Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 912 | 913 | (Page 914) | 915 | 916 | .... | 3284 | newer

  0 0
  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.
  DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
  Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
  Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
  Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.


  0 0

  Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Dkt Shirika la mawasiliano la TTCL Tanzania limekabidhi jumla ya bati 100 zenye thamani ya shilingi Milioni mbili kwa Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe Dokta Pindi Hazara Chana ambaye pia ni Naibu waziri wa maendeleo ya Jamii  Wanawake jinsia na watoto kwa ajili ya sekta ya elimu mkoani Njombe.


  Akikabidhi bati hizo  kwa niaba ya mkurugenzi kuu wa TTCL Tanzania, Kaimu mkurugenzi kanda ya nyanda za Juu kusini bwana James Mlaguzi amesema kwa kuwa shirika hilo limekuwa likifanya kazi za kijamii kupitia mapato yake hivyo limeamua kuchangia sekta ya Elimu mkoa wa Njombe kupitia Mbunge Chana kwa kutoa bati hizo.


  Amesema katika mkoa wa Njombe wametoa jumla ya bati 100 ambazo zitasaidia kupunguza changamoto katika ujenzi wa madarasa na maabara katika shule mbalimbali.


  Aidha mara baada ya kukabidhiwa bati hizo, Naibu waziri Chana na msafara wake pamoja na TTCL wameelekea katika shule ya Sekondari Mbeyela ambako amekabidhi bati 20 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.


  Taarifa  fupi ya shule ya Mbeyela Sekondari iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Emphraim Ngimba imeeleza kuwa shule hiyo yenye zaidi ya wanafunzi 500 na walimu zaidi ya 50 zitasaidia kupunguza adha ya ukarabati wa madarasa kutokana na madarasa mengi kutokamilika.

  Akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa kukabidhi bati hizo 20 Mbunge Pindi Chana ametumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi hao kujikita zaidi katika masomo ili waje kuwa viongozi makini katika Taifa la Tanzania.  0 0

   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelis Lumato akikata utepe
  kuzindua mnara wa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
  katika kijiji cha Nduruma, wilayani Arumeru Mkoani Arusha ,
  akishuhudia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton
  Majwala.
   Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Brighton Majwala akitoa msaada
  wa vitabu  Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Singisi , Hamad
  Boay , wakati wa uzinduzi wa huduma manara wa huduma za mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika kijiji cha Nduruma,
  wilayani Arumeru Mkoani Arusha.  Shule zilizofaidika na msaada wa
  vitabu ni pamoja na  sekondari za Nduruma na Singisi wilaya Arumeru.  0 0

  Beki wa Timu ya Gor Mahia ya Nchini Kenya, Harun Shakava (18) akizuia mpira uliokuwa ukimilikiwa na Kiungo wa Timu ya KMKM ya Zanzibar, Iddi Kambi Iddi (6) wakati wa mtanange wa Mashindano ya Cecafa Kagame Cup uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Gor Mahia imeshinda bao 3-1.
  Wachezaji wa Timu ya Gor Mahia ya Nchini Kenya, Aucho Khalid (10) na Karim Nizigiyimana (14) wakishangilia ushindi wao dhidi ya timu ya KMKM ya Zanzibar, katika mtanange wa Mashindano ya Cecafa Kagame Cup uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Gor Mahia imeshinda bao 3-1.
  Mchezaji wa timu ya KMKM ya Zanzibar, Juma Mbwana Faki (8) akiwania mpira na Mshambuliaji wa Timu ya Gor Mahia ya Nchini Kenya, Aucho Khalid (10) wakati wa mtanange wa Mashindano ya Cecafa Kagame Cup uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Gor Mahia imeshinda bao 3-1.

  0 0

  ‘Makala ya Kusisimua yenye matukio yenye hisia nzito.’ 

  Andy Markowitz, Tovuti ya Muziki wa Filamu Music Film Web

  ‘Tafakari ya kusisimua ya urafiki usio wa kawaida kati ya Kijana Mtengenezaji wa filamu na diva wa Zanzibar mzee wa miaka 100 Zanzibar diva’ Garth Cartwright - mwandishi, “More Miles Than Money”Umbali mkubwa kuliko fedha”

  ‘Uwasilishaji wa wa nyota …iliyofifia na kuifanya ing’are upya’ 

  Martin Mhando, Mkurugenzi ZIFF

  Nilimpiga Picha Bi Kidude “I Shot Bi Kidude”, ni makala mpya ya simulizi  iliyotayarishwa na Andy Jones, mtengenezaji wa filamu wa Uingereza  ambayo itahitimisha Tamasha la Filamu la Kimataifa hapa Zanzibar,.  Watazamaji wa Zanzibar watamsikia msimulizi mwenyewe akisimulia kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijifunza kwa muda mfupi matamshi kwa msaada wa wanamziki Wazanzibari Mim Suleiman na Bwana  Mohammed Issa Matona.


  Kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne, kuanzia 2003 mpaka 2006, Andy Jones alimfuata  Bi Kidude alipokuwa akisafiri duniani. Matokeo yake ni kupokea tuzo ya  filamu AS OLD AS MY TONGUE, ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza  katika mwaka  2006 na baadaye iliendelea kuwa kivutio kwenye matamasha ya filamu na muziki duniani kote.. 
  Baada ya kutembelea Zanzibar kila mwaka kwa karibu muongo mmoja, Jones hakuweza tena kumuona Bi Kidude kwa muda wa miaka mitatu.  Katika mwezi Agosti mwaka 2012, taarifa zilifika Uingereza zikieleza kuwa mwanamziki kinara maarufu Africa Mashariki ametekwa nyara . Haikuchukua muda mrefu Andy alirudi Zanzibar kupata ukweli wa taarifa .  

  Wiki chache tu baada ya kisa hicho kuibuliwa kwa picha zilizopigwa na Natalie Haarhoff kutoka Afrika ya Kusini , muimbaji mzee sana wa kimataifa amefariki, akiwa na umri unaosemekana kuwa zaidi ya miaka mia moja .  Jones alikurupuka kutoka nyumbani kwake huko Newcastlena kufika uwanja wa ndege wa Heathrow dadikia chache kabla ya ndege iliyopangwa kwenda Nairobi kuondoka. Alifika kwenye mazishi ambayo yalishtua kisiwa kizima..

  “I SHOT BI KIDUDE, ni simulizi yangu kuhusu mambo yalivyokuwa wakati wa mwisho wa maisha ya  Bi Kidude’ .  Kama ilivyo kwenye simulizi nyingine , kuna maelezo mbalimbali kuhusu ukweli wa jambo.  Kimsingi kuna vitu vingine ambavo si rahisi kwa mgeni kuvitambua, hata hivyo ninatumaini kuna vitu vingine haviwezi kufichika machoni . Ninaloona mimi hisia ya kusherehekea nguvu za muziki na kufanya vitu ambavyo vinatuletea furaha  pale tunapoweza ” Andy Jones anasema.

  0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya jiji la  Dar es salaam limefanikiwa kuwatia mbaroni Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa Majambazi waliovamia Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga, jijini Dar es Salaam, huku wengine watatu wakiuwawa katika mapambano ya kutupiana risasi na Polisi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni,  jijini Dar es Salaam.


  Kwa mujibu wa Kamanda Kova, tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu  maeneo ya Tuangoma. Majambazi wanaotuhumiwa kuhusika na  tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo hicho cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18. 
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao  inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikiana  na Polisi wa Mkoa wa Pwani.
  Kamanda Kova amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma, ambapo watuhumiwa wakiwa wanakapita katika  pikipiki mbili walipowasimamishwa na askari  walikaidi amri na kisha kuanza kurusha risasi. Polisi wakajibu mapigo na majambazi watatu wakauwawa.
  Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala, Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, mkoa wa Pwani.
  Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga na Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
  Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa hao wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki  15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamezihifadhi chini ya ardhi bada ya kuweka kinyesi juu yake.
  Amesema katika Shimo hilo  walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na  fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
  Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kwa kuwa huwa hailipi.

  Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishikiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanavtaarifa nazo.
  “Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.
  Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea  Julai 12, 2015  majira ya saa nne za usiku katika kituo cha Sitakishari.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara, jijini Dar es Salaam.
   Naibu Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu ya operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
    Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh. Milioni 170 zilizokutwa katika Shimo la watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakisaari na kuua askari wanne na raia watatu
   Fedha za watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishali zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi wa habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika wakati akitoa  taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa  waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari jijini Dar es salaam 
  Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na watuhumiwa wa ujambazi waliovamia Kituo cha Stakishari zikioneshwa wakati Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  0 0   Mama Shamsa Selengia Mwangunga akirudisha fomu kugombea ubunge Viti Maalum Mkoa - Dodoma


  0 0


   Modesta Joseph, mwananfunzi wa Kisutu Sekondari Dar es Salaam akipeana mkono wa pongezi na hati ya fedhana John Mngodo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kushinda tuzo ya ubunifu wa TEHAMA wa kuwawezesha wananfunzi kuwasilisha kero zao za usafiri kutumia TEHAMA kwa Taasisi ya EWURA.

   Mgimba Faustine akipokea tuzo ya fedha taslimu kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kushinda Tuzo ya Wabunifu wa TEHAMA ya kuwawezesha wateja kutumia simu ya mkononi kubaini bidhaa feki. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Simo-Pekka Parviainen na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan Mshinda

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimpatia Japhet Sekenya tuzo ya wabunifu wa TEHAMA kwa kutengeneza mtindi kwa kutumia karanga na unaoweza kutibu magonjwa mbali mbali ya binadamu kama vile vidonda tumboni, kuzuia saratani. Wa tatu kulia Naibu Balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Simo-Pekka Parviainen akishuhudia tukio hilo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH (Wa pili kulia), Dkt. Hassan Mshinda

  0 0

  Mjumbe wa Bodi ya Utendaji wa Kituo cha Ushirikiano wa kilimo na Maendeleo Vijijini cha nchi za Umoja wa Ulaya, Afrika, Karebiani na Pasifiki (CTA), ProfesaFaustin Kamuzora akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya wiki moja ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano na mitandao ya kijamii kwa wadau toka taasisi mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam.  Mafunzo hayo yanaendeshwa na CTA na Taasisi ya Nafaka ya Afrika ya Mashariki (EAGI).  


  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Esther Wanjiru anayelelewa katika Kituo cha watoto cha Mama Ngina huko Nairobi muda mfupi  baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya tarehe 19.7.2015.  Mama Salma yupo nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa Barani Afrika.
    Balozi wa Tanzania nchini Kenya Ndugu John Haule akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Intercontinental iliyoko Nairobi tarehe 19.7.2015 kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wake wa Marais wa Afrika utakaozungumzia magonjwa ya kansa ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Kenya Mama Margret Kenyatta wakati wa tafrija ya kuwakaribisha kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaozungumzia masuala ya kansa ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume. Tafrija hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Madame Lordina Draman Mahama, Mke wa Rais wa Ghana wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Niger Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa 9 wa wake wa Marais wa Africa wanaokutana Nairobi kuzungumzia kansa ya matiti, kizazi na tezi dume.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Rais wa Namibia Mheshimiwa Monica Geingob wakati wa tafrija kwa wajumbe wa mkutanon wa 9 wa wake wa Marais wa  nchi za Afrika. PICHA NA JOHN LUKUWI

  0 0

   Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani,inatarajiwa kutingisha jukwaa la
  maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni barani ulaya 6th International African Festival in Tübingen, Ujerumani,bendi hiyo maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja  itapanda jukwaani siku ya Jumamosi 27 Julai 2015 majira saa 2.00 Usiku katika
  uwanja wa Festplatz,Europa str,mjini Tübingen ,uliopo Ujerumani ya Kusini. 
  Kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa Band ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au FFU,chenye utajiri wa wanamuziki vijana waliojaa vipaji, bendi inasadikiwa kuwanasa
  washabiki kila kona duniani kutokana na mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini. bendi hiyo kwa sasa inatamba na CD mpya ya " La Mgambo" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK.
  Usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband au watupie jicho at


   Gwaride jukwaani
  Nyomi ya kufa mtu

  0 0

  SAM_3941Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akiongea katika mkutano wa hadhara katika kata mpya ya Olmoti jana ambapo wagombea 12 walipata fursa ya kujitambulisha kwa wananchi na kunadi sera zao, Mustapha panju amesema kuwa kilicho msukuma kugombea nafasi hiyo ni kuakikisha wananchi wa jimbo la arusha wanapata ridhaa ya kuwa na maendeleo ya hali ya juu ikiwemo kuweza kukua kisayansi na kuweza  kufika mwezini.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_3903Mustafa Panju akiwa na wagombea wenzake wa chama hicho jana katika kata mpya ya Olmoti jijini Arusha walipokwenda kujitambulisha kwa wananchi na kunadi sera zao pia walipata fursa ya kutembelea kata ya Olasiti,Osunyai JR
  SAM_3972Mtoto aliyefika kusikiliza sera za wagombea Ubunge wa chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa ameshikilia kipeperushi cha mgombea Ubunge jimbo la Arusha Mustafa Panju katika kata ya Osunyai JR
  SAM_3905Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano akizungumza katika kata mpya ya Olmoti jana ambapo alisisitiza wananchi kusikiliza sera za wagombea huku akiwataka kutokupiga makofi au kushangilia wakati wakijieleza
  SAM_3918Meza kuu pamoja na wagombea Ubunge jimbo la Arusha mjini
  SAM_3974

  0 0

  Na Bashir Yakubu
  Wiki  chache zilizopita, yaani Tarehe  6  JULY,  2015  mahakama  ya  Hakimu Mkazi ya Kisutu  ya jijini Dar es salaam ilitoa  hukumu  katika kesi  maarufu  na  ya  muda  mrefu   iliyokuwa  ikiwakabili  mawaziri  wa  zamani  wawili  na  katibu  mkuu  mmoja.   Blog  hii  iliripoti  kwa  ufupi   matokeo  ya  kesi  hiyo    na  kuahidi  kutoa  ufafanuzi  wa  kitaalam  hapo  baadae  kupitia  wanasheria  wake. 

   Kwa kuwa  GLOBU YA JAMII imekuwa  mstari  wa  mbele  kueleza  masuala  ya  msingi   ya  kijamii yakiwemo  yale  ya  kisheria  ambayo  hayapatikani mitandao  mingine  ya  kijamii,  imeona  ni  muhimu kuufafanulia  umma nini kilitokea  katika kesi  hii  ya kihistoria mwanzo  hadi mwisho.  Kuendelea kusoma BOFYA HAPA.

  0 0

  IMG_9354

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
  Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
  IMG_9341
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
  IMG_9348IMG_9317
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.

  0 0

  Keki maalumu iliyotengenezwa na kupambwa kwa rangi za Bendera ya Taifa la Afrika Kusini iliyokabidhiwa kwa washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya familia maskini. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Muigizaji Jacky (Rajesh Kumar ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania,Ibrahim Musa.
  Mkuu wa wiaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya mapokezi ya ugeni huo ulioanda mlima Kilimanjaro akimkaribisha keki Muigizaji Jacky mara baada ya kuteremka kutoka Mlima Kilimanjaro.
  Washiriki wa timu hiyo iliyopanda mlima Kilimanjaro kwa uratibu wa Mfuko wa Mandela wakifika katika lango la Marangu mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.


  0 0

   KOCHA Mfaransa, Patrick Liewig, akizungumzia mikakati yake ya kiufundi baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu ya soka ya Stand United ya Shinyanga, kwenye makao makuu ya kampuni ya Acacia jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 20, 2015. Mkataba huo ni chini ya udhamini mnono wa kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi mitatu ya kuchimba dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara

  Na K-VIS MEDIA

  KLABU ya soka ya Stand United ya mjini Shinyanga, imesaini mkataba wa miaka miwili na kocha Mfaransa, Patrick Liewig, ili kuinoa timu hiyo itakayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.

  Akizungumza wakati wa kutiliana saini mkataba huo kwenye ofisi za wadhamini wakuu wa timu hiyo, Acacia, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2015, mwenyekiti wa Stand United, Amani Vincent alisema, baada ya kuangalia vigezo mbalimbali ambavyo klabu hiyo ilihitaji, imeridhika pasina shaka kumuajiri kocha huyo, ili ainoe timu yake kwa misimu miwili.

  “Kocha huyu kama mjuavyo anayo sifa ya kuinua vipaji, na sisi tunataka kutengeneza vipaji kutoka chini ili wachezaji hao waweze kuichezea timu yetu”, amesema.

  Kocha huyo aliwahi kuifundisha Simba ya Dar es Salaam, kwa miezi sita kabla ya mkataba wake kusitishwa.

  Stand United ambayo inashiriki ligi nkuu ya soka Tanzania bara kwa mara ya pili, hivi karibuni ilipata udhamini mnono kutoka kampuni ya uchimbaji madini, Acacia.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Liewig, amesema, atahakikisha anajenga msingi mzuri timu hiyo kwa kuwa na timu ya kikosi cha wachezaji chipukizi ili iwe na hazina ya wachezaji. “Kinachohitajika ni kuwa na subira, kwani ninataka kujenga timu na kazi hii siyo ya mara moja.”amesema.

  Pamoja na mabo mengine, udhamini wa Acacia kwa timu hiyo  ni pamoja na malipo ya kocha.

   MWENYEKITI wa Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent, (wapili kulia), akibadilishana hati za mkataba na Kocha Mfaransa, Patrick Liewig, makao makuu ya kampuni ya Acacia, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 20, 2015. Kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano wa Acacia, Frederick Njoka
   Liewig, (kushoto), na Amani Vincent, "wakimwaga" wino
   Mwenyekiti wa Stand United, Amani Vincent, (kulia), akizungumzia maudhui ya mkataba huo na uamuzi wa klabu yake kumpatia "kandarasi"kocha huyo

   Liewig, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
  Frederick Njoka, akifungua mkutano huo wa waandishi wa habari

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta huko Nairobi kuhudhuria mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti, shingo ya kizazi na tezi dume tarehe 20.7.2015.
  Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa Afrika wakifuatilia kwa makini sherehe za ufunguzi.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika Issofou Mahammadou wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Wake wa Marais wa nchi za Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyetta (hayupo pichani) tarehe 20.7.2015.


  0 0


  Mratibu Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, akizungumza na baadhi ya watumishi wa shule ya sekondari James Sangu (hawapo pichani ) juu ya namna ya kujiunga na fao hilo kabla ya kufanyika kwa zoezi la makabidhiano ya hundi kwa Jaqline Ndyamkama ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mama yake Anna Jelle kufariki Dunia. Picha zote Emanuel Madafa, Mbeya.  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

  TAASISI ya Kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Financial Services, jana imewakabidhi wanafunzi wawili hundi ya Sh Milioni tatu, itakayowawezesha kila mwaka kupata Sh Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya ada kwenye shule zao wanazosoma kutokana na malipo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao inayoendeshwa na taasisi hiyo.


  Wanafunzi hao ni Jacqueline Ndyamkana wa shule ya sekondari ya James Sangu na Joceline Ndyamkana wa shule ya awali, huku malipo hayo yakitokana na bima ya mama yao aliyejulikana kwa jina la Anna Jelle, ambapo kwa kupewa kiasi hicho cha fedha kila mwaka, kutawafanya wasome bila usumbufu wowote katika kipindi hicho cha miaka mitatu mfululizo.

  Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura,akionyesha moja fomu maalumu zinazotumiwa na wateja wao katika hautua za awali wakati wa uombaji wa mkopo kupitia taasisi hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 912 | 913 | (Page 914) | 915 | 916 | .... | 3284 | newer