Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

MWANAHABARI GODWIN GONDWE "DOUBLE G" AJITOSA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA JIJINI MWANZA


MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA SERIKALI ZA MITAA MTWARA

$
0
0
LAPF inawakaribisha wana mtwara kutembelea banda lao ili waweze kupata huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufahamu juu ya huduma mpya zinazotolewa na LAPF kama vile mkopo wa kujikimu, Mafao ya Uzazi na mkopo wa elimu.

Pia wanachama watapata fursa ya kuangalia taarifa za michango yao, kujiunga LAPF na kupata vitambulisho.

Katika picha ni maafisa wa LAPF wakitoa huduma kwa wanachama waliotembelea banda hilo.
 Wananchi wa Mtwala wakitembelea maanda ya mfuko wa pensheni wa LAPF, Mtwara.
Wananchi wakipata maelekezo walipotembelea banda la  mfuko wa pensheni wa LAPF walipohudhuria maadhimisho ya wiki ya serikali za mitaa Mtwara.

MAGUFULI AZOA WANACHAMA WAPYA KIBAO ALIPOKUWA AKIWASHUKURU NA KUWAAGA WAKAZI WA MJI MDOGO WA MUGANZA WILAYANI CHATO LEO

$
0
0
   Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM,jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza,wilayni Chato Mkoani Geita,Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150.
  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM,jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza,wilayni Chato Mkoani Geita,Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150.Mh Magufuli yuko jimboni kwake Wilayani Chato kuwaaga na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge.  


   Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono pia na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge wao. 
   MKe wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji huo kwa mapokezi mazuri na makubwa waliyoyapata wilayani humo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara),Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza wilayani Chato mkoa wa Geita.
  Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao na pia kuwashukuru kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 ya Ubunge ndani ya jimbo hilo.
  Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo.
    Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo wakishangilia kwa  furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.


WILAYA ZA ARUSHA ZAONGOZA KWA WAGONJWA WA TRAKOMA

$
0
0
  Mratibu wa Mpango wa kitaifa wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele dkt. Upendo Mwingira, akionesha fulana yenye ujumbe wa kutokomeza magonjwa hayo toka shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani la Ending Negleted Diseases,walokuja nchini tanzania kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoani Arusha
 Mratibu wa Trakoma toka hospitali ya KCMC Patrick Masae akifanya uchunguzi wa macho kwa wananchi wa kata ya Sinya na Tinga Tinga wilayani Longido
 Wanafunzi wa shule ya msingi sinya wakiwaonesha wageni (hawapo pichani) jinsi wanavyotumia kibuyu mchirizi kwa kunawa hii ni mojawapo wa mkakati wa usafi wa mazingira na kuimarisha usafi wa kunawa mikono na usi kutokomeza ugonjwa wa trakoma, upate 

FILIKUNJOMBE ALIPOCHUKULIWA FOMU NA WAZEE ILI KUWANIA UBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA KUPITIA CCM

WAZIRI MKUU PINDA ASALIMIANA NA ALIYEKUWA MBUNGE WA MPANDA KATI KWA CHAMA CHA CHADEMA MH.ARFI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Mpanda  Kati  kwa tiketi ya CHADEMA, Said Arfi mjini Mpanda  Julai 21 2015. MheshiMiwa Pinda yuko  Katavi kwa mapumziko mafupi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Kiboko akiwa  amejeruhiwa vibaya baada ya  kushambuliwa na Simba na kukimbilia mtoni katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi Julai 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
Mamba wakiwa katika hifadhi ya Katavi Julai 21, 2015

SIMBA SPORT CLUB YAZINDUA MKAKATI UITWAO MABALOZI WA SIMBA

$
0
0
Balozi wa Simba Octa Mshiu akipokea Hati ya Ubalozi kutoka kwa Rais wa Simba Evans Aveva. Anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Imani Kajula  

Dhima yetu ya kuendeleza mabadiliko  ndani  ya Simba bado inaendelea kushika kasi, Katika  kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa, kujali  wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya  mapato.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika kukuza wigo wake wa kuwashirikisha wapenzi wake katika kuleta maendeleo ya klabu Simba Sports Club inazindua makakati wa kuwashirikisha wapenzi wenye nia ya kuwa chachu ya maendeleo kwenye klabu yao. Simba ni klabu ya wanachama na wapenzi wa Simba, hili  ndilo jambo la msingi
na kujivunia  zaidi. 

Kwa msingi huu wigo wetu wa wapenzi nimtaji muhimu katika kuetekelezamalengo mbalimbali  ya klabu ya Simba. Hivyo basi leo hii klabu ya Simba inazindua rasmi  Mabalozi wa Simba, hawa  ni  wapenzi  wa Simba ambao wako tayari kushirikiana na klabu katika kuleta maendeleo ya  klabu  yetu’’.Aveva aliendelea kusema ‘’ Katika ahadi zetu wakati wa uchaguzi tuliahidi kuwa tumenuia kwa dhati kuleta mapinduzi  ya kimaendeleo  ndani ya Simba. 

Napenda kusema safari yakuendelea  kuifanya Simba kuwa klabu bora ndani na nje ya uwanja imepamba moto. Kwa uhakika malengo mengii kiwemo la kujenga uwanja na kambi ya mazoezi ya Simba sio ndoto. Kupitia  mabalozi  wa Simba na mikakati yetu mingine ya utunishaji wa mapato tunaamini kwa dhati malengo yetu tutayafikia.

Kihistoria Simba imekua ni timu yenye kutendana kufikiriki maendeleo na kutumia nguvu za wapenzi na wanachama, tulianza kwa kuwawa kwanza kujenga jengo la klabu, Mzee Dalali aliona mbali na kununua uwanja Bunju, nasisi  tutaanza ujenzi, hii ndio dhima ya uongozi  ndani ya Simba kupokezana vijiti vya maendeleo’’.
Kwa upande wake MkurugenziMtendajiwa EAG Group LTD ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati ya biashara na masoko wa Simba ImaniKajula  alisema ‘’Zoezi la kuteua mabalozi wa Simba ni endelevu na litafika kila kona ya Tanzania. Hawa ni mashabiki ambao  mawazo, michango yao ya hali na  mali, kutumia ushawishi wao kutaleta maendeleo kwenye klabu yetu. Hawa watakuwa mstari wa mbele kwenye Simba Week kuhamasisha ufanyaji kazi za jamii na kushiriki kwa wapenzi na wapenda maendeleo katika kusukuma  maendeleo ya Simba.
Napenda kuwashukuru  sana Mabalozi hawa kwa kutenga muda na kuwa tayari kusaidia juhudi za kuiletea Simba maendeleo. Uongozi wangu utakuwa bega kwa bega nanyi katika kazi hii adhimu.

MAWAKALA WA MAXMALIPO SASA KUTOA HUDUMA ZA BENKI YA CRDB

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akibadilishana hati ya mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Maxcom Africa, Juma Rajabu baada ya uzinduzi wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia vituo vya Maximalipo. Hafla imefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande) 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Mkurugenzi wa Maxcom Africa, Juma Rajabu wakisaini hati ya mkataba wa makubaliano wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia vituo vya Maxmalipo. 
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akisaini hati ya mkataba wa makubaliano wa huduma za ‘FahariHuduma wakala’ kupitia vituo vya Maxmalipo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WARSHA YA KUPUNGUZA VIFO NA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akifungua rasmi warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Gianluca Azzon Mwakilishi wa EU Nchini Tanzania akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Tom Bishop kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMEND akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na Jumuiya ya umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.

Airtel wakabidhi jezi kwa timu zitakazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars

$
0
0
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, inayoanza tarehe 24 Julai mkoani Mbeya. katikati ni Afisa Uhusiano Airtel,Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilala Kanuti Daudi kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katikati ni Afisa Uhusiano Airtel Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu Nyenza akiongea wakati kupokea vifaa vya michezo ya Airtel Rising Stars kutoka kwa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel , Kulia Afisa Uhusiano Airtel,Jane Matinde kushoto ni Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari.

TANZIA

$
0
0

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu (mstaafu) kilichotokea tarehe 19 Julai, 2015 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu (mstaafu) alizaliwa tarehe 24 September 1938 katika kijiji cha Mlolo, Kata ya Tanangozi, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Alijiunga na masomo ya Shule ya msingi na Sekondari na kuhitimu mwaka 1959.

Marehemu Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Julai 1975. Alistaafu utumishi Jeshini tarehe 23 September 1993.

Marehemu Brigedia Dismas Stanslaus Msilu ameacha mke na watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 22 Julai 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 2:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika Mkoani Iringa tarehe 23 Julai 2015.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI DISMAS STANSLAUS MSILU (MSTAAFU)
AMINA

TANZANITE KUWAFUATA YOUNG SHE-POLOPOLO KESHO

$
0
0
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) wanatarajiwa kuondoka kesho jumatano asubuhi kwa Rwanda Air kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Young She-Polopolo.

Tanzanite inayowania kufuzu kwa Fainali za Kombe Duniwa mwaka 2016 nchini Papua New Guinea, itacheza mchezo huo wa marudano siku ya jumamosi tarehe 25 Julai, jijini Lusaka.

Katika mchezo wa awali uliofanyika takribani wiki mbili zilizopita, Tanzanite ilipoteza mchezo wake nyumbani baada ya kufungwa kwa mabao 4 – 0, hivyo kuhitaji kushinda zaidi ya mabao 5 – 0 ili kuweza kusonga katika hatua inayofuata.

Msafara wa Tanzanite utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo utajumuisha makocha Rogasian Kaijage (kocha mkuu), Edna Lema (kocha msaidizi), Peter Manyika (kocha wa makipa), Christina Luambano (Daktari), Mwanahamis Abdallah (mtunza vifaa) na Meneja Furaha Francis.

Wachezaji watakaosafiri ni Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Donisia Minja, Najiat Abbas, Neema Kiniga, Happyness Mwaipaja, Jane Lucas, Anastazia Katunzi, Anna Mwaisura, Janet Pangamwene, Gelwa Rugomba, Blandina Ambros, Amina Ramadhan, Asha Shaban, Maimuna Hamis, Zuwena Hamis, Amisa Athuman na Wema Richard.

BREAKING NYUZZZZZZ......: Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Dodoma afariki dunia

$
0
0
Taatifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoani Dodoma, Mariam Mfaki amefariki dunia leo katika Hospitali ya Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa uliokuwa ukimsumbua, familia yake imethibitisha kutokea kwa kifo hicho.Taarifa zaidi tutaendelea kuwajuza kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Mungu aiweke Roho yake mahala pema Peponi

-Amin.

SHULE YA MSINGI MLIMANI JIJINI DAR YAFAIDIKA NA MSAADA WA KOMPYUTA 20 TOKA VODACOM FOUNDATION

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam,wakiwa wamebeba baadhi ya kompyuta kati ya(20) zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation na kukabidhiwa na Mkuu wa taasisi hiyo, Renatus Rwehikiza(kulia) Msaada huo ulitolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo.
Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza(kushoto)akimkabidhi msaada wa moja ya Kompyuta kati ya(20)Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam.Msaada huo ulitolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo,Anayeshuhudia katikati ni Mwalimu wa somo la kopmyuta katika shule hiyo Sixbert Masero.
Mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam,Upendo Kujerwa(kulia)akionesha moja ya kompyuta kati ya(20)zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation kupitia mkuu wa taasisi hiyo Renatus Rwehikiza(kushoto)katikati ni Mwanafunzi wa shule hiyo Erick Uledi. Msaada huo ulitolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam,wakiwa na nyuso za furaha na kompyuta zao(20) walizopewa msaada na Vodacom Foundation na kukabidhiwa na Mkuu wa taasisi hiyo, Renatus Rwehikiza(hayupo pichani) Msaada huo ulitolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo kujifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta hizo.

SIMU TV: HABARI MCHANGANYIKO


WATUMISHI WA UMMA WAASWA KUWA WAADILIFU

$
0
0
Kaimu Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Jasper Mero (Mbele) akiingia katika ukumbi wa Kings way kufungua mafunzo ya awali (Induction course) kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yanayofanyika katika Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Msadizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bibi Eliaika Manyanga (Kulia) akizungumza na waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo katika mafunzo ya awali (Induction course) yanayofanyika katika Hoteli ya Kings Way Mkoani Morogoro.

Article 11

AZAM FC YAICHAPA 2-0 MALAIKA YA SUDAN KUSINI

$
0
0
Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocc akimtoka beki wa Malaika ya Sudan katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam imeshinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
mchezji wa Azam FC, Shah Farid Mussa akimtoka beki wa Malaika, David Stephen.
 Beki wa Azam FC, Shomari Kapombe akiwatoka wachezaji wa timu ya Malaika katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
 Beki wa Azam FC, Shomari Kapombe akiwania mpra na beki wa Malaika, Yengo Son Ngum katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam imeshinda 2-0.
 Beki wa Azam FC, Shomari Kapombe akiwania mpra na beki wa Malaika, Yengo Son Ngum katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam imeshinda 2-0. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM JUMATANO

Uchaguzi Mkuu wa Rais nchini Burundi wafanyika kwa amani

$
0
0
 Wananchi wa Burundi leo wamepiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Uchaguzi huo umefanyika katika mazingira ya amani ingawaje kwa upande wa jiji la Bujumbura wananchi walianza kujitokeza zaidi mchana
 Wananchi wakipiga kura Bujumbura  kituo cha Uchaguzi cha Ruhunja A  eneo la Rusagara katika jimbo la Gitega.
 Mawanamama akipiga kura yake  kituo cha Uchaguzi cha Ruhunja A  eneo la Rusagara katika jimbo la Gitega.
Bango la wagombea nafasi ya Urais wa Burundi
Waangalizi wa uchaguzi wa Rais nchini Burundi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na timu ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Burundi wakiwa katika kituo cha Uchaguzi cha Ruhunja A  eneo la Rusagara katika jimbo la Gitega.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images