Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Wakazi wa Dar wakiisherehea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ufukwe wa Coco Beach jioni ya leo

$
0
0
 Sehemu ya wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye ufukwe wa Coco Beach jioni ya leo, ikiwa ni sehemu ya kuisherehekea sikumbuki ya Eid El Fitr. 
 Wengi hupenda kwenda sehemu ya namna hii kwa ajili ya kupunga upepo mwanana wa Bahari. 


MUSTAFA PANJU ACHUKUA NA KURUDISHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI AAHIDI UMOJA NA MAENDELEO

$
0
0
SAM_3880
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akimkabidhi Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano fomu ya kuwania kinyang'anyiro hicho baada ya kuchukua fomu hiyo jana na kurejesha huku akisisitiza kuwa endapo atafanikiwa kupitishwa na chama hicho au laa atashirikiana na wananchi pamoja na wanaCCM katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo ambalo lipo mikononi mwa chama cha Demokrasia na maendeleo( CHADEMA)Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3827
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju ambaye ni mmoja wa wagombea wa jimbo la Arusha mjini kupitia chama cha mapinduzi CCM akionyesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano jana katika ofisi za CCM wilaya
SAM_3886
Hapa Mustafa Panju akiandika jina lake katika fomu yenye majina ya waliokuja kuchukua fomu kupitia chama hicho kwa  Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ,kushoto ni mke wake aliyemsindikiza kuchukua fomu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA SWALA YA EID EL FITRI KITAIFA MKOANI GEITA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Baadhi ya Viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) na wananchi katika swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri na waumini wa Dini ya Kiislamu iliyofanyika Kitaifa wa Mkoani Geita leo Julai 18, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa dini ya Kisslamu wakati wa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally, baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi, Kalangalala, mkoani Geita, leo Julai 18, 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa Kiislam mara baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi, Kalangalala, mkoani Geita, leo Julai 18, 2015.

KALAMU EDUCATION FOUNDATION YALA SIKUKUU YA EID FITRI NA WAGONJWA NA MAYATIMA

$
0
0
Mmoja wa Wakurugezi wa Kalamu Education Foundation Sis. Kwezi akiongozana na wakurugenzi wenzake kugawa zawadi mbali mbali za Vyakula, Vinywaji, Nguo na Pesa vyenye thamani ya TZS 1,658,000 kwa wagonjwa katika ziara yao ya Kusheherekea Sikukuu ya EID EL-Fitri katika Hospital ya Mwananyamala, Dar es salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation, Ndugu Mohamed Kamilagwa akiongozana na Makamu wake Hajjat Asha Mtwangi wakimsikiliza kwa makini mmoja wa Madaktari juu ya Changamoto za wagonjwa wasio na Ndugu na Jinsi Gani Taasisi kama Kalamu Education Foundation inaweza Kusaidiana na Hospitali hiyo kuwasaidia katika kupata tiba kwa urahisi.
Mmoja ya Wakurugenzi wa Taasisi Kalamu Education Wakili Said Abdallah Aziz akiongea na kuwapa matunda wagonjwa Mbali Mbali katika Hospitali ya Mwananyamala katika Shamra Shamra ya Kusheherekea Sikukuu ya EID Fitri.
Mwenyekiti wa Kalamu Education Foundation Ndugu Mohamed Kamilagwa (Mwenye Miwani) alipokuwa akifurahi na watoto wa Kituo Cha watoto Yatima cha Jaribu Orphanage Center Kilichopo Kijiji Cha Jaribu, Wilaya ya Rufiji ambapo Taasisi hiyo alipeleka Vyakula na Vinywaji vyenye thamani ya TZS 650,000 katika kuhakikisha sherehe za EID zinafana kwa watoto hao.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL KATIKA BARAZA LA SIKUKUU YA EID EL- FITRI KITAIFA MKOANI GEITA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Barala la Sikukuu ya Eid El- Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana ya Nyankumbu, mkoani Geita l
 Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Baraza la Sikukuu ya Eid El- Fitri, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bi Fatma Maswi, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia katika Baraza hilo lililofanyika Kitaifa Mkoani Geita l
 Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia katika Baraza hilo
 Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) Suleiman Lolila, akizungumza, kabla ya kumkaribisha Kaimu Mufti.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bi Fatma Maswi, akizungumza kuwakaribisha wageni katika hafla hiyo ya Baraza la Sikukuu ya Eid El- Fitri. 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Sheikh  Haruna Abdallah Kichwabuta, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo na Makamu wa Rais Dkt. Bilal kuhutubia. Picha na OMR

DIAMOND PLATNUMZ ANG'ARA KWENYE TUZO ZA MAMA

KUTOKA MAKTABA: ANKAL NA WANAHABARI NGULI NCHINI

$
0
0
Ankal akiwa na sehemu ya wanahabari nguli nchini katika hafla ya michezo ya wanahabari katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Haji Sunday Manara, Angetile Osiah, Samson Mfalila, Ankal, Aboubakar Liongo, Edo Kumwembe na Rashidi Kejo

Mama Salma Kikwete ajiunga na waombolezaji kwenye msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja Banza Stone aliyezikwa jijini Dar es salaam

$
0
0
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wana familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji mama mzazi wa marehemu  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na kiongozi wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta Asha Baraka  katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu   katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.
Mamia ya waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Ramadhan Masanja "Banza Stone" wakati wakiutoa mwili huo nyumbani kwao kuelekea Msikitini kwa kuswaliwa kabla ya  kwenda kuuhifandi  kwenye Makaburi ya Sinza, Jijini Dar es salaam alasiri hii.


Coventry Muslim Swahili Association (COMSWA) wafanikisha swala na sherehe za Eid el Fitr

$
0
0
BismiLlahi Rahman Rahiim, Asalam Alaikum WarahmatuLlwahi Wabarakaatuh...
Coventry Muslim Swahili Association (COMSWA) ambayo ni jumuiya ya Waislam wanaozungumza ki- Swahili nchini Uingereza (United Kingdom) hatimaye wameweza kwa mafanikio makubwa kusherehekea Eidil fitr ugenini kama walivyozoweya kusherehekea wakiwa nyumbani. 
Mafanikio hayo yamekuja ktk kipindi ambacho yalihitajika sana kwa ajili ya kufundisha vizazi vyao maadili mema ambayo yanakwenda sambamba na malengo ya dini yao na utamadunu wao. 
Malengo hasa ni kuiweka jamii pamoja kwani wanaamini kwa kufanya hivyo wataweza kuhifadhi utamaduni wao na kufanikisha malengo mbalimbali ya kimaendeleo. 
Wanapenda kutumia fursa hii kuwapa mkono wa Eid. 
Kwa ajili ya kuwafahamu zaidi tembelea www.comswa.com

WANA CCM KIBAO WAJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI

$
0
0
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini, Priscus Tarimo, akikabidhiwa fomu ya nafasi hiyo na katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Loth Ole Nesele katika ofis za chama hicho za Wilaya ya Moshi mjini.
Naibu kamanda wa Vijana wa CCM, manispaa ya Moshi, Edmund Rutaraka akipokea fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kutoka kwa katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi mjini,Donatha Mushi.
Kada wa Chama cha Mapinduzi manispaa ya Moshi Daudi Mrindoko akiwa ameambatana na mkewe alipofika kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi mjini zilizokabidhiwa kwake na katibu msaidizi wa chama hicho Donatha Mushi.
Mwakilishi wa jamii ya Bantu Union ,Omary Mwaliko akirejesha fomu za kuwania kuteuliwa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini mara baada ya kuzijaza

Uongozi mzuri siri ya maendeleo Muheza - Adadi Rajabu

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Muheza 
 Ushirikishwaji wa wananchi na uongozi mzuri ni nyenzo muhimu za kuleta maendeleo katika wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. 
 Akihutubia wananchi waliojitokeza kumuunga mkono mwishoni mwa wiki wilayani Muheza, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajabu alisema maendeleo duni katika wilaya hiyo yametokana na uongozi mbaya. Alikua akichukua fomu za kugombea ubunge jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). 
 “Muda wa mabadiliko umefika,” alisema balozi huyo na kuongeza: “ili wilaya hii iendelee tunahitaji uongozi mzuri na ushirikishwaji wananchi.” 
 Aliwaambia mashabiki wake kuwa anagombea ubunge kwa kuwa anaamini kuwa uongozi wa sasa haujachukua hatua zinazostahili katika kusaidia wananchi kupata maendeleo wanayohitaji. 
 Alisema upatikanaji wa maji safi na salama ya uhakika, barabara na elimu bora vitakuwa vipaumbele atakavyoshughulikia haraka. Alisema haikubaliki kwa kina mama kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kuahidi kumaliza tatizo hilo. “Nikiwa mbunge wenu, tatizo hili litakwisha,” aliahidi. 
 Alisema atahakikisha anaishawishi serikali kuleta walimu wa kutosha katika wilaya hiyo kwa kuwa madarasa pekee haina maana ya elimu bora kwa watoto. Bw. Rajabu alisema barabara mbovu ni kikwazo kwa maendeleo ya wakulima wa wilaya hiyo ambao wanashindwa kusafirisha mazao yao sokoni na kujiongezea kipato. 
 “Changamoto zote hizi zinahitaji muwakilishi mzalendo atakayekuwa tayari kufanya kazi na wana Muheza kumaliza tatizo la umaskini,” alisema mwana usalama huyo mzoefu mstaafu, ambaye kabla ya kuwa balozi aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika Jeshi la Polisi Tanzania.
 Aliyekua Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajabu (kulia) akipokea fomu kutoka kwa katibu wa CCM Wilaya ya Muheza, Tija Magoma kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Muheza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni wilayani Muheza.

Aliyekua Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajabu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kuchukua fomu na kuelezea nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Muheza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni.  Kulia ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo, Bw. Ali Kanyika. 

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO JULY 19

MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAJITOKEZA KUMLAKI KWA SHANGWE DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

$
0
0
 Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo.
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili leo jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.
 Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili jijini Mwanza jioni ya leo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Magufuli yuko jijini Mwanza kujitambulisha kwa Wananchi.
 Mke wa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojiotokeza kwa wingi kuwapokea,Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
 Baadhi ya Wananchi wakilikimbiza gari la  Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa shangwe kama waonekanavyo pichani ,wakati Magufuli lipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
 Baadhi ya Wananchi wa jiji la Mwanza wakiwa wamefunga barabara kwa muda wakishangilia ujio wa  Mgombea Uraisi wa CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.mchana.PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI USIKU HUU BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YA KIKAZI YA USWISI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Uswisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kurejea nyumbani baada ya ziara ya kikazi mjini Geneva
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kurejea nyumbani baada ya ziara ya kikazi mjini Geneva. PICHA NA IKULU

Akiwa mjini Geneva, Rais Kikwete ameongoza vikao vya  Jopo la Kimataifa Linalopendekeza Jinsi Dunia inavyoweza kukabiliana na majanga yajayo ya magonjwa ya milipuko ambalo kazi yake imeungwa mkono na nchi 21 ambazo zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Miongoni mwa mikutano ambayo Rais Kikwete ameiongoza katika Makao ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva ni pamoja na yeye na wanajopo wenzake kutoa maelezo kuhusu maendeleo ya kazi yao kwa nchi ambazo zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Nchi hizo ambazo zimeunga mkono kazi ya Jopo hili katika mkutano huo ni Venezuela, Umoja wa Ulaya (EU), Uholanzi, Finland, Shirikisho la Russia (Russian Federation), Norway, China, Ubelgiji, India, Ujerumani, Marekani, Uswisi, Canada, Brazil, Denmark, Uingereza, Israel, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Umoja wa Afrika (AU), Benki ya Dunia (WB), Jamhuri ya Korea na Japan.
Pamoja na kwamba wajibu mkuu wa Jopo hili siyo kuchunguza ugonjwa wa Ebola na madhara yake, bado ugonjwa huo ni msingi mkuu wa kazi ya Jopo hilo ambalo wajibu wake ni kutumia uzoefu wa Ebola kutoa mapendekezo ya jinsi dunia inavyoweza kukabiliana na majanga ya magonjwa ya milipuko katika siku zijazo.
Ugonjwa wa Ebola ambao ulilipuka katika nchi hizo tatu za Afrika Magharibi mwishoni mwa mwaka 2013 mpaka sasa umeua watu 11,000 katika nchi hizo na kusababisha mshtuko mkubwa duniani.
Hiyo ilikuwa mara ya 24 kwa ugonjwa huo kulipuka katika Afrika tokea ulipolipuka kwa mara ya kwanza mwaka 1976, miaka karibu 40 iliyopita, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakati huo ikiitwa Zaire.
Hata hivyo, katika milipuko ya kwanza 23, ugonjwa huo uliua watu wachache zaidi kuliko mlipuko wa 24.
Jopo hilo limeambiwa kuwa tofauti na matarajio ya dunia kuwa ugonjwa huo ulikuwa unamalizika katika nchi hizo hasa katika Liberia, umeanza kupata kasi tena na nchi hizo tatu zinakisiwa kuwa na wagonjwa karibu 70.
Jopo hilo lenye Wajumbe sita liliteuliwa Aprili, mwaka huu, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon na kufanya vikao vyake vya mwanzo Mei, mwaka huu, katika makao makuu ya UN, mjini New York, Marekani.
Mbali na kukutana na nchi zilizochangia mapambano dhidi ya Ebola, Rais Kikwete na Jopo lake limepata nafasi ya kumsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, wakati ugonjwa huo unalipuka Dkt. Luis Gomes Sambo wa Angola ambaye aliwaeleza wajumbe historia ya ofisi ya kanda hiyo iliyoko mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo, katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Aidha, Wajumbe wa Jopo wamemsikiliza Mkurugenzi mpya wa Kanda, Dkt. Matshidizo Rebecca Moeti ambaye amezungumza kwa njia ya mkutanomtandao (teleconference) kutoka mjini Brazzaville. Dkt. Moeti alianza kazi yake Januari Mosi, mwaka huu, 2015.
Vile vile, Wajumbe wa Jopo wamesikiliza jitihada za Jamhuri ya Rwanda kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kupitia kwa Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Agnes Binagwaho ambaye naye alizungumza kwa mkutanomtandao kutoka Kigali, Rwanda.
Nje ya vikao hivyo, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Mstaafu wa UN, Mheshimiwa Kofi Annan. Katika mkutano huo kwenye Hoteli ya Intercontinental, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbali mbali ya kimataifa, ikiwamo hali ya Burundi.
Rais pia amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kituo cha South Centre ambacho kina makao yake mjini Geneva, Dkt. Martin Kohr. Kituo hicho kilianzishwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kwa nia ya utekelezaji wa Ripoti ya Kamisheni ya Nchi Zinazoendelea (South-South Commission), ambayo iliongozwa na Mwalimu.



NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: TUMKUMBUKE RAMADHANI MWANA MASANJA BANZA STONE NUMBER ONE


JUST IN: WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKATAA KUGOMBEA TENA UBUNGE

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa  jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha. 
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili, Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.

Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati wote  na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini. 
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la Katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao. 
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenzi Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hata atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo. 
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi. 
Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 19, 2015.



FILIKUNJOMBE APELEKEWA FOMU YA UBUNGE NYUMBANI KWAKE , MWENYEWE AMPONGEZA JK ASEMA DR MAGUFULI ATEGEMEE KURA ZA KISHINDO LUDEWA

$
0
0
Msafara  wa  vijana wa Boda  boda  zaidi ya 300  waliowasindikiza  wazee wa Ludewa kumchukulia  fomu  mbunge  Deo Filikunjombe
Wazee  wakimpoelekea  fomu ya ubunge Deo Filikunjombe nyumbani kwake  kwa maandamano
Safari  ya  kuelekea  nyumbani kwa Filikunjombe kukabidhi fomu ya ubunge.
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipokea  fomu  kutoka kwa  wazee  na vijana  waliomchukulia na kwenda  kumkabidhi nyumbani kwake Ibani mjini  Ludewa. Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

African in New York Eposide 17: Music is life

$
0
0
 Whether people sing in churches or for social occasions, music and songs bring people together when they carry important and irresistible messages. Ms. Aleta Stowers a singer herself explains the role of music in worshipping and in entertaining the masses. 
Culturally speaking life becomes boring and almost sad without songs. When people feel happy, what do they do? Four things basically. They sing, dance, laugh or smile. 
All of this makes life more lovable and livable! To learn more about the role of music in our lives as well as the benefits of music to our society, this interview provides us with some interesting particulars to consider when we think about music and what music can do in our lives. 
 You are welcome to watch this show on Friday July 24th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 58 Minutes. 
The below video has only 31 minutes of the 58 minutes. To watch the entire 58 minutes of the show please see the details below. 
 Provider Channel Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998 FiOS 36 RCN 85

michael richard wambura ajitosa ubunge kinondoni

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images