mkuu Pizengo Pinda akijadiliana jambo pamoja na Kamishna wa Sensa ya watu na Makazi Tanzania Bara Hajat Amina Mrisho wakati wakiangalia Ripoti ya idadi ya watu kwa ngazi ya Utawala hapo Hyatt Legency Kilimanjaro Hoteli Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa sense ya watu na makazi Waziri Mkuu Pizengo Pinda akizindua Ripoti Ripoti ya idadi ya watu kwa ngazi ya Utawala hapo Hyatt Legency Kilimanjaro Hoteli Jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa sensa ya watu na makazi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na uongozi wa Juu wa Kamati ya Sensa nje ya Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Legency Kilimanjaro Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli. akiongea leo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo lilikoporomoka ghorofa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo, akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka. 

  Kamati hiyo imeziamuru halmashauri za Wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni kufanya tathmini ya majengo yote na kuchukua hatua mara moja zitapogundulika zimejengwa chini ya kiwango.
  Tayari watu 11 wanaotuhumiwa kuhusika katika ujenzi wa ghorofa lililoporomoka wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kuua bila kukusudia 
   
   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka akiwa eneo la jengo lilioporomoka. Nyuma yake ni jengo ambalo linajengwa na mjenzi yule yule aliyejenga liliporomoka. Kamati hiyo imetoa siku nne kwa mjenzi kubomoa jengo hilo ambalo linasemekana nalo limejengwa chini ya kiwango. 
   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk TerezyaHuvisa wakimsikiliza   Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
   Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa AnnaTibaijuka  na  Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.
    Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli akijadili jambo na Bw. Azim Dewji pamoja na mjumbe wa kamati Mhe Zakhia Meghji. Picha na mdau Sujit Bhojak

  0 0


  Habari Wadau,
  Napenda kuwafahamisha juu ya Blog mpya ya Habari za michezo na burudani kwa ujumla wake. Humu utapata updates za mambo mbalimbali kitaifa ikiwa ni habari kutoka karibu mikoa yote ya Tanzania na kimataifa.


  KARIBUNI WOTE

  Reuben Mchome,
  Presenter - ITV/RADIO ONE

  0 0  0 0

  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu Kaskazini mwa Tanzania ikitapakaa  katika mikoa ya Mara na Arusha.  Eneo lake ni kilomita za mraba 14,763  na kijiografia inaendelea kidogo ndani ya Kenya katika Hifadhi ya Masai Mara. 
  Katika hiifadhi ya Serengeti  kuna idadi kuba ya wanyama  pori. Serengeti inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, twiga , kifaru na nyati. 
  Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya wanadamu wa kale kabisa yalipatikana liko ndani ya Serengeti. Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia iko katika kaskazini-magharibi ya Tanzania na inaenea kwa kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. 
  Ina eneo la  mraba kilometa 30,000 2. Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi dunian, na hua ni tukio la nusu mwaka. Uhamiaji huu ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu. 
  Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai, yaani "Serengit" kumaanisha "mbuga isiyoisha". Mnamo mwezi wa Oktoba, karibu herbivores (yaani wanyama wanaokula majani badala ya nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. 
  Katika mwezi wa Aprili, wanyama hao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena huvuka Mto wa Mara. Jambo hili kwa mara huitwa "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu takriban 250,000 hufa safarini wakati wa uhamiaji huu. 
  Vifo hivyo mara nyingi husababishwa na kuliwa na wanyama wakali ama uchovu. Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.Kwa mnaopenda utalii wa ndani si vibaya mkapanga kutembelea hifadhi ya Serengeti
  Tembo wakiwa Serengeti
  Simba wakila pozi
  Swala
  Hawa hawana mchezo na mtu...
  Pundamilia

older | 1 | .... | 90 | 91 | (Page 92) | 93 | 94 | .... | 3283 | newer